Imamu akamatwa kwa tuhuma za uhalifu Geita

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,208
4,705
Wadau hamjamboni nyote

Taarifa hapo chini

JESHI la Polisi mkoani Geita linamshikilia Imam wa msikiti wa Nyankumbu mjini Geita, ambaye pia ni mwalimu wa madrassa, Abdulrahman Yassin akituhumiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari mjini Geita na kukanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Imam huyo ametekwa na watu wasiojulikana, bali yeye na wenzake walikamatwa na jeshi la polisi.

“Kutokana na aina ya tuhuma alizonazo, kulikuwa na watuhumiwa wengine ambao bado hawajakamatwa, hivyo suala la kukamatwa kwake ndio maana hatukuliweka wazi. “Lakini baada ya kukamilisha ukamataji wa timu nzima ambayo ilikuwa inakabiliwa na tuhuma hizo, tumeamua tuliweke wazi kwamba Imam huyu anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

“Uchunguzi unaendelea, ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili hususani kujihusisha na matukio ya kihalifu,” amesema Kamanda.

Habari Leo
 
Imamu alikuwa anatekeleza masharti ya mfungo wa Ramadhan

FREE IMAMU 📢 FREE IMAMU 📢 FREE IMAMU 📢 FREE IMAMU 📢 FREE IMAMU 📢 FREE IMAMU 📢 FREE IMAMU 📢 FREE IMAMU 📢 FREE IMAMU 📢 FREE IMAMU 📢 FREE IMAMU 📢 FREE IMAMU 📢 FREE IMAMU 📢 FREE IMAMU 📢 FREE IMAMU 📢
🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom