Riwaya: UCHU

kidi kudi

JF-Expert Member
May 17, 2011
2,419
1,981
UCHU
By A.E Musiba

SURA YA KWANZA

ARUSHA

Christopher Temu, ambaye Jumapili hii
nyumbani kwake Arusha, alikuwa amefikiwa na
ugeni mkubwa kutoka Umoja wa wanaharakati
wa Afrika (Pan African Movement PAM) kutoka
sehemu mbalimbali za Afrika. Temu alikuwa
mwanachama wa chama hicho.
Hii haikuwa mara ya kwanza kwa watu hawa
kukutana nyumbani kwa Temu kwani watatu
kati yao walikaa nyumbani kwake kwa muda
usiopungua miezi sita. Mnamo mwaka 1992 na
1993 walihudhuria mkutano uliofanyika Arusha
kuvisuruhisha vikundi mbalimbali vilivyokuwa
vikipambana katika mgogoro wa nchi ya
Rwanda, ili mgogoro huo umalizike kwa njia ya
amani
Kikundi hiki cha PAM. ambacho kilikuwa
kinahudhuria kama kikundi cha wapenda amani
wa Afrika. Kilikuwa kinaweka shinikizo kwa kila
upande uliokuwa unahusika na mgogoro huo ili
umalizike kwa amani. PAM ilianzishwa
mwanzoni mwa karne ya 19 ikiwa na lengo la
kupambana na utumwa, ukoloni mkongwe,
ukoloni mamboleo, kupigania haki ya watu weusi
na kuhakikisha kuwa waafrika wanaweza
kupambanua mambo yao wenyewe.
Hivyo, mara hii kikao kilichokuwa kinafanyika
nyumbani kwa Temu kilikuwa cha kutathmini
juhudi zote zilizofanywa kuumaliza mgogoro wa
Rwanda kwa amani, lakini bila mafanikio.
Wakiwa wamekaa kwenye bustani nzuri
iliyokuwa nyuma ya nyumba hii iliyojengwa
kisasa. Ikiwa kwenye barabara ya Njiro kwenye
kilima kidogo ikiuangalia mji wa Arusha kwa
upande wa Kijenge. Mkutano uliendelea mchana
huu wa saa kumi alasiri huku bia aina ya safari
na ndafu, iliyokuwa inachomwa hapohapo
kwenye jiko la mkaa vikiendelea kuwa
viburudisho vya wageni hawa.
"Ndugu zangu. Fundisho kwa Rwanda ni
fundisho kwetu sote, na sisi tukiwa tumejitolea
kuona Afrika inajikomboa na kujitawala kwa
amani ni lazima tukae chini kulitafakari swala
zima la Rwanda tuone makosa yalitokea wapi,
na kwanini hali ilifikia hapo ilipofikia na watu
zaidi ya milioni moja kuteketea bila Afrika wala
dunia kufanya chochote", Jackson Musoke
kutoka Uganda ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa
PAM Kanda ya Afrika Mashariki alieleza.
"Ni kweli kabisa maneno uliyosema, lakini mimi
nafikiri wakati mkutano wa amani ulipokuwa
unaendelea hapa Arusha. Ukweli wa mambo
Rwanda ulikuwa haufahamiki. Na hivyo
maamuzi mengi yaliyofanyika hayakuzingatia
hali halisi ya mambo ilivyokuwa Rwanda wakati
huo. Na ningependa niseme kuwa hata hivi sasa
tunavyokaa hapa hali halisi na ukweli wa
mambo Rwanda bado haujulikani. Ndio maana
Jumuia ya Kimataifa, Umoja wa Mataifa, Umoja
wa Nchi Huru za Afrika bado wanafanya
maamuzi ambayo yanazidi kuleta matatizo
nchini humo, na kuifanya serikali ya sasa
iyumbe katika kutekeleza shughuri zake za
kuleta amani iliyo ya kweli katika nchi hiyo",
Alfred Kimani kutoka Kenya aliongezea.
"Sasa tutafanya nini ili huo ukweli wa mambo
uweze kujulikana na matatizo yaliyo mengi
katika nchi hiyo yaweze kutatuliwa?", Temu
aliuliza.
"Mimi nafikiri tuunde tume ya uchunguzi,
ikafanye uchunguzi, ichimbe chanzo cha
matatizo Rwanda toka kabla ya uhuru mpaka
sasa, na kujaribu kuelewa kabisa tatizo ni nini
na nani anahusika na matatzo kwani mimi
siamini kuwa tatizo hasa ni kabila tu. Miaka
yote tumefikiria hivyo na kujaribu kumaliza
tofauti za kikabila lakini mambo bado yako pale
pale", Abdul Abakutsi toka Nigeria alijibu.
"Vilevile, kama tatizo ni la kikabila, lazima
uchunguzi ufanyike ili ipatikane namna ya
kulitatua tatizo hilo maana hatuwezi kukaa tu na
kusema kwa sababu ni tatizo la kikabila, basi
halina ufumbuzi", Lukaka Makwega kutoka
Zambia aliongeza.
"Tulipokuwa hapa kwa ajili ya mkutano wa
amani, ilionekana kwamba serikali tawala ndiyo
iliyokuwa inachochea ukabila. Swali hapa ni
kwanini serikali inachochea ukabila?. Ni kwa
sababu inataka kubaki madarakani kwa njia ya
gawa utawale au Rais alikuwa na sera za
kikabila yeye mwenyewe au kulikuwa na kitu
kingine kilichokuwa kinachochea hali hii, maana
kinachotisha zaidi ni jinsi mauaji hayo
yalivyotokea. Inaonekana kuwa dakika ishirini tu
baada ya ndege ilikuwa imemchukua Rais
kutunguliwa mauaji yalianza sehemu zote. Hii
inaonyesha mauaji yamepangwa kabla. Ina
maana ilijulikana kuwa Rais atauawa siku hiyo?.
Na kama Rais ndiye aliyepanga mauaji haya, je
alijuwa kuwa atauawa, na kwa hiyo akapanga
akiuawa alipiziwe kisasi?. Na kama alijuwa
atauawa kwani alirudi na ile ndege! Mimi vilevile
naanza kukubaliana na wenzangu kuwa huenda
kuna mambo zaidi yasiyojulikana ambayo
yanaleta matatizo nchini humo. Nami naamini
kuwa mambo hayo yakifichuliwa ufumbuzi wa
matatizo ya ndugu zetu hao utapatikana
haraka", Charles Malisa wa Tanzania alichangia.
"Kuna kitu kingine nilichokisema mwanzoni
ambacho kinatisha sana. Jumuia ya Kimataifa
haikufanya kitu chochote pamoja na kuona jinsi
watu walivyokuwa wakiuawa kinyama. Majeshi
ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa
yalikuwepo. Na Jeshi la Ufaransa lilikuwemo
nchini humo wakati wa mauaji. Nchi kama
Marekani ambazo zimejitokeza kama Polisi wa
dunia, vilevile haikushtuka. Na kila mtu
anakubali kuwa haya yalikuwa mauaji ya kikatili
yaliyopangwa kuliko yale ya Hitler aliyowaua
Wayahudi. Kwanini hali ilibaki hivi! Na nchi za
kiafrika nazo zilikaa tu zikiangalia kabila moja
ndani ya nchi ya kiafrika likiangamizwa kabisa
ili lisiwepo tena. Jamani hapa kuna sababu na
kuna jambo ambalo halieleweki. Uchunguzi ni
kitu cha lazima", Musoke alisisitiza.
"Abakutsi ametoa ushauri wa kuunda tume ya
uchunguzi, sijui ni tume ya watu wa namna gani
anayozungumzia, maana nchi yenyewe ya
Rwanda bado iko katika hali ya kivita bado
wanauana. Serikali ya sasa bado haina uwezo
wa kudhibiti hali ya usalama katika nchi hiyo.
Mambo yote bado shagalabagala. Tukisema
watu kama sisi twende huko kufanya uchunguzi
hakika hatutaambulia kitu kama si kutafuta
kuuawa. Uchunguzi ni muhimu lakini lazima
tufikirie uchunguzi huu ufanywe namna gani",
Makwega alishauri.
Watu wote waliohudhuria kikao hiki
walinyamaza kimya wakitafakari kwa kina
kuhusu uzito wa suala hili nyeti.
"Lete ndafu na utuongeze vinywaji, tunatakari
huku tukilegeza makoo", Temu alimwagiza
mtumishi wake. Bia baridi aina ya Safari
zikaletwa na mabwana hawa wakaendelea
kulegeza makoo na kutafuna ndafu, huku wote
wakitafakari mazungumzo yao kwa makini.
Baada ya kimya kirefu Abakotsi alivunja kimya
hicho. "Huenda ikawa ni lazima tuunde kikosi
cha siri cha upelelezi, kipeleleze kwa sirisiri
halafu kituletee taarifa maana serikali zetu zinao
vijana wanaoweza kufanya upelelezi kama huo
na ukazaa matunda. Kama bwana Makwega
alivyosema, tume ya kawaida haiwezi kuambulia
kitu, kwani mambo ni magumu huko. Nia yetu ni
kupata ufumbuzi na si kupeleka watu
wakauawe. Mnasemaje jamani?".
"Hapo umenena, hiyo ndio njia pekee ya kuweza
kuingia ndani na kupeleleza kiini cha matatizo
hayo. Mimi nakuunga mkono ila tutaiomba
serikali gani itupe msaada huo?. Nyinyi
wenyewe mliona jinsi serikali zetu
zilivyonyamaza na kuacha kana kwamba
hazikujua kuwa mauaji yalikuwa yakifanyika
Rwanda", Makwega alinena.
"Wote tunakubaliana kuwa njia nzuri ya kupata
kiini cha matatizo yaliyosababisha hali ya
Rwanda ikafikia pale ni kutuma kikosi cha
upelelezi?", Musoke aliuliza.
"Ndiyo", wote walijibu kwa pamoja.
"Basi, tuahirishe mkutano kwa leo, tuonane hapa
kesho mchana saa kama hizi ili niweze
kuwasiliana na watu fulani fulani ambao naamini
wanaweza kutusaidia bila kugongana na serikali
zetu", Musoke alisema.
Nyuso za wajumbe, ambazo kwa muda mrefu
zilikuwa zikionyesha wasiwasi, zilikunjuka na
kuonyesha furaha. Ndipo wote walipokumbuka
kuwa Musoke ndiye aliyekuwa Mkuu wa Idara ya
Upelelezi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla
haijavunjika. Hivyo, alijuana na wakuu wa idara
hizi katika Afrika Mashariki, na alisemekana hadi
sasa alikuwa akiombwa ushauri wa kiupelelezi
mara kwa mara.
Baada ya kumaliza vinywaji vyao, wote
waliondoka kuelekea kwenye hoteli zao
walikofikia. Usiku ule Musoke aliporudi hotelini
kwake, pale Mount Meru, aliwapigia simu rafiki
zake, yaani wakurugenzi wa upelelezi wa Kenya,
Uganda na Tanzania. Alizungumza nao
kidiplomasia na kila mmoja alimuomba ushauri
na kumweleza sababu za kufanya hivyo. La
kusikitisha ni kwamba, kwa vile yeye alikuwa
sasa anaongoza chombo ambacho si cha
kiserikali, serikali zisingeweza kumsaidia mtu au
kikundi cha watu, kwa vile ingeshindwa kujieleza
iwapo mkasa wowote wa kiupelelezi ungetokea.
Hilo ndilo lililokuwa jibu la kila mkurugenzi wa
upelelezi. Wote waliomba samahani kwa hilo
kwani walimheshimu sana, lakini ilikuwa nje ya
masharti yao ya kazi, hasa wakati huu ambapo
siasa za nchi hizi ni kutoingilia mambo ya ndani
ya nchi zingine!
Swala hili lilimkasilisha sana Musoke. Wakati
wenzao katika PAM wanapigania Afrika iwe
moja, wengine wanadai eti ni kuingilia mambo
ya ndani ya nchi nyingine!
"Ole wetu Afrika", Musoke alijililia. Ni wakati
alipokaribia kukata tamaa, baada ya kufikiri
sana namna ya kuweza kufanya ndipo
alipomkumbuka Mzee mmoja mstaafu. Alifikiri
huyu angeweza kumtatulia shida yake kwani ni
Mzee aliyeisaidia sana Afrika, hasa wakati wa
ukombozi wa nchi zilizo kusini mwa Afrika. Yeye
alijuana na wapelelezi wengi na maamuzi yake
yalikuwa ya pekee, na ndiye aliyekuwa kitovu
cha ukombozi Kusini mwa Afrika. Mpaka leo
wengi walimjua kwa jina la "Chifu" tu.


ITAENDELEA....
 
Katika vitabu vya musiba hiki ndo sikupata kukisoma wala kusikia uwepo wake,ntakifuatilia.
 
Mkuu kidi kudi kwa kweli hivi vitabu ni muhimu sana kuwa navyo katika maktaba ya nyumbani kuwafundishia wana maadili. mimdau ukifahamu vitabu hivyo vinapouzwa tuletee habari hapa jukwaani.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kidi kudi please shusha episode mfululizo kama alivyokuwa anashusha Willy Gamba 1 kwenye HOFU
 
Mkuu kidi kudi please shusha episode mfululizo kama alivyokuwa anashusha Willy Gamba 1 kwenye HOFU
ombi lako limesikika ntalifanyia kazi kwani hata mi' napenda niwape uhondo mwanzo mwisho
 
Sherehe za Tanzania mkuu sio Zenj tu...! Usichokoze mambo mengine watu watakula "njama" sababu ya "uchu" wao afu raia watabaki na "hofu" lakini ipo siku "kikomo" kitafika na hapo lazima tuunde "kikosi cha kisasi" ingawa itakuwa ni "kufa na kupona"....!!

ha ha ha nimekaa chini mpagani!!!! ila kesho utashangaa kuona Rais wa Tanzania hayupo na hata akiwepo asikague gwaride la heshima wala kupigiwa mizinga!!!

haya mambo huwa hatuyahoji lkn yanaweza kusababisha hofu ambayo inasababishwa na uchu. ikifikia hatua hiyo ipo siku kikosi cha kisasi kitaundwa na hapo tutamwomba Mungu turudi na roho zetu mkuu
 
Back
Top Bottom