Humble African
JF-Expert Member
- Jul 28, 2013
- 4,781
- 14,442
- Thread starter
- #81
Umeeleza vizuri mkuu...naona unataka kusema UKWELI lakini unasita.
..na ukweli wenyewe ni kwamba waTZ tukae mkao wa kula HASARA na kutoa RUZUKU kwa ATCL.
..tayari tumeshachoma Usd 100++ million kununua hizo ndege. Lakini bado tunataka kuongeza na ruzuku ya mwaka hadi mwaka. Je, hiyo ni busara, au kubana matumizi?
..Tanzania ilishaweza kuongeza idadi ya Watalii bila kuwa na shirika letu la ndege. Tunapata watalii wengi kuliko Kenya yenye shirika la ndege.
..Tulichotakiwa kufanya ni kusumbua bongo zetu tuongeze idadi ya watalii bila kujiingiza kwenye mradi wa hasara kama umiliki wa shirika la ndege.
..Binafsi siamini kama maeneo yote ya utalii yameboreshwa kuweza kupokea watalii. Vivutio vilivyoko kusini bado havina miundombinu ya kuweza kupokea watalii wengi. Zaidi, vivutio hivyo havijatangazwa vya kutosha.
..Again, binafsi naangalia OPPORTUNITY COST ya kununua hayo madege. Naamini mabilioni hayo yalipaswa kuwekezwa kwa waTz wenyewe ktk sekta ambazo zinagusa watu wengi na kuleta faida ya moja kwa moja.