Washawasha
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 16,974
- 13,429
Twende kazi mkuu,inanoga ile mbaya
Nalog off
Nalog off
Kutafutiana kesi sasà huko maana shemejio ndo mida yake ya chapa ilale.Nitakuja usiku inshallah around saa 3
Bingoooo- 17 -
Riwaya: MSAKO
Mtunzi: Japhet Nyang’oro
Frank Misanya yeye akasema ahesabu kila kitu kimeshakamilika. Akapiga simu nyingine mbili kwa vigogo. Halafu akapiga masafa marefu huko ughaibuni. Alipomaliza, alijuhusudu yeye mwenyewe; hakuna ambaye angeweza msifia kwa vile wachache waliokuwa wanajua alichokuwa anafanya. Na mbinu yake ni moja, kila aliyempa kazi alimpa kipande cha kazi, kazi kamili alikuwa akiijua yeye mwenyewe. Huyo ndiyo Ngongoseke Amos Nkwija.
*****Kitabu cha riwaya hii sasa kinachapwa kwa idadi ya wale walioweka ODA tu, kinatoka tarehe 15/6/2020. Weka ODA yako sasa 0762204166********
BAADA ya kutoka yalipo majengo ya Ofisi Fukuzi, mpelelezi Jacob Matata aliazimia kuanzia nyumbani kwa Afande Lucas. Kufutwafutwa kwa faili alilokuwa ameandaa kisha kuuawa ilikuwa dalili tosha kuwa kuna hatua alikuwa amepiga katika uchunguzi wake. Hivyo kwenda msibani na kuonana na mjane aliona kuwa lingekuwa wazo zuri. Afande Lucas alikuwa akiishi uraiani, Mwananyamala Komakoma jirani na Mwinjuma road.
Hakupata shida kuiona nyumba yenyewe, wamama wenye khanga tatu-tatu walionekana kufanya hili na lile. Upande wa kulia wa nyumba hiyo kulikuwa na turubai lililowekwa ili kuwapa watu kivuli. Aliangalia saa yake ya mkononi ilikuwa saa tano na dakika arobaini asubuhi. Kama utakumbuka wakati huu ndiyo Bi. Anita na yeye alikuwa ofisini kwake. Jacob Matata aliendesha taratibu kuliendea eneo lile. Hakukuwa na sehemu ya kuegesha gari hivyo alipitiliza kwa mwendo mdogo huku akijitahidi kutafuta sehemu ya kuegesha. Mbanano wa nyumba na ujenzi usio na mpangilio katika eneo hili ulifanya uzuri wa nyumba ambayo watu walikuwa wamejaa usionekane.
Aliiangalia ile nyumba ambayo aliamini kuwa ndiyo yalipo makazi ya marehemu Inspekta Lucas. Ilikuwa nyumba nzuri ya kisasa na thamani kubwa. Alishangaa kuona nyumba kama ile kujengwa eneo kama lile, maana nyumba kama hizo huonekana yale maeneo ya watu wazito. Kingine alichoshangaa ni kwa namna gani Askari Polisi alifanikiwa kujenga nyumba ya kifahari kama ile, ila alipokumbuka kuwa kwenye nchi yake mtu anaweza pata pesa kwa njia nyingi, alinyamaza. Kutafuta sehemu ya kuegesha kulimpeleka hadi mtaa wa nyuma ambapo kulikuwana kiwanja ambacho hakijajengwa. Hapo alikuta magari kadhaa yakiwa yameegeshwa. Kwa bahati nzuri aliona sehemu ambayo alipachika gari alilokuwa anatumia ambalo alikuwa amelikodisha. Hakuona busara kwenda nyumbani kwake baada ya yale yaliyokuwa yametokea usiku. Pia, isingekuwa akili nzuri kutumia gari lake analotumia siku zote. Hadhari lilikuwa jambo la msingi sana kwake wakati huu. Baada ya kuteremka na kufunga gari aliangaza kama anaweza pata kichochoro cha kumpeleka nyumbani kwa Afande Lucas, badala ya kuzunguka na barabara. Mara hii tena bahati ilikuwa upande wake, aliona kichochoro ambacho pia kilikuwa kikipitisha maji machafu. Haikuchukua muda alihisi yuko nyuma ya nyumba aliyokuwa akiiendea maana aliweza kusikia sauti za watu wakiongea katika hali ya kushirikiana kazi za upishi. Aliendelea mbele kidogo hadi alipokuwa usawa wa dirisha moja. Alipofika hapo alisita kidogo baada ya kusikia sauti ambayo haikustahili kusikika msibani. Alisimama kisha akajivuta ukutani jirani na lile dirishi ilikotokea ile sauti nzito ya amri.
“Kama akija mtu atakayejitambulisha kwa jina hilo tupe taarifa, maana mtu huyo ni hatari kwako na familia yako. Chukua simu hii, ukiminya tu hiki kidude utaongea na mimi moja kwa moja nami nitatuma askari wakusaidie. Pia, ukihitaji hela ziko kwenye akaunti yako ya benki.” Ilikuwa ni sehemu ya sauti hiyo nzito iliyoongea kwa amri. Jacob alitaka kuchungulia ili amwone aliyekuwa akiongea lakini kulikuwa na pazia zito hivyo hakufanikiwa. Aliharakisha kutembea ili awahi kuwaona watu hao kabla hawajatokomea. Akiwa na matumaini ya kufanikisha hilo mara uchochoro ule ukampeleka mbele ya dimbwi kubwa la maji machafu. Kwa mbele yake kulikuwa na choo ambacho kuta zake zilikuwa ni mabati na pembeni yake ambapo ndio kichochoro hiki kilipita lilichimbwa hilo shimo kubwa lililokuwa na maji machafu. Ilivyokuwa hakuwa na namna ya kuenedela na kichochoro hicho la sivyo ajitolee kutumbukia kwenye maji yale. Aliangalia kwa namna ya kukata tamaa, hii ilimaanisha asingeweza kuonana na yeyote aliyeongea kwa ile sauti. Alikata shauri kurudi na kuzunguka na barabara.
* * *
Wakati Jacob Matata akikwama kwenye kile kichochoro, Luteni Frank Misanya yeye alikuwa ndani ya gari lake akiendesha wakati simu ya Ngongoseke ilipoingia. Alipunguza mwendo wakati anakunja kushoto mbele ya Chuo cha Diplomasia akiiacha barabara ya Kilwa na kuingia Kurasini, mkono wa kushoto ulichukua simu hiyo iliyokuwa ikilia kwa fujo.
“Sema!’’ Alisema baada ya kuona namba asiyoifahamu “Ngongoseke hapa.” Alijitambulisha.
“Sema Mzee!’’ Luteni Misanya alisema.
“Nilikwambia wale vijana wamejua mengi kuhusu kazi zetu....” Ngongoseke alisema kabla hajakatizwa na Frank,
“Yaani umejuaje hapa ndio nakaribia nyumba wanayoishi, nataka nikawam...” Frank alisema lakini naye alikatishwa,“ Nilikwambia usiwaue wewe. Sasa sikiliza, sasa hivi wapeleke pale anapokaa Nanalungu, Jacob Matata, yuko hapo.” Ngongoseke alisema
“Aaaaah, aisee wewe Mzee ni kiboko!” Luteni Frank alisema, maana alishaelewa akili ya Ngongoseke.
“Ulikuwa hujui au unathibitisha tu?’’ Ngongoseke alisema kwa majivuni.
“Akili yako inafanya kazi kwa kiwango cha ajabu sana.” Frank alisema.
“Waende sasa hivi maana nimeambiwa Jacob yuko hapo muda huu. Yeye atatusaidia kuwaua.” Ngongoseke alisema.
* * *
Robo saa baada ya Ngongoseke kutoa maelekezo hayo kwa Luteni Frank Misanya, Jacob Matata yeye sasa alikuwa mbele ya mlango wa chumba alichoelekezwa kuwa mjane wa Afande Lucas alikuwemo. Kama alivyoiona kwa mbali, ilikuwa nyumba kubwa ambayo hukuhitaji elimu kubwa kuitaja kuwa ya kifahari japo ilikuwa maeneo yasiyoistahiki kuwepo. Alibisha na kukaribishwa. Aliangaza macho huku na huko. Kilikuwa chumba kilichojaa wanawake tu, ambao wengi wao macho yao yalikuwa mekundu na wengine yakiwa yamevimba. Mara alimwona msichana mmoja mrembo wa haja ambaye pembeni yake kulikuwa na kitu kama simu. Macho yake yakavutika na muundo wa ile simu, aliiangalia tena kwa makini na mara Jacob Matata akabaini kwa kilikuwa kinasa sauti. Akili ya Jacob Matata ilifanya kazi haraka, alijua yule mtu mwenye sauti ya amri ndiye aliyempatia huyo mwanamke kile kifaa akimdanganya kuwa ni simu ili aweze kurekodi mazungumzo yote ya yule Mjane wa Afande Lucas.
“Pole sana dadangu!” Jacob alisema baada ya kuwa ameinama alipokuwa ameketi yule dada. Alikuwa mwanamke, mzuri, mrembo wa umri wa kati, si mtoto si mtu mzima. Maana Jacob yeye anajua kuwa urembo na uzuri kwa manamke ni vitu viwili tofauti, lakini huyu alikuwa navyo vyote.
“Asante sana!” Alisema yule msichana kwa sauti kavu, huku akijitahidi kumwangalia Jacob Matata.
“Sijui unawe......” Kabla Jacob Matata hajamaliza alichotaka kusema, yule mwanamke haraka akaweka kidole katikati ya midomo yake kama ishara ya kumtaka Jacob Matata anyamaze. Kisha akasimama na kumwonyesha Jacob ishara kuwa amfuate.
“Bila shaka unaitwa Jacob Matata?’’ Msichana alihoji. “Kama ndiye?’’ Jacob alisema kwa mshangao.
“Ndiye wewe, maana hata jibu lako limekuwa sawa na nilivyoelekezwa na mume wangu. Naitwa Nana Lucas, marehemu mume wangu katika siku zake za mwisho alikuwa anakutafuta sana. Alijua maisha yake yako hatarini ila hakuona kama angeweza pata msaada toka kwa mtu yeyote yule mwingine zaidi yako. Juhudi zake za kukutafuta hazikuzaa matunda hadi alipouawa. Ila akawa amenielezea sifa zako akiwa na hakika kuwa kwa namna moja ama nyingine ungeingia kupeleleza kitu alichokuwa ameanza kupeleleza. Hivyo alikuwa na hakika kuwa ipo siku ungekuja kwangu. Hivyo nilivyokuona tu mara moja nikajua ndiye.” Alisema yule mwanamke huku sasa machozi yakiwa yanamtiririka. Jacob alimvuta na kuanza kumbembeleza.
“Je, unaweza kuniambia kama kuna lolote alitaka unifikishie?’’ Jacob alisema kwa sauti ya kubembeleza pia, huku akili yake ikiwa makini kabisa.
“Jumatatu wiki iliyopita ndiyo alikuja akiwa amebadilika sana. Nikamuuliza vipi, akaniambia kuna kazi amekuwa akifanya, anasema uchunguzi wake umemfikisha sehemu ambayo amegundua kuna watu wa usalama na viongozi wanahusika. Hilo halikumtisha sana, ila anasema alimtembelea Luten Frank Misanya, baada ya kuongea naye amemtishia maisha kama hatoachana na kazi hiyo. Hivyo akaniambia nikikuona nikuombe uanzie kwa Luten Frank Misanya.” Alisema yule msichana huku akilia kwa kwikwi.
“Je, kuna jingine Nana?’’ Jacob alihoji.
“Hapana Jacob, ila kuna watu walikuja wakijifanya wao ni Jacob Matata na kuniuliza kama kuna ujumbe wowote marehemu aliuacha kwa ajili yao. Lakini katika wote sikuona kama kuna mtu ana viashiria vya sifa ambazo mume wangu aliniambia. Hivyo sikusema lolote.’’
“Okay, bila shaka ndiyo waliyokupa hiyo simu ambayo pia ni kinasa sauti?’’ Jacob alihakiki.
“Ndiyo, nilipoiona niligundua. Wengi hudhani miye ni mwanamke wa kawaida tu, lakini si kweli. Ni mtu niliyepitia mafunzo mengi ya namna hiyo wafanyayo na mapenzi yangu kwa Lucas yaliyonifanya nijitulize kwake. Lakini hivi nilishapanga kama nisipokuona kesho nianze mikakati ya kisasi. Mazishi tumefanya jana, nilipanga kupumzika leo halafu kesho nianze mishe-mishe.” Nana alisema.
“Ulipanga ungeanzaje kulipa kisasi?’’ Jacob alihoji.
“Sina mpango kamili kwa sasa, ila kwa harakaharaka bila shaka ningeanza na waliokuja kunipa hii simu.” Nana alisema.
“Nadhani inaweza kuwa hatari kuliko unavyodhani.’’ Jacobo alisema kisha akamkumbatia yule Msichana ambaye sasa alianza kububujikwa na machozi.
“Nini kimekufanya uamini kuwa mimi ndiye Jacob Matata?’’ Swali hilo la Jacob lilimfanya yule msichana amsukume Jacob na kujitoa mikononi mwake. Akamwangalia kwa muda kana kwamba ndiyo kwanza anamwona. Kisha kwa sauti ya kutafakari akasema, “Wewe siyo kama askari wengine, askari ni wababe na wala siyo kama jambazi, una mvuto kwa mwanamke na ndiyo mume wangu alivyoniambia. Kitendo cha kupiga magoti pale wakati unanisalimia, muonekano wako na ulivyoitoa ile pole ilikuwa alama tosha kuwa wewe ndiye!’’ Alisema alafu akamkumbatia tena Jacob Matata huku, akilia kwa sauti na uchungu.
“Jacob, nisaidie kulipa kisasi kwa Mwenda wangu. Niko tayari kukusaidia kama ukitaka!’’ Alisema kwa uchungu, sauti yake kama iliingia kwenye masikio ya Jacob, haikuishia hapo tu bali iliingia kwenye nafsi na moyo wake. Matokeo yake akajikuta akisema,
“Tuombe uzima, Mungu atusaidie.”
"Kwa nini nisiwapigie halafu uje uwakamate Jacob?’’ Nana alihoji.
"Wazo zuri lakini sishauri ufanye hivyo. Watu hawa si wa kuwafanyia mzaha hata kidogo. Endelea kuwepo, ukiwa mtulivu na kufanikiwa kuwafanya wasijue kuwa umeonana na mimi hilo litatusaidia sana mbele ya safari tukiendelea kuwa hai. Lengo si kupata tawi bali mzizi wa mambo haya.’’ Jacob alisema huku macho yake yakiwa yametulia kifuani kwa Nanalungu. Alihusudu jinsi Afande Lucas alivyokuwa amefanikiwa kuchagua mwanamke mrembo.
Kama umesoma weka like na comment yako nijue tuko wote[emoji1488]
Utaikuta kesho.Kutafutiana kesi sasà huko maana shemejio ndo mida yake ya chapa ilale.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]pole sana unajua nimezurura mchana nimechokaKutafutiana kesi sasà huko maana shemejio ndo mida yake ya chapa ilale.
Poa poa lazima uchakarike ili mpasta Jr aende chooni boss[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]pole sana unajua nimezurura mchana nimechoka
NakujaMkao kula!
Poa kaka!Nakuja
Nasikia hadi kesho ndiyo anatoa kipande kingineMida ya kuchungulia
Kule tayari bossNasikia hadi kesho ndiyo anatoa kipande kingine
Nishapita kitamboKule tayari boss