Riwaya: UCHU

Riwaya: UCHU

USIKU WA BALAA
IX
Baada ya Bibiane kwenda bafuni kuoga,...
 
Asante Mkuu mareche. Mambo yameanza tupe aya zingine mkuu.
 
USIKU WA BALAA
IX
Baada ya Bibiane kwenda bafuni kuoga,...

pono wacha masihara. ntakutafuna kwa uchu nilionao.

kidi kudi, Willy gamba 1 na mareche, tusaidieni kuondoa kiu hii. ishakuwa too much. halafu bado siku 6 tu kutimiza mwezi tangu muanze kututamanisha, nasi kwa uchu wetu tumeng'ang'ana ka kupe
 
pono wacha masihara. ntakutafuna kwa uchu nilionao.

kidi kudi, Willy gamba 1 na mareche, tusaidieni kuondoa kiu hii. ishakuwa too much. halafu bado siku 6 tu kutimiza mwezi tangu muanze kututamanisha, nasi kwa uchu wetu tumeng'ang'ana ka kupe

Mkuu nisamehe,uchu mbaya sana!
 
Leo Jumamosi tafadhali mwenye kutoa huduma hii
 
Dah...mpaka tumeanza kuchoka sasa...
Hata kama subira yavuta heri hii ni yavuta hasira 😱😱
 
Imepoteza mvuto, hata ikija episode nyingine inakubidi urudie tatu za nyuma ili upate kasi
 

GISENYI
IX


Meja Kasubuga baada ya kuachana na
Willy Gamba, alimtafuta Col. Rwivanga
akitumia simu ya Satellite na kumweleza
kuwa Willy alikuwa amefika salama na
kwamba Willy na Bibiane walipanga
kuelekea Kibumba usiku uleule.
Col. Rwivanga alifurahi kupata simu ya
Meja Kasubuga lakini akakataa Willy na
mwenzake wasiondoke, "Hapana
mwambie Willy na mwenzake wasiondoke
mpaka kesho, kuna mabadiliko ya mipango ya kazi huku, waambie wapumzike tu hakuna tatizo. Meja Tom
Kabalisa atakuja kumuona Willy kesho asubuhi, nami nitafika huko kesho
asubuhi. Hivyo, mambo yote tutapanga
kesho baada ya sisi kufika huko".
"Nimekusoma, nitamweleza kuhusu
taarifa hii afande".
Kasubuga aliona si vyema kumweleza
Willy wakati ule, bali amwache mpaka
baadaye ili apumzike kidogo, lakini muda
si mrefu alikuja askari mmoja na kusema
kuwa wale wageni wa Msalaba Mwekundu
walikuwa wakihitaji chakula. Meja
Kasubuka akaona huo ulikuwa muda
mwafaka vilevile kuwaeleza kuhusu
maagizo kutoka kwa Col. Rwivanga.
Hivyo, akaamua yeye mwenyewe ndiye
awapelekee chakula kitakapokuwa tayari
ili awaeleza kama alivyoagizwa.
"Chakula kilipokuwa tayari Meja Kasubuga aliwapelekea yeye mwenyewe na kuwaeleza kuhusu maagizo aliyopewa kutoka kwa Col. Rwivanga.
"Sawa tumekusikia", Willy alijibu bila
kuonyesha kama alikuwa na maana gani
au alipanga kufanya nini usiku ule.

ITAENDELEA.....
 
KASHESHE


Ilikuwa yapata saa tatu na nusu usiku
wakati Willy na Bibiane walipokuwa
wakijiandaa kuelekea Kibumba, walivalia
sare za Msalaba Mwekundu huku wakiwa
wamebeba silaha mbalimbali ndani ya
mifuko ya nguo na mikoba waliyokuwa
wamebeba yenye alama ya Msalaba
Mwekundu. Walibeba silaha zote za hatari
yakiwemo mabomu ya kisasa
yaliyotolewa na Bibiane.
Willy alikuwa amevaa saa iliyoendana na
yale mabomu akiwa tayari kuyatumia
wakati wowote wakati wa safari yao.
Walipofika kwenye gari na kufungua
mlango ili waweke mikoba yao tayari kwa
safari, mara moja Meja Kasubuga
alijitokeza akitoka gizani akiwa ameshika
bastola yake mkononi akawauliza.
"Mnakwenda wapi Willy, hamkusikia
maagizo ya Col. Rwivanga kwamba
msifanye chochote wala msiende
Kibumba mpaka mtakapowasiliana nae
kesho, haraka ya nini Willy?, mimi
sintaruhusu muondoke".
"Sisi hatuendi Kibumba Meja, tuko hapa
hapa sehemu ya mpakani ili kufanya
utafiti wa hali ya usalama katika maeneo
hayo", Willy alijibu.
"Siamini, huenda mnataka kuvunja amri ili
mvuke mpaka, hilo sintaruhusu na nimeamru kikosi changu hapa kiwazuie
msiondoke hapa hotelini mpaka hiyo
asubuhi, mimi nina amri zangu. Willy naomba tafadhali rudini ndani tusije
tukavunjiana heshima kwa kuwakamata
na kuwaweka chini ya ulinzi mpaka Col.
Rwivanga atakapofika hapa", Meja Kasubuga alionya.
Willy na Bibiane waliangaliana, maana wao walikuwa wameamua kuendelea na
kazi yao usiku ule. Hawakuona sababu ya
kusubiri kesho yake kwani wao walikuwa
na mipango yao tofauti ambayo
haikuwahusu akina Col. Rwivanga. Nia
yao ilikuwa kuwasaka Col. Gatabazi,
Nkubana na Jean. Wakati lengo la Col. Rwivanga na jeshi la RPF ilikuwa kuliangamiza jeshi zima la Akazu.
"Naona kama hutuamini Meja, hakuna tatizo tutarudi ndani tukalale", Willy alijibu
kwa sauti ya unyonge sana.
"Samahani bwana Willy, mimi natii amri niliyopewa na wakubwa wangu wala
msijaribu kunitoroka maana hiyo haiwe.....", kabla hajamaliza kusema
sentensi hiyo, milio ya bunduki aina ya AK
47 ilisikika upande mwingine wa hoteli.
"Tumeingiliwa", Meja Kasubuka alisema
huku akikimbia kuelekea sehemu
ulipotokea mlipuko huku akitoa amri kwa
wanajeshi wake kujitokeza tayari kwa
mapambano dhidi ya wavamizi.

II

Wakati Jean na wenzake wanatoka Goma
kuelekea Kibumba saa moja na nusu ya
jioni ile, Nkubana akiwa na kikosi cha
askari shupavu wenye mafunzo thabiti
wapatao thelathini hivi, walielekea
mpakani kutafuta habari za Willy na
Bibiane, kwani walikuwa na hisia kuwa
lazima wangewatafuta kwa vile Bibiane
aliijua mipango yao yote.
Nia ya Nkubana ilikuwa kupeleleza ili
amuwahi Willy kabla Willy hajawawahi,
maana hii ndio sheria ya mchezo wao
huu. Nkubana na kikosi chake walipofika
mpakani upande wa Zaire ilikuwa yapata
saa mbili na nusu na ndipo walipoelezwa
na vikaragosi wao waliokuwa
wamejipenyeza ndani ya vikosi vya jeshi
la RPF pale Gisenyi kuwa mtu mgeni
aliyekuwa amefikia pale Meridien Hotel
alikuwa ofisa wa Msalaba Mwekundu na
mkewe.
"Huyo mkewe alifananaje?", Nkubana
aliuliza kwa shauku.
"Afande, ni mwanamke mrembo ajabu,
utanisamehe afande lakini kusema kweli
nilipomwangalia yule mwanamke mara
moja nilizini afande, ni mzuri sanasana
chotara yule?", askari alijibu huku
mawazo yake yakiwa yamerudi kwa yule
mwanamke na kuanza kumfikiria huku
mwili wake unasisimka.
Hata Nkubana alipokuwa anakieleza kile
kikosi chake. "Watu wetu wamefika yafaa
tupange mipango madhubuti
tuwashambulie na kuwakamata hai kama
bosi alivyoagiza", yule askari hakusikia
kabisa mpaka Nkubana alipomshitua
tena. Wewe vipi, una tatizo la kifafa",
maana alianza kutetemeka.
"Hapana afande, hapana, nafikiri ukame
umetuathiri sana mawazo".
"Ukame gani, wewe ni mwehu nini?, hetu
tufahamishe huyu jamaa na mkewe
wanakaa upande upi pale hotelini?".
Yule askari alieleza kila kitu kwa ufasaha
jinsi hotelini ilivyo na akawaelekeza
namna ya kuingia mpaka kwenye chumba
walichofikia akina Willy bila kushukiwa na
askari wa RPF waliokuwa wakilinda eneo
hilo.
"Inapofika saa tatu mara nyingi askari
wengi wanaondoka kuelekea mpakani na
wale wanaobaki mara nyingi wanakuwa
upande wa Ziwa. Hivyo itabidi tuvuke
mpaka kabla ya saa tatu na
nitawaonyesha sehemu salama ya kupita,
halafu tutajibanza sehemu mpaka hapo
askari wengi watakapotawanyika
kuelekea kwenye malindo ya usiku halafu
ndipo tutavamia kwani askari
watakaobaki tutaweza kuwamudu", yule
kikaragosi alielekeza.
"Maelezo yako ni safi sana, unafikiri
kutakuwa na askari kama wangapi, yaani
watakaokuwa wamebaki kwa ajili ya
kulinda hoteli?", Nkubana alihoji.
"Hawawezi kuzidi hamsini pamoja na
mimi, maana leo ni zamu yangu kulinda
hoteli", yule askari alieleza.
"Ulikuwa ulinde upande gani?", Nkubana
aliuliza kwa shauku.
"Unande ule niliokueleza kuwa tutapita
halafu tujibanze maana askari anayelinda
sehemu hiyo ni mtu wetu, anajuwa kila
kitu", yule askari alibainisha.
Nkubana alimwangalia kwa makini yule
askari na akaridhika kuwa alisema ukweli
na akamwamini.
"Kwanza nenda na askari wangu mmoja
mkavinjari, halafu mrudi. Kama kila kitu
kiko tayari na mambo shwari ndipo
tutaanza kazi", Nkubana aliwatuma ili
kuwa na uhakika wa mambo na
kuthibitisha maneno ya yule askari
alivyoeleza. Baada ya wale askari wawili
kuondoka. Nkubana alibaki akiwaweka
sawa askari wake tayari kwa
kuishambulia hoteli ya Meridien-Izuda ili
waweze kuwakamata Willy na Bibiane.
Wale askari waliporudi na kumweleza
Nkubana kuwa mambo yalikuwa shwari
na vilevile kupata habari kuwa yule mtu
wa Msalaba Mwekundu na mke wake
walikuwa wamelala baada ya safari ndefu
habari hizi zilimfurahisha sana Nkubana,
akafikiri kuwa angeweza kumteka Willy na
Bibiane wakiwa wamelala na huenda
wakiwa wanafanya mapenzi. Alisikia
hasira inampanda na palepale akakiamru
kikosi chake. "Haya sasa tunakwenda
kazini".

ITANDELEA
 
Back
Top Bottom