Sababu zinazonifanya nisimpende Mungu

Mungu angetak kukuangamiza haitachukua hata sekunde,kuna sabab upo hai,..maumiv unayopitia mpaka umkufulu ivi yote yanakupeleka uko unakotakiwa ufike,kua na imani na tubu dhambi zako,Mungu atakuongoza,coz ni upendo,..jitaidi uwe MTU wa sala sana zitakusaidia
Mtoa mada nina imani mungu amefurahishwa nae tena sana

Mbna mnamfanya mungu katili hivyo??mtoa mada anashindwa kumwabudu mungu bila unafiki...mpeni msaada si kumtishia hivyo...wapi amekufuru au kukufuru ni nini??

jw library
 
Mkuu,
Mwenyezimungu asingeweza kukuchoma jehanam bila ya kukuleta duniani kwanza. Cha kwanza alipokuleta akakupa akili na uwezo wa kupambanua zuri na baya,haki na batili. Akaleta mitume yake duniani yote ikiwa na lengo moja la kuwaelekeza watu wamjue yeye aliyewaleta na wamwabudu. Kuna mambo mengi ambayo ni miujiza tosha iliyopo mbele ya macho yako bila hata ya kusafiri useme nauli sina kama na Mimi ningeenda ulaya kuona ushahidi wa uwepo wa mungu. Mwenyezimungu amekupatia kila kitu afya,pumzi na ukiugua kwa uwezo wake utapona.
Mtake msamaha mungu kaa chini waone watu wenye elimu ya dini ya kutosha watakutosheleza kwa majibu ya maswali yako badala ya kukaa na maswali bila ya kuhangaika kwa makusudi ili uweze kuelewa wema wa Mungu.
Nakuombea kwa Mungu upate kumjua na kuondoa mawazo hasi juu yake.
Mkuu
Mungu hana mpango na kumtesa mtu milele,wala kumjaribu mtu kwa jambo ovu,maana yeye hamjaribu mtu kwa ovu maana ni mtakatifu...

Ukisema tupo hapa ili tupimwe akili,,si kweli,kwani yeye hazijui akili zetu si alituumba

Narudia mungu ci katili

jw library
 
Wafu wako katika hali gani?

JIBU LA BIBLIA: “Walio hai wanajua kwamba watakufa; lakini wafu, hawajui lolote kamwe, wala hawana malipo tena, kwa maana kumbukumbu lao limesahauliwa. Yote ambayo mkono wako unapata kufanya, yafanye kwa nguvu zako zote, kwa maana hakuna kazi, wala utungaji wala ujuzi wala hekima katika Kaburi, mahali unapokwenda.”*—Mhubiri 9:5, 10.

Kwa ufupi, Kaburi, ni mahali ambapo wanadamu huenda wanapokufa; na ni mahali pa mfano au hali ya kutotenda. Mwanamume mwaminifu Ayubu alielewa nini kuhusu Kaburi? Alipoteza mali zake zote na watoto wake wote kwa siku moja, na kupigwa na majipu yenye maumivu makali mwilini. Ayubu alimsihi Mungu hivi: “Laiti ungenificha katika Kaburi [“motoni,” kulingana na Biblia ya Douay Version ya Wakatoliki], kwamba ungenificha.” (Ayubu 1:13-19; 2:7; 14:13) Ni wazi kwamba, Ayubu alijua kwamba Kaburi si mahali penye moto wa mateso, ambapo angeenda kuteseka zaidi. Badala yake, alipaona kuwa mahali ambapo angepata kitulizo.
Mkuu
Shukran,

jw library
 
Bado una nafasi ya kuitafuta kweli zaidi.. Hujachelewa ila nnamini ipo siku utalia na Kuomba MUNGU akusaidie.. Ikiwa umeamka salama, smart phone mkononi na una afya njema kabisa na pengine una uhakika wa kula au kufanya chochote utakuwa na mawazo hayo.. Ni ulevi tu ulevi wa kipuudhi kabisa kujiona kuwa we ni zaidi ya wengi wanaoamini, ndio ulevi huo utakufanya uwaite wafia dini au jina lolote lile wale wanaoamini... Ila ipo siku na mda kwa mdomo wako na akili yako utamuita sana MUNGU walau ajidhihirishe kwako hta kwa dk moja.. Utakuwa pia umezungukwa na watu huku wakibubujikwa na machozi na dua zao zote zikielekezwa kwa MUNGU.. Hautakuwa na smartphone yako wala huku JF hawatojua kuwa unaexist tena ila itakuwa ni kati yako wewe na MUNGU wako... Sina neno sahihi la kukuelezea.. Lakini walau nimeweza ili kutimiza wajibu wangu kama mwanadam tu.. Kwaheri na MUNGU akubariki
Mungu wa vitisho

jw library
 
Mungu hayupo so point zako ni invalid.

Kama yupo basi anavyosema ni mwenye rehema na upendo kuliko binadamu yeyote anatudanganya maana angekua nao dunia isingekua kwenye mess hii.

Ana paradox nyingi mno kiasi kwamba his own existence can't be possible in anyway. Anasema anajua yote yatakayokuja na yaliyokuwepo,hehe meaning story ya adam n eve ka ni kweli then anamlaumu eve bure tu maana yeye alijua wazi watakachokifanya na bado akaweka mti pale, kosa ni la kwake 100% ni sawa na mzazi kujua mtoto ukimpa wembe atajikata alafu unampa then anajikata unamtupia lawama na kumuongezea adhabu juu.

Siku nilipoachana na fix za dini akili ilifunguka, kuishi kwa uoga uoga tena hakuna, mtoto ukimjaza kitu utotoni anakishika kama kilivyo, acheni watoto wenu wakue then wachague, hamtobaki na mtu anayeamimi haya maduduwasha
Mkuu
Muumba yupo tena sana...ila viongozi wanamchafua sanaa

jw library
 
Kuna maswali mengi kuhusu Mungu huwa najiuliza, mpaka SAA nyingine huwa namkasirikia Mungu (maybe nakufuru lakini acha iwe hivyo).Bcoz kwa ninavomuwazia Mungu ingekuwa ni heri nisingezaliwa.

1) Kama kweli Mungu ni upendo, kwanini aumbe jehanamu ya kutuchoma milele sisi tulio waovu (lyk for billions and trillions of years). Si heri angetumaliza tu kuliko kututesa milele? Kwenye shuhuda nyingine wakristo huenda motoni kwa dhambi moja tu ambayo hawakutubu. (I know hell was originally intended for the devil and his demons & not 4 humans)

2) Kwanini alimruhusu shetani kumjaribu Adam ikiwa alijua kuwa wanadamu wengi tutateseka duniani, tutaanguka maovuni, na atatutupa Jehanamu?

3) Kama Mungu anatuambia tukitenda dhambi na tusipomtii tutachomwa motoni, Je wakristo na waislamu (baadhi yetu) tutakuwa tunamtumikia Mungu kwasababu tunampenda na tunataka kumjua zaidi? au tutakuwa tunamtumikia kwasababu tunaogopa kwenda Jehanamu?

4) Mungu husema mawazo yake si kama ya kwetu, na njia zake zipo juu zaidi, nakubaliana na hilo. Maybe kutuchoma motoni it's in his nature, that's the way He is and we have to live with it.

5)All in all Mungu ana hekima kuliko mimi, coz ni muumba wa kila kitu. Maybe katika hekima yake yote, hii ndo decision bora aliokuja nayo. Labda ana reason nzuri behind all this ambayo mm siijui. Maybe Mungu mwenyewe akinijibu face 2 face, nitabadili mtazamo wangu kuhusu yeye.

6) Kingine kinachonikasirisha pia ni yeye kuruhusu mimi kuja hapa duniani, naona ni heri nguvu aliotumia kuniumba mimi angetumia kufanya kitu kingine, nachukia + najuta kuwa hapa duniani to see all this, dunia imejaa waovu (mm nikiwa mmoja wapo) pamoja na mateso ya kila namna.

Haya ndo mawazo yangu nimeamua ku-share nanyi, najua hata povu linitoke vipi it won't change the facts. Samahani kwa ntakaekuwa nimewakwaza humu jukwaani, naamini Mungu alishayajua mawazo yangu kuhusu yeye toka kitambo. So im just keeping it real.
Hii ni hatari sana yaani unamchukia Muumba wa mbingu na nchi usiye muona wala kumjua,,je vipi kuhusu binadam wakaribu unawachukia kwa kiwango gani...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo sahihi mkuu
Ni hakika hukumu ipo,mungu atawaondoa waovu katika kifo cha milele...watakuwa majivu yaani watateketea milele,kumbukumbu yao itasahaulika kabisa milele yote

Lakini si moto wa milele,yaan mateso ya milele katika jehanamu..

jw library
Mara unasema Mungu sio katili Mara tena unakubali kuwa watu watapewa mateso ya milele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reasoning ni part and parcel ya maisha yetu.....kila kitu kinachowezekana ni haki kuhojiwa kama hakijulikani hatuwezi kutumia hisia kukielezea.... hisia siku zote haina usahihi.

Mfano: kandambili au kiatu kikigeuka juu chini, inasemekana ni vibaya kwani ni sawa na kumkanyaga Mungu.... so wapo wanaoamini hivyo mpaka leo na ni watu wazima wenye akili zao ila kwangu haimake sense hata kidogo.

Post sent using JamiiForums mobile app
Kwahiyo wewe kwenye maisha yako hakuna jambo lolote la imani yani huna unachoamini?
 
Una maswali mazuri mkuu hasa hiyo qoute ulioiatach chini ni kweli lazma tujiulize maswali mengi kuhusu Mungu ila mkuu usiache kuabudu vile ulivyoelekezwa na Wazazi wako we endelea kuabudu na kuendelea kujiuliza maswali ipo siku utaujua ukweli
 
Una maswali mazuri mkuu hasa hiyo qoute ulioiatach chini ni kweli lazma tujiulize maswali mengi kuhusu Mungu ila mkuu usiache kuabudu vile ulivyoelekezwa na Wazazi wako we endelea kuabudu na kuendelea kujiuliza maswali ipo siku utaujua ukweli
Asante
 
Amini Mungu yupo.Amini hivyo kwani ndio ukweli.Mfano.
Kama Nyumba lazima awepo mjenzi.Ndivyo ilivyo kwa Dunia Na sayari zingine .
Mjenzi yupo naye ni Mungu.Leo Kesho Na milele.
 
Kwanz nianze na haya ndug mtoa mada:
1. unaamini uwepo wa uchawi/ushirikina/majini au waganga kuwa wanatibu?? Kam n YES...MUNGU yupo tena sanaaaa...Kam n NO ila weng huwamini shirik bas pia MUNGU yupoaaa kwel kwel
2.Ukitak kuijua dini vizur husifuate DHEHEBU wala DINI ila tafuta KWELI
3.Dini wala c kaz nzito/mzigo fulan mzito ila watekelezaj wake ndio huleta UGUMU mzito
4.Najua waamin SAYANSI na vingine ving tu vya NEWTON,GALILEO,DARWIN...waamin ila c vyote wavijua bali wafaham tu
5.Tafuta asili ya mwanadam...SAYANS au DINI kuna kimoja kitakujibu tu
6.Ishara unazo nying ktk mwili wako ambapo hakuitaji kuelezwa bali ww wajua kuwa kaz ya MUNGU hakuna awezaye
UKWELI NI KWAMBA MUNGU YUPO ILA MUNGU WA KWELI HAPATIKANI KWENYE QURANI WALA BIBLIA.
 
Amini Mungu yupo.Amini hivyo kwani ndio ukweli.Mfano.
Kama Nyumba lazima awepo mjenzi.Ndivyo ilivyo kwa Dunia Na sayari zingine .
Mjenzi yupo naye ni Mungu.Leo Kesho Na milele.
Huyo mjenzi alitoka wapi bila kuwepo mzazi wake
 
Back
Top Bottom