RTO na LATRA Dodoma na Singida: Basi la Isamilo T863 DSB limejaza abiria kuliko uwezo wake

Entim

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
4,021
2,253
RTO na LATRA mikoa ya Dodoma na Singida, basi la ISAMILO T863 DSB kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, muda huu lipo Dodoma na limepakia abiria waliosimama zaidi ya 20.

Cha ajabu basi limeingia standi kuu ya 88 Jijini Dodoma na hakuna Askari wa Usalama barabarani aliyeingia na kukagua ndani, hili siyo jambo la kawaida.

Kwa hali hii, basi linaweza kusababisha ajali mbaya.
 
tunasubiri kwanza ajali itokee ndio tuje kutoa tamko.
lisipopata ajali basi wewe ni muongo.
tutakuaminije, wapi picha?
 
Shule zimefunga Mkuuu, siku ya leo usafiri ni shida sasa wewe unataka tuachwe vituoni. Wengi ya waliosimama ni watoto wanaotoka mashuleni sasa wakishushwa huko njian watalala wapi mkuu.

Anyway hakuna jipya isipokuwa watapigwa faini ya 250,000/=
 
Hao abiria waliyojazwa kama nyanya waliingizwa kwa lazima au?

Ova
 
piga picha, chukua ba numba ya gari, rushia LATRA au hata kwenye mitandao yakijamii inatosha. piga picha kisili sili chukua hata video huku ukitaja jina la Bus make hawachelewi kukana
 
Back
Top Bottom