mbona hawagusi waislam? kwasababu wangempa ukweli wake palepale, na wasingemkaribisha fisadi. akaona ngoja nikimbilie kwa wakristo wajingawajinga ambao naweza kuwapiga mchanga wa macho tu.....hahaha. kazi kwelikweli.
Asha wewe unataka kwenda nyumbani kufanya nini ?humwogopi mkewe?
Songambele,Viongozi wa dini wamekuwa wakiwasafisha mafisadi, na hata EL alipokelewa na viongozi wa kanisa hilo hilo, na pia sio mara ya kwanza wanasiasa kunadi sera katika membari za kidini.
Huyo Mchungaji wa Usharikwa wa Kinondoni alikuwa na nia ya kuukumbatia UFISADI kama sio tamaa ya pesa na kwa nini hajamshirikisha Askofu wake katika kumwalika RA tena mtu wa dini nyingine? Heko Askofu Malasusa na wana-KKKT kwa kung'amua hilo mapema.
Tunasikitika ya kwamba kanisa halikuwa na taarifa ya ujio wa Rostam Aziz. Tunapenda kuwataarifu kwamba, taratibu za kuwaalika wageni kwenye shughuli kama hizi hazikufuatwa,
"Nawashukuru kwa kuamua kunialika kuwa mgeni rasmi leo. Hii ni ishara kwamba mmeamua kupuuza viji-maneno na upuuzi wa vijiweni. Nafurahi kuwa miongoni mwenu hamtuhumu, hamshutumu, hampendi wenye wivu na wenye chuki, mnapenda haki. Ninao watoto watatu na nataka niwalee katika misingi hii",alisema Rostam huku akishangiliwa na umati wa watu walioshiriki hafla hiyo.
"Kutokana na ukiukwaji taratibu hizi, hayo madai yaliyonukuliwa katika vyombo vya habari kwamba ujio wa Rostam katika Usharika wa Kinondoni na tafasiri ya ujio huo kuwa kanisa linatambua usafi wake, si sahihi na ni madai potofu,
2.Watuambie ni kwanini walimruhusu Askofu Dr. Laizer kumpokea Lowassa kule Arusha kwa mbwembwe nyingi na hawakumkea ili khali Mhe. Lowassa alikuwa na kashfa ya ufisadi.Kwanini wanamuonea Mchungaji huyu?Je Akofu Dr. Laizer alipewa baraka na Kanisa kufanya hivi?bila kunipa majibu haya huu niuonevu kwa mchungaji wa kanisa hilo na wengine.
Kweli dunia imekwisha!!!
Sasa hilo kanisa, au huyo binadamu (askofu, Sheik) ambaye ana uwezo wa kuchambua fedha haramu na halali yuko wapi wajameni...!!! Tuache hizi siasa kila mahali hadi makanisani.
Mtu ametoa kwa moyo wake... mwenye kujua za halali au sio za halali ni Mola wake... acheni siasa wajameni!!!!
Mkuu think BIG,Gembe, kwanza heshima mbele!
Pili kuhusu hii mada yako umechanganya mambo mengi sana, ambapo mengine yana majibu ya papo hapo na mengine ni kwa wale wenye kujua muundo na utendaji wa KKKT.
Kuhusu matukio ya "Askofu Laizer + Mh. Lowassa" na "Mch Massege + Mh. Rostam" yote yana sura ya kisiasa lakini yametokea katika mazingira tofauti.
Askofu Laizer alikuwa mmojawapo wa waalikwa katika mkutano wa kumpokea Mh. Lowassa kule Monduli kwenye uwanja wa mpira, wakati Mh. Rostam Aziz alikuwa mwalikwa rasmi kwenye ibada iliyofanyikia kanisani!
Sasa ukiangalia vizuri utaona tofauti hapo, kwanini KKKT imeweza kuingilia hili la Rostam, ni kwa sababu aliaalikwa kanisani (kama Mgeni rasmi) bila kufuata utaratibu wa KKKT, wakati Askofu Laizer alialikwa kama mtu binafsi na hata alipopewa nafasi ya kuongea kule Monduli aliongea kama mtu binafsi na si kama Askofu wa KKKT (ninayo hotuba aliyoongea naweza kukutumia).
RA alialikwa na sio mara ya kwanza kuchangia kanisani hapo, KKKT kujitoa sasa kutakuwa hakuna maana kama mpaka watu wapige kelele ndio hatua zichukuliwe.
Viongozi wa dini wamekuwa wakiwasafisha mafisadi, na hata EL alipokelewa na viongozi wa kanisa hilo hilo, na pia sio mara ya kwanza wanasiasa kunadi sera katika membari za kidini.
Sasa ni Mungu gani huyo waliyomuomba akawaambia waende kumwalika RA ili awape kwaya milioni saba na na genereta?
Mkuu think BIG,
simple Logic,Kwani Rostam hakualikwa kama mtu binafsi?na hata Rostama liongea kama mtu Binafsi na si kama Mbunge sema aliongea mambo yanayohusu Siasa na vivyo hvyo alifanya Laizer.
Lengo si kumtetea Rostam,ila uhalali wa jambo lenyewe tu na uhalisia wa Maisaha ya kila siku katika makanisa yetu
Ben Carson..Mkuu Gembe, nakubaliana na wewe moja kwa moja! Kosa si la Rostam Aziz, kosa ni la uongozi wa Kanisa KKKT Kinondoni. Kwanini hawakutoa taarifa za mwaliko wa Rostam kwenye uongozi wa juu? Hapa ndipo kwenye tatizo, lakini Rostam kama Rostam yeye hana tatizo!
Mkuu think BIG,
simple Logic,Kwani Rostam hakualikwa kama mtu binafsi?na hata Rostama liongea kama mtu Binafsi na si kama Mbunge sema aliongea mambo yanayohusu Siasa na vivyo hvyo alifanya Laizer.
Lengo si kumtetea Rostam,ila uhalali wa jambo lenyewe tu na uhalisia wa Maisaha ya kila siku katika makanisa yetu