Riwaya: UCHU

Riwaya: UCHU

MIGUU YA NYOKA

II

Willy alipofika kwenye nyumba ya Luteni Biniga taa za ndani zilikuwa zikiwaka. Nyumba hii ilikuwa imezungushiwa ua kama alivyokuwa ameelezwa na Col. Rwivanga. Badala ya kubisha hodi langoni aliamua kupita kwenye uchochoro, akapanda ukuta kisha akatumbukia ndani. Alitambaa chini kwa chini mpaka akaufikia ukuta wa nyumba hii. Dirisha la nyuma lilikuwa limefungwa, hivyo aliendelea kuambaa na ukuta. Ndipo aliposikia sauti za watu wakizungumza na kucheka. Alichungulia dirishani na kuwaona watu watatu. Wanaume wawili na mwanamke mmoja. Mazungumzo yao yalikuwa kwa lugha ya Kifaransa, ambayo Willy aliielewa vizuri sana, mazungumzo yao ndiyo yaliyomshitua na kumweka chonjo.

"Kazi mimi nimeifanya kwa ustadi mkubwa. Hiyo pesa kweli iko kwenye akaunti yangu Nairobi?", mmoja wa wale vijana alimwuliza yule mwanamke.

"Siyo wewe tu, nyote kesho pigeni simu kwenye benki zenu. Mambo safi. Nimeelezwa na wakala wa mlipaji kuwa pesa zimetumwa kwa njia ya 'swift' na tayari ziko kwenye akaunti zenu", yule mwanamke alijibu.

"Mimi nilihitaji kulipwa dola laki moja. Ndizo zilizotumwa na kuwekwa kwenye akaunti yangu?", yule mwanaume wa pili aliuliza.

"Ndio. Sasa kwenye akaunti yako kuna dola laki tatu. Zimeingia pamoja na zile za malipo ya kuwatorosha wale makamanda wa Intarahamwe kwenda Zaire", yule mwanamke alijibu.

"Kama kesho nikijuwa pesa yangu yote hiyo iko benki, basi mimi nitatoroka kwenda Kenya. Halafu Afrika Kusini. Sitaki kukaa hapa tena, tusije tukabainika kuwa tuko kwenye upinzani", mwanaume wa pili alisema.

Hapa Willy aliamini kuwa wakati wa kukabiliana ana kwa ana na watu hawa ulikuwa umefika kwani walionekana kana kwamba wanataka kuondoka. Mawazo na akili ya Willy yalivutika sana kwa yule mwanamke kuliko hata kwa wale wanaume wawili ambao alihisi ni Luteni Silasi Biniga na Juvinali Mukama. Alipogeuka tu kutaka kwenda kubisha hodi kwenye mlango wa mbele, alijikuta akiuangalia mtutu wa bunduku kubwa aina ya 'Sub Machine Gun'.

"Usisogee hata hatua moja. Hapohapo ulipo weka mikono yako juu, geuka nyuma na utembee kuelekea mlango wa mbele ya nyumba hii", Willy alimrishwa na yule askari na kutii amri kama alivyokuwa ameamriwa.

"Nani huyo tena", Silasi Biniga aliuliza katika hali ya mshangao.

"Nini Ananie", Juvinali naye aliuliza.

"Inkotanyi", Ananie alijibu.

"Bibiane wewe nenda. Sisi ngoja tujuwe huyu mtu ni nani?", Juvenali alimweleza yule mwanamke huku yeye na Luteni Biniga wakichukuwa bastola zao na kutoka nje kwenda kumkabiri mtu huyu aliyekuja kuwapeleleza ili kabla hawajamuua wajuwe ni nani na anajuwa nini kuhusu wao. Wakati Bibiane anatoka ndani alikutana na Willy pamoja na mtu aliyemkamata, wakiwa wamefika mbele ya nyumba, kwenye mlango wa mbele.

"Simama hapo", Ananie alimwamru Willy huku akiwa bado ameweka mikono yake kichwani. Bibiane alipotoka nje alimwangalia Willy. Willy naye akamtazama. Kulikuwa na mwanga wa kutosha kuweza kumtambua mtu. Bibiane alimwemweseka kwa Willy kisha akalekea kwenye lango kubwa la kutokea nje na kutokomea gizani.

"Luteni Biniga..., lazima mtu huyu ni Inkotanyi, amekuja kupeleleza kuhusu tukio la leo", Ananie alimwambia Luteni Biniga walipotoka nje pamoja na Juvinali. Luteni Biniga alimwangalia Willy na kwa sura yake akabaini kuwa mtu huyu hakuwa Mnyarwanda. Bila kuchelewa Luteni Biniga alimpiga Willy kwa kitako cha bastola kwenye paji la uso na Willy akaanguka chini. Alipoanguka Juvinali naye alimpiga teke la tumboni. Willy alipotaka kuinuka alipigwa teke la ubavuni. Ni hapa ambapo mambo yaligeuka. Baada ya Juvinali kutupa teke kali lililompata Willy vilivyo ubavuni. Willy akahisi amevunjika mbavu, kama sumaku.

Willy aliunasa mguu wa Juvinali kabla haujarudi na kuupinda, kisha akauvuta upande wake, haraka sana akamlalia juu. Hii yote ilitokea kwa haraka mno kiasi cha kuwatatanisha Luteni Biniga na Ananie wasijuwe wafanye nini kwani wangefyatua risasi wangemuua Juvinali. Bastola ya Juvinali ilianguka chini karibu yao. Tena kwa kutumia nguvu zote alizokuwa nazo Willy alimrusha Juvinali kwa Ananie aliyekuwa kama hatua mbili kutoka pale walipokuwa. Juvinali akamkumba Ananie, wakaanguka huku bunduki ya Ananie ikitema risasi zilizomwingia Juvinali na kumwua hapohapo.

Wakati Willy alipomrusha Juvinali kwa Ananie. Haraka aliirukia ile bastola na kumpiga risasi kadhaa Luteni Biniga. Kabla hajafyatua bastola yake, risasi zikampata Luteni Biniga kwenye paja la uso na kumwua pale pale. Ananie naye kwa kutumia nguvu zake zote. Alijaribu kuitoa maiti ya Juvinali ili aichukuwe tena bunduki yake. Lakini hakuwahi. Willy alimpiga tena teke la kichwa na kumtoa fahamu. Willy akaivuta maiti ya Juvinali na kuitoa juu ya Ananie na kuanza kumvuta Ananie ili aweze kumuuliza maswali. Mara akasikia mlio kama wa king'ola. Akajuwa ama yule mwanamke ameripoti au ule mlio wa bunduki na bastola umesikika. Hivyo akajuwa angekutwa pale, kwa hasira aliivunja shingo ya Ananie na kumtupa chini. Akakimbilia ukutani. Akauparamia ukuta na kuangukia kwenye uchochoro wa mtaa wa pili; akakimbilia kwa Col. Rwivanga.

Alipoingia nyumba ya Col. Rwivanga. Ndipo Col. Rwivanga alipojuwa kuwa alipokuwa ameumia sana. Col. Rwivanga alikuwa ameusikia mlio wa bunduki lakini kwa Kigali halikuwa jambo la ajabu, ingawa alikuwa na wasiwasi. Lango la ua wake lilipofunguliwa tu alikuwa nje na ndipo alipomwona Willy akiingia huku akipepesuka. Col. Rwivanga alimsaidia wakaingia ndani. Willy alikuwa anatoka damu puani, Col. Rwivanga akajuwa kuwa alikuwa ameumia sana maana alipoonekana kama ana nyuso mbili kwa vile paji lake lilikuwa limevimba vibaya sana.

"Utadhani umekanyagwa na trekta", Col. Rwivanga alisema baada ya kumwona Willy.

"Nakwambia ni zaidi ya trekta. Sijawahi kupigwa teke lenye nguvu kama lile", Willy alijibu.

Dkt. Daniel Robinson alikuwa daktari mkuu wa Hospitali ya King Faisal mjini Kigali na alikuwa rafiki mkubwa wa Col. Rwivanga kabla Dkt. Robinson hajaja Rwanda alikuwa daktari katika Hospitali ya Mulago mjini Kampala, ambako alikuwa akiishi karibu na Col. Rwivanga. Na kwa muda wote walipokuwa Kampala walikuwa marafiki wa karibu sana.

Kwa hivyo wakati RPF walipoingia tu Kigali, Col. Rwivanga ndiye aliyekuwa kiongozi wa kikosi cha kwanza kabisa kilichoongoza mapambano dhidi ya majeshi ya serikali. Na kituo cha kwanza kabisa ni kuwaokoa watu waliokuwa Hospitali ya King Faisal ambako kuliwa na maelfu ya watu wakiwa pamoja na rafiki yake Dkt. Robinson. walikuwa wamejisalimisha ndani ya Hospita, lakini baada ya Intalahamwe kuwa wamewaua watu wengi Hospitali hapo pamoja na wagonjwa.

Baada ya Col. Rwivanga kuingia na kikosi cha kulinda usalama, watu wengi walipona. Siku zilizofuata majeruhi na wengineo aliponea katika Hospitali hiyo, hivyo Col. Rwivanga alimpigia simu Daktari Robinson ambaye ni Mzungu Mwingereza na kumweleza juu ya Willy kujeruhiwa.

"Niko njiani!", Dkt. Robinson alimweleza Col. Rwivangga, wakati walipokuwa wanamsubiri Daktari, Willy alimweleza Col. Rwivanga yote yaliyotokea nyumbani kwa Luteni Silas Biniga.

"Nini maana ya Inkontanyi?, maana waliniita hivyo", Willy aliuliza baada ya kumaliza maelezo yake.

"Inkontanyi huwa ina maana ya RPF. Maana yake hasa ni mpiganaji mkali na maarufu katika Kinyarwanda. Lilikuwa ni jina lililopewa kikosi kimoja cha Mfalme wa Bugiri katika karne ya kumi na tisa hivyo. Walihisi kuwa wewe utakuwa ni mpelelezi wa RPF", Col. Rwivanga alieleza.

"Kwa hiyo. Inamaana wao siyo RPF", Willy aliuliza.

"Bila shaka, kama ulivyosikia na hili limenitia wasiwasi sana kutambua kuwa katika uongozi wa katikati. Na bila shaka wa juu wa RPF tumeingiliwa na wasalti. Kinachoonekana wazi ni kuwa hawa waliopambana nawe nao ni watu wanaofanya hivi vitendo ni wapenda pesa. Sasa mtu au kikundi hatari ni kile kinachotoa pesa hicho ndicho yafaa tukijuwe na kukiangamiza ili Rwanda iweze kurudi hali yake ya amani", Col. Rwivanga alijibu.

"Basi mtafute yule mwanamke niliyesikia wakimwita Bibiane na jibu lako utakuwa umelipata", Willy alijibu huku akionekana kuwa maumivu yalikuwa yamezidi. Mara akasikia honi ya gari.

"Daktari huyo rafiki yangu, ngoja utubiwe usife maana kazi sasa ndiyo imeaanza", Col. Rwivanga alimtia moyo Willy.
 
MIGUU YA NYOKA

III

Col. Gatabazi alikuwa kati ya watu wa kwanza kufika kwa Luteni Silas Biniga, maana alikuwa akiishi nyumba ya nne tu kutoka pale. Alipofika hakuamini macho na akili yake ilishindwa kukubali. Watu wote hawa waliouawa walikuwa watu makini katika kundi lake, watu ambao alijua ndio wangemsaidia kuchukua madaraka muda utakapofika. Hili jambo lilimshitua sana. Watu wote hawa walikuwa askari shupavu, jasiri na waliojuwa kazi yao vizuri.

Yeyote yule aliyefanya kitendo hicho hakuwa mtu wa kawaida na kama ni kikundi, hakikuwa kikundi cha kawaida. Hawa watu watatu walikuwa na uwezo wa kuangamiza kikosi kizima cha jeshi la maadui lakini leo wameuawa kirahisi na wote kwa pamoja! Suala hili lilimshitua sana Col. Gatabazi, akaingiwa na woga na wasiwasi.

Gari la jeshi lenye king'ola, lilikuwa tayari limefika pale likiwa na askari wa doria wa sehemu zile, askari hao walifika mara baada ya kusikia milio ya risasi.

"Vipi hamjaona au kukutana na mtu au watu wowote waliofanya kitendo hiki?", Col. Gatabazi aliwauliza wale askari wa doria kwa ghadhabu.

"Hapana afande, kote hapa ni shwari", mmoja wapo alijibu.

"Haiwezekani kuwa shwari wakati maafisa wanaotegemewa kama hawa wameuawa hovyohovyo hivi", Col. Gatabazi alieleza tena kwa ukali.

"Huenda wameuana wao wenyewe afande", askari wa pili wa doria alijibu.

Col. Gatabazi alimwangalia kwa jicho baya mpaka yule askari akarudi hatua moja nyuma.

"Chukueni hizi maiti pelekeni hospitali na poteeni hapa mara moja", Col. Gatabazi aliamrisha mara moja.

Col. Gatabazi alirudi nyumbani kwake ili apige simu Ufaransa. Alipofungua mlango wa mbele aliukuta uko wazi. Alishituka, akatoa bastola yake tayari kukabiliana na lolote ambalo lingetokea mbele yake. Alifungua mlango kwa ghafla huku bastola yake ikiwa tayari tayari.

"Vipi! mbona wasiwasi?", Bibiane alimuuliza huku akiweka mguu mmoja juu ya mwingine pale sebuleni alipokuwa ameketi.

"Hujui kumetokea mauaji mabaya sana usiku huu na vijana wetu watatu wameuawa?", Col. Gatabazi alihoji huku akirejesha bastola yake kwenye mkoba wake na macho yake yakiangalia mapaja ya Bibiane ambayo yalikuwa yameachwa wazi kwa kitendo chake cha kuweka miguu juu ya mwingine na kufanya nguo yake iliyokuwa fupi na ya kubana kuyaacha wazi.

Bibiane Habyarimana alikuwa mtoto wa Kinyarwanda ambaye baba yake alikuwa Mhutu na Mama yake chotara wa Kitutsi na Kifarasa. Alikuwa msichana aliyeumbika kwa sura na mrembo katika warembo. Alikuwa na urefu wa futi tano na inchi nane, hivyo, alikuwa mwanamke na urefu wa kutosha. Alikuwa na nywele ndefu za singa, macho makubwa ya blue, mashavu ya kumimina, pua ya kuchonga, midomo ya tasi, meno meupe yaliyopangika na kuacha mwanya kwenye safu ya juu. Hakika, alikuwa kapendelewa na muumbaji. Mwili wake mzima ulikuwa na muundo wa nyigu, juu mwembamba chini kajaa, akimalizia na miguu minene ivutiayo macho.

Ilimchukua Col. Gatabazi muda mrefu kupata la kusema maana kila alipoonana na msichana huyu alijikuta ulimi wake unakuwa mzito, anashindwa hata kusema. Mara nyingi alipatwa na kigugumizi kwani moyo ulimwenda mbio.

"Aliyewaua mimi nimemwona", Bibiane alieleza bila wasiwasi utafikiri alikuwa anazungumza kitu cha kawaida tu.

"Unasemaje?", Col. Gatabazi alimuuliza kwa mshangao.

"Aliyewaua nimemuona mimi. Nilikuwepo alipofika pale kwa Luteni Biniga", Bibiane alijibu tena kwa utulivu, kisha akasema, "Hamna hata kinywaji humu ndani". Kila wakati Col. Gatabazi alishangazwa na tabia ya huyu binti.

"Kinywaji kipo, huenda kweli tunakihitaji maana sasa wewe unazidi kunichanganya", Col. Gatabazi alisema na kuelekea kwenye kabati la vinywaji akatoa chupa ya whisky na gini, akaleta barafu na glasi mbili.

"Utakunywa nini?".

"Whisky niwekee barafu tu usiiharifu na maji".

"Sawa mama, ehee unamaje eti ulikuwepo kwa Luteni Biniga?", Col. Gatabazi aliuliza kwa shauku ya kutaka kujua.

Bibiane alimweleza kwa kirefu yaliyotokea pale kwa Luteni Biniga na kumalizia, "Watakati natoka ndani walikuwa wakimwuliza maswali pale nje, awaeleze yeye ni nani. Sikuwa na wasiwasi maana nilijuwa yule kaisha. Mbele ya wale wanaume hakuna ambaye angefanya kitu. Niliposikia risasi zinalia ile ya kwanza nilijuwa kauawa, lakini niliposikia milio ya risasi inazidi nikawa na wasiwasi nikarudi haraka kuchungulia na nikaona uliyoyaona, lakini mimi nilikuwa na bahati ya kumwona akiruka ukuta upande ule mwingine, akapotelea gizani. Yule ni mwanaume wa shoka na hapa kazi ipo, sina shaka yule ni Willy Gamba kama Jean alivyomwelezea. Hivyo, umeshindwa mtihani wako wa kwanza huyu mtu hakufa ndani ya ile ndege mliyoitungua. Fanya utafiti, utakuta amekuja na ndege nyingine, kakuzidi maarifa, tayari alishajuwa ni Luteni Silas Biniga aliyeamrisha ile ndege kupigwa. Mtu huyu ni hatari, mbona ni hatari sana! Kazi kwako Gatabazi. Kama unataka Uras kwanza inakubidi huyu mtu ummalize. Hizi habari zitamsikitisha sana Jean, wewe unajua.

"Usipommaliza haraka basi ujuwe wewe umekwisha kwani atakuumbua na RPF watakumaliza na utakuwa umewaangamiza Wahutu", Bibiane alimalizia na tabasamu la mauti.

Woga ulimwingia Col. Gatabazi maana naye alihisi kuwa huenda yule alikuwa Willy Gamba. Rwanda hakukuwa na mtu mwenye uwezo kama huo. Jean alimweleza kwa kirefu uwezo wa huyo Willy Gamba na sasa aliudhihilisha. Vilevile, alijuwa Jean angekasirishwa sana kuona huyu mtu amejipenyeza mpaka kuleta maafa makubwa hivi.

Mtu wa kuweza kumsaidia kumweleza Jean mpaka amwelewe na kumsaidia katika mapambano na mtu huyu alikuwa ni Bibiane. Ingawa alikuwa akimtamani sana Bibiane, lakini alikuwa mwangalifu sana asimguse maana alijuwa siku moja angeweza kumtumia.

Bibiane alikuwa karibu sana na Jean alikuwa mpenzi wake lakini vilevile Bibiane alikuwa mhitimu wa fani ya upelelezi na usalama na akiwa amesomeshwa kwa msaada wa Jean. Jean alikuwa akifanya mambo yake kwa ufasaha. Alihitaji kuwa na mtu Afrika Mashariki na Kati ambaye angeangalia mambo yake bila kuhisiwa. Pamoja na kuwa alikuwa ametumbukia katika lindi la mapenzi na Bibiane, lakini kwa upande mkubwa alimtumia Bibiane kufanikisha mambo yake yaliyokuwa yakimletea maslahi.

Sababu hizi ndizo zilizomfanya Jean amugharamie Bibiane mafunzo ya hali ya juu ya upeleelezi na kweli msichana huyu alifuzu vizuri na alikuwa mjuzi. Idara ya upelelezi na usalama ya Ufaransa inayoshughulikia usalama wa nje (DGSE) ilimuongezea ujuzi msichana huyu na mara nyingi walimtumia katika kazi zake.

Ni huyu msichana, kwa kutumwa na DGSE, alikisambaratisha kikundi cha wanajeshi waliotaka kuipindua serikali ya Hassan Gouled wa Djibouti na kufanya wakamatwe, kwani siri zao zote alitoa wa serikali kupitia DGSE mpaka leo haikujulikana jinsi alivyoweza kupata ushahidi huo ambao hata kikundi hicho cha wanajeshi kilibaki kimepigwa na butwaa. Msaada huo wa Bibiane kwa DGSE ulimwongezea Jean uhusiano wa karibu.

Hivyo hata Bibiane alitumia idara hiyo kwa kumsaidia katika mambo yake. Ni Bibiane aliyekuwa kiungo kikubwa kati ya Jean na familia ya Rais. Ingawaje na yeye aliitwa Bibiane Habyarimana hakuwa na uko na Rais kwani familia za Kinyarwanda hutumia jina lake na siyo jina la ukoo kama jamii zingine.

vilevile, msichana huyu ndiye aliyekuwa kiungo kikubwa na wakubwa wengine wa serikali katika Afrika. Kutokana na umbile na sura yake ya kuvutia, ambayo kila siku ilimuonesha kuwa msichana mdogo asiyezidi umri wa miaka kumi na minane, hakuna aliyeweza kumuhisi kama mmoja ya watu hatari waliokuwa kiungo cha uhaini na ugaidi kati ya wakuu wa serikali, wafanyabiashara na magaidi wa Ulaya. Inasemekana wakati wa mkutano wa amani uliofanyika mjini Arusha, Tanzania, Bibiane alikuwapo kama mkalimani.

Baada ya mkutano huo, rais alimpa nafasi aondoke nae kwenye ndege yake, kwani alikuja kama mkalimani wake lakini Bibiane alikataa na kuondoka na Jean kwa barabara kupitia Nairobi, nchini Kenya. Inasemekana alijua nini kingetokea, kwani yeye aliingia kwa ndege ya jeshi la Ufaransa akitokea Nairobi, mara tu baada ya marais kuuawa tarehe 6 aprili Bibiane alisaidia kumchukua mke wa rais na familia yake ya watu kumi na watano na kuwapeleka Ufaransa.

Pia. Inasemekana. Kwa kusaidiana na Jean aliwawezesha Protais Naimana na Feldinand Zigilanyilazo kuwapatia visa ya kusafiria na kuwawezesha kwenda Ulaya. Hivyo. yote hii inaweza kukuonyesha jinsi gani msichana huyu mwenye umri wa miaka ishirini na saba tu alivyoweza kufanya mambo makubwa. Alikuwa msichana hatari sana.

Lazima tumweleze Jean hali halisi", Col. Gatabazo alimweleza Bibiane.

"Piga simu!".

"Sawa. Lakini uzungumze nae kwanza".

"Sawa!", Bibiane alijibu. Alimwangalia Col. Gatabazi. Akaona kuwa ameingiwa na woga. Bibiane aliwaponda sana wanaume walioonekana waoga. Kwa mara ya kwanza alimponda Col. Gatabazi, aliwapenda sana watu jasiri mwanaume yeyote shupavu aliifanya damu yake ichemke na kuchochea tamaa zake za mwili. Lakini mwanaume mwoga hata awe mzuri na sifa aina gani alimtia baridi. Mara hii alihisi baridi na kumchukia Col. Gatabazo mawazo yake yalitembea na kumfikiria Jean. Ile kumfikiria tu alihisi damu yake ikichemka. Kwake Jean ndiye alikuwa mfano wa mwanaume ampendaye, jasiri, shupavu anayepata kile anachokitaka hata iwe kwa gharama gani, hata ikibidi kuhatarisha maisha yake.

Ndivyo Jean alivyokuwa. Bibiane alimpenda Jean kikwelikweli. Ingawa Jean alikuwa mzungu, lakini alikuwa mzungu wa aina yake. Alijuwa kupenda na alijuwa jinsi ya kumfurahisha mwanamke mpaka kumaliza haja zake za kimwili. Lakini zaidi ya yote alimpenda kwa ujasiri na ushupavu wake katika mambo yake. Iwe biashara, iwe siasa yeye alikuwa ndie bingwa wa mchezo.

Alifikiria jinsi watu wenye vyeo vikubwa, wakuu wa nchi, matajiri walivyo yeyuka kama barafu mbele ya Jean kila alipopambana nao. Kila siku ndiye aliyetokea kuwa mshindi. Hata rais alipojaribu kumgeuka na kukabiliana na mambo kinyume na matakwa yake, Jean aliibuka mshindi na rais akapoteza maisha. Hata hali ya sasa ya Rwanda, kuwepo RPF, ilikuwa kata ya mbinu zake. Na Bibiane aliamini kabisa kuwa hii ilikuwa ni mipango yake ili baadae aiondoe serikali ya RPF na kumuweka mtu wake Col. Gatabazi. Mwanzo Bibiane alirudi kwa Col. Gatabazi.

Alimfikiria na kisha akatambua mtu kama yeye ndiye angewafaa yeye na Jean, mtu mwoga, mtu anaependa fedha, mtu ambaye anafanya kile ambacho angeambiwa. Kiongozi kama viongozi wengine wa Afrika, mtu anayejifikiria yeye na wala sio nchi au watu wake, mtu mbinafsi, kama walivyo watawala wengi wa kiafrika, Col. Gatabazi alifaa sana kutawala Rwanda.

"Njoo Jean yupo kwenye simu," Col. Gatabazi alimshtua Bibiane kutoka kwenye lindi la mawazo.

"Oh asante sana"" alijibu.

"Mpenzi hujambo?" Bibiane alimsalimia Jean.

"Sijambo, pole na matatizo huko," Jean alijibu.

"Col. amekueleza?"

"Amesema wewe ndiye utanipa safi!"

"Una maana sikupagi safi?"

"Wacha masihara huu si wakati wake. Hebu nieleze imekuwaje?"

"Huwenda na mimi ningekuwepo ningekuwa nimekufa," Bibiane alijibu.

"Sawa tu hiyo ingekuwa kifo kazini," Jean alijibu kwa sauti kavu.

Mara Bibiane akasikia damu yake inasisimka kwani alitaka mwanamume kama huyu asiye na huruma. Huyu ndiye aliyekuwa mwanamume wa kiwango chake.

"Yaani ningekufa asingejali."

"Bila shaka nigejali, lakini kama ungekufa katika mstari wa kazi ni vizuri zaidi kuliko kufa kibudu," Jean alijibu na kuendelea, "Hebu nipe imekuwaje".

Bibiane alichukuwa muda kumwelezea jinsi mambo yalivyotokea.

"Yaani huyu Willy Gamba umemuona kwa macho yako?.

"Ndiyo kwanza sikumtilia maanani sana, nilishtuka kuwa ni yeye baada ya kazi aliyokuwa ameifanya. Mwanzoni nilifikiri ni ka-Inyezi kalikopata fununu ambako vijana walikuwa tayari kushughulika," Bibiane alijibu

"Lazma umsaidie Col. Gatabazi kummaliza huyu mtu, Na mimi nitafanya mipango ya kukupeni msaada wa watu wenye ujuzi wa juu wawasaidie kumuondoa huyu funza anayetaka kula nyama yetu," Jean alijibu.

"Ukisema wewe sisi tutatekeleza, tunaomba hua msaada wako haraka maana hata siye tuna wasiwasi ," Bibiane alijibu.

"Usiwe na wasiwasi, unajua watu kama huyo Willy Gamba ndio nawataka mimi,"

"Najua Jean, wewe tena! Bwana nakuwaza, nataka nije huko unikumbatie, najua huwezi kuja huku sasa!. Bibiane alijibu kwa sauti ya mahaba.

"Baada ya kazi hiyo ya Willy Gamba tuonane Nairobi hata mimi nakutamuni sana," Jean alijibu.


"Haya kazi kwanza."

"Halafu kama kazi," Jean alimalizia na kumuomba Col. Gatabazi tena.

"Kwaheri mpenzi!"

"Kwaheri Bibiane. Col. Gatabazi atakupa mipango yote," Jean alimalizia.

Jean alipozungumza na Col. Gatabazi alimweleza mipango yake ya kummaliza Willy ambayo ilikuwa ikiendelea kichwani mwake.

"Nafikiri mawazo yako ni sahihi tutafanya hivyo. Asubuhi nitawasiliana na wewe," Col. Gatabazi alijibu.
 
kidi kudi shambulia jukwaa kwa kutupia epsode zaidi. technician aksante sana kwa kuokoa jahazi maana kidi kudi kesha tufanya mbaya.

willy gamba ongeza mambo plz
 
MIGUU YA NYOKA IV

Simu ilipolia ilimshitua sana JKS, maana
alikuwa tayari amelala na ilikuwa yapata saa sita za usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
"Hallo", JKS aliita.
"Jean".
Mara moja usingizi ulikwisha.
"Ehe, salama huko?", JKS alijibu kwa shauku maana tokea alipopewa taarifa kuwa Willy Gamba alikuwa ameuawa basi roho yake ilikuwa
imetulia kabisa.
"Mambo siyo mazuri, rafiki yako hakufa na kaibuka na mambo mapya", kisha akamweleza yote yaliyotokea Kigali.
"Basi huyu ana miguu ya nyuka", JKS alijibu huku sauti yake ikionyesha wasiwasi.
Si wewe mwenyewe ulisema ni mtu hatari, na huu mchezo anaujuwa, sasa basi kazi imefika na inabidi sasa iwe kazi hasa, maana wakati wote
tumekuwa tukimchezea", Jean alijibu.
"Sasa mimi nitakusaidia vipi?", JKS aliuliza.
"Utanisaidia mimi au utajisaidia vipi?, unasema kana kwamba wewe haumo kwenye huu mchezo! mchezo huu ni hatari kwako kuliko
mimi maana huyu mtu akigundua kuwa wewe umekuwa mmoja wa watu ambao wamekuwa wakiuhujumu mwelekeo wa nchi yako kuhusu suala hili la Rwanda na masuala mengine basi
ujuwe umeisha na urais wa Tanzania
utauangalia kwenye ndoto zako tu. Kwa hiyo mtu huyu ni hatari kwako kuliko kwangu, hivyo ni kwa faida yako auawe mara moja!!", Jean
alimwasa JKS.
"Tufanye nini sasa?", JKS alijibu kwa sauti ya woga.
"Kati ya vijana wetu wazuri na mahiri na wale vijana walioko Arusha ni wazuri sana. Hao ndio
saizi ya huyu Gamba kutokana na uzoefu walionao na ujuzi pia ambao wanao. Kwa hiyo. Nataka wote wanne na kiongozi wao, Xavier
Nkubana, waende wakaimalize hii kazi. Sasa ninachotaka ufanye ni kuwatafutia pasi mpya za
kitanzania waonekane ni Watutsi ambao zamani walikimbilia Tanzania na sasa wanakwenda
kuangalia hali ilivyo. Siku zote walikuwa wakifanyakazi yao kwa siri na hakuna atakayewashitukia. Hivyo watafutie hizo pasi na usafiri. Uhakikishe kesho wako Kigali. Wakifika Kigali wawasiliane na Col. Gatabazi atawapa maelekezo ya kufanya. Lazima tusishindwe juu
ya jambo hili", Jean alisisitiza.
"Hilo ulilosema hesabu limefanyika, nitatumia nguvu za dola kuhakikisha kesho wako Kigali mapema kabisa. Nkubana amenipigia simu leo
na kusema vijana wanasikia kuchoka kukaa tu bila kazi. Hivyo, nikiwaeleza kuwa wanarudi
Kigali kwa kazi ngumu, watafurahi sana", JKS alijibu.
"Hiyo safi, basi fanya hivyo na wakishafika nipe taarifa. Hata hivyo, Col. Gatabazi atanipa
taarifa, wakiondoka tu mpigie simu Col. Gatabazi", Jean alimalizia na kukata simu.
Saa ileile JKS alipiga simu Arusha ambako ndiko Xavier Nkubana na wenzake walikuwa wakikaa.
Tokea kifo cha Rais wa Rwanda, wao walibaki Tanzania kama wakimbizi na JKS aliwafanyia mipango yote. Hakuna mtu hata mmoja aliyewahisi kwa ubaya, walikuwa wakiishi kwa
starehe na kifahari, kama kawaida ya wageni katika Tanzania.
Tanzania ni nchi ya namna ya kipekee kwani wageni ndio wanastarehe kuliko wenyeji. Kwa mtu mgeni kuishi kifahari ilikuwa ni sawa, lakini
Mtanzania akitokea kuishi hivyo basi watu humhisi kuwa si mtu mwaminifu na husumbuliwa mara kwa mara na vyombo vya dola mpaka imewafikisha watanzania mahala
ambapo hata kama wana uwezo huishi kwa kujibana kwa kuogopa kubuguziwa. Lakini mgeni hata akiishi kifahari vipi alionekana ni sawa na
hakuna chombo cha dola ambacho kingeweza kumgusa, na vilevile wananchi hubaki kumsifia
kwa ufahari wake.
Hivyo, Nkubana na wenzake waliishi Arusha kwa raha mstarehe wakiwa wameifanya Arusha kama sehemu yao ya kufanyia mipango ya kuihujumu
serikali ya RPF. Kusema kweli hawa jamaa walikuwa wauaji katili sana, na si kweli kuwa
walikuwa wamebaki Tanzania wakati wa kifo cha Rais, ila walikuwa miongoni mwa watu walioongoza mauaji ya Watutsi. Inasemekana mmoja kati yao, Felician Nzirorera, ndiye aliyekuwa akitangaza na kuchochea watu kwa
kutumia radio ya RPLM iliyokuwa ikimilikiwa na Wahutu wenye siasa kali. Radio Televisheni Libre
Des Milles Collines (RTLM),iliyokuwa radio ya uchochezi, na mauaji yalipoanza wengi wa watangazaji wake walijiunga katika mauaji na
wakubwa wao kukimbilia nje baada ya
kuchochea mauaji.
Lakini Nzirorera aliendelea kwa muda mrefu akiwa anatangaza kwa kuhama na stesheni yake ya redio kwenye gari akiwachochea Wahutu kuendelea kuwauwa Watutsi. Na ni mtu huyu
pamoja na wenzake aliyekuwa akila starehe hapo mjini Arusha akiendesha magari ya fahari badala ya kuwa amekamatwa kungojea mahakama maalumu ya wauaji hapo Arusha.
Kama si JKS kuwasaidia na kuwapa sifa tofauti kuwa wao walikuwa ni maafisa safi wa serikali
waliojikuta kwenye mapambano ambayo
hawakuwa washiriki, leo hii wangekuwa kati ya watu waliokuwa wakitafutwa na mahakama ya
kimataifa ya mauaji ya Rwanda.
Simu ililia chumbani mwa Nkubana, bahati nzuri alikuwa ndio kwanza amerudi toka hoteli Sabasaba kwenye disko ambako alijipatia
msichana wa kustarehe naye usiku huo. Simu ilipolia Nkubana alimwacha yule msichana sebuleni na kwenda kuchukua simu chumbani.
"Hello, Xavier".
"JKS".
"Shikamoo, vipi kulikoni".
"Sikiliza kwa makini".
JKS alimweleza yote kuhusu ambavyo yeye na wenzake walikuwa wakitakiwa kwenda Rwanda kumsaidia Bibiane na Col. Gatabazi kummaliza Willy Gamba.
"Hiyo safi sana, tulikuwa tunakaa hapa, tunalewa na kustarehe tu na wanawake maana hatukuwa na kazi. Sisi tuko tayari hata sasa", Nkubana
alijibu.JKS alimweleza mipango yote na jinsi ambavyo wangesafiri mpaka Kigali.
"Hakika mzee, wewe hushindwi kitu. Kweli madaraka ukijuwa kuyatumia ni matamu sana maana kila kitu kinawezekana, sijui bila wewe
tungefanya nini. Asante sana. nitawaeleza wenzangu. Hivyo, saa mbili asubuhi tutakuwa tayari. Na hesabu hiyo kazi huko Kigali imeisha
maana tuna uchu na damu", Nkubana alijibu kwa majidai.
"Asante na kwa heri".
Nkubana alikuwa amewaacha wenzake kwenye disko. Aliporudi sabuleni alimkuta yule msichana
amelala kwenye kiti.
"We, amka turudi kwenye disko".
"Kwanini, mimi nataka kulala, nimechoka".
""Kwani umekuja kulala hapa, kulala ni nyumbani kwako, hapa uko kazini, kazi ya kunistarehesha mimi, kwa vile nasikia nataka kucheza disko
tena, utanifuata".
Yule msichana akiwa anashangaa, Nkubana alimuinua na wakaelekea kwenye gari ili kurudi
disko sabasaba.

CENTRE CHRISTUS
Ilikuwa yapata saa moja ya usiku wakati Willy alipofika kwenye kituo cha kidini cha Centre Christus. Alikuwa bado anasikia
maumivu ya ubavuni yaliyotokana na
mapambano ya juzi yake. Hata hivyo,
aliamua kuendelea na kazi kwa vile muda ulikuwa hamruhusu kungoja apone
kabisa.
Langoni mwa kituo hiku alimkuta mtawa mmoja aliyemwuliza jina, na baada ya kujitambulisha mtawa huyu alimchukuwa Willy na kumpeleka kwenye nyumba ya
Padri Marcel Karangwa ambaye alimkuta akimsubiri.
"Karibu sana Willy Gamba, karibu Kigali.
Kigali inanuka mauti; hata nyumba ya
Mungu inanuka mauti", Padri Karangwa
alimkaribisha sebuleni mwa nyumba
yake.
"Nashukuru sana Padri hasa kwa kukubali mimi nije nikuone mara tu baada ya maafa yaliyotokea kwenye kituo chako hiki, nashukuru sana", Willy alijibu.
"Unakaribishwa sana, Bwana Musoke
amenieleza kila kitu, nasi tunafarijika sana kukutana na watu kama nyinyi ambao mnaweza kuleta matumaini ya amani ya nchi kama hii. Kweli, tuko tayari kukupa maelezo yoyote unayohitaji kwa
shughuli yako", Padri Karangwa
alimweleza Willy.
"Asante Padri, mimi nisingependa
nichukuwe muda wako mwingi kwa vile
una majukumu makubwa ya kukijenga
upya kituo hiki na kurudisha imani ya watu katika nyumba ya Mungu", Willy alijibu wakati mmoja wa watawa akileta chai na kahawa.
"Utakunywa chai au kahawa", Padri
Karangwa alimuuliza Willy.
"Chai ya rangi", Willy alijibu na kupewa chai ya rangi na kipande cha mkate na Padri Karangwa akapewa kahawa.
"Bwana Musoke alisema ungependa
kujuwa kwa kifupi hasa ni nini kiini cha chuki iliyokithiri kati ya makabila haya ya Kitutsi na Kihutu".
"Sawa kabisa", Willy alijibu.
"Kwanza kabisa mimi ni Mtutsi...".
Alipoanza kuongea akaingia Padri
mwingine. Padri Karangwa alimkaribisha na kumjulisha kwa Willy Gamba. "Huyu Padri Boniface Sibomana na ni mmoja wa
watu waliopona mauaji". Kisha
akamjulisha Willy Gamba. "Na huyu ni
Willy Gamba, mwandishi wa habari kutoka Tanzania, ambaye pia amekuja kama wengine wengi waliomtangulia kutupa pole na kutaka kuelewa vipi watu wa nchi moja wanaweza kugeukiana na kuuana kikatili namna hii.
Willy na Padri Sibomana walipeana
mikono na wakaketi chini kuendelea na mazungumzo.
"Kama nilivyokueleza mimi ni Mtutsi,
lakini Padri Sibomana ni Mhutu, sasa
sema tofauti yetu sisi kimaumbile ni
nini?", Padri Karangwa alimwuliza Willy.
Willy aliwaangalia wote wawili. kweli kimaumbile kati ya hawa wawili hasa hakukuwa na tofauti.
"Hakuna", Willy alijibu huku mapadri hawa wawili wakitabasamu.
"Kama hakuna jibu la swala zima la
mauaji ya Watutsi na Wahutu wenye
msimamo wa wastani, basi mauaji haya
yalishinikizwa kisiasa na kikundi cha watu wachache wenye madaraka
makubwa katika Serikali ya Rwanda.
Mara nyingi vita ya wenyewe kwa
wenyewe katika Rwanda ikisingiziwa
kuwa ni vita ya kikabila. Hii si kweli na inapotosha ukweli, ila yanapotokea mauaji kama haya ndipo ujenzi wa chuki wa kikabila unajengwa. Wahutu na Watutsi wameishi pamoja kwa karne
nyingi na tofauti zao si hizi tunazoziona leo, kwani hakukuwa na chuki kati ya makabila haya. Ni utawala wa kikoloni wa kugawa nitawale na baadaye. Serikali
zetu zilizoongozwa na ubinafsi na uchu wa madaraka uliohubiri kuwepo tofauti kati ya wahutu na Watutsi, tofauti ambazo awali hazikuwepo. Kwa kifupi ni kwamba ili mbinu za kisasa za kuyatumia makabila haya mawili ili watawala wabaki kwenye madaraka ambayo yamesababisha mauaji haya ya kikatili ambayo tumeyashuhudia", Padri Karangwa alinyamaza kidogo ili anywe kahawa yake wakati Willy na Padri Sibomana wakimsikiliza kwa makini.
Kisha Padri Karangwa aliendelea. "Kama
nilivyosema mwanzo, mauaji ya kikatili Rwanda hayakutokea ghafla tu kiwendawazimu eti kwa sababu kabila moja lilikuwa likilichukia kabila lingine.
Mauaji ya Rwanda yalikuwa yamepangwa
siku nyingi na kwa ufasaha kabisa na
watawala wa nchi yetu. Ili kulielewa hili na ili mtu asisingizie kuwa mauaji haya yametokana na ukabila inabidi kwa kifupi tuangalie historia ya Rwanda kwa maana
ya makabila haya mawili ya Watutsi na wahutu", Padri Karangwa alieleza.
"Nafikiri kweli ni vizuri tupate historia fupi ya jinsi chuki ilivyojengeka maana mauaji
haya ya Watutsi na Wahutu wenye siasa kali ni ya kinyama yaani binadamu ameweza kuwa mharibifu na mkatili kiasi
hiki", Willy alisema kwa kusikitika.
"Historia ya Rwanda inaonyesha kwamba watu wa kwanza kuishi Rwanda walikuwa wawindaji ambao ni kizazi cha kabila dogo la Watwa. Inasemekana kuwa wakulima, ambao ni Wahutu, ndio waliofuatia na kisha wafugaji ambao ni
Watutsi, ndio walikuwa wa mwisho kufika, na wote waliishi pamoja kila ukoo ukiwana utawala wake wa kichifu. Kusema kuwa Watutsi walikuja kama wavamizi na
kutaka kutawala kwa nguvu makabila
mengine si kweli, kwani wana historia wengi wameupinga usemi huo, ila kitu ambacho kilitokea ni kwamba karibu vizazi ishirini vilivyopita ukoo mmoja wa Kitutsi ulioitwa Nyinginya ulipata sifa
katikati ya Rwanda na kuanzisha utawala wa kifalme ambao ulitawanyika kwenda kusini mwa Rwanda ya sasa.
Lakini historia inaonyesha kwa bunge lao la wakati huo lilikuwa linaitwa 'abini', nalo liliwashirikisha Wahutu na Watutsi pamoja. Na kwa vile utawala wa Wanyinginya ulikuwa na nguvu, machifu
wa Kihutu katikati ya kusini mwa Rwanda walimezwa na kukubalika kama
Wanyinginya. Hapa ndipo swala la
ukabila wa Kihutu na Kitutsi
ulipotambuliwa, si kutokana na ukoo wa Kihutu au Kitutsi bali kwa kutokana na hadhi mtu aliyokuwa nayo. Ukiwa mtawala, hata ukiwa Mhutu uliitwa Mtutsi.
Kama huna mali uliitwa Mhutu, na hivyo hii hali iliashiria kuoana kwingi kati ya Wahutu na Watutsi. Ndiyo sababu hata wewe umeshindwa kututoa tofauti," Padri Karangwa alinena.
"Kama si vitambulisho hivi mara nyingi kweli huwezi kujua Mhutu ni yupi na Mtutsi ni yupi maana vile vile tunazungumza lugha moja, tofauti na nyinyi," Padri Sibomana alidakia.
"Huko ndiko ninakokwenda," Padri
Karangwa alisema na kisha kuendelea,
"Kusema kweli tofauti halisi ambayo
ilibaki ilikuwa kwa wahutu wa kaskazini ambao waliendelea na utawala wao mpaka hapo wakoloni walipofika. Pamoja na kwamba utawala wa Wahutu wa kaskazini haukumezwa na utawala wa ukoo wa Nyiginya, bado wahutu hawa na watutsi waliishi bila matatizo."
"Matatizo yalianza lini? Willy aliuliza.
"Usiwe na haraka, mimi taaluma yangu ni ualimu nakupeleka taratibu uelewe na huko tutafika," Padri Karangwa alimjibu na kisha kuendelea, "Tatizo hasa lilianza wakati wakoloni walipofika Rwanda mwishoni mwa karne ya kumi na tisa.
Wamisionari wa Kijerumani na kisha
askari wa Kijerumani walipofika Rwanda walikuta utawala uliojengeka wa ukoo wa Nyinginya ambao kama nilivyosema ulikuwa ukoo wa Kitutsi. Kama walivyokuwa wakoloni wote walitumia tawala walizozikuta kuwasaidia kutawala.
Hivyo, Wajerumani na kisha Wabelgiji
baada ya kukuta utawala wenye nguvu
ulikuwa wa kitutsi wakaamua kuutumia
huu utawala na kuubadilisha uwe wa
kinyanyasaji ili ile sera yao ya gawa
utawale iweze kufanikiwa. Kwa kusaidiwa
na wakoloni sasa watutsi walifuta nafasi
yoyote waliyokuwa nayo wahutu kabla ya
wakoloni na kuwanyang'anya mali na
madaraka, na hii yote ilichochewa na
wakoloni ili kuwagawa watu wa nchi hii.
Na, kwa vile ilikuwa vigumu
kuwatofautisha wahutu na watutsi kwa
urahisi mnamo mwaka wa 1933-34
vitambulisho vilianzishwa na wakoloni
kwa wananchi wote wa Rwanda
vikiwatambulisha kikabila yaani Wahutu,
Watutsi au Watwa na vitambulisho hivi
hivi ndivyo vilivyotumika katika mauaji
haya na mengine mengi yaliyokwisha
tokea.
"Kwa kutumia vitambulisho hivi basi
maendeleo ya Wahutu na Watwa
yalizimwa kabisa?", Willy aliuliza.
"Ndiyo, yalizimwa na hata shule nafasi
zote zilitolewa kwa Watutsi, kanisani nako
baada ya Omwami kubatizwa kuwa
mkatoliki hata kanisa liliwabagua Wahutu.
Kanisa Katoliki wakati huo ndilo lilikuwa
linamiliki karibu shule zote katika
Rwanda. Hivyo liliwasomesha Watutsi na
kuhakikisha Wahutu hawapati nafasi ya
kusoma ila walibaki na haki ya
kuhubiriwa tu", Padri Karangwa alijibu.
"Kwa hiyo vitambulisho vilikuwa moja ya
mambo yaliyojenga ukabila ndani ya
Rwanda?", Willy aliuliza tena.

ITAENDELEA
 
safi sana kidi kudi. natambua uwepo wako. technician na Willy Gamba tupieni mambo
 
"Ndiyo, kabla ya vitambulisho ilikuwa
vigumu kujuwa huyu ni kabila gani na
vitambulisho kama nilivyosema hapo
mwanzo, vilianzishwa na wakoloni wa
Kibelgiji ili kujenga ukabila ili wautumie
huu ukabila kuwagawa Wanyarwanda kwa
faida yao ili iwe rahisi kuwatawala. Baada
ya kupewa vitambulisho watu wote
waliotambuliwa kama Wahutu
walinyanyaswa na kunyimwa hazi zozote
na elimu na vilevile mali na hata Wahutu
wa Kaskazini ambao walikuwa
wakijitawala wenyewe, wakoloni mnamo
mwaka 1912 walimshinikiza na kumsaidia
Omwami atwae madaraka katika sehemu
hizi. Kutwaa madaraka Kaskazini mwa
Rwanda kwa Watutsi kulikataliwa na
Wahutu wa sehemu hii na mapigano
makali yalitokea yakiongozwa na Mhutu
aitwae Ndugutse. Kwa vile Watutsi
walikuwa wakisaidiana na wakoloni,
Wahutu walishindwa na wakatawaliwa na
Watutsi. Wahutu wengi waliuawa na huo
ndio ukawa mwanza wa uhasama na
chuki kati ya Wahutu wa Kaskazini na
Watutsi. Sasa, ukiangalia mwanzo mwa
hii vita ulikuwa umechochewa na
wakoloni maana, kama nilivyosema hapo
mwanzo, wakoloni walipofika walikuta
makabila haya yakiishi kwa amani", Padri
Karangwa alijibu.
"Ilikuwaje sasa baadaye Wahutu kuja
kutawala Rwanda", Willy aliuliza.
"Baada ya vita kuu vya pili Watutsi
walianza kuomba uhuru kama ilivyokuwa
katika nchi zingine za kiafrika. Wakoloni
wa Kibelgiji kuona hivi, na jinsi Watutsi
walivyokuwa na nguvu na walivyokuwa
wamesoma, wakaingiwa na wasiwasi,
wakajuwa Watutsi wasingewahitaji iwapo
watapata uhuru. Hivyo Wakoloni wa
Kibalgiji wakaamua kuwageuka na
kuwasaidia Wahutu kuwaunga mkono.
Viongozi wa Kihutu walikuwa wachache
na wote walikuwa na kisomo kidogo
walichopata kwa Wamisionari. Hivyo, kwa
vile hawakuwa na nguvu zozote za
kiutawala, walipoanza siasa, siasa yao
ikawa ya kikabila. Hivyo mwaka 1957
chama cha kupigania haki za Wahutu,
kikiongozwa na Gregoire Kayibanda,
kilianzishwa kikiitwa Permehutu. Na
Wakoloni wa Kibelgiji, wakiwa sasa
wamewageuka Watutsi, walianza
kukisaidia chama cha Permehutu, huku
wakikitafutia nafasi ya kuuangusha
utawala wa Watutsi. Nia yao ikiwa
kuwaingia kwenye madaraka Wahutu
ambao hawakuwa na nguvu ili waendelee
kuwategemea kama wangepata uhuru. Hii
ingewasaidia wakoloni kuendeleza
maslahi yao kwani Wahutu
wangewategemea sana kuwalinda dhidi
ya Watutsi waliokuwa na nguvu za kijeshi
na utawala. Kwa hiyo wakoloni ndio
wangeendelea kutawala kiaina kwani
watawala wa Kihutu wangekuwepo kama
mfano tu.
"Je, viongozi wa Kitutsi hawakushituka?",
Willy aliuliza.
"Walianza kushituka lakini mambo
yalitokea kwa ghafla sana wakati
Omwami Rudahigwa alipofariki kiajabu
mjini Bujumbwe mwaka 1959. Jeshi la
Ubelgiji lilisimamia kuangushwa kwa
utawala wa Kitutsi ambao ulikuwa na
umwagaji wa damu vibaya sana. Jeshi la
Ubelgiji lililowasaidia Watutsi kuanzia
mwaka 1912 sasa liliwasaidia Wahutu na
ile chuki ya mwaka 1912 ya Wahutu wa
kaskazini ilijitokeza na inasadikiwa kuwa
Watutsi wapatao elfu kumi waliuawa na
wengi wao wakakimbilia nchi jirani. Hivyo,
Wahutu ndio wakawa watawala chini ya
Kayibanda baada ya kusaidiwa na
wakoloni wa Kibalgiji kuwaweka
madarakani", Padri Karangwa alieleza.
"Kwa nini baada ya hapo vitambulisho
viliendelea, si Wahutu wangeachana
navyo sasa maana vilikuwa
vinawabagua?", Willy alitaka kujua.
"Hapana, mambo sasa yaligeuka; Wahutu
sasa ndio walikuwa watawala. Hivyo,
wakaanza kuwanyanyasa Watutsi. Na
vitambulisho hivyo hivyo vilivyowasaidia
Wahutu kuwatambua Watutsi na
kuwabagua, hata Watutsi wengine
wakabadili vitambulisho vyao na kujiita
Wahutu maana sasa kibao kilikuwa
kimewageukia. Ingawaje Watutsi ndio
waliokuwa wamesoma lakini sasa
walibaguliwa na Wahutu waliokuwa
hawana kisomo maana ndio waliochukua
madaraka serikalini. Elimju yote sasa
ilitolewa kwa wahutu na Watutsi wakabaki
kuangaika na kunyanyaswa. Wengi wao
wakaanza kukimbia. Kwa vile jeshi
asilimia kubwa lilibaki la Kibelgiji hivyo
hakuna kitu ambacho Watutsi
wangefanya. Ingawaje Watutsi
waliokimbia walijaribu kuishambulia
Rwanda kwa kuunda jeshi la msituni
lakini hawakufua dafu. Jeshi zaidi la
kuongeza nguvu liliitwa mara moja toka
Ubelgiji kuja kutokomeza maasi mara
uvamizi wa kitutsi ulipoanza. Kwa hiyo,
katika miaka yote ya sitini hali iliendelea
kuwa ya wasiwasi nchini Rwanda huku
watutsi wakiendelea kuuwawa na
kunyanyaswa",
"Ilikuwaje Habyarimana akafanya
mapinduzi, maana yeye ni Mhutu na
utawala ulikuwa Wakihutu? " Willy aliuliza.
"Swali zuri," Padri Karangwa alijibu na
kisha akaendelea, "Serikali ya Kayibanda
ilianza kuishiwa mbinu na Wabelgiji
wakaanza kuichoka maana sasa ilikuwa
inakuwepo kwa sababu ya ukabila tu.
Mnamo mwaka 1973 Kayibanda akafanya
makosa. Kwa vile Watutsi walikuwa
wamenyimwa nafasi yoyote katika
serikali, kibiashara na sehemu zingine
zozote, sehemu waloyokimbilia ilikuwa ni
ndani ya kanisa. Hivyo, Seminari nyingi
zilijaa Watutsi pamoja na vyuo vikuu
ambavyo viliitwa vyuo vya Watutsi. Kwa
hiyo, mwaka 1973 ili kuwaondoa Watutsi
katika vyombo vyote vya elimu, serikali
ilianza kushambulia seminari, shule na
vyuo vikuu. Kwa vile vyombo vyote vya
elimu vilikuwa mikononi mwa kanisa
katoliki Askofun wa kanisa katoliki
akaanza kupiga makelele na kulaani
serikali. Hata hivyo, huyu Kayibanda kabla
ya kushika madaraka alikuwa katibu wa
Askofu huyu na alikuwa akiwaunga
mkono wahutu. Hapo ndipo Wabelgiji tena
wakapata nafasi na kumtumia Meja
Generali Habyarimana kufanya mapinduzi
na kumtoa rais Kayibanda.Haybarimana
alikuwa Mhutu wa kaskazini na Kayibanda
wa kusini. Utawala wake ulipokelewa kwa
shangwa na Watutsi na Wahutu ukifikiriwa
utakuwa utawala wa haki na usawa lakini
hali haikuwa hivyo, badala ya kuwa na
mgawanyiko wa Watutsi na Wahutu
mambo yalizidi. Sasa kukawa na
upendeleo kwa Wahutu wa kaskazini na
kuwabagua Watutsi na Wahutu wa kati na
kusini. Ndiyo sababu Wahutu wenye siasa
ya wastani waliuawa katika mauaji ya
aprili wakiwamo wanasiasa, wafanyakazi
wa serikali na wafanyabiashara, wote
walikuwa wa kusini. hivyo, kufika wakati
wa sasa sera ya gawa nitawale iliendelea
katika Rwanda."
"Maelezo yako toka mwanzo
yameonyesha kuwa Wahutu na Watutsi
kama watu hawakuwa na tatizo kati yao.
Wamekuwa wakitumiwa na watawala wa
kikoloni na watawala wa kizalendo ambao
wamekuwa wakiwachonganisha ili
wakosane na kwa kukosana kwao wao
wafaidike," Willy alieleza.
"Haswa, ndiyo sababu nimeeleza yote
haya uweze kulielewa tatizo la Rwanda.
Tatizo letu si ukabila, tatizo letu ni
uongozi."
"Sasa nini kilifanya hali ifikie mauaji,
kama ni tatizo la uongozi nchi nyingi za
Kiafrika zina tatizo hilo. Na kama ni
kutumiwa na mataifa ya nje nchi nyingi
zinatumiwa hivyohivyo, mauaji kama
haya ni ya pekee katika dunia, hayana
mfano," Willy alimuuliza Padri Sibomana
ambaye alikuwa akisikiliza kwa muda
mrefu bila kusema kitu.
"Nafikiri hilo swali lako ndilo kila mtu
anajiuliza, maana mauaji haya tuliyo
yashuudia hayana mfano, hata ya Hitler
yalichukua muda mrefu maana vita
vilipiganwa kwa miaka, lakini mauaji haya
yanashinda fikra kwani yalianza dakika
chache tu baada ya kufa Rais na
kusambaa nchi nzima utafikiri moto wa
petroli," Padri Sibomana alisema.
"Wakati wa Habyarimana kulijitokeza
kikundi kidogo cha watu kilichomzunguka
ambacho ndicho kilichokuwa kinafaidika
na utawala wake. Kikundi hiki kilikuwa
cha watu wa kaskazini kutoka sehemu za
Gisenyi na Ruhengeri nacho kilijulikana
kwa jina la Akazu. Kikundi hiki
kilijilimbikizia mali na madaraka, kilijenga
ngome ya kukizunguka na hakuna kikundi
kingine kilichoweza kupenya ngome hiyo.
Hivyo, ili Rais na kikundi hiki waweze
kuendelea kujilimbikizia mali na
madaraka kilihakikisha kuwa hakuna
biashara wala nafasi ya uongozi
inayoweza kupatikana mahali popote bila
kikundi hicho kutoa ruksa. Kikundi hiki
kilikuwa cha Wahutu. Hivyo, uhalali wa
serikali ulipoanza kushitukiwa, kwa vile
kikundi hiki cha Akazu kilikuwa
kimejilimbikizia mali nyingi, kilianza
kuitumia mali hii na ya serikali kujenga
jeshi lake, redio yake, magazeti na
kutumia vyombo hivi kuwachochea
Wahutu, ambao ndio wengi, wawachukie
Watutsi ambao sasa walikuwa wanausaili
uhalali wa serikali hii wakiwemo Wahutu
wapendao amani na usawa ambao
waliitwa Wahutu wenye msimamo wa
wastani. Kufikia mwaka 1990 kulikuwa
hakuna Mtutsi mwenye madaraka katika
serikali, kwa mfano kati ya wakuu wa
mikoa kumi na moja hakukuwa na Mtutsi
hata mmoja; kati ya vyeo 143 vya juu
serikalini hakukuwa na Mtutsi hata
mmoja; kati ya mabalozi wote
walioteuliwa kwenda nje Mtutsi alikuwa
mmoja tu. Na kati ya wabunge sabini, ni
watutsi wawili tu waliokuwa wabunge.
Katika jeshi walihakikisha hakuna Mtutsi
na hasa jeshi la kumlinda Rais lote
lilikuwa na Wahutu na Wahutu hao vilevile
walikuwa ni ama ndugu za Rais au wa
mkewe", Padri Karangwa alieleza.
"Sijaelewa vizuri jinsi hali hii ilivyoashiria
kufikia mauaiji yaliyotokea", Willy alisema
huku akionyesha sasa kuwa makini zaidi.
"Huku ndiko ninakokwenda. Hawa Akazu
pamoja na familia ya Rais walifikia kujiita
miungu wadogo. Walifanya kila
walichotaka. Kuna habari za kuaminika
kuwa kuna Mzungu mmoja rafiki yake
sana na Rais ambaye alikuwa
anawatengenezea fedha kwa maana ya
kuchapisha na wao wanamlipa mazao
kama kahawa kwa bei yake, na mazao
mengine yoyote aliyohitaji; na pia kuna
tetesi kuwa hata bangi ililimwa na watu
hawa na kusambazwa na huyu Mzungu.
Kusema kweli, hawa watu walitajirika
kuzidi kiasi na wakajisahau kabisa. Ili
kubaki katika hali hii kama nilivyosema
mwanzo, ilibidi sasa wachochee ukabila.
Walikuwa wameshafilisika kisiasa, uhali
wa utawala ulikuwa hauna msimamo
tena. Hivyo, kimbilio lilikuwa ni ukabila na
kuhakikisha Wahutu wananufaika na
utawala, na ilikuwa ni rahisi sana
kuwachochea na kufanya lolote ambalo
viongozi wao wa Kihutu walitaka wafanye.
Uchochezi wa Wahutu ulizidi kuanzia
mwaka 1988 baada ya kongamano la
Watutsi lililofanyika Washington D.C
Marekani na kuamua kuiondoa serikali
tawala madarakani. Mkutano huo pia
ulihuhudhuliwa na Wahutu ambao
walikuwa wakipinga mwenendo wa
serikali tawala. Haja ya wakimbizi wa
Kitutsi kurudi nyumbani kwa njia yoyote
ile ndiyo ilikuwa msukumo wa kongamano
hili huku Marekani, kwani Rais alikuwa
akieleza kuwa wakimbizi hawana haki
tena ya kurudi Rwanda kwa kuwa nchi
ilikuwa ndogo mno na isingeweza
kuwapokea tena". Padri Karangwa
alinyamaza kidogo na kuchukua glasi ya maji.
Padri Sibomana akatumia wakati huu
kumkata kauli kidogo. akasema, "Padri
alilisahau swala la wakimbizi wa
Kibanyarwanda Uganda, maana hili lina
uhusiano mkubwa mno na hali hii yote
anayoieleza".
"Bila shaka Padri Sibomana, nilikuwa
bado niendelee huko ila kwanza nilitaka
kuonyesha mshikamano wa Wahutu
ulikuwaje", Padri Karangwa alijibu.
"Sawa Padri, endelea", Padri Sibomana
aliafiki.
"Kama alivyo kumbusha Padri Sibomana,
wakimbizi wengi walijiunga na jeshi la
NRA la Uganda katika miaka ya
themanini. Hao walimsaidia Rais wa sasa
wa Uganda kuchukua madaraka. Kwa
kawaida, wakimbizi mara kwa mara
hujiingiza kiurahisi jeshini kuliko kukaa
bure na hii vile vile huwapa tamaa ya
kutafuta njia za kijeshi kurudi kwao. Na
hivi ndivyo ilivyokuwa kwa wakimbizi wa
Kibanyarwanda waliokuwa Uganda, wengi
wao wakiwa Watutsi na Wahutu
wachache. Makamanda wengi wan NRA
walikuwa wakimbizi wa Kibanyarwanda.
Baada ya kushika madaraka Uganda
ubaguzi ulianza wa wakimbizi wa
Kinyarwanda Uganda. Waliwapinga hasa
waliokuwa wapinzani wa serikali na raia
wa kawaida wa Kiganda waliona hawa
wakimbizi kama wanaokuja
kuwanyang`anya haki zao kwa vile
walikuwa wakishika vyeo vya juu katika
jeshi la NRA ambali sasa ndilo lililokuwa
likitawala Uganda. Ilikuwa ni hali hii na
nia ya kurudi kwao kwa hali yoyote sasa,
iliyo ashiria kuzaliwa kwa RPF. Hivyo
makamanda wa Kinyarwanda walikuwa
NRA sasa waliamia RPF.
"Inasemekana Rais wa Uganda, ili asiwe
na matatizo nyumbani kwake kwa sababu
nilizozisema hapo juu, alikuwa msukumo
mkubwa wa kuisaidia RPF ili wakimbizi
hawa walazimishe kurudi kwao kwa
kutumia nguvu za kijeshi. Kutokana na
hali hii mnamo tarehe 1 oktoba 1990
watoto wa wakimbizi wa Kinyarwanda,
ambao walikuwa wapiganaji wa NRA,
walikusanyika kusini- magharibi mwa
Uganda na siku hiyo ya tarehe moja
wakaivamia Rwanda. Ingawa
hawakufanikiwa, lakini nguvu yao
ilifahamika na kusababisha kiwewe kwa
utawala wa Rwanda, na hapa ndipo
mipigano ya kuwaangamiza Watutsi wote
na Wahutu waliokuwa wanaunga mkono
jitihada za Watutsi ilipoanza kupangwa na
Akazu. Kama nilivyosema hapo mwanzo
ili uchochezi kwa Wahutu dhidi ya Watutsi
upate kufanikiwa, kundi lililokuwa
linafaidika na utawala huu liliunda jeshi
lake lililoitwa Interahamwe. Interahamwe
maana yake ni "wale wanaovamia na
kupigana pamoja". Jeshi hili liliundwa
toka sehemu mbali mbali nchi nzima na
kufundishwa na kikosi maalumu cha Rais
kataka kambi za Gabiro na Bigongwe, na
wote waliochaguliwa walikuwa Wahutu
isipokuwa kamanda wao alikuwa Mtutsi
ambaye baba yake alikuwa amechukua
kitambulisho cha Kihutu. Wengi wa
Interahamwe walikuwa ni vijana ambao
walikuwa hawana kazi, Wakipewa
vinywaji na pesa wakifundishwa
kuwachukia Watutsi na kufanya maasi ya
aina yoyote ile tokea kubaka,
kunyang`anya mpaka kuua. Wizara ya
ulinzi ndiyo iliyotoa silaha na kutoa
sehemu za kufanyia mafunzo ingawa
Interahamwe ilibaki mali ya Akazu na cha
tawala. Vilevile wakimbizi wa Kirundi nao
walichukuliwa na kuingizwa katika jeshi
hili Iterahamwe. Inasemekana kuwa hawa
wakimbizi wa Kirundi, ambao ni Wahutu,
walikuwa wakatili zaidi kuliko hata
wenzao wa Rwanda. Wakuu wa
Interahamwe hawakuishia hapo tu bali
walienda mpaka Goma, Zaire, ambako
nako walichukua askari wa kujiunga na
Interahamwe. Wazaire waliochukuliwa ni
wale wenye asili ya Kihutu lakini Wazaire
wanye asili ya kitutsi kwa jina la
Wabanyamulenge, wao walikataa kwani
wao walikuwa wanaunga mkono harakati
za RPF.
"Hawa Interahamwe walikuwa wengi kiasi
gani?" Willy aliuliza.
"Hata kufikia tarehe 6 aprili na baada ya
kifo cha Rais na mauaji kuanza
inasemekana kwamba kila Mhutu sasa
alikuwa Interahamwe, lakini Interahamwe
waliochukua mafunzo haswa walikuwa
wamefikia kiasi cha elfu kumi."
"Inasemekana yalifanyika mauaji mengi
kwa silaha hafifu kama rungu, panga na
kadhalika.Hii ni kwasababu haya
marungu yaliweza kutengenezwa kienyeji
na kwa urahisi au vipi?" Willy aliuliza.
"Hapana, marungu na mapanga haya
yaliagizwa na kundi la Akazu kutoka
China. marungu haya yalipendekezwa na
Akazu kwani kila yalipotumiwa yalitoa
maumivu ya ajabu kwa adui. Na
inasemekana kuwa watu wengi walitoa
pesa kununua kuuawa na risasi kuliko
kustaimili kifo cha rungu. Marungu haya,
kwa mfano yalianza kuingia Rwanda
tokea januari 1993 yakipakuliwa toka
Mombasa kupitia Nairobi na kuhifadhiwa
kwenye maghala Kigali na Kibungo.
Lakini, pamoja na marungu haya serikali
ya Rwanda, kati ya mwaka 1992 na 1994,
iliagiza silaha kubwa kubwa toka
Ufaransa. Vile vile silaha zingine zilitoka
Ulaya ya mashariki kupitia Zaire.
Ufaransa, hata hivyo, ndiyo iliyokuwa
mfadhili mkubwa wa siliha kwa serikali ya
Rwanda. Inasemekana yule mzungu rafiki
wa Rais na Akazu ndiye alipanga mipango
yote ya uuzaji wa silaha kati ya Ufaransa
na Rwanda. Inasemekanaq kuwa
Mfaransa huyu ambaye pia alikuwa na
uhusiano wa karibu na Ikulu ya Ufaransa
alifikia kuwa mshauri mkuu wa Rais na
ndiye aliyekuwa anamshauri Rais afanye
nini, aseme nini na hata mauaji mengi
inasemekana yalitokana na ushauri wake.
Na kwa vile Rais na watu wake walitaka
kutawala maisha, huyu mtu ambaye
alikuwa akiwapa silaha za hali ya juu ili
RPF isiweze kufurukuta, walimwonja
kama Mungu, hata ndege ya Rais
inasemekana ilitolewa kama zawadi nja
mtu maarufu wa huko Ufaransa kwa
mipango ya huyu mtu," Padri Karangwa
alieleza.
"Kwa hiyo mauaji haya ya Rwanda
yalipangwa, na siyo kwamba yalitokea tu
kwa bahati mbaya, kwa kuchukizwa na
kifo cha Rais?" Willy aliendelea kumdadisi
Padri.
"Bila shaka. Hili kundi la Akazu lilikuwa
na vyombo vya propaganda vingi
ambavyo vilisaidia kuingiza chuki kati ya
Wahutu na Watutsi ili iwe rahisi
kuwatumia Wahutu katika mpango wao
wa kuwamaliza Watutsi ili waweze
kutawala milele. Magazeti kama Kangura
na Stesheni ya Redio ya RTLM vilikuwa
vinamilikiwa na kundi hili. Gazeti hili
lilianzishwa katikati ya mwaka 1990 na
liliungwa mkono na chama tawala
pamoja na Rais na familia yake huku
likiongozwa na rafiki wa Rais. Vilevile
lilikuwa likifadhiliwa na huyo Mfaransa.
Kazi kubwa, kama nilivyo sema hapo
awali , ilikuwa ni kuchochea chuki kati ya
Wahutu na Watutsi, huku radio hiyo na
gazeti hilo vikiwahamasisha Wahutu
wajiweke tayari kuwashambulia na
kuwavamia Watutsi ambao kila wakati
liliwasema kuwa wanataka kurudisha
utawala wao wa kifalme, kila Mhutu
amwue Mtutsi aliye karibu nae. Maneno
makali kama haya ambayo yaliyotokea
kila siku katika vyombo hivi yalikuwa ni
chanzo kikubwa kwa mambo yaliyotokea
kwanzia tarehe 6 Aprili alipouawa Rais,"
Padri Karangwa alieleza.
"Naona saa zimeenda, tumezungumza
sana maana sasa yapata saa tatu na
nusu usiku. Lakini kabla hatujamaliza
Padri hasa nani alimuua Rais?" Willy
aliuliza.
Sura ya Padri alibadilika na kisha
akauliza, "Unataka maoni yangu binafsi?"
"Ndiyo kwani kwa maoni yako kutokana
na ulivyonieleza unaweza kuhisi, na hisia
zako zinaweza kuwa sahihi,willy alijibu.
"Maoni yangu binafsi ni kwamba Rais
aliuawa na Akazu. Ilipoonekana kuwa
Rais alikuwa ameamua kutia sahihi ya
makubaliano ya Arusha, hiki kikundi
chake cha Akazu kikajua huu ndio
utakuwa mwisho wao kufaidika. Hivyo
wakaamua kumuua Rais ili katika
machafuko hayo, waweze kupanga
serikali mpya na kusimika utawala wao
mpya ambao ungewahakikishia kuendelea
kufaidi. Ukweli kuwa watu wake ndio
waliomuua kwa kuogopa utawala wa
kidemokrasia ambao ungefuata baada
kutia saini makubaliano ya Arusha,
ulijitokeza katika gazeti lao la Kangura,
katika gazeti hilo ilitabiriwa kuwa Rais
angeuawa na askari wa jeshi la Rwanda
mnamo mwezi wa machi 1994 kufuatia
kukubali kwake kusaini makubaliano ya
Arusha. Gazeti hilo ambalo lilichapishwa
mnamo mwezi wa Januari 1994
liliendelea kusema kuwa atakayemwua
Rais atakuwa ni Mhutu. Na likasema kuwa
waandishi wa gazeti hilo na rafiki zake na
Rais huyo walimuasa asiweke saini
makubaliano ya Arusha lakini ilionekana
kuwa Rais alikuwa amebanwa sana na
serikali zilizokuwa zikisuluisha mgogoro
kiasi kuwa alikuwa hana msimamo.
Hivyo, gazeti hilo katika toleo hilo,
lilisema kuwa Rais atauawa na hapo
ndipo vitatokea vita na damu nyingi
itamwagika na jeshi la UNAMIR
lisingeweza kufanya kitu. Lilizidi
kumshauri Rais akatae kutia saini
makubaliano hayo vinginevyo kifo chake
hakitaepukika. Na yote yaliyoandikwa
kwenye toleo hilo ndiyo yaliyotokea. Rais
alipokubali tu kutia sahihi makubaliano ya
Arusha basi hawa watu wake wakatimizi
ahadi yao kwani wao ndio walioshika
hatamu zote za serikali kuanzia utawala
mpaka jeshini. Kwa hiyo, baada ya
kusikia amekubali makubaliano ya Arusha
basi walikiamurisha kikosi cha mizinga
cha Kanombe, na ndege ya Rais ilipokuwa
inakaribia kutua makombora matatu
yalipigwa, mawili yakaipiga ndege; Rais
na watu wote waliokuwemo, ikiwa pamoja
na Rais wa Burundi, wakauawa. Akazu
walipanga kuwa baada tu ya Rais kuuawa
basi jeshi lao la Interahamwa lingeanza
mauaji mara moja ya kuakikisha kuwa
Watutsi wote pamoja na yeyote aliyekuwa
anawaunga mkono anauawa. Mbinu hii
ilikuwan ni kutaka RPF kukosa watu wa
kuwaunga mkono ndani ya nchi hiyo na
hivyo kushindwa vita. Lakina ya mungu
mengi, mambo hayakwenda moja kwa
moja kama walivyotarajia," Padri
Karangwa alieleza na kuchukua glasi ya
maji na kunywa.
"Lo maelezo yako yameniingia vizuri na
nafkiri kutokana na ulivyoeleza kweli Rais
aliuawa na mfumo wake mwenyewe wa
kung`ang`ania madaraka kwani hata
wakati alipokuwa amefikia kubadili
mawazo yake, mfumo wake aliokuwa
ameuweka haukumpa nafasi. Hivyo, ilibidi
ummalize ili ubinafsi wa watu wake
waliomzunguka uendelee,"m Willy
alisema huku akiwa kama anajisemea
mwenyewe.
"Watu ka nyinyi basi ndio mnaotakiwa
mueneze habari hizi ili viongozi wengine
wajue kuwa utawala wa mabavu, na
wakung`ang`ania madaraka ili wewe tu
ndio ufaidike una mwisho wake, na
mwisho wake ni mbaya ata
ufanyeje,"Padri Sibomana alidakia.
"Tutajitahidi kueleza ukweli huu," Willy
alijibu.
"Nafikiri itakuwa vizuri kesho kama
ukipata nafasi uje nikuonyeshe mauaji
yalivyo fanyika, uone ukatili usio
kifani,"Padri karangwa alimweleza Willy.
"Nitajitahidi, lakini kwa vile nina shughuli
nyingi inabidi nirudi haraka Arusha. Kama
sitaweza kufika maelezo yako yanatosha.
Na kabla basi sijaondoka nikuulize swali."
"Uliza usiwe na wasiwasi, sisi tumefurahi
kuwa nawe hapa wala hatuoni kama
muda unaenda" Padri Karangwa alijibu.
"Unafikiri baada ya RPF kuchukua
madaraka kutakuwa na maana na
uelewano Rwanda? au niulize tena vingine
baada ya haya mauaji ya kikatili dhidi ya
Watutsi yalivyofanywa na Wahutu,
unafikiri kutakuwa na uelewano kati ya
makabila haya hata kama RPF itaweka
utawala wa demokrasia?"
"Hilo swali gumu lakini nafikiri ndilo swali
lenye maana kubwa sana. Uelewano kwa
sasa utakuwa mgumu. Vidonda vya
mauaji ya ndugu zao Kitutsi bado vibichi
na kama binadamu lazima kutakuwa na
kisasi, kwa hili tusijidanganye. Pili, baada
ya RPF kuchukua madaraka maelfu ya
Wahutu wamekimbia ni wakimbizi huko
Tanzania, Zaire, na nchi zinginezo. Kati
ya hawa waliokimbia na hasa
waliokimbilia Zaire, ni wale Interahamwe
na wanajeshi wa serikali ya zamani. Kwa
vyovyote, hawa nao wataanza
kujikusanya na kuunda tena jeshi la kuja
kuvamia tena Rwanda, na Serikali ya
sasa haita kubali. Hivyo, vita vitaendelea
na itaendelea kwa muda mrefu kama
jumuiya ya kimataifa itaendelea kulipa
kisogo swala hili la Rwanda. Tatu,
miongoni mwa wakimbizi wanaoumia ni
wanawake na watoto, na watoto hawa
taabu watakazozipata huko watakuwa
wanaelezwa kuwa ni sababu ya Watutsi
ambao wamewafukuza nchini mwao na
hivyo kujenga chuki tena. Watoto wa
Kitutsi vilevile watakuwa wanaelezwa
ndugu yako fulani aliuawa na Wahutu; na
kwa vile kila familia iliathirika chuki hii
itazidi kujengeka maradufu. Mimi maoni
yangu ni kwa serikali ya RPF isilipize
kisasi. Wakimbizi wote warudishwe
nyumbani. Wale ambao wanajulikana
kabisa ndio waliusika na kuongoza
mauaji haya ya kikatili, wakamatwe
kokote duniani waliko na wafikishwe
maakamani. Kama dunia hii isivyokuwa
na usawa, wale wote walioongoza mauaji
haya kwa vile wana pesa tayari wapo nchi
za nje wanakula starehe. Wanaohangaika
sasa ni wanawake na watoto; hii si sawa.
Lazima hawa watu wakamatwe hasa
kundi la Akazu, wote wakamatwe
wafikishwe maakamani,"Padri Karangwa
alimalizia huku sasa machozi
yakimlengalenga.
"Kwa kweli, hali ya nchi yetu hii itayumba
kwa muda mrefu. Wote wanachotegemea
sasa ni serikali ya RPF iweze
kuwahamasisha wananchi waweze
kusameheana ili tujenge taifa jipya.
Nakubaliana na Padri Karangwa kuwa ili
tukio kama hili lisitokee tena, wote
waliohusika na kitendo hiki wafikishwe
mbele ya maakama wahukumiwe na
adhabu kali itolewe ili kitu kama hiki
kisitokee tena popote duniani, maana ni
kitu cha kutisha ambacho kinafanya akili
isikubali kuwa binadamu anaweza kuwa
katili na mharibifu namna hii kama
ilivyotutokea sisi hapa. Hapa Willy, dunia
isinyamaze mpaka hapo wote waliohusika
wameadhibiwa," Padri Sibomana alitoa
maoni yake.
Huku akiinuka, Willy alishukuru na
kusema, "kusema kweli sina maneno ya
kuweza kueleza jinsi ninavyo shukuru
kwani naweza kurudi Arusha kesho
maana yote nimepata niliyotaka kujua
kwenu na nimejifunza mengi, asante
sana. Nipatapo nafasi nitawatembelea
tena. Nikishindwa kuja kesho mara
nyingine nitakuja kwa mapumziko.
Asanteni sana, tena sana."
"Nasi tunashukuru sana kwani kuja kwako
kumetufariji kumbe kuwa huko duniani
kuna watu wanaoyajali matatizo yetu
yaliyotupata. Asante sana," Padri
Karangwa alimalizia, kisha
wakamsindikiza Willy mpaka kwenye gari
lake; akaondoka.


ITAENDELEA...
 
UCHU

BIBIANE
Ilikuwa yapata saa nne usiku wakati Willy
Gamba alipokuwa akielekea nyumbani
kwa Col. Rwivanga, akitokea Centre
Christus. Walikuwa wamekubaliana na
Col. Rwivanga kuonana baada tu ya Willy
kutoka kwa Mapadri. Wakati anakaribia
kukata kona kuingia Barabara inayoingia
sehemu ya Kimihurura ili aelekee
nyumbani kwa Col. Rwivanga alipitwa na
gari nyingine aina ya Landrover 110,
lililokuwa likienda kasi sana na kama
asingekuwa makini katika uendeshaji
wangeweza kumgonga maana pamoja na
kuonyesha ishara ya taa kuwa anahitaji
kuingia kushoto lakini gari hilo lilipita kasi
bila kujali ishara ya taa.
"Hawa wanajeshi ndio sababu hupata
ajali mara kwa mara, uendeshaji wao ni
wa ovyo sana", Willy alijisemea moyoni
na kisha akakata kushoto kuelekea
nyumbani kwa Col. Rwivanga.
"Endesha kwa tahadhali Felician,
tungeweza kumgonga yule mtu ikaleta
balaa hata kabla hatujaanza kazi. Kazi
yetu ni kummaliza Willy Gamba na wala si
kugonga magari ya watu ovyo", Xavier
Nkubana alikaripia Felician.
Nkubana na wenzake waliwasili jioni ile
mjini Kigali kwa ndege ya serikali ya
Tanzania ambayo iliwasili na ujumbe wa
Serikali ya Tanzania uliofika kuchunguza
tukio la kulipuliwa kwa ndege ya Tanzania
iliyokuwa inamilikiwa na Kampuni ya
ndege ya Tanzaiar. Ndege hii iliwaleta
maafisa kutoka idara ya usalama wa
anga, mambo ya nje, polisi na waandishi
wa habari. Nkubana na wenzake
walifanyiwa mpango na kupanda ndege
hii kama wafanyabiashara wa
kinyarwanda waishio Tanzania walikuwa
wakirudi nyumbani Rwanda kuangalia hali
ya nchi ilivyo kwa wakati huu ili kama
ikiwezekana waanzishe biashara tena kati
ya Tanzania na Rwanda. Waliingia
Rwanda bila tatizo lolote na kupokelewa
vizuri na viongozi wa serikali ya Rwanda
na kupelekwa kwenye Hoteli ya Des Mills
Collines. Kwa vile walijulikana kama
wafanyabiashara, baada ya kufikishwa
hotelini waliachwa ili waendelee na
mambo yao, na wale maofisa wa serikali
ya Tanzania wakaanza kushugulikiwa na
wenzao kuhusu mambo ya hotelina
mambo mengine ya kiusalama.
Baada ya kuchukuwa vyumba na kuoga.
Nkubana aliondoka na kuelekea
nyumbani kwa Co. Gatabazi na kuwaacha
wenzake wakipumzika, kwani ratiba yao
ya kazi ilikuwa usiku ule ule. Ilikuwa
yapata saa moja hivi Nkubana alipowasili
nyumbani kwa Col. Gatabazi aliyekuwa
akimsubiri.
"Karibu sana", Col. Gatabazi alimkumbatia
Nkubana kwani walikuwa hawajaonana
kwa muda mrefu.
"Asante, naona mambo mazuri", Nkubana
alijibu.
"Mambo mazuri gani haya! Mambo
yatakuwa mazuri baada ya sisi wenyewe
kuchukuwa madaraka ya nchi hii. Kila
siku nasikia uchungu moyoni kuona
'Inyenzi' inazidi kujiimalisha hapa.
Lazima mambo yafanyike haraka kabla
hawajajizatiti sawasawa, karibu ndani",
Col. Gatabazi alijibu huku akiwa
ameushikilia mkono wa Nkubana kisha
akamwongoza kuelekea sebuleni.
"Utakunywa nini?", Col. Gatabazi
alimuuliza.
"Nipe chai kama ipo".
"Tena na mimi sasa hivi nilikuwa
nakunywa chai", Col. Gatabazi alijibu na
kwenda kuchukuwa chupa ya chai na
vikombe viwili vya chai, wakakaa mezani
pale sebuleni.
"Karibu".
"Asante sana". Nkubana alichukua
kikombe chenye chai na kuanza kunywa.
"Ehee, hamkupata tatizo lolote?".
"Wewe unacheza na mipango ya JKS
nini?, atakapokuwa Rais wa Tanzania na
wewe hapa mbona tutakula kuku mpaka
tuchoke! Tumekuja kwa heshima zote na
kupokelewa na 'Inyenzi', na kutupeleka
mpaka hotelini. Wangeweza hata kutulipia
hoteli lakini sisi tumekataa maana
tumekuja kama wafanyabiashara hivyo ni
vizuri kujitegemea", Nkubana alijibu.
"Vijana wako katika hali nzuri?".
"Wako na moto kama nini, maana
wanataka kumaliza kazi usiku huuhuu, na
baada ya hapa tunaelekea Bukavu
tukasaidie kupanga mapambano dhidi ya
'Inyenzi', JKS ametueleza mipango yote
nasi tumeafiki".
"Hiyo safi, lakini kwanza mambo ya hapa.
Huyu Willy Gamba ni mtu hatari kabisa.
Inabidi tumfanyie mkakati mzuri. Siyo mtu
wa kawaida", Col. Gatabazi alieleza lakini
kabla hajajendelea Nkubana alimkata
kauli.
"Yaani huna maana sisi watu watano
ambao ni sawa na jeshi zima la askari
shupavu, bado una wasiwasi? Hivi
umesahau kuwa sisi ni makomandoo,
tupe mipango tujuwe yuko wapi, kazi
ingine tuachie sisi wenyewe", Nkubana
alijigamba.
"Imebidi nikutahadharishe kwanza, msije
mkamwendea kwa pupa. Ni lazima
tupange mipango mathubuti. Inabidi
kwanza kueleza nyendo zake kutokana na
upelelezi niliofanya toka mambo
yaliyotokea juzi usiku", Col. Gatabazi
alijibu.
"Sawa endele", Nkubana alijibu huku
akionyesha kuwa Col. Gatabazi alikuwa
anazidi kupoteza muda kwani anaamini
hakuna mtu. Hata awe wa uwezo wa
aaina gani asingeweza kutamba mbele ya
kikosi chake.
Nkubana alikuwa kati ya askari
waliopatiwa mafunzo ya kijeshi na
kijasusi kwa pamoja. Alikuwa na cheo cha
Meja Jeshini lakini aliingia hata katika
kambi za RPF huko Uganda na
kuchukuwa habari na ndiye ambaye mara
nyingi aliifanya RPF isifanikiwe katika
mashambulizi yake kwani yalijulikana
mapema. Inasemekana mauaji yote
yaliyofanywa kwa watu na wanajeshi
waliokuwa wakitoa habari kwa RPF
yalifanywa na yeye. Alikuwa jasiri na
shupavu lakini uso wake kila siku
utadhani wa padri hata namna yake ya
kusema akiwa na watu wa kawaida. Pia
inasemekana kuwa 'Akazu' walimchagua
kufuatilia maofisa ambao baadaye
waliwafundisha Intarahamwe, na kuwapa
amri kumi ili wazieneze kwa Wahutu.
Mhutu yeyote ambaye asingezifuata na
kuzitekeleza basi auawe hapohapo.
Na hizi amri kumi za Wahutu zilikuwa
kama ifuatavyo.
1. Kila Mhutu ajue kuwa mwanamke wa
Kitutsi kokote aliko, yuko kwa manufaa ya
watutsi. Kwa hiyo mtu yeyote
atakayeoa, kufanya urafiki au kumwajiri
mwanamke wa Kitutsi kama mfanyakazi
wake au mkewe basi Mhutu huyo ni
msaliti, lazima auawe.
2. Kila Mhutu ajue kuwa ni mwanamke wa
Kihutu tu anjayefaa kama mke, kama
rafiki na kama mfanyakazi wake ofisini.
3. Wanawake wote wa Kihutu lazima
wewe imara na wawahamasishe waume
zao, kaka zao na watoto wao wa kiume
kumchukia Mtutsi.
4. Kila Mhutu lazima ajue kuwa Mtutsi
yeyote si mwaminifu katika biashara.
Hivyo, Mhutu anayefanya biashara na
Mtutsi, anayewekeza fedha zake au za
serikali katika kampuni za Kitutsi,
anayekopesha ama kukopa kwa Mtutsi,
anayewasaidia wafanyabiashara wa
Kitutsi ni msaliti, anatakiwa kuuawa.
5. Kazi zote za juu katika siasa, utawala,
uchumi, jeshi na usalama lazima wapewe
Wahutu.
6. Katika sekta ya elimu (walimu, watoto
wa shule na nguo), lazima wengi wawe
Wahutu.
7. Jjeshi la Rwanda liwe kwa Wahutu tu.
Na mwanajeshi haruhusiwi kuona Mtutsi.
8. Wahutu waache kuwaonea huruma
Watutsi, unyama unyama tu dhidi ya
Watutsi.
9. Wahutu popote walipo duniani lazima
wawe na umoja kwa kila njia na wajaribu
kuzima propaganda za Watutsi na
kuungana katika kuwaangamiza Watutsi.
10. Mapinduzi ya kijani ya mwaka 1959
na itikadi za Kihutu lazima zifundishwe
kwa kila Mhutu. Na Mhutu yeyote
anayemwonea Mhutu mwenzake kwa
kueneza itikadi hizi basi huyo Mhutu
auawe, maana ni msaliti.
Kwa kutumia askari wa vikosi
alivyovifundisha Nkubana alihakikisha
kuwa amri hizi zinatekelezwa na
zinachochea chuki ya Wahutu dhidi ya
Watutsi kama alivyoagizwa na Akazu.
Huyu ndiye Nkubana, mtu jasiri,
aliyehitimu katika shule mbalimbali za
kijeshi, kijasusi na kikomandoo
ulimwenguni, lakini mafunzo yake yote
yalikuwa ya dhamira moja tu, ya
kuhakikisha kuwa utawala wa Kihutu
uliokuwa madarakani unaendelea
kutawala milele na milele kwa njia moja
tu kuhakikisha Watutsi wote wanafyekwa
ili wasiwepo tena duniani. Hivyo, kwake
mtu yeyote aliyemuunga mkono Mtutsi
lazima afe na yeyote aliyesaidia Mhutu
basi yeye Nkubana alimsaidia kwa lolote.
Hivyo ndivyo walivyoweza kuelewana na
kundi la Jean kwani lilikuwa upande wa
Akazu. Na habari za Willy Gamba kuwa
alikuwa anajaribu kuharibu mipango ya
Wahutu kurudi madarakani, zilimuudhi
sana na kusikia hasira isiyo kifani dhidi
ya Willy Gamba.
"Lazima usiku huu huu afe", Nkubana
alijishitukia amesema kwa hasira hata
Col. Gatabazi aliyekuwa ameanza kueleza
mipango akashituka. Akashtuka.
"Haya sasa endelea, huyu mtu ameniudhi
sanasana, tayari hukumu yake ya kifo
imeshapita".
Col. Gatabazi ilibidi aanze upya kumpa
mipango ya usiku ule kama walivyokuwa
wamepanga na Jean na JKS.

ITAENDELEA
 
migogoro yao. au Musiba alikuwa kuwadi wa watutsi? sidhani. story inaeleza kwa kiasi kikubwa yaliyotokea uganda
 
Yes....ila iko biased....
Imekaa kitutsi zaidi

ni kweli lkn lengo ni kuresolve. naongea na mhutu mmoja baba mhutu na mama mtutsi, anasema japo waliapa kusameheana mbele ya hadhira, lkn bado wahutu ni daraja la pili na wanafundwa kutokuona
 
  • Thanks
Reactions: RR
Napenda si kidogo...hata ndugu yako naweza kumsahau kabisa nikizama kwenye riwaya

shem, hongera sana unaweza ukanisaidia kunafahamisha kitabu cha riwaya ambacho unakipenda na unataka na mimi nikisome.
 
Back
Top Bottom