Rufaa ya Babu Seya, tumuombee atoke?

Hakimu Mkazi Kisutu, Addy Lyamuya alitoa hukumu kwa mwanamziki huyo pamoja na watoto wake kwa kutumia mawazo yake binafsi.

Katika rufani hiyo, Nguza (babu Seya) pamoja na watoto wake - Papi Ngunza, Nguza Mbangu na Francis Nguza - wameiomba mahakama hiyo, kupitia mwenendo mzima wa ushahidi uliopelekea wao kutiwa hatiani na kusababisha kuhukumiwa kifungo hicho.

Wakili Mabere Marando ambaye anawatetea washitakiwa hao, aliwasilisha hoja hizo mbele ya Jopo la Majaji watatu lililokuwa likiongozwa na Nathalia Kimaro pamoja na wenzake ambao ni Jaji Mbarouk Salim Mbarouk na Jaji Salum Massati.

Marando alidai kuwa Babu Seya alikuwa na mpenzi wake aliyemtaja kwa jina la Farida ambaye mara baada ya kuachana alimuambia kuwa atamkomesha ambapo alidai kuwa kunauwezekano kesi hiyo ikawa ni kisasi cha mwanamke huyo ambaye alitoa vitisho hivyo.

Aliendelea kudai kuwa kunauwezekano wa Farida kuwafundisha watoto hao wanaodaiwa kubakwa, kusema uongo Mahakamani ili kuweza kumfunga Babu Sey na wanawe kama kisasi alichodai kumlipia.

Awali Marando alidai Mahakamani hapo kuwa upande wa utetezi unaondoa sababu za kutaka rufani hizo ambazo ni sababu ya 1,2,3,5,6,7,8,11,14 na 15 ambapo alidai kuwa katika rufani hiyo wataanza na sababu namba tisa kutokana na misingi ya kisheria.

Alidai kuwa sababu hiyo inaeleza maelezo ya anayeitwa Mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi ambapo alidai kuwa mujibu wa sheria za motto kutoa ushahidi Hakimu ananatakiwa kumuhoji kabla ya kutoa ushahidi wake ili aweze kuona kama motto anauelewa gani juu ya kiapo cha ushahidi.

Marando alidai kuwa katika rufani ya awali katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam, nchini ya Jaji Thomas Mihayo alisema kuwa utaratibu uliokuwa umetumiwa na hakimu aliyekuwa ametoa hukumu hiyo ilikuwa na makosa kutokana na watoto ambao walitoa ushahidi kutohojiwa kabla ya kutoa ushahidi wao.

Alidai kuwa mahojiano ya awali na mtoto anayetoa ushahidi ni ili kupata maamuzi na kujua kama mtoto anajua maana ya kiapo ambapo mahojiano hayo baina ya hakimu na mtoto yanatakiwa kuhojiwa.

"Kwa kutozingatia mambo hayo ushahidi ambao utakuwa umetolewa na mtoto huyo utakuwa batili na hauna maana yoyote," alidai Marando.

Aliongeza kuwa muelekeo wa Jaji Mihayo aliyesikiliza rufani hiyo kwa mara ya kwanza haukuwa mzuri kutokana na sheria mbalimbali alizozitumia kugongana ambapo alidai kuwa kutokana na hali hiyo Jaji huyo alifanya kosa kisheria.

Wakili huyo alidai kuwa mashahidi 10 kati ya tisa wa upande wa Jamuhuri ambao walitoa ushahidi wao hawakuapishwa wala kuangalia uwezo wao kama wanaelewa maana ya kiapo.

Pia alidai kuwa katika rufani iliyosikilizwa na Jaji Mihayo alisema kuwa hakimu aliyetoa hukumu hiyo kwakuangalia ushahidi wa pande mbili ambapo alidai kuwa Jaji huyo alikosea kwakua ushahidi wa utetezi haukuangaliwa vyema.

" Katika nyaraka rejea zilizotumiwa na hakimu aliongeza mawazo yake binafsi kutokana na kupingana na maelezo ya mashahidi, katika ukurasa wa 532 mstari wa saba katika hukumu hii, hakimu anapingana na shahidi aliyejitambulisha kwa jina la Lubaba ambaye mama yake ni Mzaramo na baba yake Mkongo.

"Lakini katika maelezo ya hakimu anaonyesha kijana huyo ni Mzaramo wakati si kweli, hiyo yote inaonyesha jinsi gani hakimu alivyokuwa akiweka mawazo yake binafsi," alidai Marando.

Marando alidai kuwa kwa muda wa miaka 30 ambayo amefanya kazi ya uwakili hajawahi kuona hukumu ya namna hiyo ambayo hukumu inatolewa kwa kufuata mawazo ya hakimu badala ya ushahidi wa pande mbili.

Aliendelea kudai kuwa hakuna ushahidi ambao ulionesha mshitakiwa wa pili alibaka au kulawiti kabla au baada ya kufanya safari zake za kimuziki katika mikoa ya Mwanza na Arusha ambapo alisema kuwa hakimu aliweza kuweka mawazo yake binafsi ili kuwezesha mshitakiwa huyo kuwa na hatia ya kumfunga gerezani.

"Mbali na hayo mshitakiw ahuyo wa pili alidai kuwa kati ya Agosti na Septemba alikuwa akirekodi albamu yake na mwanamuziki Lady Jee dee , lakini badala ya hakimu kuandika maelezo hayo na matokeo yake aliandika ‘So what?'," alidai wakili huyo.

Alidai kuwa hakimu huyo hakuandika maelezo ya mashahidi wa upande wa utetezi na badala yake aliandika idadi ya mashahidi ambao walifika kutoa ushahidi wa upande wa utetezi ambapo wakili huyo alihoji hali hiyo iliyofanywa na hakimu huyo.

Wakili huyo alidai kuwa kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na watoto ambao wanadaiwakufanywa vitendo vya ubakaji na kulawitia walitaja baadhi ya watu ambao hawakuweza kuitwa na upande wa mashitaka kufika Mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi wao.

Alidai kuwa watoto hao walimtaja Mangi ambaye anauza duka ambalo lipo karibu na nyumbani kwa Babu Seya ambaye anadaiwa kuona watoto hao wakati wakiingia na kuchukuliwa na mshitakiwa huyo wa kwanza na pia anadaiwa kusikia wakati watoto hao wakilia wakati wakifanyiwa vitendo hivyo.

Pia mbali na Mangi pia ilidai kuwa watoto hao walimtaja dada na bibi ambao walikuwa wakikutwa katika nyumba hiyo ambapo Marando alihoji kutokuitwa kwa watu hao kufika kutoa ushahidi ili kuweza kuthibitisha madai hayo.

"Kitu cha kushangaza zaidi ni madai ambayo yalitolewa kuwa watoto hao walifanyiwa vitendo hivyo tarehe 11 Oktoba wakati siku hiyo ilikuwa ni Jumamosi na pia mshitakiwa wa kwanza alikuwa amekamatwa na katika maelezo ya watoto hao inadaiwa kuwa walikuwa wakifanyiwa vitendo hivyo wakati wakitoka shule.

"Je siku hiyo ya jumamosi mbona haikutajwa wakati maelezi yanadai kuwa walifanyiwa siku za katikati ya wiki, Jamuhuri ingeweza kufanya uchunguzi ili kuweza kubaini mtu ambaye aliweza kuwabaka watoto hao na si kama jinsi inavyodaiwa," alidai.

Alidai kuwa baadhi ya shahidi mtoto alishindwa kumtambua Babu Seya na mwingine alikanusha kubakwa na mshitakiwa wa 3 na 4 ambapo alidai kuwa hakimu aliandika kuwa kutokana na watoto hao kujuana alihisi kuwa ni lazima watoto hao walibakwa licha ya watoto hao kutothibitisha.

Aliongeza kuwa katika kielelezo kilichotolewa na Hospitali ya Mwananyamala kilidai kuwa mtoto mmoja aliambukiza Kisonono ambapo washitakiwa hao kupitia mawakili wao waliomba kwenda kuwapima washitakiwa hao ili kuweza kuona ni mshitakiwa yupi aliyekuwa amemuambukiza ugonjwa huo wa zinaa.

Alidai kuwa licha ya ombi hilo upande wa Jamuhuri ulikataa kuwapeleka washitakiwa hospitali kwa ajili ya kuweza kuwapima ugonjwa huo ambapo alidai kuwa mtoto mwingine katika maelezo yake alidai kuwa alilazimishwa na Babu Seya kumkamua vipele vilivyokuwa katika sehemu zake za siri vilivyokuwa vikitoa usaha na maji.

Hata hivyo wakili huyo alidai kuwa upande wa Jamuhuri haukuwa tayari kuwafikisha watuhumiwa hao katika kituo cha afya ili kuweza kuthibitisha madai hayo yaliyokuwa yamedaiwa.

"Mshitakiwa wa nne ambaye alikuwa ni mwanafunzi naye pia anadaiw akushiriki katika vitendo hivyo lakini upande wa Jamuhuri haukuwahi kumuita Mkuu wa shule ya sekondari ya Mbezi ambayo alikuwa anasoma ili kuweza kuthibitisha kama mwanafunzi wake alikuwa hafiki shule.

"Lakini mambo yote hayo hayakuweza kufanywa wakati kila mmoja anaelewa kuwa muda ambao anatoka mwanafunzi huyo watoto hao wanakuwa tayari hawapo lakini hazikuweza kufanyika jitihada mbalimbali," alidai.

Alidai kuwa katika jarada la kesi hiyo, mashitaka mawili yalikuwa yakiingiliana ambapo shitaka moja lilidai kuwa watoto hao walifanyiwa vitendo hivyo Oktoba ambapo shitaka jingine lilidai kuwa watoto hao walifanyiwa vitendo vinvyo kwanzia April hadi Oktoba.

Alidai kuwa katika maelezo ya mashahidi hakuna shahidi aliyedai kuwa alifanyiwa vitendo hivyo kati ya Aprili hadi Julai na kwamba kwa kipindi hicho ambacho kimetajwa mshitakiwa wa 2 na 3 walikuwa wakishinda katika kambi yao ya mazoezi ya FM Academy.

Naye wakili wa upande wa Jamuhuri uliokuwa ukiongozwa na Justuce Mlokozi alikili watoto hao kutorekodiwa na pia kutofanyiwa kiapo ambapo alidai kuwa Mahakama iliegemea ushahidi wa Jamuhuri na kwamba hata kama kulikuwa na makosa madogomadogo yanaweza kutibika chini ya sheria namba 388 ya mwenendo wa mashahidi.

Mlokozi alidai kuwa waliamua kuwaleta watoto katika ushahidi huo kutokana na wao ndio walikuwa walengwa zaidi na wakati wakifanyiwa kitendo hicho hakuna watu wengine waliokuwa wakiona.

Aliendelea kudai kuwa kuhusu kutofautiana kwa miezi katika jarada la kesi hiyo alidai kuwa hakukuw ana tarehe maalum ambayo watoto hao wlaifanyiwa vitendo hivyo na kwamba walikuwa wakifanyiwa kwa nyakati tofauti.

Aliongeza kuwa kuhusu kusafiri kwa mshitakiwa wa 2 alidai kuwa hiyo si hoja kuwa hajatenda kosa ambapo alidai kuwa anaweza kuwafanyia kipindi ambacho anakuwa hapa jijini Dar es Salaam na kudai kuwa kuhusu Farida haiwezekani kuwafundisha watoto wote kusema uongo kama inavyodaiwa na utetezi.

Mjisomee maelezo hayo hapo juu hawa wanatoka kumbe sheria zilipindishwa.
 
Mjisomee maelezo hayo hapo juu hawa wanatoka kumbe sheria zilipindishwa.

Mpwa hiyo ni kwa mujibu wa Wakili wa upande wa Utetezi(Marando),tumsubiri wakili wa Jamhuri naye atakuja na nini...kadiri siku zinavyoenda tutaona na kusikia mengi..
 
Mpwa hiyo ni kwa mujibu wa Wakili wa upande wa Utetezi(Marando),tumsubiri wakili wa Jamhuri naye atakuja na nini...kadiri siku zinavyoenda tutaona na kusikia mengi..

Wakili wa Jamhuri kachemka kabisa si unajua walivyo vilaza mawakili wa serikali yaani kachemka kabisa hebu angalia hapa kashindwa kuzipangua hoja.

Naye wakili wa upande wa Jamuhuri uliokuwa ukiongozwa na Justuce Mlokozi alikili watoto hao kutorekodiwa na pia kutofanyiwa kiapo ambapo alidai kuwa Mahakama iliegemea ushahidi wa Jamuhuri na kwamba hata kama kulikuwa na makosa madogomadogo yanaweza kutibika chini ya sheria namba 388 ya mwenendo wa mashahidi.

Mlokozi alidai kuwa waliamua kuwaleta watoto katika ushahidi huo kutokana na wao ndio walikuwa walengwa zaidi na wakati wakifanyiwa kitendo hicho hakuna watu wengine waliokuwa wakiona.

Aliendelea kudai kuwa kuhusu kutofautiana kwa miezi katika jarada la kesi hiyo alidai kuwa hakukuw ana tarehe maalum ambayo watoto hao wlaifanyiwa vitendo hivyo na kwamba walikuwa wakifanyiwa kwa nyakati tofauti.

Aliongeza kuwa kuhusu kusafiri kwa mshitakiwa wa 2 alidai kuwa hiyo si hoja kuwa hajatenda kosa ambapo alidai kuwa anaweza kuwafanyia kipindi ambacho anakuwa hapa jijini Dar es Salaam na kudai kuwa kuhusu Farida haiwezekani kuwafundisha watoto wote kusema uongo kama inavyodaiwa na utetezi.

katika Yote, inawezekanaje watu wazima wanne wakawaingilia watoto wa miaka kati ya sita na nane mbele na nyuma, kisha wakatembea ?
hakika miaka yote yakuhukumiwa babu seya na vijana wake hili ndilo swali ambalo mimi naomba wana sayansi watuweke wazi hapa//
 
Mahakamani hakuna haki bali kuna sheria! Ngoja tuone Bw Marando atakavyo spin hii kesi! Hivi Nyange kwa nini alijitoa? Kwa nini Marando alibadili maelezo ya rufaa ya mwanzo ambayo Nyange aliisubmit mahakama ya rufani?
 
hakika miaka yote yakuhukumiwa babu seya na vijana wake hili ndilo swali ambalo mimi naomba wana sayansi watuweke wazi hapa//

Mkuu soma hapo hoja za Marando nashangaa Mahakama ilikataa kwenda kuwapima washitakiwa inasemekana kuna mtoto alikuwa na gonjwa la zinaa lakini washitakiwa hawakupimwa ili mahakama iweze kujiridhisha. Kuna mambo mengi Marando kayaongea.
 
katika Yote, inawezekanaje watu wazima wanne wakawaingilia watoto wa miaka kati ya sita na nane mbele na nyuma, kisha wakatembea ?
hakika miaka yote yakuhukumiwa babu seya na vijana wake hili ndilo swali ambalo mimi naomba wana sayansi watuweke wazi hapa//

Kwani unadhani kesi ilianzaje? Si baadhi ya hao watoto walikuwa wanatembea tofauti ndio wazazi/walezi wakashituka!
 
Mkuu soma hapo hoja za Marando nashangaa Mahakama ilikataa kwenda kuwapima washitakiwa inasemekana kuna mtoto alikuwa na gonjwa la zinaa lakini washitakiwa hawakupimwa ili mahakama iweze kujiridhisha. Kuna mambo mengi Marando kayaongea.

Hiyo hoja bado isingekuwa na nguvu. Mtoto kuwa na gono na mtuhumiwa kuwa na gono peke yake haitoshi kuthibitisha kwamba mtuhumiwa ndio amemwabukiza. What if kama kuna mtu mwingine alikuwa pia anavichezea hivyo vitoto?
 
Mkuu soma hapo hoja za Marando nashangaa Mahakama ilikataa kwenda kuwapima washitakiwa inasemekana kuna mtoto alikuwa na gonjwa la zinaa lakini washitakiwa hawakupimwa ili mahakama iweze kujiridhisha. Kuna mambo mengi Marando kayaongea.
Yeah nimesoma Fidel80
Alichoshangaa Marando ambacho hajawahi kukiona miaka 30 ya uwakili wake ni hukumu ya hovyo kama hii,kuna mtoto mmoja alibakwa hadi kutoka damu, lakini kuna taarifa ya daktari inasema alikuwa bado bikira.
sasa kali zaidi ni kua ile report nzima ya daktari wa Mwananyamala serikali kwa kushirikiana na mahakama ya kisutu kwa sababu wanazozijua wao waligoma kuiweka wazi kwa mawakili wa utetezi kina nyange, kisha Lyamuya akatumia ujuzi wake kutoa hukumu.
bado nashangaa kweli mtoto wa miaka sita umuingilie mbele na nyuma anewaje kutembea ?
 
Kwani unadhani kesi ilianzaje? Si baadhi ya hao watoto walikuwa wanatembea tofauti ndio wazazi/walezi wakashituka!
nilibahatika kusoma sehemu ya hukumu hiyo miaka miwili nyuma, mzazi wa kwanza aligundua baada ya kuhisi harufu ya mtoto wake, kwa maana tayari gonjwa la zinaa lilikua limemla, maana yake si tatizo la siku moja, inadaiwa ilikua kama wiki ya nne tangu kufanyika kwa unyama huo.
bado hakua mtoto mmoja, walikua zaidi ya sita, kweli wazazi sita wate walishindwa kugundua hadi wiki ya nne /
bado nashangaa waliwezaje kutembea pamoja nakukandamizwa mbele na nyuma. ?
 
Mmmh sheria ipo tusubiri lolote laweza kutokea
pamoja na yote ipo nafasi ya kujadili na kitu cha kujifunza katika sakata lote...kama usemavyo nataka kuona ninini ambacho mahakama itaamua, ila kipo kitu kinanisisimua
waliwezaje kutembea baada ya kulawitiwa na kunajisiwa ?
 
Mpwa hiyo ni kwa mujibu wa Wakili wa upande wa Utetezi(Marando),tumsubiri wakili wa Jamhuri naye atakuja na nini...kadiri siku zinavyoenda tutaona na kusikia mengi..
Balantanda we uko wapi? mahakama imefunga rufaa hii, hakuna maelezo mengine kutoka kwa utetezi na wala kwa jamuhuri, kinachosubiliwa ni maamuzi ya hakimu tu.
 
nilibahatika kusoma sehemu ya hukumu hiyo miaka miwili nyuma, mzazi wa kwanza aligundua baada ya kuhisi harufu ya mtoto wake, kwa maana tayari gonjwa la zinaa lilikua limemla, maana yake si tatizo la siku moja, inadaiwa ilikua kama wiki ya nne tangu kufanyika kwa unyama huo.
bado hakua mtoto mmoja, walikua zaidi ya sita, kweli wazazi sita wate walishindwa kugundua hadi wiki ya nne /
bado nashangaa waliwezaje kutembea pamoja nakukandamizwa mbele na nyuma. ?
Inji hii bwana, mtu anakuweka ndani hivi hivi!!!!! malengo mangapi yamehalibiwa? kama watoto walikuwa wana harufu mbona watuhumiwa hawakupimwa? inauma saaana bwana
 
mambo ya babu seya ndiyo yale yale ya liyumba................kikwete nyuma yao................watajuuuuuta kumjua.........kwani mmesahau tule tustori tunato muhusisha jk na hawa jamaaa mbona mnajifnaya mmesahau sasa hivi..........
 
pamoja na yote ipo nafasi ya kujadili na kitu cha kujifunza katika sakata lote...kama usemavyo nataka kuona ninini ambacho mahakama itaamua, ila kipo kitu kinanisisimua
waliwezaje kutembea baada ya kulawitiwa na kunajisiwa ?[/QUOTE

amka2.gif

MAWAKILI wanaomtetea mwanamuziki mahiri wa muziki wa dansi nchini, Nguza Viking maarufu ‘Babu Seya’ na wanawe watatu, wameiomba mahakama kuwaachia huru warufani kwa kuwa kesi hiyo ilikuwa ya kupangwa.
Sambamba na hilo, mawakili hao; Mabere Marando na Hamidu Mbwezeleni, walieleza kuwa tangu waanze kazi ya uwakili miaka 30 iliyopita, hawajawahi kuona hukumu ya ovyo kama hiyo.
Mawakili hao walieleza hayo jana mbele mbele ya jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Nataria Kimaro, walipokuwa wakiwasilisha sababu za kupinga rufaa ya Mahakama Kuu iliyolewa na Jaji Msaafu, Thimas Mihato na hukumu iliyotolewa na Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Addy Lyamuya ambao wote walitia hatiani kwa makosa ya kubaka.
Majaji wengine wanaounda jopo hilo ni Salum Massati na Mbarouk Mbarouk.
“Waheshimiwa majaji, sisi tunasema jaji na hakimu huyo walikosea kisheria, kwani sheria inaitaka mahakama kabla haijaanza kuchukua ushahidi wa mtoto ni lazima ijiridhishe mtoto huyo ana akili timamu na anaelewa maana ya kiapo na kisha irekodi hayo kwenye jalada la kesi, lakini Hakimu Lyamuya hakufanya hivyo.
“Mashahidi 10 ambao ni watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 6-8 ambapo upande wa mashitaka ulidai walibakwa na kulawitiwa na warufani, walipofika Mahakama ya Kisutu kutoa ushahidi wao hawakuhojiwa na wala mahakama haikujiridhisha kama wana akili timamu, kwa sababu hiyo tunasema kwamba ushahidi wa watoto hao ni batili na tunaliomba jopo lenu lisiukubali,” alidai Marando.
Marando alidai kuwa wakati akitoa hukumu hiyo, Hakimu Lyamuya aliandika maoni yake binafsi ambayo yanapishana na mashahidi wa upande wa utetezi, kitu ambacho kinapingana na sheria za nchi.
“Katika hukumu hiyo utaona wazi hakimu anabishana na shahidi baada ya kumbishia shahidi huyo kwamba si Mzaramo, wakati shahidi huyo aliiambia mahakama mama yake ni Mzaramo na baba yake ni Mkongo... haya ni mambo madogo, lakini yanaonyesha ni jinsi gani hakimu alivyopuuza ushahidi wa upande wa utetezi,” alieleza na kuongeza:
“Waheshimiwa majaji sijawahi kuona hukumu kama hii kwa miaka 30 tangu nianze kazi ya uwakili, kwani sote tunachojua maoni ya hakimu katika hukumu yanaandikwa pembeni, lakini katika hukumu hii hakimu ameweka maoni yake,” alidai Marando na kusababisha watu kuangua vicheko.
Akimuelezea mrufani Papi Kocha, alidai kuwa mrufani huyo alimweleza katika kipindi hicho alikuwa mikoani kwa ziara za kikazi, lakini hakimu Lyamuya katika hukumu yake akaweka mawazo yake kwa kusema hata kama alikuwa safari anaweza kutenda makosa hayo.
“Lakini majaji katika rufaa ya Mahakama Kuu hakuna ushahidi uliotolewa unaoonyesha warufani walibaka... hayo yalikuwa ni mawazo ya hakimu kwamba lazima Babu Seya na watoto wake waende gerezani, narudia tena sijawahi kuona hakimu wa aina hii na hukumu ya aina hii ambayo hakimu aliamua kuweka maoni yake binafsi.
“Ni wajibu wa mahakama kutafakari ushahidi wa utetezi hata kama hauna uzito, sasa huyu Lyamuya katika hukumu yake amewataja mashahidi wa utetezi waliokuja kutoa ushahidi bila kueleza mashahidi kwa mapana walieleza nini,” alidai.
Aidha, alidai mmoja wa mashahidi wa upande wa upande wa mashitaka ambaye hakuapishwa, alidai shahidi huyo alifundishwa kusema uongo wa dhahiri kwani mtoto aliiambia mahakama walikuwa wakifundishwa Kiingereza na aliyekuwa mshitakiwa wa tano ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Mashujaa, Sigirinda Ligomboka ambaye aliachiliwa huru.
“Ushahidi wake alidai Babu Seya alimbaka, lakini hakuna rekodi yoyote inayoonyesha shahidi huyo alimtaja. Shahidi huyo alitaja majina ya vijana waliomkamata ni Cheupe na Sembe na katika warufani hao hakuna mrufani mwenye majina hayo na upande wa mashitaka wala hawakuwaleta mahakamani watu hao, ili wawe mashahidi,” alidai Marando.
Akiendelea kuuchambua ushahidi huo, alidai kuwa ushahidi huo unaonyesha kuwa mtoto huyo alikuwa akibakwa hata siku ambazo si za shule na kutoa mfano kuwa Oktoba 11, mwaka 2004 ilikuwa Jumamosi na tayari Babu Seya alikuwa ameishakamatwa, lakini shahidi huyo alieleza kuwa siku hiyo alikuwa amebakwa.
Akichambua kwa ujumla ushahidi wa watoto hao, alidai kuwa hakuna shahidi wa upande wa mashitaka aliyeiambia mahakama kuwa makosa hayo yalitendekea Aprili, Mei, Juni, Julai, Agosti, Septemba na Oktoba isipokuwa hati ya mashitaka inasomeka kwamba makosa yote yalitendeka kati ya Septemba na Oktoba, lakini juaji na hakimu huyo wakaridhia.
Aidha, alidai mmoja wa watoto hao alidai kubakwa hadi kutoka damu, lakini taarifa ya daktari iyowasilishwa mahakamani hapo ilionyesha kuwa mtoto huyo ni bikira na wala haonyeshi aliwahi kubikiriwa wala kuingiliwa kinyume na maumbile.
Pamoja na hayo, alihoji kilichofanya upande wa mashitaka kuficha ripoti ya daktari aliyewafanyia uchunguzi watoto hao wanaodaiwa walibakwa na kushindwa kuleta mashahidi ambao ni wanamuziki wa bendi ya Achigo, mama wa Babu Seya na mke wa Babu Seya kwa sababu waliona mashahidi hao wangewaumbua.
“Kesi hii ni ngumu kwetu sote na kama mahakama na sisi tunaona warufani walifanya haya makosa tuwalaani ila mimi Marando nasema nimejiridhisha hawajafanya hayo makosa.
“Hivi tujiulize, kibaiolojia kweli inawezekana mtoto wa miaka sita abakwe na wanaume hawa (warufani) nyuma na mbele halafu mtoto huyo aweze kutembea? Haiingii akilini hata kidogo, nasema kesi hii ni ya kutunga, kwani hata mwanamke mwenye umri wa utu uzima akifanyiwa unyama huo hawezi kutembea,” alidai Marando.
Akijibu hoja za mrufani, wakili Mkuu wa Serikali Justus Mulokozi, alidai kitendo cha shahidi kushindwa kumtambua mshitakiwa mahakamani si sababu inayosababisha ushahidi wa shahidi huyo kuonekana hauna thamani, jibu lililosababisha umati wa watu kuangua vicheko.
Mulokozi alidai pia mahakama ikiamini upande mmoja, hailazimiki kuangalia upande mwingine, hoja ambayo ilipingwa na Marando ambaye alidai kuwa hoja hiyo haikupaswa kutolewa na wakili mwandamizi kama Mulokozi kwani hoja hiyo inatofautiana na sheria za nchi na kauli ya wakili huyo wa serikali imedhihirisha ni kweli Lyamuya aliegemea ushahidi wa upande wa mashitaka.
Jaji Kimaro alisema jopo hilo tayari imeishamaliza kusikiliza rufaa hiyo na akasema jopo lake litatoa taarifa ya hukumu. Mbali na Babu Seya, warufani wengine ni Papii Kocha Nguza, Nguza Mbangu na Francis Nguza.
 
Yeah nimesoma Fidel80
Alichoshangaa Marando ambacho hajawahi kukiona miaka 30 ya uwakili wake ni hukumu ya hovyo kama hii,kuna mtoto mmoja alibakwa hadi kutoka damu, lakini kuna taarifa ya daktari inasema alikuwa bado bikira.
sasa kali zaidi ni kua ile report nzima ya daktari wa Mwananyamala serikali kwa kushirikiana na mahakama ya kisutu kwa sababu wanazozijua wao waligoma kuiweka wazi kwa mawakili wa utetezi kina nyange, kisha Lyamuya akatumia ujuzi wake kutoa hukumu.
bado nashangaa kweli mtoto wa miaka sita umuingilie mbele na nyuma anewaje kutembea ?
Sasa wale woooote waliokuwa wanamuona Babu seya na wanawe ni wauaji, someni hapa muone jinsi walivyo kandamizwa, Marando kaweka wazi, sio kila aliye selo anastahili kuwa kule bwana,
 
kama kesi hiyohiyo moja mtu kakutwa na hatia.................kesi hiyo hiyo moja mtu anaondolewa hatia.........na hii inatokea kwenye kesi kibao..............PANA SHERIA KWELI HAPO YA KUSUBIRI ICHUKUE MKONDO WAKE?........sheria gani inawaogopa mafisadi?
nawambia hivi '''SIKU ZOTE USAWA HAUPATIKANI KWA MZANI KUWA SAWA....INATEGEMEA NA MPIMAJI MWENYEWE'' maamuzi ya mwisho yapo mikononi mwa watu na sio kwenye vitabu vya sheria.....................................DUNIANI SHERIA....HAKI KWA MUNGU.
Mmmh sheria ipo tusubiri lolote laweza kutokea
 
Back
Top Bottom