Riwaya: UCHU

Riwaya: UCHU

Asante kwa kipande hicho I hope kitakushawishi kuendeleza mapema zaidi.
 
duh hii riwaya imetutesa na itatutesa sana. im very sad kidi kudi
 
Pamoja sana kidikudi tutafika shaka ondoa riwaya ndo ulevi wetu.
 
Hahahahaaaa watafrahi Kwa Gamba kazi wanayo
 
only one week left to count a month since the first post by kidi kudi on 11th Jan 2015.
 
only one week left to count a month since the first post by kidi kudi on 11th Jan 2015.

Mkuu hii story hii nadhani waandaaji wake wanajua ni nzuri na wengi tumeipenda, hivyo wanaamua kutuburuza.

ushauri wangu tuvumilie wamalize baada ya hapo kila mtu kwa nafasi yake anaanza upya ili kuipata kwa ukamilifu wake.

bado nina imani na waandaaji wanaotuletea.
 
UCHU
GISENYI
VIII
Willy Gamba na Bibiane walisafiri salama
kutoka Kigali mpaka Gisenyi bila kukutana
na kituko cha aina yoyote Barabarani. Lile
gari lenye alama ya Msalaba Mwekundu
liliwafanya wasafiri bila kupata usumbufu
na habari zilikuwa zimetumwa mapema
na wale askari watatu waliotumwa
kutangulia mbeke ili lile gari la maofisa
wa Msalaba Mwekundu lisibugudhiwe.
Walipofika Ruhengeri walipumzika huku
kila mmoja wao akili yake ikifanya kazi
jinsi ya kukabiliana na jambo lililokuwa
mbele yao.
Baada ya mapumziko ya saa moja hivi,
Willy na Bibiane waliendelea na safari yao
na kuwasili Gisenyi saa nane za mchana.
Moja kwa moja walikwenda Hoteli
Meridien-Izuba, ambako walipanga
kuonana na maofisa ambao Col.
Rwivanga alikuwa amewapasha habari
waonane nao na wawape habari kamili
kuhusu uhalifu unaofanywa huko Gisenyi
na Kibumba, ili kama walikuwa
wamebahatisha kupata habari zozote
wazipate hapo.
Meridien Hoteli Izuza ilikuwa moja ya
hoteli nzuri sana ingawa vita vya
wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda
vilikuwa vimeiathiri kidogo hoteli hii, lakini
ilibaki kuwa safi pamoja na misukosuko
ilivyokuwa sehemu hii. Ikiwa kwenye
ufukwe wa Ziwa Kivu, mpakani mwa
Zaire, huku kwa mbali ukiangalia milima
ya volkano ya Virunga, kweli Meridien-
Izuda palikuwa mahali pazuri sana pa
kupumzika.
"Umepapenda hapa?", Bibiane alimuuliza
Willy Gamba.
"Mbona wewe unapenda kusoma mawazo
yangu?", Willy aliuliza.
"Ubaya uko wapi Willy, fikiri kama
tungekuwa tunakuja hapa kwa ajili ya
mapumziko na si hii kazi ya hatari, huoni
kuwa ingekuwa raha sana, mimi naona
tungestarehe sana", Bibiane alijibu.
Huku akitabasamu Bibiane alitoa mkoba
wake ndani ya gari huku Willy akijibu.
"Sawa mama umeshinda".
Baada ya gari la Msalaba Mwekundu
lililokuwa likitumiwa na Willy na Bibiane
kusimama, askari wanne walielekea
kwenye gari hilo, walipofika karibu mmoja
wao moja kwa moja akauliza. "Natumaini
nyinyi ni Bwana na Bibi George Mambo
wa Msalaba Mwekundu kutoka Makao
Makuu Nairobi?".
"Bila shaka", Willy alijibu bila kusita huku
Bibiane amejikausha utafikiri kweli
alikuwa mke wake, baada ya
kutambulishwa vile, Willy alitambua kuwa
huyu mwanamke alikuwa kweli
amefundishwa vizuri mambo ya upelelezi
maana Willy hakumweleza mapema jinsi
ambavyo wale askari wangetambulishwa
hapa. Kazi yote hii ilikuwa imefanywa na
Col. Rwivanga.
"Kamanda Kasubuga anawasubiri pale
ofisini kwake", yule askari alimweleza
Willy Gamba.
"Twende", Willy alimweleza Bibiane.
"Hapana, wewe nenda tu, mimi
nitakusubiri hapa", Bibiane alijibu na Willy
akaelewa maana na sababu ya Bibiane
kubaki pale, akafurahi moyoni kuwa kweli
alikuwa amepata mshirika katika kazi.
Kamanda Kasubuga alikuwa mtu mwenye
rika la Willy na baada ya Willy kuingia
ofisini kwake aliinuka kwenye kiti
alichokuwa amekaa akisoma faili moja
hivi, huku akitabasamu akamlaki Willy.
"Karibu sana", Kamanda Kasubuga
alimkaribisha Willy.
"Asante", Willy alijibu huku wakishikana
mikono na Kamanda Kasubuga
alimwonyesha ishara yule askari
aliyemleta Willy awape faragha kidogo,
yaani aondoke awaache peke yao.
Baada ya yule askari kutoka Kasubuga
alisema, Lo! Bwana Willy Gamba ni wewe
huyu, Sifa zako na wewe mwenyewe
hufanani. Col. Rwivanga amenieleza yote
na mimi nikamweleza kuwa nimekusikia
sana nilipokuwa Tanzania. Mimi
nimefanya kazi na Jeshi la Tanzania na
vyeo vyangu vyote mpaka hiki cha umeja
nimevipata nikiwa Tanzania".
"Alaa! nashukuru sana", Willy alijibu na
kuketi kwenye kiti.
"Oke, bila kupoteza wakati, habari kutoka
kwa kijana wetu ambaye juzi tu tumeweza
kumnunua kutoka katika jeshi la Zaire
linalolinda mpaka na sisi zinaeleza kuwa
leo hii yapata saa kumi na mbili na nusu
asubuhi waliwasili watu wawili upande ule
wa Zaire na kupokelewa kwa heshima
zote za kijeshi na kisha wakaondoka
kuelekea kwenye makambi ya wakimbizi
kule Kibumba. Baada ya maelezo ya jinsi
wale watu walivyofanana tulielewa mara
moja kuwa mmoja wao alikuwa Col.
Gatabazi. Hivyo, Col. Gatabazi kafika na
yuko Kibumba", Meja Kasubuga alieleza.
"Hizo ni bahari njema sana, sasa ngoja
na sisi tupumzike halafu giza likiingia na
sisi tutakwenda Kibumba", Willy alijibu
huku Meja Kasubuga akimwemwesa.
"Sawa mzee, ila tumewawekea chumba
kimoja maana ni mimi tu ninajua wewe ni
nani, hawa askari wengine wote wanajua
kweli wewe ni afisa wa Msalaba
Mwekundu na kwamba kwa vile unajua
utakaa Rwanda kwa muda mrefu umekuja
na mke wako", Meja Kasubuga
alimweleza Willy.
"Hapa taabu", Willy alijibu kwa mkato.
"Safari ya Kibumba, tumeagizwa na Mkuu
wetu kuwa tufuatane, maana siku zote
nimetaka kuvuka na kikosi changu cha
hapa lakini nimekuwa nakatazwa, lakini
leo nimeamriwa tufuatane wote, sijui
safari itakuwa saa ngapi?".
"Sijui, tutaangalia wakati huo si na wewe
unakaa hapa hapa hotelini?".
"Ndiyo mzee, niko chumba namba 110,
nyie mtakuwa nambari 220 kwenye
vyumba vinavyofuata".
"Sawa", Willy alijibu na kuaga. Aliporudi
pale kwenye gari alimkuta Bibiane
anapiga soga na wale askari.
"Tupelekeni chumba namba 220", Willy
aliwaeleza wale askari.
Askari mmoja aliingia ndani ya gari baada
ya kushusha mizigo yao, akawapeleka
kwenye banda lililokuwa na chumba
nambari 220. Yule askari alipoondoka
Bibiane akasema, "Kwa vile kuna kitanda
kimoja tu wewe utalala ng'ambo ile na
mimi ng'ambo hii".
"Lo, kumbe ulikuwa unajidai bure, sasa
umeanza masharti".
"Si tulisema kazi kwanza?", Bibiane alijibu
huku akifunga mlango kwa funguo na
kuanza kuvua nguo huku akiendelea
kusema, "mimi nitaoga kwanza.
"Sawa mama", Willy alijibu huku mawazo
yake yakiwa tayari yameanza kupanga
mipango ya usiku ule. "Tukimaliza wote
kuoga tuitishe chakula kidogo halafu
tupumzike angalau kwa masaa mawili
ndipo safari ya Kibumba ianze", Willy
alimwambia Bibiane.
"Amri itatoka kwako baba, mimi kazi
yangu ni kutii amri tu", Bibiane alijibu
huku sasa akiwa amevua nguo zote pale
kitandani.
 
Dah! Afadhali kiu imepugua kidogo... bila shaka kidi kudi na mareche mtaimalizia kabisa
 
Back
Top Bottom