SoC02 Sababu za kasi ndogo ya maendeleoya nchi nchini Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Philosopher 122

New Member
Sep 8, 2022
2
1
images (2).jpeg
download.jpeg

Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye utajiri wa asili mkubwa duniani, lakini pamoja na kuwa na utajiri huo kasi ya maendeleo ya nchi ni ndogo sana ukilinganisha na rasilimali tulizonazo .

Nini chanzo cha hayo yote?1.Kukosekana kwa dira ya taifa.

Maendeleo yanahitaji dira kuu ya Taifa ili kufikia lengo la kuisogeza nchi mbele kimaendeleo kama alivyowahi kusema mbunge wa kawe ndugu Josphat Gwajima kuwa " Lazima kuwe na dira ya Taifa ambayo inaelekeza nini kifanyike ili tuweze kuendelea kama taifa".

Kila kiongozi wa nchi anayeingia madarakani huwa na vipaumbele vyake kuhusu nchi hali ambayo husababisha kutokamilika kwa baadhi ya mipango yenye kuleta maendeleo iliyopangwa na viongozi waliotangulia kushika madaraka.

Tanzania tumepitia sera tofauti tofauti kuanzia enzi za mwalimu Nyerere na "ujamaa na kujitegemea "mpaka wakati huu wa "kazi iendelee" ya Mama Samia Suluhu Hassan, ambapo sera kama za "ubinafsishaji "na mzee Makala pamoja na "Tanzania ya viwanda" hazina nafasi tena katika uongozi uliopo kwani kila awamu ina vipaumbele vyake.

Halii hii ya kukosa dira ya taifa inasababisha matumizi makubwa ya fedha kwa ajili ya uwekezaji ambao baadae hautiliwi maanani sana.
 
Back
Top Bottom