Mfahamu Mwanariadha Mtanzania John Stephen Akhwar alivyotoa somo la uzalendo Mexico 1968

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Ukifungua ukurasa wa Google au YouTube kisha ukaandika John Stephen Akhwari hakika kile ambacho utakiona kitakufanya utamani kutazama mpaka mwisho.

Jina la mtu huyo litajitokeza mara nyingi kwenye kurasa hizo na k a m a u n amfahamu b a s i itakufanya utamani kumtazama na kuona historia yake kwa mara nyingine, kama ni mara yako ya kwanza bila shaka kuna kitu utajifunza hata kama siyo cha kimichezo basi kimaisha.

Historia ya tukio lake lililotokea mwaka 1968 nchini Mexico bado inakumbukwa hadi leo, taswira ya kile

wakati akikimbia kiliwafanya Wazungu wengi wakitambue kama ‘The Greatest Last- Place Finish Ever in the Olympic games’.

Maana isiyo rasmi ya sentensi hiyo ni kuwa ni mtu wa mwisho bora kuwahi kumaliza katika michezo ya Olimpiki, yaani alikuwa wa mwisho lakini ni bora kuwahi kutokea na hadi leo kila anayetazama video yake au picha yake wakati anapokuwa anamaliza kukimbia atajifunza kuwa katika maisha hutakiwi kukata tamaa.

Miaka ya 1968, 1974 hadi 1980, Tanzania ilikuwa ni miongoni mwa nchi ambazo zilikuwa zinasifika kwa riadha, wengi walifanya vizuri mfano katika mita 1,500 mashindano ya Madola mwaka 1974, Filbert Bay na mshindi wa mita 5,000 Olimpiki ya Urusi mwaka 1980, Suleiman Nyambui wote walifanya vizuri.

KWA NINI JOHN AKHWARI?
Licha ya kina Bayi na Nyambui kufanya vizuri, lakini alichofanya Akhwari ndani ya ardhi ya Mexico kwa kumaliza mbio ndefu akiwa anachechemea baada ya kuumia, aliifanya Tanzania ijivunie ujasiri wake.

Wakati ulimwengu mzima ukimshangaa kwa kitendo chake cha kutokata tamaa licha ya wenzake kumaliza taktibani saa moja zaidi huku yeye akijivuta, alitamka:

“My country did not send me to Mexico City to start the race. They sent me to finish.” (Nchi yangu haikunituma Mexico City kuanza mbio bali kumaliza mbio).

safari hadi nyumbani kwa Akhwari wilayani Mbulu mkoani Manyara kuzungumza naye kiundani kuhusu mchezo huo:

HISTORIA YAKE
Alizaliwa Machi 27, 1938 Kijiji cha Khaday, Kata ya Sanu, Tarafa ya Endagikot wilayani Mbulu Mkoa wa Manyara. Alianza riadha mwaka 1958 baada ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 1962, mwaka 1976 ndiyo ambao aliachana rasmi na mchezo huo.

KWA NINI RIADHA?
“ Tangu enzi za ukoloni kulikuwa na mashindano ya sherehe ya malkia, sasa tulikuwa tunapelekwa umbali mrefu kisha tunarudi kwa miguu, lazima ukimbie, hiyo ikachangia nianze kupenda riadha, pia wakati ule ilikuwa fahari kushiriki mchezo huo.

ULIPOSHINDA ULIPEWA NINI?
“Hakukuwa na medali, tulikuwa tukipewa jani la heshima lisilokauka, baadaye ikaja vikombe kisha ndiyo medali ya dhahabu, ya fedha na medali ya fedha nyekundu.

CHANGAMOTO ULIZOKUTANA NAZO
“Enzi zetu viongozi hawakuwa na elimu ya kutosha juu ya riadha, mimi ndiyo nilifungua mlango wa kwenda nje, kwa hiyo nilipata matatizo makubwa sana lakini nilivumilia.

ULISHINDA MBIO ZIPI?
“Mwaka 1962 nilishinda mashindano ya taifa ya km 3 na 6 Dar, pia Marathon ya Afrika Mashariki iliyofanyika Nairobi, nafasi ya 6 mbio za Jumuiya ya Madola km 42 iliyofanyika West Australia na mbio za Sri Lanka km 3 nafasi 2.

“Mwaka 1963 nafasi ya 2 km 42 nchini Ugiriki, 1967 mshindi wa kwanza km 42 Afrika mashariki ilifanyika Kampala nchini Uganda, 1970 mshindi wa 5 km 42 kati ya watu 56 mashindano ya Jumuiya ya Madola.

TUKIO LA MEXICO CITY MWAKA 1968
“Olimpiki ya mwaka 1968, nia yangu ilikuwa ni kushinda tatizo kwetu Tanzania, viongozi wa chama cha Riadha Taifa (Tanganyika Africa Athletics Association-TAA) chini ya mwenyekiti wa wakati huo, Mustapha Nyang’anyi badala ya kutupeleka kufanya mazoezi kwenye ukanda wa juu ya bahari wakatupeleka kwenye usawa wa bahari.

“Unaambiwa ukitaka kuzoea hali ya huko lazima ukafanye mazoezi miezi sita ndiyo uzoee, matokeo yake niliumia misuli na nikawa wa mwisho.

“Nilipoanza kukimbia sikuwa na hofu yoyote, nilikuwa naongoza, ghafla nikaanza kuhisi kizunguzungu, nikapoteza fahamu. Nilipozinduka nikakuta watu wa huduma ya kwanza wananihudumia, wakanitaka niingie katika ambulance, nikakataa, nikasimama na kuanza kukimbia tena.

“Nilikuwa nahisi maumivu makali sana, na nikawa natokwa na damu, niliumia magoti yote lakini sikujali hilo kwa kuwa lengo langu ilikuwa ni kumaliza. Nilitimiza hilo kwa saa 3:25:27. Baada ya hapo nilitumia wiki mbili nikitibiwa kisha ndiyo nikarejea Tanzania.

“Lengo lilikuwa kutimiza uzalendo wangu wa kile ambacho nchi ilinituma na ninashukuru nilitimiza ahadi niliyojiwekea.”

TUKIO LA KIZALENDO LILITOKEAJE
Wakati wanaanza mbio hizo walikuwa washiriki 75, lakini mwisho wakamaliza 57 huku 18 wakiishia njiani, Mtanzania huyo akawa mtu wa 57 ambapo mshindi wa kwanza alikuwa ni Mamo Wolde wa Ethiopia aliyetumia sa 2:20:26.

Hiyo inamaana kuwa Akhwari alimaliza mbio ikiwa ni saa moja na dakika 5 tangu mshindi alipopatikana, mashabiki na waandishi wakiwa wameshasahau kama kulikuwa na mshiriki mwingine ambaye alikuwa hajamaliza kukimbia.

Alipofuatwa na kuulizwa sababu za kuendelea kukimbia wakati alikuwa hoi kwa maumivu ndipo akasema: “My country did not send me to Mexico City to start the race. They sent me to finish.” Kauli ambayo imetumika katika matukio mengi ya kuhamasisha jamii mbalimbali.


Video: Hili ni tukio likionesha namna John Akhwar alivyopambana

VIPI KUHUSU TUZO ZA HESHIMA?
“Mwaka 1995 nilitunukiwa nishani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais Ali Hassan Mwinyi, 2008 nilipewa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Riadha, tuzo ambayo ilitolewa Afrika Kusini, mwaka huohuo nilikwenda Beijing, China kufungua mashindano ya Olimpiki na kukimbiza Mwenge wa Olimpiki, 2012 nilitunukiwa Nishani ya Sanaa na Michezo iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete.

KUNA MBIO ZIMEANZISHWA KWA JINA LA AKHWARI
“Nazijua na nilishirikishwa, nafurahi kuona vijana wanaendelea kuthamini mchango wangu katika riadha, kwangu ni jambo la pekee kuona mashindano ya riadha yanaitwa jina langu, natamani kuona wanariadha wetu wa sasa wanafanya makubwa kuliko mimi na kuiletea heshima Tanzania,” anasema.

TUZO YA HESHIMA MAREKANI
Watanzania waishio Marekani wametambua mchango wa mkongwe huyu na kuamua kumpatia Tuzo ya Heshima (Tunu Adimu) ambazo zilitolewa Aprili 29, 2018 jijini Dallas, Texas.

Lengo kubwa ya tuzo hizo ni kwa watu waliotoa mchango mkubwa kwa taifa la Tanzania.
 
Kina Filbert Bayi wapo kwenye uongozi wa riadha toka mtoto anazaliwa mpaka anamaliza chuo kikukuu
 
Mwamba katisha
Wahenga tunamuelewa sana na huo ndio uzalendo
Alikimbia mpaka usiku tena akiwa kaumia
Shujaa haswa huyo
Halafu utasikia majina ya ajabu kwenye madaraja na Ndege hata barabara zetu ila hawa wamesahaulika kabisa

Wengi sana hawamjui kwa sababu hatutilii maanani sana historia zetu
 
Back
Top Bottom