NI KWA NAMNA GANI WANANCHI WANANWEZA KUPATA MSAADA WA KISHERIA

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
19,675
59,775
Nchi nyingi huwa na ofisi za huduma za kisheria zinazotoa msaada wa kisheria kwa wananchi wasio na uwezo wa kulipia huduma za mawakili binafsi. Huduma hizi zinaweza kujumuisha ushauri wa kisheria, usuluhishi wa migogoro, na hata uwakilishi kisheria kwa mahakamani.

Kuna mashirika mengi ya kutoa msaada wa kisheria ambayo yanaweza kutoa ushauri na msaada wa kisheria kwa wananchi. Mashirika haya yanaweza kuwa ya kiraia au yanaweza kuungwa mkono na serikali.
1704025609845.png

View attachment 2858507

Taasisi binafsi zipo, mfano Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wanatoa msaada wa kisheria.
 
Kuna jamaa mmoja alikuwa anasema kuna baadhi ya hizi taasisi wakiona kesi inahusisha mwananchi mnyonge ameshtaki kiongozi maarufu au serikali huwa wanaogopa kumsaidia.
Wanatoa msaada ktk kesi fulani Fulani kama vile kesi za ardhi, au Mirathi, lakini mara nyingi huwa hawajihusishi sana na masuala ya Kesi za Jinai.
LHRC kwa kiasi kikubwa sana wamekuwa wakijitahidi kuwasaidia watu, hasa wale wenye vipato vidogo. Kwa hili ninazo shuhuda nyingi za kuweza kuwatetea LHRC, wamekuwa wakijitahidi kwa kweli. Lazima tuseme ukweli juu yao kuhusu jambo hili.
 
Back
Top Bottom