Je, unamfahamu Kajala Masanja?

Status
Not open for further replies.

Nobunaga

JF-Expert Member
Mar 22, 2019
1,169
4,985
KAJALA MASANJA: KUZAMA KUZIMU NA KUIBUKA TENA KILELENI.
IMG_20221014_122531.jpg

Moja ya wanawake wanaopaswa kupigiwa mfano kwa aina ya maisha ya ajabu sana ambayo ameyapitia basi ni mwanadada Kajala Masanja. Misukosuko, changamoto, makosa aliyoyafanya na hatimaye leo hii kuweza kuibuka kuwa moja ya wanawake maarufu anayehusudiwa na wanawake wengi wakubwa kwa wadogo, ni stori halisi ya maisha yenye kusisimua.

Winniefrida Kajala Masanja amezaliwa mwaka 1982 katika familia ya maisha ya kawaida sana kwenye kota za polisi Oysterbay. Baba yake na Mama yake wote wawili walikuwa ni maaskari polisi.
IMG_20221014_121808.jpg


Akapata elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Mbuyuni iliyoko pale pale maeneo ya Oysterbay na baadae akachaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule ya Iringa Girls. Hata hivyo alipomaliza tu kidato cha kwanza Kajala akawapa shinikizo wazazi wake wamuhamishe shule akijieleza kwamba anashindwa kuhimili hali ya hewa ya baridi kali la mkoani Iringa.

Wazazi wake wakakubaliana naye na kumtafutia nafasi shule ya Sekondari ya Jitegemee. Kajala akatakiwa kurudia tena kidato cha kwanza ili aweze kupata nafasi ya kusoma shuleni hapo. Kwa hiyo shule zilipofunguliwa, Kajala akaanza upya kidato cha kwanza hapo Jitegemee.

Hiki kitendo cha Kajala kuhamishiwa shule ya Jitegemee lilikuwa ni kosa kubwa sana ambalo wazazi wake walikuwa wamelifanya. Sababu ndani ya muda mfupi tu baada ya Kajala kuanza masomo hapo Sekondari ya Jitegemee mwenendo wake kitabia ulibadilika vibaya mno.
IMG_20221014_121747.jpg


Hapo shuleni Kajala akapata 'mashosti ambao ni watoto wa mjini na kumuingiza Kajala kwenye aina ya maisha ya hatari sana. Kajala na marafiki zake shule kwao haikuwa kipaumbele badala yake waligeuka kuwa wasichana wadogo wanaopenda starehe kupindukia.

Kajala na wenzake walikuwa na uwezo wa kutohudhuria shule hata mwezi mzima.. wanatoka nyumbani vizuri kila siku wakijifanya kama wanaenda shule lakini wanaishia mtaani na kwenda kwenye misele yao.

Kajala na wenzake ilikuwa hauwezi kuwakosa kwenye tukio lolote muhimu la starehe hapa mjini. Iwe ni show ya msani, klabu, matamasha na sehemu zote za starehe, Kajala na wenzake, wasichana wadogo wa kidato cha kwanza lakini lazima utawakuta.
IMG_20221014_131247.jpg


Kutokana na utoro wa shule na tabia zao, wazazi wao walIkuwa wanaitwa mara kwa mara shuleni kuonywa kuhusu mwenendo mbaya wa watoto wao. Kitendo hiki kilisababisha kuharibu sana uhusiano kati ya Kajala na wazazi wake.

Wazazi wake wote walikuwa ni polisi, kwa hivyo utemi walikuwa wanaujua haswa. Wakaanza kumuwekea masharti makali ya kuishi nyumbani. Kajala akawa haruhusiwi kutoka nyumbani isipokuwa kwenda shule tu. Na akirudi shule haruhusiwi kutoka nyumbani kwenda popote pale.

Kitendo hiki cha wazazi kumbana Kajala hakikusaidia badala yake kilimfanya Kajala kuwa mtukutu zaidi. Kajala akaanza tabia akiondoka nyumbani kwenda shule anaweza kupotea hata wiki nzima inakatika bila kurudi nyumbani na hajulikani alipo. Kajala na marafiki zake walifikia hatua mpaka wanapanga chumba mahala na wanaishi pamoja hata watu kumi. Kwenye kipindi hiki Kajala ndio alikuwa amecharuka kweli kweli.
IMG_20221014_131315.jpg


Akajifunza kunywa pombe na akafikia hatua mpaka ya kuchora tattoo mwilini. Kama ukimwangalia Kajala kwenye titi lake la kushoto ana tattoo ambayo kama ni mzoefu utagundua imechorwa kienyeji. Hii tattoo Kajala aliichora kipindi hicho yuko sekondari na alichorwa maeneo ya Temeke enzi hizo walikuwa wanatoa huduma ya kuchora tattoo kwa njia ya kizamani kama unatona kwa sindano ya mkono.
IMG_20221014_121941.jpg


Japokuwa alikuwa ni msichana mdogo wa sekondari lakini kipindi hicho hakuna klabu hapa mjini ulikuwa unaweza kwenda ambayo hawakuwa wakimjua Kajala. Pale Billcanas enzi hizo palikuwa ni kama nyumbani kwake. Mji mzima wa Dar es Salaam ulikuwa ni wa kwake. Huu ukanda wa maeneo ya Kinondoni, Oysterbay, Mikocheni, Msasani mpaka Masaki Kajala alikuwa anajulikana vyema sana na matukio yake. Hakuwa msanii wa muziki wala hakuwa mwigizaji, Kajala alikuwa anajulikana kwa kuwa binti.

Kipindi ameingia kidato cha pili, Kajala akawa dancer kwenye maklabu ya usiku. Hapa Kinondoni zamani kulikuwa na Klabu inaitwa 'Club Asset' na mara nyingi Kajala hapa ndio alikuwa anafanyia kazi yake kama dancer japo baadae alikuwa dancer kwenye klabu nyingine nyingi hapa mjini.
IMG_20221014_131356.jpg


Katika hizi shughuli zake za kuwa dancer kwenye sehemu za starehe ndio kwa mara ya kwanza mtayarishaji wa muziki P-Funk Majani alimuona Kajala na kuvutiwa naye na Kuanza kufanya juhudi za kumpata.

Kajala sio tu kwamba alikuwa mapepe bali pia alikuwa ni mrembo kweli kweli. Hii shepu unayoiona anayo sasa hivi kipindi icho ndiyo ilikuwa hatari haswa. Binti alikuwa na sura, alikuwa na shepu, alikuwa mtoto wa mjini. Akipita sehemu kunazizima na vijana shingo zinakaribia kukatika kwa kumtazama. Enzi za usichana wake, Kajala alikuwa ni tafsiri sahihi ya binti mrembo aliyejaaliwa kila kitu.

Kipindi hicho Kajala alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na jamaa anaitwa 'Mudi Masta'. Huyu jamaa ni kaka wa damu kabisa wa msanii TID. Kitendo cha P-Funk kuanza kumtongoza Kajala kilifanya kutokea kwa bifu kubwa sana kati ya Kaka yake TID, TID mwenyewe na P-Funk.
images (16).jpeg


Kuna siku akina TID, kaka yake na washkaji zao walikutana na P-Funk na washkaji zake usiku pale Club Billicanas. Ulitokea ugomvi mkubwa sana kati ya kundi la kina TID na washkaji wa P-Funk. Kama unakumbuka pale Billcanas kwenye milango ya kuingilia kwa juu kulikuwa na balcony kubwa sana.

Sasa hawa akina P-Funk na kundi la akina TID ugomvi ulikuwa mkubwa, kaka yake TID na P-Funk wakazichapa kutoka ndani ya klabu mpaka wakafika juu kwenye balcony. Ilikuwa bado kidogo watupane chini toka kule juu. Ugomvi wote huu walikuwa wanamgombea mrembo Kajala, msichana wa kidato cha pili shule ya Sekondari Jitegemee.

Hata baada ya ugomvi huu, P-Funk hakuacha kumtongoza Kajala. Alitumia nguvu nyingi sana na hela mpaka kumtoa Kajala kwa kaka yake TID na hatimaye kummiliki. Kipindi walipoanza mapenzi yao, P-Funk alimchukua Kajala na kumfungia nyumbani kwao Masaki kwa muda wa karibia wiki mbili wakila raha.
images (17).jpeg


Shuleni Jitegemee walimu wanamtafuta Kajala kwa wiki mbili alikuwa hajahudhuria shule. Nyumbani kwao wazazi hawajui mtoto wao yuko wapi. Ilifika muda kulikuwa na difenda ya polisi ilikuwa inazunguka kumtafuta Kajala kwa marafiki zake na kumbi za starehe ambazo alikuwa anajulikana kupenda kuhudhuria. Kajala alikuwa anatafutwa kila kona ya jiji na wazazi wake hajulikani yuko wapi, wakati huo binti yuko Masaki nyumbani kwa akina P-Funk akila raha.

Kuna siku Kajala akamuomba P-Funk ampeleke kwao kuna vitu kadhaa pamoja na nguo zake akachukue. Majani akachukua gari ya mama yake na wakaondoka mpaka kota za polisi Oysterbay nyumbani kwa akina Kajala. Wao walikuwa hawajui kwamba Kajala alikuwa anatafutwa kila kona ya jiji na polisi. Kwa hiyo Polisi wa Oysterbay walipowaona tu maeneo yale, wakawakamata wote wawili na kuwaweka mahabusu wote, Kajala na boyfriend wake mpya P-Funk.
IMG_20221014_131955.jpg


Wazazi wa Kajala walipopata taarifa toka kwa polisi wenzao kwamba Kajala ameonekana na kijana chotara wa kizungu na wamewakamata na wako mahabusu, wazazi wa Kajala wakapiga msumari zaidi kwamba wawili hao wasiachiliwe badala yake walale mahabusu huko huko.

Kesho yake ndio mama yake P-Funk akasikia kwamba mwanaye amelazwa mahabusu polisi Oysterbay na ndio akaenda kumtoa mwanaye na Kajala. Baada ya kuwatoa mahabusu, Mama yake P-Funk na wazazi wa Kajala wakafanya kikao cha kuwaonya watoto wao kuhusu hicho kilichotokea kwa P-Funk kumtorosha mwanafunzi wa kidato cha pili kwa muda wa wiki mbili.

Ubaya ni kwamba japokuwa P-Funk alikuwa amemchukua Kajala na kukaa naye kwao kwa muda wa wiki mbili lakini mama yake hakuwa anajua kwamba P-Funk anaishi na mwanamke hapo kwao.
IMG_20221014_132202.jpg


Wasanii wengi wanapafahamu nyumbani kwa kina P-Funk pale Oysterbay. Ndani ya uzio kuna nyumba kubwa ambayo ndio anaishi mama yake na ndugu zake wengine, halafu kuna nyumba ndogo kwa pembeni kama 'servants quarters' hivi ambapo nyumba hiyo ndogo ndio alikuwa anakaa P-Funk na studio yake ya kurekodi mziki ilikuwa humo humo. Kwenye hicho kinyumba kidogo anachokaa P-Funk na kwenye studio yake huko ndiko alikuwa amemfungia Kajala kwa wiki mbili nzima.

Baada ya wazazi kusuluhisha,P-Funk na mama yake wakaondoka na Kajala akarudi kwao. Lakini kama wiki moja tu nyingine Kajala akatoroka tena na kwenda nyumbani kwa kina P-Funk na kukaa siku kadhaa. Safari hii wazazi wake wakanyoosha mikono juu na kukubali kwamba wamemshindwa mtoto wao na tabia zake. Wakawa kama wamemsusa kabisa.

Ndio Kajala na P-Funk wakaanza kuishi pamoja na Kajala akaacha kabisa shule. Na wazazi wake wakakata kabisa mawasiliano naye, wakam-disown kabisa. Hata Kajala alipopata ujauzito wa mtoto wake Paula kwa miezi yote tisa hakukuwa na ndugu yeyote wala mama yake mzazi ambaye alikwenda kumuona. Na alipojifungua zilipita kama wiki mbili hivi ndipo mama yake akakunjua moyo na kwenda kumuona mjukuu wake.
IMG_20221014_132325.jpg


Kwa muda wa miaka tisa P-Funk na Kajala waliishi pamoja. Ukimuuliza mtu yeyote anaye wajua watu hawa wawili atakuambia kwamba P-Funk licha ya kutoka na wanawake wengi sana hapa mjini lakini hajawahi kumpenda mwanamke yeyote kufikia kiwango ambacho alimpenda Kajala. Upendo wake huo ulimfanya P-Funk kuwa na wivu kupindukia.

Kajala alikuwa haruhusiwi hata kutoka nyumbani. Na japokuwa P-Funk alikuwa na tuhuma za kuchepuka sana lakini ilikuwa akiona hata dalili ndogo tu ya kwamba Kajala anachepuka hata kama hakuna ushahidi wa kutosha, Kajala atashusiwa kipigo kikali sana.

P-Funk mwenyewe amewahi kukiri kwamba moja ya siku ambayo anaijutia sana ni siku ambayo alikuwa amelewa chakari na akawa anampiga Kajala, mama yake mzazi (mama yake P-Funk) akaingilia kumtetea Kajala, kutokana na ulevi P-Funk akampiga mpaka mama yake.
IMG_20221014_132414.jpg


Maisha yao ya mizozo namna hii yalidumu mpaka mwaka 2010 ambapo Kajala aliamua kuvunja mahusiano yake na P-Funk na kuamua kurudi nyumbani kwao kota za polisi Oysterbay. Kitendo hiki cha kuachana kilivuruga maisha ya wote wawili.

P-Funk licha ya kwamba alikuwa anachepuka sana na kushutumiwa kumpiga sana Kajala lakini ukweli ni kwamba bado alikuwa anampenda sana Kajala. Kitendo cha Kajala kumkimbia kilimvuruga mno P-Funk. Watu wengi hawafahamu kwamba, kitendo cha Kajala kumkimbia P-Funk ndio ilikuwa sababu kubwa iliyomfanya P-Funk aache kutengeneza mziki na apotee kabisa kwa miaka kadhaa.

P-Funk alikuwa kama amechanganyikiwa baada ya kuachwa na Kajala. Akawa mlevi sana, akazidisha bangi, akaacha kutengeneza mziki. Ni kama alidata kabisa.
IMG_20221014_122305.jpg


Juzi juzi hapa watu walikuwa wanamshangaa mdogo wetu Konde Boy namna ambavyo alikuwa analia kila siku kumuomba msamaha Kajala mpaka kumuahidi kumnunulia magari. Watu walikuwa wanahisi dogo anaigiza labda ili apate ku-trend mtandaoni. Lakini watu wanaojua historia ya Kajala hawakushangaa kabisa sababu wanajua Kajala wanaume wake wote anaoachana nao lazima wachanganyikiwe na kumlilia.

Huyu mwanamke anachowapaga wanaume zake ni siri yake anaijua mwenyewe. Lakini hakuna mwanaume ambaye amewahi kuwa kwenye mapenzi serious na Kajala halafu wakaachana na mwanaume huyo asimlilie.
IMG_20221014_122436.jpg


Kaka yake TID nusura watupane chini toka ghorofani na P-Funk pale Billicanas baada ya kupigana wakimgombea Kajala. Au waulizeni hata watu wa karibu wa msanii 'Quick Rocka' alikuwa na hali gani mara baada ya kuachana na Kajala. Fikiria legend kama P-Funk Majani, moja ya watu walioutengeneza na kuanzisha huu muziki wa Bongofleva, lakini anadata mpaka anaacha kabisa muziki sababu tu ya kuachwa na Kajala.

Kwa hiyo mdogo wenu Konde Boy mueleweni tu mkimuona amedata kwa huyu mwanamke. Siri ya mtungi aijuaye kata.
IMG_20221014_122135.jpg


Kajala naye licha ya kumkimbia P-Funk lakini bado naye alikuwa anampenda. Mwenyewe akidhania kama sehemu ya kumsahau haraka P-Funk, miezi michache tu baada ya kuachana na Majani, Kajala akaingia kwenye mahusiano na jamaa fulani anaitwa Faraji Chambo. Huyu jamaa alikuwa anafanya kazi benki ya NBC.
images (12).jpeg


Haraka haraka tu ndani ya miezi mitatu tu baada ya kuanza mahusiano, Kajala na Faraji wakatangaza kufunga ndoa. Ndoa ikapita haraka haraka na wawili hawa wakaanza kuishi pamoja kama mke na mume.

Huyu jamaa licha ya kufanya kazi benki lakini alikuwa ni "mtoto wa mjini" sana. Ukienda vijiwe vya Leaders Club au pale Break Point, huyu jamaa anafahamika vyema na watu watakupa michapo yake ya kimjini mjini. Kwa mfano, kuna mchongo mmoja uliwahi kupigwa huyu jamaa akihusika... hela ya kama milioni mia saba hivi ilipigwa halafu huyu jamaa akatumia uzoefu wake wa benki kutakatisha hicho kiasi.
images (11).jpeg


Mchongo ulianzia kwenye akaunti ya TTCL kitu kama milioni 670 na ushee ikahamishwa kwenda akaunti ya NBC ya taasisi ya TUCTA halafu ikaripotiwa hiyo hela kama imelipwa kwa ajili ya semina. Halafu ikatolewa toka akaunti ya TUCTA ikahamishwa CRDB kwenye akaunti ya kampuni inaitwa Millenium Promotions. Halafu ikatolewa CRDB ikahamishwa tena kurudi akaunti ya NBC ya kampuni nyingine inaitwa Romos Technology. Hlafu watoto wa mjini waka-withdraw hela yote. Wiki kadhaa baadae huu msala ukabumburuka wote. Ilikuwa kizaazaa kweli kweli mjini hapa.

Sasa, kipindi hicho Kajala ameolewa na mume wake walijengaga nyumba yao nzuri tu maeneo ya Salasala. Baadae hii nyumba ikahusishwa na ule mchezo wa kutakatisha hizo fedha kama milioni 700 hivi ambao mumewe alihusika. TAKUKURU wakaipiga pini ile nyumba ya akina Kajala kwamba isiuzwe, wala kupangishwa wala kuifanya chochote mpaka kesi ya mumewe iishe.
images (8).jpeg


Lakini kipindi upelelezo wa Takukuru na polisi unaendelea, mumewe alikuwa yuko nje kwa dhamana anaendelea na maisha kama kawaida.
Mambo yalipopoa kidogo, Kajala na mumewe wakatafuta mteja na kuuza ile nyumba, nyumba ambayo imewekewa zuio na serikali kwamba isiuzwe wala kupangishwa. Hapo ndio msala ukawa mkubwa, walichezea sharubu za serikali.

Mumewe Kajala alifanikiwa kukimbia kabla ya kukamatwa, lakini Kajala akakamatwa na kushikiliwa na polisi. Ubaya ni kwamba mumewe alipokimbia alikuwa hajui kama huku nyuma kwamba mkewe Kajala amekamatwa na polisi.

Polisi wakamshikilia kajala mahabusu kwa siku kadhaa na wakamwambia kuwa hatoachiwa mpaka mumewe akamatwe, kwa hivyo ili kujinusuru ni bora ashirikiane na polisi kumkamatisha mumewe.
images (9).jpeg


Kajala akakubali. Kajala akaanza kuwasiliana na mumuwe akijifanya kama yuko kawaida tu nyumbani wakati ukweli ni kwamba yuko mikononi mwa polisi. Wakawasiliana kwa siku kadhaa mpaka wakafikia hatua ya kupanga waonane. Mumewe akamwambia Kajala asafiri mpaka mkoani Morogoro halafu atamwambia ni wapi waonane.

Kajala akapakiwa kwenye gari la polisi na wakasafiri naye mpaka Morogoro. Alipofika Morogoro mumewe akamweleza hoteli aliyopo. Kajala na polisi wakaenda mpaka kwenye hiyo hoteli na mumewe akakamatwa.

Baada ya mumewe kukamatwa ndiyo wote wawili wakaja kufunguliwa kesi ya kutakatisha fedha. Jiji lote lilizizima ilipotangazwa kuwa Kajala yuko mikononi mwa polisi kwa shutuma za kuhusika kwenye mchoro wa kutakatisha mamilioni ya fedha.
images (10).jpeg


Ubaya ni kwamba kesi ya namna hii haina dhamana, kwa hiyo Kajala na mumewe wakakaa gerezani mwaka mmoja na miezi miwili mpaka siku ya hukumu mwezi March mwaka 2013. Mumewe akahukumiwa kwenda jela miaka 7 au faini ya shilingi milioni 200. Kajala akahukumiwa kwenda jela miaka 5 au faini ya shilingi milioni 10. Kwa bahati nzuri Kajala akamudu kulipa hiyo faini ya milioni 10.

Kuna maneno mengi sana juu ya nani hasa alilipa hela ile huku watu wengi wakiamini kuwa ile milioni 10 ililipwa na Pedeshee maarufu miaka ile aliyeitwa 'CK'. Lakini vyovyote vile, hatuwezi kukataa kwamba Wema Sepetu na Dr. Cheni hata kama hela hawakutoa wao lakini ndio watu waliopambana kweli kweli siku ile ya hukumu mpaka milioni 10 inalipwa na Kajala kuachiwa huru.

Bahati mbaya mumewe hakuweza kumudu faini ya milioni 200 na kwa hivyo akapelekwa jela ambako alitumikia kifungo mpaka mwaka 2017 alipoachiwa kutokana na tabia njema na hivyo kuondolewa sehemu ya adhabu (theluthi moja ya kifungo).
images (14).jpeg


Watu walio karibu na Kajala na mumewe wanaeleza kwamba kipindi mume wa Kajala anatumikia kifungo mwanzoni Kajala alikuwa anakwenda kumuona, lakini baadae akakata mguu. Kajala mwenyewe anadai kwamba alihisi kama ndugu wa mumewe hawataki anavyojiweka karibu na ndugu yao. Walikuwa na kinyongo naye. Pengine walikuwa na kinyongo naye kwa kushirikiana na polisi kumkamatisha ndugu yao, au labda pengine walikuwa na kinyongo kwa stori zilizokuwa zinaenea mtaani kuhusu mahusiano mapya ya Kajala baada ya kutoka jela.

Hata kuna kipindi mumewe akiwa bado gerezani aliumwa na kulazwa Muhimbili. Kajala akawa anakwenda kumuona. Lakini muda mwingine ndugu walikuwa wanamzuia asimuone mumewe. Siku nyingine Kajala akienda ndugu wa mumewe wanamuita aje mwanamke mwingine ambaye mumewe alizaa naye huko siku za nyuma, kitendo ambacho Kajala hakuwa akipenda.

Kwa hiyo akaacha kwenda kumuona mumewe. Hata mumewe alipotoka gerezani hawakuwahi kuwasiliana naye mpaka siku ambayo alipigiwa simu kwamba mumewe anataka talaka.

Mpaka leo hii Kajala na mumewe bado wako kwenye baraza la usuluhishi la kanisa wakiomba ruhusa ya kupeana talaka ili kila mmoja aendelee na maisha yake mengine ya kuishi na wenza wao wapya kwa amani na ikibidi kufunga ndoa tena na watu walionao kwenye mapenzi sasa hivi.
images (15).jpeg


Licha ya misukosuko yote hii ya maisha yake ambayo yawezekana mpaka leo hii bado haja-recover kwa asilimia mia moja, lakini Kajala bado anaendelea kukaa kileleni kama moja ya wanaweka mastaa wa daraja la kwanza nchini Tanzania.

Kuna watu wengine kama wangepitia hata nusu tu ya mitihani aliyopitia mwanamke huyu yawezekana mpaka sasa tungelikuwa tumeshawazika. Lakini Winniefrida Kajala bado amesimama imara.

Kajala ni mfano mzuri wa kuwafunza binti zetu wasikurupukie maisha, ujana maji ya moto na kutozuzuka na uzuri wao na kuchezea elimu na maisha. Lakini pia Kajala ni mfano mzuri pia wa kuwafunza mabinti hata kama wanapitia mitihani mizito kiasi gani, kamwe wasikate tamaa na maisha. Unaweza kupitia misukosuko ukajihisi kama uko kuzimu, lakini ukipambana lazima siku moja utaibuka na kurejea kileleni. Kajala ni mfano sawia wa mazuri na mabaya ya ujana.
IMG_20221014_122032.jpg


Credit: Habibu Anga Kupitia Mange Kimambi App.
 
Kwa maana siku ya Nyerere ndiyo watanzania hawaendelei na mambo yao mengine?

Inawezekana ni siku ya muhimu kwako, lakin kwa wengine it's a shit day.
Vitoto vya watoza tozo hao mkuu, they think we have sleeping day like them, hawajui kwetu sisi hii siku inafanya tusipeleke mkono vinywani sababu watu hawajaja makazini mwao.
 
Hana hata carrier ya maana ya kusema anaingiza pesa kwa kupitia kitu Fulani alafu ndo barua yote hiyo. Yes she is beautiful lakini msipotoshe watoto wetu, we need them to Believe in HARD WORK, DISCIPLINE AND EDUCATION. AMEN
Hata mimi hapo pamenipa ukakasi sana, pamoja na andiko la page 8 lakini sijaona mahali wamegusia anafanya nini maishani mwake...
 
Naona hizo dondoo humu kitambo mbona tushazigusa

Ila faraji alimpa hela kajala atambae kajala yeye akawa anajirusha tu mjini

Na nikweli kajala ndy alimseti faraji kwa wazee mpaka kukamatwa kwake
Na faraji alipokuwa anakuja dar kutokea tanga ili akatane na kajala
Faraji alimwambia kajala kuwa yeye atakuwa amevaa baibui,kajala mtonyo
Wote aliwapa maskari,faraji kushuka tu ubungo aka dakwa
Kesi iliyokostisha kajala ni ya kutaka kufoji signature ili aiuze nyumba ile ya salasala
Kajala kukamatwa kwake mara ya kwanza alikamatiwa nje ya lilltle pharmacy ambapo ni mitaa ya airtel moroco
Kajala shule aliyomalizia ilikuwa kumbukumbu huko alikuwa na washkaji zake wakina Joan na wengineo

Ova
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom