Mkuu
Synthesizer Unaposema YESU alipaa mbinguni baada ya Siku 40 una maanisha ahadi aliompa yule mwizi ilikuwa ya uwongo?? Nilichotaka uone ni kwamba yule mwizi pale msalabani walimuua pia na akazikwa lakini YESU aliondoka nae na hakuondoka na mwili wake,,,Kuna andiko linasema Je! Hamjui miili yenu ni hekalu la Roho mtakatifu?!# MIILI yenu/+/=# kuna wewe na mwili wako??? Mwili wako(wewe)
Hapana Mkuu, Yesu hata siku moja hakusema uongo, na wala hakusema uwongo kwa yule mwizi. Na wala hakusema uongo aliposema siku inakuja wale waliomo makaburini (wafu) wataisikia sauti yake na kutoka. Nilichotaka kukuonyesha ni kwamba usomaji wa maandiko bila kuwa makini unaweza kufanya upotoke sana katika kuelewa jambo.
Angalia sentensi mbili hapa chini uniambie ni ipi Yesu alitamka kwa yule mwizi. Angalia sentensi hizi zina maneno sawa kabisa;
1. Amini nakuambia, leo hii utakuwa nami peponi.
2. Amini nakuambia leo hii, utakuwa nami peponi.
Umegundua kitu? Sasa niambie, ni sentensi ipi kati ya hizo mbili Yesu aliitoa kwa yule mwizi?
Ili kuzidisha uthibitisho wa umuhimu wa kusoma na kutafsiri vizuri, maana kutafsiri mara nyingine ndio kinakuwa chanzo cha tatizo, angalia tena sentensi zifuatazo ambazo pia zina maneno sawa;
1. A woman without her man is nothing
2. A woman, without her, man is nothing
Umegundua tena taswira mbili zinazotolewa na hizo sentensi hapo juu?
Basi kwa kusikitisha sana, vitu kama hivi hata vimechngia watu kuzidi kuamini Yesu na yule mwizi siku hiyo walipokufa walienda peponi (paradiso). Na wengine, baada ya kuelewa Yesu alipaa baada ya siku 40, hata wamedhani alitoa ahadi ya uwongo kwa yule mwizi.
Hata hivyo, haimaanishi kwamba Yesu alikwenda mbinguni na yule mwizi baada ya siku 40. Kumbuka Yesu aliahidi "utakuwa nami peponi" kama kitu cha baadaye. Sasa suala la msingi, ni lini yule mwizi alikuja kuwa au atakuwa na Yesu peponi?
Na huwezi kutofautisha mwili na roho katika kupata thawabu ya uzima wa milele au mshahara wa dhambi, kifo. Suala la miili ya damu na nyama linategemea tu makazi yako ni wapi. Ukiwa duniani basi inabidi uwe na mwili wa nyama, na ukiwa na makazi mbinguni utakuwa na mwili wa roho. Angalia Yesu, alikuwa mbinguni akiwa na mwili wa roho, akaja duniani akazaliwa katika mwili wa nyama, akarudi mbinguni akiwa na mwili wa roho. Sasa haina maana katika hizi awamu tatu Yesu alikuwa ni mtu tofauti - alikuwa ni Yesu yule yule, kuonyesha kwamba hii theory ya watu kusema sijui roho inatoka mwili unabaki si ya kweli. Ni mambo mawili - aidha una mwili huu au ule. Sio kwamba inaunganishwa au kutenganishwa. Unakuwa na one form or the other, lakini ni mtu yule yule. Kuna watu walifufuliwa toka mwili wa nyama kurudi mwili wa nyama - mfano Lazaro. Na kuna watu wanafufuliwa toka mwili wa nyama kwenda mwili wa roho - mfano Yesu.
Ila Biblia inasema kwamba Mungu anaweza kukubadilisha kwa kufumba na kufumbua kutoka mwili mmoja kuwa mwingine. Alimdadilisha Yesu toka mwili wa roho kuwa wa nyama kama kiini katika tumbo la Maria. Note kwamba alimbadilisha, hakumuua. Ila katika hali ya kawaida, lazima kifo kitokee ili ubadilike ikiwa unatakiwa ufufuliwe ili ukaishi mbinguni. Ila ikiwa unatakiwa ufufuliwe uishi duniani basi utakufa katika mwili wa nyama na kufufuliwa katika mwili wa nyama - ukiwa na utu wako ule ule. Na kumbuka, whether ni kutoka mwili wa nyama kwenda wa roho au wa nyama tena, katika hali ya kawaida, lazima ufufuo utokee, sio kitendo ambacho ni automatic kwa mtu yeyote anaekufa. Kama wewe sio mtu wa kufufuliwa ukifa ndio basi tena, huendi tena kwenye mwili wa nyama au roho. Ingekuwa kupata mwili wa roho ni automatic mara tu ukifa, basi Yesu asingesubiri siku tatu ili afufuliwe, angekuwa na mwili wa roho mara tu baada ya kufa pale pale alipotundikwa!