Rostam Aziz aachia ngazi CCM

Rostam Aziz aachia ngazi CCM

Justice has been done. Congratulations to RA for this Stiff Decision!

It is now a good time for AC and EL to follow the footsteps for betterment of CCM.


Hakuna jusitce yoyote hapo, huyu fisadi anapaswa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Kama kweli CCM wamekuwa na guts za kumlazimisha kujiuzulu kwa madai ya ufisadi, kwanini wasimfikishe mahakamani kwa tuhuma hizohizo?!
 
naitoshi na wasituletee zengwe,afilisiwe kabisa na wengine wafate,apa tunafatilia kwa makini tbc
mana bado mirija yao ipo katika nchi yetu
shenzy taipu
 
Alikuwa wapi siku zote kama si shinikizo la NEP MNA na sera yake ya magamba.
Asituvunge nishinikizo na kukosa kwake mvuto ndani na nje ya chama chake.
 
Mbona hii news iko JF toka asubuhi na maelezo yake kwa urefu na wazee wa Igunga! Au hampendi kusoma Thread ndefu!
 
this is very sad , lakini wanasema wagombanao ndio wapatanao.....tusubiri tuone.
 
JK alimfananisha RA na mchezaji muhimu kwenye timu kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu huko Igunga.Hii ni Embarrasement(fedheha) miezi 9 baada ya kampeni za uchaguzi
 
Malaria sugu yuko wapi?

Alionekana Tabora katika mkutano wa RA na waandishi wa habari 🙂 Si ajabu kibarua chake toka kwa RA cha kuwachafua Viongozi wa juu wa CHADEMA na chama chao hapa jamvini kikaota nyasi 🙂 baada ya RA kujiuzulu.
 
  • Thanks
Reactions: Aza
Wakuu hebu someni mafanikio ya RA igunga

"
Miongoni mwa mafanikio makubwa tuliyoyafikia kupitia ushirikiano wetu na uongozi wa pamoja ni kwamba, mwaka 1994 Igunga ilikuwa ni wilaya ya mwisho kwa maendeleo mkoani Tabora lakini leo ndiyo ya kwanza, taa za barabarani, bima ya afya kwa kila kaya, zahanati kila kijiji na shule nyingi kuliko idadi ya kata zilizomo kwenye wilaya."


Hongera Rostam Aziz, una tuhuma nzito nyingi tu, lakini kwa hili nakupongeza ndugu yangu.


 
Defacto......quits strategically.it's just a retreat,long battle ahead.Kwanza CCM wanamgwaya,na yeye kwa jeuri amesubiria hadi siku 90 zimeisha na hawajathubutu kumfanya kitu mpaka ameamua mwenyewe katika mazingira yanayotia shaka.CCM hawana cha kujisifu wala kushangilia hapa ni bora wakae Kimya kabisa na hasa katibu mwenezi wao Nape Nnauye

Sasa kama amehusishwa na tuhuma za ufisadi,chama na serikali yake inazo nyaraka na ushahidi wa kutosha.Kitendo cha kuitikia wito wa chama chake uliosukumwa na ushahidi mzito wa kumtaka kujivua nyadhifa zake zote na yeye akachukua hatua hiyo basi CCM na serikali yake waende mbele zaidi kuonyesha dhamira yake ya dhati ya kupambana na ufisadi kwa kumfungulia mashtaka.Vinginevyo culture hii ya impunity iataendelea kuwapa hell.

Rostam ametekeleza wajibu wake,sasa CCM na serikali yake itekeleze wajibu wake kuhakikisha haki inatendeka kwa watanzania na hela za walipa kodi zinarudishwa.

Pia,nimtahadharishe Bashe,asije akawa na wazo la kugombea Igunga akitazamia kupata sapoti kutoka kwa Rostam Aziz,atakuwa amejizika kisiasa.Ana haki ya kugombea kikatiba though lakini angalie dhamira yake.

Na sisi CHADEMA kama habari hii ni yakweli,basi ni muda wetu sasa tujipange kikamilifu tuwapatie wanaigunga Mwakilishi maanake naamini jimbo hilo limekuwa wazi vipindi vinne mfululizo ambavyo RA amekuwa Mbunge!

Hivi Ben, umeandika nini hapa, ni wazi ulikuwa na mgongano wa mawazo kwenye kichwa chako. Ulianza kwa akili yako na umakini ambao unao siku zote. Haahaahaa baadaye ukakumbuka kuwa unatakiwa uendeleze kile alichotuonya RA kwenye hotuba yake, "yaani siasa za kuchafuana" maana huo ndiyo mtaji wa chama chako. Hii ni mbaya sana ni afadhali ungenyamaza tu kuliko kujiweka katika kundi la wafuata upepo. Nimekerwa sana na hii post nadhani hii ni miongoni mwa comment mbovu kuwahi kutokea kwa mtu kama wewe "Mwanasiasa kijana".
 
There are currently 1133 users browsing this thread. (241 members and 892 guests)


Jiandaeni sasa kuchukua hilo jimbo.
 
Amesema jamani hajajivua gamba kwa sababu yeye mwili mzima ni Gamba mpaka damu, ila ameachana na siasa uchwara
 
Back
Top Bottom