BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,383
- 8,132
Utafiti wa #UmojaWaMataifa (UN) na #BenkiYaDunia (WB), umeonesha maisha marefu yanategemea mambo 3 makuu: Maumbile, Jinsia, na Mtindo wa Maisha unaojumuisha Usafi, Chakula Bora na Mazoezi, Upatikanaji wa Huduma Bora za Afya, na Viwango vya Uhalifu.
Hadi kufikia mwaka 2023 umri wa Binadamu kuishi ni miaka 70 kwa #Wanaume na miaka 76 kwa #Wanawake sawa na wastani wa miaka 73.4 huku matarajio ya maisha yakitofautiana kulingana na eneo au Nchi. Kwa #Afrika umri wa chini ni miaka 57.7 na miaka 82 kwa #Ulaya.
Umri wa kuishi umeongezeka kutoka miaka 5.5 kati ya mwaka 2000 na 2016 hadi miaka 10.3 kwenye baadhi ya Nchi za Afrika. Sababu ni Kuboreshwa kwa kiwango cha Maisha ya Watoto wenye Miaka 0-5 na upatikanaji wa Matibabu ya kurefusha maisha kwa wenye #VVU na #UKIMWI.
DATA: UMOJA WA MATAIFA/ BENKI YA DUNIA