mtzmweusi
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 8,700
- 9,070
- Thread starter
- #161
- 19 -
Riwaya: MSAKO
Mtunzi: Japhet Nyang’oro
Saa tisa na robo alasiri, wakati Jacob Matata anakata shauri kuanzia Upanga NHC nyumba namba 41A, Poka Kingu na yeye alikuwa kwenye hesabu zake.
“Wapelelezi ni kama Inzi tu, wanapoona kinyesi hawaachi kuzungukia hapo. Nina hakika atarudi tena kwa Nana, hivyo watatu mtakwenda nyumbani kwa marehemu Lucas Mwenda kumngoja Jacob Matata. Nina hakika baada ya kuona kile kifaa tulichomwachia Nanalungu kwa vyovyote atataka kwenda ili asubiri yeyote atakeyekwenda akabiliane nae na kuweza kutufikia. Hakuna anayeweza kukabiliana na Jacob Matata hapa kati yenu, hivyo mtakachofanya mkimuona tu ni kumfuatilia kila anapokwenda na kunipa taarifa. Nataka kujua ameweka kambi wapi. Maana sasa anatafutwa sana na vyombo vya usalama hivyo najua kuna sehemu amejizika ili isijulikane alipo.” Poka Kingu alisema kwa vijana wake ambao alikuwa amewakusanya wamsaidie kufanya kazi ya kukusanya taarifa na kufuatilia watu huku yeye akiwa amejiwekea kazi ya kung’oa visiki.
Wakati Poka Kingu akiwa anatoa maelezo hayo, Luteni Frank Misanya na Nanalungu Bin Muhusin walikuwa wanaanza maongezi yao kwa njia ya simu.
“Naona mambo yanatunyookea!’’ Nana alisema.
“Haswa, wale vijana tuliokuwa nao siku ile tunamhoji Sabodo Sumari wote wameuawa leo!’’ Frank alisema.
“Oooh! maskini, wanaoneka walikuwa vijana wakakamvu sana. Imekuwaje, vifo vyao ni sehemu ya mkakati au janga limewafika?’’ Nana alihoji.
“Sehemu ya mkakati, Mzee aliwakabidhi kwa Jacob Matata, Jamaa kawaswaga wote!’’ Frank alisema kwa sauti baridi.
“Miye nilijua Jacob kawekewa watu makini baada ya kuwataarifu kufika pale msibani. Nilifanikiwa kumfanya ajue kuwa niko upande wake. Halafu niliona jinsi alivyonitamani. Jacob mgonjwa wa wanawake aisee, yaani katika mazingira kama yale ya msiba bado akawa ananimezea mate! Ila ni bonge la mkaka, bsi tu! Sasa mkakati hapo ni upi?’’ Nanalungu ambaye ni mke wa Inspekta Mwenda alisema.
“Ni sehemu ya kukulinda wewe Nana. Tungekosea Jacob angewahi kujua kuwa wewe ulitupa taarifa zake. Ila kwa hivi tulivyofanya Jacob Matata ataendelea kukuamini. Lakini nahisi kama Mzee hatuamini kuwa tunaweza kukabiliana na Jacob au kuna namna anataka asife sasa.” Frank Misanya alisema.
“Halafu nina ujumbe wako toka kwa mzee” Frank Misanya alisema
“Nini tena, niko msibani jamani au hamjui? Nana alisema kwa mshituko.
“Anasema umeshamaliza kazi ngumu, baada ya kuwaua Inspekta Menda na Sabodo unatakiwa upumzike. Hivyo kasema nenda kajichimbie kule Masaki kwenye nyumba uliyojengewa na Sabodo Sumari, hadi hapo utakapopewa maelekezo mengine.” Misanya aliongeza.
********
ILIPOFIKA saa kumi kasoro dakika kumi na tano alasiri wakati ambao msako dhidi yake ulikuwa umepamba moto, Jacob Matata aliingia mtaani nia yake sasa ikiwa ni kwenda Upanga NHC nyumba namba 41A. Hatimaye alifika Mzumbe University Cumpas ya Dar es salaam, akiwa katika mavazi yenye utata, ambayo si rahisi mtu kumtambua. Kwa vile alijua kuwa alikuwa anatafutwa, aliamua kubadili sana uvaaji na mwoneka wake. Kufanya isiwe rahisi kujulikana hadi atakapofikia hatma ya kisa hiki. Japo hakuwa na hakika ya kumaliza akiwa hai au la.
Alitembea taratibu, ungedhani anaelekea Regent. Lakini akaiacha hiyo barabara na kuchukua ile ya vumbi. Hapo alitembea taratiibu, hadi kwa mbali aliweza kuiona ile nyumba na 41A ya shirika la nyumba.
Alipapasa bastola yake kiunoni, huku akiendelea kutembea taratibu hadi alipokuwa amesimama kwenye mlango wa kuingilia ndani upande wa uani. Eneo la nje lilimwashiria wazi kuwa hakukuwa na mtu aliyekuwa akiishi eneo hilo. Hata hivyo sheria mojawapo ya upelelezi ni kutokuamua mambo kwa kudhani. Mara nyingi ukionacho ni tofauti na uhalisia wake, usione ukadhani.
Hivyo dakika chache baadae alikuwa ameshaingia ndani, alizunguka maeneo yote bila kuona dalili yoyote ya kuwa na mtu anaishi ndani. Alikagua sehemu ya chini kabla ya kupanda ngazi kwenda upande wa juu, maana nyumba hiyo ilikuwa na ghorofa moja. Alipanda kwa hadhari kubwa. Alifika kwenye kibaraza cha sehemu ya juu. Alianza kuangalia chumba kimoja baada ya kingine hadi alipofungua malango wa chumba cha tatu taratibu huku mapigo yake ya moyo yakienda kasi. Bastola ikiwa imara mkono wake wa kulia. Taratibu aliingia ndani. Chumba kilikuwa ukiwa huku kukiwa na mifupa ya mtu iliyokuwa imelala chini. Inaonyesha mtu huyo alikufa siku nyingi, akaoza na sasa mifupa ikawa pale chini kama mti. Jacob Matata alishangaa sana.
Kama mtu alikufa, akaoza, mwili ukaliwa na wadudu hadi sasa amebakia mifupa inamaana hakuna mpangaji mwingine kwenye ile nyumba kwa muda mrefu sana?
Ina maana hata majirani hawakutambua kuwa jirani yao alitoweka?
Ina maana majirani hao hawakusikia hata harufu ya ule mwili?
Kama hakuna mpangaji shirika limechukua hatua gani?
Kama kuna mpangaji, huyo mpangaji ni nani?
Maswali yote hayakuwa na majibu.
Tofauti na alivyopanga, saa kumi na robo jioni, Jacob Matata alikuwa amesimama nyuma ya mlango wa Afisa Mahusiano ya wateja wa Shirika la Nyumba Makao Makuu.
Alikaribishwa na mama mmoja wa makamo. Baada ya kujitambulisha mahojiano yalianza.
"Kama nilivyokutaarifu kwenye simu, kazi yangu imenifikisha nyumba namba 41A. Ningependa kujua nini unajua kuhusiana na nyumba hii hasa ukizingatia kuwa ni mali yenu. Nani mpangaji wake kwa sasa?’’ Jacob Alisema huku macho yake yakiwa katikati ya uso wa huyo mama. "
Asante, mara baada ya kunipigia nimeitisha faili linalohusiana na hiyo nyumba. Nyumba hiyo ina mpangaji wa muda mrefu sana." Aliongea yule mama huku akiwa anapekuapekua lile faili.
"Okay, je, ni nani huyo mpangaji wa muda mrefu?’’ Jacob Alihoji.
"Si utamaduni wetu kutaja majina ya wateja wetu kwa mamlaka zisizo rasmi......" Yule Afisa alisema na kukatishwa na Jacob.
"Kujua siri ndiyo kazi yangu, hivyo usijali hapa ndiyo nyumbani kwake na Mr. Siri." Jacob alisema.
“Hiyo haitowezekana kaka yangu.” Mama aliweka ngumu. “Sawa mama, nakutakia kazi njema.” Jacob Matata alisimama na kuondoka.