Umeandika mengi sana lakini umeignore kitu kimoja kwamba mashirika kama Qatar airline, fly Emirates haya yameanzishwa kwa motives za kuburst uchumi via logic and facts kuhusu hii business na kwa uchumi wao wale waarabu hata wapate hasara miaka 100 haiwezi kuyumbisha wala kufikisha uchumi wao.
Tofauti na sisi tumenunua ndege kwa political motives na sio economical reasons ndio maana hatujatumia facts wala logic katika kufikiria outcomes.. Na ndio sababu ndege imeandikwa "hapa kazi tu" huku ya Kenya ikiandikwa "Serengeti plain" its way more political and prestige motives than economical.
We are doomed to fail sir!
Mkuu mbona nimeelezea economic logic za kuwa na shirika la ndege la ATCL kwa kirefu sana? Napata hisia kuwa husomi majibu hoja zangu unajibu tu kusisitiza msimamo wako ule ule. Au kama unasoma vizuri hoja zangu huelewi au hutaki kuelewa. Yaani unaona waarabu ndio wanajua economic logic na sisi hatujui. Nimekuelewesha kwamba waarabu hawapati hasara sababu ungawa mashirika yao hayaingizi faida na yanatumia ruzuku, multiplier effect yake ni kubwa kwenye kukuza miji yao na sekta nyingine za maendeleo.
Kuhusu hoja yako ya mambo ya siasa haina mashiko. Sababu Dreamliner hiyo hiyo imeandikwa "The Land of Kilimanjaro". Kumbuka miundombinu yetu mikubwa ina majina ya hao hao wanasiasa (Nyerere Bridge, Jakaya Kikwete Heart Institute etc). Je, unashauri majina haya yasitumike? By the way, kauli ya "Hapa kazi tu" ingawa imeanzishwa na wanasiasa inabidi isisitizwe kila mahali sababu watanzania wengi wavivu, waoga (hawana big ambitions) na wana mawazo hasi sana (negativity).