Rostam Aziz aachia ngazi CCM

agrrrrrr .

RA alishafanikiwa kufanya alichotaka kukifanya

amefanya ufisadi wa kutosha thats all , mission accomplished

to him this is a honorary exit plan
 
Confirmed: Huu ni uzushi tena mkubwa sana. Rostam et al wamekutana na JK jana Serengeti na wameendelea kuweka mambo yao sawa. Ndoa ya mapacha na Jk iko waswahili wanasema MSWANO!
 
Tathmini aliyoitoa NAPE jana haikuonyesha kama kuna mtu atavuliwa wadhifa wowote, popote. Alinywea sana. Alichokuwa anakihubiri kwenye majukwaa tangu alipoteuliwa kwenye Ukatibu wa Itikadi sicho kitakachofanyika.
 
vyanzo vyangu vyote vinasema hakuna kitu kama hicho.......

ila nianchojua ni kwamba jk anakutana na Rostam leo jion huko serengeti Bilila lodge kempinski ambako jk ameenda kwa ajili ya mapumziko.....

jk na lowasa walishamaliza kuongea mda mrefu + chenge

hakuna atakaye fukuzwa toka ccm
 
Wanajamvi:

Habari za kuaminika ni kwamba Rostam Azizi asubuhi hii atatangaza kujivua gamba rasmi katika mkutano na waandishi haabari Tabora. Anajiuzulu nyadhifa zote nakubakia na kadi ya CCM tu.

Swala hapa ni kurudisha kazi, au kufukuzwa Chama. Hiyo ndio maana halisi ya kujivua gamba aliyosema Nape Nnauye. Rostam alishaachishwa nyadhifa kubwa, uweka hazina wa chama na ujumbe wa kamati kuu. kabakia na mjumbe sijui wa nini CCM, ubunge na kadi ya CCM. Sasa kama kaamua kujivua gamba arudishe kadi ya chama na ubunge na fedha za EPA nk halafu tumpige pingu afikishwe kisutu haki itendeke. Bila hivyo yote ni mazingaumbwe. Kuvua gamba ni kwenda keko au lukaranga, maweni, segedance nk.
 
Wanajamvi:

Habari za kuaminika ni kwamba Rostam Azizi asubuhi hii atatangaza kujivua gamba rasmi katika mkutano na waandishi haabari Tabora. Anajiuzulu nyadhifa zote nakubakia na kadi ya CCM tu.

hiyo kadi ndilo gamba lenyewe sasa anabaki nalo la nini wakati kaamua kujivua.
 
hiyo kadi ndilo gamba lenyewe sasa anabaki nalo la nini wakati kaamua kujivua.
Dah! Dhana haikueleweka basi kama ni hivo. Urais wa JK tunautenganisha vipi na "juhudi binafsi" za RA na EL? Hawa wawili wanaweza kuwa magamba kweli?
 
Akijivua gamba ajiandae kwenda jela, Dk W. Slaa naona unachungulia hapa, hembu tujuze hizi habari
 
vyanzo vyangu vyote vinasema hakuna kitu kama hicho.......

ila nianchojua ni kwamba jk anakutana na Rostam leo jion huko serengeti Bilila lodge kempinski ambako jk ameenda kwa ajili ya mapumziko.....

jk na lowasa walishamaliza kuongea mda mrefu + chenge

hakuna atakaye fukuzwa toka ccm

Naungana nawe. Ila RA amekuatana na jk jana kulingana na chanzo changu.
 
Faiza ubunge ni nini?
Ubunge sio nyadhifa, ubunge ni uwakilishi na wanaomchagua ni wananchi. Tazama Shibuda alipotemwa CCM akaukwaa Ubunge kupitia cdm. Au umesahau, nikukumbushe na Slaa? Alipopigwa chini akaukwaa ubunge kupitia wapi? Kuweni makini kidooogo. Kwa kiwango alichofika Rostam anaweza kuwatumikia wananchi bila ya kuwa Mbunge. Hilo likumbuke.
 
Hakuna kitu kama hicho wewe sema tu unatafuta maoni ya wananchi usikie watasemaje. Ajivue gamba kwa kosa gani alilotenda.
 
Back
Top Bottom