Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,889
Tunapiga vita rushwa hadi tumeiundia taasisi. Na wengine wanasema nchi za Africa haziendelei sababu ya rushwa. Hili suala limefanyiwa utafiti na limeonekana halina ukweli. Imeonekana kuwa mtu anapokula rushwa na kuwekeza kwenye uchumi huo huo kunakuwa hakuna madhara yoyote ya maana kwenye uchumi.
Tatizo kubwa kwenye uchumi wa Africa ni utoroshwaji wa fedha. Viongozi wengi wa Africa wamekuwa wakiiba pesa na kwenda kuwekeza huko Ulaya au kuzitunza mabenki ya nje. Hapo wanaenda kukuza uchumi wa nchi hizo na kudhoofisha huku. Hili jambo linaathari kubwa sana kwa uchumi kuliko rushwa.
Matajiri wakubwa nao wamekuwa wakihamisha fedha nyingi kwenda nje ya nchi. Mambi haya yanaathari kubwa kiuchumi kuliko rushwa.
Pengine sasa PCCB waongezewe nguvu kubwa ili waweze kupambana na utoroshaji wa pesa, huo ndio moja ya adui wakubwa wa maendeleo yetu.