Kisutu, Dar: Robert Kisena apandishwa Kizimbani kwa Utakatishaji fedha, asomewa mashitaka 33

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,789
11,931
IMG_20220509_182358_578.jpg

Robert Kisena (wa kwanza kulia) akiwa na washtakiwa wenzake

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (UDART) Robert Kisena na wenzake watatu wamesomewa mashtaka 33 katika kesi mbili tofauti kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikiwemo Utakatishaji wa fedha na kuongoza genge la uhalifu.

Kwenye kesi namba 21 ya mwaka 2022 inawahusu Kisena na wenzake wawili ambapo ni Charles Newe (48) na Tumaini Kulwa (44) wanadaiwa kujipatia kwa njia ya udanganyifu kaisi cha cha Shilingi 4.5 Bilioni huku wakituhumiwa kutakatisha na kusababisha hasara serikali kiasi hicho hicho.

Katika kesi namba 20 ya mwaka 2022 Kisena na washtakiwa watatu akiwemo Newe, Kulwa na John Samangu (66) wanadaiwa kutakatisha kiasi cha Shilingi Milioni 750 ambazo zinadaiwa kuwa ni zao la kughushi na kulaghai.

Washtakiwa hawakuwa na haki ya kujibu chochote kwa Mahakama hiyo kwani haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo kisheria.

Watuhumiwa wamerejeshwa mahabusu ya magereza mpaka tarehe 23 Mei 2022 shauri hilo litakapotajwa.

Wote Wamekosa dhamana.


PIA, SOMA:

- Robert Kisena wa UDA na wenzake, wafikishwa Mahakamani Kisutu, wasomewa Mashtaka 19
- Kisutu: Robert Kisena afutiwa Mashtaka ya utakatishaji fedha na Mahakama. Yeye na Mkewe wakamatwa tena, wafunguliwa mashtaka mapya
 
Haya mambo inaonekana nyuma yake kuna mkono mrefu usioonekana.

Huyu jamaa kawekwa kati na makundi mawili ya wapigaji, moja kiongozi wao alishatwaliwa, na jingine kiongozi wake bado yupo, ndilo limeshika hatamu kwa sasa, hakika ana mtihani.
 
Hivi kuna kesi ya upigaji wa fedha ndefu kiasi hicho ilishawahi mkalisha mtu jela mpaka Sasa..?
 
Back
Top Bottom