Rwandair kuleta ndege 2 za b737/800 aug/sept 2011

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,144
jamani nimeenda kwa rafiki yangu akanieleeza haya mambo nilichukua muda kukubali nikasema Mungu hivi Tanzania umeamua kuitenga kabis ajamani......kampuni ambayo aina hata miaka mitatu inaleta ndege mbili za B737/800 tena ndani ya miezi 2 august na sept uwiiii anyway embu fungua hii web sikuamini

rwandair.com | Ikaze Iwacu


Looking forward to taking delivery of two Boeing 737-800NG in Aug & Sep 2011.
[h=4]The Sky Interior cabin concept will be the first on the African continent...[/h][h=4]Delivery in 41 Days, 6Hrs, 39Mins, and 22secs...
[/h]
 

Attachments

  • tumekuja kuwashika.png
    tumekuja kuwashika.png
    95.4 KB · Views: 238
Hata wazee wetu walisema penye miti mingi hapana wajenzi...wacha waje tu watafute pesa zao wachukue bai...bora tubaki na umasikini wetu maana mafisadi wataongezeka bure.
 
Tena ni mpya toka kiwandani siyo mitumba, tatizo la TZ hatuna uTanzania/uzalendo, hatujali maslahi ya taifa hili, unajua hata ungekuwa na mihela kiasi gani ya kupata kwa mikataba mibovu bado hujakwepa fedheha ya Tanzania kuwa ni nchi maskini ambayo kila kitu ni shida, umeme shida, maji shida, chakula shida. kwa sasa hivi Tanzania ni nchi pekee duniani labda ukiacha Sudani ya kusini ambayo haina ndege.

Sijui nchi yangu hii emelaaniwa namna gani, imelala usingizi wa pono, tunabakia kulalamika tu, tuna vitu vingi vya kujivunia ambavyo vingetumika na kutangazwa ipasavyo tungekuwa mbali. Kenya wanatuzidi kwa mbali sana kiuchumi, hawa watu hawana Gesi-sisi tunayo kwa wingi, hawana dhahabu-sisi tunayo kwa wingi, hawana almasi sisi tunayo, tumepakana na nchi nyingi ambazo zipo landlocked kuliko kenya, lakini Mombasa ndo ipo busy kwa mbali sana ukilinganisha na Bandari zetu zote kwa pamoja, yaani Dar, Tanga na Mtwara.

Kwenye utalii ndo usiseme tuna vivutio zaidi kuliko Kenya, lakini watalii wengi wanaokuja Tanzania, huwa wanakuwa kwanza wamepitia Kenya. Sababu ni nini?? kwenye utalii hatuna National carrier. Uwanja wa KIA upo very under utilized, kungekuwa na DIRECT flights za shirika letu la ndege angalau London-KIA, Dubai-KIA, Doha-KIA na kwineko ongezeeni, utalii ungeshamiri sana. haya maua yalimwe Arusha tena karibu na KIA lakini yanasafirishwa kupitia Nairobi.

Angalia magari yanayongia Tanzania kupitia Bandari ya Mombasa kwenye entry za Namanga na Holili, najiuliza viongozi wetu wanafikiri nini??? MUNGU tusaide
 
You are doing well Kagame! Raisi usiyependa sifa za kijinga, na wala huna safari zisizo kuwa na tija, ulianza na mradi wa ngombe wa maziwa kila kaya na sasa unaleta ndege. Hongera sana, sisi na CCM yetu tutabaki kuwa watazamaji Kagame, we unaakili sana nasikitika kwa nini9 hukuzaliwa Tanzania?
 
CCM chama changu basi twendeni sumbawanga tukatengeneze zile za asili kama hizi za kizungu zimetushinda
 
Tatizo la TZ ni kupeana vyeo kwa undugu hata mtu akiharibu hakuna wa kumuwajibisha
matokeo yake anahamishiwa sehemu nyingine.
angalia kuna waziri yuko kwenye wizara ni ya nne sasa ndani ya miaka hii sita lakini
hajapafomu chochote na bado hata baraza likivunjwa atabadilishwa kuliko aachwe!
the same to viongozi wa ngazi zingine.
kuna ziara hata leo nimeisoma ya rais kuambatana na wafanyabiashara kwenda sehemu mbalimbali
wanatumia kodi za wananchi wakirudi hakuna jipya .......hatuna viwanda..........hawaonyeshi hata kujadili walichojifunza etc etc etc
:mod::mod::mod:
 
You are doing well Kagame! Raisi usiyependa sifa za kijinga, na wala huna safari zisizo kuwa na tija, ulianza na mradi wa ngombe wa maziwa kila kaya na sasa unaleta ndege. Hongera sana, sisi na CCM yetu tutabaki kuwa watazamaji Kagame, we unaakili sana nasikitika kwa nini9 hukuzaliwa Tanzania?

mkuu umesahau tumekuta mradi wa nyumba za wananchi walio na vipato vidogo wanajenga wachina kwa fujo yaani na ameunda tume kupitia walioaly na kabla awajapewa anaenda mwenye kuhakikisha kweli huyu mtu ana kipato cha chini na mwisho wa saini kwenye mkaataba kunajina lake
wataiba majani labda..huyu jama tungepata wawili sidhan tungejaza thread za kina lowassa chenge na azimu.r
 



Ndio maana Mungu kawapa na watoto wa kike wazuri wenye upendo kama father christmass
 
Habari ndo hiyo! Kwa sisi wakristo yesu alijitoa sadaka akapata mateso sana msalabani hii yote ni kwa ajili ya kutukomboa sisi wanadamu. Hata hao wanya Rwanda msione sasa hivi uchumi wao unakua kwa kasi mkafikiri umekuja hivi hivi na wao miaka ya nyuma ufisadi ulikuwa umetapakaa kila sehemu lakini baada ya kutwangana kisawasawa sasa hivi full heshima sasa hivi wanyaRWANDA wote wanaheshimiana kila raia wa Rwanda anauzalendo na nchi yake ndo mana uchumi wao unakua kwa kasi. Hivi nyie mnafikiri waTZ bila KUTWANGANA kwanza hata siku moja hatutaweza kuheshimiana. Sasa hivi kama hauna pesa ujue kwenye hii nchi yetu hauna haki hata kidogo, nchi hii imebaki mikononi kwa watu wenye kipato. TAFAKARI KISHA CHUKUA HATUA.
 
Tena ni mpya toka kiwandani siyo mitumba, tatizo la TZ hatuna uTanzania/uzalendo, hatujali maslahi ya taifa hili, unajua hata ungekuwa na mihela kiasi gani ya kupata kwa mikataba mibovu bado hujakwepa fedheha ya Tanzania kuwa ni nchi maskini ambayo kila kitu ni shida, umeme shida, maji shida, chakula shida. kwa sasa hivi Tanzania ni nchi pekee duniani labda ukiacha Sudani ya kusini ambayo haina ndege. Sijui nchi yangu hii emelaaniwa namna gani, imelala usingizi wa pono, tunabakia kulalamika tu, tuna vitu vingi vya kujivunia ambavyo vingetumika na kutangazwa ipasavyo tungekuwa mbali. Kenya wanatuzidi kwa mbali sana kiuchumi, hawa watu hawana Gesi-sisi tunayo kwa wingi, hawana dhahabu-sisi tunayo kwa wingi, hawana almasi sisi tunayo, tumepakana na nchi nyingi ambazo zipo landlocked kuliko kenya, lakini Mombasa ndo ipo busy kwa mbali sana ukilinganisha na Bandari zetu zote kwa pamoja, yaani Dar, Tanga na Mtwara. Kwenye utalii ndo usiseme tuna vivutio zaidi kuliko Kenya, lakini watalii wengi wanaokuja Tanzania, huwa wanakuwa kwanza wamepitia Kenya. Sababu ni nini?? kwenye utalii hatuna National carrier. Uwanja wa KIA upo very under utilized, kungekuwa na DIRECT flights za shirika letu la ndege angalau London-KIA, Dubai-KIA, Doha-KIA na kwineko ongezeeni, utalii ungeshamiri sana. haya maua yalimwe Arusha tena karibu na KIA lakini yanasafirishwa kupitia Nairobi. Angalia magari yanayongia Tanzania kupitia Bandari ya Mombasa kwenye entry za Namanga na Holili, najiuliza viongozi wetu wanafikiri nini??? MUNGU tusaide


Safi Freeman! Viongozi wetu ni chanzo cha matatizo yote haya, lakini pia mentality (fikra) za jumla za watanzania zipo chini sana. Tumezoea kuchagua viongozi (hasa) marais wasiojua biashara, wasiokuwa aggressive, wasiojali, wasio na upeo wala uchungu na nchi yetu, na haya ndio matokeo yake.

Ni wakati sasa wa kuchagua watu wanaojua uchumi, biashara, uongozi, watu wenye upeo na aggressiveness ya kutosha bila hivyo tutaendelea kubaki nyuma zaidi
 
Hawa jamaa watatufunika vibaya sana na tutabaki kulalamika tu!!
We are not a match to Rwanda...infact walishatufunika mara tu baada ya genocide. Fuatilia international development index..governance, economic growth (siyo size),quality of livehood etc ...sisi viongozi wamekalia viduku na mipasho bungeni see where we are now ...tunapambana na nchi zenye vita kwa kwenda mbele etc kama Somalia
 
You are doing well Kagame! Raisi usiyependa sifa za kijinga, na wala huna safari zisizo kuwa na tija, ulianza na mradi wa ngombe wa maziwa kila kaya na sasa unaleta ndege. Hongera sana, sisi na CCM yetu tutabaki kuwa watazamaji Kagame, we unaakili sana nasikitika kwa nini9 hukuzaliwa Tanzania?
Dhahab ailiyoporwa Congo imeingia humu janvini, watu wanampigia debe utafikiri wametumwa: BTW- huyu ni fisadi aliyekubuhu na familia yake yaishi maisha ya anasa wakati wananchi wako hohehahe.
 
Tanzania kisiwa cha amani, watanzania wanajua na dunia inajua!
Tanzania tumepiga hatua kubwa kimaendeleo miaka 50 ya uhuru, watanzania wanajua na dunia inajua!
Tumefanya maamuzi magumu, shule za kata, UDOM, Kujiuzulu cabinet,watanzania wanajua na dunia inajua!
Tumeuni nembo ya kisasa ya shirika letu la Ndege, watanzania wanajua na dunia inajua!
Hivi karibuni tutapata chenji ya rada toka Uingereza, watanzania wanajua na dunia inajua!
Tumeamua kujivua gamba, Rostam kaondoka na wengine wanakuja, watanzania wanajua na dunia inajua!

Ni mtazamo tu, msikasirike wadau, hii ndio Tanzania zaidi ya uijuavyo.
Aliye na macho haambiwi tazama, wasio taka kuishi Tanzania waende Rwanda au Somalia kwenye vita, watanzania wanajua na dunia inajua!
 
Back
Top Bottom