GISENYI--VII
Mpinda alipofika kwenye nyumba
aliyokuwa amefikia, aliteremka haraka
kutoka ndani ya gari na kuingia ndani ya
nyumba hii, akawagongea wenzake
waliokuwa ndani ya vyumba, akiwataka
kwenye mkutano pale sebuleni.
Alifikiria na kuona kwamba Mwenyezi
Mungu alikuwa ameyajibu maombi yake.
Hii ilikuwa nafasi aliyoisubiri kwa muda
mrefu sana. Na yeye vilevile kama
wenzake wa Rwanda aliona nafasi hii
ilikuwa inazifaa pande zote tatu
zilizokuwa zinahusika kwenye harakati
hizi za mapambano. Kati ya wote
waliokuwa katika sakata hilo, alijiona
ndiye mwenye fursa ya kufaidika zaidi
ingawaje Serikali ya Rwanda ndio
ingefaidika zaidi kwa kuhakikisha kuwa
haina mgogoro au wasiwasi wa
kushambuliwa na Wahutu wenye
msimamo mkali chini ya wanamgambo
wa Intarahamwe na Banyamulenge
ambao nao wangefaidika kwa
kutobuguziwa tena na Serikali ya Zaire,
na wangeendelea na maisha yao raha
mstarehe.
Makamanda hawa walipokusanyika pale
sebuleni Mpinda aliwaeleza kila kitu jinsi
mambo yalivyokuwa wamejipa.
"Tunachotakiwa kufanya ni kukishawishi
na kukikahakikishia kikao cha Serikali ya
Rwanda na viongozi wa Banyamulenge
kuwa tutakapoanzisha vita hii ni kweli
uwezo wa kushinda tunao?. Pande zote
zimekubali kuwa sababu tunayo na nia
tunayo, swala hapa ni uwezo, wakiridhika
kuwa uwezo upo, basi mambo tayari",
Mpanda aliwaeleza wenzake.
"Mkuu, wala tusipoteze muda wa kufikiri,
sisi tumekuwa hapa tukijaribu
kuwashawishi siku zote, tusingekuwa na
uhakika na uwezo wetu kivita tusingekuja
kuomba watuunge mkono, uwezo tunao.
Nenda kawaeleze kwa uhakika kama
watatoa msaada kidogo tu, basi nchi yetu
tumeikomboa kutoka kwenye mikono ya
utawala wa Kidikteta na kifashisti", Col.
Mkengeri, mmoja wa makamanda wa
wapinzani wa serikali ya Zaire alijibu.
Wenzake wote walitingisha vichwa
kukubali maneno yake.
"Azimio, tunakwenda wote kushiriki kikao
hicho", Mpinda alijibu.
ITAENDELEA