Sababu zinazonifanya nisimpende Mungu

Sababu zinazonifanya nisimpende Mungu

Kwahiyo kipimo cha mtu kuwa na akili sana ni kufanya chochote kile anachojisikia kufanya?

Kwa kipimo hicho nadhani machizi ndiyo watakuwa wanaongoza kwa akili maana ndiyo wana uhuru huo wa kufanya kile wanachojisikia.
Mkuu sikuwa na maana hii... nimeboresha nilichokuwa nataka kukifikisha.
 
Fenesi lina radha gani.?? Nakuuliza swali hili haliyakuwa nimezaliwa na ulemavu wa kutambua radha ya vitu..(swali lisilo jibika hili naamini)..mungu yupo beyond your sense hii hali ya ukomo wa utambuzi inaconfuse ndiomaana hapo juu umesema mungu anaweza kua shangazi kwa sababu umemuomba pocket money akakupa.
Ukiwa kipofu unaweza kusema kwamba unaamini hauoni?
Ukiwa hauhisi unaweza kusema naamini sihisi?
Ukiwa hausikii unaweza kusema naamini sisikii?
Je, visivyoingia kwenye context ya imani una maana ni vile vinavyoonekana kwa macho tu?
 
Nilikuwa na maana hawafungwi na kifungu chochote cha kimaandiko ya kidini....
Sasa hapo kuna mahusiano gani na kuwa na akili sana? hebu funguka mkuu pengine una point ya msingi.
 
Ukiwa kipofu unaweza kusema kwamba unaamini hauoni?
Ukiwa hauhisi unaweza kusema naamini sihisi?
Ukiwa hausikii unaweza kusema naamini sisikii?
Je, visivyoingia kwenye context ya imani una maana ni vile vinavyoonekana kwa macho tu?
Kote majibu yapo ila hapo kwenye kiziwi ni kazi kumuuliza!
 
Kuna maswali mengi kuhusu Mungu huwa najiuliza, mpaka SAA nyingine huwa namkasirikia Mungu (maybe nakufuru lakini acha iwe hivyo).Bcoz kwa ninavomuwazia Mungu ingekuwa ni heri nisingezaliwa.

1) Kama kweli Mungu ni upendo, kwanini aumbe jehanamu ya kutuchoma milele sisi tulio waovu (lyk for billions and trillions of years). Si heri angetumaliza tu kuliko kututesa milele? Kwenye shuhuda nyingine wakristo huenda motoni kwa dhambi moja tu ambayo hawakutubu. (I know hell was originally intended for the devil and his demons & not 4 humans)

2) Kwanini alimruhusu shetani kumjaribu Adam ikiwa alijua kuwa wanadamu wengi tutateseka duniani, tutaanguka maovuni, na atatutupa Jehanamu?

3) Kama Mungu anatuambia tukitenda dhambi na tusipomtii tutachomwa motoni, Je wakristo na waislamu (baadhi yetu) tutakuwa tunamtumikia Mungu kwasababu tunampenda na tunataka kumjua zaidi? au tutakuwa tunamtumikia kwasababu tunaogopa kwenda Jehanamu?

4) Mungu husema mawazo yake si kama ya kwetu, na njia zake zipo juu zaidi, nakubaliana na hilo. Maybe kutuchoma motoni it's in his nature, that's the way He is and we have to live with it.

5)All in all Mungu ana hekima kuliko mimi, coz ni muumba wa kila kitu. Maybe katika hekima yake yote, hii ndo decision bora aliokuja nayo. Labda ana reason nzuri behind all this ambayo mm siijui. Maybe Mungu mwenyewe akinijibu face 2 face, nitabadili mtazamo wangu kuhusu yeye.

6) Kingine kinachonikasirisha pia ni yeye kuruhusu mimi kuja hapa duniani, naona ni heri nguvu aliotumia kuniumba mimi angetumia kufanya kitu kingine, nachukia + najuta kuwa hapa duniani to see all this, dunia imejaa waovu (mm nikiwa mmoja wapo) pamoja na mateso ya kila namna.

Haya ndo mawazo yangu nimeamua ku-share nanyi, najua hata povu linitoke vipi it won't change the facts. Samahani kwa ntakaekuwa nimewakwaza humu jukwaani, naamini Mungu alishayajua mawazo yangu kuhusu yeye toka kitambo. So im just keeping it real.
kabla ya kumlaumu MUNGU ni vyema ukamshukuru hata kwa akili,maarifa ,uzima, utashi, ufahamu n.k alivyokujalia vinavyokupa kibuli, jeuri ghazabu, chuki n.k. Si kila mwanadamu ana akili/ufahamu/utashi/ufahamu n.k kama zako je wewe ungekuwa kama wao ingekuwaje. yako maswali ambayo sisi binadamu tunajiuliza lakini majibu sahihi hatuna nipo tunafikia kusema mwacheni MUNGU aitwe MUNGU. jaribu kuwaza sisimizi mdogo au mdudu yeyote mdogo anavyohangaika huku na kule lakini kwa kidole chako tu unakatisha maisha yake ndiyo sisi tulivyo kwa MUNGU ni kama sisimizi tu sisi ni kitu kidogo sana kwake. akili/maarifa utashi/ufahamu uzima yeye ndiyo ametupa au kutujaalia vivyo ni vyema tukavitumia vizuri mwisho Nenda kwa watumishi wa MUNGU utapata msaada/majibu ya maswali yako.
 
Huwezi kumpenda Mungu wakati humpendi Binadamu mwenzako unayemwona kwa macho yako mawili.
Kama ungekuwa na Upendo japo kidogo tu basi ungemjua Mungu aliyekuumba.
Maana Mungu ni Upendo.
Watu wasiompenda au kumjua Mungu aliyewaumba ni watu wakatili sana.
Hawaogopi chochote, hawamwogopi yeyote.

Sisi tunawaangalia tu, ila iko siku mtaujua Ukweli na kumrudia Mungu kama yule Mzee wa chama, ambaye Mauti yalimwonyesha Mungu alipo na akatubu.
Kama hutapata bahati ya kumjua Mungu hadi Kifo chako basi una bahati mbaya sana.
Mungu yupo na anakupenda ndio maana alikuumba ukiwa na sura nzuri na afya njema, bila kulipia chochote.

Wewe umpende au usimpende ni shauri yako, kwani kuna mabilioni ya watu wanampenda Mungu.
 
na kweli acha tu umchukie maana mpka hapo tu we ni wa jikoni hta kabla hujafa nyumbani kwako ni jahanam fill nar
 
Hata hujui maana ya kumchukia Mungu!!....Kumchukia Mungu maana yake ni kutenda maovu na kwenda kinyume na upendo!....Kama unatenda mema na kupenda wengine automatic unampenda Mungu!
 
Baadhi ya Watu wakipata chakula wakala wakashiba, basi hapo wameshakuwa wajanja.
wanabaki kutamba tu na kusema hawamjui au wanamchukia Mungu.
Wengi wao ni watoto wenye wazazi wanaojitoshereza kimapato.
Sisi tuliopitia maisha magumu tumeuona Mkono wa Mungu ukituokoa mara nyingi tu.
Tuliposhindwa kwenda kutibiwa kwenye hospitali za ghalama, kutokana na magonjwa sugu, Mungu aliingilia kati na kutuponya.
Tulipokosa chakula, Mungu alitulisha vyakula vya jalalani na hatukuugua matumbo.
Tulipofiwa na wazazi, Mungu alitulea mitaani hadi tukakua na kujitegemea maisha.
Tulipoonewa Mungu alitulinda na kupata haki yetu.
Tulipotaka kuuwawa na wenye nguvu, Mungu alizuia risasi zisitudhuru mwilini.
Tulipokosa mavazi na kutembea matako yakionekana, Mungu alituficha na uso wa aibu, tulienda shule hivyohivyo hadi tukahitimu na kufaulu.
Nakadhika nakadhalika nakadhalika nakadhalika.
Leo hii tunashuhudia kuwa Bila Upendo wa Mungu, sisi tusingekuwepo hapa tukiandika mada hizi.
Ni upendo wa Mungu uliotufikisha hapa tulipo.
Hongereni wenzetu ambao mlikuwa na nguvu ya kupata mahitaji yenu yoote kwa Pesa za wazazi wenu. Kwa vyeo vya walezi wenu.
Kwenu Mungu hana maana, hayupo, hana mchango wowote, sio chochote na mnasema kwa sasa mnamchukia.
Mnanguvu nyingi, mnajitegemea, mnajiweza kwa lolote.
Sisi bila Mungu hatuwezi chochote, hata kuamka asubuhi tunamtegemea Mungu, hata kutembea, hata kufumbua macho hatuwezi bila yeye kutupa nguvu.
Kwenu wenye nguvu Hakuna Mungu, kwetu sisi wanyonge Mungu yupo na ndio tegemeo letu.
Tunampenda sana sana sana, tunampenda mara Zilioni.
Asante Mungu kwa Upendo wako usio na mipaka, kwa kuwapenda watu wote, hata hao wanaosema wanakuchukia.
 
Wooow this is it...mkuu umemaliza kitu...May Alah bless you for the wisdom and truth...thank you very much kwa kuniwaikilisha kimawazo
 
Itakuwa umeanza kuwakosea wazazi wako kwanza then unamlalamikia Mungu. Hayo yote uliyonayo hukuyapata tu umeyatengeneza mwenyewe.
 
pole saana...najus si kosa lako n shetan aliyekutawla hapo ehehee
 
Hayo maswali yote majibu yake yanspatikana tena kwa urahis mno kuwa na Bible kisha mtafute mchungaji yeyote wa kanisa LA wokovu atakujibu tena sio lazima pastor hata mwamini wa kawaida anae lijua neno atakufafanulia jambo LA msingi hutakiwi kuwa na papara mambo ya kiroho hayahitaji reasoning za kisomisomi lakini ukitulia yanamake sense
 
( رَّبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ فَاتَّخِذْهُ وَكِيلًا )

المزمل (9) Al-Muzzammil

Mola Mlezi wa mashariki na magharibi, hapana mungu isipo kuwa Yeye, basi mfanye kuwa Mtegemewa wako.
 
Je wa Africa tulikua na imani kabla ya Toleo hili la pili la kiimamani? Kama jibu ni ndio ni Wazi kua tulikua na MUNGU wetu. Wengi wanafikili kwamba Ukoroni ulikuja kuchukua, madini, pembe za Ndovu na kadhalika... Kumbe Mzungu alikuja "kupola... Kila kitu... Madini yetu Imani zetu..kuvuruga tamaduni zetu... Wao wanawafinyanga watoto wao kitawala Dunia.. Sisi Ufalme wa Bwelele Mbinguni ooo My God... Niishie hapa, kataa ukibwetele.
 
Usilaumu yeye kukuleta duniani. Mlaumu kwa kuruhusu uzaliwe ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom