Riwaya: UCHU

Riwaya: UCHU

Naomba mmalizie wakukuu niliko mimi ni 6:00 usiku nisilale hivi hivi jamani.

mdau pole sie ndo tunazisubir dk 11 kufikia 00:00 siku mpya. kama vipi tafta za Joram Kiango-Nataka kuua tena. japo haijaisha lkn iko vizuri. utakuwa unaishi kwa kubahitisha kati ya Willy Gamba na Joram Kiango
 
Napenda kuwapongeza wote wanaleta uhondo huu

Na pia kuwalaani wote wenye kejelee na wasefu wa subiraa pale mhusika anapocheleweshaa
 
GISENYI--II

Ilipofika saa nne asubuhi JKS alikuwa
tayari ameshapata kibali kutoka kwa Rais
ili aweze kwenda Uingereza kwa
matibabu. Daktari alikuwa ameiandikia
serikali barua kufanya haraka na kila njia
JKS aondoke siku ileile kwani alihisi
kuendelea kusubiri kungeweza kumletea
shinikizo la damu lenye nguvu kubwa
ambalo huenda wao wasingeweza
kumsaidia kabisa.
Ni barua hii ya Daktari iliyomfanya Rais
akubali kutoa kibali harakaharaka na
kuamru kuwa ifikapo jioni ile JKS awe
ameondoka kwenda Uingereza kwa
matibabu. Hadi saa saba mchana Wizara
ya Afya ilikuwa imefanya mipango yote na
ikawa wamempatia usafiri kuondoka na
ndege ya shirika la ndege la Uingereza
usiku ule.
JKS alikataa kusindikizwa na maofisa wa
serikali kwa kisingizio kuwa atapokelewa
na watoto wake walioko mjini London,
Uingereza ambao alisema watamwangalia
kwa karibu zaidi wakati wa matibabu
yake. Bila watu kujua, alifanya mipango
yake mwenyewe ili usiku uleule aweze
kuunganisha ndege kwenda hadi Geneva,
Uswisi, kitu ambacho alifanikiwa. "Hakika
Willy Gamba hataniweza, nikirudi na
mapesa yote yale, hakika naamini ataiona
dunia na ardhi ya Tanzania chungu", JKS
alijisemea mwenyewe huku mapigo ya
moyo yakimwenda mbio.
.....................................................................
........................................................
III
Wakati Willy na Bibiane wanaondoka
Kigali kuelekea Goma, saa kumi na mbili
asubuhi. Col. Gatabazi na Nkubana
walikuwa wanapokelewa na Col. Marcel
Bazimaziki na kikundi cha wanajeshi wa
jeshi la Zaire kikiongozwa na Meja
Massamba kwenye mpaka wa nchi hizo
za Rwanda na Zaire.
"Pole sana na safari, ulipokaribia kufika
Gisenye natumaini umepita ile njia yetu na
nadhani hukupata shida", Col. Bazimaziki
aliwasalimia kuwapa wageni wake mkono
huku kila kikundi cha askari kikijiweka
sawa kutoa heshima kwa gwaride rasmi
lililoandaliwa kwa ajili ya Col. Gatabazi
ambaye kama walivyokuwa
wameelekezwa kuwa baada ya muda si
mrefu ndiye atakuwa kiongozi wa Rwanda.
"Safari ilikuwa safi kabisa na hizi Benz ni
gari imara sana ha hata kile kinjia
tulichopita hatukupata taabu sana. Asante
kwa kutuma mtu wa kutuongoza, maana
tungeweza kubabaika kufika hapa", Col.
Gatabazi alijibu.
"Jean tulizungumza kwenye simu yetu
aliyoleta hivi karibuni ya Satellite. Sasa
mawasiliano ni mazuri sana kati yake na
sisi. Hata kabla ya kuja kukupokea
tulizungumza nae, alikuwa akielekea
uwanja wa ndege, nae tayari amepanda
ndege na imeondoka Paris tangu saa
kumi na mbili.
"Anatumia ndege yake ile ya Falcon,
atakuwa hapa saa kumi na mbili jioni,
maana atapitia Kinshasa kuonana na
viongozi wa serikali kule, mkutano
utafanyika uwanja wa ndege ili waweke
msimamo, halafu watakuja na Jenerali
Kasongo ili kuangalia hali pamoja na
wewe mwenyewe ukiwepo ili mkiridhika
na hali kazi ianze", Col. Bizimaziki alieleza
na kisha Col. Gatabazi akaelekea kwenye
gwaride ili apokee heshima zake kutoka
kwa kikundi cha wanajeshi wa Zaire.
Baada ya kupokea heshima na kukagua
gwaride. Col. Gatabazi na wenyeji wake
waliamua kuondoka kuelekea Kibumba
kwanza na kisha jioni ndio waelekee
Goma kwenda kuonana na Jean na
maofisa wengine wa juu.
"Acheni hilo gari hapa mpakani, hakuna
matatizo askari wa jeshi la Zaire wapo
wataliangalia maana kule kwenye
makambi lazima kwenda na magari ya
jeshi la Zaire ndio idara na taasisi za
Kimataifa zinazoshughurikia wakimbizi
haziwezi kushituka", Col. Bizimaziki
alieleza.
"Sawa, vipi minong'ono kwamba watu
wetu wanajitayarisha kuishambulia tena
Rwanda huku wakitumia kinga ya
wakimbizi?", Col. Gatabazi aliuliza.
"Usijali kabisa kuhusu hilo, serikali ya
Zaire itakanusha vikali huku sisi tumetia
pamba masikioni. Na kama ujuavyo
kiongozi wa baraza la Akazu, Anatoile
Kabuga. Alitusihi tusisikilize propagada za
vyombo hivi isipokuwa tujiimarishe kijeshi
tayari kwa kuikomboa nchi yetu kutoka
kwa wavamizi wa Kitutsi. Kwanza nilitaka
kusahau, vilevile Bwana Kabuga anakuja
pamoja na Jean ili maamuzi yaweze
kufanyika, ameeleza kuwa mjumbe
mwingine wa Akazu ambaye anaweza
kufika ni John Ngeze ambaye sasa yuko
Afrika Kusini, lakini ameambiwa apande
ndege ya shirika la ndege la Afrika Kusini
inayoingia mjini Kinshasa saa sita na
kama akiwahi atawasubiri pale uwanjani
na wao wakiwahi watamsubiri|.
"Lo, kumbe tutakuwa na mkutano
mkubwa", Col. Gatabazi alinena.
"Wakati umefika kwa wewe Col. Gatabazi
kuchukua nchi kutoka mikononi mwa
wavamizi wa Kitutsi. Siri zote za adui yetu
unazijua, nguvu ya RPF yote unaijua, ya
kijeshi na kisiasa. Sasa nini kitazuia?,
wao hawajui nguvu yetu wanafikiri
tunacheza. Utaenda sasa hivi kujionea
mwenyewe salaha za kisasa, magari,
vifaru. Tuna silaha ambazo zina uwezo
wa kupiga masafa marefu hadi kilomita
mia mbili, na kuna mafunzo makali
yanayoendelea kutoka kwa askari wale
tuliowakodi kutoka Afrika Kusini na wana
kazi kubwa na vijana wetu wana ari
kubwa maana wanajua tusiposhika nchi
tena maisha yao yako hatarini. Ni kweli
kama ulivyosikia wakimbizi tumewazuia
kurudi ili siku tutakapoamua kuanza kazi
ndiyo siku ambayo wakimbizi wote
wanaume tutaandamana nao. Wakirudi
wakati huu uhalali wa kuivamia tena
Rwanda hatutakuwa nao. Hii vurugu ya
wakimbizi kwanza inaficha mambo yote
tunayoyafanya, pili itatupa uhalali na
nguvu za kuvamia. Rafiki zetu wote
watasema. "mlitaka wafanye nini, yaani
mamilioni ya watu yabaki kuwa wakimbizi
nje ya nchi yao", Col. Bazimaziki alieleza,
kisha wakaelekea kwenye kambi.
Walipofika huko kambini walitumia muda
mrefu kuangalia aina mbalimbali za
silaha za kisasa kabisa, mafunzo makali
ya kijeshi, ari ya vijana wa Kihutu, hasa
wale Intarahamwe waliotaka siku hiyohiyo
kwenda kuvamia Inyenzi na kurejesha
madaraka yao. Kutokana na aina ya
silaha walizonazo na mafunzo
waliyokuwa wakipata na moto waliokuwa
nao wa kutaka kupigana na adui. Col.
Gatabazi aliamini kabisa kuwa
wakisaidiwa na Wahutu waliokuwa ndani
ya Rwanda ushindi ulikuwa wao asilimia
mia. Col. Gatabazi alipandwa na mori
akatamani kama vita vingeanza saa ile.
Kisha, wakaondoka kuelekea Goma.
ITAENDELEA
 
daaah haya wakuu. siku ikiisha itanibidi tu nitenge muda nianze upya. maana kwa sasa sikumbuki epsode ya nyuma kwa ukamilifu wake. ila nikisoma kwa mfululizo nitakuwa na kumbukumbu ya muda mrefu
 
asante mkuu kidi kudi nakuombea umalizie kipande kilichobakia, tunakutegemea mkuu pia wenzako Tech, Willy na yule ... wanakuangalia wewe kwenye riwaya hii.
 
GISENYI-IV

Ilikuwa saa kumi na moja na nusu jioni,
Jeana na wenzake walipowasili kwenye
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Goma.
Baada ya kuwasiliwa, walipokelewa na
Col. Gatabazi aliyesindikizwa na askari
wake. Jean aliwasili akiwa pamoja na
kiongozi wa Akazu, Bwana Anatoile
Kabuga, Bwana John Ngeze, ambaye ni
Mjumbe wa Baraza la Akazu, Jenerali
Kasongo, ambaye ni mshauri wa Rais wa
Zaire, Meja Karongo, Mkuu wa kikosi cha
jeshi linalomlinda Rais wa Zaire, Bwa,
George Karikutis, ambaye ni dalali wa
mamluki aliyefanya mipango yote ya
kuwawezesha Jean na wenzake wa Akazu
kupata askari wa kukodi.
Baada ya kuwasili uwanja wa ndege
walipelekwa moja kwa moja hadi Ikulu,
ambako Rais alitoa kibali Jean na
wenzake wafikie kwenye jumba hilo. Ikulu
hii ilikuwa ya kifahari sana. Ili uweze
kuelewa kwa kifupi, vyoo, bafu na vyumba
vya kulala alivyokuwa akitumia Rais
vilijengwa kwa vito vya dhahabu tupu.
Sasa naamini utakuwa umeelewa maana
yake. Karibu na Ikulu hii kulikuwa na
Jumba jingine kubwa ambalo Majemedari
wa jeshi wa ngazi za juu walikuwa
wakifikia. Ndani ya jumba hilo ambalo pia
lilikuwa la kifahari sana, ndimo alipofikia
Col. Gatabazi na wenzake. Kisha,
wakaenda kukaa kwenye sebule ya
kifahari ajabu. Wasichana warembo sana
wapatao kumi hivi walijitokeza kwa ajili
ya kutoa huduma, wakiwa wamevaa
kaputula fupi, matiti nje, yaani asilimia
tisini walikuwa uchi.
"Hivi ndivyo mzee anavyoishi hapa
duniani Jean, hapa panaweza kuwa
peponi ukitaka. Mzee ameyafanya maisha
yake hapa duniani kuwa sehemu ya
peponi. Hivyo, na wewe onja pepo kidogo
ukiwa hapa", Jenerali Kasongo
alimweleza Jean, ambaye wakati huo
alikuwa akitikisa kichwa, maana pamoja
na utajiri wake mkubwa usio kifani
alikuwa hajawahi kukalia viti na meza za
kahawa vilivyotengenezwa kwa dhahabu
tupu, ukiacha sehemu za kukaa ambazo
zilivishwa kwa ngozi ambazo hata yeye
hakuwahi kuziona kabisa duniani.
Huku wale wasichana wakiendelea
kuwahudumia, kila mmoja alikuwa
amejichagulia mrembo wa kumhudumia,
wakileta vinywaji vya kila aina
vilivyokuwa ndani ya jumba hilo. Baada
ya muda mazungumza yalianza.
"Ehe, hebu Nkubana tueleze ilikuwaje hata
huyu Willy Gamba akachafua mipango
yetu namna hii, maana inaniuma sana
kufikia hatua ya Bibiane kuwa mikononi
na mshenzi huyu. Hebu tueleze", Jean
aliuliza kwa hasira.
Huku akitetemeka Nkubana alieleza jinsi
mambo yalivyokuwa huku wote
wakimsikiliza kwa makini sana, kisha
akamalizia kwa kusema, "Tulichukua
tahadhali ya kila aina, lakini nafikiri huyu
Willy Gamba alikuwa na bahati kuliko sisi.
Katika biashara kama hii yetu, wakati
mwingine ni bahati tu inaweza
kukusaidia", Nkubana alijitetea.
"Unafikiri huyu mtu ana mipango gani
sasa?", Jenerali Kasongo aliuliza.
"Sijui, lakini naamini Bibiane anaweza
kumleta huku. Hizi ni hisia zangu, maana
Bibiane atakuwa na uchungu wa kutaka
kulipiza kisasi na siri zetu zote anazijua.
Hivyo, atataka amtumie Willy Gamba
baada ya kuona umahiri wake, alipize
kisasi", Nkubana alijibu.
"Mbona hiyo itakuwa raha, maana nitaua
ndege wawili kwa jiwe moja, Col.
Bazimaziki na Meja Massamba, moja ya
kazi zenu ni kuweka kikosi imara chenye
wapiganaji jasiri cha kuweza kuwakamata
hawa watu wawili, nataka Nkubana
akiongoze kikosi hicho, Nkubana,
ukiweza kuwakamata usiwaue hao ni
halali yangu. Nataka niwafanyie kitu
ambacho wakiwa ahera wasinisahau
milele", Jean aliamru.
"Sawa bosi", Nkubana alijibu hku Col.
Bazimaziki na Meja Massamba wakiitikia
kwa vichwa vyao.
"Ratiba ikoje?", Jean alimuuliza Col.
Gatabazi.
"Nafikiri kwanza twendeni wote
tukaangalie hali ya vikosi vyetu ilivyo,
hasa hapa Kibumba, maana mtapata
mwanga baada ya kuona jinsi
tulivyojiandaa tayari kwa vita. Tumetuma
habari kwa vikosi vyetu vingine vilivyoko
karibu na Bukavu, navyo vijiweke tayari.
Ile simu moja kati ya simu nne za Satellite
ulizoleta tuliwapelekea na sasa
tunawasiliana vizuri sana kati ya hapa na
sehemu zingine zote ambako kuna vikosi
vyetu, lakini kwa kuwa nguvu yetu kubwa
iko hapa nafikiri twende mara moja
Kibumba mkajionee wenyewe, kwani ni
kilomita thelathini tu kutoka hapa Goma.
Halafu tukirudi tutakula chakula hapa na
baadaye kidogo tutaanza mkutano wetu.
Mimi naamini kuwa mkishaona kama
nilivyoona mimi mkutano wa leo
utaruhusu tuanze uvamizi leoleo", Col.
Gatabazi alimalizia.
Wote walikubaliana naye. Kabla
hawajaondoka alichukua simu ya Satellite
akapiga simu Tanzania. Nia yake ilikuwa
kumpata JKS ili ampatie habari za wakati
ule kuhusu nyendo za Willy Gamba kama
alikuwa amezipata kutoka kwenye vyanzo
vyake vya habari. Kwa mshangao alipata
habari kutoka kwa mke wa JKS kuwa
alikuwa ameumwa ghafla na kuondoka
jioni ile Tanzania kuelekea Uingereza kwa
ajili ya matibabu. Na mama huyo alieleza
kuwa mumewe aliondoka kwa ndege ya
shirika la ndege la Uingereza. Mara moja
Jean alihisi kuna tatizo. huku akitingisha
kichwa huku wengine wakimwangalia kwa
kustaajabu, Jean aliwaambia wenzake
wote wamsubiri nje.
Walipotoka nje Jean alipiga simu zingine
tatu zilizomchukua dakika kama kumi hivi
na baada ya kuzipiga aliagua kicheko
kwa sauti mpaka askari aliyekuwa karibu
akashangaa akifikiri kuwa huyu mzungu
alianza kupata uchizi kwa kucheka peke
yake hivi. Jean alipoangalia saa yake
ilikuwa yapata saa moja na nusu jioni,
hivyo aliungana na wenzake wakaondoka
kuelekea Kibumba.
ITAENDELEA
 
GISENYI

V

Mjini Kigali baada ya Willy Gamba na Bibiane kuondoka wakielekea mpakani mwa Zaire, Col. Rwivanga alikwenda moja kwa moja kuonana na Mkuu wa Majeshi mnamo saa mbili, akamweleza yote aliyoyapata kutoka kwa Willy kutokana na maelezo ya msichana mrembo Bibiane.

"Kamanda, hali ni mbaya, tusipofanya haraka tunaweza kuvamiwa," Col. Rwivanga alimuasa Mkuu wa Majeshi.

"Sasa tunafanyaje?" Mkuu wa Majeshi, Jenerali Bunyenyezi, alimuuliza Col. Rwivanga.

"Nafikiri mpigie simu Rais aitishe kikao cha Baraza la Mawaziri na makamanda wa vikosi vyote haraka ili tuliangalie swala hili kwa undani zaidi, maana tukifanya mchezo hawa Interahamwe wanaweza kutuvamia, wamepania sana kufanya hivyo, wanaweza kutuvamia, silaha wanazo tena kali na za kisasa, mafunzo wanapewa na askari wa kukodi, maana wapiganaji wao hawana njia nyingine ila kupigana tu ili warudi. Wamekataza hata wakimbizi halali wanawake kwa watoto wasirudi Rwanda kwa hiari yao ili wawatumie katika uvamizi huu. Kamanda, hii ni hatari na ni hatari sana lazima uamuzi upatikane leo", Col. Rwivanga alishauri.

Jenerali Bunyenyezi alimpigia simu Mkuu wa nchi, nae aliposikia uzito wa swala lenyewe aliamua kuitisha mkutano saa sita na nusu ili watu wote wanaohusika waweze kuwepo maana swala hili lilikuwa na maana ya kuanzisha vita dhidi ya Interahamwe waliokuwa mpakani mwa Zaire na Rwanda.

Baada ya Col. Rwivanga kuona umuhimu wa mkutano huu aliwasiliana na Col. Tom Kabalisa, Kiongozi wa Banyamulenge, Baada tu ya kuwasiliana na Mkuu wa Majeshi kwa njia ya simu ya Satellite ambayo serikali ya Rwanda ilikuwa imewapa kurahisisha mawasiliano na kumweleza ajitayarishe kuja Kigali kwenye mkutano muhimu na kwamba angemtumia helikopta ya kumchukua awe Gisenyi saa nne na watu wasiozidi watatu wa ngazi za juu katika uongozi wao wanaoweza kufanya maamuzi. Kwa miezi mingi Col. Tom Kabalisa alikuwa anasubiri huo muda hivyo alifurahi sana kupata habari hizi.
 
asante m2n shukrani. Upatapo muda usisite kuweka kipande kingine.
 
duh hii kitu lazima niirudie. no way out!! ngoja nivumilie tu
 
Back
Top Bottom