Basi la abiria premier express lapata ajali

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Basi la abiria kampuni ya Premier Express lililokuwa likitoka Jijini Mwanza kuelekea Mbeya limepata ajali na kupinduka kwenye mteremko wa kuelekea Ipogolo Manispaa ya Iringa na kusababisha majeruhi kwa baadhi ya abiria na dereva huku chanzo kikitajwa kuwa ni kukatika kwa breki.

Basi hilo lililoanza safari yake jana saa 12 asubuhi katika Stendi ya mabasi ya Nyegezi Jijini Mwanza lilifika eneo hilo la mteremko mkali majira ya saa saba usiku ndipo ajali hiyo ikatokea sababu ikitajwa kuwa ni kukatika kwa breki.

Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, ACP Allan Bukumbi, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo usiku wa saa saba na kusema kuwa hakukuwa na vifo zaidi ya dereva kupata majeraha makubwa zaidi.

Akiongea na Mwananchi Digital leo Agosti 12, 2023 eneo la tukio, Jacob John ambaye ni abiria wa basi hilo, akitokea Igunga, mkoani Tabora, amesema alipelekwa hospitali kutibiwa majeraha madogo aliyoyapata na kwamba bado ana maumivu sehemu nyingine za mwili kama vile shingo.

"Asilimia kubwa ya vitu vya watu vipo ndani ya gari kwahiyo tunasubiri waje wainue basi tuchukue vitu vyetu tujue utaratibu unaofuata,"

"Kuhusu fidia ya vitu vyetu kama nauli wamesema watakuja kuongea na sisi lakini mpaka sasa bado hawajafika kuongea na sisi ndio bado hatuelewi mpaka muda huu (Saa sita mchana)," amesema Jacob.

Kwa upande wa Emma Muhagama pia abiria wa basi hilo akitokea Mwanza kwenda Ludewa, mkoani Njombe, amemshukuru dereva wa basi hilo kwa kuwaokoa kwani nadhani madhara yangekuwa makubwa kama siyo juhudi zake.

"Nilikuwa naelekea Ludewa, ajali imetukuta hapa Iringa, kikubwa ni gari kukatika breki lakini cha kumshukuru Mungu, ulikuwa sio uzembe wa dereva; alijitahidi kadri ya uwezo wake, dereva alituokoa,"

"Changamoto ni kwamba tumepotelewa vitu vyetu kama hela, simu na vitu vingine vipo ndani ya gari, kuna madereva bajaji na bodaboda walifika kutusaidia sasa hatujui vitu vyetu vimeenda na hao au vipi majibu zaidi tutapata gari likiinuliwa," amesema Emma.

(Imeandikwa na Ahazi Mvela)
#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa
 
Saa 12 asubuhi mnatoka Nyegezi, mnafikaje Ipogoro saa saba usiku? Changamoto ziliqnza mapema.
 
Back
Top Bottom