Robert Kisena atangaza kufilisika kwa UDA

Robert Kisena atangaza kufilisika kwa UDA

Kujitangaza kufilisika ni njia ingine ya kukwepa kulipa madeni ikiwemo kodi za serikali.

Sidhani kama itasaidia! Kwa serikali makini utalipa Kodi hata kwa mali iliyonje ya Kampuni husika! . Kilicho muhimu ni TRA kukuhakikia na kusema kweli tupu kuwa unadaiwa!. Mazingara hayo ya eti umefilisika hayatakuepeusha na dai la Deni hata kama dhamani ya vitu vilivyopo haitoshi kulipa kodi husika.
 
Lile gazeti lililoandika juu ya UDA na kukiihusisha na kiongozi mkuu mstaafu lilieleza kuwa kampuni ya ukaguzi wa hesabu (siikumbuki jina) iliweka wazi kuwa kampuni hii haikuwa na uzoefu wa masuala ya usafirishaji. Pia lilieleza kuwa kwa mmiezi miwili ya maisha ya kampuni iliweza kutengeneza faida ya Sh billion 1 huku ikiwa haijalipa kodi stahiki za serikali.
Kinachonichekesha na kunishangaza hapa ni jinsi kampuni inavyoweza kutengeneza bilioni za faida bila kufanya kazi yoyote wakati huo huo inafilisika wakati imepewa monopoly ya njia ya kivukoni pamoja na mambasi yaendayo kasi. Na ajabu kabisa wamiliki bado wana ujasiri wa kuitisha press conferences na kuongea wanachotaka! Watanzania hatuwezi kukwepa experiment ya vizazi vijavyo kufukua mafuvu yetu kujua tu aina gani ya viumbe!

Wonders will never end....another episode!
 
Wonders will never end....another episode!
NDO MAANA UNAAMBIWA HUYU KISENA HAKUWA NA UWEZO WA KUMILIKI UDA SO NI CARE OF ZA WENGINE KIDUMUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU CCM

HALAFU UTASIKIA LOWASA FISADI KWANI HUU SIO UFISADI?
 
Habari wadau,

Mmiliki wa UDA Ndugu Robert Kisena atangaza kufilisika kwa UDA kutokana na Madeni makubwa anayodaiwa ambayo inazidi fedha zilizomo kwenye account ya UDA.

Kampuni hiyo ambayo amesema ina magari kwa sasa 50 ambayo ni spana mkononi.

Madeni hayo ni bilioni 2 alizokwepa mwaka 2012 alipoingiza mabasi nchini na kutopeleka Michango ya NSSF na PAYE za wafanyakazi.

Chanzo: Dira
Picha ndio kwanza linaanza kuanzia na lile la home shopping centre
 
SIMON GROUP CO.LTD inayojitambulisha kununua shirika la usafiri Dar es Salaam ni wawakilishi wa viongozi wa Tanzania katika kufisadi mali za Umma.

Anae jitambulisha kama Robert Simon Kisena ambae alisoma Nsumba Sekondari School akijulikana kwa jina JOKALA KISEANA na kumaliza Kidato cha Nne mwaka 1991 baada ya hapo alijiunga na Kidato cha Tano Shule ya Sekondari Mirambo Tabora mwaka 1992, hapa alifukuzwa akiwa Kaka Mkuu baada ya kuwasaliti wanafunzi wenzake aliokuwa kiwachongea kwa mwalimu mkuu na wanafunzi kuungana na kusababisha kusimamishwa, baada ya hapa JOKALA KISENA ambae leo anajulikana kwa majina ya Robert kisena bila kutoa sababu za kubadilisha jina lake la awali alikuwan akikaa na rafiki yake uku akifanya kazi NCU Ushirika kanda ya ziwa-Nyanza,walikosana na rafiki yake aliyekuwa anakaa kwake baada ya kumpa mimba dada wa rafiki yake aliyekuwa akikaa kwake.

Katika Uchaguzi mkuu wa 1995 Kisena alichukuliwa na John Cheyo wakati huo Cheyo akiwa mgombea urais na kumuweka kuwa kama masidizi wa kusimamia mali zake Shinyanga,hapa ndio kisena alipata pesa kidogo isiyoweza kununua UDA.kisena katika kusimamia mali za cheo alifanikiwa kujenga nyumba Tatu zote zipo Nyegezi mwanza eneo lijulikanalo kwa jina la CALIFONIA.

Baada ya hapo ndio akaanzisha SIMON Agency iliyokuwa inajishughulisha na uuzaji wa spare za magari kwa muda na baadae akajiunga na Profesa Juma Kapuya akiwa waziri ambapo walifanikiwa kuanzisha kampunin iliyofahamika kwa jina la ROBASIKA-Robert Simon Kapuya na kufanikiwa kuchota bilioni 13 za wananchi kupitia Benki ya NMB mwanza kwa ushawishi wa kapuya na kuanzisha ginery ya pamba katika jimbo la kapuya .

Ndio maana ukifuatilia pesa zilizolipwa kwenye account ya Iddy Simba imelipwa na Robasika kwa niamba ya Simon Group ili wafanikiwe kuchukua UDA na Kapuya akiwamo uku Simon Group wakidai kuwa ni malipo iliyokuwa ikidaiwa na Simon Group kutoka kwa Robasika kutokana na mkataba kati ya Simon Group na Robasika wa kusafirisha mizigo.Robet kisena ni chambo tu katika kuwafanikishia watu maalum kazi.

Watanzania hapa kuna ujambazi wa mchana, tunaibiwa, Juma Kapuya, Iddy Simba, Didas Masaburi wanahujumu watanzania kupitia UDA.
asante sana mkuu , Mungu akupe ulinzi , PDG KAPUYA alishatajwa siku nyingi na ni kati ya wahusika wakuu lakini sijui kwanini hatajwi sana .
 
Lile gazeti lililoandika juu ya UDA na kukiihusisha na kiongozi mkuu mstaafu lilieleza kuwa kampuni ya ukaguzi wa hesabu (siikumbuki jina) iliweka wazi kuwa kampuni hii haikuwa na uzoefu wa masuala ya usafirishaji. Pia lilieleza kuwa kwa mmiezi miwili ya maisha ya kampuni iliweza kutengeneza faida ya Sh billion 1 huku ikiwa haijalipa kodi stahiki za serikali.
Kinachonichekesha na kunishangaza hapa ni jinsi kampuni inavyoweza kutengeneza bilioni za faida bila kufanya kazi yoyote wakati huo huo inafilisika wakati imepewa monopoly ya njia ya kivukoni pamoja na mambasi yaendayo kasi. Na ajabu kabisa wamiliki bado wana ujasiri wa kuitisha press conferences na kuongea wanachotaka! Watanzania hatuwezi kukwepa experiment ya vizazi vijavyo kufukua mafuvu yetu kujua tu aina gani ya viumbe!
Hivo hiyo kampuni ndio iliyo nunuliwa na prince akiwa na miaka 9?
 
It was a matter of time. Tangu awali Kisena hakuonesha dalili za kuwa na uwezo wa kutoa huduma ya usafiri wa jiji kubwa kama la Dar es Salaam. Anaweza kuwa na nia nzuri ya kuwa Mtanzania 'nguli' wa biashara ya public transport lakini aliharakisha sana kufia azma yake. Kwa sasa hivi angetafuta kampuni nyingine auze shares zake afanye mambo mengine. Usafiri Dar bado.
 
Yaani nguvu zimeniishia kabisa baada ya kusikia upumbavu huu....

Hivi jamani hili linakwenda wapi...mbona kama ni linchi la wendawazimu......

Yaani kila siku yanazuka mapya...

Nasemaje wakwepa kodi na wahujumu uchumi wote wachinjwe hadharani tena wachinjwe kwa msumeno....
 
Sidhani kama itasaidia! Kwa serikali makini utalipa Kodi hata kwa mali iliyonje ya Kampuni husika! . Kilicho muhimu ni TRA kukuhakikia na kusema kweli tupu kuwa unadaiwa!. Mazingara hayo ya eti umefilisika hayatakuepeusha na dai la Deni hata kama dhamani ya vitu vilivyopo haitoshi kulipa kodi husika.
Mkuu,
Kufilisika in Accounting Term means Mali unazozimiliki (Assets) ni Chache kuliko Madeni Unayodaiwa (Liabilities). Yaani ukiuza mali zako ZOTE hazitoweza kulipia madeni unayodaiwa. Kwahiyo sio wote watakaolipwa madeni yao 100%.

Sasa basi although kodi za serikali ni priority katika ulipaji wa madeni lakini inategemea kama hiyo kodi ishakadiriwa na kupitishwa (assessed and due). Kama haiko assessed au/na due basi imekula kwa serikali hiyo.
 
Yaani nguvu zimeniishia kabisa baada ya kusikia upumbavu huu....

Hivi jamani hili linakwenda wapi...mbona kama ni linchi la wendawazimu......

Yaani kila siku yanazuka mapya...

Nasemaje wakwepa kodi na wahujumu uchumi wote wachinjwe hadharani tena wachinjwe kwa msumeno....
Haha, kiongozi kwa sheria za nchi hatuwezi kufanya hivyo. Labda huko kwa wakomunisti. Kinachoniumiza nafsi ni kuwa, watu wanahitaji utawala wa sheria, lakini serikali ikijaribu kuendesha nchi kwa sheria sisi ndio tunaoanza kulia ovyo...
Inasikitisha...
 
Juzi juzi wametoka kukanusha kuwa ile familia ya wapi vile? Eti haina hisa na kwamba yeye kisena anaimiliki na familia yake na kutaja uwekezaji wa mabilioni ya fedha MARA LEO TENA IMEFILISIKA! !!!!! Halafu jamani wana JF mbona kila kampuni inayohusishwa na ile familia ghafla inatangaza kufilisika! !!!!!!!!!!! HSC ghafla tukaambiwa imefilisika. Mheshimiwa rais POMBE hebu closely watch that and please whoever you appoint to do that make sure was not appointed by.......kwasababu mjomba kuna masalia umeachiwa hahahahah TZ NCHI YANGU mweeeeh!
Siku zote njia ya muongo ni fupi kuliko mkojo.. hawa jamaa walituhadaa enzi hizo leo hii wameona ncji imekaa in a straight way wanaanza kusakiziana kila mtu abebe gunia la misumari. Kweli sasa tumepata kiongozi atakayetupeleka angalau ahatua moja mbele. Ila naamaini ahawezi kumaliza uchafu wote. Maana taka zilikuwa nyingi sana hapa nchini.
 
Haha, kiongozi kwa sheria za nchi hatuwezi kufanya hivyo. Labda huko kwa wakomunisti. Kinachoniumiza nafsi ni kuwa, watu wanahitaji utawala wa sheria, lakini serikali ikijaribu kuendesha nchi kwa sheria sisi ndio tunaoanza kulia ovyo...
Inasikitisha...
Lakini pia mkuu tuna sheria nyepesi sana za kupambana na ufisadi...rejea hukumu ya wale mawaziri wawili waliosababisha hasara kwa serikali zaidi ya bilionj tatu lakini hukumu waliyokutana nayo ni kichekesho kitupu....
 
amejifilisi au amehamisha, alete mapato na matumizi, afadhali ifilisike tubaki na ya zamani kwani haya msaada na line za kariakoo to feri zitarudi MUNGU amesikia kilio chetu sie wanyonge
 
Habari wadau,

Mmiliki wa UDA Ndugu Robert Kisena atangaza kufilisika kwa UDA kutokana na Madeni makubwa anayodaiwa ambayo inazidi fedha zilizomo kwenye account ya UDA.

Kampuni hiyo ambayo amesema ina magari kwa sasa 50 ambayo ni spana mkononi.

Madeni hayo ni bilioni 2 alizokwepa mwaka 2012 alipoingiza mabasi nchini na kutopeleka Michango ya NSSF na PAYE za wafanyakazi.

Chanzo: Dira
Only in Tanzania
 
Wana JF,

Tayari baada ya simtomfahamu ya siku nyingi kati ya UDA na serikali, sasa uDA imefilisika rasmi, wananchi kwa ujumla tumefurahi kwani zilikuwa hazina msaada wowote richa ya kuwa sehemu ilidhaniwa kuwa ni mali ya serikali kumbe tushapigwa changa la macho na watu kujichukulia kwa fedha kiduchu, baada ya hapo wakaanziasha ruti fupi fupi kudhurumu watu, ndipo mkono wa Mungu ukaingilia kati na UDA kufilisika.

Hata hivyo ni janja ya kukwepa kodi, inabidi walipe tu wakishindwa wakauziwe nyumba zao.
 
Back
Top Bottom