Maisha haya! Kwa siasa za kiafrika politics its all about "influence" and not "facts" once ukijitokeza una facts, logics, and innovative idea unaonekana traitor and snitch asie mzalendo lakini nafahamu siasa na facts havikai sehemu moja na Daima siasa inapoingilia dirishani kwenye nyumba uhalisia unatokea mlangoni..hivi havijawai kukaa sehemu moja labda kwa wenzetu wa majuu ambao wamepevuka tangu zamani kiakili.
Hili suala la kununuliwa kwa Dreamliner limemebwa zaidi kisiasa kuliko uhalisia na hata mkuu wa kaya alisema dhumuni lingine pia mbali na mingine yote ilikuwa ni kuondoa aibu..! Loh! Siasa ilitawala then uhalisia ukaruka dirisha ukaondoka zake maana hawa wawili ni Nuru na Giza kamwe akiwepo mmoja sharti mwingine aondoke. Baada ya kununuliwa Dreamliner siasa aliingilia dirishani na uhalisia utakuwa ushatutoroka na ndio maana hata mtandaoni tunabishana kwa siasa bila uhalisia wa mambo.
Nimebahatika kufahamu mechanism ya haya mawili ndio maana nakuletea uhalisia huu toka Rwandair ili tujue kwamba kuanzisha successful airline ni rahisi sana kusema ili utekelezaji wake ni Pasua kichwa...kwa hizi rekodi fupi zilizovuja zinathibitisha Rwandair ilipata hasara kwa miaka minne mfululizo kuanzia 2013.
Kwenye hii picha hapa chini inaonyesha statement of comprehensive income ya Rwandair kwa mwaka 2013-2014 ambapo kwa mwaka 2013 ilipata hasara ya dola milion 48 na serikali ikatoa dola milion 54 ili kuipiga jeki shirika liendelee kufanya kazi na waendelee kupata national prestige wakati kihualisia wanagugumia machungu. Nasisitiza juhudi zetu sisi wakosoaji wa hili suala sio kudidimimiza juhudi za serikali bali kutoa angalizo kwamba vita tulivyochagua kuvipigana ni vita vigumu na wanaoshinda ni wale walio na huge capital, innovative idea, resourceful, strong determined ambao ni wachache sana hapa afrika na Dunia.
Ila kwa vile hatukujiandaa vya kutosha kwenye hili...sio siri I can't see at the end of the tunnel.
Picha zingine za statement of comprehensive income nazileta kwenye comments hapa chini.
Stick around!
View attachment 809296