Robert Kisena atangaza kufilisika kwa UDA

Robert Kisena atangaza kufilisika kwa UDA

Kununua mabasi ya Eicher lilikuwa kosa kubwa sana (grave mistake)... Hayo mabasi hayana uimara wa kuhimili mikiki mikiki ya kibiashara. Bora hata wengenunua ma DCM yangewatoa kibiashara kuliko hayo mabasi ya Eicher...
 
Kununua mabasi ya Eicher lilikuwa kosa kubwa sana (grave mistake)... Hayo mabasi hayana uimara wa kuhimili mikiki mikiki ya kibiashara. Bora hata wengenunua ma DCM yangewatoa kibiashara kuliko hayo mabasi ya Eicher...
Eicher si ndio DCM mpya sema tu yamekuwa nyanya kuliko DCM original!
 
Eicher si ndio DCM mpya sema tu yamekuwa nyanya kuliko DCM original!
Hakuna uhusiano kati ya Eicher na DCM. Sema hiyo ilikuwa strategy ya jamaa kuingia sokoni waliwandanganya wateja kuwa DCM imerudi tena sasa inaitwa Eicher. But it was not true. DCM ni gari ya Mjapani ya Toyota (Dyna Cliper) wakati Eicher ni magari ya kihindi yanayotengenezwa kwa uangalizi wa Mitsubishi....
 
sasa lile zoezi la kupora mali za UDA ndio linaingia episode ya mwisho. kuna depot kubwa inapakana na bandari kurasini. hili ni eneo lenye thamani kubwa na tayari linatumika kama bandari kavu au litakua kwa shughuli hiyo kama bado. pia kipo kiwanja cha bus station pale oppossite na TRA. hizo tu ni mali za uda za thamani kubwa. huyu kisena amekua anajidai amewekeza kiasi kikubwa uda huku wajuzi walikua wanasikiluzia mwisho wa hivyo vibasi nyanya vya kihindi ambavyo kwa usafiri wa mjini ni upuuzi tu. sasa watatafuta mfilisi ili wakopeshaji wa kihindi wapore mali iliyokua ya umma kwa manufaa binafsi.
Habari wadau,

Mmiliki wa UDA Ndugu Robert Kisena atangaza kufilisika kwa UDA kutokana na Madeni makubwa anayodaiwa ambayo inazidi fedha zilizomo kwenye account ya UDA.

Kampuni hiyo ambayo amesema ina magari kwa sasa 50 ambayo ni spana mkononi.

Madeni hayo ni bilioni 2 alizokwepa mwaka 2012 alipoingiza mabasi nchini na kutopeleka Michango ya NSSF na PAYE za wafanyakazi.

Chanzo: Dira
a
 
Kwa nini ni lazima huo mradi wa DART ukaendeshwa na hao wapigaji wa UDA kwa nini isitangazwe Tenda akapatikana mzabuni wa uhakika kuriko huyu inaonekana kuna ujanja ujanja fulani katika hii kazi..
 
Kutumia mabasi ya eicher ndio kosa kubwa alilolifanya na wengine tulisema sababu tulikuwa nayo na gharama kuyahudumia pamoja na life span ni fupi sana ukilipa mkopo tu unabaki na kimeo. Fidhahussein (africarriers) yeye keshapiga hela na uda wanaendelea kununua vipuri kutoka kwake ambavyo ni ghari sana.
 
Update record zako mkuu. Simon Group anamiliki 76% ya share baada ya kununua share za jiji na serikali (hazina) bado inamiliki 23%, hivyo technically inatuhusu.
Ok. Kama ndio asilimia 23 tu ndio za serikali inazimiliki basi ni kweli kwa mujibu wa Public Corporation Act Uda sio shirika la umma. Kwani ili liwe shirika la umma inabidi serikali imiliki asilimia 51 or above.
 
Kwa mda mrfu nchi hii ilikosa kiongozi kwa ilikuwa inajitawala kiasi kwamba kila mwenye uwezo wa kuchuma alichuma anavyo weza, inashangaza sana kwa nn hizi campuni zinafirisika wakati huu? na zote zinazo husishwa na Familia ya mzee wa msoga.
 
TAARIFA KWA UMMA

Kumekuwepo na taarifa za uwongo kwenye vyombo vya habari, hasa kijarida cha Dira ya Mtanzania, na mitandao ya kijamii kuhusu uongo kuwa kufilisika kwa Shirika la Usafiri Dar Es Salaam (UDA) Limited.

Menejimenti ya Shirika la Usafiri Dar Es Salaam inakanusha uwongo huo kuwa UDA haijafilisika na haina dalili zozote za kufilisika isipokuwa ni Shirika la namba moja nchini na Afrika Mashariki na Kati linalokuwa kwa kasi ya ajabu kimaendeleo na kibiashara.

Zifuatazo ni takwimu zinazodhihirisha ukweli huu:

  1. UDA imeongeza idadi ya mabasi kutoka mabasi 7 makukuu na mabove Mwaka 2012 na kufikia takribani mabasi 400 mwaka 2015 yakiwemo mabasi 255 ya kawaida na mabasi makubwa - Hercalus, mapya na ya kisasa kabisa duniani (ya BRT) 140.
  2. Ndani ya miaka 3, kampuni ya UDA imekuwa kwa zaidi ya asilimia 5,000
  3. Kampuni hii imeweza kufanya maandalizi yote ya kuwezesha kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project) kwa ufanisi mkubwa. Mbali na kununua mabasi, kampuni imeweze kununua mtambo bora na wa kisasa kabisa duniani wa kukusanya nauli na kuongezea mabasi (Intelligent Transportation System – ITS) wenye thamani kubwa kutoka Ubelgiji na Ujerumani. Vile vile kampuni imeweza kusaili na kufundisha madereva wa Kitanzania zaidi ya 300 na kuwaajiri kwa ajiri ya kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project)
  4. Kampuni imejenga karakana bora na imara na kununua vitendea kazi vya kisasa kwa ajiri ya mabasi yake ya kawaida na mwendo haraka.
  5. Kampuni imepeleka watendaji wake kwenye miradi mbalimbali ya BRT duniani ili kupata uzoefu wa kuwawezesha kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project) kwa ufanisi. Vile vile Kampuni imeweza kuajiri wataalam kutoka nje (expatriates) kwa ajiri kuongezea nguvu wataalam wake wa ndani.
Kwa takwimu chache hizo hapo juu, Kampuni ya UDA ni namba moja Afrika kwenye sekta ya usafirishaji wa abiria barabarani kwa idadi ya watu inaosafirisha, idadi ya mabasi na ubora wa menejimenti.

Mafanikio haya ya Kampuni ya UDA yanatokana na umahiri wa uendeshaji kutoka Simon Group chini Uongozi thabiti wa Mwenyekiti wake Ndugu Robert Simon Kisena na si vinginevyo, kama washindani wetu wavyojaribu kutuchafua kwamba kuna wanasiasa nyuma yake.

Tunawataka washindani wetu waache tabia ya fisi ya kumfuata mtu anayetembea kwa haraka wakidhani atandondosha mkono wapate kitoweo vinginevyo watakufa njaa.

Imetolewa na Uongozi wa SHIRIKA LA USAFIRI DAR ES SALAAM (UDA) LIMITED


Habari wadau,

Mmiliki wa UDA Ndugu Robert Kisena atangaza kufilisika kwa UDA kutokana na Madeni makubwa anayodaiwa ambayo inazidi fedha zilizomo kwenye account ya UDA.

Kampuni hiyo ambayo amesema ina magari kwa sasa 50 ambayo ni spana mkononi.

Madeni hayo ni bilioni 2 alizokwepa mwaka 2012 alipoingiza mabasi nchini na kutopeleka Michango ya NSSF na PAYE za wafanyakazi.

Chanzo: Dira
 
Ok. Kama ndio asilimia 23 tu ndio za serikali inazimiliki basi ni kweli kwa mujibu wa Public Corporation Act Uda sio shirika la umma. Kwani ili liwe shirika la umma inabidi serikali imiliki asilimia 51 or above.
Serikali haina significant control ila ina significant influence na UDA na uda ikipata hasara anaadhirika pia,maana yeye ni associate
 
Mkuu Shark upo sawa hapo. Bankruptcy maana yake assets ni chache kuliko liabilities. Ambacho sijamuelewa Kisena ni hoja yake kwamba pesa zilizopo kwenye account hazitoshi kulipa madeni? Hii ni hoja mufilisi maana asset sio cash kwenye account tu. Kuna fixed assets, kuna receivables, cash yenyewe nk. Akajipange upya declaration of bankruptcy is not that easy!
 
Back
Top Bottom