Kampeni ya Masaada wa Kisheria ya Mama Samia

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
19,675
59,783

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA NI NINI?

Kampeni ya Masaada wa Kisheria ya Mama Samia
(Mama Samia Legal Aid Campaign #MSLAC ) imejikita katika kutoa elimu ya kisheria kwa wananchi hususan katika masuala ya ukatili wa kijinsia, migogoro ya ardhi, mirathi, usuluhishi wa migogoro kwa njia mbadala, na masuala yahusuyo haki za binadamu kwa ujumla.

#MSLAC ni mchakato wa kupata ushauri au msaada kutoka kwa wataalamu wa sheria ili kutatua masuala ya kisheria au kupata ufafanuzi kuhusu haki na wajibu wa mtu. Kampeni Hii inajumuisha mambo kama vile ushauri wa kisheria, msaada wa kisheria au uwakilishi wa kisheria katika mahakama.

1704862845440.png

1704863083526.png

"Usaidizi wa Kisheria" au "Msaada wa Kisheria" unaweza kutofautiana kidogo kulingana na muktadha wa kisheria wa nchi fulani.

Kampeni ya Masaada wa Kisheria ya Mama Samia #MSLAC inatoa msaada wa kisheria kwa watu ambao hawawezi kumudu huduma za kisheria kikamilifu au wanaohitaji msaada wa kisheria.
 
1704863600394.png

Kampeni ya Masaada wa Kisheria ya Mama Samia #MSLAC imejikita kutoa msaada wa kisheria ambao unaweza kujumuisha:-

#MSLAC inatoa Ushauri wa Kisheria kwa watu wanaohitaji msaada na mwongozo katika masuala mbalimbali ya kisheria, kama vile masuala ya familia, makazi, au ajira.

#MSLAC Kuwapatia watu wasiojiweza rasilimali za kutosha ili kupata huduma za kisheria au kuwawakilisha mashauri yao mahakamani.

#MSLAC inakuwakilisha Mahakamani kwa Kutoa msaada wa kisheria kwa watu ambao wanaweza kuhitaji wakili kuwawakilisha katika masuala ya kisheria mahakamani.

#MSLAC inatoa elimu na ufahamu kuhusu haki za kisheria na jinsi ya kuzitumia.

#MSLAC inasimamia Usuluhishi wa Migogoro, kwa Kusaidia katika kutatua migogoro nje ya mahakama kupitia njia za usuluhishi au mazungumzo.
 
Sasa tutajuaje Leo IPO mkoa gani ?
Kuna watu wamechukuliwa ardhi zao kwa nguvu na matajiri ...huku baadhi ya viongozi Serikali ya mtaa wakiwatetea matajiri ..
Hili ndio pungufu kubwa la hii kampeni. Ilipaswa iwe inapatikana nchi nzima kwa wakati mmoja.
 
KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA NI NINI?

Kampeni ya Masaada wa Kisheria ya Mama Samia
(Mama Samia Legal Aid Campaign #MSLAC ) imejikita katika kutoa elimu ya kisheria kwa wananchi hususan katika masuala ya ukatili wa kijinsia, migogoro ya ardhi, mirathi, usuluhishi wa migogoro kwa njia mbadala, na masuala yahusuyo haki za binadamu kwa ujumla.

#MSLAC ni mchakato wa kupata ushauri au msaada kutoka kwa wataalamu wa sheria ili kutatua masuala ya kisheria au kupata ufafanuzi kuhusu haki na wajibu wa mtu. Kampeni Hii inajumuisha mambo kama vile ushauri wa kisheria, msaada wa kisheria au uwakilishi wa kisheria katika mahakama.

View attachment 2867082

Asante VS for this, ilipoanza nilitoa ushauri ufuatao Uzinduzi wa Mama Samia Legal Aid Campaign - Sheria ya Ardhi ni ya Mwaka 1999 na Sio 1995
P
 
Asante VS for this, ilipoanza nilitoa ushauri ufuatao Uzinduzi wa Mama Samia Legal Aid Campaign - Sheria ya Ardhi ni ya Mwaka 1999 na Sio 1995
P
Ushauri Wangu kwa Kampeni Hii
Mimi kama mtu wa habari na publicity, kampeni hii ni jambo jema, jambo kubwa na jambo zuri, tatizo ni Watanzania wengi hawajui haki zao, hivyo nashauri, watekelezaji wa kampeni hii, waandamane na media kila waendapo, media itangaze kila kinachofanyika, sio tuu ili kuhamasisha watu wajitokeze kwa wingi, bali pia kutoa fursa ya kutoa elimu ya sheria na elimu ya haki kwa Wananchi.

Usahuri wako huu Comrade. Umekaa vizuri sana. Watu wa Media itabidi kuhusishwa kwa 100%
 
Kampeni hii inaweza kuchangia sana katika kujenga jamii yenye ufahamu zaidi wa sheria na kuwasaidia watu kutatua masuala yao ya kisheria.
 
Back
Top Bottom