Rostam aliangukia Kanisa
Mwandishi Wetu
Daily News; Monday,July 07, 2008 @00:01
"...Ninao watoto watatu na nataka niwalee katika misingi hii,''
"Tutumie makanisa kukemea vitu hivi ili kurejesha taifa katika mstari ulio sahihi,'' alisema.
Hao waliomshangalia RA ni watumwa wa AKILI na hao waliomwalika wachunguzwe na SAID Mwema kwenye kusaidia UCHUNGUZI!Habari za Kitaifa Habari zaidi!
Rostam aliangukia Kanisa
Mwandishi Wetu
Daily News; Monday,July 07, 2008 @00:01
Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz amesema taifa liko katika wakati mgumu katika siasa na jamii na ameomba watu watumie makanisa kulirejesha katika mstari sahihi. Rostam alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana katika sherehe ya uzinduzi wa albamu ya kwaya ya Amkeni ya Usharika wa Kinondoni wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambako alikuwa mgeni rasmi.
Alisema waumini wa dini hawamtuhumu mtu, hawamshutumu, hawapendi wenye wivu na wenye chuki bali wanapenda haki na hivyo ni vizuri wakaitumia fursa hiyo kuliombea taifa. Nawashukuru kwa kunialika kuwa mgeni rasmi leo hii ni ishara kwamba mmeamua kupuuza vijimaneno na upuuzi wa vijiweni.
Nafurahi kuwa miongoni mwenu .hamtuhumu, hamshutumu, hampendi wenye wivu na wenye chuki, mnapenda haki. Ninao watoto watatu na nataka niwalee katika misingi hii, alisema Rostam huku akishangiliwa na umati wa watu waliofurika katika hafla hiyo. Alisema inasikitisha kuwa katika zama hizi watu wanachukiana hadi kufikia hatua ya kuzushiana uchawi na kuombeana vifo.
Tutumie makanisa kukemea vitu hivi ili kurejesha taifa katika mstari ulio sahihi, alisema. Mbunge huyo ambaye katika siku za karibuni jina lake limekuwa likitajwa katika mijadala mbalimbali bungeni alisema licha ya matatizo ya kisiasa yanayolikabili taifa sasa, kuna matatizo ya jamii ambayo alisema ni vizuri yakashughulikiwa kama ya ndoa kuvunjika, kuongezeka kwa watoto wa mitaani, madanguro, kukithiri kwa matumizi ya dawa za kulevya na mengine yanayoongeza mmomonyoko wa maadili.
Katika hafla hiyo Rostam alitoa mchango wa Sh milioni tano kuchangia seti za vyombo vya muziki za kwaya ya Amkeni na jenereta yenye thamani ya Sh milioni 2.6. Mwaka 2005 Aziz alichangia ujenzi wa jengo la Kanisa hilo ambalo sasa linatumika kama sehemu ya Chuo Kikuu cha Tumaini.
Mama kanisani zinaenda hela zote,chafu na nzuri na ndio maana kuna dhana ya kutakasa vipaji.Au wee unasemaje?
Yeye Rostam ni muumini wa Dini gani?
Daily News, tafadhali!
Sheria zilizowekwa zikiwa ni za Watu...Then ni sheria za Mungu!
Kama ni HAKI...Then HAKI ni SHERIA!
Sauti ya watu ni sauti ya Mungu.
Hatuwezi kusema kama kipindi hiki ni kile cha Musa jangwani!
Sheria zote za Duniani zimetokana na AMRI KUMI ZA MUNGU!
Sasa Sheria ndio haki kwa Mtanzania aliyopewa na MUNGU NA si MILIONI SABA NA VITISHO!
Makanisa nayo kwa kukumbatia majambazi ndio wenyewe, hivi kuna haja gani ya kupokea michango ya watu kama Rostam?
Makanisa hayo hayo yanamweka viti vya mbele fisadi Mkapa. Pia walisema JK katumwa na mungu, makanisa siku hizi yamegeuka kuwa biashara. Ni aibu kweli kweli.
Makanisa nayo kwa kukumbatia majambazi ndio wenyewe, hivi kuna haja gani ya kupokea michango ya watu kama Rostam?
Muacheni Rostam alete hela, kwani mnauhakika gani sadaka zote zinazotolewa na waumini huko makanisani kwamba ni safi....!?
Kwani hata Chenge nae si muumini na anatoa sadaka kanisani pia? Je zake ni safi au chafu? So Muacheni Rostam atoe sadaka hata kama ni chafu, cha muhimu ambacho mi NAPINGA ni yeye kujitafutia ujiko kwa kutoa sadaka na kuanza kujisifu kwamba amesaidia kanisa. Hilo ndio mimi silikubali.
Lakini sioni kama kuna makosa mtu kutoa sadaka/zaka.
Wanafunzi wa chuo cha tumaini SUSIENI MASOMO kishinikizeni chuo chenu kama hakitaki kujenga majengo mengine basi ninyi muache masomo.
Maana baadhi ya majengo yenu yamejengwa na fisadi,.
"Katika hafla hiyo Rostam alitoa mchango wa Sh milioni tano kuchangia seti za vyombo vya muziki za kwaya ya Amkeni na jenereta yenye thamani ya Sh milioni 2.6. Mwaka 2005 Aziz alichangia ujenzi wa jengo la Kanisa hilo ambalo sasa linatumika kama sehemu ya Chuo Kikuu cha Tumaini."
Wewe ni mmoja wa wale ambao mnawatetea mafisadi kwa kila hali na hatimaye kuzorotesha vita dhidi ya mafisadi. Mafisadi wanaiba mabilioni wakijenga vidarasa vichache vya milioni 20 mnataka kuwatukuza na kuwapa heshima wasiyostahili.
Yeye kishaiba bilioni 20 akitoa milioni 20 kujenga vidarasa ili mmuone wa maana na kuacha kumsakama kama fisadi, basi kishafanikiwa kutimiza lengo lake la 'kuuma huku anapuliza' ili Watanzania tusimshtukie. Acha udanganyika kaka fungua macho uone mafisadi wanavyoiangamiza nchi.
Wewe ni mmoja wa wale ambao mnawatetea mafisadi kwa kila hali na hatimaye kuzorotesha vita dhidi ya mafisadi. Mafisadi wanaiba mabilioni wakijenga vidarasa vichache vya milioni 20 mnataka kuwatukuza na kuwapa heshima wasiyostahili.
Yeye kishaiba bilioni 20 akitoa milioni 20 kujenga vidarasa ili mmuone wa maana na kuacha kumsakama kama fisadi, basi kishafanikiwa kutimiza lengo lake la 'kuuma huku anapuliza' ili Watanzania tusimshtukie. Acha udanganyika kaka fungua macho uone mafisadi wanavyoiangamiza nchi.