RPC Arusha na ulinganishi wa vyeo JWTZ na PT

RPC Arusha na ulinganishi wa vyeo JWTZ na PT

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Huyo anatawala commission. Kama unavyosikia kamishina wa fedha,kamishina wa mafunzo kamishina wa utawala. Cp ndiyo cheo cha mwisho polisi baada ya hapo ni hisani ya Raisi tu nani ampe nafasi ya IGP .sasa Nyota moja ya jeshi la Wananchi anaitwa Commissioned officer jiulize anaongoza Commission gani? .Narudia tena fananisha hadhi anayopewa MAMBOSASA AU SHANA kama inapishana na Bregadia General .wrote wamepewa nyumba safi gari V8 walinzi na wanaongoza mikoa au kanda katika level za kijeshi.Fikirini tena.Na Leo nimebaini kitu kikubwa mno kuna uwezekano haya majeshi katika silabasi zao hawafundishwi juu ya majesji mengine hasa hawa ngazi ya mafunzo ya awali maana kwa upande wangu sijawahi ona maofisa wa polisi na jeshi kuanzia Nyota moja sijawahi kuona wakigombana au kufedheheshana ila hawa vumilia vumbi yaani coplo,Sargent,staff Sargent na constable/private. Yaani ni mijinga kweli halafu yamesahau yote yalikuwa kozi moja JKT .Mimi nafikiri matumizi ya Bhangi katika majeshi yetu has a askari wa vyeo vya chini yamekuwa makubwa sana.
 
A wishful thinking!! Polisi ni idara ya kiraia. Kijeshi kuna commissioned na non commissioned. Sasa huwezi kumlinganisha gazetted officer wa polisi na commissioned officer a jeshi. Vyeo vya makamishina hutolewa na rais, ambapo kuanzia luteni usu jwtz. Mwenye nyota moja jw ni kamishna, hiyo ni fact, huwezi kumlinganisha na gazetted officer.
Haaaaaaaaaaaa.Hoja Dhaifu sana .Nyie wote walinzi tu .kuanzia ACP hadi CP wote wamepewa walinzi na V8 ya kutendea kazi yaani sana na Luten canal na Bregedia general yaani anapewa V8 na ulinzi .kwa ufupi ndiyo wamepewa mikoa au kanda kuongoza sasa wewe askari jingajinga unafananisha kanyota kamoja luteni Usu ambaye anawekwa nyuma ya landrover bovu na anaishi nyumba utafikiri mahabusu ya Butimba .Neno commissioned Officer linawachanganya sana narudia tena kamishina wa polisi anaongoza Commission ila Luten anaongoza platoon tu ya watu 27. Rejea vitani kule kagera kama hao polisi hawaendi vitani au si wanajeshi hicho cha kifo cha ACP Hans Pope alikuwa anaongoza nini Kule vitani katika Vita ya kagera na Iddy Amin akatangaza wameua askari wa kukodiwa wa Kichina .Mfikiri kwa kina halafu muache mbwembwe nyie maaskari mbumbumbu .Watu wote nchini tunaongozwa na katiba na katiba imewalinganisha narudia tena acheni mbwembwe .majeshi yamewekwa na katiba .Hivyo vialama vya mabegani visiwatie uchizi maana ikitokea vita hadi Mgambo na Sungusungu wanashika bunduki.
 
Kiitifaki ya kupigiwa saluti,Commisioned officer (CP) wa polisi ni sawa na commisioned officer (2lt wa nyota moja) wa Jwtz.

Chini ya Commisioned rank, vyeo hivyo huitwa other ranks.

Kwa hiyo kwa cheo chake cha ACP ukilinganisha na Jwtz ni cheo cha pili kurudi chini ya commisioned officer ambacho ni Warrant officer class2 na hata mishahara ukiichunguza inalingana.

Asijikweze, sababu hata vita vikizuka, akishikizwa jeshini, lazima atapewa mafunzo (refresher) wakufunzi wakiwa ni hao other ranks na atakasimiwa na kuvishwa vyeo vya other ranks na hilo halina ubishi ni kanuni.

Halafu tukija kwenye sheria za kijeshi (military defence act) hao civilian police ni idara za kiraia zinazofanya kazi zinazofanana na za kijeshi, wakiwemo magereza na zimamoto.
Hivyo Jwtz hawaruhusiwi kumkamata raia na kumuweka rumande za jeshi akiwemo yeye, kwa sababu anahesabika kuwa ni raia kwenye vitabu vya sheria za majeshi.
Mkuu hebu agiza Balimi kubwa ya baridi...bili ije kwangu
 
mshahara wa kamishna wa police ni sh ngapi?tuanzie hapo kwanza
 
Mkuu ni mwiko kisheria raia kuswekwa ndani ya mahabusu za jeshi. Ipo hivii? Wakikukamata unavunja sheria makambini kwao, wanatakiwa wakupeleke polisi na kama ni mashitaka utaenda kufunguliwa huko.
Hilo linajulikana na bado wanafanya hivyo kila siku, yaani kila sehemu washashuhudia uonevu wao wa kijinga.
Wakija bar wakaanzisha ugomvi wakapigwa basi watakuja na karandinga kibaaao kupiga watu, dukani wakinunua kitu kikaharibika wanalazimisha wabadilishiwe ama wapewe pesa zao na mwenye duka akikataa anakula kisago, yaani kiufupi wanajeshi wanazingua.
Ufike muda kila mtu awajibike bila kujali kazi yake na cheo chake na kuhusu ndoa ningeshauri waoane wao kwa wao, wasichangamane na raia wa kawaida.
 
Kama nakuelewa hv mkuu, ndo mana nikauliza huyu RPC ametumia vigezo gani kulinganisha!?
kaangalia decorations mabegani wakati zina maana tofauti, skills tofauti, mafunzo tofauti na uvalishwaji tofauti
 
Sio jeshi? wajifunze kiswahili

Kuna

Jeshi la Wananchi Tz
Jeshi la Polisi
Jeshi la Kujenga Taifa
Jeshi la Magereza
Rafiki wameamua kutamka tu!
ili walau kupata heshima katika jamii
 
Huu uzi naona wajeda kama wote..
Heshima yenu wakuu
 
Tunaomba uchambuzi na unyumbulishaji kuhusu hili mkuu maana hapa kuna kudanganywa
Watu Wasiojua Mngekaa Kimya Tu, Jeshi Yaani ACP Alingane Na Brigade General
Hakuna Hata Utaratibu Huo


ACP Hata Huwezi Kulinganisha Na Warrant Officer Class One
 
Watu Wasiojua Mngekaa Kimya Tu, Jeshi Yaani ACP Alingane Na Brigade General
Hakuna Hata Utaratibu Huo


ACP Hata Huwezi Kulinganisha Na Warrant Officer Class One
Mabakamabaka wamemsikia akibwabwaja hivyo? Shauri yake, asije akajikojolea akikutana na kisajenti cha JW!
 
Back
Top Bottom