Sababu kuu zinazofanya wanawake kuwanyima wanaume Unyumba

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,343
51,910
SABABU KUU ZINAZOFANYA WANAWAKE WALIOOLEWA KUNYIMA WAUME ZAO UNYUMBA!.

Na, Robert Heriel.

Maelezo haya ni baada ya kufanya uchunguzi binafsi ambao ulikuwa huru kabisa. Hivyo maelezo haya sio yakujitungia, ni matokeo ya uchunguzi huru nilioufanya. Aidha uchunguzi huu usichukuliwe kuwa Rasmi Kwa sababu haukupitia kwenye vyombo Rasmi vya utafiti. Hata hivyo uchunguzi huu unaweza kuwa msaada Kwa watu wenye matatizo ya ndoa ya kumtukana tendo la ndoa.

Niite Taikon wa Fasihi mchunguzi huru, katika Nyanja za kijamii.

Ninapenda kukaa na watu wazima, wenye umri ulioenda, 80% ya muda wangu wa kuingiliana na watu nachangamana na watu walionizidi Umri. Hii ni tabia tangu nikiwa mtoto Mdogo. Hivyo sio ajabu kumkuta Taikon akiwa anapiga Stori za maisha na Mtu WA miaka 45-60, ni nadra Sana kunikuta na vijana WA umri wangu au chini yangu yaani 27-30 mara nyingi nawachukulia Kama watoto.
Sisemi nawadharau Hasha! Ila najaribu Kueleza vile nilivyo.

Ninapochangamana na watu hao (wenye age 35-70) ninapenda Sana Zogo, kubisha ili Wazee hao wanithibitishie wanayoyaongea ni sahihi, kikawaida watu wasio na Ujuzi WA mambo mengi wanaopenda kulazimisha mambo wananiona ninawadharau kumbe Mimi lengo la kuwabishia na kuwakosoa (Criticise) ni kupata madini yaliyojificha zaidi katika fikra zao.

"Mimi mke wangu hawezi ninyima tendo la ndoa" Wazee kwenye mada zao hunikemea😀😀 husema nisiseme hivyo, na wengi hukiri kuwa wananyimwa UNYUMBA,
Basi tunabishana wee! Nawauliza wakinyimwa UNYUMBA huwa wanafanyaje?

Wapo walionijibu kuwa wanachepuka Kwa wanawake wengine, hawa wapo makundi Yafuatayo;
i. Hawa ni Wale wenye uwezo wa kifedha ambazo huzitumia kuwapa Wadada wengine Kama Kodi ya nyumba, kununua zawadi n.k.

ii. Kuna Wale wenye haiba na vipaji vya kushawishi.
Hawa ni Wale waliooa wenye mvuto wa nje, Handsome, au wenye kujua kulaghai wanawake. Huchepuka pia endapo watanyimwa UNYUMBA na wake zao.
Kundi hili mara nyingi huwapenda wanawake wenye vipato au Wafanyakazi WA serikalini na makampuni Makubwa binafsi.
Wapo wanawake wenye pesa ambao hutoka na waume za watu wenye mivuto ya kimaumbile.
Unakuta Mdada anakazi nzuri, anamtoto/watoto wawili lakini Hana mume kazi yake kutoka na waume za watu na kuwapa pesa. Hii IPO zaidi DAR ES SALAAM.

iii. Wanaume wachawi au washirikina au wenye connection ya waganga au wachawi.
Lipo kundi ambalo hutumia Uchawi kuchepukia.
Kwa wale wachawi halisi humaliza kiu zao Kwa kutembea na wanawake kwenye ndoto usiku watu walalapo.
Kundi hili hufanywa zaidi na Wazee wenye umri mkubwa kidogo kuanzia miaka 60-80 huko.
Unakuta Mzee hana pesa, hana Mali, Hana mvuto Kwa sababu keshazeeka ngozi ishasinyaa lakini anataka pisi Kali iliyopo mtaani, mbinu waitumiayo ni kulala na pisi Kali ndotoni, hudukua mfumo wa ndoto za Mwanamke, kisha humlala mwanamke wakati huo mwanamke anajiona Kama anaota anafanywa na Mwanaume Yule anayemtoleaga udenda huko ofisini au mitaani kumbe anatoka na Babu kizee. Wengi huita Jinni mahaba Ila mara nyingi ni wachawi WA mtaani wanajipigia tuu.

Sitaki nikuchoshe!

Baada ya kuhoji kina Mama na Baba nikazipata sababu zinazofanya wanawake walioolewa kuwanyima waume zao UNYUMBA;

1. Wanaume wengi kutowafikisha Wake zao kileleni.
Wanawake wengi wamelalamika kuwa waume zao huwaacha hewani bila kuwafikisha Kibo(kileleni).
Sababu za kutofikishwa kileleni zilizoripotiwa;
i. Wanaume kumwaga upesi chini ya dakika tano.
ii. Wanaume wengi kushindwa na kutokujua Sanaa ya kufanya Mapenzi. Kushindwa kuutumia vizuri mwili WA mwanamke, kushindwa kumwandaa mwanamke, kushindwa kutumia sauti ya kiume kuzivuta hisia za mwanamke mpaka awe tayari kuingiliwa, hivyo wanaume wengi humuingilia wanawake wakiwa Wakavu na kuwasababishia maumivu makali.

iii. Uhuru wakati WA tendo.
Wanaume wengi sio rafiki na wake zao. Hivyo mwanamke Hana Uhuru wa kutosha Kwa Mumewe. Mwanamke anapokuwa Hana Uhuru na mumewe nafasi ya kufika kileleni ni ndogo Sana. Wanawake wengi wanawaogopa waume zao. Huona aibu kueleza hisia zao wakati WA tendo Kwa kuhofia kuonekana Malaya.
Hii husababisha hata Kama Mwanamke anaumia kukaa kimya, au kama anajisikia Raha kushindwa kusema hapo hapo endelea.

iv. Wanawake wengi wameolewa na wanaume wasiowapenda Kwa mioyo Yao yote. Wengi husema nipo pale tuu kupitisha muda, nasubiri watoto wakue. Na wengi wanakiri kuwa wanawakumbuka mwanaume Fulani waliyempenda Kwa moyo wote.

2. UCHAFU KWA WANAUME WALIOWENGI.
Wanawake wengi wanawaogopa kulisema hili wawapo Kwa wanaume Ila wao Kwa wao huyateta kuwa mume wangu ni mchafu au ananuka. Nimeshaelezea sababu ya kushindwa kusema ni kutokuwa huru na ubabe wa kipumbavu wa wanaume waliowengi ambao hufikiri ubabe ndio Uanaume.

Wanawake wote Duniani wanasifa ya Kupenda mwanaume mtanashati WA mavazi na mwili. Hupenda mwanaume msafi.

Wanawake wengi hukosa hamu ya kuwapa waume zao tendo la ndoa Kwa sababu unakuta mwanaume ananuka jasho, haogi vizuri akatoa uchafu, hafui boxer au nguo za ndani zinanuka fuu! Ananuka mdomo,

Moja ya vitu vinavyoondoa mood ya kufanya tendo la ndoa ni pamoja na harufu mbaya. Sio Kwa wanawake haya Kwa Sisi wanaume.
Wanaume mtakubaliana na Mimi kuwa mwanamke kama ananuka jasho au uchi hausafishi vizuri mpaka ukatoa harufu inapoteza hamu ya kufanya ngono.

Wanaume hili tubadilike, umetoka mizunguko oga vizuri uhakikishe hunuki, Kama umnywaji wa pombe au mvuta sigara na Mkeo hafanyi hayo ni Bora ukapige Mswaki na kutafuna Big G ili kuweka mambo Sawa.

Ukiwa unanukia vizuri hata mkeo akikaa karibu yako anapata hamu, huo ujasiri WA kukunyima unatokea wapi.

Nafahamu wapo wanaofanya kazi za kutoa jasho, jitahidini muoge.
Alafu muache ubishi na ubabe wa kipumbavu. Ukiona Mkeo anakuambia kaoge muelewe, usitake akuambie unanuka. Wewe ni mtu mzima bhana.

Hoja hii pia wanawake muwe wasafi maana wapo wanawake ni wachafu wananuka Kama nini.

3. UCHOVU WA KAZI NYINGI.
Kama kuna mambo yanayoondoa hamu ya mwanamke kufanya tendo la ndoa ni kazi nyingi. Mwanamke akichoka hawezi kuwa na hamu ya tendo la ndoa.
Unakuta mwanamke kutwa nzima umemfanyisha makazi, amepika, kafua, kapiga deki, kachota Maji alafu unategemea usiku akupe😀😀 Thubutuu! Akikupa kakupa Kwa kukupenda Sana au kukuogopa.

Nashauri Kama Mkeo anakunyima UNYUMBA jaribu kuangalia mfumo wa kazi zake, kisha mpunguzie hizo kazi.
Na Kama ukimpunguzia basi kwenye tendo la ndoa ufanye kweli sio upapase umuache hewani.
Kuna namna mbili za kumfanya mwanamke asichepuke Kwa sababu ya hamu ya Mwili wake;
I. Kumfikisha kileleni na kukata kiu yake
ii. Kumfanyisha makazi mengi mpaka mwiki uchoke.

Wewe fuata mbinu ya Kwanza.
Lakini kama Mkeo ni lile kundi la wanawake wenye nyege Kali, basi mfanyishe kazi nyingi kisha mfikishe kileleni Ukate kiu yake.

Kama atachepuka atachepuka Kwa shida zingine lakini sio haja ya Mwili wake.
Shida zingine zaweza kuwa pesa, au kisasi.

4. MAJINI NA WACHAWI.
Wapo wanawake wanaonyima waume zao tendo la ndoa Kwa sababu usiku wanashughulikiwa na wachawi WA mtaani hapo, hasa Wazee. Au Majini. Kundi hili wapo wachache Sana.
Kutokana na kuwa Mfumo wa kufikia ndoto unabadilika kila ndoto, yaani ni kusema kila ndoto inakuwa na code zake ambazo mchawi au Jinni linapaswa lidukue Code hizo.

5. MAGONJWA.
Yapo magonjwa yanayoweza kumfanya mwanamke akosea hamu ya kufanya Mapenzi na Mwanaume. Endapo mke wako anafangasi ambazo unapomuingilia anasikia maumivu makali inaweza kusababisha akakunyima tendo la ndoa. Pia magonjwa mengine ya mifumo ya damu ambayo humfanya mwanamke hisia zake za mapenzi ziwe mbali.

6. MVUTO.
Kijana ambaye hujaoa hakikisha mvuto ulionao sasa haupotei hata siku ukiingia kwenye ndoa.
Asikudanganye mtu hata wanawake hisia zao zinachangiwa na mvuto wa mwanaume.
Ipo kasumba kuwa Mwanaume hasifiwi mvuto lakini hiyo ni Dhana potofu, hakikisha mwili wako unakuwa Standard, fanya mazoezi, jiweke kisasa kulingana na umri na rika lako.

Sio unaoa tuu unaanza kufuga manyama uzembe hovyo hovyo, huweki nywele zako vizuri, hujiweki Kama Mwanaume anayetakwa na wengi.

WANAWAKE wanapenda ushindani, wanapenda vitu vinavyopiganiwa na wengi. Wewe Kama hujajiweka katika Hali na nafasi ya kupiganiwa na wanawake wengi unahatari.
Wanawake wanapenda kusifiwa kuwa naye kapata mume WA maana.

Kila mtu anaomvuto wake, Ila wengi wetu tunaharibu mivuto yetu Kwa Dhana potofu zilizopo kwenye jamii.

Wewe uliona wapi ukawa na mvuto alafu mwanamke akunyime tendo la ndoa, hiyo haipo.

Mwanamke ni Kama Mwanaume tuu. Tofauti iliyopo baina yetu ni ndogo Sana.

Kama vile Sisi wanaume tunavyoshindwa kujizuia mbele ya wanawake wenye mivuto ya kike ndivyo na wanawake wanavyoshindwa kujizuia Kwa mwanaume mwenye MVUTO.

Mkeo anakuambia Hapendi mandevu, wewe unafuga tuu.
Anakuambia hapendi kitambi, wewe unalipwa tuu,
Kwa nini baadaye umlaumu??

Ni Sawa na Mwanamke unaambiwa na Mumeo hapendi tumbo lako linavyokua na kuwa kitambi, wewe unakula tuu michipsi na Mafuta, anakuambia kuwa msafi wewe kazi kujinukiza majasho, alafu yakitokea yakutokea unasema wanaume ni Mbwa. Shenzi wewe! Mbwa Baba yako.

Niishie hapa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Jamaa angu Haruni mdutch wa kule Manzese ndoa yake changa ina miaka mitatu mke wake alikuwa hampi unyumba anampa kwa kusuasua akaniambia ngoja nimuonyeshe

Alichokifanya hakumuomba tena akawa anapoa zake kwa mchepuko wake au Riverside ikapita miezi kadhaa mpka mke ana shangaa mbona huyu anisumbui mke alikuja juu akasema nitakushtaki kwa wazee

So dawa yake nimeipenda siku nikioa nikizinguliwa nawa kama mdutch hata mwaka simgusi
 
Jamaa angu Haruni mdutch wa kule Manzese ndoa yake changa ina miaka mitatu mke wake alikuwa hampi unyumba anampa kwa kusuasua akaniambia ngoja nimuonyeshe


Alichokifanya hakumuomba tena akawa anapoa zake kwa mchepuko wake au Riverside ikapita miezi kadhaa mpka mke ana shangaa mbona huyu anisumbui mke alikuja juu akasema nitakushtaki kwa wazee





So dawa yake nimeipenda siku nikioa nikizinguliwa nawa kama mdutch hata mwaka simgusi


Inategemea na Mwanamke na Mwanamke.
Mwingine ndio inakuwa kuvuja Kwa pakacha.

Unatoka naye ndio anapata nafasi ya kutoka Kwa wengine.

Lazima ufuatilie sababu ya kunyimwa UNYUMBA ni ipi? Ukiijua itatue.

Lakini kama anakufanyia makusudi mfukuze aende kwao kisha is mwingine.

Asikuletee upuuzi wake
 
Mm huwa navunga siku akitaka yeye..napiga show kwa hisiaa yan dakika 10 teyar kama kuku. then nalala na muacha amefuraaa anapiga kitandaa..nilimfanyia mwezi akaachaa mwenyew
 
Back
Top Bottom