Riwaya ya Kijasusi: "Msako wa Mwehu"

mtzmweusi

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
8,593
8,876
-1-

“KWA NINI UMEMCHAGUA POKA KINGU, wakati siku za karibuni kumejitokeza mafundi wengi wa kufanya mauaji, kwa ustadi wa hali ya juu?’’

“Huyu anafaa! Aliongea Ngongoseke
“Ndiyo niambie sasa, kwa nini anafaa?
“Poka Kingu ni mvivu.” Akajibu Ngongoseke kwa utulivu huku akifikiri.

“Uvivu ni sifa nzuri ya kumchagua mtu?” Mzungumzaji wa upande wa pili wa simu, ambaye ni mzungu. Akauliza kwa mshangao.

“Hasa!” Ngongoseke akasisitiza.
“Yaani unataka mtu mvivu, kwenye kazi ngumu na hatari kama hii?” Mzungu huyo akauliza, kutoka upande wa pili wa simu. Katika mshangao usiyoelezeka.

“Ndiyo! Nimepitia mafaili takribani saba, niliyoletewa mezani, yenye sifa za watu ninaowahitaji, kwa ajili ya kazi hii. Nimejiridhisha kuwa, Poka Kingu ana vigezo vya kuwazidi wengine. Kutokana na kazi ninayotaka ifanyike.” Akaongea Ngongoseke kwa hakika. Mkono wake mmoja ameshika kiwambo cha simu sikioni, mkono wake mwingine, ukipapasa waya wa simu hiyo ya mezani.

“Sifa yenyewe ndiyo iwe uvivu?”
“A killer on the payroll isn't good for business. Sitaki mazoea, nataka msisimko wa kazi.” Ngongoseke akasisitiza.
“Unadhani mtu aliyeko kwenye orodha ya malipo, hafai kwa kazi hiyo?” Mzungumzaji wa upande wa pili, akauliza kwa udadisi. Akionekana kutoridhishwa na uamuzi wa Ngongoseke.

“Vidole vyao ni vizito kwa shabaha, mishipa yao imejaa mafuta kwa sababu wanalipwa mishahara minono na kula ovyo. Hawana njaa wala mdadi wa kazi.” Akafafanua Ngongoseke.

“Hii kali! Yaani uvivu umekuwa sifa kwa muuaji tishio!” Akashangaa Mzungu simuni.
“Sitaki mtu anayeua kwenye muda wa nyongeza, yaani, extra time killer. Mtu ambaye ananiweka kwenye wasiwasi kwa muda mwingi. Nataka muuaji anayekamilisha kazi yake bila kutoa jasho, ndani ya sekunde za awali za tukio.” Ngongoseke akafafanua.

“Okay! Sifa nyingine ni ipi?”
“Poka Kingu anaweza kuishi kama mzimu. Kwa vile ana hulka ya uvivu, hapendi kupambana na mtu kwa muda mrefu. Hivyo hujua namna ya kujificha na kuua haraka, pale anapopata nafasi finyu ya kufanya hivyo. Kwenye kazi hii, sitaki mtu wa kuremba. Kumbuka watu tunaokwenda kupambana nao, hawastahili kupata nafasi ya kuishi mara mbili. Lazima wafe hata kwenye mpenyo mdogo wa kupitisha wembe.

“Uvivu wake umemfanya awe mtu anayeshika rekodi ya juu barani Afrika. Rekodi ya kuua watu wengi ndani ya muda mfupi zaidi kwa mapambano ya ana kwa ana. Uvivu umemfanya awe stadi wa mapigo ya kifo, kwa vile asivyopenda kupoteza muda. Hapendi kushughulika na mtu au jambo fulani kwa muda mrefu, kwa vile anavyopenda kupumzika na kustarehe. Hivyo amejifunza kupiga mapigo machache ya kifo. Hataki kumpiga mtu muda mrefu. Namfananisha na wembe upitavyo kwa wepesi kwenye mnofu wa nyama. Huyu atatufaa sana. Inadhaniwa kuwa ndiye mtu makini anayeweza kuua haraka bila silaha.” Ngongoseke akaweka kituo huku akitazama picha ya Poka Kingu kwenye jalada juu ya meza iliyokuwa mbele yake.

“Okay! sikuwahi kuwaza kuwa uvivu unaweza kuwa sifa ya muuaji hatari wa kukabidhiwa kazi hatari kama hii.” Mzungu akaongea kwa shauku huku wasifu wa Poka Kingu ukionekana kumuelea vyema.

“Wauaji wasio makini hawaoni shida kukwambia, watu uliowatuma kuwaua wamewaponyoka kwa bahati mbaya. Japo watakuambia kuwa wamefanikiwa kuwajeruhiwa vibaya. Mbaya zaidi, watakueleza kuwa hawafahamu aliyenusurika kuuawa amekimbilia wapi. Poka Kingu hafanyi makosa ya namna hiyo. To me, when a serial killer have to kill the same target twice in one week, then there's either something wrong with his skills or something wrong with instructions. Nataka akipiga amepiga, tumesahau na tunaongelea habari nyingine.” Alisema Ngongoseke huku akiweka msisitizo kwa lugha ya Kiingereza.

“Okay! Sasa naanza kuafikiana na wewe. Hata hivyo bado nina shaka.”
“Shaka gani?” Ngongoseke akauliza kwa udadisi.

“Poka Kingu yuko kifungoni, tena kwenye gereza la wafungwa hatari, linalolindwa kwa ulinzi mkali, masaa ishirini na nne, siku saba kwa wiki. Bila shaka kumbukumbu zangu ziko sahihi, sivyo?” alihoji Mzungu huyo
“Upo sahihi kabisa. Usijali suala hilo niachie mimi. Unajua huwezi kujua kila kitu kabla ya kuanza kutekeleza jambo lenyewe. Ujuvi wa jambo huja wakati jambo hilo likiwa linaendelea kutendeka. Kukaa na kusubiri ujue kila kitu kabla ya kuanza kutekeleza jambo, ni sawa na kupoteza muda. Tunachotakiwa ni kuwa tayari kwa mambo yasiyojulikana.” Ngongoseke akajitapa na kuongeza.

“Tunachopaswa kufanya sasa ni kutafuta watu wa kufanya nao kazi. Wiki chache zijazo, nitakuwa nimetengeneza timu ya kazi na kuanza fujo ndani ya jiji hili la Dar es Salaam.”

“Hebu niambie juu ya hiyo timu unayotarajia kuitumia.” Mzungumzaji wa upande wa pili, akazidi kuhoji.
“Poka, Naomi, Misanya, Nyoso na Mheshimiwa, wataongoza timu hiyo katika mazingira na nyakati tofauti.” Ngongoseke akabainisha mpango wake.

“Mh! Mbona sioni mchanganyiko mzuri kati ya Poka Kingu na yule mrembo Naomi?” Mzungu akatia shaka kwa mara nyingine.

“Hawa viumbe wawili, ni kama pande mbili za sarafu. Hazifanani lakini zinafanya thamani ya pesa. Ni kama jua linavyotawala mchana, na mbalamwezi unavyoangaza usiku, vyote huangaza dunia. Naomi na Poka wanaunganishwa na hewa iliyopo pande zote, yaani, mchana na usiku. Uwanja wa Poka Kingu ni sehemu ya jua kali na misukosuko. Sehemu yenye upole na mwanga hafifu wa mbalamwezi, yenye hamasa za mahaba, ni ya Naomi Nanalungu. Wote wapo kwenye sayari moja ya matukio ya kutisha, wakiishi kwa kuvuta hewa moja, mchana na usiku.” Ngongoseke akafafanua nadharia yake kwa ujivuni.

“Kwa hivyo Poka unamfananisha na Jua, anafanya kazi mchana kwenye mazingira magumu. Naomi kama mwezi, anafanya kazi usiku kwenye mazingira laini yenye mahaba. Umesema wanaunganishwa na hewa ambayo iko mchana na usiku. Sasa hewa ndiyo nani kwenye nadharia yako?” Mzungu akahoji.

“Hiyo sehemu ya hewa ndiyo mimi. Sionekani lakini nitawaunganisha vyema.” Ngongoseke akaongea kwa utulivu na kuweka kituo. Baada ya ukimya mfupi wa tafakuri, mtu wa upande wa pili akasema.
“Lo! Nimevutiwa sana na mkakati wako. Nadhani mpango wetu utafanikiwa bila shaka.” Kauli hiyo ikafuatiwa na kimya kifupi.

“Nataka Tanzania ichafuliwe, nataka kusiwe na ripoti yoyote kuhusiana na gesi ya Mtwara. Sijui nikueleze vipi ili uelewe namna wakubwa watakavyofurahi, baada ya kufanikiwa kwa tukio hili. Makampuni takribani kumi na tano ya nchi za ulaya na Marekani, yatasaini mkataba wa kuendelea kununua gesi kutoka PAW & Company. Mpango huu ukishindwa, makampuni yote yatakimbilia kwenye gesi ya Mtwara. Ambayo itakuwa rahisi kwao kununua, na upatikanaji wake ni endelevu wa muda mrefu, kutokana na siasa tulivu za Tanzania”

“Hivi sasa kampuni zote zimeshaweka angalizo kuwa hazina hakika kama zitaongeza mkataba wa kununua gesi kwetu. Baada ya kutathimini angalizo lao hilo, tumejiridhisha kuwa zinasubiri hiyo ripoti ambayo inaandaliwa sasa kuhusu gesi ya Mtwara. Ni wazi kuwa tukiharibu utaratibu mzima wa ripoti hiyo katika kiwango ambacho kitaifanya Tanzania itake siyo chini ya mwaka mmoja kuandaa ripoti nyingine. Tutakuwa tumefanikiwa kuyalazimisha makampuni hayo kuendeleza mkataba wa kibiashara baina yetu. Nasi tutawabana walau mkataba mpya uwe wa miaka kumi, ili hata kama Tanzania ikijipanga upya, ikute tumeshatawala soko. Hivyo kazi hii ni muhimu sana kwako na kwetu, bwana Ngongoseke.”

“Ondoa shaka! Japokuwa inaonekana ni kazi ngumu, lakini itafanyika tu. Nikimaliza hii kazi, nitakuja Washington kununua zile nyumba, ulizoniambia habari yake. Nifanyie mpango.” Ngongoseke akaongea kwa hakika, huku akisimama.

“Bila shaka. Kesho nitakutumia picha za nyumba unazoweza kununua, zilizopo maeneo mazuri.” Mzungu akaongea kwa matumaini, upande wa pili wa simu.

“Nitashukuru sana. Basi tutawasiliana wiki ijayo baada ya mambo kuanza.” Ngongoseke akasisitiza.

“Sawa! Natarajia kusikia kasheshe huko. Nimetuma malipo ya awali, malipo ya pili yatafanyika nitakapopata kiboksi cheusi cha kurekodi safari ya ndege. Malipo ya mwisho yatafanyika pale itakapothibitika, kuwa timu yako imefanikiwa kuondoa na kuharibu nakala zote za ripoti ya gesi ya Mtwara.” Mzungu akafafanua.
“Mtathibitishaje kuwa nakala zote zimefutwa?” Ngongoseke akahoji.
“Ni rahisi sana.”

“Kwa vipi?”
“Tanzania itakapoanza upya mchakato wa kupima na kuandika ripoti mpya kuhusu; mchanganuo, aina, ubora na thamani halisi ya gesi ya Mtwara. Jambo ambalo litawachukua takribani mwaka mzima kulifanya. Hapo tutajua kuwa mpango wetu ulifanikiwa na kampuni yetu itakuwa imefanikisha azma yake. . Na ndiyo hapo tutajua kuwa ulifanya vema kazi yako.”
“Nashangaa unatia hofu wakati unajua rekodi yangu ya kazi.”

Njoo tena saa 12:00 jioni.

Like au Comment ili nijue kuna watu wanafuatilia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
-2-

Imetungwa na kuandikwa na Japhet Nyangoro

BAADA YA KUMALIZA MAONGEZI YALE, Ngongoseke akatembea kwa utulivu akizunguka ndani ya chumba alichokuwa akifanyia yale maongezi. Bado alikuwa akitafakari maongezi yaliyopita. Vilevile akitathmini kazi iliyokuwa mbele yake.

Jina lake kamili anaitwa Ngongoseke Amos Nkwija. Akiwa na umri wa miaka arobaini na sita lakini tayari anaogelea katika mafanikio ya hali ya juu ya hapa duniani. Mafanikio ya kifedha na kiuchumi. Kwa wanaomfahamu, mafanikio hayo haikuwa ni jambo la ajabu wala bahati mbaya. Maana angekosaje kuwa na mafanikio wakati Mungu alimtunuku akili njema ambayo alionekana kuitumia vyema. Wakati shetani alimvika ukatili na ujasiri wa kufanya mambo gizani na kuweza kuingia sehemu ambazo haziingiliki kwa urahisi?

Safari yake ya mafanikio ilianza kama utani tu. Alianza kwa kuuza mawazo na mipango, kwa kuwasaidia matajiri kupanga mipango mizuri ya uwekezaji. Akitumia vyema talanta ya akili aliyopewa na Mungu. Haikumchukua muda mrefu kubaini kuwa, siyo kila mtu mwenye pesa ana akili. Isipokuwa wenye pesa ni wale watu wanaojua kutumia akili za wenzao, kuweza kupata pesa na kuongeza pesa. Hivyo Ngongoseke, kwa miaka kadhaa akajikuta kama walivyo vijana wengi ambao hutumia akili zao na taaluma, kuwapa au kuwaongezea pesa watu wengine kwa makubaliano ya kulipwa visenti vichache, mwisho wa mwezi.

Lakini ikatokea siku ile ambayo Ngongoseke akapata ukatili na ujasiri ovu, ndipo mambo yalipobadilika. Alivitumia vipawa vyake vyote, kupora mali za matajiri wachache waliokuwa wakitumia akili yake kujinufaisha. Sasa yeye ndiyo akawa zaidi yao, akiitumia akili yake vyema, ukatili na ujasiri wa kishetani kutengeneza pesa. Kwa muda mfupi Ngongoseke akajikuta ameingia kwenye ramani ya watu wenye utajiri mkubwa wa kuogopwa.

Pamoja na kuwa na watoto watatu, ambao wote wanaishi na kusoma ulaya, lakini hukuwa na mke. Mama wa watoto hao hawakuwepo. Si kwa bahati mbaya wala mapenzi ya Mungu, bali hilo liliamuliwa na Ngongoseke mwenyewe. Mtu mwenye akili ambazo siyo za kufanyia majaribio, akipanga jambo amepanga, yeyote hawezi kosoa. Akipangua amepangua, hakuna wa kupanga. Mtu mwenye akili kubwa yenye shabaha kali, ya kuweza kuunganisha mambo mengi kwa muda mfupi na kuweza kuona matokea tarajiwa kwa uwazi. Akili hizo ndiyo zilizomtuma kumuua kwa siri kila mwanamke aliyezaa naye. Alitaka wanawe wasiwe na mama, wawe wanawe peke yake.

Jumba hili alilokuwa akiishi, lilikuwa kielelezo tosha kuwa alikuwa akiogelea katika utajiri wa kutisha. Ni katika jumba hili la kifahari ndiyo alikuwa akifanya mzungumzo ya simu na mzungu huyo wa upande wa pili. Utajiri wake ulikuwa miongoni mwa watu wanaotafuta namna tofauti za kutumia pesa, wenyewe wanaita kuchoma pesa, hivyo hawabishani bei na hawanunui vitu vya bei nafuu. Jumba lake lilikuwa kwenye kitongoji chenye makazi ya watu wakwasi. Muonekano wa jumba hilo la kifahari ulivuta macho ya wapita njia kwa namna lilivyopendeza. Ukiliangalia unapata tafsiri halisi ya utajiri uliowekezwa kwenye jumba hilo. Bustani kubwa yenye ndege wa rangi tofauti za kupendeza, bwawa kubwa kuogelea, bar ya ndani ya nyumba na sehemu mbalimbali za starehe. Nafsi ya mtu yeyote ingeweza kujihisi burudiko la kifahari kuwepo eneo hilo. Jumba hilo kubwa lililindwa kwa mfumo maalumu wa umeme wa kuzuia wezi au mtu yoyote kuingia na kutoka bila ridhaa ya mwenyeji. Ngongoseke hakuajiri mlinzi isipokuwa kijana mmoja, ambaye kazi yake ilikuwa kuhudumia, bustani ya kupendeza ya jumba hilo.

* * *

USIKU WA SIKU HIYO ambayo Ngongoseke alitoka kuongea kwa simu na yule mzungu wa nje ya nchi, Halfan Mwaruko, askari wa Kituo cha Polisi cha Msimbazi, jijini Dar es Salaam alikuwa akiandika majina ya washukiwa wa uhalifu waliokuwa wamefikishwa kituoni hapo usiku huo.

Ilikuwa saa tatu na robo usiku, washukiwa watatu kati ya sita waliochukuliwa maelezo yao na kuswekwa rumande walikuwa wanawake.
“Nyinyi wanawake sogeeni hapa!” Akafoka kwa sauti ya ukali.
“Taja jina lako.’’ Akaanza na mwanamke wa kwanza kufika.
“Joanita Mwaikambo.” Mwanamke huyo akachukuliwa maelezo kisha akaswekwa mahabusu. Mwingine akafuatia.
“Joan Mwainunu.” Afande Halfan akamtazama mwanamke huyo kwa udadisi, kisha akaanza kumchukua maelezo kama yule wa awali huku akipiga mwayo hafifu. Alipomaliza akachukua maelezo ya mwanamke wa mwisho. Lakini kabla hajaandika, akamtazama msichana huyo kwa mshangao.
“Jina lako?’’ Akauliza huku akimtazama msichana huyo mrembo mwenye mavazi yaliyochafuka, kuashiria kukamatwa kwake kulikuwa mshikemshike.
“Jo…Mwa.”
“Acha mzaha! Ndiyo jina gani hilo?” Afande Halfan akatilia shaka. Akamtazama msichana huyo kwa udadisi. Macho yake hatimaye yakaweka kituo kiunoni kwake kwa sekunde kadhaa, kabla ya kumeza mate na kumwangali usoni.
“Hilo swali labda ungewauliza wazazi wangu.” Msichana huyo akajibu kwa dharau.
“Jo Mwa!’’ Afande Halfan akarudia kutamka jina hilo lililoonesha walakini kichwani mwake.
“Hujakosea.” Akasisitiza msichana huyo kwa sauti ya kilevi.
Afande Halfan akaandika maelezo ya msichana huyo huku akitingisha kichwa, nusu kukubali nusu kukataa. Wakati akiendelea kuandika, mara akaingia mkuu wa kituo hicho cha polisi, katika mavazi yake ya kiafande.
“Sajini! mahabusu yetu imejaa na leo ni ijumaa. Hivyo nimefanya utaratibu baadhi ya hawa mahabusu wapelekwe gereza maalumu hadi jumatatu.” Mkuu wa kituo hicho cha polisi akaweka bayana.
“Ndiyo afande.” Sajini Halfan akaitikia kwa saluti.

* * *

Saa nne asubuhi ya siku iliyofuata, ndani ya gereza maalumu jijini Dar es Salaam, timu ya watu wanne ilikuwa ikifanya kazi yake kwenye gereza hilo.
“Zimebaki dakika kumi tu!’’ Mmoja akafoka.
“Chumba kiko upande gani?’’ Mwingine akauliza.
“Usiniambie kuwa umesahau ramani...?” Mmoja akauliza kwa mashaka. Baada ya ukimya mfupi mwenzake akapendekeza.
“Bila shaka nadhani ni ule mlango wenye rangi nyekundu pale mbele.” Mwingine akasisitiza kwa sauti ya kunong’ona. Walipoufikia mlango huo na kugundua kuwa ulikuwa umefungwa. Kitasa cha mlango huo kilifumuliwa kwa risasi mbili kisha mlango ukasukumwa kwa teke kali. Mlango huo ulipofunguka, watu hao hatari wakajikuta wakitazamana na chumba kidogo sana, mfano wa chumba cha lifti kwenye jengo refu la ghorofa.

Ndani ya chumba hicho alikuwepo mtu mmoja dhaifu sana. Mtu huyo alikuwa amesimama katikati ya chumba hicho. Miguu na mikono yake, imefungwa madhubuti kwa minyororo. Mtu huyo alitia shaka na huruma kama kuku aliyesimama chini ya mti baada ya kunyeshewa sana na mvua.

Ilikuwa wazi kuwa alisimama ghafla, baada ya kusikia hatua za watu hao kuukaribia mlango wa chumba hicho. Vumbi jepesi lililotibuka baada ya watu hao kufanya uvamizi, lilikuwa limesambaa kila mahali humo ndani. Mtu huyo alikuwa akitetemeka kwa vile alivyokuwa dhoofu, dhahiri akionekana mwenye afya dhaifu.

Kilikuwa chumba kidogo ndani ya jengo kubwa, lililozungukwa na ukuta mrefu wenye ulinzi mkali. Ndani ya jengo hilo kulikuwa na wafungwa wachache, ambao kila mmoja alifungwa kwenye chumba chake kama huyu. Lilikuwa gereza moja maalumu la jijini Dar es Salaam.
“Mfungueni haraka tuondoke. Hamsikii kelele za ving’ora?” Kiongozi wa wavamizi hao wa gereza, akawatahadharisha wenzake. Kisha akamtazama mfungwa huyo mbele yake kabla ya kusema.
“Nakuonya! Usilete hila yoyote, vinginevyo risasi yangu moja ya kichwa, itahitimisha uhai wako humu ndani.”
Mtu huyo alikuwa amevaa magwanda meusi, kofia nyeusi ya mfuko yenye matundu mdomoni na machoni, na miwani myeusi yenye vishikio vyekundu. Mtu mwenye umbo kubwa na kovu la kutisha juu ya jicho lake la kushoto. Mara baada ya amri yake. Mvamizi mwenzake, mfupi kwa kimo, mwenye shingo nene na nywele nyingi. Alimsogelea yule mfungwa kwa tahadhari ndani ya hicho chumba.
“Jonas! wewe nenda kawashe gari na kuiweka tayari. Hatuna muda wa kupoteza, tukiingia tu ni kuondoka. Mwambie yule mheshimiwa atangulie, tutamkuta La Grado Casino. Nahofia asijeshindwa kasi ya matukio tukampoteza hapa.” Kiongozi wao akapendekeza. Mtu huyo aliyeitwa Jonas akaondoka bila kutaka ufafanuzi wa ziada, dhahiri akionekana kumwogopa kiongozi wao.
“Weka mikono yako kichwani.” Akasema yule mtu mfupi mwenye shingo nene. Amri yake ilipotekelezwa, akamsogelea yule mfungwa.
“Haya tembea mbele!” Akaamuru tena.
“First…., I need my lunch! Napenda chakula cha hapa. Haraka ya nini jamani? Mwili uliokufa haufi tena.” Yule mfungwa akaongea kwa sauti dhaifu yenye kujiamini.
“Wewe fala! hivi umemsikia vizuri Misanya? Yaani unaokolewa halafu unaleta masharti?” Yule mvamizi mfupi mwenye shingo nene, akafoka kwa hasira na kumchakaza yule mfungwa kwa mapigo manne yaliyokusudiwa tumboni. Hata hivyo akastaajabu kuona hakuna pigo hata moja lililompata. Pamoja na mfungwa huyo kufungwa kwa minyororo, mikononi na miguuni, lakini aliweza kukwepa mapigo yote ya mvamizi huyo mfupi na kujihami kwa kutupa mapigo mawili safi, yenye athari. Mvamizi akajibu mapigo kwa ngumi mbili makini za shingoni, zilizompunguza ukaidi yule mfungwa.

“Pumbavu..!” Mtu mfupi akafoka kwa hasira.

“Usiwe na hasira kijana..” Alisema mfungwa kwa sauti dhaifu. Akayatafuta mate kinywani kabla ya kuendelea

“Wakati wa ujana watu wengi huwa tuna ndoto moja; kwa mfano kutumikia taifa kama walimu, madaktari, wanajeshi na mengineyo. Wengi wetu ndoto hizo hufutika haraka, baada ya kuvutwa na mambo ambayo huja kugundua ni muhimu zaidi kuliko hizo ndoto. Mambo kama vile kuwa na familia, kupata pesa au kuasi tu. Wengine hugundua kuwa siyo rahisi kubadilisha jamii wanazotoka, watu hao hubadilika na huwa kama mimi. Watu ambao huamua kutumia vipawa vyao kwa njia mbaya. Wewe na mimi tuko kwenye kundi moja, maana sioni tofauti ya mimi na wewe kwa kweli. Hivyo twende taratibu tu, usijifanye mtakatifu kwa vile mimi nimesimama hapa wewe umesiamama hapo!’’ Yule mfungwa akaongea kwa sauti thabiti.

“Tofauti yetu ni kuwa, wewe ni mfungwa, mimi niko huru!’’ Akadakia yule mtu mfupi huku akimsogelea tena yule mfungwa.

“Hakuna mtu amewahi kukamatwa kwa mauaji au makosa aliyofanya. Wote waliokamatwa ni kwa sababu walishindwa kupangilia vizuri mauaji ama makosa hayo. Kilichofanywa wafungwe ni kwa sababu ushahidi dhidi yao ulipatikana, yaani walishindwa kupangilia vema makosa yao na kuyaficha baada ya kufanya. Lakini wapo wengi huko nje ambao wanaitwa watakatifu ila kwa sababu tu wanajua kuficha makosa na dhambi zao, amabazo ni kubwa kuliko iliyofanya mimi niwe hapa.” Alisema yule mfungwa kwa sauti ya chini.
“Hebu acha mahubiri wewe, hatuna muda wa mahubiri hapa. Lazima tuondoke hapa haraka. Tunataka kukutoa hapa gerezani uwe huru” Alisema Misanya, ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa wavamizi wa gereza.

“Sawa, najua hamjaja kunisaidia, bali mna shida na mimi. Siku zote ujue kuwa, ukiwa na manufaa makubwa mikononi mwa watu wasiosahihi, wewe si huru tena. Wewe kuwa hapa na mimi hatuna tofauti, nguruwe mchanga wewe! shenzi!.” Yule mfungwa akafoka na kuongeza tena, “Nguruwe wakubwa wakikosa chakula, nguruwe wachanga kama wewe wanaliwa. Huna tofauti na maji ya kutawadhia. Inashangaza maji kama hayo kujinadi kuwa masafi kuliko mkono wa mtawadhaji.” Mfungwa akaongea kwa tabasamu

Kama unafuatilia nione like yako na comment.

Japhet Nyangoro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
- 3 -

“Sawa, najua hamjaja kunisaidia, bali mna shida na mimi. Siku zote ujue kuwa, ukiwa na manufaa makubwa mikononi mwa watu wasiosahihi, wewe si huru tena. Wewe kuwa hapa na mimi hatuna tofauti, nguruwe mchanga wewe! shenzi!.” Yule mfungwa akafoka na kuongeza tena, “Nguruwe wakubwa wakikosa chakula, nguruwe wachanga kama wewe wanaliwa. Huna tofauti na maji ya kutawadhia. Inashangaza maji kama hayo kujinadi kuwa masafi kuliko mkono wa mtawadhaji.” Mfungwa akaongea kwa tabasamu la dhihaka.

“Wewe! hebu mwache huyo, siyo kiwango chako. Mpe hiki chakula kwanza. Ndiyo maana nilikusisitiza tuje na mlo huo. Namjua huyu fala! tabia zake ni za ajabu sana.” Akasisitiza kiongozi wa wavamizi mwenye magwanda meusi, akimwamuru mvamizi mwingine mrefu na mweupe, mwenye nywele nyekundu na sura ya tabasamu.

Sauti ya ving’ora vya magari ya polisi, ikazidi kuhanikiza jirani na eneno lile. Wote wakaingiwa na hofu. Kiongozi wa kundi hilo akaanza kuona shida. Shida ya namna ya kuweka sawa uwiano kati ya mipango na ufinyu wa muda. Aliona muda ulikuwa ukikimbia wakati mipango ilikuwa ikienda taratibu. Alipoitupia macho saa yake ya mkononi, akajikuta akilaani mwenendo wa majira ya saa hiyo.
“Sijui kama waliopanga mipango walizingatia hilo!’’ Akawaza kabla ya kusema.
“Nadhani ni bora tumchukue kwa nguvu kabla polisi hawajafika. Hili gereza ni dogo lakini lina wafungwa muhimu sana. Hivyo najua vitakuja vikosi vya imara.” Mtu mfupi mwenye shingo nene akapendekeza huku akijishikashika usoni baada ya kipigo. Alikuwa amefura kwa hasira. Alitaka kumshushia mfungwa kipigo lakini bosi wake aliwahi kumzuia.
“Bora upambane na jeshi la watu mia kuliko kumlazimisha huyu mpuuzi kuondoka hapa. Haya Poka kula haraka, tunatakiwa kuondoka hapa haraka sana.” Kiongozi wa wavamizi akaongea kwa utulivu huku akitazama upande ambao kulikuwa na lango kuu la kuingilia. Mahali kulipokuwa na miili ya walinzi wa eneo hilo.

“Wewe nawe nenda katusubiri kwenye gari, jiandaeni na kuandaa vifaa endapo kutatokea makabiliano na polisi. Mwambie Naomi atupokee.” Kiongozi akasisitiza.

“Naomi ndiyo nani?’’ Akahoji mtu huyo aliyepewa maelekezo.

“Oooh! Okay! Jo…Mwa.” Akatoa maagizo huku akichomoa bastola yake kisha. akamwangalia yule mfungwa aliyemwita kwa jina la Poka wakati akimalizia kula. Kasi aliyotumia kula ilikuwa wazi kuwa hakuwa mtu wa kawaida. Baada ya kula alifanya kama anajinyoosha, hapo sauti ya mifupa kujiweka sawa ikasikika mwilini, kama vijiti vikavu vilivyokanywagwa na buti za jeshi msituni.

“Twende zetu, Poka kuwa makini. Nadhani sina haja ya kujitambulisha kwako kuwa mimi ni mtu wa namna gani.” Alisema yule jamaa mwenye magwanda.

“Usihofu Luteni Misanya, siwezi kuwa mkorofi kwa mkombozi wangu. Hasa baada ya kunipa chakula kitamu kama hiki.” Kauli ya Poka ikakatishwa na mlio wa risasi. ‘Hakuna namna, Life is too short to spend another moment imprisoned by the will of another’ Poka akawaza wakati akijiweka tayari kwa vitendo.

“Kazi imeiva.” Luteni Misanya akaongea kwa kihoro huku akifikiri hatari iliyokuwa mbele yao.

* * *

“SAJINI HALFAN, HEBU TUELEZE VIZURI. Ina maana siyo wewe uliyeandika hili jina?’’ Inspekta Lucas Mwenda akauliza kwa mshangao.

“Nakumbuka majina ya wasichana wawili yalikuwa yanafanana afande. Mmoja alijitambulisha kwa jina la Joanita Mwaikambo. Mwingine alijitambulisha kuwa anaitwa Joan Mwainunu. Halafu yule wa tatu, akajitambulisha kuwa anaitwa Jo Mwa. Nilimuuliza mara mbilimbili huyu msichana wa tatu, maana siyo kawaida kupata majina ya namna hiyo kwenye makabila ya hapa nchini.” Sajini Halfan akafafanua.

“Ulipomuuliza alisemaje?’’ Inspekta Lucas akadadisi.

“Alisema swali hilo nilitakiwa kuwauliza wazazi wake!’’ Sajini Halfan akafafanua huku akionesha kukereka na maswali hayo. Mahojiano haya yalichukua saa nne.
“Kwa hiyo Sajini unataka kutuhakikishia kuwa, hukuandikisha majina mawili yanayofanana? Maana kwa mujibu wa kitabu cha taarifa za awali pale kituoni, jina la Joan Mwainunu limeandikwa mara mbili na hakuna jina la Jo Mwa, kama unavyotuaminisha!’’ Inspekta Lucas akaonesha dukuduku lake.

“Hapana! Inawezekana kuna kitu hapo. Joan Mwainunu iliandikwa mara moja. Ni ajabu kuwa hakuna jina la Jo Mwa!’’ Sajini Halfan akaonesha mshangao wa dhahiri usoni.

“Hii inaonesha kuwa huyu mwanamke aliyejiita Jo Mwa, ndiye aliyehusika na mpango wa kuvamia gereza maalumu. Hebu nipe hilo daftari nione!’’ Inspekta Lucas Mwenda akanyoosha mkono kupokea daftari kubwa lililokuwa na orodha ya majina ya wahalifu walioswekwa mahabusu ya pale kituo cha polisi cha Msimbazi. Alipopewa daftari hilo, akapitisha macho kwenye kurasa kadhaa kabla ya kuweka kituo kwenye ukurasa fulani. Hapo macho na akili yake, vikajenga shauku.

“Okay! Sasa nimeanza kupata picha. Japo mwandishi alijitahidi sana kuiga hati, lakini hili jina Joan Mwainunu halikuandikwa na mtu mmoja. Wino wa kalamu iliyotumika ni uleule isipokuwa helufi ‘Jo’ na helufi ‘an’ zimeandikwa na watu wawili tofauti. Kama ilivyo kwenye helufi ‘Mwa’ na helufi ‘inunu’. Inaonekana huyu msichana alikuwa akifanya mambo yake kwa mahesabu na umakini sana. Hivyo kutaja jina la Jo Mwa, alikuwa akijipa nafasi ya kubadilisha jina kama ingehitajika. Aliposikia kuwa watu wale wangegawanywa, wengine wangepelekwa Keko na wengine gereza maalumu. Ndiyo akaamua kuwe na Joan Mwainunu wawili, ili wakati majina ya mahabusu yakiitwa, achague kule alikotaka kwenda. Swali ni je! alibadilishaje jina wakati alikuwa mahabusu?’’ Inspekta Lucas, ambaye anasifika kwa umakini wa kuibua hoja, akamaliza uchambuzi wake kwa swali.

“Usiku ule baada ya kumaliza kuandika majina yao na kuwasweka mahabusu, kalamu niliyotumia kuandika sikuiona tena. Afande! Ndiyo maana utagundua kuwa majina yaliyofuatia nilitumia kalamu nyingine. Sasa ndiyo naelewa kuwa huenda yule msichana alichukua kalamu yangu kwa hila ili afanye atakacho. Kwa kweli hata mimi najiuliza swali kama lako afande. Alitokaje nje ya mahabusu na kwenda kaunta kubadilisha jina?’’ Sajini Halfan akaonesha mashaka yake.

“Labda alikuwa na ufunguo wa bandia. Anaonekana mwenye hila nyingi. Ukitathmini juu ya kile kilichofanyika kwenye gereza maalumu, utagundua huyu msichana ni mtu hatari sana.” Askari mmoja akachangia huku wengine wakiafiki kwa kutikisa vichwa.

“Lazima kuna zengwe limefanyika hapa!” Inspekta Lucas akasisitiza.

Tuonane jioni ya saa 12:00

like na comments zinaonyesha kuna watu wanafuatilia.

karibisha watu 10 wajiunge na group.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
- 4 -

“Labda alikuwa na ufunguo wa bandia. Anaonekana mwenye hila nyingi. Ukitathmini juu ya kile kilichofanyika kwenye gereza maalumu, utagundua huyu msichana ni mtu hatari sana.” Askari mmoja akachangia huku wengine wakiafiki kwa kutikisa vichwa.

“Lazima kuna zengwe limefanyika hapa!” Inspekta Lucas akasisitiza.

* * *

Saa moja na robo jioni mitaa ya matajiri jijini Dar es Salaam.
Sabodo Msumari, aliendesha gari kwa mwendo wa taratibu huku akisikiliza muziki mtamu, uliokuwa ukizalishwa na spika zenye nguvu na ubora, za gari lake jipya la kifahari. Huku mluzi mwembamba ukimtoka kinywani kufuatisha muziki huo kwa furaha. Moyoni aliona ulimwengu wote ni wake, mambo yalikuwa yamemnyookea.

Kuwa Waziri wa Ulinzi na usalama kwenye nchi kama hii, halikuwa jambo dogo. Nyota yake ilikuwa imeng’aa sana. Kwa sababu hiyo akajikuta akifikiri zawadi ya kumpelekea mtaalamu wake wa mambo ya nyota kule Bagamoyo. Wakati akisikiliza muziki na mwendo huo wa taratibu, macho yake yalikuwa yakitalii kuangalia nyumba chache kubwa za kifahari zilizokuwa kando ya barabara hiyo eneo ya Masaki. Nyumba hizo zilijengwa kwa nafasi na hivyo kufanya mandhari nzuri ya kupendeza. Sabodo alikuwa anatoka ufukweni, alikokuwa amejipumzisha baada ya kupata dharura. Alikuwa akielekea nyumbani kwa mchepuko wake, umbali mfupi kutoka eneo alilokuwa amejipumzisha ufukweni. Mchupuko ulikuwa umemtaka afike haraka kwa vile hapo nyumbani wezi walikuwa wamevunja na kuiba.

Hivyo alikuwa ameitikia wito wa kwenda kuona athari za wizi aliopewa habari yake. Hakuwa na shida ya muda, kwani wakati huu alikuwa anatumia muda wa ziada, pesa za ziada, mapenzi ya ziada, kwa mtu wa ziada. Walikuwa wote ufukweni lakini kwa sababu ambazo bado hazikumwingia akilini, msichana huyo mchepuko alitaka kurejea nyumbani haraka kwa dharura. Sabodo hakuwa na kizuizi, penzi la binti huyo mrembo lilikwishamlevya, chochote ambacho angeambiwa alikuwa mwepesi kusikiliza na kutii. Alimradi penzi la mrembo huyo lisimponyoke. Hakupenda kumwekea mipaka wala kumchunga, alipenda uhuru kwani tabia hiyo hupendwa na wapenzi wengi. Hivyo alikuwa amemruhusu kimada huyo aende nyumbani kwa dharura kama alivyoomba, kwa maelewano kuwa angerudi ndani ya dakika chache baadaye. Sabodo akabaki ufukweni akibarizi kwa upepo mwanana wa bahari. Hata hivyo starehe hiyo haikudumu sana kwani muda mfupi baadaye, simu ya kimwana huyo aitwaye Nana Muhusin, ilimfanya akatishe alichokuwa akifanya na kumfuata nyumbani.

Aliendelea kuendesha gari, ambalo sasa lilikuwa na muda wa wiki mbili tangu alitoe bandarini kwa usajili wa jina la Nana Muhusin. Hakuwa na nguo nyingine mwilini zaidi ya chupi. Hakuona shida kwa hilo. Ulikuwa muda wa ziada, kufanya mambo ya ziada na mtu wa ziada, sehemu za ziada, kwa pesa ya ziada.

Wakati anakata kona kuingia mtaa ambao kulikuwa na nyumba aliyomjengea Nana, ghafla mambo mawili yakatokea kwa pamoja. Simu yake ya kiganjani ikaita. Wakati akiipokea, mara akasikia sauti ya kishindo cha mpasuko. Alipotanabahi kumbe lilikuwa jiwe kubwa limerushwa kwenye kioo cha mbele cha gari. Kioo kikapasuka. Kwa hamaki akageuka kutazama uelekeo wa jiwe hilo lilipotokea. Wakati huohuo akipokea simu.

“Baby! Mbona hufiki? Nasikia kuna watu wanagonga mlango wangu kwa nje.” Upande wa pili wa simu Nana alilalamika kwa hofu. Sabodo aliisikia sauti hiyo kwa makini lakini mawazo yake yalikinzana na kile alichokuwa akikiona mbele yake. Upande huo liliporushwa lile jiwe, alimwona kijana mmoja amesimama akimwonesha ishara ya kumtusi, kwa kunyoosha kidole cha kati cha mkono wake. Akasikia moyo wake ukisukuma damu kwa kasi na kupiga kite kwa nguvu. Akashikwa na hasira nusu ya kulipuka kwa jazba.

“Shenzi sana wewe kijana! Hivi unajua mimi ni nani?’’ Sabodo akafoka kwa hasira huku akishuka kwenye gari bila kulizima. Mkononi ameshika bastola, aliyoichukua kutoka chini ya kiti cha dereva. Alikuwa kama anayeenda kuogelea, mwilini amejisitiri kwa chupi nyeusi pekee. Akaanza kutimua mbio akielekea upande huo alipokuwa yule kijana. Kuona hivyo, yule kijana akashikwa na taharuki na kuanza kukimbia, akielekea upande ambao kulikuwa na nyumba ambayo haijamalizwa kujengwa. Mheshimiwa Sabodo akiwa amepandwa na hasira, akaendelea kutimua mbio akimfukuza yule kijana. Ilikuwa kama vichekesho, jinsi alivyokimbia huku amevaa chupi tu, na mtikisiko wa kitambi chake.

“Jitokeze uone! Ngedere weh!” Sabodo akafoka baada ya kufika kwenye ingo lisiloisha, alilokimbilia yule kijana. Akaanza kuangaza macho huku na kule, lakini kabla hajajikita kumtafuta yule kijana kwenye ingo hilo. Mara akasikia kishindo kutoka kule alikokuwa ameegesha gari lake. Alipogeuka kutazama hakuamini macho yake. Lori moja la taka, lililovurumishwa kwa kasi, lilifeli breki na kugonga gari lake kwa mbele. Moto mkubwa akalipuka.
“Shiiit…!” Akahamaki kwa kihoro, halafu akiwa katika mshtuko huo akaanza kuhisi kizunguzungu. Akabanwa na pumzi halafu akasikia sauti ya mtu akiongea nyuma yake.
“Jonas! Wewe sogeza gari pale barabarani, mimi na Luteni Misanya, tutambeba huyu fala.” Akasisitiza yule mtu mwenye nywele nyekundu.
“Mpigie Nana, amwambie mzee atukute La Grado Casino, saa nne na nusu usiku huu. Lazima tumalize kazi usiku huu ili kesho tukabidhi na kuondoka hapa jijini.” Luteni Misanya akasisitiza.
“Mzee ana roho ngumu yule!” Jonas akadakia.
“Mzee yupi?” Misanya akauliza kwa udadisi.
“Ngongoseke! Pamoja na lile jeraha la risasi la asubuhi kule gerezani, lakini bado yuko fiti tu!’’ Jonas akaongea kwa mshangao. Kisha akaondoka eneo hilo na kuwaacha wenzake watatu, wakimbeba Sabodo ambaye sasa alikuwa amelala chini hajitambui.

* * *

Fahamu zilipomrejea vizuri Sabodo, tayari ilikuwa imetimu saa tatu na robo usiku.
“Makadirio yangu yalikuwa sawia, tusingeweza kuwahi miadi kule La Grado Casino!” Luteni Misanya akawaza. Alikuwa mtaalamuu na mzoefu wa hali ya juu katika mambo haya. Sabodo Alipofumbua macho, hakupata shida kufahamu kuwa, alikuwa kwenye chumba alichokifahamu vyema. Alikuwa kwenye mojawapo ya vyumba vya nyumba aliyokuwa amempa kimada wake, Nana. Nyumba ambayo alikuwa mbioni kuifikia, kabla ya kukutana misukosuko iliyompelekea kupoteza fahamu. Hakuwa peke yake ndani ya chumba.

Ndani ya nyumba kulikuwa na jumla ya watu wane. Miongoni mwao aliwatambua, Nanalungu na mtu ambaye aliyerusha jiwe kwenye gari alilokuwa akiendesha. Hawa wengine; Luteni Misanya na mtu mfupi mwenye shingo nene, hakuwatambua. Alikuwa amefungwa kwenye kiti cha mbao, kwa namna ambayo watu hao walikuwa, ni kama wanaomsubiri arejewe na fahamu ili wamuhoji. Lakini mshangao mkubwa ulikuwa kwa Nana, ambaye alionekana kuwafahamu vyema wale watu.

“Nana! wewe unaweza kwenda, jamaa yako asije akarudi nyumbani na kukukosa na kuleta shida. Si unajua kuwa hata yeye tunamuhitaji sana! Hii kazi uliyofanya tangu jana, kwenye kituo cha polisi, kule gerezani na sasa kutusaidia kumpata huyu bwege, unastahili pongezi. Endelea kututumia taarifa zozote utakazopata kutoka kwa mumeo.” Luteni Misanya akaongea huku akitabasamu. Nana akatingisha kichwa kuafiki.

“Mkitoka mtanifungia nyumba yangu vizuri, hakikisheni haingii kwenye kumbukumbu zozote za mkasa huu. Hakikisheni mifupa yake mnaipeleka kwenye eneo la ajali, ili uchunguzi ukifanyika, ijulikane kuwa alifia kwenye gari kwa kuungua na moto. Misanya, nitakutumia namba ya nyumba ya Nana mwingine, ambaye ndiye ataonekana kuwa mmiliki wa gari hilo.” Nana akasisitiza wakati akiukaribia mlango wa kutoka nje ya chumba.

“Nana utalipa kwa haya unayofanya. Binti mdogo na mrembo kama wewe, kumbe upo kwenye mambo hatari kama haya. Natamani Inspekta Lucas Mwenda angejua kuwa hana mk, bali jangili tu. Shenzi na mwovu mkubwa weh!’’ Sabodo akafoka kwa hasira, lakini hakuna aliyemjali.

“Wewe na uzee wako hujui ule msemo usemao usione vyaelea ujue vimeundwa? Shenzi mwenyewe na usirudie tena kuniita mwovu! Hasa kwa vile wewe ni mwanaume. Waovu na wema hutoka kwenye tumbo la mwanamke, lakini wengi sana ukiwemo wewe Sabodo, husahau kuwa mwanaume ndiye anayeweka mtoto kwenye tumbo la mwanamke? Leo hii ndiyo unajua kuwa mimi ni malaya, sivyo? Nilivyokuwa nakupa raha hukuliona hilo? Kaa ukijua Lucas na wewe hamna tofauti. Unachomzidi ni pesa tu. Kwa vile yeye ni Inspekta wa kawaida wa jeshi la polisi, anayetegemea mshahara wa mwisho wa mwezi. Wewe na yeye ni walewale tu! Hata yeye nitammaliza hivi karibuni!” Nana akasema kwa dharau huku akichezesha kifua chake kilichokuwa na matiti ya ukubwa wastani.
“Utajutia kwa kitendo hiki. Subiri utaona.” Sabodo akafoka bila matumaini.
“Unajifariji tu kwani wakati huo utakuwa umekufa!’’ Nana akaongea kwa majigambo kisha akatoka kwa kukabamiza mlango nyuma yake.

Asanteni mnao like na ku-comment, maana mnaniwezesha kujua tuko pamoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
- 5 -

Imetungwa na kuandikwa na Japhet Nyang'oro Sudi

“Bwana Sabodo, una machaguo mawili tu. Kufanya kifo chako kiwe cha mateso makali au kije kwa urahisi sana. Naweza kukudunga sindano hii itakayokulaza usingizi wa milele. Au naweza kutumia nyundo hii kupondaponda viungo vyako mwilini hadi utakapokufa. Upi huru kuchagua, kwani kufa utakufa tu, tena leo hii hii. Hebu niambie, kile kikasha cheusi cha kurekodi taarifa ya safari ya ndege iliyoanguka na kuua watu juzi, kiko wapi? Pili, Judith Muga anaishi wapi?”
Kusikia swali, Sabodo macho yakamtoka kwa mshangao. Akiwa na wadhifa wa Waziri wa Ulinzi, mambo haya mawili yalikuwa kipaumbele cha juu katika ofisi yake, ndani ya siku hizi tatu. Hakuamini kuwa jambo aliloliona kama mzaha, sasa lilikuwa linaelekea kuwa hatari namna hiyo, kama ambavyo aliulizwa na huyo mtu. Akashusha pumzi. Kwa mara ya kwanza, akaona jinsi mambo yalivyomuwia magumu. Akajilaumu kwa kutochukua tahadhari ya kutosha.

**** ***** ***

ALITEMBEA taratibu kurudi pale alipokuwa amekaa hapo awali. Alipotaka kukaa ndipo akagundua kuwa kiti chake kilikuwa na damu mbichi. Macho yake yaliyosaidiwa na mwanga wa taa hafifu zilizowashwa ukumbini usiku huo, yaliweza kumtanabahisha kuwa kuna kitu cha tofauti pale kitini. Kwa kutumia ncha ya ufunguo wa gari, akagusa kile kitu na kukinusa puani. Harufu ya damu ikamgutusha. Akaangaza macho huku na kule, kuona kama kuna mtu yeyote aliyekuwa akifuatilia tukio hilo kwa makini. Akajiridhisha kuwa kila mtu alikuwa amezama kwenye starehe zilizokuwa zikiendelea La Grado Casino. Kasino ya watu matajiri na maarufu. Akatoa kitambaa kutoka mfuko wa suruali yake na kufuta damu hiyo, kisha kwa maumivu makali akaketi huku akifinya uso wake. Akiwa ameketi, akaingiza mkono wake wa kulia kwenye koti lake na kupapasa jeraha kubwa na bichi, lililokuwa likiendelea kuvuja damu mgongoni. Taratibu akalitomasa jeraha hilo kama vile muuguzi afanyavyo. Alipotazama majira kwenye saa yake ya mkononi, akagundua ilikwishatimu saa nne na dakika tano usiku. Zilisalia dakika ishirini na tano kabla ya kufika muda ambao Luteni Misanya, alimwahidi kuwa angekuwa pale na kundi lake ili kuleta taarifa ya kazi waliyopata kutoka kwa Sabodo Msumari. Kusubiri kwa muda wa saa moja na nusu, kwake ilikuwa sawa na mwaka. Alikuwa na shauku ya kupata taarifa aliyokuwa akiisubiri, kwani taarifa hiyo ingefanya mipango yake iende sawa kama alivyokuwa amekusudia hapo mwanzoni, wakati akianza kazi hii.
“Oh my God! Shiiit...!’’ Akafoka na kulaani kwa uchungu, pale kidole chake kilipopapasa tundu la risasi mwilini mwake. Akachukua simu yake ili ampigie mtu Fulani, lakini kabla hajatimiza azma yake, simu hiyo ikaanza kuita. Alipoitupia macho akaona jina la Dr. Kuselekwa lilijitokeza kwenye kioo cha simu yake.
“Vipi dokta?’’ Akauliza kwa hamasa. Sauti yake ilijawa na kitetemeshi cha maumivu makali ya jeraha.
“Nipe dakika kumi na tano, nitakuwa nimefika hapo, Bwana Ngongoseke.” Dr. Kuselekwa akasisitiza upande wa pili wa simu, huku sauti ya muungurumo wa injini ya gari lake ukihanikiza.
“Jitahidi kufika mapema, nazidi kupoteza damu kwenye jeraha. Saa sita nina kazi muhimu sana ambayo lazima niifanye. Haijalishi kama risasi hii mwilini itakuwa imetolewa au la!” Ngongoseke akasisitiza kwa sauti ya amri.
“Ondoa shaka. Kazi yangu unaifahamu vyema!” Dr. Kuselekwa akasisitiza upande wa pili wa simu.
“Halafu…’’ Ngongoseke akawa kama aliyekumbuka kitu.
“Sema mzee! Nakusikiliza.”
“Kama kawaida! Siri ndiyo ajenda kubwa hapa. Sawa…?’’
“Huna haja ya kunikumbusha hilo mzee. Mimi na wewe hatujaanza leo. Ili kuhakikisha hilo, ndiyo maana hata gari nimeamua kuendesha mwenyewe.’’ Dr. Kuselekwa akasisitiza.

Baada ya simu hiyo, Ngongoseke akaendelea kunywa taratibu huku akiyaacha macho yake yakistarehe kwa warembo waliokuwa wakijipitisha eneo hilo. Lengo lao likiwa; watamaniwe, waitwe, wasemeshwe, wasifiwe na hatimaye wapate pesa, ambazo wao waliziita malipo baada ya kuwaburudisha watu wa namna hiyo. Watu matajiri ambao akili yao haina raha, japo wanaishi sehemu zenye raha. Wanatumia vitu vyenye raha na kufanya vitu vyenye raha nyingi. Watu ambao wanajua kutumia pesa ili kupata pesa. Watu ambao hujua kuona fursa, watu ambao jamii ya kawaida huwaogopa na kuwaita matajiri. Watu ambao ni pale tu wanapomaliza shughuli ndipo hukumbuka kuwa wanahitaji kuburudishwa. Watu hao hupendelea kufika sehemu kama hizi na kukaa kwa saa nyingi. Wakiburudika kwa fahari ya macho, halafu dakika za mwisho hununua na kwenda kutumia. Japokuwa siyo watumiaji wazuri. Mfumo wa maisha yao umewafanya wasiwe watumiaji wazuri wa starehe hiyo. Kwa vile ni watafutaji wazuri wa pesa, vilevile ni wepesi wa matumizi na kuhonga. Tabia hiyo ndiyo huwavuta warembo, katika kucheza vyema turufu zao za kutafuta pesa.

Tofauti na siku nyingine, leo Ngongoseke alionekana mtu mwenye mawazo sana.
“Naona tajiri wetu leo hayuko poa!’’ Dada mmoja akimnong’oneza mwenzake.
“Kweli shoga, hata mimi nimemuona. Tangu ameingia naona ana chupa moja tu ya Whisky. Hajachangamka kabisa.’’ Mwenzake akachangia.

Saa nne na nusu ilipogonga, Ngongoseke akainua macho yake na kuyatembeza humo ukimbini. Akashangaa kuona kwenye meza yake kuliongezeka watu wengine wanne. Akashangaa kwamba hakuweza kusikia wala kuhisi, wakati watu hao walipofika na kuketi kwenye meza yake.

“Pole sana mzee, inaonekana jeraha limekuletea shida sana.” Luteni Misanya akaongea kwa utulivu.
“Acha tu, sina namna! Mtaka cha uvunguni sharti ainame!” Ngongoseke akaweka kituo, kabla ya kuendelea.
“Even in hell, there are rules. Haya hebu leta habari.”
“Tumemhoji Sabodo, amesema kisanduku cheusi kipo sehemu fulani inaitwa safe house. Ingawa yeye ni Waziri wa Ulinzi lakini hajui hiyo safe house iko wapi. Kuna watu wanne tu hapa nchini, wanaofahamu mahali ilipo hiyo safe house. Watu hao ni; Rais, Waziri Mkuu, Mkuu wa Majeshi na Mama mmoja anaitwa Bi. Anita. Ambaye ni mkuu wa kitengo cha kijasusi kiitwacho, Ofisi Fukuzi” Luteni Misanya akaongea kwa umakini.
“Good! Suala hilo niachieni mimi. Vipi kuhusu Judith Muga?” Ngongoseke akauliza huku akipisha tafakuri.
“Judith Muga amepanga nyumba namba 0713C, eneo la Masaki, Mtaa wa Chakechake.” Luteni Misanya akaongea kwa tabasamu hafifu. Kazi aliyopewa alikuwa ameikamilisha.
“Vizuri sana Luteni. Siku zote huwa nakwambia huko jeshini unapoteza muda! Wewe ulifaa ufanye kazi za kujitegemea tu. Usiku huu utakuwa na kazi gani ya kufanya? Ngongoseke akauliza kwa furaha.
“Nitakwenda kwa msichana mmoja huko Mbagala, kwa ajili ya kupandikiza zile karatasi za umiliki wa gari, iliyokuwa ikiendeshwa na Sabodo.” Luteni Misanya akaongea kwa majigambo.
“Kupandikiza…! Kivipi? Ngongoseke akahoji.
“Gari iliyokuwa ikitumiwa na Sabodo, ilikuwa imesajiriwa kwa jina la Naomi Nanalungu. Sasa kuna msichana mmoja kule Mbagala mwenye jina kama hilo. Nitaweka nyaraka za lile gari ndani ya nyumba ya huyo msichana na mambo yatakuwa sawa. Nana wetu atakuwa salama. Baada ya hapo nitarudi nyumbani kupumzika.” Luteni Misanya akaongea kwa utulivu.
“Badala ya kwenda kupumzika, nataka Judith Muga achukuliwe usiku huu. Yeye, kompyuta yake na makabrasha yake yote. Ni wazi kuwa, baada ya ile ndege kuanguka, ni yeye pekee ndiyo mwenye ule mkataba. Huko kwengine kote tumeshaondoa kumbukumbu. Kilichobaki ni kushughulika na yeye. Tukifanikiwa na malengo yetu yatakuwa yametimia.” Ngongoseke akaongea kwa hakika. Luteni Misanya akaitikia kuafiki. Kisha wakasimama na tayari kwa kuondoka.
“Vipi kuhusu hilo jeraha?’’ Luteni Misanya akauliza.
“Tangu lini ukanihurumia?’’ Ngongoseke akauliza kwa mshangao.
“Sijawahi kukuona katika hali hiyo. Wewe ni mtu wa vita ya akili na mipango. Haya mambo ya vita ya risasi na mapambano ya kutumia nguvu, hujayazoea. Haikuwa busara kulazimisha kuja kule gerezani, wakati tukimchukua Poka. Unajua ukidhurika na mpango mzima ndiyo umekufa?’’ Luteni Misanya akaongea huku akiwaonesha ishara vijana wake watangulie kutoka.
“Okay! Dr. Kuselekwa atakuwa hapa, ndani ya dakika tano zijazo. Bila shaka amewasaidia kumhoji Sabodo baada ya presha yake kupanda.’’ Ngongoseke akaongea kwa utulivu.
“Ametusaidia sana. Yule mtu anaifahamu vyema kazi yake.’’ Luteni Misanya akasisitiza.
“Kesho asubuhi nenda kafuatilie taarifa za akaunti yako benki. Utakuta tayari nimefanya mambo. Ukishamchukua Judith, mweke sehemu salama hadi nitakapokupa maagizo mengine.” Ngongoseke akapendekeza. Alitaka kusema kitu lakini akasita. Badala yake akainua kichwa kutazama huku na kule, kisha akainama. Luteni Misanya, naye akainama kusikiliza.
“Hawa vijana wako waliofanya kazi leo, wameshajua mambo mengi sana. Hawafai kuishi.”
“Unashauri vipi?”
“Kuna namna nzuri ya kuwaua. Nitakupigia kukupa maagizo ya namna ya kufanya. Nataka kifo chao kiwe cha kimyakimya.” Ngongoseke akapendekeza kwa sauti ya chini.
“Count it done, mzee. Lakini hujaniambia kuwa unataka kufanya nini na Poka Kingu?” Luteni Misanya akauliza huku akiondoka. Ngongoseke akapisha tabasamu la kifidhuli lenye uchungu ndani yake bila kutia neno. Ilikuwa ishara tosha kuwa, hakuwa tayari kuongelea mpango wake juu ya Poka Kingu.
Luteni Misanya alipofika mlangoni, akapishana na Dr. Kuselekwa aliyeingia kwa mwendo wa haraka. Nusura wakumbane kwa bahati mbaya. Walipotazamana, tabasamu jepesi likachomoza kwenye nyuso zao. Dr. Kuselekwa akaongeza mwendo kuelekea upande ambao Ngongoseke alikuwa amek

* * *

Wiki mbili baadaye...

WATU WAWILI walikuwa ndani ya nyumba moja, kati ya nyumba nyingi zinazotazamana na Slipway Hotel. Katika mtaa wa Ngomgoro, eneo la Msasani, jijini Dar es Salaam. Mawimbi ya bahari yalikuwa yakisikika kwa mbali, kutoka kwenye sebule waliyoketi. Sura zao na namna walivyoketi, ilikuwa dhahiri walikuwa kwenye mazungumzo magumu. Mmoja alikuwa mwanamke wa umri wa makamo. Mwingine alikuwa mwanaume wa kati ya miaka thelathini na nane na arobaini na mbili. Mwanamke alionekana mwenye siha njema na kipato cha kueleweka. Kwa namna ya mwonekano wake, vito vya thamani alivyovaa shingoni na masikioni, pamoja na mavazi yake ghali mwilini. Alikuwa amevaa suti nyeusi ya suruali na miwani nzuri ya kupendeza, iliyoyapelekea macho yake makali kuona vyema. Masikioni alitoga herini ndogo za almasi mfano wa punje ndogo za mchele. Kucha zake ziliwaka kwa rangi nyekundu ya kuvutia, miguuni alivaa viatu vyenye visigino virefu. Hakuwa mnene wala mwembamba. Kifua chake kilibeba matiti yenye ukubwa wa wastani na hivyo kusanifu vyema mwonekano wake. Huyo mwanamke aliitwa Bi. Anita, mkuu wa kitengo cha siri kinachoshughulika na masuala ya upelelezi na ujasusi. Kitengo hicho maalum ambacho hufanya kazi chini ya Rais, huitwa Ofisi Fukuzi.

Mwanaume aliyekuwa akizungumza naye humo ofisini, aliitwa Jacob Matata. Miongoni mwa wapelelezi mahiri wa kuaminiwa, katika idara hiyo ya kijasusi – Ofisi Fukuzi.
“Hadi sasa sielewi tatizo liko wapi?" Mpelelezi Jacob Matata akasema kwa mashaka.

Tuko pamoja? Asante kwa like na comment yako.

Tuendelee kesho

Nzuri mkuu. Thanks.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
- 6 -

“Labda ngoja nikupe picha halisi ya jambo hili, ndiyo utaelewa mambo yalivyo.” Bi. Anita akadokeza.

“Nitashukuru sana, kwani bado nashindwa kuunganisha matukio.” Jacob Matata akapiga mwayo hafifu akijipa utulivu kichwani, tayari kusikiliza.

“Nyerere katika awamu ya mwisho ya utawala wake, alipata taarifa za za siri. Taarifa hizo zilibainisha kuwa, kulikuwa na uwezekano mkubwa wa Tanzania kuwa na hazina kubwa ya nishati ya gesi, huko pwani ya Mtwara. Zilikuwa habari za kutia hamasa kwa nchi hii masikini. Hususan kwa kiongozi ambaye alikuwa akipambana sana kutafuta vyanzo vipya vya pato la taifa, vitakavyoinua uchumi na hali duni za maisha ya raia wake.” Bi. Anita akaweka kituo kumeza mate, kisha akaendelea.

“Kwa jinsi Nyerere alivyokuwa kiongozi makini, haraka akaanza kuzifanyia kazi taarifa hizo. Uchunguzi ukafanyika na majibu yakapatikana. Hata hivyo, hakuwa tayari kupitisha mchakato wa kupima na kuanza kuchimba gesi hiyo.”

“Kwa sababu gani?” Jacob Matata akauliza kwa udadisi.
“Kwa sababu alijua kuwa ingechukua miaka mingi hadi utafiti juu ya gesi hiyo na uchimbaji wake kuanza.” Bi. Anita akaweka kituo na kuendelea. “Kwa vile nchi yetu ilivyokuwa masikini na nyuma kwa teknolojia. Katikati ya ulimwengu wenye ushindani na fitina nyingi. Hakutaka kukimbilia haraka suala hilo kama nafuu ya haraka ya uchumi wa nchi.”

“Ilikuwaje?” Jacob Matata akajenga shauku.

“Aliamua kwenda kwa hekima na mahesabu makali. Aliwaendea washirika wake muhimu wa wakati huo. Ambao ni China na Urusi, kuwaomba ushauri wa kitaalamu. Baada ya mashauriano, mwafaka ukapatikana.”

“Mwafaka upi?”

“Kabla ya uchimbaji wa gesi hiyo, ilishauriwa nchi yetu iwe kwanza na wataalamuu wake. Hivyo wakachaguliwa watanzania kumi na wawili wenye akili safi. Watu hao wakapelekwa nchini Urusi kusomea utaalamuu wa mambo ya gesi asilia. Kwa kuzingatia ushauri wa kijasusi na msaada mkubwa aliokuwa amepewa na rafiki zake hao wawili; China na Urusi. Kati ya watanzania hao, ilionekana wawili walipaswa kufanya mafunzo ya ziada. Hivyo watu hao wakaingizwa katika mpango wa mafunzo ya juu ya ujasusi.” Bi. Anita akaweka kituo.

“Kwanini ilionekana ni muhimu kuwapa watu hao wawili tu, mafunzo hayo hatari ya kijasusi?’’ Jacob Matata akauliza kwa udadisi.

“Kumbuka kuwa wakati huo dunia ilikuwa imegawanyika katika makundi mawili. Kundi la kwanza, lilifuata mrengo wa sera za nchi za magharibi, zilizokuwa zikiamini katika nadharia ya Ubepari. Kindi la pili, lilifuata mrengo wa sera za nchi za mashariki, zilizokuwa zikiamini katika nadharia ya Ujamaa. Kinara wa kundi la magharibi alikuwa ni nchi ya Marekani na uingereza. Wakati kinara wa kundi la mashariki ilikuwa ni nchi ya China na Urusi. Nyerere aliamini kwenye sera za kundi la mashariki. Huko ndiyo alipoibuka na sera yake ya Ujamaa na Kujitegemea.” Bi. Anita akaweka kituo akifikiri kabla ya kuendelea.

“Endelea, nakusikiliza vyema!” Jacob Matata akaendelea kutega sikio kwa makini.

“Kitu kimoja kilikuwa wazi. Kitu hicho ni kwamba, nishati nyingi na malighafi, vilikuwa kwenye nchi za mashariki. Hivyo nchi nyingi za Magharibi zikajikuta kwenye mkakati mzito wa kuhakikisha kuwa, zinatafuta namna yoyote ya kujenga mahusiano na nchi za kijamaa. Baada ya kufanikiwa kwa mpango huo, nchi hizo za kibepari ziliazimia kufyonza rasilimali za nchi za kijama na kuzisilimisha kwenye sera zao za kibepari. Hivyo ilitakiwa viongozi wa nchi za kijamaa waje na Plan B, au mpango mbadala wa kukabiliana na hila za nchi za magharibi. Ili ikitokea kuwa, mfumo wa dunia ukawalazimisha bila kupenda, kukubaliana na sera za uchumi wa magharibi, yaani Capitalist economy. Wawe na namna ya kuweza kwendana na sera hizo bila kutetereka.” Bi. Anita akaweka kituo kufikiri. Jacob Matata alikuwa amejenga umakini sana kufuatilia maelezo hayo. Bi. Anita akaendelea.

"Kwa vile Nyerere alikuwa rafiki wa karibu wa Rais wa China na Urusi wa wakati huo, akabahatika kuingia kwenye maandalizi ya mpango mbadala wa makabiliano hayo. Ili kama sera ya ujamaa ikishindwa, basi kuwe na uwezekano wa kuendana na sera za Ubepari. Hivyo China, Urusi na mataifa mengine ya kijamaa, yakawa yanawaandaa watu wao watakaoingia kwenye umoja wa mataifa. Watu hao walipaswa kuwa wenye taaluma kubwa za masuala mbalimbali, lakini ilikuwa ni lazima wawe na uwezo mkubwa wa kufanya ujasusi. Kwa namna nyingine naweza kusema walikuwa wanapandikiza majasusi ndani ya umoja wa mataifa.”

“Duh! Sasa ikawaje?”

“Wasiwasi wa Nyerere juu ya hatma ya gesi ya Mtwara, ulipewa uzito mkubwa na nchi marafiki. Hivyo wakati wa kupandikiza watu kwenye Umoja wa Mataifa, wale watanzania wawili waliopewa mafunzo ya ziada, walipewa nafasi ya kuingia kwenye kamati ya kudumu ya Umoja wa Mataifa, inayoshughulikia mambo ya nishati. Lakini kumbuka kuwa nchi masikini hazina uwezo wa kuwa na uwakilishi mkubwa na wa kudumu kwenye kamati hizo. Japokuwa nchi nyingi masikini ndiyo zenye rasilimali nyingi duniani."

"Ili kuwawezesha watanzania hao kuingia kwenye kamati ya kudumu ya Umoja wa Mataifa, mpango kamambe uliandaliwa. Wale watanzania wawili wakapewa uraia wa Urusi. Hilo lilifanikiwa. Si unajua tena, japokuwa kamati hizo husemwa kuwa ni za Umoja wa Mataifa, lakini nyuma ya pazia maamuzi na tafsiri ya mambo hufanywa kwa kutegemea nani anaegemea wapi.” Bi. Anita akafafanua."

“Sasa kulikuwa na ulazima gani kwa hao watanzania kupata mafunzo ya kijasusi na mbinu za mapigano?” Jacob Matata akahoji.

“Kama unavyojua, sehemu kubwa ya dunia inaendeshwa kwa uamuzi, ambao chimbuko lake ni taarifa za kijasusi. Upatikanaji wa taarifa za kijasusi siyo jambo rahisi, kwa vile taarifa hizo hupatikana kwenye vyanzo vinavyolindwa sana."

"Hivyo isingekuwa sahihi kuwachukua watu muhimu ambao taarifa zao zinategemewa, halafu uwaweke na majasusi wenye uwezo mkubwa wa mapigano. Vinginevyo ni sawa na kuwachanganya kondoo na mbwa mwitu kwenye zizi moja. Hivyo ili kutafuta usawa kwenye kamati hizo, ilibidi kuwaandaa watu wetu kwa namna hiyo. Nadhani sasa umenielewa?”

“Naam! Nimekupata vyema.” Jacob Matata akaitikia huku akitikisa kichwa kuafiki.

“Baada ya miaka kadhaa, hofu ya viongozi wa kijamaa ilikuja kuthibitika kuwa kweli. Baada ya miaka kadhaa, nchi nyingi za kijamaa, ilibidi zifungue mlango kwa mfumo wa uchumi wa kibepari. Ndiyo maana sasa hivi unaona nchi nyingi duniani zinafuata uchumi wa kibepari. Lakini maandalizi yalishafanyika miaka mingi iliyopita.” Bi. Anita akaweka kituo na kushusha pumzi ndefu akifikiri. Baada ya kitambo kifupi cha ukimya wa tafakuri akaendelea.

“Sasa turudi kwenye kisa chetu, kilichokupelekea uniite hapa siku ya leo. Hayo uliyosema yanauhusiano gani na wito wangu?’’ Jacob akauliza huku akipiga mkupuo mkubwa wa sharubati iliyokuwa kwenye bilauri.

Hii ni sehemu ya SITA ya riwaya iitwayo MSAKO ambayo Imetungwa na kuandika na Japhet Nyang'oro

Bila shaka umeshasoma sehemu ya 1 hadi ya 5

Jioni ya saa 12:30 nitakuwekea sehemu ya 7 Hapahapa

Tokelezea basi mzee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom