Je, umewahi kujiuliza kuhusu ukimya wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na uuzwaji wa Bandari za Tanganyika?

HANGAYA THE CHIEF

JF-Expert Member
Sep 10, 2021
329
947
Utangulizi:
Ukisoma katiba ya JMT ibara ya 59 (1) imeanzisha ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, na ibara ndogo ya (3) ya ibara hiyo ya 59, inaeleza wajibu mkuu ni kuishauri serikali katika mambo yote yanayohusu sheria, zaidi sana ibara ya 59 (5) kwa hadhi ya ofisi yake mwanasheria mkuu amepewa hadhi ya ubunge, kwa kifupi ni Mbunge wa JMT.

ukienda zaidi kusoma kwa pamoja sura ya 268 ya sheria ya ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kazi na wajibu wake yaani, the office of the Attorneys General ( Discharge of Duties Act), Cap. 268, hasa kifungu cha 8 1) (a), (section 8 (1) (a) ya sheria hiyo inaeleza kazi mbalimbali za mwanasheria mkuu, ikiwa pamoja na kushauri serikali kuu, serikali za mitaa, wizara mbali mbali, taasisi za serikali, mashirika ya umma.

Nimefanya tafiti kidogo kwenye tovuti yao, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AGCTZ) | Mikataba na Makubaliano, utagundua na utaona wana hadi department (division ya mikataba) imegawanyika katika sehemu tatu yaani; mikataba ya ununuzi wa umma, mikataba ya makubaliano ya kimataifa na mikataba ya uwekezaji wa maliasili.

Je, mwanasheria wa taasisi au wizara ana mamlaka ya kuishauri serikali kuingia kweye mikataba ya kimataifa?

1.
Kulingana na katiba yetu na sheria zetu tajwa hapo juu ni hapana. lakini kumekuwa na mwanasheria anaitwa Hamza Johari, kutwa kuchwa anatolea ufafanuzi kuhusu mikataba walioingia kati ya JMT na Manispaa ya Dubai, lakini kwangu mimi nadhani anatukosea watanganyika, kwa sababu kusoma kwangu sijaona mamlaka yake, au anawajibika vipi kwenye taifa letu la mikataba aliyoiingiza yeye katika nafasi yake, au utueleze ana uhusiano gani na mikataba hiyo?

Je, Spika wa Bunge alikuwa sahihi, kuchukua nafasi ya mwanasheria mkuu bungeni?
2. Jibu ni hapana
, katika kuongoza nchi, kuna mihimmili mitatu, yaani serikali, bunge na mahakama, kwa muktadha huo serikali ilipeleka mkataba ule kwenye mhimili wa Bunge, na kazi ya Bunge ni kuangalia nini, serikali imeleta, je ni kwa manufaa ya nchi na wananchi wake?, na kama wawakilishi wa wananchi, wana wajibika kuangalia maudhui yake na faida zake, kwa kuihoji serikali yaani, (check and balance, )hiyo Spika aliingilia kazi ya serikali, na kwa kuwa ilihusu mikataba na mikataba ni sheria basi ulikuwa ni wajibu ambatano wa mwanasheria mkuu wa serikali kutolea ufafanuzi, kwa nini serikali wameridhia, kifungu fulani wana nini wanatarajia. maana waliokuwa kwenye negotiation ya mkataba huo ndio "wao" kwa maana wenye mamlaka hayo.
kwa hiyo, kwa kuingilia nafasi ya mwanasheria mkuu, spika analitaarifu taifa alichukua, au alikuwepo wakati wanakubaliana (negotiation), na hivyo anajua maudhui ya nini kinachoelezwa.

3. Je, ukimya wa mwanasheria mkuu unamaanisha nini? (mtazamo binafsi)
katika dhana ya uwajibikaji, alipashwa ajihudhuru kwa upendo, si kwa sababu ameshindwa kazi, lakini kwa sababu ya mazingira hayo hapo juu. yaani bungeni na mitaani;

(a) inaonekana hakushirikishwa vizuri kadili ipaswazo kwa mujibu wa katiba na sheria, kutoa ushauri wa kisheria kuhusu mkataba huu, ndio maana sehemu zote ambazo anapashwa kuongea ameaamua kuchagua kukaa kimya, bungeni ni kama alinawa mikono. kuashiria sihusiki na kinachoendelea malizaneni wenyewe.

(b) huku mitaani, Hamza Johari amekuwa ndio mwanasheria mkuu, akitolea ufafanuzi wa kwa nini waliamua kuingia mkataba.

4. Je, nani alimshauri Rais wa JMT kuridhia kuingia makubaliano hayo ya uwekezaji?
Bado Sina Jibu, najua wazi kuwa Rais wetu si mwanasheria, sina shaka lazima atakuwa kaomba ushauri kabla ya kutoa ruhusa ya kuiingiza nchi katika mkataba huu aliomba ushauri wa kisheria,

Je, kama aliyemshauri ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, basi ndio alipaswa kuwa msemaji mkuu wa kadhia yote iliyotufikisha hapa, au kama si yeye nadhani wasiwasi wangu unarudi kwa mwanasheria Hamza Johari, Je ni nani hasa na ana interest gani katika mkataba huu?

5. Nani alaumiwe? na nini kifanyike?
kwanza sitaacha kuwalaumu waandishi wa habari, kwani wametuangusha sana, katika tafiti zote za habari kabla hujaenda site, lazima ujue key informers (nani atakupa habari sahihi?), si kila mtu anapaswa kuulizwa kwenye vitu ambavyo vinaitaji majibu ya moja kwa moja, mpaka sasa nimeona midahalo, magazeti, radio, tv, kwa bahati mbaya sana wanaoalikwa si watu sahihi.

Nimalizie, hapo.
 
Yote uliyoyaainisha na mengine yatakayokuja nyakati zingine huko mbele ya safari zinasababishwa na zitaendelea kusababishwa na mikanganyiko iliyomo ndani ya Katiba yetu.

Kwa mfano umeeleza kwamba Nchi kwa kawaida inaendeshwa na mihimili mitatu.

Swali kubwa hapo ni je hiyo mihimili mitatu nguvu zake zipo sawasawa?!

Katiba mpya bora ni muhimu!

Tatizo letu wabongo siku zote tunaangalia tulipoangukia badala ya kuangalia wapi tulipojikwaa !! Ni maoni yangu tu.
 
Katika kichwa chako cha habari ondoa neno "UUZWAJI" Hakuna bandari inayouzwa unachofanya ni uchonganishi kwa umma.
Eleza wewe, bandari imefanywa nini?

Nakubaliana nawe kuwa haijauzwa maana kama ingekuwa imeuzwa, angalao tungeambiwa imeuzwa kwa bei gani.

Hatuwezi kusema imekodishwa maana kama ingekuwa imekodishwa, tungeambiwa inakodishwa kwa dola ngapi, na imekodishwa kwa kipindi gani.

Kwa hiyo, kwa ujumla, kwa lugha rahisu, IMEPORWA.
 
Yote uliyoyaainisha na mengine yatakayokuja nyakati zingine huko mbele ya safari zinasababishwa na zitaendelea kusababishwa na mikanganyiko iliyomo ndani ya Katiba yetu.

Kwa mfano umeeleza kwamba Nchi kwa kawaida inaendeshwa na mihimili mitatu.

Swali kubwa hapo ni je hiyo mihimili mitatu nguvu zake zipo sawasawa?!

Katiba mpya bora ni muhimu!

Tatizo letu wabongo siku zote tunaangalia tulipoangukia badala ya kuangalia wapi tulipojikwaa !! Ni maoni yangu tu.
Katiba haina shida yoyote mkuu achana nayo
 
Mkuu upo sahihi sana, sijaona mawanasheria mkuu akitolea ufafanuzi hoja za wabunge juu ya huo mkataba wala sijamwona kwenye media. Huku kwenye media wameonekana wanasheria nguli Dr. kasheku na mbawala ndo waliokuja kufafanua kifungu kwa kifungu.​
 
Eleza wewe, bandari imefanywa nini?

Nakubaliana nawe kuwa haijauzwa maana kama ingekuwa imeuzwa, angalao tungeambiwa imeuzwa kwa bei gani.

Hatuwezi kusema imekodishwa maana kama ingekuwa imekodishwa, tungeambiwa inakodishwa kwa dola ngapi, na imekodishwa kwa kipindi gani.

Kwa hiyo, kwa ujumla, kwa lugha rahisu, IMEPORWA.
Mh, poleni sana haters wa mama!!!
 
Wa kuwapuuza tu hao, wanataka mwanasheria wa serikali ajiropokee tu kama wao? Ana utaratibu wake na muda wake ukifika ataongea km kuna ulazima wowote
Ataongea wapi tena wakati alitakiwa kutolea ufafanuzi hoja za wabunge pale mjengoni, hili jukwaa limejaa vilaza hatari.
 
Utangulizi:
Ukisoma katiba ya JMT ibara ya 59 (1) imeanzisha ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, na ibara ndogo ya (3) ya ibara hiyo ya 59, inaeleza wajibu mkuu ni kuishauri serikali katika mambo yote yanayohusu sheria, zaidi sana ibara ya 59 (5) kwa hadhi ya ofisi yake mwanasheria mkuu amepewa hadhi ya ubunge, kwa kifupi ni Mbunge wa JMT.

ukienda zaidi kusoma kwa pamoja sura ya 268 ya sheria ya ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kazi na wajibu wake yaani, the office of the Attorneys General ( Discharge of Duties Act), Cap. 268, hasa kifungu cha 8 1) (a), (section 8 (1) (a) ya sheria hiyo inaeleza kazi mbalimbali za mwanasheria mkuu, ikiwa pamoja na kushauri serikali kuu, serikali za mitaa, wizara mbali mbali, taasisi za serikali, mashirika ya umma.

Nimefanya tafiti kidogo kwenye tovuti yao, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AGCTZ) | Mikataba na Makubaliano, utagundua na utaona wana hadi department (division ya mikataba) imegawanyika katika sehemu tatu yaani; mikataba ya ununuzi wa umma, mikataba ya makubaliano ya kimataifa na mikataba ya uwekezaji wa maliasili.

Je, mwanasheria wa taasisi au wizara ana mamlaka ya kuishauri serikali kuingia kweye mikataba ya kimataifa?

1.
Kulingana na katiba yetu na sheria zetu tajwa hapo juu ni hapana. lakini kumekuwa na mwanasheria anaitwa Hamza Johari, kutwa kuchwa anatolea ufafanuzi kuhusu mikataba walioingia kati ya JMT na Manispaa ya Dubai, lakini kwangu mimi nadhani anatukosea watanganyika, kwa sababu kusoma kwangu sijaona mamlaka yake, au anawajibika vipi kwenye taifa letu la mikataba aliyoiingiza yeye katika nafasi yake, au utueleze ana uhusiano gani na mikataba hiyo?

Je, Spika wa Bunge alikuwa sahihi, kuchukua nafasi ya mwanasheria mkuu bungeni?
2. Jibu ni hapana
, katika kuongoza nchi, kuna mihimmili mitatu, yaani serikali, bunge na mahakama, kwa muktadha huo serikali ilipeleka mkataba ule kwenye mhimili wa Bunge, na kazi ya Bunge ni kuangalia nini, serikali imeleta, je ni kwa manufaa ya nchi na wananchi wake?, na kama wawakilishi wa wananchi, wana wajibika kuangalia maudhui yake na faida zake, kwa kuihoji serikali yaani, (check and balance, )hiyo Spika aliingilia kazi ya serikali, na kwa kuwa ilihusu mikataba na mikataba ni sheria basi ulikuwa ni wajibu ambatano wa mwanasheria mkuu wa serikali kutolea ufafanuzi, kwa nini serikali wameridhia, kifungu fulani wana nini wanatarajia. maana waliokuwa kwenye negotiation ya mkataba huo ndio "wao" kwa maana wenye mamlaka hayo.
kwa hiyo, kwa kuingilia nafasi ya mwanasheria mkuu, spika analitaarifu taifa alichukua, au alikuwepo wakati wanakubaliana (negotiation), na hivyo anajua maudhui ya nini kinachoelezwa.

3. Je, ukimya wa mwanasheria mkuu unamaanisha nini? (mtazamo binafsi)
katika dhana ya uwajibikaji, alipashwa ajihudhuru kwa upendo, si kwa sababu ameshindwa kazi, lakini kwa sababu ya mazingira hayo hapo juu. yaani bungeni na mitaani;

(a) inaonekana hakushirikishwa vizuri kadili ipaswazo kwa mujibu wa katiba na sheria, kutoa ushauri wa kisheria kuhusu mkataba huu, ndio maana sehemu zote ambazo anapashwa kuongea ameaamua kuchagua kukaa kimya, bungeni ni kama alinawa mikono. kuashiria sihusiki na kinachoendelea malizaneni wenyewe.

(b) huku mitaani, Hamza Johari amekuwa ndio mwanasheria mkuu, akitolea ufafanuzi wa kwa nini waliamua kuingia mkataba.

4. Je, nani alimshauri Rais wa JMT kuridhia kuingia makubaliano hayo ya uwekezaji?
Bado Sina Jibu, najua wazi kuwa Rais wetu si mwanasheria, sina shaka lazima atakuwa kaomba ushauri kabla ya kutoa ruhusa ya kuiingiza nchi katika mkataba huu aliomba ushauri wa kisheria,

Je, kama aliyemshauri ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, basi ndio alipaswa kuwa msemaji mkuu wa kadhia yote iliyotufikisha hapa, au kama si yeye nadhani wasiwasi wangu unarudi kwa mwanasheria Hamza Johari, Je ni nani hasa na ana interest gani katika mkataba huu?

5. Nani alaumiwe? na nini kifanyike?
kwanza sitaacha kuwalaumu waandishi wa habari, kwani wametuangusha sana, katika tafiti zote za habari kabla hujaenda site, lazima ujue key informers (nani atakupa habari sahihi?), si kila mtu anapaswa kuulizwa kwenye vitu ambavyo vinaitaji majibu ya moja kwa moja, mpaka sasa nimeona midahalo, magazeti, radio, tv, kwa bahati mbaya sana wanaoalikwa si watu sahihi.

Nimalizie, hapo.
Uchambuzi makini sana,chakushangaza AG yupo mule Bungeni kudefend serikali lakini matokeo yake Spika alipoka mamlaka ya AG.Ndipo niliposhangaa waafrica tumelogwa na nani, ilihali tunaòhisi ni wasomi wakiblunder bila Soni. Maweee!!
 
Eleza wewe, bandari imefanywa nini?

Nakubaliana nawe kuwa haijauzwa maana kama ingekuwa imeuzwa, angalao tungeambiwa imeuzwa kwa bei gani.

Hatuwezi kusema imekodishwa maana kama ingekuwa imekodishwa, tungeambiwa inakodishwa kwa dola ngapi, na imekodishwa kwa kipindi gani.

Kwa hiyo, kwa ujumla, kwa lugha rahisu, IMEPORW
Bosi usinifokee, naumia sana na nchi yangu kuliko siasa zenu, narudia tena sijaandika uuzwaji kwa bahati mbaya, au kwa kupotosha umma. nimeandika kwa tafsiri ya kisheria ambayo tayari nilishaitolea maelezo huko nyuma katika maandiko mengine.

narudia tena swali lako lilipaswa kuwa kwa nini unasema uuzwaji? ningekujibu kistaarabu kadili nilivyosoma mkataba, kwa sababu unajifanya ujuaji kaa na maana yako, sisikilizi wanasiasa wanitafsirie mkataba, kama wewe nimesoma na kuuelewa ndio maana natoa tafsiri kadili ninavyoelewa na ilivyo katika sheria. tofauti yako mimi na wewe ni tuna line of diference, your making politics and am not a politician.

usinifundishe eti niseme imekodishwa kwa sababu hakuna bei iliyowekwa au nieleze imeandikwa shilingi ngapi? sasa , kwani umeambiwa imekodishwa kwa shilingi ngapi?, au umeelezwa bei ya ukodishwaji? au imekodishwa bure?

nasisitiza ule ni uuzwaji, na sio ukodishaji, kama issue ni pesa hata kukodisha wangesema imekodishwa kwa shilingi ngapi. period
 
Utangulizi:
Ukisoma katiba ya JMT ibara ya 59 (1) imeanzisha ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, na ibara ndogo ya (3) ya ibara hiyo ya 59, inaeleza wajibu mkuu ni kuishauri serikali katika mambo yote yanayohusu sheria, zaidi sana ibara ya 59 (5) kwa hadhi ya ofisi yake mwanasheria mkuu amepewa hadhi ya ubunge, kwa kifupi ni Mbunge wa JMT.

ukienda zaidi kusoma kwa pamoja sura ya 268 ya sheria ya ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kazi na wajibu wake yaani, the office of the Attorneys General ( Discharge of Duties Act), Cap. 268, hasa kifungu cha 8 1) (a), (section 8 (1) (a) ya sheria hiyo inaeleza kazi mbalimbali za mwanasheria mkuu, ikiwa pamoja na kushauri serikali kuu, serikali za mitaa, wizara mbali mbali, taasisi za serikali, mashirika ya umma.

Nimefanya tafiti kidogo kwenye tovuti yao, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AGCTZ) | Mikataba na Makubaliano, utagundua na utaona wana hadi department (division ya mikataba) imegawanyika katika sehemu tatu yaani; mikataba ya ununuzi wa umma, mikataba ya makubaliano ya kimataifa na mikataba ya uwekezaji wa maliasili.

Je, mwanasheria wa taasisi au wizara ana mamlaka ya kuishauri serikali kuingia kweye mikataba ya kimataifa?

1.
Kulingana na katiba yetu na sheria zetu tajwa hapo juu ni hapana. lakini kumekuwa na mwanasheria anaitwa Hamza Johari, kutwa kuchwa anatolea ufafanuzi kuhusu mikataba walioingia kati ya JMT na Manispaa ya Dubai, lakini kwangu mimi nadhani anatukosea watanganyika, kwa sababu kusoma kwangu sijaona mamlaka yake, au anawajibika vipi kwenye taifa letu la mikataba aliyoiingiza yeye katika nafasi yake, au utueleze ana uhusiano gani na mikataba hiyo?

Je, Spika wa Bunge alikuwa sahihi, kuchukua nafasi ya mwanasheria mkuu bungeni?
2. Jibu ni hapana
, katika kuongoza nchi, kuna mihimmili mitatu, yaani serikali, bunge na mahakama, kwa muktadha huo serikali ilipeleka mkataba ule kwenye mhimili wa Bunge, na kazi ya Bunge ni kuangalia nini, serikali imeleta, je ni kwa manufaa ya nchi na wananchi wake?, na kama wawakilishi wa wananchi, wana wajibika kuangalia maudhui yake na faida zake, kwa kuihoji serikali yaani, (check and balance, )hiyo Spika aliingilia kazi ya serikali, na kwa kuwa ilihusu mikataba na mikataba ni sheria basi ulikuwa ni wajibu ambatano wa mwanasheria mkuu wa serikali kutolea ufafanuzi, kwa nini serikali wameridhia, kifungu fulani wana nini wanatarajia. maana waliokuwa kwenye negotiation ya mkataba huo ndio "wao" kwa maana wenye mamlaka hayo.
kwa hiyo, kwa kuingilia nafasi ya mwanasheria mkuu, spika analitaarifu taifa alichukua, au alikuwepo wakati wanakubaliana (negotiation), na hivyo anajua maudhui ya nini kinachoelezwa.

3. Je, ukimya wa mwanasheria mkuu unamaanisha nini? (mtazamo binafsi)
katika dhana ya uwajibikaji, alipashwa ajihudhuru kwa upendo, si kwa sababu ameshindwa kazi, lakini kwa sababu ya mazingira hayo hapo juu. yaani bungeni na mitaani;

(a) inaonekana hakushirikishwa vizuri kadili ipaswazo kwa mujibu wa katiba na sheria, kutoa ushauri wa kisheria kuhusu mkataba huu, ndio maana sehemu zote ambazo anapashwa kuongea ameaamua kuchagua kukaa kimya, bungeni ni kama alinawa mikono. kuashiria sihusiki na kinachoendelea malizaneni wenyewe.

(b) huku mitaani, Hamza Johari amekuwa ndio mwanasheria mkuu, akitolea ufafanuzi wa kwa nini waliamua kuingia mkataba.

4. Je, nani alimshauri Rais wa JMT kuridhia kuingia makubaliano hayo ya uwekezaji?
Bado Sina Jibu, najua wazi kuwa Rais wetu si mwanasheria, sina shaka lazima atakuwa kaomba ushauri kabla ya kutoa ruhusa ya kuiingiza nchi katika mkataba huu aliomba ushauri wa kisheria,

Je, kama aliyemshauri ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, basi ndio alipaswa kuwa msemaji mkuu wa kadhia yote iliyotufikisha hapa, au kama si yeye nadhani wasiwasi wangu unarudi kwa mwanasheria Hamza Johari, Je ni nani hasa na ana interest gani katika mkataba huu?

5. Nani alaumiwe? na nini kifanyike?
kwanza sitaacha kuwalaumu waandishi wa habari, kwani wametuangusha sana, katika tafiti zote za habari kabla hujaenda site, lazima ujue key informers (nani atakupa habari sahihi?), si kila mtu anapaswa kuulizwa kwenye vitu ambavyo vinaitaji majibu ya moja kwa moja, mpaka sasa nimeona midahalo, magazeti, radio, tv, kwa bahati mbaya sana wanaoalikwa si watu sahihi.

Nimalizie, hapo.
Hongera sana. UMEMENENA KISOMI
 
Back
Top Bottom