Gushleviv
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 3,457
- 5,322
Jana nilishirikina kumaliza RDM. Katika malengi yangu moja ni kushiri marathon angaau mara moja. Na jana nimetimiza kwa kushiriki na kumaliza nusu marathon ambayo ni km21.1.
Niliamka saa kumi usiku ili nifike eneo ka kuanzia mapema,inabidi uwe pale saa 11 na nusu asubuhi ili uanze saa 12 asubuhi.
Kushiriki inabidi ulipe 35,000 na niliongeza na wrost band za charity 5,000 jumla 40,000 ili nishiriki.
Siku ilianzza vibaya kwa kucheleweshwa kuanza mbio hizi.
Tulisimama masaa mawili na kuanza saa mbili badala ya saa 12 asubuhi. Kwa kweli tulikimbia na jua kali sana. Ingawa wanaandaji wanasema sababu ilikuwa nje ya uwezo wao mimi nasema ni uzembe wao. Sababu sitaisema hapa ila haikuja bahati mbaya. Ni sababu ambayo ipo kwenye ratiba mwaka mzima na RDM WANATAKIWA WAJUE. Hilo ni moja ya mambo yaliyovunja moyo washiriki wengi kama sio wote.
Kubwa kuliko na baya kuliko yote ni ukosefu wa medali za kutosha kwa washiriki. RDM wameandikisha watu zaidi ya 10,000(nikiri hili nimesikia tu sina uhakika) huku wameandaa meddali 1,500! Matokeo yake washiriki wengi waliomaliza HATUKUPATA MEDALI! Fikiria mtu aliekimbia km42 anakosa medali huku mtu alietembea km9 anapata medali kwasababu amewahi kumaliza, yaani medali zilikuwa chache aloewahi kurudi ndio anapata hivyo wa kutembea km9 huwa anawahi kuliko mkimbiaji wa km21/42.
Nimesikitishwa sana na huu uzembe, sijui utapeli au kutojali tu kwa waandaji wa RDM. Lengo la kushiriki ni kuweka kumbukumbu kwenye maisha yangu kuwa nishashiriki marathon lakini nimeshiriki na sina uthibitisho wowote, yaani sina tofauti na alieishia njiani akaamua kula kona! Nimesikia wanasema wataandaa utaratibu kutupatia medali kuwa kuna majina wameandika, sijui wanaandika majina ya nini wakati wanayo au walitoa medali bila kuangalia wanampa nani?
Hii ni marathon yangu ya kwanza na ya mwisho kushiriki nasikitika imekuwa kama ilivyotokea.
Tatizo bongo hizi shughuli zanachanganywa na njaa ya watu wachache kitu kinachopelekea shughuli nzima kukosa ubora.