Uchaguzi 2020 Robert Amsterdam amuandikia barua Rais Magufuli siku 5 kabla ya Uchaguzi

Kwani Robert kasemaje? Naona wanaomponda wote hawajaelewa alichosema. Mm kwa kweli siwapendi watu wanaoingilia Uhuru wa nchi za watu. Uhuru wa watu na sio hawa wanaosema boksi la kura liheshimiwe. Tume ni ya Tz, tupo salama. Tl akapigwe kwenye boksi la kura na si vinginevyo.

Sijui kama unaelewa ulichokisema! Kuna 15 presidential candidates. Hivi kama kila candidate atatafuta foreign actors wa kuipa nchi maelekezo, hii nchi itakuwa taifa la aina gani?
 
Mimi ni miongoni mwa wasio na chama, ila kwa barua hizi za kuingilia uhuru wetu toka nje ya mipaka yetu, kura yangu nitampigia Magufuli kwa kweli.

Hii ni dharau kwa uhuru wetu.

Imagine. Tena wanaomshabikia Amstadamz wengi eti ni Wanaume. Dah Tanzania nchi yangu wale wanaume majasiri kama simba wameishia wapi. Yaani wenye misimamo na wanaoweza kuthamini na kutetea utu wao kama wewe Tanzania wamebaki wachache mnooo

Tarehe 28 tukampe 5tena jemadari John Pombe Magufuli
 
Hali ya Libya ikoje sasa? Kwa hiyo, unataka taifa letu nalo liingie kwenye huo mtego, ambao umeinasa na kuiua Libya?
Hayo yapo mikinoni mwa Rais Magufuli
Libya Sasa hivi wale vijana waliokua na kiburi kama kheri james wapo jela wanafanywa vibaya wengine ni wakimbizi
Afadhali Libya kuliko Tanzania ya akina James
 
Sijui kama unaelewa ulichokisema! Kuna 15 presidential candidates. Hivi kama kila candidate atatafuta foreign actors wa kulipa taifa maelekezo, hii nchi itakuwa taifa la aina gani?
Swala siyo kwamba unaambiwa na wangapi,swala ni msingi wa unavyoambiwa & kwenye kesi Hii hoja ya msingi ipo
 
Hujui unachokisema. Tembelea Libya ukajaribu kushinda JF kama unavyofanya sasa kisha utupe mrejesho!
Libya mchaka mchaka wake sio mdogo
Wanasema msiba wa wengi harusi
Hakuna cha polepole wa Mavi 8 wala maJames wote kimbembe tu
Lakini bongo kuna watu wanakula kuku wengine wanateseka Sana
Mimi naona kama noma na iwe noma na kama neema iwe neema sio wengine wanaonea wengine
 
Ila kuliingiza jeshi kwenye siasa ni jambo baya sana iwapo limefanyika.

Ikitokea vita (hatuombei) unadhani tunaweza kuwa wamoja tena?Mwalimu alituongoza kushinda vita vya uganda,je kwa hivi leo hali ilivyo watu wanavyochukiana na tena jeshi nalo lijiingize,mbona ni hatari?

Hivi kweli hakuna watu wenye hekima nchi hii kila mtu anawaza tu tumbo lake?Hasha siamini.Najua mpo wenye hekima.Vaeni ujasiri,muondoe hali hii.Mungu atawabariki kwa ajili ya nchi yetu.
Jiwe amepandikiza chuki na mafarakano nchini, uzalendo kwa sasa umeshuka sana
 
Kwa mtu anayejua jinsi ya ku shape siasa za Marekani-Washington atamwambia nguvu ya Lobby Firms,hawa jamaa wana ushawishi mkubwa mnoo na ndiyo maana hata ukiangalia tokea jamaa anamwakilisha Lissu Marekani imekua inaongelea siasa za Tanzania kwa ukaribu sana,na jamaa keshasema anakusanya ushahid ili kuapply sanctions kwa viongozi wa serikali kupitia US & UK magnitsky Law-NEC siyo Wajinga wanaporekebisha baadhi ya mambo huyu jamaa anayoyakosowa-& infact Amsterdam keshasema tumesha qualify for sanctions and its a guarantee there will be sanctions.
Bora kuwekewa vikwazo kuliko kuwa na kiongozi kibaraka au wakala wa wanyonyaji.
Heri kufa masikini kuliko kukubali kuwa mtumwa wa wanyonyaji.
Heri kufa tukiwa tumesimama kuliko kuishi tukiwa tumempigia magoti mnyonyaji.
 
Libya mchaka mchaka wake sio mdogo
Wanasema msiba wa wengi harusi
Hakuna cha polepole wa Mavi 8 wala maJames wote kimbembe tu
Lakini bongo kuna watu wanakula kuku wengine wanateseka Sana
Mimi naona kama noma na iwe noma na kama neema iwe neema sio wengine wanaonea wengine

Wewe unayeishi maisha kama ya Libya unawezaje kushinda na sisi hapa JF? Kama kweli unaielewa Libya, tueleweshe juu ya hili.
 
Back
Top Bottom