Rostam Aziz aachia ngazi CCM

Rostam Aziz aachia ngazi CCM

Itashangaza sana Kama katibu Mwenezi wa CCM atajitapa kwamba hayo ni mafanikio.........Sidhani kama atakuwa desparate kiasi hicho katika kurejesha imani ya wananchi kwa chama chake,Naamini hatafanya hivyo badala yake nadhani atanadi busara ya kuchukua hatua zaidi na kuishinikiza serikali ya chama chake kumburuza mahakamani na au kutaifisha mali zake kutokana na ushahidi waliokuwa nao na kumtaka kuachia nyadhifa
 
Kashfa ingine kwa CCM ya akina Nape. Kumbe walichakachua maamuzi ya kikao chao, na kumbe ni vita ya makundi ya kuchaguana na kuchafuliana kisiasa. Hii ni tuhuma nzito na ni ufisadi mwingine hatari zaidi. Itabidi waweke minutes za kikao wazi. Viinginevyo, watatumia the next three years kukanusha kashfa mpya ambayo ni nzito zaidi kuliko hiyo iliyomfanya ajiuzulu.
 
Ubunge sio nyadhifa, ubunge ni uwakilishi na wanaomchagua ni wananchi. Tazama Shibuda alipotemwa CCM akaukwaa Ubunge kupitia cdm. Au umesahau, nikukumbushe na Slaa? Alipopigwa chini akaukwaa ubunge kupitia wapi? Kuweni makini kidooogo. Kwa kiwango alichofika Rostam anaweza kuwatumikia wananchi bila ya kuwa Mbunge. Hilo likumbuke.

Ni kweli anaweza kuwatumikia wananchi bila kuwa mbunge. Lakini hawezi kuwa mbunge bila kupitia chama chochote cha siasa. Mfano ulioutoa wa Shibuda na Dr. Slaa wasingekuwa wabunge kama wasingejiunga na chama chochote. Hivyo ndivyo Katiba inavyosema mbidada wewe!
 
Kiini macho hicho, ameacha amesuka line ili aendelee kukamua pesa ya wadanyika.
Hujasikia kuwa walipa kodi wanalipa kupitia vodapesa??? Hichi kiumbe achana nacho. Ili kukomesha huyu bwana ni kumfukuza nchini tu Agrrrrrrrrrrr
 
Magamba wanashabikia nini kwa hatua hii?? hivi hii ni success story?? nadhani iliwapasa mkae kimya kwa aibu ya kumiliki majizi ya nchi hii katika chama chenu. Ingelikuwa heri kama mngelikuwa wa kwanza kufichua wezi hawa wa rasilimali za nchi. lakini CDM walipowafichua mliwaita wasema hovyo, leo hii 4 years later ndo mnaamka. hii inaonesha bado mpo gizani. Mnaloliona leo wenzenu walishaliona last 4 years. kwa kasi mnayoendanayo, mtaachiwa manyoya na CDM. Bado wezi wengine tunawasubiri...halahala chama kisije kikabaki bila viongozi mana tunapata shida mmno kumsaka mwadilifu ndan ya magamba
 
Itashangaza sana Kama katibu Mwenezi wa CCM atajitapa kwamba hayo ni mafanikio.........Sidhani kama atakuwa desparate kiasi hicho katika kurejesha imani ya wananchi kwa chama chake,Naamini hatafanya hivyo

Ngoja tumsubiri yule Kikwete kama atatia neno kuhusiana na kujiuzulu kwa RA, mtu ambaye alimuweka Kikwete na Serikali yake yote mifukoni mwake.
 
Jamani mimi nnachotaka kufahamu ni kama mipaka ya nchi imefungwa, ili jamaa asichupe ng'ambo na pesa yetu
.
 
Kashfa ingine kwa CCM ya akina Nape. Kumbe walichakachua maamuzi ya kikao chao, na kumbe ni vita ya makundi ya kuchaguana na kuchafuliana kisiasa. Hii ni tuhuma nzito na ni ufisadi mwingine hatari zaidi. Itabidi waweke minutes za kikao wazi. Viinginevyo, watatumia the next three years kukanusha kashfa mpya ambayo ni nzito zaidi kuliko hiyo iliyomfanya ajiuzulu.

Hii ni sawa na ile theory ya negative feedback mechanism,na tutaendelea kuwalima tu
 
Baada ya pacha mmoja kujivua gamba je Mapacha wawili wanao uwezo wakufanya hivyo??Kama mwenzao alivyofanya?
- Kwanza wana jeuri kiburi!
- Pili chama kinawafahamu kwakuwa na kiburi!
- Tatu chama chao kinawafahamu walivyo na nguvu kwe nye chama!
Swali watakubali kujivua gamba ili kuifurahisha CCM??Je wapo tayari kupoteza malengo ya 2015?
Weredi na wasubiri hapa najua wachambuzi mpo!
 
Duh. Nimeamini JF ni kidume nimetoka speed huko ukumbini kuja kupost topic hii nakuja tayari watu wamepost ! nimekosa cheap popularty leo. any way sasa sijui atalala hapa hapa Tz au anaelekea Canada kama kina marehemu Jamal
 
Write a comment...

https://www.jamiiforums.com/

[h=6]January Makamba
tweets: Rostam Aziz, MP for Igunga, resigns from the Parliament and NEC Membership. Submitted a letter to CCM Chairman this morning.[/h]
app_2_115463795461_6981.gif
48 minutes ago via Selective Tweets ·LikeUnlike ·

 
Mara tu baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ambacho kilichagua wajumbe wapya wa Kamati Kuu na kuidhinisha uundwaji wa Sekretarieti mpya, dhana ya kujivua gamba ambayo naamini Mwenyekiti wetu aliianzisha kwa nia njema ilianza kuenezwa ikichukua tafsiri na mwelekeo tofauti na ule wa awali.

Wajumbe wawili wa Sekretarieti, Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara), Mhe. John Chiligati, na Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Mhe. Nape Nnauye, walisikika wakitangaza kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa ilikuwa imefikia uamuzi wa kuwapa siku tisini wale walioitwa watuhumiwa wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi ndani ya chama kujitoa katika nafasi zao za uongozi vinginevyo watafukuzwa na chama.
Wazee wangu, baada ya kushinikizwa sana na vyombo vya habari wawataje kwa majina wanasiasa waliokuwa wakituhumiwa kwa ufisadi ambao ni wajumbe wa NEC na ambao wanapaswa kujiuzulu nyadhifa zao, wajumbe hao wa Sekretarieti walikwenda mbele zaidi.

Baada ya awali kuwaeleza waandishi wa habari kwamba majina ya watuhumiwa hao yalikuwa yakifahamika kutokana na kuhusishwa katika kashfa tofauti kama zile za Richmond, EPA na ununuzi wa rada, mwishoni viongozi hao walikaririwa wakiyataja majina ya wanasiasa watatu kuwa ndiyo ambao walikuwa wakilengwa na maamuzi hayo.
Wazee wangu, nilishangazwa na kushitushwa na namna porojo na fitina za kisiasa zilivyofinyangwa kwa mara nyingine tena baada ya kusikia jina la mbunge wenu ambaye ni mimi, likitajwa kuwa miongoni mwa yale matatu ya viongozi waliokuwa wakitakiwa eti kupima wenyewe na kisha kuchukua uamuzi wa kujiuzulu nafasi zao za uongozi ndani ya NEC katika kipindi cha siku tisini.

Katika ulimwengu wa kibiashara wa leo, vita hivi ambavyo vinaweza kuonekana kuwa ni vidogo tu vyenye malengo ya kuchafuana kisiasa, vinakuwa na athari kubwa katika uhusiano wa kibiashara kuliko hata wale wasioelewa wanavyoweza kukadiria. Ndiyo maana nimeona ni afadhali sasa niwape nafasi wale wanaoendesha siasa hizi uchwara na zisizo na tija waendelee na siasa zao hizo ambazo kwa bahati mbaya kwao, mimi sina muda nazo na siwezi kuwa sehemu yake. Na mimi kwa upande wangu niendelee na maisha yangu.
[QUOTE]Napenda kuliweka hili sawa sawa. Uamuzi wangu wa kuachia nafasi zangu zote za uongozi nilizopata kwa tiketi ya CCM haukutokana na wala haumaanishi kukubaliana na shinikizo lililopotoshwa kuhusu azma ya utekelezaji wa dhana ya kujivua gamba, la hasha, bali dhamira ya dhati ya kuachana na siasa hizi uchwara (gutter politics) na kutumia muda wangu kushughulika na biashara zangu.
[/QUOTE]

Msukumo huo si mwingine bali ni ule wa kuamua kuachia nafasi zangu zote za uongozi ndani ya chama, nikianzia na ile ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa nikiuwakilisha Mkoa wa Tabora na hii ya ubunge wa Igunga ambazo kama si kwa baraka za chama changu nisingelikuwa nazo.

Kwa mfanya biashara kujihusisha na mambo ya siasa vigumu kutenganisha shughuli hizo mbili maana kuna vishawishi vingi vyenye msukumo wa kutumia nafsi katika siasa kufanikisha biashara
 
Utakuwa huru pale utakapo kuwa umeingia Kaburini.................................
 
habari nilizozipa punde kutoka igunga ni kwamba yule Kigogo na Kada wa CCM Mh. Rostam Hazizz amejivua nyazifa zake zote za CCM leo hii ametangaza Rasmi jimboni kwake Igunga
 
Duuh jamaa biashara zilianza muendea mrama.. nilisafiri nae wiki chache zilizopita na aliyekua akizungumza nae kikubwa alichokua akilalamikia ni hili la biashara kutokwenda vyema maana kila mmoja anaogopa kushirikiana nae kwa hizi kashfa zilizomuandama. It is a strategic kuhakikisha anaendesha maisha yake binafsi bila bughudha za magazeti.

Ana mikataba ya muda mrefu ya kuchimba michanga kwenye migodi ya kuchimba madini (Mwadui, Barrick,n.k.), hivyo kama alikuwa analalamika ni bosheni tu au kwa makusudi maana nadhani alishtukia ukimsikiliza!
 
Back
Top Bottom