Rwandair kuleta ndege 2 za b737/800 aug/sept 2011




Ndio maana Mungu kawapa na watoto wa kike wazuri wenye upendo kama father christmass
Na ni watamu pia. Kilichowaponza kumchagua JK asimamishe maendeleo ya nchi kwa miaka 10 ndicho kinawacost. Mtalikuta train la maendeleo limepack pale Kigoma wakati nyie mko mmelala dar
 
jamani nimeenda kwa rafiki yangu akanieleeza haya mambo nilichukua muda kukubali nikasema Mungu hivi Tanzania umeamua kuitenga kabis ajamani......kampuni ambayo aina hata miaka mitatu inaleta ndege mbili za B737/800 tena ndani ya miezi 2 august na sept uwiiii anyway embu fungua hii web sikuamini

rwandair.com | Ikaze Iwacu


Looking forward to taking delivery of two Boeing 737-800NG in Aug & Sep 2011.
[h=4]The Sky Interior cabin concept will be the first on the African continent...[/h][h=4]Delivery in 41 Days, 6Hrs, 39Mins, and 22secs...
[/h]

2 years ago aliyekuwa balozi wa USA hapo Dar alijitolea kufacilitate deal kati ya ATC na Boeing ili ATC wakopeshe 6 brand new Boeing aircrafts from Seattle. Boeing walikuwa tayari lakini waziri na ATC CEO walitakataa kwa madai kuwa lazima hiyo deal ipitie kwa agent sijui middleman! Boeing walisema wanadeal directly na clients na sio middlemen ama agents......akina Matakka na waziri walikuwa wanataka mshiko! Yule balozi akaona ujinga na akaajiachia. Hatusaidiki!
Ndege ya raisi mnayo na kila siku anasafiri sasa mnataka nini zaidi?
Kuhusu Rwanda, wasingefika hapo walipo kama sio kushikishana adabu, sasa wadanyanyika kuanzia raisi, mawaziri, viongozi, CCM na sisi wananchi woooteee ni kelele na porojo na kulalalama kila kukicha lakini hamtaki kuingia mitaani ili kuleta madadiliko eti sababu mna amani na upole na uvumilivu. Haya kaeni na amani yenu na muendelee KUZIRAI wakati wengine wakijiuzulu
 
we are not fair at all to our beloved TANZANIA.....!
WE ARE THE CHAMPS ..YES CHAMPIONS OF OUR FAILURES YET WE ARE THE CHAMPS OF MALALAMIKO
hebu tujiambie ukweli...!
1.TTCL MOBILE
2.ATCL
3.NYUMBU
4.POSTA CASH
5.POSTAL BANK
Nimetoa mifano michache ambayo wewe na mimi kwa kiwango cha zaidi ya 90% hatushiriki katika kuhakikisha tunavitumia ipasavyo.....NDEGE hatupandi za shirika letu bado tunanyanyua midomo kama kahaba ambaye hakulipwa pesa zake,simu za TTCLMOBILE tunayo lakini bado tunatumia simu ya ROST TAMU huku tunamtuhumu ni fisadi ilhali tunamneemesha, BANK asili inayomilikiwa na TANZANIA kwa zaidi ya 80% hatuitumii lakini bado tunalalamika haina wateja.....!
Sisi ni chanzo cha yote hayo ..lawama tusizitupe kwa wengine .....WE ARE DIRTY ..YES WE ARE....tubadilike, tutvitumie,visipojiendesha TURUSHE MAKOMBORA KULIKO YALE YA TORA BORA
SAMAHANI KWA LUGHA NILIYOTUMIA
 
Dhahab ailiyoporwa Congo imeingia humu janvini, watu wanampigia debe utafikiri wametumwa: BTW- huyu ni fisadi aliyekubuhu na familia yake yaishi maisha ya anasa wakati wananchi wako hohehahe.
Huwezi kulinganisha ufisadi wa Kagame na wa Kikwete. At least Kagame anafanya mambo kwa wananchi yake yanayoonekana matunda yake./ Kikwete amebaki tu kumfanya Riz1 ajulikane kuwa young billionaire na mkiugua anawaleteeni ambulance za bajaj wakati mwenyewe ana ambulance ya kisasa katika msafara wa magari yake. Huwezi kuwalinganisha hawa wawili hata kidogo!
 
Mnaonaje tukachukue nchi yetu kule kivukoni maana nilikuwa congo ukipandisha bei ya mkate mpaka raia watake sio sisi unaamka nauli juu, kisa mafuta soko la dunia wakati d'saalam kila kituo cha mafuta bei kipanga chenyewe, bila kukimbizana hatuheshimiani.
 
Tena ni mpya toka kiwandani siyo mitumba, tatizo la TZ hatuna uTanzania/uzalendo, hatujali maslahi ya taifa hili, unajua hata ungekuwa na mihela kiasi gani ya kupata kwa mikataba mibovu bado hujakwepa fedheha ya Tanzania kuwa ni nchi maskini ambayo kila kitu ni shida, umeme shida, maji shida, chakula shida. kwa sasa hivi Tanzania ni nchi pekee duniani labda ukiacha Sudani ya kusini ambayo haina ndege.

Sijui nchi yangu hii emelaaniwa namna gani, imelala usingizi wa pono, tunabakia kulalamika tu, tuna vitu vingi vya kujivunia ambavyo vingetumika na kutangazwa ipasavyo tungekuwa mbali. Kenya wanatuzidi kwa mbali sana kiuchumi, hawa watu hawana Gesi-sisi tunayo kwa wingi, hawana dhahabu-sisi tunayo kwa wingi, hawana almasi sisi tunayo, tumepakana na nchi nyingi ambazo zipo landlocked kuliko kenya, lakini Mombasa ndo ipo busy kwa mbali sana ukilinganisha na Bandari zetu zote kwa pamoja, yaani Dar, Tanga na Mtwara.

Kwenye utalii ndo usiseme tuna vivutio zaidi kuliko Kenya, lakini watalii wengi wanaokuja Tanzania, huwa wanakuwa kwanza wamepitia Kenya. Sababu ni nini?? kwenye utalii hatuna National carrier. Uwanja wa KIA upo very under utilized, kungekuwa na DIRECT flights za shirika letu la ndege angalau London-KIA, Dubai-KIA, Doha-KIA na kwineko ongezeeni, utalii ungeshamiri sana. haya maua yalimwe Arusha tena karibu na KIA lakini yanasafirishwa kupitia Nairobi.

Angalia magari yanayongia Tanzania kupitia Bandari ya Mombasa kwenye entry za Namanga na Holili, najiuliza viongozi wetu wanafikiri nini??? MUNGU tusaide
watnzania wapewe chawa wajikune hawataki kujikomboa . (ufisadi tu)
 
Nyerere alipofanya kila kitu mali ya umma alitegemea anajenga taifa aina gani? Mali zinakuwa aidha za Tajiri au Serikali hakuna kitu kinachoitwa mali ya umma halafu kikabaki.

Kama kuna shirika ambalo bado ni mali ya umma hutoliona kuendelea kwani kila mtu hapo kuanzia ofisi boi mpa mkurugenzi mpaka bodi ya wakurugenzi na wenyeviti wao watataka wachukuwe chao. Unategemea nini?

Tanzania si tunaona mashirika ya ndege binafsi yanavyoendelea? bora iwe hivyo hivyo. Si lazima kuwa na shirika la umma la ndege ambalo litaliwa na kufa bila ya huruma kama mashirika mengine yote yaliyokufa. Uzi huu huu wa kubinfsisha na awezae afunguwe shirika la ndege hazuiliwi na mtu.
 
jamani hata uda kupewa wageni? du/ wanngepewa machinga wakawezeshwa na benki wngeweza kuendesha hili shirikaa. viongozi nchi hii hatuna.:smow:
 
Si viongozi watendaji, hapana. Nakataa.

Tanzania imeharibiwa kwa misingi mibovu aliyoiweka Nyerere, tukipenda tusipende huo ndio ukweli. Tatizo la Tanzania ni kuwa ukweli tunaukimbia siku zote. Ukweli huwa unauma lakini hubaki kuwa ukweli. Na kama hatujona makosa yetu tuliyonayo kiukweli, basi hata aje kiongozi kutoka mwezini, tutabaki hivihivi.

Tunachotajiwa kufanya kwanza ni kubadili kabisa mfumo wa mitaala ya masomo yetu, ili kila mwanafunzi anaeingia kusoma afundwe kuanzia mdogo kuwa hakuna kitu mali ya umma na hakuna "ndugu" kwa asiye nduguyo. Hayo ndio yanayotuumiza.

Mali zote za umma, kila mtu ndugu yako, tutaendelea hapo?

Kuna watu humu wanaiba, wanakopa wananyang'ganya ili tu aonekane kachangia harusi kiasi kikubwa kuliko mwenzake, yote hiyo imeletwa na u"ndugu" usio na mpango. Halafu kwa kuwa tunaamini kabisa katika mioyo yetu kuwa hakuna kutajirika ila kwa kuiba, kwa sababu tu, mjombako aliiba kwa kuwa alipotoka ilikuwa hakuna mali ya fulani bali ilikuwa ya umma. Basi na wewe ni lazima uibe ukitaka kujenga, na huko unako jenga kuanzia mlinzi mpaka mbebaji wote watakuibia, eti kwa sababu tu wanaona kuwa wewe unaejenga hiyo mali uliiiba. Hiyo ndio Tanzania.

Tumejazwa ujinga miaka yote ya nyerere, bila kufuta huo ujinga hatutoendelea kawe, hata kama siku hizi watu wanajua kuvaa suti, hayo si maendeleo.

Roho mbaya zimetujaa, kila mmoja ana mganga au sangoma wake wa kumsaidia kupata cheo kazini au kumfichia kwa anayoyaiba.

hatuwajibiki, kila siku shaagazi kafa, kesho mama mgonjwa , kesho kutwa jirani kafiwa, inahusu nini katika kazi yote hayo? Hiyo ndio tutaendelea. na yote kwa kuwa tunakale kaujinga kaundugu ndio inafikia mpaka tunadanganyana na kuua ukoo mzima ili tuu upate kupinda kazini.

Na ukiona mtanzania (majority si wote) wakwanza kufika kazini na wa mwisho kuondoka na hana kufiwa wala kuuguwa wala kuuguliwa akaacha kazi, ujue hapo kuna wizi anaufanya.


Ni mengi ya kijinga tulionayo, tuliyorithishwa.
 
Huwezi kulinganisha ufisadi wa Kagame na wa Kikwete. At least Kagame anafanya mambo kwa wananchi yake yanayoonekana matunda yake./ Kikwete amebaki tu kumfanya Riz1 ajulikane kuwa young billionaire na mkiugua anawaleteeni ambulance za bajaj wakati mwenyewe ana ambulance ya kisasa katika msafara wa magari yake. Huwezi kuwalinganisha hawa wawili hata kidogo!
Atleast JK is not trying to slaughter anyody: 'Kayumba/prof mwaikusa! Et al.
 
Back
Top Bottom