Riwaya: Siri

Riwaya: Siri

Safi sana mkuu mbududa
Tunasuburia muendelezo
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 3 : EPISODE 1
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Saa tisa za alasiri
televisheni ya taifa ilikatisha
kipindi kilichokuwa
kinaendelea na kujiunga na
matangazo ya moja kwa moja
kutoka ikulu jijini Dar es
salaam ambako Rais wa
jamhuri ya muungamo wa
Tanzania alitarajia kutoa
hotuba kwa watanzania.Kama
ilivyokuwa siku
iliyotangulia,simu janja zote
ambazo zilikuwa zimewashwa
muda huo ziliunganishwa na
matangazo yale ya moja kwa
moja kutoka ikulu kwa lengo la
kumuwezesha kila mwananchi
kusikiliza ujumbe ambao Rais
wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania alitaka kuwapa
watanzania.Tayari wanahabari
walikwisha weka sawa kamera
zao na aliyekuwa akisubiriwa
ni Rais
Mlango ulifunguliwa na
Rais Dr Fabian Kelelo
akajitokeza akiwa
ameambatana na Mufti wa
Tanzania Sheikh Seleman
Majid.Muongozaji wa shughuli
ile alitoa maelezo machche na
kumkaribisha Rais aweze
kuzungumza na
watanzania.Rais alianza kwa
kuwatania kidogo waandhishi
wa habari kisha akaendelea
“Ndugu watanzania
wenzangu awali ya yote
ninamrejeshea utukufu Mungu
wetu aliye juu kwa
kutukutanisha tena siku
hii.Poleni sana wale wote
ambao mmeendelea
kuwapoteza wapendwa wenu
kufuatia vurugu zinazoendelea
na wale wote ambao mnauguza
majeraha nawatakiwa uponaji
wa haraka.
Ndugu watanzania,jana
nilizungumza nanyi kwa kirefu
na kuwasisitiza umuhimu wa
kutunza amani
yetu.Ninashukuru sana kwa
wengi kunielewa na taarifa
niliyoipata ni kwamba vurugu
zimepungua na hii ni dalili
njema kwamba tunaelekea
kuzuri.Bado naendelea
kuwasihi ndugu watanzania
tuachane na vurugu hizi
ambazo hazina maslahi kwetu
na hata kwa dini
zetu.Tunachokivuna katika
machafuko haya ni hasara
badala ya faida.Ndugu zetu
wengi wamepoteza
maisha,wengine hawajulikani
walipo,wengine wamepata
ulemavu wa kudumu na
wengine wanaendelea kuuguza
majeraha hospitali.Wengi wetu
tumepoteza mali,nyumba
zimechomwa moto,majengo ya
serikali yamechomwa na
kuharibiwa,miundo mbinu
imeharibiwa,biashara
zimefungwa nk.Ndugu zangu
kwa ujumla tunachovuna
katika machafuko haya ni
hasara kubwa na tuna kazi
kubwa ya kuijenga nchi yetu
baada ya machafuko haya
kumalizika” Rais akanyamaza
kidogo halafu akaendelea
“Jana baada ya kumaliza
kutoa hotuba yangu,nilipigiwa
simu na Mufti wa Tanzania
akaniomba tuonane leo
tuzungumze.Leo kuanzia
asubuhi nilikuwa na kikao
kirefu naye na kubwa
tulilolijadili ni kuhusiana na
vurugu hizi zinazoendelea
nchini namna tutakavyoweza
kuzmaliza.Imekuwa ni desturi
yetu kukaa mezani kila pale
inapojitokeza mikwaruzano
baina ya dini zetu na mara zote
katika mazungumzo ya pamoja
tumekuwa tukimaliza tofauti
na amani ikamalaki.
Tumezungumza mambo
mengi katika kikao hicho
kirefu na tumekubaliana kuwa
na kikao kikubwa
kitakachowahusisha viongozi
wakuu wa dini zote hapa
nchini ili tutafute
muafaka.Naahidi kikao hicho
kitafanyika mapema sana ili
tukae meza moja serikali na
viongozi wa dini tujikwamue
hapa tulipokwama na maisha
yarejee kama kawaida.Kwa
kuwa mambo mengi
nilizungumza jana leo naomba
nimpe nafasi Mufti ana neno la
kuzungumza na watanzania.”
akasema Dr Fabian na
kumkaribisha mufti wa
Tanzania Sheikh Seleman
Majid ambaye alianza kwa dua
kisha akaendelea
“Ndugu zangu,awali ya
yote nami nataka nianze kwa
kuwapa pole nyingi wale wote
ambao wamepoteza ndugu zao
hadi sasa katika machafuko
haya yanayoendelea hapa
nchini kwetu na wale wote
waliopata majeraha mbali
mbali nawaombea wapate
nafuu ya haraka.
Ndugu zangu watanzania
kwa siku kadhaa sasa nchi yetu
imekumbwa na machafuko
makubwa kabisa kuwahi
kutokea hapa
nchini.Machafuko haya
yalianzia katika nchi ya jirani
na yakaenea kama moto wa
nyika hadi kufika hapa
Tanzania.Ndugu zangu dunia
inashangaa nini kimetokea
Tanzania?Katika historia ya
nchi yetu hakujawahi kutokea
machafuko kama haya
yanayoendelea ya waumini wa
dini
kushambuliana.Mheshimiwa
rais alieleza kwa kirefu jana
namna ambavyo watanzania
tumekuwa tukiishi kwa amani
na upendo mkubwa licha ya
tofauti zetu za kidini.Tumeishi
kindugu tukishirikiana katika
mambo mbali mbali
sherehe,misiba n.k.
Hatujawahi kubaguana hata
siku moja kwa imani zetu.Nini
kimetufikisha hapa? Swali hili
ameliuliza Rais jana wakati
anatoa hotuba yake na kwa
swali hilo ndiyo lilinifanya
nitake kuonana na
mheshimiwa Rais ili kwa
pamoja tutafute majawabu ya
nini kimetufikisha hapa.
Tumekuwa na kikao kirefu
na tumezungumza kwa upana
kuhusu jambo
hili.Tumekubaliana kwamba
tuwe na kikao kikubwa cha
viongozi wakuu wote wa dini
ili kwa pamoja tuweze
kuzungumza na kutafuta
muafaka lakini wakati kikao
hicho kikiandaliwa
tumekubaliana kwamba sisi
viongozi wa dini
tuwahamasishe waumini wetu
watulie na waache
vurugu.Suala hili ni pana zaidi
ya tunavyodhani hivyo basi
tunataka kuipa serikali nafasi
iweze kulishughulikia hili
jambo na kupata chanzo
chake.Tunapoendelea
kushambuliana na kuuana
tunaifanya serikali ishindwe
kulishughulikia suala hili hivyo
Rais ametuomba kila kiongozi
wa dini ajitahidi kuhakikisha
anawahamasisha waumini
wake watulie waache vurugu ili
serikali ishughulikie kutafuta
chanzo cha jambo hili.
Ndugu zangu kufuatia
maelekezo hayo ya Rais,niko
hapa kuzungumza na ndugu
zangu wa upande wa waislamu
kuwasihi wasiendelee kushiriki
katika vurugu.Uislamu ni dini
ya amani na hata
tunaposalimiana tunasema
Assalam alaikum maana yake
amani iwe nawe. Dini ya
Uislamu ina mitazamo
inayofanana na dini nyingine
kuhusu suala hili la amani na
usalama.Katika mtazamo wa
Uislamu usalama una maana
ya amani na utulivu katika
jamii. Neno amani kwa ujumla
limezungumziwa katika karibu
aya 140 za Qur'ani ambacho ni
kitabu kitakatifu cha
Mwenyezi Mungu.Usalama na
amani vina mfungamano na
Mwenyezi Mungu Muumba.
Mwenyezi Muumba
mwenyewe amejitaja kuwa ni
"Assalam" kwa maana ya
amani na Mwenye amani na
salama na kwa msingi huo kila
usalama na amani ni mwangwi
wa dhati yake tukufu. Dhati ya
mwanadamu pia daima huwa
katika hali ya kustawi na
kufanya harakati za kuelekea
kwenye amani na utulivu
kamili ambao haupatikani ila
kwa amani na usalama , yaani
dhati ya Mwenyezi Mungu
Muumba.Aya ya 208 ya
Suratul Baqara inasema:
Enyi Mlioamini!
Ingieni katika usalama
nyote. Wala msifuate
nyayo za She'tani; hakika
yeye kwenu ni adui
aliyewazi.
Vilevile aya ya 61 ya Suratul
Anfal inasema:
Na (wapinzani wako)
wakielekea kwenye
amani nawe pia elekea,
na mtegemee Mwenyezi
Mungu. Hakika Yeye
ndiye Mwenye kusikia na
Mwenye kujua.
Neno "Islam" pia
linatokana na msingi wa neno
"Silm", na kwa hakika lina
maana ya kumfuata Mwenyezi
Mungu ambaye Yeye
mwenyewe ndiye amani na
usalama mutlaki na utulivu
kamili.
Neno jingine ni "sulh" ambalo
lina maana na amani,
maelewano na uhusiano
mwema baina ya wanadamu.
Uislamu umetumia neno hilo
ukitaka kuwepo upendo,
kuheshimiana, kujiepusha na
uchokozi na uhasama na
kuchupa mipaka ya wanadamu
wengine.
Ili kuweza kupatikana
amani na uadilifu, Uislamu
umeweka safari yenye awamu
tatu tofauti. Kwanza ni
usalama na amani ya ndani ya
nafsi. Katika awamu hii watu
wote wa jamii wanatakiwa
kutakasa nafsi zao na
kuzipamba kwa taqwa na
uchamungu.Katika awamu hii,
muumini anapaswa
kukomesha mpambano na vita
liyopo baina ya matamanio na
matakwa yake ya kinafsi na
yale ya kiroho, na kufikia
amani na usalama wa ndani ya
nafsi ili pande hizo mbili za
kinafsi na kiroho ziishi pamoja
kwa amani na kumsaidia
mwanadamu kufikia kilele cha
ukamilifu. Ni baada ya hapa
ndipo mwanadamu
anapokuwa tayari kwa ajili ya
harakati ya kijamii na
wanadamu wenzake kuelekea
kwenye malengo aali na ya juu
zaidi. Aya ya 103 ya Suratu Aal
Imran inasema:
“Na shikamaneni na
Kamba ya Mwenyezi
Mungu nyote kwa
pamoja, wala
msifarikiane”
Kwa msingi huo amani ya
ndani ya nafsi ndiyo msingi wa
ukamilifu wa kimaadili na
kiroho kwa ajili ya kuwa na
taathira kubwa zaidi katika
jamii ya Kiislamu.
Awamu ya pili ya amani na
usalama katika Uislamu ni
amani na usalama wa jamii.
Baada ya kuwa tayari kinafsi
kwa kuitakasa na kuisafisha,
mwanadamu huwa
ametengeneza mazingira
mazuri kwa ajili ya muungano
mpana zaidi wa kijamii na
wanadamu wenzake. Hapa
ndipo inapokuja amri ya
Mwenyezi Mungu inayowataka
Waislamu kuwa na umoja na
kujenga udugu. Sehemu moja
ya aya ya kwanza ya Suratul
Anfal inasema:
“Basi mcheni
Mwenyezi Mungu na
msuluhishe mambo baina
yenu, na mtiini Mwenyezi
Mungu na Mtume wake
ikiwa nyinyi ni
waumini.”
Kwa utaratibu huo
Waislamu hutoka katika
minyororo ya ubinafsi,
ubaguzi, dhulma na sifa
nyingine mbaya na kuwa watu
wema na wenye faida kwa
jamii.
Awamu ya tatu ya amani
na usalama inahusiana na
usalama na amani kwa wasio
Waislamu. Miongoni mwa
misingi na kanuni
zinazotawala jamii ya Kiislamu
ni kuishi kwa amani na
usalama na wasio Waislamu.
Kinyume na fikra na dhana za
wanafikra wengi wasio
Waislamu na propaganda
chafu za nchi za Magharibi,
Uislamu ni dini ya amani na
kuishi kwa usalama na wasio
Waislamu. Hii ni pamoja na
kwamba, huwezi kupata hata
aya moja ya Qur'ani
inayowalazimisha watu
kukubali dini hiyo kwa vita na
mabavu. Vita katika Uislamu
vina sura ya kujihami na
kujilinda mbele ya
mashambulizi yanayolenga
jamii ya Waislamu au watu
wengine wanaodhulumiwa au
kwa ajili ya kuzuia uchokozi na
hujuma za adui.
Suala la kuishi kwa amani
na usalama na wasio
Waislamu limesisitizwa sana
katika aya za Qur'ani tukufu na
hadithi, sira na mwenendo wa
Mtume na Aali zake
watoharifu. Suala hili pia
limejengeka juu ya nguzo ya
utukufu wa kiumbe
mwanadamu. Katika mtazamo
wa Uislamu wanadamu wasio
Waislamu wana heshima na
utukufu wa kidhati na
kimaumbile kutokana na
kushirikiana kwao na
Waislamu katika maumbile na
ubinadamu japo
wanatofautiana katika dini na
imani. Uhakika huu
unathibitishwa na sira,
mwenendo na maisha ya
Mtume Muhammad (saw).
Mfano wa wazi wa
mwenendo huo wa amani na
suluhu na wasio Waislamu ni
Mapatano ya Ungwana
yaliyofikiwa baina ya Mtume
(saw) na washirikina wa
Makka kabla ya kutangazwa
dini ya Uislamu, Mapatano ya
Hudaibiyya, mwenendo wa
Mtume Muhammad (saw) na
jinsi alivyokuwa akiamiliana
na tawala na wafalme wa
maeneo mbalimbali kama Iran
na Roma na kutumia njia ya
kutuma barua kwa watawala
na wafalme wa zama hizo
baada ya kuunda dola la
Kiislamu mjini Madina. Kwa
mfano tu Mtume (saw) alisema
katika amri aliyompa Amru
bin Hazm wakati alipomtuma
Yemen kwamba: Kila Myahudi
au Mkristo atakayekubali
Uislamu na kudhihirisha
Uislamu halisi atakuwa
mmoja kati ya waumini,
atakuwa na haki sawa na za
Waislamu na kushirikiana
nao katika vipindi vyote vya
shida na raha. Na kila
mtu atakayeamua kubakia
katika dini yake ya Uyahudi
au Unaswara kamwe
hatalazimishwa kuacha dini
yake, kwa sababu ujumbe wa
dini na risala za Mitume wote
wa Mwenyezi Mungu ni
kuleta amani, uadilifu,
kueneza masuala ya
kiroho,kumkamilisha
mwanadamu na kumfikisah
kwenye saada na ufanisi",
mwisho wa kunukuu.
Kwa msingi huo, katika
mtazamo wa Uislamu suala la
usalama na kuishi kwa amani
na wanadamu wengine wenye
itikadi na imani tofauti, ni
jambo lenye thamani na
umuhimu mkubwa. Hii ni
kutokana na ukweli kwamba,
ni katika mazingira ya amani
na usalama ndipo wanadamu
wanapoweza kuelekea kwenye
ukamilifu wa kimaada na
kiroho, bali hata kuweza
kumjua na kumwabudu
Mwenyezi Mungu.
Hivyo suala la kujenga na
kuimarisha amani na usalama
na vilevile juhudi za kulingania
amani na usalama wa
kimataifa na kuishi pamoja
kwa amani wanadamu wote
kwa msingi wa Tauhidi na
kumpwekesha Mwenyezi
Mungu, uadilifu na usafi wa
nafsi bila ya kujali dini, rangi,
na tofauti zao nyingine ndio
lengo la mwisho la Uislamu na
wafuasi halisi wa dini hiyo. Ni
wazi kuwa, kufuata
mafundisho ya dini hiyo
kunaweza kuwa suluhisho la
kumwondoa mwanadamu
katika kinamasi cha vita,
mapigano na migogoro ya
dunia ya sasa.
Ndugu zangu waislamu
nimejaribu kutoa ufafanuzi
mrefu kidogo kuhusu uislamu
na amani.Dini zote hapa
duniani zinahubiri amani.Hata
akija kiongozi wa dini ya
kikristu ataeleza namna biblia
takatifu inavyosisitiza
amani.Ninawataka ndugu
waislamu na wasio waislamu
mnaonisikiliza hivi sasa kokote
mliko wekeni silaha zenu chini
na turejee kuishi kwa amanai
kama ilivyokuwa hapo
kabla.Tuiachie serikali ilifanyie
uchunguzi jambo hili tujue
nani katufikisha hapa? Nani
waliotufarakanisha hadi ndugu
tukaanza kuuana? Nawasihi
tuweke mbele maslahi ya nchi
yetu.Tuna nchi moja tu na
tazameni kilichotupata baada
ya kuvuruga amani.Tumekosa
hata sehemu ya kukimbilia
kwani sisi kwa miaka mingi
tumekuwa ni kimbilio la wale
wote ambao amani imepotea
katika nchi zao.
Mufti alimaliza hotuba
yake kwa kuendelea
kuwasisitiza waumini wa dini
ya kiislamu na wa dini
nyingine kuachana na vurugu
ili amani irejee.Baada ya
kumaliza kutoa hotuba Mufti
na Dr Fabian wakaenda
kupata chakula cha mchana
pamoja.
WASHINGTON DC –
MAREKANI
Saa tano za asubuhi, Mark
Piller makamu wa Rais wa
Marekani aliwasili katika
nyumba kubwa aliyokuwa
akiishi jenerali Akiki
Rwamirama.Lilikuwa ni jumba
kubwa la kifahari lililokuwa na
viwanja vya michezo mbali
mbali kama vile mpira wa
kikapu,mpira wa wavu na
tenisi.Kulikuwa na miti mingi
kulizunguka jumba hilo na
kulifanya kuwa na utulivu
mkubwa,ni sauti za ndege
mbali mbali ndizo zilisikika.
Jenerali Akiki hakuwa na
taarifa kama Mark Piller
angekwenda
kumtembelea.Alikuwa ndani
ya sebule kubwa akitazama
runinga akifuatilia taarifa za
habari za vyombo mbali mbali
vya habari duniani na kubwa
alilokuwa analifuatilia ni
taarifa za kuhusiana na kile
kilichokuwa kinaendelea
Afrika mashariki hususan
nchini Uganda.
Mlango mkubwa wa
sebuleni ukagongwa na mmoja
wa walinzi wake akaenda
kuufungua akakutana na
walinzi wa makamu wa
Rais.Nje tayari msafara wa
makamu wa Rais ulikwisha
wasili na alikwisha shuka
akipiga hatua kuelekea
ndani.Jenerali Akiki
alipojulishwa kuwa ni makamu
wa Rais amefika akainuka
haraka na kwenda kumpokea
“Mheshimiwa Rais habari
yako” akasema Mark Piller
“Mark niite Akiki
inatosha.Hayo mambo ya Rais
yamekwisha pita.Mimi si Rais
tena wa Uganda” akasema
Jenerali Akiki
“Jenerali Akiki sisi
tunaendelea kukutambua
kama Rais halali wa Uganda
hivyo tutaendelea kukupa
heshima yako ya Rais”
akasema Mark
“Nashukuru sana
Mark.Karibu”
“Ahsante jenerali
Akiki.Tunaweza kutembea
tafadhali” akasema Mark na
Jenerali Akiki akamuongoza
wakaelekea katika uwanja wa
gofu.
“Jenerali Akiki vipi maisha
yako yanakwendaje
hapa?Unayafurahia?akauliza
Mark Piller
“Maisha yanakwenda
vizuri sana mheshimiwa
makamu wa Rais.
Ninayafurahia maisha.Tayari
akili yangu imekwisha anza
kuzoea maisha haya.Kwa
ujumla hakuna tatizo
lolote.Ninashukuru sana kwa
namna
mnavyonihudumia.Ninapata
kila ninachokihitaji”akasema
Jenerali Akiki
“Ninafurahi kusikia hivyo
mheshimiwa Rais.Ninakuahidi
utaishi maisha mazuri kama
uko peponi.Utapata kila
unachokihitaji na utayasahau
maisha yako yaliyopita”
akasema Mark Piller
“Ahsante
Mark.Sikutegemea kama
baada ya kuondolewa
madarakani ningekuwa na
maisha mazuri kama
haya.Washenzi wale
wametaifisha mali zangu zote
na bila ninyi ningekuwa
masikini wa kutupwa”
akasema Jenerali Akiki
“Niliwahi kukwambia
Jenerali Akiki kwamba
yanapofanyika mapinduzi rais
aliyepinduliwa mara nyingi
lengo huwa ni kumuua lakini
kama akinusurika akakimbia
basi mali zake zote ndani na
nje ya nchi hutaifishwa na
serikali iliyochukua
madaraka.Lakini hilo
lisikuumize kichwa kwa sasa
wewe ni tajiri na utakuwa na
mali mara mbili zaidi ya zile
ulizokuwa nazo ulipokuwa
madarakani.Hata kama
ukitaka familia basi unao
uwezo wa kuanzisha familia
tena kubwa.Kila kitu
kinawezekana mheshimiwa
Akiki”akasema Mark Piller
“Mambo yanaendeleaje
Afrika Mashariki ?akauliza
Jenerali Akiki
“Mambo yanakwenda
vizuri mheshimiwa Akiki.Meli
zetu kubwa za mafuta
zimepanga foleni katika
bandari ya Tanga zikipakia
mafuta.Kwa ujumla kila kitu
kinakwenda vyema”
“Safi sana.Nataka
ikiwezekana mchukue mafuta
yote yaliyopo Uganda
muyalete huku kwa watu
ambao wana shukrani na
utu.Nimeijenga Uganda lakini
shukrani zake ni hizi.Mark
kama upo uwezekano wa
kuongeza zaidi uchukuaji wa
mafuta fanyeni hivyo
tafadhali”akasema Jenerali
Akiki
“Jenerali Akiki hilo ndilo
lililonileta hapa kwako.Jana
nilikuwa na mazungumzo
marefu na Rais kuhusiana na
mpango huu
unaoendelea.Katika
mazungumzo yetu
tumekubaliana kwamba
tutanue zaidi operesheni
hii.Unajua Afrika Mashariki ni
tajiri sana.Tunataka tusiishie
kwenye mafuta peke tunataka
twende mbali zaidi tuingie
hadi katika rasilimali nyingine
kama vile madini.Nchi kama
Tanzania imebarikiwa madini
ya kila aina.Nchi kama
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo nayo vile vile ina
madini ya thamani.Tanzania
kwa mfano ina madini ya
dhahabu,almasi,na mengine
mengi bila kusahau madini ya
Tanzanite ambayo
hayapatikani sehemu nyingine
yoyote duniani zaidi ya
Tanzania pekee.Tunataka
operesheni yetu sambamba na
mafuta iende pia katika
maeneo hayo
niliyoyataja.Nimekuja hapa
kwako kupata ushauri
unadhani nini tufanye kutanua
operesheni hii Afrika
mashariki? Akauliza Mark
Piller
“Mheshimiwa makamu wa
Rais tena imekuwa vizuri
umefika.Muda mfupi kabla
hujafika hapa nilikuwa
natazama kile kinachoendelea
Afrika mashariki.Leo kuna
jambo limetokea nchini
Tanzania”
“Kumetokea nini Tanzania
?akauliza Mark Piller
“Rais wa Tanzania
amekutana na Sheikh mkuu
wa Tanzania na wamekuwa na
kikao kirefu wakizungumzia
vurugu zinazoendelea.Kikao
hicho kinaonekana kuwa na
mwelekeo mzuri wa kumaliza
vurugu hizo
zinazoendelea.Nimezisikiliza
hotuba aliyoitoa Mufti na kwa
kiasi kikubwa inaweza
kuwashawishi waumini
kuachana na vurugu
zinazoendelea.Kwa kawaida
waumini wa dini ni watiifu
mno kwa viongozi wao hivyo
kama wameambiwa na
kiongozi wao waache vurugu
basi watafanya
hivyo.Watanzania ni wepesi
sana wa kumaliza mambo kwa
amani na kwa mujibu wa
taarifa ambayo imetolewa
leo,tayari vurugu zimeanza
kupungua nchini Tanzania na
hii inatokana na hotuba ya
jana ya Rais Dr Fabian”
akanyamaza akamtazama
Mark Piller
“Mpango huu uliojadiliana
na Rais wako ni mpango mzuri
sana na wenye manufaa kwa
Marekani lakini ili mpango
huo ufanikiwe tunaihitaji mno
Tanzania.Vurugu lazima
ziendelee nchini Tanzania ili
majeshi ya Marekani
yaendelee kukaa nchini humo
na kama ikiwezekana basi
wanajeshi waongezezwe
zaidi.Tanzania haitakiwi ipate
amani kwani ikiwa shwari
hakutakuwa na ulazima wa
vikosi vya Marekani kuendelea
kuwepo na hivyo hatutaweza
tena kuendelea na uchukuaji
wa mafuta na rasilimali
nyingine” akasema Jenerali
Akiki
“Nini unashauri kifanyike
Jenerali Akiki? Tunategemea
sana ushauri wako kwa kuwa
wewe unalifahamu vyema eneo
la Afrika mashariki.Ushauri
wowote utakaoutoa
tutauzingatia” akasema Mark
Piller
“Kunatakiwa kufanyike
kitu cha haraka sana
kuhakikisha hali inaendelea
kuwa tete nchini Tanzania ili
vikosi vya Marekani viendelee
kukaa huko kwa muda mrefu
zaidi na kama ikiwezekana
viongezwe vikosi vingine”
akasema Jenerali Akiki
“Nini basi unashauri
kifanyike kwa haraka?Mimi na
mheshimiwa Rais tulifikiria
kuanzisha kikundi cha waasi
ambacho tutakiwezesha kwa
silaha na zana nyingine za
kijeshi ambacho kitaendesha
mapigano na serikali za Afrika
mashariki ili tupate nafasi ya
kuongeza wanajeshi zaidi
katika eneo la Afrika
Mashariki.Unaonaje kuhusu
mpango huo?akauliza Mark
Piller
“Huo ni mpango mzuri
lakini si muafaka kwa
sasa.Kuanzisha kikundi cha
waasi ni mpango wa muda
mrefu.Si jambo jepesi
kuanzisha uasi hasa katika
nchi kama Tanzania.Kwa nchi
ya jamhuri ya kidemo krasia ya
Congo kule hakuna shida
kwani wamekwisha zoea
mambo kama hayo lakini kwa
sasa tunalenga zaidi Tanzania
hivyo wazo la kuanzisha
kikundi hicho cha uasi
tuliweke pembeni
tutalishughulikia
taratibu”akasema Jenerali
Akiki
“Vipi kuhusu kuwatumia
IS kufanya mashambulio mbali
mbali ya kigaidi na kuua
watu?akauliza Mark Piller
“Hilo nalo ni wazo zuri
lakini bado si mpango mzuri
tunaouhitaji kwa
sasa.Tunatakiwa kufanya kitu
cha haraka”
“Nini basi unashauri
kifanyike kwa haraka jenerali
Akiki?akauliza Mark Piller na
Jenerali akiki akainamisha
kichwa akafikiri kisha akasema
“Hapa Marekani mnao
wanasayansi wa hali ya
juu.Nataka muwatumie
wataalamu hao kutengeneza
kirusi ambacho kitakuwa ni
hatari na ambacho kinaweza
kusababisha maangamizi
makubwa kitakachokwenda
kusambazwa nchini Tanzania”
“Kirusi? Akauliza Mark
Piller
“Ndiyo Mark.Mnatakiwa
kutengeneza kirusi ambacho
kinaweza kuwa hatari zaidi na
kwenda kukisambaza nchini
Tanzania ambacho kitasambaa
kwa haraka zaidi na
kusababisha vifo vya watu
wengi.Baada ya hali kuwa
mbaya Marekani itaongeza
wanajeshi Tanzania kwa lengo
la kwenda kutoa msaada wa
kibinadamu.Faida za mpango
huu ni kwamba vikosi vya
Marekani vitaongezwa na
kukaa kwa muda mrefu Afrika
mashariki na kuendelea
kuchukua mafuta na rasilimali
nyingine kama madini”
akasema Jenerali Akiki
“Jenerali Akiki wazo lako
ni zuri lakini linaonekana ni la
hatari kubwa.Wasi wasi wangu
ni vipi kama kirusi hicho
kitaweza kuvuka katika
mipaka ya Tanzania na
kusambaa sehemu mbali mbali
duniani na hatimaye kikafika
hadi Marekani? Tunaweza
kuwa tumetengeneza silaha
ambayo inakuja kutuua sisi
wenyewe.Wanajeshi wetu
walioko Tanzania wanaweza
wakaambukizwa ugonjwa huo
wakafa au wakaja kusambaza
virusi hivyo huku Marekani”
“Mark Piller hiyo ndiyo
njia pekee na ya haraka
ambayo mnaweza mkaitumia
ili vikosi vya Marekani
viendelee kukaa Afrika
Mashariki na hasa
Tanzania.Wanasayansi wenu
watakapotengeneza kirusi
hicho hatari watatengeneza pia
na kinga yake na wanajeshi
watakaokuwa Tanzania na
wale watakaopelekwa huko
watapata kinga hiyo hivyo wao
hawatadhurika na hicho
kirusi” akasema Jenerali
Akiki.Mark Piller alishindwa
ajibu nini wakabaki
wamesimama wakitazama
farasi kila mmoja akiwaza lake.
“Unalionaje wazo hilo
Mark?akauliza Jenerali Akiki
“Jenerali Akiki
ninashindwa kukupa jibu la
haraka haraka kwani mpango
huu ni mkubwa na wa hatari
sana”
“Nini hofu yako
Mark?akauliza Jenerali Akiki
“Hofu yangu ni kwamba
tunaweza kutengeneza kirusi
hicho hatari halafu kikageuka
na kuwa kisu cha
kutuangamiza sisi
wenyewe.Kitu kama kirusi
kinaweza kusambaa kwa
haraka sana na kufika hadi
Marekani kitu ambacho
hatutaki kitokee na ndiyo
maana umeona Marekani
hatupigani vita nyumbani
tunamfuata adui huko huko
aliko.Tunataka raia wetu wawe
salama siku zote ndiyo maana
ninahofu kwamba tunaweza
kutengeneza kirusi na
kikasambaa na kufika hadi
Marekani na kuua watu wetu”
akasema Mark Piller
“Hakuna haja ya kuwa na
hofu Mark.Nimesema
wanasayansi watengeneze
kirusi na kinga yake na kila
juhudi lazima zifanyike
kuhakikisha kwamba kirusi
hicho hakivuki nje ya mipaka
ya Tanzania.Mzilenge nchi za
Tanzania,Uganda na jamhuri
ya kidemokrasia ya
Congo.Tena mkitaka
kufanikiwa zaidi tengenezeni
kirusi ambacho kitasambaa
kwa njia ya hewa ili kiweze
kusambaa kwa haraka
zaidi.Nakuhakikishia Mark
kwamba hii ndiyo njia pekee
nyepesi ya kuweza kuongeza
vikosi Afrika mashariki na
kuendelea kuchota
rasilimali.Njia nyingine kama
makundi ya waasi hizo zitakuja
baadae” akasema Jenerali
akiki
“Jenerali Akiki naomba
nilichukue suala hili na
kwenda kujadiliana na
wenzangu tuone namna
tutakavyoweza kulitekeleza
lakini ni suala zuri na ahsante
sana kwa wazo hili zuri”
akasema Mark Pilller
“Mark muda unakwenda
kwa kasi na taratibu amani
imeanza kurejea Tanzania na
kama Tanzania ikiwa na amani
basi hata Uganda nako
kutakuwa na amani.Hampaswi
kuacha jambo hili likatokea
.Wakati wakiendelea na
mikutano yao ya kutafuta
amani wanatakiwa wapigwe
tena pigo lingine kabla
majeraha yao hayajapona”
akasema Jenerali Akiki
“Ahsante sana jenerali
Akiki tutalizingatia
hilo.Ninakwenda kuzungumza
na wenzangu halafu nitakupa
mrejesho nini tumekubaliana.
RIYADH – SAUDI ARABIA
Kiza kimeanza kutanda
katika anga la jiji la
Riyadh.Katika makazi ya
Habiba Jawad idadi ya watu
waliofika kuhudhuria msiba
wa mwanae Najma aliyezikwa
mchana wa siku hiyo baada ya
kujiua kwa kujipiga risasi
ilikuwa kubwa.Ulikuwa ni
msiba mkubwa kwa Habiba
Jawad ambaye huyu alikuwa ni
mtoto wake wa pili kufariki
baada ya Edger Kaka.
Wakati watu wakiendelea
na maombolezo Habiba Jawad
aliyekuwa katika mojawapo ya
nyumba zilizopo katika makazi
yake akiwa na akina mama
waliofika kumfariji, simu yake
ikaita akaitoa haraka haraka
kutazama mpigaji kisha
akaikata ile simu.Taratibu
akainuka na kuaga anakwenda
maliwato.Hakutaka mtu yeote
amsindikize.Alitoka ndani ya
ile nyumba akafuata ujia
kuelekea katika nyumba yake
na moja kwa moja akaenda
katika ofisi yake akawasha
runinga kubwa na akaonekana
David Walker.
“Habari yako Habiba”
akasema David Walker
“Nzuri David habari yako”
“Habiba unaonekana
hauko sawa leo.Kuna tatizo
lolote?akauliza David
“Nina msiba
David.Mwanangu amefariki
jana na leo tumemzika”
“Pole sana
Habiba.Hukutujulisha kama
una msiba”
“Usijali David.Nini
kinaendelea huko? Akauliza
Habiba
“Habiba kuna jambo
ambalo limejitokeza na
tunahitaji msaada wako”
“Sema David nini
mnahitaji?akauliza Habiba
“Tumekuwa tunafuatilia
kwa karibu sana kile
kinachoendelea Tanzania na
siku ya leo Rais wa Tanzania
amekutana na kiongozi wa dini
na kubwa walilolizungumza ni
kuhusiana na vurugu
zinazoendelea katika ukanda
huo wa Afrika
mashariki.Mazungumzo hayo
ya leo kati ya rais na kiongozi
huyo yanaonekana kwa na
mwelekeo wa kumaliza vurugu
zile za kidini zinazoendelea
Afrika Mashariki.Endapo
vuruguzile zitamalizika basi
hakutakuwa na ulazima wa
vikosi vyetu kuendelea kuwepo
Afrika mashariki na lengo letu
ni kuendelea kukaa hapo kwa
muda mrefu na hata kuongeza
wanajeshi zaidi.Kwa hiyo
tumeamua kufanya kitu cha
haraka ambacho
kitatuwezesha kupeleka vikosi
zaidi vya jeshi na kukaa Afrika
mashariki kwa muda mrefu
zaidi” akasema David Walker
“Mmekuja na mpango
gani? Habiba akauliza
“Tunataka kutengeneza
kirusi ambacho kitafanya
maangamizi makubwa
ambacho kitakuwa hatari
kuzidi kirusi cha
Ebola.Tutakwenda
kukisambaza kirusi hicho
Tanzania na baada ya hali
kuwa mbaya tutatuma vikosi
zaidi vya jeshi kwenda huko
kwa lengo la kutoa msaada
lakini papo hapo operesheni
zetu zikiendelea kama
kawaida”
“David hili la kusambaza
kirusi huoni kama ni jambo la
hatari?Ni vipi kama kirusi
hicho kitavuka mipaka na
kusambaa sehemu nyingine
duniani?Mnao wanajeshi wenu
kule ni vipi kama wakipata
virusi hivyo? Akauliza Habiba
“Hilo tayari tumekwisha
lijadili kwa kirefu
sana.Mwanasayansi
anayeandaa kirusi hicho
tumempa maelekezo ya
kuhakikisha kwamba
atakapokamilisha kutengeneza
kirusi hicho aandae na kinga
yake kwa ajili ya wanajeshi
wetu na tahadhari endapo
kirusi hicho kitavuka mipaka
ya Afrika Mashariki na kuenea
sehemu nyingine duniani.Hilo
halina tatizo kabisa Habiba”
“Nini natakiwa kufanya
kwa upande wangu?akauliza
Habiba ambaye hakuonekana
kutaka maongezi marefu
“Kwa upande wako
tunataka utusaidie kupata mtu
ambaye atapeleka kirusi hicho
Tanzania.Tunataka mtu
kutoka kundi la IS”akasema
David
“David kwa nini lazima
awe ni mtu kutoka IS?akauliza
Habiba
“Habiba hili ni shambulio
la kibaolojia hivyo basi mtu
huyo hapaswi kuwa
mmarekani.Tunataka
kumtuma mtu wa kundi la IS
ili hata kama akigundulika basi
ijulikane kuwa ni kundi la IS
ndio waliofanya shambulio
hilo.Nataka ufanye
makubaliano na kundi la IS
wape fedha za kutosha waweze
kutupatia huyo mtu ambaye
anatakiwa hapa Marekani
haraka sana ili aanze
kuandaliwa.Mtu huyo
atawekewa kwanza kinga ya
kumkinga dhidi ya kirusi hicho
halafu atapandikizwa kirusi
hicho ambacho atakwenda
kukisambaza Tanzania”
akasema David Walker
“Lini huyo mtu
anahitajika?akauliza Habiba
“Tunamuhitaji haraka
iwezekanavyo.Tunataka kabla
ya amani haijarejea Tanzania
basi tuwapige na hicho
kirusi.Hatutaki kuwapa nafasi
ya kupumua.Namuhitaji huyo
mtu haraka sana.Fanya kila
uwezalo mtu huyo aweze
kupatikana haraka sana”
akasema David
“Sawa David nitajitahidi”
“Ahsante sana Habiba na
pole sana kwa tatizo hili
kubwa.Kuna chochote
tunaweza kusaidia?
“Ahsante
David.Tutawasiliana pale
nitakapokuwa nimempata
huyo mtu” akasema Habiba na
kuzima ile runinga
“Mauaji yanayoendelea
hivi sasa nchini Tanzania bado
hayatoshi na wanataka
kusambaza tena virusi na
kuendelea kuua watu.Yote hii
ni kwa sababu ya kutaka
kuchukua rasilimali ambazo
Mungu amewajalia watu wa
Afrika Mashariki.Lazima
nitafute namna ya kufanya ili
niweze kuzuia mpango huu
usifanikiwe.Ningeweza
kumpigia simu Mathew
Mulumbi lakini sifahamu
mahala alipo hivi sasa.Hata
hivyo lazima nifanye kitu.Huu
lazima uwe ni mwisho wa hiki
kikundi chenye kufanya
maangamizi makubwa
duniani” akawaza Habiba na
kuwasiliana na mtu mmoja
kutoka kundi la IS akampa
maelekezo kama alivyokuwa
ameelekezwa na David na mtu
Yule akamtaka Habiba ampe
muda alishughulikie lile suala
kisha atamjulisha.Alimtajia
kiasi cha fedha ambacho
angetakiwa kukitoa kwa ajili ya
suala lile.Baada ya kulimaliza
hilo suala Habiba akarejea
katika nyumba waliko akina
mama waliokuja kuungana
naye katika msiba.
Saa tatu za usiku
wakawasili Abu Dahir na mke
wake Nawal.Kama ilivyokuwa
kwa Mathew na Najma nao pia
walikuwa
mapumzikoni.Habiba Jawad
aliwapa wanae wote
mapumziko ya miezi
minne.Abu Dahir na Nawal
hawakuweza kuwahi mazishi
ya Najma kutokana na
kutopata taarifa kwa
haraka.Baada ya kuwasili Abu
Dahir alikwenda kuungana na
waombolezaji wengine
waliofika pale nyumbani
kuwafariji.Nawal yeye
alikwenda kuungana na akina
mama waliokuwa wanamfariji
Habiba.
Saa tano za usiku tayari
watu wengi walikwisha
ondoka.Ni watu wachache tu
waliokuwa wamebaki na ndipo
Abu Dahir alipoweza kupata
nafasi ya kuzungumza na
mama yake ili aweze
kumueleza kile kilichotokea
hadi kupelekea Najma kujiua
kwa kujipiga risasi.Habiba
Jawad akawataka Abu Dahir
na Nawal waelekee nyumbani
kwake akawakaribisha katika
sebule yake
“Mama utatusamehe sana
kwa kushindwa kuwahi
mazishi ya Najma.Tuliipata
taarifa kwa kuchelewa na
tulijitahidi sana kwa kila
namna ili tuweze kuwahi leo
lakini ilishindikana ” akasema
Abu Dahir
“Usijali Abu.Nilifahamu
hamtaweza kuwahi mazishi”
akasema Habiba
“Mama nini hasa
kilichotokea? Kwa nini Najma
alijiua?Abu Zalawi yuko
wapi?akauliza Abu Dahir
akionekana kuwa na shauku
sana ya kutaka kufahamu kila
kitu kuhusiana na tukio lile.
“Poleni sana vijana wangu
kwa hiki kilichotokea.Mpaka
sasa bado siamini kama kweli
Najma binti yangu wa pekee
amekwenda na hatutamuona
tena.Najma ameondoka na
afya na uzuri
wake.Imeniumiza sana”
akasema Habiba Jawad
“Nini hasa kimetokea
mama hadi kupelekea Najma
kuchukua maamuzi haya
magumu namna hii? Akauliza
Abu Dahir
“Ni hadithi ndefu Abu
lakini lazima nikiri kwamba
mimi ndiye niliyesababisha
kifo chake”
“Wewe ndiye uliyesabisha
kifo chake? Kivipi mama? Abu
Dahir akauliza
“Sikumuua kwa mkono
wangu lakini kuna maneno
nilimueleza na hayo ndiyo
yaliyopelekea akachukua
maamuzi yale ya kujiua”
“Ulimweleza nini mama?
Akauliza Nawal na Habiba
akamtazama Abu Dahir kisha
akasema
“Nilimueleza ukweli”
“Ukweli? Abu Dahir
akashangaa
“Ndiyo Abu.Dada yako
nilimueleza ukweli”
“Sijakuelewa
mama.Ukweli upi uliomueleza
hadi akaamua kujipiga risasi?
Abu Dahir akauliza
“Kuna mambo mengi
ambayo wewe na ndugu zako
hamkuwa mkiyafahamu hasa
kuhusu mimi na kile
kinachoendelea katika maisha
yangu.Nadhani ni wakati wa
kuweka mambo wazi ili wewe
pia ufahamu” akasema Habiba
na Nawal akasimama
“Nawal unakwenda wapi?
Habiba akauliza
“Ninadhani mazungumzo
haya yanawahusu zaidi ninyi”
akasema Nawal
“Hapana Nawal kaa.Wewe
pia ni mwanafamilia na ni
sehemu ya haya ninayotaka
kuyazungumza.Umefika
wakati wa kila kitu kuwekwa
mahala peupe” akasema
Habiba
“Huyu mama anataka
kufanya nini tena?Mbona
muelekeo wake
siuelewi?akajiuliza Nawal
“Mama kabla hujaendelea
nataka kufahamu yuko wapi
Abu Zalawi? Abu Dahir
akauliza
“Abu Zalawi hayupo na
hajui kama mke wake Najma
amefariki dunia”
“Hajui kuhusu kifo cha
Najma? Akauliza Nawal
“Ndiyo hajui chochote
kuhusu kifo cha Najma”
“Mama nashindwa
kuelewa.Hawa walikwenda
mapumzikoni kama
tulivyofanya sisi.Nini kili…..”
“Niliwarudisha mimi”
akasema Habiba na
kumkatisha Abu Dahir
“Nilimuhitaji Abu Zalawi
hivyo nikawasiliana nao na
kuwataka warudi nyumbani
mara moja.Baada ya kurejea
mimi na Abu Zalawi tulifanya
safari ya kwenda Marekani na
Abu Zalawi alibaki huko”
“Alibaki huko? Nawal
akauliza
“Ndiyo.Alibaki huko na
ninapenda kuwajulisha
kwamba AbuZalawi hatarejea
tena hapa kwetu.Amekwisha
ondoka katika maisha yetu”
“Mama sijakuelewa.Nini
kinaendelea hapa? Mama
naomba tafadhali unieleze kila
kitu.Naona kuna mambo
mengi yamejificha
hapa”Akasema Abu Dahir
“Abu kama unavyofahamu
kwamba baba yako alikuwa
mstari wa mbele sana katika
kupigania haki na aliuawa
akiwa katika mapambano ya
kudai haki za
wapalestina.Baada ya kifo
chake nilivaa viatu vyake na
kuendelea na harakati za kudai
haki.Nimekuwa nikitoa
msaada wa kifedha kwa
vikundi mbali mbali
vinavyoendesha harakati za
kudai haki za wapalestina
kutoka kwa taifa la Israel.Si
vikundi vya kipalestina tu
ambavyo vimekuwa vikipokea
msaada kutoka kwangu katika
kufanikisha harakati mbali
mbali za kudai haki bali
nimekuwa nikifadhili makundi
mengine kama vile IS
kufanikisha mipango yao
mbali mbali.Kundi la IS
linajulikana kama kundi hatari
zaidi la kigaidi kwa sasa
duniani na kitendo cha
kulifadhili kimenifanya
niwindwe na mashirika mbali
mbali ya kijasusi na hasa
Mossad.Pamoja na kuwindwa
huko na Mossad lakini hadi leo
hii hawajawahi
kunikamata.Umeshawahi
kujiuliza swali kwa nini?
Akauliza Habiba na Abu Dahir
akatikisa kichwa kwamba
hajaui.
“Kuna siri imejificha hapa
kwa nini sijawahi kukamatwa
licha ya kutajwa kuwa mfadhili
mkubwa wa makundi ya ugaidi
duniani” Habiba akanyamaza
na kuwatazama Abu Dahir na
Nawal
“Siri ambayo
hamuifahamu ni kwamba
ninafanya ufadhili huu kwa
makundi ya magaidi kwa niaba
ya Marekani”
“Marekani ? Abu Dahir
akashangaa
“Ndiyo Abu.Mimi ni
wakala wao.”
“Marekani wanafadhili
ugaidi? Abu akazidi kushangaa
“Ni vigumu kuamini Abu
lakini huo ndio ukweli”
“Marekani imekuwa
ikiendesha vita dhidi ya ugaidi
duniani na tumekuwa tukiona
namna inavyopata mafanikio
makubwa katika vita dhidi
hiyo.Iweje kwa upande wa pili
wawe na ushirika na magaidi?
Akauliza Abu
“Hiyo ni siri kubwa Abu
Dahir.Ni siri ambayo hata Rais
wa Marekani haifahamu”
akasema Habiba na
kunyamaza kidogo
“Ndani ya shirika la
ujasusi la Marekani CIA kuna
kitengo maalum ambacho
kinashughulika na jambo
hilo.Ni kitengo cha siri sana na
hata waliomo ndani ya CIA
hawakifahamu” Habiba
akanyamza baada ya Nawal
kuonyesha mshangao
“Kitengo hiki kazi yake
kubwa ni kushughulikia
mahusiano na makundi ya
kigaidi kwa maslahi ya
Marekani.Baba yako ndiye
aliyekuwa akitumiwa katika
kufadhili ugaidi na aliuawa
baada ya kwenda kinyume na
matakwa ya Marekani.Baada
ya kuuawa nilivaa viatu vyake
na kuendelea na kile
alichokuwa anakifanya”
“Siamini hayo
unayonieleza mama.Kwa muda
huu wote mmekuwa mkifanya
kazi kwa niaba ya Marekani?
“Ndiyo Abu.Tumekuwa
tukifanya kazi kwa niaba ya
Marekani.Alianza baba yako
na mimi nimefuata na utajiri
huu wote tulionao umetokana
na hicho
tunachokifanya.Wameniwezes
ha utajiri mkubwa niweze
kuutumia kufadhili ugaidi kwa
niaba yao.Hawataki
kujulikana”
“Kwa nini ukakubali mama
kubeba jukumu hili kubwa
mabegani mwako?Kwa nini
ukakubali kuchafua jina lako
kwa kuwa mfadhili wa ugaidi
duniani wakati kumbe
wafadhili wakuu wa ugaidi
wapo? Akauliza Abu Dahir
“Ilikuwa ni lazima nifanye
hivyo Abu.Hii imekuwa ni siri
yangu kubwa sana na
sikupanga kuwaeleza lakini
imebidi mfahamu kila kitu”
akasema Habiba
“Kwa nini umeamua
kutueleza mama? Akauliza
Nawal
“Kwa sababu ni wakati
muafaka kwa ninyi kufahamu
kile kinachoendelea” akajibu
Habiba
“Kama nilivyokueleza Abu
kwamba baba yako ndiye
aliyekuwa wa kwanza kuifanya
kazi hii na mimi niliendelea
pale alipoishia
yeye.Nimeifanya kazi hii kwa
muda mrefu kwa maslahi ya
marekani na sasa umefika
wakati ambao sitaki kuendelea
tena na hiki ninachokifanya
kwani hakipendezi machoni pa
Mungu.Nimekwisha kuwa
mzee sasa na ninahitaji
kujiweka karibu na Mungu
wetu na sitaki tena kuendelea
kukatili roho za watu wasio na
hatia.Katika makubaliano yetu
na kikundi hiki ni kwamba
nitaifanya kazi hii ya kufadhili
ugaidi kwa niaba yao hadi pale
nitakapovuta pumzi yangu ya
mwisho na ndiyo maana
wameniwezesha kuwa na
utajiri mkubwa sana.Kitendo
chochote cha kutaka kujiondoa
katika jambo hili ni
kuhatarisha usalama wangu na
wa familia yangu.Hivi
tuzungumzavyo ninyi wanangu
wote mnafuatiliwa na muda
wowote ambao nikijaribu
kwenda kinyume na matakwa
yao watawaondoa ndiyo
maana nimekuwa kimya
sijawahi kuwaeleza kuhusu
jambo hili.Nataka muwe
salama” akasema Habiba
“Unataka tuwe salama?
Akauliza Abu Dahir kwa ukali
“Abu chunga ulimi wako
unapozungumza nami !
akafoka Habiba akionekana
kutopendezwa na namna
mwanae alivyouliza kwa ukali
“Mama ingekuwa vyema
ungeendelea kubaki na siri hii
na ukafa nayo.Kuamua
kutueleza ukweli ni
kuhatarisha zaidi maisha
yetu.Tazama umemueleza
ukweli Najma na akaamua
kujiua” akasema Abu Dahir
“Abu imenilazimu
niwaeleze ukweli ili hata
ikitokea nikiondoka leo mjue
ni kitu gani kilikuwa
kinaendelea katika maisha
yangu” akasema Habiba na
kunyamaza akamtazama Abu
“Ili niweze kujiondoa
katika jambo hili ilinilazimu
kuja na mpango maalum na
hapo ndipo nilipoamua
kuwaleta hapa Abu Zalawi na
Nawal” akasema Habiba na
kunyamaza.Nawal alionyesha
wasi wasi mwingi
“Abu Dahir,kuna jambo
ambalo hujalifahamu bado”
akasema Habiba
“Mama una siri nyingi
umetuficha.Tafadhali kama
umeamua kueleza ukweli
tueleze kila kitu” akasema Abu
Dahir
“Ni kuhusu Abu Zalawi na
Nawal” akasema habiba
“Mama” akaita Nawal
“Nawal muache mama
aseme anachotaka kukisema”
akasema Abu Dahir
“Nawal usiwe na
hofu.Nataka kila kitu kiwe
wazi leo” akasema Habiba
“Endelea mama.Kuna nini
kuhusiana na hawa watu
wawili? Akauliza Abu Dahir
“Abu Zalawi na Najma
nimewatoa katika lililokuwa
kundi la Ammar Nazari
brigades.Wawili hawa ni
majasusi na walikuwa katika
misheni maalum na siyo
magaidi.Niliamua kuwachukua
na kushirikiana nao kwa ajili
ya kw……….”
“Mama
sijakuelewa.Umesema Nawal
na Abu Zalawi ni majasusi na
si magaidi?Nawal si alikuwa
mke wa Ammar Nazari?
Akauliza Abu Dahir na kabla
Habiba hajajibu Nawal
akasimama
“Ni kweli Abu Dahir hiki
anachokisema mama yako”
Akasema Nawal na kutazama
na Abu
“Siamini masikio yangu !
akasema Abu Dahir
“Mama yako ameamua
kuweka kila kitu wazi hivyo
hakuna haja ya kuficha
chochote.Ni kweli mimi na
Abu Zalawi ni majasusi na
tulikuwa katika kundi la
Ammar Nazari Brigades kwa
misheni maalum.Mimi ni
jasusi toka CIA Marekani na
mwenzangu Abu Zalawi
anatokea Mossad.Jina lake
halisi ni Mathew Mulumbi na
si Abu Zalawi kama
anavyojulikana.Katika kundi la
Ammari Nazari Brigades mimi
nilikuwa na kazi ya kumsaka
gaidi mmoja ambaye ana
undugu na Ammar Nazari
ambaye aliwahi kufanya
mauaji makubwa Marekani na
kukimbia hivyo niliuganishwa
na Ammar na nikawa mke
wake.Abu Zalawi yeye alitokea
Mossad na alikuwa na misheni
maalum aliyotumwa
kuitekeleza ambayo ni kumuua
Habiba Jawad.Mossad
wanafahamu kwamba Habiba
amekuwa akifadhili makundi
mbali mbali ya wanamgambo
wa kipalestina ambao
wamekuwa wakiendesha
mashambulio mbali mbali
ndani ya Israel hivyo
wanamtafuta sana Habiba na
wakamtumia Abu Zalawi ili
kuungana na Ammari Nazari
na kutengeneza njia ya kufika
kwa Habiba Jawad.Baada ya
Ammar Nazari kuuawa na
vikosi vya Israel mimi na Abu
tuliondoka na kuanza harakati
za kumsaka Habiba Jawad
lakini tulipofika hapa misheni
ikabadilika.Ile mipango ya
kumuua Habiba Jawad
ikatoweka na badala yake
tukajikuta tukiungana na
Habiba Jawad katika mipango
yake na kuwa wanafamilia”
akasema Nawal na Abu Dahir
akaonekana kuchanganyikiwa.
“Abu Zahir anachokisema
mama yako ni………..” akasema
Nawal na Abu
akamnyamazisha
“Nyamaza ! akasema Abu
Dahir kwa sauti kali
“Wewe na huyu
mwanamke wote mko
sawa.Wote mama yenu
mmoja.Wote ni mashetani
waongo wakubwa.Nawal
nilikupenda sana na nikawa
tayari kufanya chochote kwa
ajili yako.Kwa nini nawe
ukashiriki uongo huu mkubwa
wa mama? Na wewe mama
kwa nini ukanishawishi
nimuoe Nawal wakati
ukifahamu kwamba ni jasusi?
Kwa nini hukunieleza ukweli?
Akafoka Abu aliyekuwa
amepandwa na hasira
“Nilikuwa na sababu
maalum za kutaka umuoe
Nawal”
“Ulikuwa unachunguza
maisha yetu mimi na Najma
ndiyo maana ukatutaka tuwe
na mahusiano na hawa
majasusi ? Abu akauliza
“Hapana sijawahi
kuwachunguza.Nilitaka
kuwalinda”
“Mama wewe una roho ya
kishetani kabisa ndiyo maana
hujawahi kusikitika hata siku
moja kwa watu wanaouawa na
magaidi ambao
unawafadhili.Najuta kuzaliwa
nawe Habiba ! akasema kwa
ukali Abu Dahir na Nawal
aliyekuwa karibu yake
akamnasa kofi
“Iwe ni mara ya kwanza na
ya mwisho kumtusi mama
yako.Pamoja na yote
anayoyafanya na aliyoyafanya
huyu bado ni mama yako na
ataendelea kuwa mama yako
daima.Huyu ndiye
aliyekubeba tumboni mwake
miezi tisa na akakulea hadi
umefika hapa
ulipofika.Nakuonya tena
ukithubutu kumtusi mama
yako mbele yangu
nitakufundisha adabu.Hapa
unaponiona mimi sina uwezo
wa kuzaa mtoto.Nimekwisha
ondolewa kizazi.Unajua ni
uchungu gani ninaupata kwa
kukosa mtoto?Usirudie tena
kumtusi mama yako ! akasema
Nawal kwa ukali huku
akilengwa na machozi.Abu
Dahir akamtazama Nawal kwa
macho ya mshangao.
“Huna kizazi?! Akauliza
akiwa ameshika shavuni
mahala aliponaswa kofi
“Ndiyo sina kizazi na
siwezi kupata mtoto ! akajibu
Nawal bila hofu
“Nawal toka tumefunga
ndoa tumekuwa katika jitihada
mbali mbali za kutafuta mtoto
na umekuwa unanihakikishia
kwamba tutapata mtoto hivi
karibuni ! Oh Mungu wangu !
akasema Abu kwa masikitiko
“Ulikuwa ni uongo.Sina
uwezo wa kubeba mimba !
akasema Nawal.
Ghafla Abu Dahir akainua
taa ya mezani iliyokuwa katika
meza ndogo pembeni na pale
alipokuwa amekaa na kumpiga
nayo Nawal ikapasuka.Abu
Dahir akachukua birika na
kumrushia Nawal
akalikwepa.Abu alionekana
kama vile amepatwa na kichaa
“Ninyi wanawake leo
mtanitambua mimi ni nani !
akafoka Abu huku akirusha
vitu kumpiga navyo Nawal
“Abu acha ujinga huu
tafadhali ! akafoka Habiba
“Wewe mama ndiye
uliyeyataka haya yote.Una
roho mbaya sana! Akafoka Abu
na kuinua chungu cha maua
kilichokuwa dirishani kwa
lengo la kumpiga nacho mama
yake lakini Nawal alikwisha
isoma dhamira yake akajiinua
pale chini alipokuwa akaruka
na kukipiga teke chugu kile
kikaanguka na
kuvunjika.Nawal ambaye
hasira zilikwisha mpanda
akamrukia Abu mateke mawili
mfululizo yaliyomrusha Abu
hadi ukutani akajigonga kwa
kishindo na kuanguka chini
halafu akamfuata Habiba
“Mama uko
sawa?Hajakuumiza
huyu?akauliza Nawal
“Nimeumia
kidogo.Ahsante kwa kuniokoa”
akasema Habiba na Nawal
akageuka kumtazama Abu
Dahir ambaye alikuwa amelala
pale chini akionekana
kutokuwa na fahamu.Haraka
haraka akamfuata na kujaribu
kumtikisa huku akimuita jina
lake lakini hakuitika.Akageuka
kumtazama Habiba Jawad
ambaye naye alionyesha hofu
baada ya kuiona sura ya
Nawal,akainuka na kumfuata
akamtazama Abu Dahir
ambaye hakuwa na
fahamu.Bila kupoteza muda
Habiba akampigia simu
daktari wake anayeishi
pembeni ya nyumba yake
ambaye alifika mara moja
akampima Abu kisha akasema
“Anatakiwa akimbizwe
hospitali haraka sana !
Habiba akainuka
akachukua simu na kuwapigia
wasaidizi wake ambao walifika
haraka haraka na kumchukua
Abu Dahir wakamuingiza
garini wakamkimbiza
hospitali.Habiba na Nawal nao
wakaingia garini wakaelekea
hospitali.
“Mama ni vipi kama
nimempiga Abu sehemu
mbaya? Akauliza Nawal
akionekana kuwa na hofu
“Usijilaumu
Nawal.Ulifanya ulichopaswa
kukifanya.Kama usingefanya
vile Abu angenipiga na kile
chungu na pengine ningeweza
hata kupoteza maisha.Kwa
sasa tumuombee ili aweze
kuwa salama.Sitaki kupoteza
tena mtoto
mwingine.Nimekwisha poteza
watoto wawili tayari na
nimebaki na huyu mmoja”
akasema Habiba na kufuta
machozi
“Lakini mama kwa nini
uliamua kufanya hivi
ulivyofanya?Kwa nini uliamua
kuwaeleza ukweli
wanao?akauliza Nawal
“Ilikuwa lazima wafahamu
Nawal.Sikutaka kuendelea
kuwaficha kwani endapo
ningefariki dunia bila
kuwaeleza ukweli yawezekana
nao wangeendelea kufanya kile
ambacho mimi na baba yao
tumekuwa tunakifanya.Sitaki
watoto wangu waendelee
kufadhili ugaidi,sitaki
waendelee kumwaga damu za
watu kama nilivyofanya mimi”
akasema Habiba
“Ulifanya kitu kizuri
kuwaeleza ukweli lakini kwa
bahati mbaya mambo
hayakwenda kama ulivyokuwa
umekusudia” akasema
Nawal.Habiba akafuta machozi
na kusema
“Nadhani Mungu
ananiadhibu kwa mambo
niliyoyafanya.Nimefanya
mambo mengi maovu.Damu
nyingi imemwagika kwa
sababu yangu na haya ndiyo
mapigo ninayoyapata.Naomba
Mungu asimchukue Abu Dahir
kwani ni mtoto pekee
niliyebaki naye” akasema
Habiba na kuchukua simu
akampigia mmoja wa
madaktari katika hospitali
alikoelekeza apelekwe Abu
Dahir akamjulisha kuwa
mwanae amepatwa na
matatizo na anapelekwa pale
hospitali akaomba
ashughulikiwe haraka
Abu Dahir alifikishwa
hospitali ambako tayari
wauguzi walikuwa
wamejiandaa
wakimsubiri,akashushwa
haraka haraka katika gari na
kuweka katika kitanda
kikakimbizwa ndani katika
chumba cha wagonjwa
mahututi ambako alianza
kupatiwa matibabu.Dakika
chache baada ya Abu Dahir
kuingizwa katika chumba cha
wagonjwa mahututi,Habiba
Jawad na Nawal
wakawasili.Habiba
alifahamika pale hospitali
akapokewa na kupelekwa
sehemu ya kusubiri madaktari
watakapomaliza
kumuhudumia mgonjwa wake.
Baada ya dakika saba
mlango wa chumba cha
wagonjwa mahututi
ukafunguliwa na daktari
akatoka.Habiba akasimama na
kumfuata daktari akamtaka
waelekee ofisini kwake
“Kijana wangu
anaendeleaje daktari?akauliza
Habiba akionekana kuwa na
hofu
“Mama Habiba
tumejitahidi kadiri ya uwezo
wetu lakini tumeshindwa
kuokoa maisha ya
mwanao.Uchunguzi wa awali
unaonyesha ana jeraha
kichwani.Nini hasa
kilimtokea? Amepata ajali?
Akauliza Daktari na Habiba
Jawad akashindwa
kumjibu.Yeye na Nawal
wakakumbatiana wakilia.
“Ahsante Mungu kwa kila
jambo.Wewe ndiye mwenye
kutoa na kutwaa kwa muda
uutakao.Hatuwezi kupingana
na maamuzi yako japo
tungependa tuendelee kuwa
pamoja na Abu Dahir lakini
nakushukuru kwa muda
ambao umempa hapa
duniani.Naomba utupe nguvu
ya kulihimili jambo hili”
akasema Habiba machozi
yakimwagika
Habiba Jawad na Nawal
wakapelekwa katika chumba
ulikokuwa mwili wa Abu Dahir
“Saa chache zilizopita
tulikuwa wote ndegeni
tukirejea Riyadh kuhudhuria
msiba wa dada yako,sikuhisi
kama ulikuwa unayafuata
mauti yako.Abu Dahir mimi
ndiye nimesababisha kifo
chako nitalia machozi gani kwa
hili nililolifanya? Najua
ulikuwa unanipenda sana
lakini umekufa ukiwa na
hasira nami baada ya
kuufahamu ukweli kuhusu
maisha ya mama yako na
kuhusu mimi.Najuta kwa nini
sikukueleza ukweli kuhusu
mimi kuwa ni jasusi wa
CIA.Najuta kwa nini
sikukueleza ukweli kama sina
uwezo wa kukupatia mtoto
kwani ni jambo hili ndilo
lililokupa hasira
zaidi.Nisamehe Abu Dahir
huko uliko.Nisamehe ! akalia
Nawal akiwa amesimama
pembeni ya mwili wa Abu
Dahir.Wote wawili Habiba na
Nawal machozi yalikuwa
yanawabubujika.Walitumia
dakika kumi ndani ya kile
chumba kisha wakatoka na
kuondoka kurejea nyumbani
“Mama nimemuua mume
wangu.Nimemuua mwanao
pekee aliyesalia” akasema
Nawal wakiwa garini huku
akimwaga machozi.Habiba
akageuza shingo akamtazama
Nawal na kumuinamisha
kifuani kwake akamkumbatia
“Nawal narudia
kukusisitiza kwamba haya yote
yanayotokea ni mipango ya
Mungu na hupaswi kujilaumu
kwa hili lililotokea.Ilikuwa iwe
hivyo.Abu Dahir aliandikiwa
afe kifo cha namna ile hivyo
hakuna namna ambayo
ungeweza kukwepa.Lakini
tambua kwamba haya yote
yanayoendelea hivi sasa ni
matokeo ya maisha niliyoishi
mimi.Ni mapigo yatokanayo
na matendo yangu.Nimetesa
watu wengi sana.Machozi ya
akina mama waliopoteza
watoto wao katika
mashambulio yaliyofanywa na
makundi ya kigaidi ambayo
ninayafadhili hayajaniacha
salama.Machozi ya watoto
ambao wamebaki yatima
baada ya kuwapoteza wazazi
wao katika mashambulo ya
kigaidi niliyoyafadhili haya
ndiyo malipo yake.Nimepoteza
watoto wangu wote niliowazaa
na sasa nimebaki
mwenyewe.Pamoja na mapigo
haya lakini Mungu
hajaninyima kila
kitu.Amewachukua watoto
wangu lakini ameniletea
watoto wengine ambao ni
wewe na Mathew” akasema
Habiba na Nawal akainua
kichwa chake
“Mama umeongea kuhusu
Mathew.Nataka kufahamu
mahala alipo.Sijamuona katika
msiba wa Najma” akauliza
Nawal
“Mathew ameondoka
hatarejea tena kama
nilivyowaambia na hilo ni
moja kati ya mambo
yaliyopelekea Najma
akachukua maamuzi ya kujiua”
akasema Habiba
“Mathew amekwenda
wapi? Amekufa?
“Hapana hajafa.Nawal
tutazungumza baadae lakini
kwa sasa tujielekeze katika
msiba wa Abu na
tutakapomaliza tutazungumza”
akasema Habiba
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Ndege ya jeshi aliyopanda
Mathew iliwasili jijini Dar es
salaam.Kutoka angani ni
sehemu chache tu za jiji la Dar
es salaam ambazo zilionekana
kuwa na umeme.Sehemu
kubwa ya jiji la Dar ilikuwa
gizani kutokana na miundo
mbinu ya umeme kuharibiwa
katika machafuko yaliyokuwa
yanaendelea.
“Nimezoea kuliona jiji la
Dar es salaam kutokea angani
likiwaka taa kila sehemu lakini
leo hii jiji limetanda giza kila
sehemu.Kwa tamaa ya mali
ambazo Mungu ametujalia
ziwepo katika nchi
zetu,mabepari wametufikisha
hapa.Ni mara ya kwanza
Tanzania tumefikishwa hatua
hii ya kuchinjana wenyewe
kwa wenyewe.Ninaapa kwa
gharama zozote zile lazima
kikundi hiki cha hawa watu
waliotufikisha hapa kwa tamaa
za mali yetu nikifutilie mbali
na dunia lazima ifahamu kile
ambacho mataifa makubwa
yanafanya katika nchi
ndogo.Huu ni unyama
uliopitiliza.Ni unyonyaji usio
na mfano.Naamini haya ni
maongozi ya Mungu hadi
akanifikisha katika kundi hili
ambalo limeigeuza nchi yetu
uwanja wa mauaji.Tayari
nimefahamu kuwa ni
Marekani ndio waliotengeneza
machafuko haya kwa manufaa
yao.Hawako peke yao lazima
kuna watu wa hapa nchini au
katika nchi za Afrika mashariki
ambao wanashirikiana nao
katika kuanzisha na kuchochea
vurugu hizi.Hawa ndio
wanaotakiwa kusakwa kwa
haraka sana na kujulikana ni
akina nani na kama
tukifanikiwa kuwapata hawa
basi tutakuwa tunaweza
kusaidia kumaliza vurugu
hizi.Kuna nguvu mbili hapa
ambazo zimeifikisha Tanzania
hapa tulipofika.Ipo nguvu ya
ndani na nguvu ya nje.Inabidi
kuanza na nguvu ya ndani
kisha nitaendelea na wale wa
nje.Naapa hakuna aliyeifikisha
Tanzania hapa atabaki
salama”akawaza Mathew na
kumkumbuka Ruby
“Nilijaribu kumpigia simu
Ruby lakini
hakupatikana.Nina wasi wasi
sana na usalama wake.Gosu
Gosu naye sijui
anaendeleaje.Nawahitaji sana
hawa watu kama watakuwa
wazima katika kuhakikisha
tunaiokoa nchi yetu kutoka
katika
machafuko.Ninachoelewa
hawa jamaa kwa vile
wamekwisha ingia Afrika
Mashariki lazima wataotesha
mizizi na kuhakikisha kwamba
wanaendelea kuchota utajiri
wetu.Naomba niwakute wote
wako salama” akawaza
Mathew na kutaarifiwa
kwamba ndege inakaribia
kutua katika uwanja wa ndege
wa Julius Nyerere ambao toka
vurugu zilipoanza ulikuwa
umefungwa na ukilindwa na
wanajeshi .
Ndege ile ya jeshi la
Marekani ikiwa na vifaa mbali
mbali vya wanajeshi wa
Marekani waliokuwa nchini
Tanzania ikatua salama.Mizigo
ikapakuliwa na kuingizwa
katika magari kisha wanajeshi
waliokuja na ndege ile
wakaingia katika magari
maalum ya jeshi la Marekani
na msafara ukaondoka
kuelekea katika kambi yao
Mathew Mulumbi akiwa ni
mmoja wao
“Hawa jamaa hawajui
kama hapa nimefika
nyumbani.Watakapogundua
kwamba mimi ni mtanzania
tayari watakuwa wamechelewa
sana lakini kwa sasa ngoja
niendelee kujifanya mimi ni
mgeni wa hapa Tanzania ili
niendelee kuusoma mtandao
wao” akawaza Mathew na
kuona namna alivyokuwa
anachungwa.Ndani ya gari
alilokuwa amepanda kulikuwa
na wanajeshi wanne wenye
silaha na gari lile liliwekwa
kati kati ya msafara.
“Nadhani wameelekezwa
wanichunge ndiyo maana
wameniweka
katikati.Hawapaswi kuwa na
hofu nitafanya walivyonieleza
lakini watajuta sana na
kumlaumu Habiba Jawad kwa
kuwakutanisha na mimi.Safari
hii ninataka nifanye kitu
ambacho kitakuwa cha
kihistoria.Tumeonewa vya
kutosha na sasa ni wakati wa
kuwaonyesha haya mataifa
makubwa kwamba hata sisi
tunao uwezo na tumechoshwa
na mambo wanayotufanyia”
akawaza Mathew akiyaelekeza
macho yake nje
“Dar es salaam haikuwa
hivi.Hili ni jiji lililokuwa
linakesha lakini muda huu
barabara tupu hakuna watu
mitaani.Sipati picha namna
maisha yalivyo magumu hivi
sasa.Maduka
yamefungwa,upatikanaji wa
chakula na mahitaji muhimu
imekuwa ni shida lakini baadhi
ya watu wachache wao
wanaishi maisha mazuri na
kupata kila wanachokihitaji
wakisahau kwamba kuna
mamilioni ya watu
wanaoteseka huku Tanzania
na Afrika mashariki kwa
sababu yao.Tunatakiwa
kupambana kuhakikisha
tunairejesha nchi yetu
ilivyokuwa na ili kumaliza
vurugu hizi ni lazima
kuuchimbua mzizi wenyewe
ambao ni kikundi kile kidogo
ndani ya CIA” akawaza
Mathew huku wakiendelea
kukata mitaa ya jiji la Dar es
salaam ambayo kwa usiku huu
ilikuwa kimya.Mioto ya
matairi na moshi mzito
vilionekana katika baadhi ya
barabara na hata majengo
yanayoungua moto pia
yalikuwepo.Katika baadhi ya
barabara walikuta zimefungwa
kwa mawe makubwa
“Hali ilivyo Dar es salaam
utadhani kuna filamu
inatengenezwa kumbe ni hali
halisi .Inasikitisha sana !
Narudia tena kuahidi kwamba
wale wote waliotufikisha hapa
hakuna atakayebaki
salama.Tanzania hatukupaswa
kufikishwa hapa.Lakini hili ni
funzo kwa watanzania ili wawe
macho kulinda amani
yao.Wamekuwa wakihubiriwa
kwa miaka mingi kwamba siku
amani hii ikipotea
watajuta.Wamejaribu
kuchezea amani na wameona
madhara yake.Hakuna sehemu
ya kukimbilia imelazimu
wayakimbie makazi yao na
kujificha katika makambi.Kwa
haya wanayokutana nayo
naamini hata akija tena mtu
mwingine siku nyingine
kutaka kuwarubuni kuchezea
amani yao hawatajaribu tena”
Mathew akatolewa mawazoni
baada ya msafara wao
kukutana na kundi kubwa la
vijana waliokuwa wamebeba
mienge na silaha huku
wakiimba.Ikalazimu wanajeshi
wa Marekani kutumia risasi za
moto kuwatawanya kwani
baadhi yao walikuwa na silaha
na walianza kushambulia
magari katika ule
msafara.Baada ya kundi lile la
vijana kutawanyika magari
yakaongeza mwendo na moja
kwa moja wakaelekea katika
uwanja wa uhuru ambako
ndiko kulikuwa na kambi
kubwa ya wanajeshi wa
Marekani na vifaa vyao vyote
vilikuwa vinahifadhiwa
huko.Kambi nyingine ilikuwa
ufukweni mwa bahari ya
Hindi.
Mathew alishushwa garini
na kukabidhiwa kwa mmoja
wa viongozi wa kambi ile
ambaye alimpeleka hadi katika
hema.
“Karibu Tanzania.Jina
lako nani? Akauliza Yule jamaa
“Abu Zalawi” akajibu
Mathew kikakamavu
“Abu Zalawi nimeelekezwa
na viongozi wangu kwamba
nikupokee na kisha
nitakukabidhi kwa mtu
ambaye atakuja hapa
kukuchukua.Umewahi kufika
Tanzania kabla? Akauliza
“Hapana sijawahi” akajibu
Mathew
“Hali ni mbaya sana hasa
hapa Dar es salaam na jiji la
Tanga pia.Nadhani umejionea
hali halisi huko mitaani wakati
mkija hapa”
“Ndiyo mkuu.Tumekutana
na kundi kubwa la vijana
wakiwa na silaha na
kushambulia msafara wetu”
“Basi hiyo ndiyo hali
tunayokutana nayo kila siku
katika kujaribu kurejesha hali
ya amani tukishirikiana na
vikosi vya ulinzi vya Tanzania”
“Endelea kupumzika na
atakapofika mwenyeji wako
nitakufahamisha” akasema
Yule mwanajeshi na kutoka nje
ya lile hema akamuacha
Mathew peke yake.
“Naamini huyo mtu
anayekuja kunichukua ni
mmoja kati ya watu wa IS na
atakuwa anatumiwa na CIA
katika kuratibu na kuchochea
hizi vurugu
zinazoendelea.Imekuwa vyema
wamenielekeza sehemu husika
kwani huyo jamaa ndiye wa
kuanza naye” akawaza Mathew
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 3 : EPISODE 1
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Saa tisa za alasiri
televisheni ya taifa ilikatisha
kipindi kilichokuwa
kinaendelea na kujiunga na
matangazo ya moja kwa moja
kutoka ikulu jijini Dar es
salaam ambako Rais wa
jamhuri ya muungamo wa
Tanzania alitarajia kutoa
hotuba kwa watanzania.Kama
ilivyokuwa siku
iliyotangulia,simu janja zote
ambazo zilikuwa zimewashwa
muda huo ziliunganishwa na
matangazo yale ya moja kwa
moja kutoka ikulu kwa lengo la
kumuwezesha kila mwananchi
kusikiliza ujumbe ambao Rais
wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania alitaka kuwapa
watanzania.Tayari wanahabari
walikwisha weka sawa kamera
zao na aliyekuwa akisubiriwa
ni Rais
Mlango ulifunguliwa na
Rais Dr Fabian Kelelo
akajitokeza akiwa
ameambatana na Mufti wa
Tanzania Sheikh Seleman
Majid.Muongozaji wa shughuli
ile alitoa maelezo machche na
kumkaribisha Rais aweze
kuzungumza na
watanzania.Rais alianza kwa
kuwatania kidogo waandhishi
wa habari kisha akaendelea
“Ndugu watanzania
wenzangu awali ya yote
ninamrejeshea utukufu Mungu
wetu aliye juu kwa
kutukutanisha tena siku
hii.Poleni sana wale wote
ambao mmeendelea
kuwapoteza wapendwa wenu
kufuatia vurugu zinazoendelea
na wale wote ambao mnauguza
majeraha nawatakiwa uponaji
wa haraka.
Ndugu watanzania,jana
nilizungumza nanyi kwa kirefu
na kuwasisitiza umuhimu wa
kutunza amani
yetu.Ninashukuru sana kwa
wengi kunielewa na taarifa
niliyoipata ni kwamba vurugu
zimepungua na hii ni dalili
njema kwamba tunaelekea
kuzuri.Bado naendelea
kuwasihi ndugu watanzania
tuachane na vurugu hizi
ambazo hazina maslahi kwetu
na hata kwa dini
zetu.Tunachokivuna katika
machafuko haya ni hasara
badala ya faida.Ndugu zetu
wengi wamepoteza
maisha,wengine hawajulikani
walipo,wengine wamepata
ulemavu wa kudumu na
wengine wanaendelea kuuguza
majeraha hospitali.Wengi wetu
tumepoteza mali,nyumba
zimechomwa moto,majengo ya
serikali yamechomwa na
kuharibiwa,miundo mbinu
imeharibiwa,biashara
zimefungwa nk.Ndugu zangu
kwa ujumla tunachovuna
katika machafuko haya ni
hasara kubwa na tuna kazi
kubwa ya kuijenga nchi yetu
baada ya machafuko haya
kumalizika” Rais akanyamaza
kidogo halafu akaendelea
“Jana baada ya kumaliza
kutoa hotuba yangu,nilipigiwa
simu na Mufti wa Tanzania
akaniomba tuonane leo
tuzungumze.Leo kuanzia
asubuhi nilikuwa na kikao
kirefu naye na kubwa
tulilolijadili ni kuhusiana na
vurugu hizi zinazoendelea
nchini namna tutakavyoweza
kuzmaliza.Imekuwa ni desturi
yetu kukaa mezani kila pale
inapojitokeza mikwaruzano
baina ya dini zetu na mara zote
katika mazungumzo ya pamoja
tumekuwa tukimaliza tofauti
na amani ikamalaki.
Tumezungumza mambo
mengi katika kikao hicho
kirefu na tumekubaliana kuwa
na kikao kikubwa
kitakachowahusisha viongozi
wakuu wa dini zote hapa
nchini ili tutafute
muafaka.Naahidi kikao hicho
kitafanyika mapema sana ili
tukae meza moja serikali na
viongozi wa dini tujikwamue
hapa tulipokwama na maisha
yarejee kama kawaida.Kwa
kuwa mambo mengi
nilizungumza jana leo naomba
nimpe nafasi Mufti ana neno la
kuzungumza na watanzania.”
akasema Dr Fabian na
kumkaribisha mufti wa
Tanzania Sheikh Seleman
Majid ambaye alianza kwa dua
kisha akaendelea
“Ndugu zangu,awali ya
yote nami nataka nianze kwa
kuwapa pole nyingi wale wote
ambao wamepoteza ndugu zao
hadi sasa katika machafuko
haya yanayoendelea hapa
nchini kwetu na wale wote
waliopata majeraha mbali
mbali nawaombea wapate
nafuu ya haraka.
Ndugu zangu watanzania
kwa siku kadhaa sasa nchi yetu
imekumbwa na machafuko
makubwa kabisa kuwahi
kutokea hapa
nchini.Machafuko haya
yalianzia katika nchi ya jirani
na yakaenea kama moto wa
nyika hadi kufika hapa
Tanzania.Ndugu zangu dunia
inashangaa nini kimetokea
Tanzania?Katika historia ya
nchi yetu hakujawahi kutokea
machafuko kama haya
yanayoendelea ya waumini wa
dini
kushambuliana.Mheshimiwa
rais alieleza kwa kirefu jana
namna ambavyo watanzania
tumekuwa tukiishi kwa amani
na upendo mkubwa licha ya
tofauti zetu za kidini.Tumeishi
kindugu tukishirikiana katika
mambo mbali mbali
sherehe,misiba n.k.
Hatujawahi kubaguana hata
siku moja kwa imani zetu.Nini
kimetufikisha hapa? Swali hili
ameliuliza Rais jana wakati
anatoa hotuba yake na kwa
swali hilo ndiyo lilinifanya
nitake kuonana na
mheshimiwa Rais ili kwa
pamoja tutafute majawabu ya
nini kimetufikisha hapa.
Tumekuwa na kikao kirefu
na tumezungumza kwa upana
kuhusu jambo
hili.Tumekubaliana kwamba
tuwe na kikao kikubwa cha
viongozi wakuu wote wa dini
ili kwa pamoja tuweze
kuzungumza na kutafuta
muafaka lakini wakati kikao
hicho kikiandaliwa
tumekubaliana kwamba sisi
viongozi wa dini
tuwahamasishe waumini wetu
watulie na waache
vurugu.Suala hili ni pana zaidi
ya tunavyodhani hivyo basi
tunataka kuipa serikali nafasi
iweze kulishughulikia hili
jambo na kupata chanzo
chake.Tunapoendelea
kushambuliana na kuuana
tunaifanya serikali ishindwe
kulishughulikia suala hili hivyo
Rais ametuomba kila kiongozi
wa dini ajitahidi kuhakikisha
anawahamasisha waumini
wake watulie waache vurugu ili
serikali ishughulikie kutafuta
chanzo cha jambo hili.
Ndugu zangu kufuatia
maelekezo hayo ya Rais,niko
hapa kuzungumza na ndugu
zangu wa upande wa waislamu
kuwasihi wasiendelee kushiriki
katika vurugu.Uislamu ni dini
ya amani na hata
tunaposalimiana tunasema
Assalam alaikum maana yake
amani iwe nawe. Dini ya
Uislamu ina mitazamo
inayofanana na dini nyingine
kuhusu suala hili la amani na
usalama.Katika mtazamo wa
Uislamu usalama una maana
ya amani na utulivu katika
jamii. Neno amani kwa ujumla
limezungumziwa katika karibu
aya 140 za Qur'ani ambacho ni
kitabu kitakatifu cha
Mwenyezi Mungu.Usalama na
amani vina mfungamano na
Mwenyezi Mungu Muumba.
Mwenyezi Muumba
mwenyewe amejitaja kuwa ni
"Assalam" kwa maana ya
amani na Mwenye amani na
salama na kwa msingi huo kila
usalama na amani ni mwangwi
wa dhati yake tukufu. Dhati ya
mwanadamu pia daima huwa
katika hali ya kustawi na
kufanya harakati za kuelekea
kwenye amani na utulivu
kamili ambao haupatikani ila
kwa amani na usalama , yaani
dhati ya Mwenyezi Mungu
Muumba.Aya ya 208 ya
Suratul Baqara inasema:
Enyi Mlioamini!
Ingieni katika usalama
nyote. Wala msifuate
nyayo za She'tani; hakika
yeye kwenu ni adui
aliyewazi.
Vilevile aya ya 61 ya Suratul
Anfal inasema:
Na (wapinzani wako)
wakielekea kwenye
amani nawe pia elekea,
na mtegemee Mwenyezi
Mungu. Hakika Yeye
ndiye Mwenye kusikia na
Mwenye kujua.
Neno "Islam" pia
linatokana na msingi wa neno
"Silm", na kwa hakika lina
maana ya kumfuata Mwenyezi
Mungu ambaye Yeye
mwenyewe ndiye amani na
usalama mutlaki na utulivu
kamili.
Neno jingine ni "sulh" ambalo
lina maana na amani,
maelewano na uhusiano
mwema baina ya wanadamu.
Uislamu umetumia neno hilo
ukitaka kuwepo upendo,
kuheshimiana, kujiepusha na
uchokozi na uhasama na
kuchupa mipaka ya wanadamu
wengine.
Ili kuweza kupatikana
amani na uadilifu, Uislamu
umeweka safari yenye awamu
tatu tofauti. Kwanza ni
usalama na amani ya ndani ya
nafsi. Katika awamu hii watu
wote wa jamii wanatakiwa
kutakasa nafsi zao na
kuzipamba kwa taqwa na
uchamungu.Katika awamu hii,
muumini anapaswa
kukomesha mpambano na vita
liyopo baina ya matamanio na
matakwa yake ya kinafsi na
yale ya kiroho, na kufikia
amani na usalama wa ndani ya
nafsi ili pande hizo mbili za
kinafsi na kiroho ziishi pamoja
kwa amani na kumsaidia
mwanadamu kufikia kilele cha
ukamilifu. Ni baada ya hapa
ndipo mwanadamu
anapokuwa tayari kwa ajili ya
harakati ya kijamii na
wanadamu wenzake kuelekea
kwenye malengo aali na ya juu
zaidi. Aya ya 103 ya Suratu Aal
Imran inasema:
“Na shikamaneni na
Kamba ya Mwenyezi
Mungu nyote kwa
pamoja, wala
msifarikiane”
Kwa msingi huo amani ya
ndani ya nafsi ndiyo msingi wa
ukamilifu wa kimaadili na
kiroho kwa ajili ya kuwa na
taathira kubwa zaidi katika
jamii ya Kiislamu.
Awamu ya pili ya amani na
usalama katika Uislamu ni
amani na usalama wa jamii.
Baada ya kuwa tayari kinafsi
kwa kuitakasa na kuisafisha,
mwanadamu huwa
ametengeneza mazingira
mazuri kwa ajili ya muungano
mpana zaidi wa kijamii na
wanadamu wenzake. Hapa
ndipo inapokuja amri ya
Mwenyezi Mungu inayowataka
Waislamu kuwa na umoja na
kujenga udugu. Sehemu moja
ya aya ya kwanza ya Suratul
Anfal inasema:
“Basi mcheni
Mwenyezi Mungu na
msuluhishe mambo baina
yenu, na mtiini Mwenyezi
Mungu na Mtume wake
ikiwa nyinyi ni
waumini.”
Kwa utaratibu huo
Waislamu hutoka katika
minyororo ya ubinafsi,
ubaguzi, dhulma na sifa
nyingine mbaya na kuwa watu
wema na wenye faida kwa
jamii.
Awamu ya tatu ya amani
na usalama inahusiana na
usalama na amani kwa wasio
Waislamu. Miongoni mwa
misingi na kanuni
zinazotawala jamii ya Kiislamu
ni kuishi kwa amani na
usalama na wasio Waislamu.
Kinyume na fikra na dhana za
wanafikra wengi wasio
Waislamu na propaganda
chafu za nchi za Magharibi,
Uislamu ni dini ya amani na
kuishi kwa usalama na wasio
Waislamu. Hii ni pamoja na
kwamba, huwezi kupata hata
aya moja ya Qur'ani
inayowalazimisha watu
kukubali dini hiyo kwa vita na
mabavu. Vita katika Uislamu
vina sura ya kujihami na
kujilinda mbele ya
mashambulizi yanayolenga
jamii ya Waislamu au watu
wengine wanaodhulumiwa au
kwa ajili ya kuzuia uchokozi na
hujuma za adui.
Suala la kuishi kwa amani
na usalama na wasio
Waislamu limesisitizwa sana
katika aya za Qur'ani tukufu na
hadithi, sira na mwenendo wa
Mtume na Aali zake
watoharifu. Suala hili pia
limejengeka juu ya nguzo ya
utukufu wa kiumbe
mwanadamu. Katika mtazamo
wa Uislamu wanadamu wasio
Waislamu wana heshima na
utukufu wa kidhati na
kimaumbile kutokana na
kushirikiana kwao na
Waislamu katika maumbile na
ubinadamu japo
wanatofautiana katika dini na
imani. Uhakika huu
unathibitishwa na sira,
mwenendo na maisha ya
Mtume Muhammad (saw).
Mfano wa wazi wa
mwenendo huo wa amani na
suluhu na wasio Waislamu ni
Mapatano ya Ungwana
yaliyofikiwa baina ya Mtume
(saw) na washirikina wa
Makka kabla ya kutangazwa
dini ya Uislamu, Mapatano ya
Hudaibiyya, mwenendo wa
Mtume Muhammad (saw) na
jinsi alivyokuwa akiamiliana
na tawala na wafalme wa
maeneo mbalimbali kama Iran
na Roma na kutumia njia ya
kutuma barua kwa watawala
na wafalme wa zama hizo
baada ya kuunda dola la
Kiislamu mjini Madina. Kwa
mfano tu Mtume (saw) alisema
katika amri aliyompa Amru
bin Hazm wakati alipomtuma
Yemen kwamba: Kila Myahudi
au Mkristo atakayekubali
Uislamu na kudhihirisha
Uislamu halisi atakuwa
mmoja kati ya waumini,
atakuwa na haki sawa na za
Waislamu na kushirikiana
nao katika vipindi vyote vya
shida na raha. Na kila
mtu atakayeamua kubakia
katika dini yake ya Uyahudi
au Unaswara kamwe
hatalazimishwa kuacha dini
yake, kwa sababu ujumbe wa
dini na risala za Mitume wote
wa Mwenyezi Mungu ni
kuleta amani, uadilifu,
kueneza masuala ya
kiroho,kumkamilisha
mwanadamu na kumfikisah
kwenye saada na ufanisi",
mwisho wa kunukuu.
Kwa msingi huo, katika
mtazamo wa Uislamu suala la
usalama na kuishi kwa amani
na wanadamu wengine wenye
itikadi na imani tofauti, ni
jambo lenye thamani na
umuhimu mkubwa. Hii ni
kutokana na ukweli kwamba,
ni katika mazingira ya amani
na usalama ndipo wanadamu
wanapoweza kuelekea kwenye
ukamilifu wa kimaada na
kiroho, bali hata kuweza
kumjua na kumwabudu
Mwenyezi Mungu.
Hivyo suala la kujenga na
kuimarisha amani na usalama
na vilevile juhudi za kulingania
amani na usalama wa
kimataifa na kuishi pamoja
kwa amani wanadamu wote
kwa msingi wa Tauhidi na
kumpwekesha Mwenyezi
Mungu, uadilifu na usafi wa
nafsi bila ya kujali dini, rangi,
na tofauti zao nyingine ndio
lengo la mwisho la Uislamu na
wafuasi halisi wa dini hiyo. Ni
wazi kuwa, kufuata
mafundisho ya dini hiyo
kunaweza kuwa suluhisho la
kumwondoa mwanadamu
katika kinamasi cha vita,
mapigano na migogoro ya
dunia ya sasa.
Ndugu zangu waislamu
nimejaribu kutoa ufafanuzi
mrefu kidogo kuhusu uislamu
na amani.Dini zote hapa
duniani zinahubiri amani.Hata
akija kiongozi wa dini ya
kikristu ataeleza namna biblia
takatifu inavyosisitiza
amani.Ninawataka ndugu
waislamu na wasio waislamu
mnaonisikiliza hivi sasa kokote
mliko wekeni silaha zenu chini
na turejee kuishi kwa amanai
kama ilivyokuwa hapo
kabla.Tuiachie serikali ilifanyie
uchunguzi jambo hili tujue
nani katufikisha hapa? Nani
waliotufarakanisha hadi ndugu
tukaanza kuuana? Nawasihi
tuweke mbele maslahi ya nchi
yetu.Tuna nchi moja tu na
tazameni kilichotupata baada
ya kuvuruga amani.Tumekosa
hata sehemu ya kukimbilia
kwani sisi kwa miaka mingi
tumekuwa ni kimbilio la wale
wote ambao amani imepotea
katika nchi zao.
Mufti alimaliza hotuba
yake kwa kuendelea
kuwasisitiza waumini wa dini
ya kiislamu na wa dini
nyingine kuachana na vurugu
ili amani irejee.Baada ya
kumaliza kutoa hotuba Mufti
na Dr Fabian wakaenda
kupata chakula cha mchana
pamoja.
WASHINGTON DC –
MAREKANI
Saa tano za asubuhi, Mark
Piller makamu wa Rais wa
Marekani aliwasili katika
nyumba kubwa aliyokuwa
akiishi jenerali Akiki
Rwamirama.Lilikuwa ni jumba
kubwa la kifahari lililokuwa na
viwanja vya michezo mbali
mbali kama vile mpira wa
kikapu,mpira wa wavu na
tenisi.Kulikuwa na miti mingi
kulizunguka jumba hilo na
kulifanya kuwa na utulivu
mkubwa,ni sauti za ndege
mbali mbali ndizo zilisikika.
Jenerali Akiki hakuwa na
taarifa kama Mark Piller
angekwenda
kumtembelea.Alikuwa ndani
ya sebule kubwa akitazama
runinga akifuatilia taarifa za
habari za vyombo mbali mbali
vya habari duniani na kubwa
alilokuwa analifuatilia ni
taarifa za kuhusiana na kile
kilichokuwa kinaendelea
Afrika mashariki hususan
nchini Uganda.
Mlango mkubwa wa
sebuleni ukagongwa na mmoja
wa walinzi wake akaenda
kuufungua akakutana na
walinzi wa makamu wa
Rais.Nje tayari msafara wa
makamu wa Rais ulikwisha
wasili na alikwisha shuka
akipiga hatua kuelekea
ndani.Jenerali Akiki
alipojulishwa kuwa ni makamu
wa Rais amefika akainuka
haraka na kwenda kumpokea
“Mheshimiwa Rais habari
yako” akasema Mark Piller
“Mark niite Akiki
inatosha.Hayo mambo ya Rais
yamekwisha pita.Mimi si Rais
tena wa Uganda” akasema
Jenerali Akiki
“Jenerali Akiki sisi
tunaendelea kukutambua
kama Rais halali wa Uganda
hivyo tutaendelea kukupa
heshima yako ya Rais”
akasema Mark
“Nashukuru sana
Mark.Karibu”
“Ahsante jenerali
Akiki.Tunaweza kutembea
tafadhali” akasema Mark na
Jenerali Akiki akamuongoza
wakaelekea katika uwanja wa
gofu.
“Jenerali Akiki vipi maisha
yako yanakwendaje
hapa?Unayafurahia?akauliza
Mark Piller
“Maisha yanakwenda
vizuri sana mheshimiwa
makamu wa Rais.
Ninayafurahia maisha.Tayari
akili yangu imekwisha anza
kuzoea maisha haya.Kwa
ujumla hakuna tatizo
lolote.Ninashukuru sana kwa
namna
mnavyonihudumia.Ninapata
kila ninachokihitaji”akasema
Jenerali Akiki
“Ninafurahi kusikia hivyo
mheshimiwa Rais.Ninakuahidi
utaishi maisha mazuri kama
uko peponi.Utapata kila
unachokihitaji na utayasahau
maisha yako yaliyopita”
akasema Mark Piller
“Ahsante
Mark.Sikutegemea kama
baada ya kuondolewa
madarakani ningekuwa na
maisha mazuri kama
haya.Washenzi wale
wametaifisha mali zangu zote
na bila ninyi ningekuwa
masikini wa kutupwa”
akasema Jenerali Akiki
“Niliwahi kukwambia
Jenerali Akiki kwamba
yanapofanyika mapinduzi rais
aliyepinduliwa mara nyingi
lengo huwa ni kumuua lakini
kama akinusurika akakimbia
basi mali zake zote ndani na
nje ya nchi hutaifishwa na
serikali iliyochukua
madaraka.Lakini hilo
lisikuumize kichwa kwa sasa
wewe ni tajiri na utakuwa na
mali mara mbili zaidi ya zile
ulizokuwa nazo ulipokuwa
madarakani.Hata kama
ukitaka familia basi unao
uwezo wa kuanzisha familia
tena kubwa.Kila kitu
kinawezekana mheshimiwa
Akiki”akasema Mark Piller
“Mambo yanaendeleaje
Afrika Mashariki ?akauliza
Jenerali Akiki
“Mambo yanakwenda
vizuri mheshimiwa Akiki.Meli
zetu kubwa za mafuta
zimepanga foleni katika
bandari ya Tanga zikipakia
mafuta.Kwa ujumla kila kitu
kinakwenda vyema”
“Safi sana.Nataka
ikiwezekana mchukue mafuta
yote yaliyopo Uganda
muyalete huku kwa watu
ambao wana shukrani na
utu.Nimeijenga Uganda lakini
shukrani zake ni hizi.Mark
kama upo uwezekano wa
kuongeza zaidi uchukuaji wa
mafuta fanyeni hivyo
tafadhali”akasema Jenerali
Akiki
“Jenerali Akiki hilo ndilo
lililonileta hapa kwako.Jana
nilikuwa na mazungumzo
marefu na Rais kuhusiana na
mpango huu
unaoendelea.Katika
mazungumzo yetu
tumekubaliana kwamba
tutanue zaidi operesheni
hii.Unajua Afrika Mashariki ni
tajiri sana.Tunataka tusiishie
kwenye mafuta peke tunataka
twende mbali zaidi tuingie
hadi katika rasilimali nyingine
kama vile madini.Nchi kama
Tanzania imebarikiwa madini
ya kila aina.Nchi kama
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo nayo vile vile ina
madini ya thamani.Tanzania
kwa mfano ina madini ya
dhahabu,almasi,na mengine
mengi bila kusahau madini ya
Tanzanite ambayo
hayapatikani sehemu nyingine
yoyote duniani zaidi ya
Tanzania pekee.Tunataka
operesheni yetu sambamba na
mafuta iende pia katika
maeneo hayo
niliyoyataja.Nimekuja hapa
kwako kupata ushauri
unadhani nini tufanye kutanua
operesheni hii Afrika
mashariki? Akauliza Mark
Piller
“Mheshimiwa makamu wa
Rais tena imekuwa vizuri
umefika.Muda mfupi kabla
hujafika hapa nilikuwa
natazama kile kinachoendelea
Afrika mashariki.Leo kuna
jambo limetokea nchini
Tanzania”
“Kumetokea nini Tanzania
?akauliza Mark Piller
“Rais wa Tanzania
amekutana na Sheikh mkuu
wa Tanzania na wamekuwa na
kikao kirefu wakizungumzia
vurugu zinazoendelea.Kikao
hicho kinaonekana kuwa na
mwelekeo mzuri wa kumaliza
vurugu hizo
zinazoendelea.Nimezisikiliza
hotuba aliyoitoa Mufti na kwa
kiasi kikubwa inaweza
kuwashawishi waumini
kuachana na vurugu
zinazoendelea.Kwa kawaida
waumini wa dini ni watiifu
mno kwa viongozi wao hivyo
kama wameambiwa na
kiongozi wao waache vurugu
basi watafanya
hivyo.Watanzania ni wepesi
sana wa kumaliza mambo kwa
amani na kwa mujibu wa
taarifa ambayo imetolewa
leo,tayari vurugu zimeanza
kupungua nchini Tanzania na
hii inatokana na hotuba ya
jana ya Rais Dr Fabian”
akanyamaza akamtazama
Mark Piller
“Mpango huu uliojadiliana
na Rais wako ni mpango mzuri
sana na wenye manufaa kwa
Marekani lakini ili mpango
huo ufanikiwe tunaihitaji mno
Tanzania.Vurugu lazima
ziendelee nchini Tanzania ili
majeshi ya Marekani
yaendelee kukaa nchini humo
na kama ikiwezekana basi
wanajeshi waongezezwe
zaidi.Tanzania haitakiwi ipate
amani kwani ikiwa shwari
hakutakuwa na ulazima wa
vikosi vya Marekani kuendelea
kuwepo na hivyo hatutaweza
tena kuendelea na uchukuaji
wa mafuta na rasilimali
nyingine” akasema Jenerali
Akiki
“Nini unashauri kifanyike
Jenerali Akiki? Tunategemea
sana ushauri wako kwa kuwa
wewe unalifahamu vyema eneo
la Afrika mashariki.Ushauri
wowote utakaoutoa
tutauzingatia” akasema Mark
Piller
“Kunatakiwa kufanyike
kitu cha haraka sana
kuhakikisha hali inaendelea
kuwa tete nchini Tanzania ili
vikosi vya Marekani viendelee
kukaa huko kwa muda mrefu
zaidi na kama ikiwezekana
viongezwe vikosi vingine”
akasema Jenerali Akiki
“Nini basi unashauri
kifanyike kwa haraka?Mimi na
mheshimiwa Rais tulifikiria
kuanzisha kikundi cha waasi
ambacho tutakiwezesha kwa
silaha na zana nyingine za
kijeshi ambacho kitaendesha
mapigano na serikali za Afrika
mashariki ili tupate nafasi ya
kuongeza wanajeshi zaidi
katika eneo la Afrika
Mashariki.Unaonaje kuhusu
mpango huo?akauliza Mark
Piller
“Huo ni mpango mzuri
lakini si muafaka kwa
sasa.Kuanzisha kikundi cha
waasi ni mpango wa muda
mrefu.Si jambo jepesi
kuanzisha uasi hasa katika
nchi kama Tanzania.Kwa nchi
ya jamhuri ya kidemo krasia ya
Congo kule hakuna shida
kwani wamekwisha zoea
mambo kama hayo lakini kwa
sasa tunalenga zaidi Tanzania
hivyo wazo la kuanzisha
kikundi hicho cha uasi
tuliweke pembeni
tutalishughulikia
taratibu”akasema Jenerali
Akiki
“Vipi kuhusu kuwatumia
IS kufanya mashambulio mbali
mbali ya kigaidi na kuua
watu?akauliza Mark Piller
“Hilo nalo ni wazo zuri
lakini bado si mpango mzuri
tunaouhitaji kwa
sasa.Tunatakiwa kufanya kitu
cha haraka”
“Nini basi unashauri
kifanyike kwa haraka jenerali
Akiki?akauliza Mark Piller na
Jenerali akiki akainamisha
kichwa akafikiri kisha akasema
“Hapa Marekani mnao
wanasayansi wa hali ya
juu.Nataka muwatumie
wataalamu hao kutengeneza
kirusi ambacho kitakuwa ni
hatari na ambacho kinaweza
kusababisha maangamizi
makubwa kitakachokwenda
kusambazwa nchini Tanzania”
“Kirusi? Akauliza Mark
Piller
“Ndiyo Mark.Mnatakiwa
kutengeneza kirusi ambacho
kinaweza kuwa hatari zaidi na
kwenda kukisambaza nchini
Tanzania ambacho kitasambaa
kwa haraka zaidi na
kusababisha vifo vya watu
wengi.Baada ya hali kuwa
mbaya Marekani itaongeza
wanajeshi Tanzania kwa lengo
la kwenda kutoa msaada wa
kibinadamu.Faida za mpango
huu ni kwamba vikosi vya
Marekani vitaongezwa na
kukaa kwa muda mrefu Afrika
mashariki na kuendelea
kuchukua mafuta na rasilimali
nyingine kama madini”
akasema Jenerali Akiki
“Jenerali Akiki wazo lako
ni zuri lakini linaonekana ni la
hatari kubwa.Wasi wasi wangu
ni vipi kama kirusi hicho
kitaweza kuvuka katika
mipaka ya Tanzania na
kusambaa sehemu mbali mbali
duniani na hatimaye kikafika
hadi Marekani? Tunaweza
kuwa tumetengeneza silaha
ambayo inakuja kutuua sisi
wenyewe.Wanajeshi wetu
walioko Tanzania wanaweza
wakaambukizwa ugonjwa huo
wakafa au wakaja kusambaza
virusi hivyo huku Marekani”
“Mark Piller hiyo ndiyo
njia pekee na ya haraka
ambayo mnaweza mkaitumia
ili vikosi vya Marekani
viendelee kukaa Afrika
Mashariki na hasa
Tanzania.Wanasayansi wenu
watakapotengeneza kirusi
hicho hatari watatengeneza pia
na kinga yake na wanajeshi
watakaokuwa Tanzania na
wale watakaopelekwa huko
watapata kinga hiyo hivyo wao
hawatadhurika na hicho
kirusi” akasema Jenerali
Akiki.Mark Piller alishindwa
ajibu nini wakabaki
wamesimama wakitazama
farasi kila mmoja akiwaza lake.
“Unalionaje wazo hilo
Mark?akauliza Jenerali Akiki
“Jenerali Akiki
ninashindwa kukupa jibu la
haraka haraka kwani mpango
huu ni mkubwa na wa hatari
sana”
“Nini hofu yako
Mark?akauliza Jenerali Akiki
“Hofu yangu ni kwamba
tunaweza kutengeneza kirusi
hicho hatari halafu kikageuka
na kuwa kisu cha
kutuangamiza sisi
wenyewe.Kitu kama kirusi
kinaweza kusambaa kwa
haraka sana na kufika hadi
Marekani kitu ambacho
hatutaki kitokee na ndiyo
maana umeona Marekani
hatupigani vita nyumbani
tunamfuata adui huko huko
aliko.Tunataka raia wetu wawe
salama siku zote ndiyo maana
ninahofu kwamba tunaweza
kutengeneza kirusi na
kikasambaa na kufika hadi
Marekani na kuua watu wetu”
akasema Mark Piller
“Hakuna haja ya kuwa na
hofu Mark.Nimesema
wanasayansi watengeneze
kirusi na kinga yake na kila
juhudi lazima zifanyike
kuhakikisha kwamba kirusi
hicho hakivuki nje ya mipaka
ya Tanzania.Mzilenge nchi za
Tanzania,Uganda na jamhuri
ya kidemokrasia ya
Congo.Tena mkitaka
kufanikiwa zaidi tengenezeni
kirusi ambacho kitasambaa
kwa njia ya hewa ili kiweze
kusambaa kwa haraka
zaidi.Nakuhakikishia Mark
kwamba hii ndiyo njia pekee
nyepesi ya kuweza kuongeza
vikosi Afrika mashariki na
kuendelea kuchota
rasilimali.Njia nyingine kama
makundi ya waasi hizo zitakuja
baadae” akasema Jenerali
akiki
“Jenerali Akiki naomba
nilichukue suala hili na
kwenda kujadiliana na
wenzangu tuone namna
tutakavyoweza kulitekeleza
lakini ni suala zuri na ahsante
sana kwa wazo hili zuri”
akasema Mark Pilller
“Mark muda unakwenda
kwa kasi na taratibu amani
imeanza kurejea Tanzania na
kama Tanzania ikiwa na amani
basi hata Uganda nako
kutakuwa na amani.Hampaswi
kuacha jambo hili likatokea
.Wakati wakiendelea na
mikutano yao ya kutafuta
amani wanatakiwa wapigwe
tena pigo lingine kabla
majeraha yao hayajapona”
akasema Jenerali Akiki
“Ahsante sana jenerali
Akiki tutalizingatia
hilo.Ninakwenda kuzungumza
na wenzangu halafu nitakupa
mrejesho nini tumekubaliana.
RIYADH – SAUDI ARABIA
Kiza kimeanza kutanda
katika anga la jiji la
Riyadh.Katika makazi ya
Habiba Jawad idadi ya watu
waliofika kuhudhuria msiba
wa mwanae Najma aliyezikwa
mchana wa siku hiyo baada ya
kujiua kwa kujipiga risasi
ilikuwa kubwa.Ulikuwa ni
msiba mkubwa kwa Habiba
Jawad ambaye huyu alikuwa ni
mtoto wake wa pili kufariki
baada ya Edger Kaka.
Wakati watu wakiendelea
na maombolezo Habiba Jawad
aliyekuwa katika mojawapo ya
nyumba zilizopo katika makazi
yake akiwa na akina mama
waliofika kumfariji, simu yake
ikaita akaitoa haraka haraka
kutazama mpigaji kisha
akaikata ile simu.Taratibu
akainuka na kuaga anakwenda
maliwato.Hakutaka mtu yeote
amsindikize.Alitoka ndani ya
ile nyumba akafuata ujia
kuelekea katika nyumba yake
na moja kwa moja akaenda
katika ofisi yake akawasha
runinga kubwa na akaonekana
David Walker.
“Habari yako Habiba”
akasema David Walker
“Nzuri David habari yako”
“Habiba unaonekana
hauko sawa leo.Kuna tatizo
lolote?akauliza David
“Nina msiba
David.Mwanangu amefariki
jana na leo tumemzika”
“Pole sana
Habiba.Hukutujulisha kama
una msiba”
“Usijali David.Nini
kinaendelea huko? Akauliza
Habiba
“Habiba kuna jambo
ambalo limejitokeza na
tunahitaji msaada wako”
“Sema David nini
mnahitaji?akauliza Habiba
“Tumekuwa tunafuatilia
kwa karibu sana kile
kinachoendelea Tanzania na
siku ya leo Rais wa Tanzania
amekutana na kiongozi wa dini
na kubwa walilolizungumza ni
kuhusiana na vurugu
zinazoendelea katika ukanda
huo wa Afrika
mashariki.Mazungumzo hayo
ya leo kati ya rais na kiongozi
huyo yanaonekana kwa na
mwelekeo wa kumaliza vurugu
zile za kidini zinazoendelea
Afrika Mashariki.Endapo
vuruguzile zitamalizika basi
hakutakuwa na ulazima wa
vikosi vyetu kuendelea kuwepo
Afrika mashariki na lengo letu
ni kuendelea kukaa hapo kwa
muda mrefu na hata kuongeza
wanajeshi zaidi.Kwa hiyo
tumeamua kufanya kitu cha
haraka ambacho
kitatuwezesha kupeleka vikosi
zaidi vya jeshi na kukaa Afrika
mashariki kwa muda mrefu
zaidi” akasema David Walker
“Mmekuja na mpango
gani? Habiba akauliza
“Tunataka kutengeneza
kirusi ambacho kitafanya
maangamizi makubwa
ambacho kitakuwa hatari
kuzidi kirusi cha
Ebola.Tutakwenda
kukisambaza kirusi hicho
Tanzania na baada ya hali
kuwa mbaya tutatuma vikosi
zaidi vya jeshi kwenda huko
kwa lengo la kutoa msaada
lakini papo hapo operesheni
zetu zikiendelea kama
kawaida”
“David hili la kusambaza
kirusi huoni kama ni jambo la
hatari?Ni vipi kama kirusi
hicho kitavuka mipaka na
kusambaa sehemu nyingine
duniani?Mnao wanajeshi wenu
kule ni vipi kama wakipata
virusi hivyo? Akauliza Habiba
“Hilo tayari tumekwisha
lijadili kwa kirefu
sana.Mwanasayansi
anayeandaa kirusi hicho
tumempa maelekezo ya
kuhakikisha kwamba
atakapokamilisha kutengeneza
kirusi hicho aandae na kinga
yake kwa ajili ya wanajeshi
wetu na tahadhari endapo
kirusi hicho kitavuka mipaka
ya Afrika Mashariki na kuenea
sehemu nyingine duniani.Hilo
halina tatizo kabisa Habiba”
“Nini natakiwa kufanya
kwa upande wangu?akauliza
Habiba ambaye hakuonekana
kutaka maongezi marefu
“Kwa upande wako
tunataka utusaidie kupata mtu
ambaye atapeleka kirusi hicho
Tanzania.Tunataka mtu
kutoka kundi la IS”akasema
David
“David kwa nini lazima
awe ni mtu kutoka IS?akauliza
Habiba
“Habiba hili ni shambulio
la kibaolojia hivyo basi mtu
huyo hapaswi kuwa
mmarekani.Tunataka
kumtuma mtu wa kundi la IS
ili hata kama akigundulika basi
ijulikane kuwa ni kundi la IS
ndio waliofanya shambulio
hilo.Nataka ufanye
makubaliano na kundi la IS
wape fedha za kutosha waweze
kutupatia huyo mtu ambaye
anatakiwa hapa Marekani
haraka sana ili aanze
kuandaliwa.Mtu huyo
atawekewa kwanza kinga ya
kumkinga dhidi ya kirusi hicho
halafu atapandikizwa kirusi
hicho ambacho atakwenda
kukisambaza Tanzania”
akasema David Walker
“Lini huyo mtu
anahitajika?akauliza Habiba
“Tunamuhitaji haraka
iwezekanavyo.Tunataka kabla
ya amani haijarejea Tanzania
basi tuwapige na hicho
kirusi.Hatutaki kuwapa nafasi
ya kupumua.Namuhitaji huyo
mtu haraka sana.Fanya kila
uwezalo mtu huyo aweze
kupatikana haraka sana”
akasema David
“Sawa David nitajitahidi”
“Ahsante sana Habiba na
pole sana kwa tatizo hili
kubwa.Kuna chochote
tunaweza kusaidia?
“Ahsante
David.Tutawasiliana pale
nitakapokuwa nimempata
huyo mtu” akasema Habiba na
kuzima ile runinga
“Mauaji yanayoendelea
hivi sasa nchini Tanzania bado
hayatoshi na wanataka
kusambaza tena virusi na
kuendelea kuua watu.Yote hii
ni kwa sababu ya kutaka
kuchukua rasilimali ambazo
Mungu amewajalia watu wa
Afrika Mashariki.Lazima
nitafute namna ya kufanya ili
niweze kuzuia mpango huu
usifanikiwe.Ningeweza
kumpigia simu Mathew
Mulumbi lakini sifahamu
mahala alipo hivi sasa.Hata
hivyo lazima nifanye kitu.Huu
lazima uwe ni mwisho wa hiki
kikundi chenye kufanya
maangamizi makubwa
duniani” akawaza Habiba na
kuwasiliana na mtu mmoja
kutoka kundi la IS akampa
maelekezo kama alivyokuwa
ameelekezwa na David na mtu
Yule akamtaka Habiba ampe
muda alishughulikie lile suala
kisha atamjulisha.Alimtajia
kiasi cha fedha ambacho
angetakiwa kukitoa kwa ajili ya
suala lile.Baada ya kulimaliza
hilo suala Habiba akarejea
katika nyumba waliko akina
mama waliokuja kuungana
naye katika msiba.
Saa tatu za usiku
wakawasili Abu Dahir na mke
wake Nawal.Kama ilivyokuwa
kwa Mathew na Najma nao pia
walikuwa
mapumzikoni.Habiba Jawad
aliwapa wanae wote
mapumziko ya miezi
minne.Abu Dahir na Nawal
hawakuweza kuwahi mazishi
ya Najma kutokana na
kutopata taarifa kwa
haraka.Baada ya kuwasili Abu
Dahir alikwenda kuungana na
waombolezaji wengine
waliofika pale nyumbani
kuwafariji.Nawal yeye
alikwenda kuungana na akina
mama waliokuwa wanamfariji
Habiba.
Saa tano za usiku tayari
watu wengi walikwisha
ondoka.Ni watu wachache tu
waliokuwa wamebaki na ndipo
Abu Dahir alipoweza kupata
nafasi ya kuzungumza na
mama yake ili aweze
kumueleza kile kilichotokea
hadi kupelekea Najma kujiua
kwa kujipiga risasi.Habiba
Jawad akawataka Abu Dahir
na Nawal waelekee nyumbani
kwake akawakaribisha katika
sebule yake
“Mama utatusamehe sana
kwa kushindwa kuwahi
mazishi ya Najma.Tuliipata
taarifa kwa kuchelewa na
tulijitahidi sana kwa kila
namna ili tuweze kuwahi leo
lakini ilishindikana ” akasema
Abu Dahir
“Usijali Abu.Nilifahamu
hamtaweza kuwahi mazishi”
akasema Habiba
“Mama nini hasa
kilichotokea? Kwa nini Najma
alijiua?Abu Zalawi yuko
wapi?akauliza Abu Dahir
akionekana kuwa na shauku
sana ya kutaka kufahamu kila
kitu kuhusiana na tukio lile.
“Poleni sana vijana wangu
kwa hiki kilichotokea.Mpaka
sasa bado siamini kama kweli
Najma binti yangu wa pekee
amekwenda na hatutamuona
tena.Najma ameondoka na
afya na uzuri
wake.Imeniumiza sana”
akasema Habiba Jawad
“Nini hasa kimetokea
mama hadi kupelekea Najma
kuchukua maamuzi haya
magumu namna hii? Akauliza
Abu Dahir
“Ni hadithi ndefu Abu
lakini lazima nikiri kwamba
mimi ndiye niliyesababisha
kifo chake”
“Wewe ndiye uliyesabisha
kifo chake? Kivipi mama? Abu
Dahir akauliza
“Sikumuua kwa mkono
wangu lakini kuna maneno
nilimueleza na hayo ndiyo
yaliyopelekea akachukua
maamuzi yale ya kujiua”
“Ulimweleza nini mama?
Akauliza Nawal na Habiba
akamtazama Abu Dahir kisha
akasema
“Nilimueleza ukweli”
“Ukweli? Abu Dahir
akashangaa
“Ndiyo Abu.Dada yako
nilimueleza ukweli”
“Sijakuelewa
mama.Ukweli upi uliomueleza
hadi akaamua kujipiga risasi?
Abu Dahir akauliza
“Kuna mambo mengi
ambayo wewe na ndugu zako
hamkuwa mkiyafahamu hasa
kuhusu mimi na kile
kinachoendelea katika maisha
yangu.Nadhani ni wakati wa
kuweka mambo wazi ili wewe
pia ufahamu” akasema Habiba
na Nawal akasimama
“Nawal unakwenda wapi?
Habiba akauliza
“Ninadhani mazungumzo
haya yanawahusu zaidi ninyi”
akasema Nawal
“Hapana Nawal kaa.Wewe
pia ni mwanafamilia na ni
sehemu ya haya ninayotaka
kuyazungumza.Umefika
wakati wa kila kitu kuwekwa
mahala peupe” akasema
Habiba
“Huyu mama anataka
kufanya nini tena?Mbona
muelekeo wake
siuelewi?akajiuliza Nawal
“Mama kabla hujaendelea
nataka kufahamu yuko wapi
Abu Zalawi? Abu Dahir
akauliza
“Abu Zalawi hayupo na
hajui kama mke wake Najma
amefariki dunia”
“Hajui kuhusu kifo cha
Najma? Akauliza Nawal
“Ndiyo hajui chochote
kuhusu kifo cha Najma”
“Mama nashindwa
kuelewa.Hawa walikwenda
mapumzikoni kama
tulivyofanya sisi.Nini kili…..”
“Niliwarudisha mimi”
akasema Habiba na
kumkatisha Abu Dahir
“Nilimuhitaji Abu Zalawi
hivyo nikawasiliana nao na
kuwataka warudi nyumbani
mara moja.Baada ya kurejea
mimi na Abu Zalawi tulifanya
safari ya kwenda Marekani na
Abu Zalawi alibaki huko”
“Alibaki huko? Nawal
akauliza
“Ndiyo.Alibaki huko na
ninapenda kuwajulisha
kwamba AbuZalawi hatarejea
tena hapa kwetu.Amekwisha
ondoka katika maisha yetu”
“Mama sijakuelewa.Nini
kinaendelea hapa? Mama
naomba tafadhali unieleze kila
kitu.Naona kuna mambo
mengi yamejificha
hapa”Akasema Abu Dahir
“Abu kama unavyofahamu
kwamba baba yako alikuwa
mstari wa mbele sana katika
kupigania haki na aliuawa
akiwa katika mapambano ya
kudai haki za
wapalestina.Baada ya kifo
chake nilivaa viatu vyake na
kuendelea na harakati za kudai
haki.Nimekuwa nikitoa
msaada wa kifedha kwa
vikundi mbali mbali
vinavyoendesha harakati za
kudai haki za wapalestina
kutoka kwa taifa la Israel.Si
vikundi vya kipalestina tu
ambavyo vimekuwa vikipokea
msaada kutoka kwangu katika
kufanikisha harakati mbali
mbali za kudai haki bali
nimekuwa nikifadhili makundi
mengine kama vile IS
kufanikisha mipango yao
mbali mbali.Kundi la IS
linajulikana kama kundi hatari
zaidi la kigaidi kwa sasa
duniani na kitendo cha
kulifadhili kimenifanya
niwindwe na mashirika mbali
mbali ya kijasusi na hasa
Mossad.Pamoja na kuwindwa
huko na Mossad lakini hadi leo
hii hawajawahi
kunikamata.Umeshawahi
kujiuliza swali kwa nini?
Akauliza Habiba na Abu Dahir
akatikisa kichwa kwamba
hajaui.
“Kuna siri imejificha hapa
kwa nini sijawahi kukamatwa
licha ya kutajwa kuwa mfadhili
mkubwa wa makundi ya ugaidi
duniani” Habiba akanyamaza
na kuwatazama Abu Dahir na
Nawal
“Siri ambayo
hamuifahamu ni kwamba
ninafanya ufadhili huu kwa
makundi ya magaidi kwa niaba
ya Marekani”
“Marekani ? Abu Dahir
akashangaa
“Ndiyo Abu.Mimi ni
wakala wao.”
“Marekani wanafadhili
ugaidi? Abu akazidi kushangaa
“Ni vigumu kuamini Abu
lakini huo ndio ukweli”
“Marekani imekuwa
ikiendesha vita dhidi ya ugaidi
duniani na tumekuwa tukiona
namna inavyopata mafanikio
makubwa katika vita dhidi
hiyo.Iweje kwa upande wa pili
wawe na ushirika na magaidi?
Akauliza Abu
“Hiyo ni siri kubwa Abu
Dahir.Ni siri ambayo hata Rais
wa Marekani haifahamu”
akasema Habiba na
kunyamaza kidogo
“Ndani ya shirika la
ujasusi la Marekani CIA kuna
kitengo maalum ambacho
kinashughulika na jambo
hilo.Ni kitengo cha siri sana na
hata waliomo ndani ya CIA
hawakifahamu” Habiba
akanyamza baada ya Nawal
kuonyesha mshangao
“Kitengo hiki kazi yake
kubwa ni kushughulikia
mahusiano na makundi ya
kigaidi kwa maslahi ya
Marekani.Baba yako ndiye
aliyekuwa akitumiwa katika
kufadhili ugaidi na aliuawa
baada ya kwenda kinyume na
matakwa ya Marekani.Baada
ya kuuawa nilivaa viatu vyake
na kuendelea na kile
alichokuwa anakifanya”
“Siamini hayo
unayonieleza mama.Kwa muda
huu wote mmekuwa mkifanya
kazi kwa niaba ya Marekani?
“Ndiyo Abu.Tumekuwa
tukifanya kazi kwa niaba ya
Marekani.Alianza baba yako
na mimi nimefuata na utajiri
huu wote tulionao umetokana
na hicho
tunachokifanya.Wameniwezes
ha utajiri mkubwa niweze
kuutumia kufadhili ugaidi kwa
niaba yao.Hawataki
kujulikana”
“Kwa nini ukakubali mama
kubeba jukumu hili kubwa
mabegani mwako?Kwa nini
ukakubali kuchafua jina lako
kwa kuwa mfadhili wa ugaidi
duniani wakati kumbe
wafadhili wakuu wa ugaidi
wapo? Akauliza Abu Dahir
“Ilikuwa ni lazima nifanye
hivyo Abu.Hii imekuwa ni siri
yangu kubwa sana na
sikupanga kuwaeleza lakini
imebidi mfahamu kila kitu”
akasema Habiba
“Kwa nini umeamua
kutueleza mama? Akauliza
Nawal
“Kwa sababu ni wakati
muafaka kwa ninyi kufahamu
kile kinachoendelea” akajibu
Habiba
“Kama nilivyokueleza Abu
kwamba baba yako ndiye
aliyekuwa wa kwanza kuifanya
kazi hii na mimi niliendelea
pale alipoishia
yeye.Nimeifanya kazi hii kwa
muda mrefu kwa maslahi ya
marekani na sasa umefika
wakati ambao sitaki kuendelea
tena na hiki ninachokifanya
kwani hakipendezi machoni pa
Mungu.Nimekwisha kuwa
mzee sasa na ninahitaji
kujiweka karibu na Mungu
wetu na sitaki tena kuendelea
kukatili roho za watu wasio na
hatia.Katika makubaliano yetu
na kikundi hiki ni kwamba
nitaifanya kazi hii ya kufadhili
ugaidi kwa niaba yao hadi pale
nitakapovuta pumzi yangu ya
mwisho na ndiyo maana
wameniwezesha kuwa na
utajiri mkubwa sana.Kitendo
chochote cha kutaka kujiondoa
katika jambo hili ni
kuhatarisha usalama wangu na
wa familia yangu.Hivi
tuzungumzavyo ninyi wanangu
wote mnafuatiliwa na muda
wowote ambao nikijaribu
kwenda kinyume na matakwa
yao watawaondoa ndiyo
maana nimekuwa kimya
sijawahi kuwaeleza kuhusu
jambo hili.Nataka muwe
salama” akasema Habiba
“Unataka tuwe salama?
Akauliza Abu Dahir kwa ukali
“Abu chunga ulimi wako
unapozungumza nami !
akafoka Habiba akionekana
kutopendezwa na namna
mwanae alivyouliza kwa ukali
“Mama ingekuwa vyema
ungeendelea kubaki na siri hii
na ukafa nayo.Kuamua
kutueleza ukweli ni
kuhatarisha zaidi maisha
yetu.Tazama umemueleza
ukweli Najma na akaamua
kujiua” akasema Abu Dahir
“Abu imenilazimu
niwaeleze ukweli ili hata
ikitokea nikiondoka leo mjue
ni kitu gani kilikuwa
kinaendelea katika maisha
yangu” akasema Habiba na
kunyamaza akamtazama Abu
“Ili niweze kujiondoa
katika jambo hili ilinilazimu
kuja na mpango maalum na
hapo ndipo nilipoamua
kuwaleta hapa Abu Zalawi na
Nawal” akasema Habiba na
kunyamaza.Nawal alionyesha
wasi wasi mwingi
“Abu Dahir,kuna jambo
ambalo hujalifahamu bado”
akasema Habiba
“Mama una siri nyingi
umetuficha.Tafadhali kama
umeamua kueleza ukweli
tueleze kila kitu” akasema Abu
Dahir
“Ni kuhusu Abu Zalawi na
Nawal” akasema habiba
“Mama” akaita Nawal
“Nawal muache mama
aseme anachotaka kukisema”
akasema Abu Dahir
“Nawal usiwe na
hofu.Nataka kila kitu kiwe
wazi leo” akasema Habiba
“Endelea mama.Kuna nini
kuhusiana na hawa watu
wawili? Akauliza Abu Dahir
“Abu Zalawi na Najma
nimewatoa katika lililokuwa
kundi la Ammar Nazari
brigades.Wawili hawa ni
majasusi na walikuwa katika
misheni maalum na siyo
magaidi.Niliamua kuwachukua
na kushirikiana nao kwa ajili
ya kw……….”
“Mama
sijakuelewa.Umesema Nawal
na Abu Zalawi ni majasusi na
si magaidi?Nawal si alikuwa
mke wa Ammar Nazari?
Akauliza Abu Dahir na kabla
Habiba hajajibu Nawal
akasimama
“Ni kweli Abu Dahir hiki
anachokisema mama yako”
Akasema Nawal na kutazama
na Abu
“Siamini masikio yangu !
akasema Abu Dahir
“Mama yako ameamua
kuweka kila kitu wazi hivyo
hakuna haja ya kuficha
chochote.Ni kweli mimi na
Abu Zalawi ni majasusi na
tulikuwa katika kundi la
Ammar Nazari Brigades kwa
misheni maalum.Mimi ni
jasusi toka CIA Marekani na
mwenzangu Abu Zalawi
anatokea Mossad.Jina lake
halisi ni Mathew Mulumbi na
si Abu Zalawi kama
anavyojulikana.Katika kundi la
Ammari Nazari Brigades mimi
nilikuwa na kazi ya kumsaka
gaidi mmoja ambaye ana
undugu na Ammar Nazari
ambaye aliwahi kufanya
mauaji makubwa Marekani na
kukimbia hivyo niliuganishwa
na Ammar na nikawa mke
wake.Abu Zalawi yeye alitokea
Mossad na alikuwa na misheni
maalum aliyotumwa
kuitekeleza ambayo ni kumuua
Habiba Jawad.Mossad
wanafahamu kwamba Habiba
amekuwa akifadhili makundi
mbali mbali ya wanamgambo
wa kipalestina ambao
wamekuwa wakiendesha
mashambulio mbali mbali
ndani ya Israel hivyo
wanamtafuta sana Habiba na
wakamtumia Abu Zalawi ili
kuungana na Ammari Nazari
na kutengeneza njia ya kufika
kwa Habiba Jawad.Baada ya
Ammar Nazari kuuawa na
vikosi vya Israel mimi na Abu
tuliondoka na kuanza harakati
za kumsaka Habiba Jawad
lakini tulipofika hapa misheni
ikabadilika.Ile mipango ya
kumuua Habiba Jawad
ikatoweka na badala yake
tukajikuta tukiungana na
Habiba Jawad katika mipango
yake na kuwa wanafamilia”
akasema Nawal na Abu Dahir
akaonekana kuchanganyikiwa.
“Abu Zahir anachokisema
mama yako ni………..” akasema
Nawal na Abu
akamnyamazisha
“Nyamaza ! akasema Abu
Dahir kwa sauti kali
“Wewe na huyu
mwanamke wote mko
sawa.Wote mama yenu
mmoja.Wote ni mashetani
waongo wakubwa.Nawal
nilikupenda sana na nikawa
tayari kufanya chochote kwa
ajili yako.Kwa nini nawe
ukashiriki uongo huu mkubwa
wa mama? Na wewe mama
kwa nini ukanishawishi
nimuoe Nawal wakati
ukifahamu kwamba ni jasusi?
Kwa nini hukunieleza ukweli?
Akafoka Abu aliyekuwa
amepandwa na hasira
“Nilikuwa na sababu
maalum za kutaka umuoe
Nawal”
“Ulikuwa unachunguza
maisha yetu mimi na Najma
ndiyo maana ukatutaka tuwe
na mahusiano na hawa
majasusi ? Abu akauliza
“Hapana sijawahi
kuwachunguza.Nilitaka
kuwalinda”
“Mama wewe una roho ya
kishetani kabisa ndiyo maana
hujawahi kusikitika hata siku
moja kwa watu wanaouawa na
magaidi ambao
unawafadhili.Najuta kuzaliwa
nawe Habiba ! akasema kwa
ukali Abu Dahir na Nawal
aliyekuwa karibu yake
akamnasa kofi
“Iwe ni mara ya kwanza na
ya mwisho kumtusi mama
yako.Pamoja na yote
anayoyafanya na aliyoyafanya
huyu bado ni mama yako na
ataendelea kuwa mama yako
daima.Huyu ndiye
aliyekubeba tumboni mwake
miezi tisa na akakulea hadi
umefika hapa
ulipofika.Nakuonya tena
ukithubutu kumtusi mama
yako mbele yangu
nitakufundisha adabu.Hapa
unaponiona mimi sina uwezo
wa kuzaa mtoto.Nimekwisha
ondolewa kizazi.Unajua ni
uchungu gani ninaupata kwa
kukosa mtoto?Usirudie tena
kumtusi mama yako ! akasema
Nawal kwa ukali huku
akilengwa na machozi.Abu
Dahir akamtazama Nawal kwa
macho ya mshangao.
“Huna kizazi?! Akauliza
akiwa ameshika shavuni
mahala aliponaswa kofi
“Ndiyo sina kizazi na
siwezi kupata mtoto ! akajibu
Nawal bila hofu
“Nawal toka tumefunga
ndoa tumekuwa katika jitihada
mbali mbali za kutafuta mtoto
na umekuwa unanihakikishia
kwamba tutapata mtoto hivi
karibuni ! Oh Mungu wangu !
akasema Abu kwa masikitiko
“Ulikuwa ni uongo.Sina
uwezo wa kubeba mimba !
akasema Nawal.
Ghafla Abu Dahir akainua
taa ya mezani iliyokuwa katika
meza ndogo pembeni na pale
alipokuwa amekaa na kumpiga
nayo Nawal ikapasuka.Abu
Dahir akachukua birika na
kumrushia Nawal
akalikwepa.Abu alionekana
kama vile amepatwa na kichaa
“Ninyi wanawake leo
mtanitambua mimi ni nani !
akafoka Abu huku akirusha
vitu kumpiga navyo Nawal
“Abu acha ujinga huu
tafadhali ! akafoka Habiba
“Wewe mama ndiye
uliyeyataka haya yote.Una
roho mbaya sana! Akafoka Abu
na kuinua chungu cha maua
kilichokuwa dirishani kwa
lengo la kumpiga nacho mama
yake lakini Nawal alikwisha
isoma dhamira yake akajiinua
pale chini alipokuwa akaruka
na kukipiga teke chugu kile
kikaanguka na
kuvunjika.Nawal ambaye
hasira zilikwisha mpanda
akamrukia Abu mateke mawili
mfululizo yaliyomrusha Abu
hadi ukutani akajigonga kwa
kishindo na kuanguka chini
halafu akamfuata Habiba
“Mama uko
sawa?Hajakuumiza
huyu?akauliza Nawal
“Nimeumia
kidogo.Ahsante kwa kuniokoa”
akasema Habiba na Nawal
akageuka kumtazama Abu
Dahir ambaye alikuwa amelala
pale chini akionekana
kutokuwa na fahamu.Haraka
haraka akamfuata na kujaribu
kumtikisa huku akimuita jina
lake lakini hakuitika.Akageuka
kumtazama Habiba Jawad
ambaye naye alionyesha hofu
baada ya kuiona sura ya
Nawal,akainuka na kumfuata
akamtazama Abu Dahir
ambaye hakuwa na
fahamu.Bila kupoteza muda
Habiba akampigia simu
daktari wake anayeishi
pembeni ya nyumba yake
ambaye alifika mara moja
akampima Abu kisha akasema
“Anatakiwa akimbizwe
hospitali haraka sana !
Habiba akainuka
akachukua simu na kuwapigia
wasaidizi wake ambao walifika
haraka haraka na kumchukua
Abu Dahir wakamuingiza
garini wakamkimbiza
hospitali.Habiba na Nawal nao
wakaingia garini wakaelekea
hospitali.
“Mama ni vipi kama
nimempiga Abu sehemu
mbaya? Akauliza Nawal
akionekana kuwa na hofu
“Usijilaumu
Nawal.Ulifanya ulichopaswa
kukifanya.Kama usingefanya
vile Abu angenipiga na kile
chungu na pengine ningeweza
hata kupoteza maisha.Kwa
sasa tumuombee ili aweze
kuwa salama.Sitaki kupoteza
tena mtoto
mwingine.Nimekwisha poteza
watoto wawili tayari na
nimebaki na huyu mmoja”
akasema Habiba na kufuta
machozi
“Lakini mama kwa nini
uliamua kufanya hivi
ulivyofanya?Kwa nini uliamua
kuwaeleza ukweli
wanao?akauliza Nawal
“Ilikuwa lazima wafahamu
Nawal.Sikutaka kuendelea
kuwaficha kwani endapo
ningefariki dunia bila
kuwaeleza ukweli yawezekana
nao wangeendelea kufanya kile
ambacho mimi na baba yao
tumekuwa tunakifanya.Sitaki
watoto wangu waendelee
kufadhili ugaidi,sitaki
waendelee kumwaga damu za
watu kama nilivyofanya mimi”
akasema Habiba
“Ulifanya kitu kizuri
kuwaeleza ukweli lakini kwa
bahati mbaya mambo
hayakwenda kama ulivyokuwa
umekusudia” akasema
Nawal.Habiba akafuta machozi
na kusema
“Nadhani Mungu
ananiadhibu kwa mambo
niliyoyafanya.Nimefanya
mambo mengi maovu.Damu
nyingi imemwagika kwa
sababu yangu na haya ndiyo
mapigo ninayoyapata.Naomba
Mungu asimchukue Abu Dahir
kwani ni mtoto pekee
niliyebaki naye” akasema
Habiba na kuchukua simu
akampigia mmoja wa
madaktari katika hospitali
alikoelekeza apelekwe Abu
Dahir akamjulisha kuwa
mwanae amepatwa na
matatizo na anapelekwa pale
hospitali akaomba
ashughulikiwe haraka
Abu Dahir alifikishwa
hospitali ambako tayari
wauguzi walikuwa
wamejiandaa
wakimsubiri,akashushwa
haraka haraka katika gari na
kuweka katika kitanda
kikakimbizwa ndani katika
chumba cha wagonjwa
mahututi ambako alianza
kupatiwa matibabu.Dakika
chache baada ya Abu Dahir
kuingizwa katika chumba cha
wagonjwa mahututi,Habiba
Jawad na Nawal
wakawasili.Habiba
alifahamika pale hospitali
akapokewa na kupelekwa
sehemu ya kusubiri madaktari
watakapomaliza
kumuhudumia mgonjwa wake.
Baada ya dakika saba
mlango wa chumba cha
wagonjwa mahututi
ukafunguliwa na daktari
akatoka.Habiba akasimama na
kumfuata daktari akamtaka
waelekee ofisini kwake
“Kijana wangu
anaendeleaje daktari?akauliza
Habiba akionekana kuwa na
hofu
“Mama Habiba
tumejitahidi kadiri ya uwezo
wetu lakini tumeshindwa
kuokoa maisha ya
mwanao.Uchunguzi wa awali
unaonyesha ana jeraha
kichwani.Nini hasa
kilimtokea? Amepata ajali?
Akauliza Daktari na Habiba
Jawad akashindwa
kumjibu.Yeye na Nawal
wakakumbatiana wakilia.
“Ahsante Mungu kwa kila
jambo.Wewe ndiye mwenye
kutoa na kutwaa kwa muda
uutakao.Hatuwezi kupingana
na maamuzi yako japo
tungependa tuendelee kuwa
pamoja na Abu Dahir lakini
nakushukuru kwa muda
ambao umempa hapa
duniani.Naomba utupe nguvu
ya kulihimili jambo hili”
akasema Habiba machozi
yakimwagika
Habiba Jawad na Nawal
wakapelekwa katika chumba
ulikokuwa mwili wa Abu Dahir
“Saa chache zilizopita
tulikuwa wote ndegeni
tukirejea Riyadh kuhudhuria
msiba wa dada yako,sikuhisi
kama ulikuwa unayafuata
mauti yako.Abu Dahir mimi
ndiye nimesababisha kifo
chako nitalia machozi gani kwa
hili nililolifanya? Najua
ulikuwa unanipenda sana
lakini umekufa ukiwa na
hasira nami baada ya
kuufahamu ukweli kuhusu
maisha ya mama yako na
kuhusu mimi.Najuta kwa nini
sikukueleza ukweli kuhusu
mimi kuwa ni jasusi wa
CIA.Najuta kwa nini
sikukueleza ukweli kama sina
uwezo wa kukupatia mtoto
kwani ni jambo hili ndilo
lililokupa hasira
zaidi.Nisamehe Abu Dahir
huko uliko.Nisamehe ! akalia
Nawal akiwa amesimama
pembeni ya mwili wa Abu
Dahir.Wote wawili Habiba na
Nawal machozi yalikuwa
yanawabubujika.Walitumia
dakika kumi ndani ya kile
chumba kisha wakatoka na
kuondoka kurejea nyumbani
“Mama nimemuua mume
wangu.Nimemuua mwanao
pekee aliyesalia” akasema
Nawal wakiwa garini huku
akimwaga machozi.Habiba
akageuza shingo akamtazama
Nawal na kumuinamisha
kifuani kwake akamkumbatia
“Nawal narudia
kukusisitiza kwamba haya yote
yanayotokea ni mipango ya
Mungu na hupaswi kujilaumu
kwa hili lililotokea.Ilikuwa iwe
hivyo.Abu Dahir aliandikiwa
afe kifo cha namna ile hivyo
hakuna namna ambayo
ungeweza kukwepa.Lakini
tambua kwamba haya yote
yanayoendelea hivi sasa ni
matokeo ya maisha niliyoishi
mimi.Ni mapigo yatokanayo
na matendo yangu.Nimetesa
watu wengi sana.Machozi ya
akina mama waliopoteza
watoto wao katika
mashambulio yaliyofanywa na
makundi ya kigaidi ambayo
ninayafadhili hayajaniacha
salama.Machozi ya watoto
ambao wamebaki yatima
baada ya kuwapoteza wazazi
wao katika mashambulo ya
kigaidi niliyoyafadhili haya
ndiyo malipo yake.Nimepoteza
watoto wangu wote niliowazaa
na sasa nimebaki
mwenyewe.Pamoja na mapigo
haya lakini Mungu
hajaninyima kila
kitu.Amewachukua watoto
wangu lakini ameniletea
watoto wengine ambao ni
wewe na Mathew” akasema
Habiba na Nawal akainua
kichwa chake
“Mama umeongea kuhusu
Mathew.Nataka kufahamu
mahala alipo.Sijamuona katika
msiba wa Najma” akauliza
Nawal
“Mathew ameondoka
hatarejea tena kama
nilivyowaambia na hilo ni
moja kati ya mambo
yaliyopelekea Najma
akachukua maamuzi ya kujiua”
akasema Habiba
“Mathew amekwenda
wapi? Amekufa?
“Hapana hajafa.Nawal
tutazungumza baadae lakini
kwa sasa tujielekeze katika
msiba wa Abu na
tutakapomaliza tutazungumza”
akasema Habiba
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Ndege ya jeshi aliyopanda
Mathew iliwasili jijini Dar es
salaam.Kutoka angani ni
sehemu chache tu za jiji la Dar
es salaam ambazo zilionekana
kuwa na umeme.Sehemu
kubwa ya jiji la Dar ilikuwa
gizani kutokana na miundo
mbinu ya umeme kuharibiwa
katika machafuko yaliyokuwa
yanaendelea.
“Nimezoea kuliona jiji la
Dar es salaam kutokea angani
likiwaka taa kila sehemu lakini
leo hii jiji limetanda giza kila
sehemu.Kwa tamaa ya mali
ambazo Mungu ametujalia
ziwepo katika nchi
zetu,mabepari wametufikisha
hapa.Ni mara ya kwanza
Tanzania tumefikishwa hatua
hii ya kuchinjana wenyewe
kwa wenyewe.Ninaapa kwa
gharama zozote zile lazima
kikundi hiki cha hawa watu
waliotufikisha hapa kwa tamaa
za mali yetu nikifutilie mbali
na dunia lazima ifahamu kile
ambacho mataifa makubwa
yanafanya katika nchi
ndogo.Huu ni unyama
uliopitiliza.Ni unyonyaji usio
na mfano.Naamini haya ni
maongozi ya Mungu hadi
akanifikisha katika kundi hili
ambalo limeigeuza nchi yetu
uwanja wa mauaji.Tayari
nimefahamu kuwa ni
Marekani ndio waliotengeneza
machafuko haya kwa manufaa
yao.Hawako peke yao lazima
kuna watu wa hapa nchini au
katika nchi za Afrika mashariki
ambao wanashirikiana nao
katika kuanzisha na kuchochea
vurugu hizi.Hawa ndio
wanaotakiwa kusakwa kwa
haraka sana na kujulikana ni
akina nani na kama
tukifanikiwa kuwapata hawa
basi tutakuwa tunaweza
kusaidia kumaliza vurugu
hizi.Kuna nguvu mbili hapa
ambazo zimeifikisha Tanzania
hapa tulipofika.Ipo nguvu ya
ndani na nguvu ya nje.Inabidi
kuanza na nguvu ya ndani
kisha nitaendelea na wale wa
nje.Naapa hakuna aliyeifikisha
Tanzania hapa atabaki
salama”akawaza Mathew na
kumkumbuka Ruby
“Nilijaribu kumpigia simu
Ruby lakini
hakupatikana.Nina wasi wasi
sana na usalama wake.Gosu
Gosu naye sijui
anaendeleaje.Nawahitaji sana
hawa watu kama watakuwa
wazima katika kuhakikisha
tunaiokoa nchi yetu kutoka
katika
machafuko.Ninachoelewa
hawa jamaa kwa vile
wamekwisha ingia Afrika
Mashariki lazima wataotesha
mizizi na kuhakikisha kwamba
wanaendelea kuchota utajiri
wetu.Naomba niwakute wote
wako salama” akawaza
Mathew na kutaarifiwa
kwamba ndege inakaribia
kutua katika uwanja wa ndege
wa Julius Nyerere ambao toka
vurugu zilipoanza ulikuwa
umefungwa na ukilindwa na
wanajeshi .
Ndege ile ya jeshi la
Marekani ikiwa na vifaa mbali
mbali vya wanajeshi wa
Marekani waliokuwa nchini
Tanzania ikatua salama.Mizigo
ikapakuliwa na kuingizwa
katika magari kisha wanajeshi
waliokuja na ndege ile
wakaingia katika magari
maalum ya jeshi la Marekani
na msafara ukaondoka
kuelekea katika kambi yao
Mathew Mulumbi akiwa ni
mmoja wao
“Hawa jamaa hawajui
kama hapa nimefika
nyumbani.Watakapogundua
kwamba mimi ni mtanzania
tayari watakuwa wamechelewa
sana lakini kwa sasa ngoja
niendelee kujifanya mimi ni
mgeni wa hapa Tanzania ili
niendelee kuusoma mtandao
wao” akawaza Mathew na
kuona namna alivyokuwa
anachungwa.Ndani ya gari
alilokuwa amepanda kulikuwa
na wanajeshi wanne wenye
silaha na gari lile liliwekwa
kati kati ya msafara.
“Nadhani wameelekezwa
wanichunge ndiyo maana
wameniweka
katikati.Hawapaswi kuwa na
hofu nitafanya walivyonieleza
lakini watajuta sana na
kumlaumu Habiba Jawad kwa
kuwakutanisha na mimi.Safari
hii ninataka nifanye kitu
ambacho kitakuwa cha
kihistoria.Tumeonewa vya
kutosha na sasa ni wakati wa
kuwaonyesha haya mataifa
makubwa kwamba hata sisi
tunao uwezo na tumechoshwa
na mambo wanayotufanyia”
akawaza Mathew akiyaelekeza
macho yake nje
“Dar es salaam haikuwa
hivi.Hili ni jiji lililokuwa
linakesha lakini muda huu
barabara tupu hakuna watu
mitaani.Sipati picha namna
maisha yalivyo magumu hivi
sasa.Maduka
yamefungwa,upatikanaji wa
chakula na mahitaji muhimu
imekuwa ni shida lakini baadhi
ya watu wachache wao
wanaishi maisha mazuri na
kupata kila wanachokihitaji
wakisahau kwamba kuna
mamilioni ya watu
wanaoteseka huku Tanzania
na Afrika mashariki kwa
sababu yao.Tunatakiwa
kupambana kuhakikisha
tunairejesha nchi yetu
ilivyokuwa na ili kumaliza
vurugu hizi ni lazima
kuuchimbua mzizi wenyewe
ambao ni kikundi kile kidogo
ndani ya CIA” akawaza
Mathew huku wakiendelea
kukata mitaa ya jiji la Dar es
salaam ambayo kwa usiku huu
ilikuwa kimya.Mioto ya
matairi na moshi mzito
vilionekana katika baadhi ya
barabara na hata majengo
yanayoungua moto pia
yalikuwepo.Katika baadhi ya
barabara walikuta zimefungwa
kwa mawe makubwa
“Hali ilivyo Dar es salaam
utadhani kuna filamu
inatengenezwa kumbe ni hali
halisi .Inasikitisha sana !
Narudia tena kuahidi kwamba
wale wote waliotufikisha hapa
hakuna atakayebaki
salama.Tanzania hatukupaswa
kufikishwa hapa.Lakini hili ni
funzo kwa watanzania ili wawe
macho kulinda amani
yao.Wamekuwa wakihubiriwa
kwa miaka mingi kwamba siku
amani hii ikipotea
watajuta.Wamejaribu
kuchezea amani na wameona
madhara yake.Hakuna sehemu
ya kukimbilia imelazimu
wayakimbie makazi yao na
kujificha katika makambi.Kwa
haya wanayokutana nayo
naamini hata akija tena mtu
mwingine siku nyingine
kutaka kuwarubuni kuchezea
amani yao hawatajaribu tena”
Mathew akatolewa mawazoni
baada ya msafara wao
kukutana na kundi kubwa la
vijana waliokuwa wamebeba
mienge na silaha huku
wakiimba.Ikalazimu wanajeshi
wa Marekani kutumia risasi za
moto kuwatawanya kwani
baadhi yao walikuwa na silaha
na walianza kushambulia
magari katika ule
msafara.Baada ya kundi lile la
vijana kutawanyika magari
yakaongeza mwendo na moja
kwa moja wakaelekea katika
uwanja wa uhuru ambako
ndiko kulikuwa na kambi
kubwa ya wanajeshi wa
Marekani na vifaa vyao vyote
vilikuwa vinahifadhiwa
huko.Kambi nyingine ilikuwa
ufukweni mwa bahari ya
Hindi.
Mathew alishushwa garini
na kukabidhiwa kwa mmoja
wa viongozi wa kambi ile
ambaye alimpeleka hadi katika
hema.
“Karibu Tanzania.Jina
lako nani? Akauliza Yule jamaa
“Abu Zalawi” akajibu
Mathew kikakamavu
“Abu Zalawi nimeelekezwa
na viongozi wangu kwamba
nikupokee na kisha
nitakukabidhi kwa mtu
ambaye atakuja hapa
kukuchukua.Umewahi kufika
Tanzania kabla? Akauliza
“Hapana sijawahi” akajibu
Mathew
“Hali ni mbaya sana hasa
hapa Dar es salaam na jiji la
Tanga pia.Nadhani umejionea
hali halisi huko mitaani wakati
mkija hapa”
“Ndiyo mkuu.Tumekutana
na kundi kubwa la vijana
wakiwa na silaha na
kushambulia msafara wetu”
“Basi hiyo ndiyo hali
tunayokutana nayo kila siku
katika kujaribu kurejesha hali
ya amani tukishirikiana na
vikosi vya ulinzi vya Tanzania”
“Endelea kupumzika na
atakapofika mwenyeji wako
nitakufahamisha” akasema
Yule mwanajeshi na kutoka nje
ya lile hema akamuacha
Mathew peke yake.
“Naamini huyo mtu
anayekuja kunichukua ni
mmoja kati ya watu wa IS na
atakuwa anatumiwa na CIA
katika kuratibu na kuchochea
hizi vurugu
zinazoendelea.Imekuwa vyema
wamenielekeza sehemu husika
kwani huyo jamaa ndiye wa
kuanza naye” akawaza Mathew
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 3 : EPISODE 2
Mathew alitikiswa bega na
kustuka,alikuwa amepitiwa na
usingizi.Saa yake ya mkononi
ilionyesha ni saa tisa za usiku.
“Abu Zalawi muda wa
kuondoka, mwenyeji wako
tayari amefika” akasema Yule
mwanajeshi aliyempokea
Mathew kisha akamuongoza
wakaenda hadi nje ya uwanja
ambako kulikuwa na magari
matatu.Katika gari la kati kati
kulikuwa na watu wanne
wenye silaha wakiwa
wamesimama
wamelizunguka.Mmoja wa
wale jamaa akamfungulia
Mathew mlango akaingia
ndani ambako alimkuta jamaa
mmoja
“Abu Zalawi” akasema
Yule jamaa
“Assad Ismail? Akauliza
Mathew
“Farhad Seif” akasema
Yule jamaa na Mathew
akaonyesha wasiwasi
“Yuko wapi Assad Ismail?
Akauliza
“Usihofu tafadhali.Karibu
Dar es salaam” akasema Yule
jamaa na gari likawashwa
msafara ule wa magari
ukaondoka katika uwanja wa
uhuru ukitanguliwa na gari la
jeshi la Marekani ambalo
lilikuwa na mwanajeshi akiwa
amejitokeza nje akiwa na
bunduki kubwa tayari
kukabiliana na makundi
yoyote ya vurugu.
“Vipi safari yako? Akauliza
Farhad
“Ilikuwa nzuri” akajibu
Mathew na safari ikaendelea
kimya kimya.
Walikatisha mitaa
mbalimbali ya jiji huku
wakikutana na magari ya doria
ya polisi na jeshi hadi
walipofika katika kituo cha
basi cha Botha.Mahala hapa
panaitwa jina hilo kutokana na
awali mzungu mmoja kutoka
Afrika Kusini aliyejulikana kwa
jina moja tu la Botha kuishi
eneo hilo na kujenga shule ya
awali kwa watoto wadogo
pamoja na kutoa huduma ya
maji bure kwa wananchi
waliokuwa wanamzunguka
hivyo akawa maarufu.
Magari yalisimama na
Farhad akashuka akaenda
kuzungumza na wale
wanajeshi wa Marekani
akaagana nao wakageuza gari
wakaondoka.Farhad na
wenzake nao wakaendelea na
safari yao
“Mbona wale wanajeshi
wamerudi? Huko tuendako ni
salama?akauliza Mathew
“Una hofu yoyote?
Akauliza Farhad
“Wakati tukielekea katika
kambi ya wanajeshi
tumekutana na makundi
makubwa ya vijana wakiwa na
silaha kwa bahati nzuri
wanajeshi walikuwa na silaha
kali wakawatawanya” akasema
Mathew
“Usihofu Abu Zalawi uko
salama.Hili ni eneo letu”
akasema Farhad na safari
ikaendelea kimya kimya huku
eneo hili la kwa Botha likiwa
kimya sana.Geti jeusi
lilifunguliwa na gari zile
zikaingia.Ndani kulikuwa na
nyumba iliyopakwa rangi ya
bluu halafu kukawa na
majengo mawili yaliyoonekana
kama mabohari.Mathew
akaelekezwa kushuka garini
kisha akamfuata Farhad
wakaelekea ndani ya ile
nyumba.Kulikuwa na mlinzi
mlangoni akawafungulia
mlango wakaingia
ndani.Sebuleni kulikuwa na
watu wawili wamekaa chini
katika zuria wakizungumza.
“Karibuni sana” akasema
mmoja wa wale jamaa kwa
lugha ya kiarabu.Mathew na
Farhad wakaketi
“Pole na safari ndefu”
akasema Yule jamaa
aliyewakaribisha
“Ahsante sana nashukuru”
akajibu Mathew
“Naitwa Marwan Hossam”
akasema Yule jamaa
“Yuko wapi Assad
Ismail?akauliza Mathew
“Usiwe na hofu utaonana
na Assad kutakapopambazuka
lakini kwa sasa unatakiwa
upumzike kwa safari hii ndefu”
akasema Marwan na kuinuka
akampeleka Mathew katika
mojawapo ya chumba
akamtaka apumzike.
“Hii nyumba ndimo
wanamoishi magaidi wa IS
ambao jukumu lao kubwa ni
kuendelea kuchochea
machafuko.Mpaka sasa
wanaamini mimi ni gaidi
mwenzao na kesho nitaonana
na huyo Marwan mkubwa wao
naamini atanieleza mengi”
akawaza Mathew huku
akikikagua kile chumba
“Wakati nikiendelea
kuwasoma hawa jamaa
natakiwa kutafuta namna
nitakavyoweza kuwasiliana na
akina Gosu Gosu ili niweze
kuwapa taarifa za jambo hili
linaloendelea.Sina hakika
kama wanafahamu chanzo cha
vurugu hizi.Haya yote lazima
yafanyike kesho” akawaza
Mathew na kujilaza kitandani
“Mathew hakikisha
unafanikisha malengo
yako.Ifanye dunia
ikukumbuke kwa vizazi na
vizazi.Maliza kundi la kigaidi
la IS na makundi
mengine.Kisafishe kikundi
hiki kidogo cha watu hawa
ambacho ndicho
kinachohatarisha amani ya
dunia.Hii ni misheni kubwa
na ya hatari.Lolote linaweza
kutokea katika misheni hii
mimi ninakuombea uimalize
salama na kila pale
nitakapokuwa na uwezo wa
kukusaidia nitafanya
hivyo.Jambo la mwisho
baada ya kumaliza misheni
hii kama utakuwa salama
tafadhali usirejee tena
Riyadh.Nenda nyumbani
kaendelee na maisha
yako.Kaungane tena na
familia yako kwani lengo lako
litakuwa limetimia kuhusu
kupambana na ugaidi.Kuhusu
Najma usiwe na hofu
nitazungumza naye na
ataelewa.Narudia tena
usirejee Saudi Arabia kwani
hadi wakati huo sintakuwepo
tena” Mathew akiwa amejilaza
kitandani akayakumbuka
maneno ya Habiba Jawad
“Habiba hana uhakika
kama nitamaliza salama
operesheni hii ndiyo maana
akaniambia kwamba ile
ilikuwa ni mara yetu ya
mwisho kuonana.Habiba
amekuwa akiniambia kwamba
atakufa hivi karibuni lakini
hakuwahi kunieleza nini hasa
kinachomsumbua ingawa
ukimtazama huwezi kugundua
chochote kama afya yake ina
matatizo.Ninamuomba Mungu
aniwezeshe niikamilishe
salama operesheni hii na
lazima nirejee Riyadh
kumuona Najma na pili kujua
maendeleo ya Habiba na kama
atakuwa amefariki basi
nitapenda kuliona kaburi lake
kwani mama Yule anastahili
pongezi kwa mambo ambayo
amenifanyia.Yeye ndiye
aliyenifikisha hapa nilipofika
hadi nikafahamu mambo
mengi na mengine makubwa
kabisa ambayo wengi duniani
hawayajui” akawaza Mathew
halafu akazima taa na
kusimama mlangoni akatega
sikio kama kuna mtu yeyote
yuko mlangoni alipohakikisha
kuko shwari akaenda dirishani
na kulichunguza kama ni
dirisha analoweza kupita lakini
ilikuwa ni dirisha imara
ambalo halikuwa na uwazi kwa
mtu kupita.
“Ngoja nipumzishe kichwa
na kesho nitajua nini cha
kufanya” akawaza Mathew na
kupanda kitandani
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 3 : EPISODE 3
Kumepambazuka na kijua
tayari kimeanza
kuchomoza.Asubuhi hii
Tanzania iliamshwa na taarifa
mbaya za kifo cha Mufti wa
Tanzania ambaye aliuawa
usiku yeye na familia yake
baada ya nyumba yake
kushambuliwa kwa
mabomu.Ilikuwa ni taarifa
iliyostua wengi na kuleta hofu
kubwa.
Kitasa cha mlango wa
chumba cha Mathew
kikaminywa kwa nguvu lakini
alikuwa amefunga mlango kwa
ndani.Mtu aliyeminya kile
kitasa akagonga mlango kwa
nguvu na Mathew akainuka na
kwenda kufungua.Alikuwa ni
Marwan
“Habari yako Abu
Zalawi?akauliza Marwan
“Habari nzuri Marwan”
“Amka
kumekucha.Jiandae kwa ajili
ya kuianza siku” akasema
Marwan na kumuelekeza
Mathew bafu akaenda kuoga
halafu akakaribishwa sebuleni
kwa ajili ya kupata kifungua
kinywa.Mle sebuleni kulikuwa
na watu zaidi ya kumi wote
wakipata kifungua
kinywa.Mathew akawasalimu
kisha naye akaketi na kupata
chai.Baada ya kupata kifungua
kinywa wale watu karibu wote
wakatoka na kwenda katika
zile nyumba mbili zilizojengwa
kwa mfano wa bohari Mathew
akabaki na Marwan
“Yuko wapi Assad
?Mathew akauliza
“Usihofu Abu Zalawi
utaonana naye.Atafika hapa
muda si mrefu”
“Haishi hapa?
“Hapana yeye haishi hapa”
“Nimeona kuna watu
wengi hapa,shughuli gani
inafanyika katika nyumba
hii?akauliza Mathew
“Abu Zalawi unaonekana
unataka kufahamu mambo
mengi kwa wakati
mmoja.Jielekeze katika kile
kilichokuleta hapa na kama
kuna swali lolote unataka
kuuliza utamuuliza Assad
atakapofika” akasema Marwan
na kutoka akamuacha Mathew
peke yake mle
sebuleni.Mathew akasimama
na kuchungulia nje akaanza
kuyasoma mazingira ya
mahala pale
“Inaonekana hii ni sehemu
ambako wanapanga mikakati
yao ya kigaidi.Katika yale
majengo mawili mfano wa
bohari kuna nini? Ngoja
nimsubiri Assad anaweza
akanieleza kila kitu kuhusiana
na mahala hapa” akawaza
Mathew na kuendelea
kuangaza angaza macho.
Geti lilifunguliwa na gari la
jeshi la Marekani likaingia
huku nyuma yake kukiwa na
gari lingine lenye rangi
nyeusi.Kutoka katika lile gari
jeusi wakashuka watu wawili
na mmoja wao akaufungua
mlango wa kati kati na jamaa
mmoja aliyevaa kanzu ya kijivu
na koti jeusi
akashuka.Kichwani hakuwa
amevaa kofia na kichwa chake
hakikuwa na nywele hata
moja.Macho yake aliyafunika
kwa miwani myeusi.Mkononi
alikuwa ameshika sigara
akivuta.Akaagana na
wanajeshi wale wa Marekani
wakaondoka.Jamaa Yule
aliyeshuka garini akasalimiana
na Marwan wakazunguma kwa
dakika chache halafu
wakaelekea katika zile nyumba
mbili mfano wa
bohari.Mathew alikuwa
dirishani akiwatazama.
Baada ya dakika kumi
wakatoka katika zile nyumba
na kuingia sebuleni,Mathew
akasimama
“Abu Zalawi ! akasema
Yule jamaa aliyeongozana na
Marwan huku akimpa mkono
Mathew wakasalimiana
“Nasikia umekuwa
unaniulizia sana ukitaka
kuniona.Ndiye mimi Assad
Ismail.Karibu sana Tanzania”
akasema Assad
“Nashukuru sana Assad”
akajibu Mathew
“Hii sura yako si
ngeni.Umewahi kutembelea
nchi yoyote ya Afrika
Mashariki?akauliza Assad
“Ndiyo niliwahi kwenda
Kenya.Nilikwenda kumuua
mkurugenzi wa Mossad katika
ukanda wa Afrika Mashariki”
“Ndiyo maana nilipokuona
tu nikahisi kama nimewahi
kukuona sehemu
Fulani.Umewahi kufika
Tanzania?
“Hapana ni mara ya
kwanza ninafika Tanzania”
Mathew akajibu
“Karibu sana Abu
Zalawi.Nimefurahi
kukutana
nawe.Nimeelezwa kwamba
Habiba
Jawad ndiye aliyekupendekeza
uje huku” akasema Assad huku
akiendelea kuvuta sigara
“Ndiyo ni Habiba ambaye
alinipeleka Marekani na
kunikutanisha na CIA ambao
wamenituma huku”
“Vizuri sana.Vipi
maendeleo ya Habiba?
“Habiba anaendelea vizuri
sana”
“Nafurahi kusikia
hivyo.Hebu nipe historia yako
kwa ufupi namna ulivyokutana
na Habiba hadi akakuamini
kiasi hiki” akasema Assad
“Baada ya kumuua mkuu
wa Mossad kanda ya Afrika
Mashariki na kati nilikamatwa
na Mossad nikafungwa
gerezani kwa miaka mitatu na
hapo ndipo nilipokutana na
Ammar Nazari kiongozi wa
kundi la Ammar Nazari
Brigades.Nilifanikiwa kutoroka
gerezani nikiwa na Ammar na
nikajiunga katika kundi
lake.Nikiwa katika kundi hilo
nilitekeleza mashambulio
kadhaa likiwemo lile la kituo
cha mabasi jijini
Jeruslaem.Vikosi vya Israel
vilishambulia makazi ya
Ammar na kufanikiwa kumuua
mimi nilitoroka nikiwa na
Nawal mke wa Ammar na huyo
ndiye aliyenielekeza kwamba
tumtafute Habiba Jawad kwa
ajili ya kupata hifadhi kwani
alikuwa ni rafiki wa
Ammar.Tulifanikiwa kuonana
na Habiba Jawad akatupa
hifadhi na ndipo alipoanza
kunishirikisha katika shughuli
zake akatokea kuniamini
baada ya kuridhiswa na
utendaji wangu wa kazi.Hiyo
ndiyo historia fupi ya namna
nilivyoweza kukutana na
Habiba Jawad” akasema
Mathew
“Abu Zalawi mimi naitwa
Assad Ismail.Ninasimamia
kundi la IS kwa ukanda huu
wa Afrika Mashariki na kati
makazi yangu ni
Mombasa.Nimekuja Tanzania
kwa ajili ya operesheni
maalum.Nadhani ulipokwenda
Marekani umefahamishwa kile
kinachoendelea hapa Tanzania
na Afrika Mashariki kwa
ujumla”
“Ndiyo.Nilielezwa kwa
kifupi sana na kuambiwa
kwamba nitapata maelezo
kamili nitakapofika hapa.Hata
maelekezo yote kuhusiana na
kazi ninayokuja kuifanya hapa
Tanzania nimeambiwa
kwamba nitayapata kutoka
kwako” akasema Mathew na
Assad akaonyesha kushangaa
“Hawakukueleza unakuja
kufanya nini Tanzania?
Akauliza Assad
“Wamenieleza kwamba
ninakuja kulipua ubalozi wa
Marekani lakini kila kitu
kuhusiana na misheni hiyo
nimeambiwa kwamba nitapata
kutoka kwako” akasema
Mathew
“Nitakueleza kwa kifupi ili
uweze kupata picha ya kile
kinachoendelea hapa
Tanzania.Ni kwamba
Marekani wana mipango yao
hapa Afrika Mashariki na ili
iweze kufanikiwa
wamelazimika kututumia sisi
kwa malipo ya fedha na
silaha.Kumekuwa na upungufu
mkubwa wa mafuta duniani
kutokana na wazalishaji
kupunguza kiwango kwa lengo
la kupandisha bei katika soko
la dunia.Sababu hiyo ndiyo
iliyopelekea Marekani
kugeukia Afrika Mashariki
ambako kuna rasilimali ya
mafuta kutoka Uganda nchi
ambayo ina akiba kubwa sana
ya mafuta ambayo
husafirishwa kwa bomba
kutoka Hoima hadi jijini Tanga
hapa Tanzania.Ili kuweza
kuyapata mafuta hayo
ililazimu kuliingiza eneo la
Afrika Mashariki katika
machafuko na machafuko
ambayo yanaweza kusambaa
kwa haraka mama moto wa
petroli ni machafuko ya
kidini.Katika nchi hizi tatu
Tanzania,Kenya na Uganda
dini kubwa ni mbili wakristu
na waislamu hivyo kwa
kushirikiana na baadhi ya
wanasiasa na baadhi ya
viongozi wa dini tuliweza
kufanya mauaji ambayo
yalileta uhasama mkubwa na
waumini wa dini hizo mbili
wakaanza kushambuliana
wakichomeana nyumba za
ibada na hata
kuuana.Machafuko hayo
yalianza Uganda na kuenea
Tanzania na Kenya lakini sana
tumelenga nchi za Tanzania na
Uganda kwani ili Marekani
waweze kupata mafuta ya
Uganda lazima watumie
bandari ya Tanga hivyo lazima
nchi hizi mbili ziingie katika
machafuko.Hicho ndicho
ambacho tumekuwa
tunakifanya hapa Tanzania na
ndiyo maana nimeondoka
Mombasa kuja hapa Tanzania
kuhakikisha kila kitu
kinakwenda vizuri kwani
misheni hii ni ya fedha nyingi
sana” akasema Assad
“Hongera sana Assad kwa
kazi kubwa uliyoifanya.Nchi
kama Tanzania ni nchi ngumu
sana kwa watu wake kuingia
katika machafuko makubwa
kama haya yanayoendelea”
akasema Mathew
“Ni kweli.Haikuwa
rahisi.Ililazimu kushirikiana
na wanasiasa na baadhi ya
viongozi wa dini kutengeneza
mtandao wa kuchochea vurugu
ndipo tukafanikiwa na kwa
mara ya kwanza Tanzania
imeingia katika machafuko ya
wenyewe kwa wenyewe.Hata
hivyo watanzania hawajazoea
vurugu kwani kulianza
kujitokeza dalili za amani
kurejea.Rais wa Tanzani
alikutana na mufti wa
Tanzania wakawa na
mazungumzo marefu na baada
ya mazungumzo hayo mufti
akazungumza na waislamu na
kuwataka wasijihusishe na
vurugu.Kwa kiasi kikubwa
watu wameonekana
kumuelewa na vurugu
zimeripotiwa kupungua sana
kwa usiku wa kuamkia leo.Kwa
siku ya leo Rais alipanga
kuendelea na mikutano na
viongozi wengine wa dini ya
kikristu.Kwa kiasi kikubwa
juhudi za kutafuta amani
zinaonekana kuanza kuzaa
madini na kazi yetu ni
kuhakikisha kwamba amani
haipatikani Tanzania ili vikosi
vya Marekani viendelee kukaa
Afrika Mashariki kwa muda
mrefu zaidi na ili kuvuruga
jitihada za kutafuta amani
ambazo zimeanza kuonekana
usiku wa leo tumemuua mufti
wa Tanzania kwa bomu”
akasema Assad na Mathew
akahisi mwili unamsisimka
akajikaza asiweze kuonyesha
namna alivyostuka.
“Hii haiwezi kujenga
taswira kama kuna kikundi cha
watu ambacho kinalenga
viongozi wa dini?Unadhani
waislamu wataamini kwamba
ni wakristu ndio waliomuua
kiongozi wao? Akauliza
Mathew
“Usiwe na hofu Abu
Zalawi.Tumekwisha jipanga
vizuri na kila kitu kitakwenda
vizuri.Kwa hili tulilolifanya ni
kama kumwagia petrol katika
moto ambao umeanza
kuzimika na moto ukapata
nguvu mpya.Tunao watu wetu
ndani ya wakristu na waislamu
pia ambao huchochea vurugu
hizi.Kwa mfano kwa mauaji
haya ya Mufti wapo watu
ndani ya uislamu ambao
watawachochea waislamu
kulipiza kisasi” akasema Assad
“Tuachane na hilo nataka
kufahamu kuhusiana na kazi
yangu niliyokuja kuifanya”
akasema Mathew
“Ulichokuja kukifanya
huku Tanzania kama
ulivyoelezwa ni kulipua ubalozi
wa Marekani hapa
Tanzania.Tayari maandalizi ya
bomu litakalotumika
yameanza.Litakuwa ni bomu
kubwa ambalo litasababisha
uharibifu mkubwa sana.Kuna
raia wa Marekani ndani ya
ubalozi huo pamoja na raia wa
nchi nyingine waliojihifadhi
hapo wakisubiri vurugu
zipungue na wengi watapoteza
maisha kufuatia shambulio
hilo litaipa sababu Marekani
kuongeza vikosi zaidi
Tanzania” akasema Assad na
kunyamaza baada ya watu
wawili kuingia mle ndani
wakazungumza na walipotoka
Assad akaendelea.
“Hawa jamaa waliotoka ni
wataalamu wanao unda bomu
utakalolitumia kulipua ubalozi
huo wa Marekani” akasema
Assad
“Kwa sasa ubalozi wa
Marekani unalindwa na
wanajeshi wao walioko hapa
nchini.Mpango wa namna
utakavyoingia katika ubalozi
huo uko namna hii.Kwanza
kabisa naomba ufahamu kuwa
suala hili linawahusisha pia
baadhi ya viongozi wa vikosi
vya jeshi vilivyoko hapa
Tanzania na kama ulivyoona
wewe mwenyewe wamekuwa
wakinipa msaada
mkubwa.Kutokana na
ushirikiano huo tutatumia gari
la jeshi la Marekani kuweka
bomu kisha utavaa sare za
jeshi hilo na kuonekana kama
mwenzao.Wanajeshi
watakaokuwa na gari hilo
watadai kwamba walitekwa na
gari lao kuporwa” Assad
akanyamaza
“Wanajeshi watakaokuwa
wakilinda ubalozi huo
wakiliona gari la jeshi la
Marekani hawatakuwa na wasi
wasi na wataamini ni
mwenzao.Watakuruhusu
kuingia ndani kisha utakwenda
kuliegesha gari hio mahala
utakapoelekezwa.Ndani ya gari
hilo utakuwa umebeba watoto
ambao utadai kuwa
umewaokota njiani wakiwa
hawana msaada.Ukisha egesha
gari mahala utakapoelekezwa
utashuka na kuondoka hapo
ubalozini ukidai kwamba
unawafuata watoto uliowaona
wako katika hatari.Endapo
watakuzuia unaruhusiwa
kutumia silaha kuwamaliza
walinzi hao.Ukisha toka
ubalozini hapo utaelekezwa
mahala ambako utakuta gari
linakusubiri na hapo ndipo
utakapolipua bomu na usiku
huo huo utaondoka kuelekea
nchini Kenya na siku
itakayofuata utakamatwa na
makachero wa CIA na baada
ya hapo sisi tutakuwa
tumekamilisha jukumu letu
kwa upande wako na
tutaendelea na jukumu letu la
kuchochea machafuko”
akasema Assad
“Nimekuelewa
Assad.Ahsante kwa mpango
huu mzuri.Lini jambo hili
litafanyika?Mathew akauliza
“Kwa sasa tunaendelea na
utengenezaji wa bomu ambalo
tutalitumia.Naamini hadi
usiku wa leo litakuwa
limekamilika kwani kuna vifaa
vichache ambavyo tulikuwa
tunavisubiri na tayari
tumevipata hivyo basi naamini
hadi usiku wa leo wataalamu
wetu wanaounda bomu hilo
watakuwa wamekamilisha
kazi.Kesho jioni tukio hilo
litafanyika” akasema Assad
“Kuna muda mrefu hadi
kesho jioni.Hakuna chochote
ninachoweza kusaidia
kufanya?akauliza Mathew
“Pumzika Abu kwani una
safari ndefu sana.Una siku
mbili tu leo na kesho za
kupumzika kwani baada ya
hapo utakabiliwa na kipindi
kigumu sana” akasema Assad
“Nalifahamu hilo Assad
lakini mimi ni mtu wa
kazi.Sijazoea kukaa bila kuwa
na kazi yoyote.Nielekeze kama
kuna kazi yoyote ninaweza
kusaidia” akasema Mathew
“Abu Zalawi usihofu.Kila
kitu hapa kinakwenda vizuri
wewe tutakuomba upumzike
hadi hiyo kesho jioni
utakapoianza safari yako.Una
kazi ngumu mno inakukabli
mbele yako hivyo tumia muda
huu kupumzika.Ninaomba
nikakutambulishe kwa watu
wangu wakufahamu kwani
wengine wanakuona hapa
lakini hawakuelewi wewe ni
nani” akasema Assad na
kumchukua Mathew wakaenda
katika moja ya nyumba
iliyojengwa kama
bohari.Ndani ya nyumba ile
kulikuwa na nafasi kubwa na
kati kati ya nyumba ile
kulikuwa na meza kubwa
iliyokuwa imezungukwa na
watu zaidi ya kumi.Shughuli ya
uundaji wa bomu ilikuwa
inaendelea.Assad akawaomba
wamsikilize kwa dakika chache
“Awali ya yote napenda
kwanza niwashukuru kwa kazi
nzuri iliyofanyika usiku wa leo
ya kumuondoa Mufti wa
Tanzania.Baada ya kutekeleza
shambulio lile naamini sasa
zile vurugu ambazo zilikuwa
na mwelekeo wa kumalizika
zitaanza upya.Jambo la pili
ambalo nataka kuwajulisheni
ni kwamba jana tumepokea
mgeni hapa katika kambi
yetu.Nadhani tayari nyote
mmekwisha muona anaitwa
Abu Zalawi.Anatokea Saudi
Arabia.Alikuwa katika kundi la
Ammar Nazari
Brigades.Amekuja hapa kwa
kazi maalum ambayo ni
kulitumia bomu hilo
mnaloliandaa.Nimeona
nimtambulishe kwenu ili
mfahamu kwamba kazi hiyo
inatakiwa imalizike kwa
haraka ili kesho Abu Zalawi
aifanye kazi iliyomleta hapa”
akasema Assad na kumtaka
Abu Zalawi kwenda
kupumzika wakati shughuli ya
uundaji wa bomu
ikiendelea.Mathew akatoka na
kuanza kuzunguka zunguka
katika nyumba ile akiyasoma
mazingira yalivyo
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 3 : EPISODE 4
Inakaribia dakika arobaini
sasa,Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dr
Fabian Kelelo akizungumza na
Ruby kwa simu.Taarifa ya
mauaji ya Mufti wa Tanzania
ilimstua sana.Baada ya
kumaliza kuzungumza na Rais
simuni,Ruby akamgeukia Gosu
Gosu
“Rais amechanganyikiwa
kwa mauaji haya ya Mufti
ambaye alikuwa mstari wa
mbele katika kutafuta
amani.Mauaji haya yameleta
wasi wasi mkubwa sana wa
kuongezeka kwa
vurugu.Tuliamini muda si
mrefu hali itakuwa shwari
lakini kwa mauaji haya kuna
uwezekano wa vurugu kuanza
upya” akasema Ruby
“Swali la kujiuliza je ni
watu wa imani nyingine ndio
waliotekeleza mauaji hayo ya
Mufti?Binafsi siamini kama ni
watu wa imani ya kikritu ndio
waliofanya mauaji haya”
akasema Gosu Gosu
“Nakubaliana nawe Gosu
Gosu mauaji haya ya Mufti wa
Tanzania hayaonekani kama
yana mlengo wa kidini bali
yanaonekana ni kutaka
kuchochea zaidi vurugu ili
waislamu waamini kuwa ni
upande mwingine ndio
waliotekeleza mauaji hayo na
hapo waumini wa dini hizo
wataendelea
kushambuliana.Mauaji haya
yametokea wakati kukiwa na
kila dalili za machafuko
kutulia.Rais alikuwa na
program ya kuendelea
kukutana na viongozi wakuu
wa dini na alianza na mufti
wakakutana wakazungumza na
Mufti akawasihi waislamu
asiendelee na vurugu zile.Leo
hii Rais alikuwa na mipango ya
kukutana na viongozi wengine
wa dini katika mwendelezo ule
wa kutafuta amani lakini kwa
hiki kilichotokea sina hakika
kama mazungumzo hayo
yataendelea tena kwani
viongozi wakuu wa dini
wataogopa kuzungumza na
Rais kwa hofu ya kuuawa
kama ilivyomtokea Mufti wa
Tanzania.Hali inazidi kuwa
tete” akasema Ruby
“Tunahitaji kuongeza
juhudi za kuutafuta mzizi wa
vurugu hizi.Tukifanikiwa
kuupata mzizi wake
tutafahamu
mengi.Tulimuomba Rais
atusadie kupata taarifa za
Joshua Lulangwa wa
Uganda.Kuna chochote
amekueleza?akauliza Gosu
Gosu
“Ndiyo.Amesema kwamba
taarifa alizopewa kutoka
Uganda ni kuwa Joshua
Lulangwa ametoweka na
hajulikani alipo.Wanasema
mara ya mwisho kuonekana
nchini Uganda ni siku ambayo
machafuko yalianza jijini
Kampala.Baada ya hapo
hajaonekana tena na wala
hajulikani alipo na toka wakati
huo simu yake imezimwa”
akasema Ruby
“Yale yale tuliyoyakuta
kwa Karim na wenzake.Ruby
ninahisi huu ni mtandao
mmoja.Wote wana sifa
zinazofanana.Wote simu zao
zimezimwa mara tu
machafuko yalipoanza na wote
hawajulikani walipo.Swali
ambalo bado hatujalipatia
majibu ni je wanahusika kwa
namna yoyote ile na vurugu
hizi zinazoendelea Tanzania na
Uganda?akauliza Gosu Gosu
“Hapo ndipo tulipokwama
Gosu Gosu.Tunatakiwa
kutafuta kila namna ya kuweza
kujikwamua hapo
tulipokwama.Nina uhakika
mkubwa sana kwamba kuna
kitu hapa ambacho kama
tukiweza kukifahamu basi
kinaweza kutusaidia sana
kujua mzizi wa vurugu hizi
zinazoendelea”akasema Ruby
“Hapa ndipo
ninapomkumbuka Mathew”
akasema Gosu Gosu
“Me too.I miss him so
much ! akasema Ruby na
kuinamisha kichwa akazama
mawazoni
“Mimi ni mwanajeshi
nimefundishwa kupigana na
kuua,sina utaalamu mkubwa
katika mambo ya
kipelelezi.Ninachofahamu
mimi ni kushika silaha na
kupambana.Wewe ni mchawi
wa kompyuta na hujabobea
sana katika mambo haya ya
kiuchunguzi ndiyo maana
kuna mambo tunashindwa
kuyapatia majibu kama hili
linaloendelea sasa” akasema
Gosu Gosu
“Uko sahihi Gosu
Gosu.Mimi utaalamu wangu ni
katika msauala ya kompyuta
na mawasiliano.Masuala ya
kipelelezi sijabobea huko japo
nimefanya kazi katika taasisi
za kipelelezi lakini nikiwa
kama mtaalamu wa
kompyuta.Lazima nikiri
kwamba idara hii ya SNSA
japo imekua ikifanya kazi zake
vizuri na kwa mafanikio
makubwa lakini hakuna
mpelelezi mwenye kiwango
cha juu ambaye anaweza
akakaribiana na Mathew
Mulumbi” akasema Ruby
“Ruby hakuna ubishi
kwamba tunahitaji sana
msaada kwa hapa tulipofika na
msaada pekee ambao
tunauhitaji kuupata hivi sasa
ni Mathew Mulumbi” akasema
Gosu Gosu na ukimya ukapita
halafu Gosu Gosu akasema
“Ruby tunafahamu mahala
alipo Mathew na unazo namba
za simu za mtu ambaye
anaweza akatusaidia
kutuunganisha naye.Mpigie
muombe atuunganishe na
Mathew tuzungumze naye
tumueleze hali halisi ilivyo kwa
sasa hapa nchini.Ruby nina
uhakika mkubwa Mathew
akifahamu kile kinachoendelea
hapa nchini hivi sasa lazima
atakuja” akasema Gosu Gosu
na Ruby akafikiri kidogo na
kusema
“Gosu Gosu unachokisema
ni cha kweli.Ngoja nimpigie
Yule mwanamke aliyenipigia
akajitambulisha kuwa ni mke
wake” akasema Ruby na
kuchukua simu yake
akazitafuta namba za Najma
akapiga lakini simu yake
haikupatikana.Akapiga mara
ya pili jibu likawa lile lile simu
ya Najma haikuwa ikipatikana
“Simu yake
haipatikani.Nitajaribu tena
baadae” akasema Ruby
“Tumekwama tena”
akasema Gosu Gosu
“Gosu Gosu hatupaswi
kushindwa.Machafuko
yanakwenda kuanza upya na
inaonekana wazi kwamba upo
mtandao ambao unachochea
machafuko hayo.Lazima kwa
namna yoyote ile tuufahamu
mtandao huo.Kwa sasa
tuendelee kufuatilia hali ya
vurugu inavyondelea jijini Dar
es salaam huku tukiendelea
kuchimbua zaidi kuhusu hawa
jamaa waliotoweka.Nina
uhakika tunaweza kupata kitu
Fulani” akasema Ruby
RIYADH – SAUDI ARABIA
Msafara wa watu
waliokwenda makaburini
kumzika Abu Dahir ulirejea
katika makazi ya Habiba
Jawad.Ilikuwa ni simanzi
kubwa na watu wengi walifika
kumpa pole Habiba kwa
kuwapoteza watoto wawili
ndani ya muda mfupi.Kifo cha
Abu Dahir kiliwasikitisha
wengi.
Saa moja za jioni Habiba
Jawad akaomba akina mama
waliokuwa wanamsaidia
kumpeleka katika nyumba
yake kwani mwili wake
haukuwa na nguvu hivyo
alihitaji
kutegemezwa.Akasaidiwa
kunyanyuka kisha
akategemezwa kuelekea katika
nyumba yake.Aliomba aachwe
katika sebule ya chini kabisa
halafu akaomba aitiwe Nawal
mjane wa Abu Dahir ambaye
aliletwa kisha akawataka wale
akina mama wawaache
wapumzike.Habiba akamtaka
Nawal amsaidie wakaingia
katika lifti kwani hakuwa na
nguvu za kupanda
ngazi.Waliingia katika sebule
maalum ya Habiba
akamuomba mtumishi wake
amtengenezee kahawa ambayo
ililetwa ndani ya muda
mfupi.Habiba akanywa kidogo
na kumtazama Nawal
aliyekuwa ameinamisha
kichwa huku machozi
yakiendelea kumtoka
“Pole sana Nawal najua
umeumia kwa kifo cha Abu
Dahir” akasema Habiba.Nawal
akafuta machozi halafu
akasema
“Mama mimi ndiye
ninayepaswa kukupa
pole.Unapitia kipindi kigumu
sana mama
yangu.Umewapoteza watoto
wawili ndani ya kipindi
kifupi.Hakuna ajuaye ni
maumivu kiasi gani
unayoyapitia hivi sasa na mimi
ni mmoja wa waliochangia
kukusababishia maumivu haya
makubwa.Nisamehe sana
mama sikukusudia kumuua
Abu Dahir.Imetokea bahati
mbaya tu” akasema Nawal
“Nawal nimekwisha
kwambia na ninarudia tena
kukwambia kwamba katu
usihisi hatia katika jambo
hili.Halikuwa kusudio lako na
ulikuwa unaniokoa
mimi.Kama usingekipiga kile
chungu kingenipata na
yawezekana mimi ndie ambaye
ningepoteza maisha badala
yake.Siwezi kukulaumu badala
yake ninapaswa
kukushukuru.Haya
yanayonitokea ni adhabu
kufuatia mambo mabaya
niliyoyafanya.Watu wengi
wamekufa kwa sababu
yangu.Ninamini Mungu
ananiadhibu na ninastahili
adhabu hii.Nawal hakuna
chochote kizuri nilichokipata
kwa haya yote niliyoyafanya
zaidi ya kuchuma
dhambi.Awali waliponifuata
wakaniambia wanataka
kunitumia kufadhili makundi
ya wanamgambo
walinidanganya kwamba ni
kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa
kifo cha mume wangu ambaye
niliamini aliuawa na vikosi vya
Israel kumbe aliuawa na
Marekani.Pamoja na kumwaga
damu ya watu wengi lakini
mume wangu hajarudi na
sijapata amani niliyotegemea
kuipata kwa kulipiza
kisasi.Baadae nilikuja
kugundua kwamba ni
Marekani ndio waliomuua
mume wangu na toka hapo
nikawa na hasira sana nao na
nikaanza kutafuta namna ya
kulipiza kisasi hadi
mlipojitokeza ninyi” akasema
Habiba na kunyamaza
“Mama kuna kitu nataka
kukwambia” akasema Nawal
“Sema usohofu Nawal”
“Baada ya haya yote
yaliyotokea sidhani kama
nitakuwa na amani kama
nitaendelea kuishi
hapa.Nimetafakari sana
nimeamua kurejea nyumbani
Marekani” akasema Nawal na
Habiba aliendelea kukaa
kimya akitafakari halafu
akasema
“Nawal hapa ni nyumbani
kwako.Wewe na Mathew ni
watoto ambao nimebaki nao
hivyo huna sababu ya kurejea
nyumbani” akasema Habiba
“Mama Habiba nafahamu
namna unavyotupenda mimi
na Mathew Mulumbi lakini
utanisamehe kwa maamuzi
haya.Naomba uniruhusu
niende nyumbani” akasema
Nawal
“Nawal bado ninakuhitaji
sana” akasema Habiba
“Nafahamu mama lakini
naomba uniruhusu niende
nyumbani.Sintakuwa na amani
hapa.Niache nikatulize akili na
pale nitakapokuwa sawa
nitarejea” akasema Nawal
“Nawal najua uko katika
wakati mgumu kufuatia kifo
cha Abu Dahir lakini
nakuhitaji kwa ajili ya misheni
muhimu sana” akasema
Habiba
“Misheni ipi
mama?akauliza Nawal
“Halafu hujanieleza alipo
Mathew.Yuko salama?akauliza
tena Nawal
“Nilitaka kukueleza
kuhusu Mathew lakini
likatokea lile tatizo na kila kitu
kikavurugika” akasema Habiba
na kunyamaza kidogo
“Mathew yuko katika
misheni kubwa hivi sasa”
“Misheni ipi
mama,unaweza ukanieleza?
“Nilikueleza kwamba
Marekani ndio waliomuua
mume wangu wa pili ambaye
ni baba yake Abu Dahir.Baada
ya kulifahamu hilo niliumia
sana na nikaanza mipango ya
kukisambaratisha kikundi
kidogo ndani ya CIA ambacho
kimekuwa kinashirikiana na
makundi mbali mbali ya
kigaidi.Niliwarejesha akina
Mathew waliokuwa katika
kisiwa cha Fiji kwani
nilimuhitaji Mathew kwa ajili
ya operesheni hiyo muhimu”
“Ni operesheni ipi hiyo
mama? Nawal akauliza
“Nadhani tayari
umekwisha sikia kwamba Rais
wa Uganda alipinduliwa na
jeshi”
“Ndiyo nilisikia taarifa
hizo tukiwa jijini Cairo
kutazama mapiramidi”
akasema Nawal
“Basi mpango ule ulisukwa
na hiki kikundi kidogo ndani
ya CIA kinachojihusisha na
mashirikiano na makundi ya
kigaidi.Mpango huu ni
kuiwezesha Marekani kupata
mafuta ya kutoka nchini
Uganda na ili waweze kufikia
lengo lao ililazimu kuchochea
vurugu za kidini na ndiyo
chanzo cha machafuko
makubwa yanayoendelea
Afrika mashariki hivi
sasa.Wanawatumia kundi la IS
katika kuchochea machafuko
hayo.Watu wanaendelea
kuuana huku Marekani
wakifurahia neema ya
mafuta.Huu ni unyama
mkubwa” akasema Habiba
“Mathew Mulumbi
ameenda huko ndiyo maana
hakuonekana katika msiba wa
Najma? Akauliza Nawal
“Mathew Mulumbi yuko
Afrika Mashariki lakini katika
misheni tofauti”
“Ni misheni gani
imempeleka Mathew
huko?akauliza Nawal
“Marekani na Iran ziko
katika mgogoro mkubwa hivi
sasa na marais wa nchi hizo
mbili wamekuwa wakitupiana
maneno mazito ya
vitisho.Katika mwendelezo
huo wa kutoleana vitisho Rais
wa Iran ametishia kuanza
kuwashambulia washirika wa
Marekani na baada ya hapo
ataishambulia Marekani na
kuiharibu kabisa.Hilo
limewatisha wamarekani na
kuwafanya wasimamishe
kwanza mipango yao ya
kuishambulia kijeshi Iran kwa
hofu kwamba yawezekana Iran
ikawa inamiliki silaha kama
kama inavyojitapa.Ukweli ni
kwamba mpaka sasa Marekani
bado hawana taarifa za
uhakika kuhusiana na silaha
ambazo Iran inazimiliki hivyo
wameamua kumtumia Mathew
Mulumbi katika misheni
maalum”
“Wanamtumia Mathew
Mulumbi? Nawal akashangaa
“Ndiyo Nawal.Nilitaarifiwa
na kiongozi wa idara hiyo
ndogo ndani ya CIA na
kunitaka nimtafutie gaidi
ambaye anafahamu mbinu za
kijasusi kwa ajili ya kumtuma
Iran kutekeleza kazi
maalum.Kwa kuwa tayari
nilikwisha kuwa na mipango
ya kuimaliza idara hiyo
niliamua kumpelekea Mathew
Mulumbi.Wamempokea
wakampima wakamuamini
kuwa anafaa na tayari
amekwisha tumwa kwenda
kuanza kutekeleza misheni
hiyo ambayo inaanzia nchini
Tanzania” akasema Habiba
“Mama hii ni misheni ya
hatari sana umemuingiza
Mathew.Atawezaje kuingia
nchini Iran?Nawal akauliza
“Mipango imeandalia na
ndiyo maana amekwenda
nchini Tanzania.Kule
anakwenda kulipua ubalozi wa
Marekani kisha atakamatwa na
dunia nzima itajua kwamba
Marekani imemkamata gaidi
ambaye amelipua ubalozi wake
jijini Dar es salaam.Baada ya
kumkamata watamuunganisha
na wanasayansi wa Iran ambao
walitekwa na Marekani na
baadae utatengenezwa
mpango ili Mathew aweze
kutoroka na wanasayansi hao
wa Iran na hiyo itakuwa ni
tiketi yake ya kuingia Iran.Kwa
hicho alichokifanya
kuwakomboa wanasayansi wa
Iran atapokelewa kama shujaa
na hapo ndipo atakapoanza
kuifanya kazi aliyotumwa”
“Mungu wangu ! akasema
Nawal
“Ni misheni ya hatari sana
hii mama na sina hakika kama
Mathew anaweza
akafanikiwa.Kwanza jina lake
litachafuka na dunia nzima
watamjua kuwa yeye ni gaidi
na muuaji.Vipi kuhusu ndugu
na familia yake?Unadhani
wataumia kiasi gani?Vipi
kuhusu nchi yake unadhani
watamuamini tena baada ya
taarifa kusambaa kwamba ni
gaidi na amelipua ubalozi wa
Marekani? Mama umeyafanya
maisha ya Mathew yawe
magumu sana na hata kama
akikamilisha misheni hii
maisha yake hayatakuwa sawa
tena na wewe utakuwa
umechangia kwa kiasi kikubwa
kuyaharibu” akasema Nawal
“Nawal nafahamu hiki
alichokwenda kukifanya
Mathew ni kitu cha hatari sana
lakini ni lazima aende katika
misheni hii ili aweze kumaliza
ugaidi duniani.Nimempeleka
makusudi ili aweze kufahamu
ni nani wanaofadhili makundi
mbali mbali ya ugaidi duniani
hivyo anatakiwa kuwa karibu
nao awasome na kisha
awamalize.Dunia nzima haijui
kama mzizi wa ugaidi uko
katika nchi inayopinga ugaidi
kwa nguvu zote.Hili hata
wamarekani wenyewe
hawalifahamu kama mzizi huu
uko ndani ya nchi yao.Hawajui
kama vita ambayo imekuwa
ikiendeshwa na nchi yao na
kupata ushindi ni kama hadaa
kwao na kwa
dunia.Watashangaa kujua
kwamba mashambulio mbali
mbali ambayo yamekuwa
yakifanywa na magaidi katika
nchi mbali mbali duniani.Ni
jukumu la Mathew Mulumbi
kuhakikisha kwamba dunia
inafahamu kila kitu kuhusiana
na hiki kinachofanywa na
Marekani kupitia idara hii
ndogo ndani ya CIA na ili
aweze kuimaliza idara hii
ndogo lazima ashirikiane nao
afahamu mambo yao na
akusanye ushahidi wa kutosha
kisha awamalize na dunia ijue
kila kitu” akasema Habiba
“Nafahamu ni misheni ya
hatari sana lakini ni lazima
Mathew aifanye na kama
akiikamilisha salama itakuwa
na faida kubwa kwa
dunia.Ninamuamini Mathew
na kuna sauti ndani mwangu
inayoniambia kwamba
Mathew ataitekeleza misheni
hiyo kama
alivyotumwa.Mathew atakuwa
salama.Nimejiuliza zaidi ya
mara elfu moja kama
nimefanya kitu sahihi
kumpeleka Mathew Mulumbi
katika misheni hii? Jibu
nililolipata ni kwamba
nimefanya kitu sahihi.Mathew
Mulumbi ni mtu sahihi.Ni
kweli jina lake litachafuka
baada ya kukamatwa kwa
kulipua ubalozi wa Marekani
jijini Dar es salaam lakini
mwisho wa misheni hii jina
lake litaandikwa kwa
dhahabu.Dunia nzima
itamuheshimu kwa kile
atakachokifanya.Nawal
umefika wakati wa kuifanya
dunia kuwa sehemu salama ya
kuishi lakini ni nchi hizi kubwa
ambazo zinafanya dunia isiwe
sehemu salama kwa kuchochea
machafuko hasa katika nchi za
kiafrika na zile ambazo
zimebarikiwa utajiri mkubwa”
akasema Habiba
“Mama lazima na mimi
uniunganishe na misheni
hii.Mathew hawezi kuifanya
peke yake.Anahitaji mtu wa
kumsaidia.Tafadhali mama”
akasema Nawal
“Hapana Nawal.Wewe una
misheni nyingine ambayo
unakwenda kuitekeleza
ambayo nayo ni ya muhimu
sana” akasema Habiba
“Misheni ipi hiyo
mama?akauliza Nawal
“Meli za Marekani
zimepanga foleni jijini Tanga
Tanzania zikipakia mafuta
yatokayo nchini
Uganda.Kumekuwa na dalili za
kupatikana kwa amani nchini
Tanzania na hii itaathiri kwa
kiasi kikubwa uchukuaji wa
mafuta kwani amani
ikipatikana, Tanzania
haitahitaji tena msaada wa
vikosi vya Marekani na zoezi la
uchukuaji wa mafuta
litakoma.Marekani wanahitaji
vikosi vyao kuendelea kuwepo
nchini Tanzania na Uganda ili
waendelee kuchukua mafuta
hivyo basi wamekuja na
mpango mwingine ambao
utawafanya waongeze vikosi
zaidi nchini Tanzania” Habiba
akanyamaza
“Hivi sasa wanasayansi wa
Marekani wanatengeneza
kirusi hatari ambacho
kitapelekwa kusambazwa
nchini Tanzania.Kirusi hicho
ambacho bado hakijajulikana
jina lake kinatarajiwa
kusababisha maangamizi
makubwa na kupelekea
Marekani kuongeza wanajeshi
zaidi nchini Tanzania kwa ajili
ya kutoa msaada hivyo vikosi
vya Marekani kuendelea kukaa
muda mrefu Afrika
Mashariki.Nataka ukavuruge
misheni hiyo” akasema Habiba
“Hiyo ni misheni ya hatari
sana mama lakini niko tayari
kuifanya kwa ajili ya kuzuia
njama ovu za
Marekani.Siamini kama nchi
yangu imefikia hatua hii ya
kutojali utu kwa ajili tu ya
kujipatia mafuta.Huu ni ukatili
mkubwa sana” akasema Nawal
“Wanaofanya hivi ni kundi
la watu wachache sana na hata
Rais wa Marekani hafahamu
chochote kwani ni kundi
linaloendeshwa kwa siri kubwa
sana na Rais hapaswi
kufahamu” akasema Habiba
“Hata kama ni kundi dogo
lakini linaiwakilisha Marekani
na endapo ikijulikana dunia
haitaelewa kama ni kundi la
watu wachache bali
watakachofahamu kuwa ni
Marekani.Nielekeze mama ni
namna gani nitaweza kuzuia
mpango huu usifanikiwe?
Akauliza Nawal
“Wanataka kutumia mtu
kutoka mtandao wa IS kwenda
kusambaza kirusi hicho nchini
Tanzania.Kesho mtu huyo
atakuja hapa kwa ajili ya safari
ya kuelekea Marekani
kuandaliwa kwa zoezi hilo la
kwenda kusambaza kirusi
Tanzania.Itakulazimu kwenda
nchini Tanzania” akasema
Habiba na kumtazama Nawal
“Kuna machafuko
makubwa na hadi sasa kiwanja
cha ndege kimefungwa lakini
ni lazima uende kwani bila
kuzuia mpango huo
usifanikiwe kirusi hicho
kinaweza kuwa hatari sana
kwa dunia”
“Mimi niko tayari kwenda
huko Tanzania mama siogopi
machafuko.Nataka nikaonane
na Mathew” akasema Nawal
“Misheni yako ni tofauti na
ya Mathew na hutatakiwa
kuonana na Mathew kwani
unaweza ukavuruga misheni
yake”
“Nani basi atakuwa
mwenyeji wangu
Tanzania?Sijawahi fika huko
na kama ningeweza kuonana
na Mathew ambaye yuko huko
Tanzania angenisaidia sana”
“Kumpata Mathew ni
ngumu kwa sasa lakini kuna
mtu ambaye Mathew ana
ukaribu naye yuko
Tanzania.Tutawasiliana naye
ili awe mwenyeji
wako.Naamini tukimwambia
kwamba wewe ni mtu wa
karibu na Mathew lazima
atakubali kukupokea” akasema
Habiba
“Itakuwa vizuri kama
akikubali”
“Ni mtu muhimu kwa
Mathew hivyo lazima
atakubali.Kesho huyo mtu
ambaye atakwenda kusambaza
kirusi hicho Tanzania atafika
hapa kabla ya kuelekea
Marekani.Baada ya
kumfahamu mtu huyo ni
nani,utaondoka kuelekea
Tanzania na nitaendelea
kuwasiliana nawe kukupa
taarifa za kila kinachoendelea
kuhusianana mpango huo”
akasema Habiba na ukimya
mfupi ukapita
“Nawal hii ni misheni
muhimu sana na haitakiwi
kushindwa kwani ukishindwa
kuzuia kirusi hicho
kusambazwa basi kinaweza
kuvuka mipaka ya Tanzania na
kuwa janga la dunia.Najua ni
jukumu zito lakini ni lazima
kwa namna yoyote ile
ulitimize” akasema Habiba
“Mama usiogope
nitalitimiza na kuhakikisha
mpango huo
haufanikiwi.Nifanyie
maandalizi na kila kitu
kitakapokuwa tayari nijulishe”
akasema Nawal.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Saa mbili za usiku jijini
Dar es salaam Mathew na
wenzake walimaliza kupata
chakula cha usiku kisha haraka
haraka masanduku ya silaha
yakapakiwa katika magari
halafu kila mmoja akashika
bunduki yake na kuingia
garini.Mathew akatakiwa
kwenda chumbani kwake
kupumzika.Hakutaka
kuwauliza wanakwenda wapi
lakini ni wazi kwa namna
walivyojiandaa walikuwa
wanakwenda kufanya
shambulio sehemu Fulani.Geti
likafunguliwa magari yale
yakatoka halafu jenereta
likazimwa na kukawa
giza.Ndani ya bohari dogo
ambako shughuli ya uundwaji
wa bomu ilikuwa inaendelea
walikuwa wanatumia jenereta
dogo lisilotoa sauti
Mathew aliingia chumbani
kwake akaubamiza mlango ili
walinzi wasikie kwamba tayari
yuko chumbani
“Lazima nitoke hapa usiku
huu nikawasake akina Ruby
nijue kama wako salama au
vipi” akawaza Mathew na
taratibu akaufungua mlango
na kunyata kuelekea katika
mlango wa jikoni ambao
haukuwa
umefungwa,akausukuma na
kuingia ndani ya jiko akatulia
kusikiliza kama kuna mtu
yeyote,kulikuwa na ukimya
mkubwa.Jikoni kulikuwa na
mlango wa kutokea nje
akakiminya kitasa taratibu
mlango ukafunguka akatoka
nje na kujibanza ukutani
kusikiliza lakini hakusikia
sauti yoyote zaidi ya sautio za
wadudu.Mchana wa siku ile
aliutumia vyema kuyasoma
mazingira ya mahala pale
hivyo alikwisha fahamu ni
wapi atapita.Kutoka pale jikoni
akatembea kwa tahadhari hadi
katika magari mawili mabovu
yaliyokuwa yameegeshwa
karibu na ukuta,pembeni ya
magari yale kulikuwa na lundo
la matofari
yamepangwa,akapanda
matofari yale na kuushika
ukuta.Alijilaza juu ya ukuta na
alipohakikisha kuko salama
akajirusha nje bila kuoa
ukelele.
“Sasa nielekee nyumbani
kwangu.Kutoka hapa hadi
nyumbani kwangu kuna
umbali kidogo lakini
nitajitahidi kukimbia na
kutumia njia za mkato.Sina
silaha yoyote lakini Mungu
atanifikisha salama” akawaza
Mathew huku akifuata
uchochoro uliompeleka hadi
barabarani.Mtaa wote ulikuwa
kimya kabisa na giza.Ni sauti
za mbwa wakibweka ndizo
zilisikika.Bila upoteza muda
Mathew akaanza kukimbia
akielekea katika barabara
kubwa
“Mimi si mgeni wa maeneo
haya hivyo siwezi kupata taabu
wakati wa kurudi” akawaza
Mathew akiendelea kukimbia
hadi alipoikuta barabara kuu
akaanza kuifuata.Mpaka
wakati huo hakuwa amekutana
na mtu hata mmoja
“Bado mapema sana lakini
jiji la Dar es salaam ni
tupu,liko kimya wakati jiji hili
limezoeleka ni jiji la
kukesha.Lazima hili jambo
limalizike haraka sana”
akawaza Mathew akiendelea
kukimbia.
Alikimbia kwa dakika
hamsini na mara kwa mbali
akashuhudia moto mkubwa na
kusikia makelele ya
watu.Akaendelea kukimbia
kwa tahadhari kubwa hadi
alipokaribia eneo lile
akakutana na kundi la watu
wakifurahia baada ya
kulichoma gari.Wengine
walikuwa na bunduki.Mathew
akaungana nao lakini ghafla
zikaanza kusikika risasi za
moto na kundi lile
likatawanyika.
“Twendeni huku ! akapiga
ukelele jamaa mmoja
aliyekuwa na bastora
mkononi,Mathew na watu
wengine wanne wakaanza
kumfuata
“Risasi zile zimetokea
wapi?akauliza Mathew wakati
wakikimbia
“Wanajeshi wamefika !
akajibu Yule jamaa mwenye
bastora huku akihema kwa
kasi Walikatisha vichochoro
kadhaa na mara mmoja wao
akajikwaa katika jiwe
akaanguka na kuanza kupiga
makelele ya kuvunjika
mguu.Mathew akawataka
wasubiri,akamuinua Yule
jamaa akamuweka begani
akaanza kukimbia naye.Baada
ya muda wakajikuta katika njia
ya kuelekea bonde la mto
Msanzi.Bado Mathew
aliendelea kumbeba Yule
jamaa mabegani hadi
walipofika katika lundo la
mchanga
wakapumzika.Mathew
akamuweka chini Yule jamaa
na wote wakaanza
kumtazama.Alikuwa
amevunjika mguu na vile vile
alichomwa na kipande cha
chupa tumboni.Hali yake
haikuwa nzuri kwani alipoteza
damu nyingi
“Tunamsaidiaje
huyu?akauliza Mathew
“Tunasubiri wenzetu waje
tujipange tuone namna ya
kumsaidia huyu
mwenzetu”akasema mmoja wa
wale jamaa.
“Hapana hatuwezi
kusubiri hadi wenzetu wafike
tutampoteza huyu jamaa”
akasema Mathew
“Unashauri nini?Mwingine
akauliza
“Tumpelekeni hospitali”
“Hospitali?! Huoni hali
ilivyokuwa mbaya huko
mtaani?
“Mnataka tumuache huyu
mwenzetu afie hapa?Mathew
akauliza kwa ukali
“Hii si sawa hata
kidogo.Hatuwezi kumuacha
mwenzetu afe wakati tunao
uwezo wa kumsaidia.Lazima
tumpeleke hospitali” akasema
Mathew
“Hospitali gani
tumpeleke?Karibu hospitali
zote zimejaa majeruhi”
“Tujaribu hospitali yoyote
ile lakini hatuwezi kumuacha
mwenzetu hapa.Kama ninyi
hamtaki mimi nitampeleka
mwenyewe ! akasema Mathew
kisha akamuinua Yule jamaa
akaanza kuondoka naye.Wale
jamaa wakashauriana halafu
wakaamua kuambatana na
Mathew wakasaidiana
kumbeba Yule jamaa
kupandisha kilima hadi
walipofika barabarani.Mathew
akamuweka begani Yule jamaa
na kuanza kutembea haraka
haraka wakiwahi
hospitali.Wakati wakitembea
Mathew akakiona kituo cha
mafuta kandoni mwa barabara
“Hiki ni kituo cha
mafuta?akauliza huku
akimulika kwa tochi ya mmoja
wa wale jamaa aliokuwa nao
“Ndiyo ni kituo cha
mafuta,kwa nini
umeuliza”akauliza mmoja wao
“Kuna gari zimeegeshwa
pale.Tunahitaji gari kwani
hatuwezi kuokoa maisha ya
mwenzetu kama tukiendelea
kutembea kwa miguu”
“Hatuwezi kupata gari
hapa.Watu wameweka hapa
magari yao kisha wakakimbia
na funguo zao” akasema Yule
jamaa
“Kuna yeyote ana kisu
hapa?:akauliza Mathew na
mmoja wao akampa kisu
kidogo
“Wewe mwenye bastora
nifuate” akasema Mathew
kisha kwa tahadhari
wakaelekea katika kituo kile
cha mafuta na kunyata hadi
katika magari yaliyokuwa
yameegeshwa pale
kituoni.Mathew akachagua
gari moja lenye rangi nyeusi
akakipiga teke kioo cha
upande wa dereva kikavunjika
akaingiza mkono ndani na
kuufungua mlango.Akamtaka
Yule jamaa amulike tochi ya
simu ndani ya gari,na kwa
kutumia kisu akang’oa sehemu
ya funguo kisha akakata nyaya
na kuzichuna akazigusanisha
na mara gari likawaka.Yule
jamaa aliyekuwa naye
hakuamini macho
yake.Mathew akaliondoa gari
wakampakia yule mgonjwa na
safari ya kuelekea hospitali
ikaanza.
“Umefanyaje hadi gari
likawaka?akauliza Yule jamaa
aliyekuwa na bastora
“Nina utaalamu kidogo na
magari”akajibu Mathew na
kupunguza mwendo wa gari
baada ya kukuta mawe
makubwa
barabarani.Wakashuka na
kwenda kuyatoa mawe yale na
safari ikaendelea.Walipita
barabara kadhaa hadi
walipofika katika hospitali ya
Mtodora ambako kulikuwa na
ulinzi mkali sana.Mathew
akawajulisha walinzi kwamba
kulikuwa na majeruhi garini
na walipomuona haraka
haraka wakafungua geti na
akina Mathew wakaingia
ndani.Haraka haraka majeruhi
Yule akachukuliwa na kwenda
kuanza kupatiwa huduma.
“Nini kinafuata?Mathew
akawauliza wale jamaa
“Kwa sasa ni kufuatilia
kujua kama wenzetu wako
salama na tujue tunakutana
wapi” akajibu mmoja wa wale
jamaa huku akitoa simu
akawasiliana na watu kadhaa
akawajulisha kwamba wao
wako katika hospitali ya
Mtodora kuna mwenzao
wamempeleka pale
ameumia.Alipomaliza
kuzungumza Mathew
akamfuata na kumuomba simu
yake awasiliane na mtu Fulani
na alipompa Mathew
akaziandika namba za simu za
Ruby
“Nina bahati ubongo
wangu una uwezo mkubwa wa
kuhifadhi vitu kwani
ninazikumbuka namba za simu
za Ruby” akawaza Mathew na
kupiga simu ikaanza kuita bila
kupokelewa.Akapiga tena
“C’mon Ruby pick up !
akawaza Mathew na safari hii
simu ikapokelewa.
“Hallow ! ikasema sauti ya
upande wa pili ambayo
Mathew aliitambua ni sauti ya
Ruby.
“Hallow Ruby ! akasema
Mathew
“Nazungumza na
nani?Ruby akauliza
“Ni mimi Mathew
Mulumbi.Uko salama Ruby?
“Mathew?! Ruby
akashangaa
“Ruby tuokoe muda.It’s
me Mathew.Uko wapi
tafadhali?
“Mathew?!! Ruby akauliza
tena
“Sikiliza Ruby nahitaji
kuonana nawe usiku huu.Ni
muhimu sana” akasema
Mathew
“Wewe ni Mathew
yupi?Mathew Mulumbi
ninayemfahamu hayupo
Tanzania”
“C’mon Ruby It’s me
Mathew.Ni mimi mpenzi
wako.Niko hapa Tanzania”
akasema Mathew na sekunde
kadhaa za ukimya zikapita
kisha Ruby akauliza
“Uko sehemu gani
Mathew?
“Niko hapa hospitali ya
Mtodora” akajibu Mathew
“Sawa ninatuma watu waje
hapo kukuchukua” akajibu
Ruby na kukata simu.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 3 : EPISODE 5
Ruby alihisi mwili wote
unamtetemeka baada ya
kuzungumza na Mathew
simuni.
“Huyu niliyeongea naye ni
Mathew kweli?Lakini sauti ni
yake .Kama kweli ni yeye
amekuja lini
Tanzania?Mathew mbona ana
maajabu namna hii?Alinipigia
simu Najma kutoka Saudi
Arabia lakini leo hii Mathew
yuko hapa amewezaje kuingia
nchini? Akawaza Ruby akiwa
amejishika kiuno.
“Nilidhani ninamfahamu
Mathew vizuri kumbe bado
sana.Itanichukua muda mrefu
kidogo kumfahamu huyu ni
mtu wa namna gani” akawaza
Ruby na kuchukua simu
akampigia Gosu Gosu
akamtaka aende mara moja
ofisini kwake.Gosu Gosu
ambaye alikuwa amekwenda
katika chumba chake
kupumzika akafika mara moja
ofisini kwa Ruby
“Kuna nini Ruby?akauliza
Gosu Gosu
“Gosu Gosu nimetoka
kuzungumza na Mathew muda
mfupi uliopita”
“Umezungumza na
Mathew? Akauliza
“Ndiyo nimezungumza
naye.Yuko hapa Dar es
salaam”
“Mathew yuko Dar es
salaam?! Gosu Gosu naye
akashangaa
“Ndiyo.Mathew yuko hapa
Dar es salaam.Nimezungumza
naye akiwa katika hospitali ya
Mtodora”
“Is he okay? Akauliza Gosu
Gosu
“I don’t know.Hajasema
chochote kuhusu anafanya nini
hapo hospitali ila amesema
kwamba anataka kuonana
nami usiku huu ni muhimu
sana” akasema Ruby
“Ruby una uhakika mtu
uliyezungumza naye simuni ni
Mathew Mulumbi? Gosu Gosu
akauliza
“Naifahamu sauti
yake.Sina shaka ni yeye.Lakini
swali ni je amefikaje hapa
nchini? Ameingiaje? Ni juzi tu
nimepigiwa simu na Yule
mwanamke Najma kutoka
Saudi Arabia akisema kwamba
Mathew alikuwa ananitafuta
halafu leo hii yuko hapa
nchini.Haya ni maajabu Gosu
Gosu”
“Si maajabu Ruby.Ni kweli
kabisa.Huyo ndiye Mathew
Mulumbi ambaye haishiwi
maajabu”
“Una uhakika ni yeye?
akauliza Ruby
“Nina uhakika
Ruby.Ninakwenda huko
Mtodora kumchukua”
akasema Gosu Gosu
“Hapana huwezi kwenda
peke yako.Utaongozana na
kikosi cha makomando wetu
kwenda huko hospitali”
akasema Ruby na kumuita
ofisini kwake kiongozi wa
kikosi kile cha makomando
ambaye alifika haraka
akamtaka achukue
makomando0 wanne
waongozane na Gosu Gosu
kuelekea hospitali ya Mtodora
kumchukua Mathew Mulumbi.
Haraka haraka waliingia
katika gari lao maalum
lisilopenya risasi wakaondoka
kuelekea hospitali ya Mtodora
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 3 : EPISODE 6
Gosu Gosu na timu ya
makomando waliwasili katika
hospitali ya Mtodora kisha
wakamjulisha Ruby kuwa
tayari wamewasili na Ruby
akapiga namba ile ya simu
ambayo aliitumia Mathew
kuwasiliana naye.Simu
ikapokelewa na sauti nyingine
“Samahani kaka kuna mtu
mmoja ametumia simu hii
kuwasiliana nami si muda
mrefu sana.Uko naye
karibu?Ninaweza kuzungumza
naye?akauliza Ruby akiwa na
wasiwasi
“Sawa niko naye hapa
karibu” akasema Yule jamaa
na kumfuata Mathew
akampatia simu
“Kuna mtu anataka
kuzungumza nawe” akasema
Yule jamaa na kumpa simu
Mathew
“Hallo” akasema Mathew
“Mathew kuna watu
nimewatuma hapo hospitali
waje kukuchukua
wakiongozwa na Gosu
Gosu,tayari wamekwisha fika
wako getini” akasema Ruby
“Ahsante Ruby” akasema
Mathew na kukata simu
akamfuata Yule jamaa
“Mimi
ninaondoka.Hakikisheni
mwenzenu amepata nafuu
ndipo muondoke hapa
hospitali” akasema Mathew
ambaye alikuwa amechafuka
damu
“Unakwenda wapi? Ni
hatari sana huko mitaani”
akasema yule jamaa ambaye
hadi muda huo hawakuwa
wamefahamishana majina yao
“Usijali nitakuwa salama”
akasema Mathew na kuanza
kupiga hatua kuondoka halafu
akageuka
“By the way gari lile
mtalirejesha mahala
tulipolichukua.Kingine
nawashauri baada ya
mwenzenu kupata nafuu
rudini nyumbani msiendelee
kushiriki katika vurugu hizi
ambazo hazina manufaa
yoyote kwenu” akasema
Mathew na kuondoka zake
akaenda getini na mara
akasikia akiitwa
“Mathew”
Mathew aliitambua sauti
ile akasimama kutazama
ilitoka wapi na mara
akamuona mtu mmoja akiwa
ameinua mkono akimuelekeza
mahala alipo akamfuata
“Gosu Gosu ! akasema
Mathew kwa furaha
wakakumbatiana
“Mathew siamini kama
nimekuona tena kaka yangu !
akasema Gosu Gosu
“Mimi ndiye siamini kama
nimefanikiwa kuonana tena
Gosu Gosu ukiwa katika hali
hii.Vipi maendeleo yako?
“Ni kama
unavyoniona.Ninaendelea
vyema kabisa” akasema Gosu
Gosu
“Vipi kuhusu Ruby?Naye
anaendeleaje?
“Naye vile vile anaendelea
vyema kabisa” akasema Gosu
Gosu na kumuongoza Mathew
kuelekea katika gari ambalo
kulikuwa na watu watatu
wanne wamesimama nje
wakiwa na bunduki .Gosu
Gosu akawajulisha watu wale
kwamba mtu waliyemfuata
pale hospitalini ni Yule
aliyeongozana naye.Mathew
akawasalimu wale
makomando kisha wakaingia
garini na safari ya kuelekea
makao makuu ya SNSA
ikaanza.
“Tunaelekea wapi?Ruby
yuko wapi?akauliza Mathew
“Tunaelekea SNSA pale
ndipo tumeweka kambi kwa
sasa kufuatia vurugu hizi
zinazoendelea” akasema Gosu
Gosu
“Nawe pia uko SNSA?
Akauliza Mathew
“Ndiyo niko SNSA Ruby
aliniomba niwe msaidizi
wake.Nilikubali ili kuhakikisha
anakuwa salama muda wote
kwani kazi anayoifanya ni ya
hatari kubwa” akasema Gosu
Gosu
“Ahsante sana Gosu Gosu
kwa kuhakikisha Ruby
anakuwa salama.Vipi kuhusu
Lucy naye yuko salama?
“Lucy yuko salama kabisa
ninakwenda kila siku kujua
maendeleo yake.Kwa bahati
mbaya pale katika kambi yetu
wanaoruhusiwa ni
wafanyakazi tu wa SNSA
vinginevyo ningemchukua pale
ili awe salama zaidi” akasema
Gosu Gosu
Walifika ofisi kuu ya SNSA
salama.Hawakupata matatizo
yoyote njiani.Mathew
aliongozana na Gosu Gosu
wakaingia ndani na moja kwa
moja wakaelekea katika ofisi
ya Ruby ambaye hakujua
kama tayari
wamerejea.Alikuwa
amejiegemeza katika kiti
akionekana kuwa katika
mawazo mengi.Gosu Gosu
ndiye aliyemstua baada ya
kugonga mlango na kufungua
akaingia ndani huku Mathew
akimfuata kwa nyuma.Ruby
alipomuona Mathew akainuka
na kumkumbatia kwa nguvu.
“Mathew my love !
akasema Ruby
“Habari Ruby” akasema
Mathew
“Siamini kama kweli leo
hii niko nawe tena.Huu ni
kama muujiza kwangu”
akasema Ruby
“Huu si muujiza Ruby.Ni
kweli niko hapa” akasema
Mathew lakini Ruby bado
alisimama akiendelea
kumshangaa
“Ruby nimefurahi
kuwaona wewe na Gosu Gosu
mko salama lakini sina muda
mrefu sana wa kukaa hapa”
akasema Mathew
“Mathew tafadhali kabla
hujatueleza chochote
nihakikishie kama uko salama”
“Niko salama kabisa.Hizi
damu nilimsaidia mtu
aliyeumia nikamfikisha
hospitali lakini mimi niko
salama kabisa msihofu”
akasema Mathew na kuketi
kitini
“Nashukuruni ndugu
zangu nimefanikiwa
kuwaoneni tena mkiwa
salama.Nilikuwa nahofia sana
usalama wenu kwani ninyi ni
watu wangu wa pekee kabisa”
akasema Mathew
“Tuko salama
Mathew.Tumeweka kambi
hapa katika ofisi yetu na
wafanyakazi wetu wote
wanaishi hapa” akasema Ruby
“Ruby nina muda mchache
sana wa kuwepo nanyi hapa
hivyo nataka nijielekeze moja
kwa moja katika yale ya
msingi.Nina mambo machache
ya kuwaeleza moja ni kwamba
nimeingia hapa nchini jana
usiku.Nimekuja nchini kwa
operesheni maalum.Pili ni
kuhusiana na hizi vurugu
zinazoendelea hapa nchini hivi
sasa.Nataka kujua kuna
chochote mnakifahamu hadi
sasa kuhusiana na vurugu hizi?
Mmekwisha zifanyia
uchunguzi?akauliza Mathew
“Ndiyo.Tumeanza
kuzifanyia uchunguzi tayari ili
kuupata mzizi wake” akasema
Ruby na kumuelezea Mathew
namna walivyofanya
uchunguzi na mahala
walipofikia katika uchunguzi
wao
“Kwa hapo mlipofika
ilikuwa lazima mkwame kwa
sababu suala hili lina nguvu
kubwa kutoka nje ya nchi”
akasema Mathew
“Ndani ya idara ya ujasusi
ya Marekani CIA kuna idara
ndogo ambayo
inajishughulisha na
mahusiano na makundi mbali
mbali ya kigaidi
duniani.Wanayatumia
makundi hayo ya kigaidi kwa
ajili ya manufaa ya
Marekani.Wamekuwa
wakilitumia sana kundi la IS
katika eneo la Mashariki ya
kati.Wanalitumia kundi hili
kuanzisha mashambulio
sehemu Fulani kisha hupeleka
vikosi vyao kwa kigezo cha
kuwasaka magaidi kumbe
wanakuwa na agenda ya siri
nyuma yake na mara nyingi
hufanya hivyo kwa nchi zile
ambazo zinakuwa na utajiri wa
kitu Fulani” Mathew
akanyamaza akamtazama
Ruby ambaye alikuwa anafuta
machozi
“Machafuko haya
yanayoendelea hapa nchini na
Uganda ni mpango wa
Marekani”
“Mpango wa
Marekani?Ruby akashangaa
“Ndiyo Ruby”
“Marekani wamekitumia
kikundi cha kigaidi cha IS
kuchochea vurugu hizi
zinazoendelea hivi sasa na
lengo kubwa la kufanya hivyo
ni ili wapate nafasi ya kuleta
vikosi vyao hapa Tanzania na
kuchukua mafuta kutoka
Uganda.Hivi tuzungumzavyo
meli kubwa za mafuta za
Marekani zmepanga foleni
katika bandari ya Tanga
zikipakia mafuta kutoka
Uganda”
“Jesus Christ ! akasema
Gosu Gosu
“Mathew nakubaliana
nawe na ahsante kwa
kutufumbua macho kwani bila
wewe ingetuchukua miaka
kuweza kuligundua
hili.Vurugu hizi zilianzia
nchini Uganda kwa kiongozi
mmoja wa dini ya kiislamu
kuuawa kisha likatokea
shambulio la bomu la kujitoa
mhanga katika kanisa ambalo
lilisababisha vifo vya watu
wengi.Baada ya hapo wakristu
wakaanzisha vurugu kwa
kuchoma nyumba za ibada za
waislamu na kisha wakaanza
kushambuliana.Kwa hapa
Tanzania vurugu hizi zilianzia
jijini Tanga ambako nako
kulifanyika mashambulio
katika makanisa na misikiti
mashambulo yaliyowalenga
viongozi wa dini na kupelekea
waumini wa dini hizi mbili
kuanza kushambuliana na
machafuko yakaenea hadi jijini
Dar es salaam.Ukitazama miji
ambayo imekuwa na
machafukoi makubwa kwa
hapa Tanzania ni Dar es
salaam na Tanga na baada ya
maelezo haya ya Mathew sasa
picha imeonekana kwamba
vurugu hizi ziko kimkakati
zaidi.Huwezi kuchukua mafuta
ya Uganda bila kudhibiti
bandari ya Tanga na ndicho
walichokifanya” akasema Ruby
“Lakini IS hawako peke
yao.Kuna watu wa ndani ya
nchi ambao wanashirikiana
nao katika jambo hili na
yawezekana miongoni mwao
ni hao ambao tayari mmeanza
kuwafanyia uchunguzi na
hawajulikani mahala
walipo.Suala hili halitaweza
kumalizika hadi pale
litakapochimbwa hadi mzizi
wake.Tumekwisha fahamu
nani walio nyuma ya hizi
vurugu lakini lazima vile vile
kujua wanaochochea vurugu
hizi hapa nchini ni akina nani
na baada ya kuwabaini basi
wawekwe wazi dunia iwajue na
hii ndiyo itawafumbua macho
wananchi kwamba
walishawishiwa kuingia katika
zile vurugu bila kujua”
akasema Mathew
“Toka mwanzo niliamini
kwamba hili suala linaweza
kuwa na mkono kutoka nje ya
nchi na sasa tumeufahamu
ukweli” akasema Gosu Gosu
“Rais alikutana na kufanya
mazungumzo na mufti wa
Tanzania halafu mufti akatoa
hotuba yake akiwahusia
waislamu kuachana na vurugu
zile lakini usiku wa kuamkia
leo aliawa” akasema Mathew
“Mauaji haya ya mufti
yamekwamisha juhudi za
kutafuta amani kwani viongozi
wengine wa dini ambao
walihitaji kuzungumza na Rais
wameingiwa na woga”
akasema Ruby
“IS ndio waliomuua mufti
ili kuchochea vurugu hizi kwa
maelekezo ya
Marekani.Ilionekana vurugu
zinaanza kupungua na
Marekani wanahitaji vikosi
vyao kuendelea kukaa Afrika
mashariki kwa muda mrefu
zaidi hivyo walipanga mauaji
yale ya mufti wakiwatumia IS
ili kuwachochea waislamu na
wakristu waendelee
kushambuliana”
“Tumejiuliza sana kuhusu
mauaji yale ya mufti tukakosa
jibu.Tunashukuru Mathew
kwa kutufumbua macho”
“Nimekuja hapa kuwapeni
taarifa hizi ili ziwasaidie katika
uchunguzi wa suala hili.
akasema Mathew
“Mathew we need you !
akasema Ruby
“I know. I know”akasema
Mathew na kumtazama Ruby
“Ruby I’m very sorry
sintaweza kushirikiana nanyi
katika suala hili.Nina misheni
nyingine kubwa zaidi ambayo
imenileta hapa Tanzania ila
nitakachoweza kuwasaidia ni
kuwapa taarifa muhimu
ninazozifahamu na ninyi
mtaendelea.SNSA ni idara
kubwa naamini mtaweza
kulifanikisha suala hili”
akasema Mathew
“Mathew we real need
you.Tumekwama na
hatutaweza kulitatua jambo
hili bila wewe” akasema Ruby
“Jambo hili lina pande
mbili.Kuna upande wa ndani
na upande wa nje.Ninyi
mtashughulika na upande wa
ndani mimi nitashughulikia
upande wa nje.Upande wa
ndani kuna kundi la IS na
kuna watu ambao
wanawasaidia IS kufanikisha
lengo lao la kuchochea
vurugu.Hapa mnatakiwa
kuwatafuta watu hao ni akina
nani pamoja na kulimaliza
kundi la IS hapa
Tanzania.Kuwakamata watu
wa ndani wanaoshirikiana na
IS kuchochea vurugu hizi bado
haitakuwa imesaidia kumaliza
tatizo kwani nguvu ya nje ni
kubwa zaidi na wanaweza
wakafanya lolote ili mradi
kuendeleza machafuko ili
waendelee kuchota
rasilimali.Mimi nitashughulika
na nguvu hii ya nje.Mambo
haya yote yanafanywa na
kikundi kidogo cha watu
ambao wao wanadai Marekani
iko katika mikono yao na
wanaiendesha
watakavyo.Kikundi hicho
kidogo ndicho
kinachoisumbua dunia hivi
sasa na kusababisha
machafuko kila sehemu.Kila
ukifungua taarifa za habari
hukosi kukuta kuna taarifa za
tukio la kigaidi sehemu Fulani
na mengi ya matukio haya
yanafanikishwa na kikundi
hiki.Umefika wakati wa
kukimaliza kikundi hiki na
kupunguza kama si kumaliza
kabisa ugaidi duniani kwa
sababu vikundi vingi vya
ugaidi vinategemea ufadhili
kutoka kwa kikundi hiki
kidogo.Ninaomba mniamini
ndugu zangu kwamba
ninakwenda kukimaliza
kikundi hiki.Ni misheni
ngumu na ya hatari sana lakini
lazima
niikamilishe.Wamemwaga
damu ya ndugu zetu na siwezi
kukubali damu ya mtanzania
ikapotea bure lazima ilipwe
hivyo nawataka muhakikishe
mnawashughulikia watu wa
ndani wakati mimi
nikishughulika na watu wa
nje.Kwa pamoja tutalifanikisha
hili jambo” akasema Mathew
“Mathew ni asubuhi ya leo
mimi na msaidizi wangu Gosu
Gosu tulipokwama hatujui nini
tufanye tulianza kukujadili
kwamba laiti ungekuwepo
ungetusaidia kutuondoa katika
mkwamo huu kwani sisi
hatuna ujuzi mkubwa katika
masuala haya kama
wewe.Nilimpigia Najma ili
niweze kuzungumza nawe
lakini simu yake haikuwa
ikipatikana” akasema Ruby na
sura ya Mathew ikabadilika
baada ya kusikia jina la Najma
likitajwa
“Umesema Najma?
Akauliza Mathew
“Ndiyo”
“Najma yupi ulimpigia
kutaka kuzungumza nami?
“Najma mke wako.Huna
mke anaitwa Najma?akauliza
Ruby na Mathew akavuta
pumzi ndefu wakatazamana
“Kuna kitu unataka
kukisema Mathew? Ruby
akauliza
“Umefahamuje kuhusu
Najma?Ulikuwa unanifuatilia?
Mathew akauliza
“Ndiyo maana uliniambia
nisikufuatilie ili nisifahamu
kama umebadili jina lako na
unaitwa Abu Zalawi raia wa
Saudi Arabia na pia umemuoa
Najma? Akauliza Ruby
“Ulinifuatilia
ukayafahamu haya?Kwa nini
ukapuuza maelekezo yangu
Ruby?akauliza Mathew
akimtazama Ruby kwa macho
makali.
“Sikukufuatilia
Mathew.Ninaheshimu
makubaliano yetu.Nilipigiwa
simu na Najma mwenyewe
akajitambulisha kwangu kama
mke wako na kwamba ulikuwa
unanitafuta simuni
hukunipata.Alinipigia kuuliza
kama ninakufahamu lakini
alikutaja kwa jina la Abu
Zalawi na si Mathew
Mulumbi.Nilimweleza
sikufahamu na wala sina rafiki
anaitwa kwa jina hilo.Baadae
nilimpigia na kumtaka
anitumie picha za huyo Abu
akadai kwamba hana
picha.Nilipatwa na wasi wasi
labda Uingereza wameanza
kunitafuta ikanilazimu kuingia
mtandaoni kutafuta ndipo
nikakupata” akasema Ruby
akamtazama Mathew.Macho
yake yalilengwa
machozi.Mathew akavuta
pumzi ndefu kisha akasema
“Ni kweli.Yote
aliyokwambia Najma ni kweli
kabisa lakini hapa si mahali
pake tutayazungumza hayo
siku nyingine.Nataka
tujielekeze katika jukumu lililo
mbele yetu” akasema Mathew
na Ruby akafuta machozi
“Mathew naomba
utuamini kwamba tumekwama
na tunahitaji sana msaada
wako.Tafadhali endelea na
misheni yako baada ya
kuhakikisha kwamba
tumelimaliza hili suala na nchi
iko salama.Nisingekuomba
haya kama tungekuwa na
uwezo huo” akasema Ruby
“Ruby siwezi.Misheni
ninayokwenda kuitekeleza ni
kubwa na yenye manufaa kwa
dunia nzima.Ninakwenda
katika misheni ya hatari kuliko
misheni zote nilizowahi
kushiriki”
“Mathew ni misheni ipi
hiyo unayokwenda kuifanya
ambayo ni muhimu kuliko
kuisaidia nchi yako?akauliza
Ruby
“Ninakwenda kukiondoa
kikundi hiki kidogo ambacho
kimekuwa kikishirikiana na
magaidi na kuharibu amani ya
dunia”
“Mathew ..! akasema Ruby
lakini Mathew akamkatisha
“Don’t say anything
Ruby.Tayari ninafahamu kile
unachotaka kukisema.Kikundi
hiki ndicho mzizi wa haya
machafuko yanayoendelea
hapa nchini hivyo misheni hii
pia ni mwendelezo wa
kuisaidia nchi yetu na dunia”
akasema Mathew na ukimya
ukapita
“Kuna mambo ambayo
mtayasikia kuhusu mimi lakini
nawaomba mtakapoyasikia
msiyaamini hata kidogo.Niko
katika misheni nzito na hayo
yatakayotokea na kunihusisha
mimi ni sehemu ya misheni
hiyo.Utakuwa ni mshangao
kwa wengi lakini ninyi
nawaomba msishangae kuweni
na imani na mimi.Baada ya
kuikamilisha misheni hiyo
nitarejea nyumbani”akasema
Mathew na kuwatazama akina
Ruby ambao kila mmoja
alibaki na maswali kichwani
“Tuachane na suala
hilo.Kuna mtu anaitwa Assad
Ismail.Huyu anaongoza kundi
la IS katika ukanda huu wa
Afrika Mashariki na
kati.Makazi yake ni Mombasa
Kenya lakini kwa sasa yuko
hapa nchini na ndiye
anayesimamia jukumu la IS la
kuchochea vurugu.Yeye na
watu wake ndio waliomuua
mufti jana na wao ndio
waliofanya na wanaoendelea
kufanya mauaji ya viongozi
wadini ili kuchochea
vurugu.Mnatakiwa kumpata
huyu Assad kwani atawasaidia
sana kufahamu mambo mengi
kuhusiana na watu
wanaoshirikiana nao hapa
nchini na mnaweza
mkafahamu vile vile kuhusiana
na wale ambao mnahisi
wanahusika katika machafuko
haya lakini wamepotea na
hawajulikani walipo.Sifahamu
Assad anaishi wapi hapa Dar
es salaam lakini kuna mtu
ambaye anaweza akawaongoza
kujua mahala alipo Assad.Mtu
huyo anaitwa Marwan
Hossam.Huyu anaishi kwa
Botha nyumba namba 604.Hii
ni nyumba wanamoishi
magaidi wa IS na mipango yao
yote ya mashambulio
hupangwa katika nyumba
hii.Mkivamia nyumba hii
mtapata mambo mengi
yanayoweza kuwasaidia
kufahamu mambo mengi
kuhusiana na hili suala”
akasema Mathew
“Mathew tunashukuru
sana kwa taarifa hii.Nashauri
kwa nini tusiende kuvamia
nyumba hiyo usiku huu tukiwa
pamoja nawe kabla
hujaendelea na misheni yako?
Akauliza Gosu Gosu
“Kwa leo haiwezekani
Gosu Gosu.Jambo hili
mtalifanya usiku wa kesho
baada ya mimi kuondoka.Mimi
ninamaliza misheni yangu
kesho usiku na kuondoka na
ninyi mtaenda kuvamia
nyumba hiyo na kumkamata
Marwan Hossam ambaye
atawapeleka mahala alipo
Assad”
“Kwa nini leo haiwezekani
Mathew?Tunao makomando
wetu ambao watatusaidia
kuvamia nyumba hiyo”Ruby
naye akasisitiza.
“Haiwezekani kwa sababu
ninaishi ndani ya nyumba
hiyo” akasema Mathew na
mstuko uliowapata Ruby na
Gosu Gosu ulikuwa mkubwa.
“Unashirikiana
nao?akauliza Ruby akionyesha
sura ya wasi wasi
“Ni sehemu ya misheni
yangu ndiyo maana
nikatangulia kuwaomba
kwamba msistuke kwa
mtakachokisikia kuhusu mimi
hapo baadae” akasema
Mathew
“Kitu gani umekuja
kukifanya Mathew?
Umewezaje kuingia hapa
nchini? Akauliza Ruby
“Ruby natamani sana
niwaeleze lakini sitakiwi
kufanya hivyo.Ninawaomba
mniamini ndugu
zangu.Naamini utafika wakati
ambao nyote mtashikwa na
butwaa lakini naomba ninyi
wawili muendelee kuwa na
imani nami.Yote mtakayosikia
ni sehemu ya misheni yangu
kubwa” akasema Mathew
“Mathew unatuogopesha
sana kwa haya maneno
yako.Nini kinakwenda
kutokea?akauliza Gosu Gosu
“Usihofu Gosu Gosu
utasikia tu.Nawaombeni
ndugu zangu kwa sasa
tuliweke pembeni hilo na
tujielekeze katika hiki
kinachoendelea hapa
nyumbani.Suala hili ni kubwa
na ninawaomba muwe na
umakini mkubwa sana
mnapolishughulikia.Magaidi
hawa wa IS wana silaha nzito
na wanapata msaada kutoka
kwa vikosi vya Marekani.Kwa
mfano Assad anapotoka
mahala anakoishi kwenda
katika nyumba hiyo ambayo ni
kambi ya magaidi
husindikizwa na gari la doria la
vikosi vya Marekani.Hali ni
mbaya huko mtaani na kwa
hili walilolifanya la kumuua
Mufti litaongeza zaidi
machafuko haya.Usiku huu
wameondoka tena na silaha
nzito naamini kuna mahali
wamekwenda kufanya
shambulio” akasema Mathew
“Mathew nakushukuru
sana kwa kuja.Kwa mara
nyingine tena umedhihirisha
ni namna gani ulivyo na
umuhimu mkubwa kwa nchi
hii.Hatukuwa tukifahamu
chochote kuhusu haya
yanayoendelea.Tulifika mahala
tukakwama na hatujua wapi
kwa kutokea lakini umetokea
wewe na kutumulikia mwanga
sasa tumepata sehemu ya
kuanzia.Naamini misheni hiyo
uliyonayo ni muhimu sana
kwani hujawahi hata mara
moja kukataa kufanya misheni
kwa ajili ya nchi
yako.Tumekuelewa Mathew na
tunakutakia kila la heri katika
hiyo misheni yako ambayo
kama ulivyotuhakikishia ni
kwamba itakuwa na manufaa
makubwa sana kwa nchi na
dunia nzima.Sisi tutaendelea
kusimama nawe na
kukuombea uweze kumaliza
salama operesheni hiyo.Muda
wowote utakapohitaji msaada
wetu sisi tupo tayari
kukusaidia” akasema Ruby
“Ruby ninashukuru kwa
kunielewa.Muda wowote
nitakapohitaji msaada wenu
nitawasiliana nanyi haraka
sana” akasema Mathew na
ukimya ukapita
“Ruby na Gosu Gosu
ninashukuru tena kwa
kuonana nanyi ndugu zangu
na kuhakikisha mko
salama.Nilikuwa na wasiwasi
mkubwa kuhusiana na
usalama wenu lakini kwa sasa
nina amani na hata huko
nitakapokuwa nitakuwa na
amani kwamba ndugu zangu
wako salama.Naomba sasa
mniruhusu niondoke lakini
naomba mnipatie mavazi
nibadilishe” akasema Mathew
na Gosu Gosu akaenda
kumletea mavazi ya
kubadilisha kwani nguzo zile
alizokuwa amevaa zilikuwa
zimechafuka damu.
“Mathew sijui niseme
nini.Sijui ni………” akasema
Ruby baada ya Gosu Gosu
kuondoka
“Don’t say anything.Pray
for me.I promise I’ll come
back” akasema Mathew
“Mathew nina wasi wasi
sana kuhusu usalama wako”
“Usihofu Ruby.Nitakuwa
salama na nitarejea.Narudia
tena kuwaomba hakikisheni
kwa namna yoyote ile
mnawapata hawa watu
niliowapa taarifa zao ili nchi
iwe na amani.Tanzania
haikupaswa kuwa namna
hii.Mambo kama haya
tulikuwa tunayaona katika
nchi nyingine lakini sasa
yamefika kwetu.Hali ni mbaya
sana huko
mitaani.Nakuhakikishia Ruby
kwa hiki walichokifanya
kumwaga damu za watanzania
namna hii huku wao
wakiendelea kushangilia
neema ya mafuta kutoka
Uganda hawatabaki
salama.Nitahakikisha kikundi
hiki kidogo cha hawa watu
ninakifutilia mbali.Ni misheni
ndefu na ya hatari lakini
nitakufa nikijaribu.Bila
kukiondoa kikundi hiki dunia
haitakuwa mahala salama”
akasema Mathew
“Mathew sijui kwa nini
ninahisi baridi kila
unapotamka kuhusiana na
misheni hiyo ya hatari ambayo
umeshindwa kutueleza ni
misheni gani.Kama ingekuwa
ni kwa ridhaa yangu
ningekuzuia usiende huko
lakini siwezi.Oh Mathew !
akasema Ruby na kuinamisha
kichwa machozi yalikuwa
yanamtoka
“Ruby huu si wakati wa
kumwaga machozi.Damu za
watanzania wenzetu
zinamwagika hivyo hatupaswi
kumwaga machozi tunatakiwa
kupambana kuhakikisha
tunarejesha maisha kuwa ya
kawaida” akasema Mathew na
Gosu Gosu akaingia.Mathew
akavua zile nguo zilizochafuka
damu na kuvaa nguo
alizopewa na Gosu Gosu.Ruby
akasimama na kumkumbatia
Mathew
“Mathew please be safe my
love” akasema Ruby
“I will” akajibu Mathew na
kumuachia Ruby
wakaongozana kutoka nje
wakaelekea katika gari lile la
makomando Mathew
hakugeuka nyuma kumtazama
Ruby akaingia garini na gari
likaondoka,Ruby akarejea
ofisini kwake akajifungia
akilia.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 3 : EPISODE 7
Mathew aliwataka akina
Gosu Gosu wamuache karibu
na mtaa ilipo nyumba ile ya
magaidi .
“Gosu Gosu tafadhali
hakikisha Ruby anakuwa
salama.Hakikisheni pia amani
inarejea hapa nchini tayari
nimekwisha wapa mwanga
sehemu ya kuanzia” akasema
Mathew
“Mathew ninakushukuru
sana kwa taarifa hizi
ulizotupa.Nakuahidi hakuna
atakayesalia.Tutawasaka wote
hadi mtu wa mwisho” akasema
Gosu Gosu
“Ahsante Gosu
Gosu.Mbaki salama” akasema
Mathew kisha akaanza
kukimbia kuelekea katika mtaa
alikofikia.Kulikuwa na ukimya
mkubwa.Alifika katika nyumba
yao akazunguka upande wa
nyuma akapanda ukuta na
kurukia ndani bila kutoa
ukelele.Hakukuwa na mtu
yeyote mahala pale akatembea
kwa tahadhari kuelekea katika
mlango wa nyuma akaufungua
na kuingia jikoni kisha
akaelekea moja kwa moja
chumbani kwake.Ilipata saa
kumi kasoro za alfajiri.Mathew
akajilaza kitandani.
“Ahsante Mungu kwa
kunirejesha salama bila hawa
watu kujua” akasema kwa
sauti ndogo.
“Nimefurahi kuwakuta
Ruby na GosuGosu wakiwa
salama.Hiki ndicho kitu
ambacho nilikuwa naomba
sana kuwakuta watu hawa
wako salama.Ninashukuru vile
vile kwa Gosu Gosu kuungana
na Ruby na hii inanipa uhakika
mkubwa kwamba Ruby
atakuwa salama.Hata hivyo
kuna kitu ambacho
sikukitegemea kabisa.Najma
kumpigia simu Ruby na
kujitambulisha kuwa yeye ni
mke wangu.Nilistuka
sana.Sikutegemea kabisa kitu
kama hiki kutokea.Sikutaka
Ruby afahamu chochote
kuhusu maisha yangu kule
Saudi Arabia.Nimejaribu
kumtuliza lakini ameumia.Kwa
nini Najma alimpigia simu
Ruby? Akajiuliza Mathew na
kukumbuka kitu.
“Nakumbuka siku ile
tuliporejea kutoka Fiji na
Habiba akanieleza kuhusu
machafuko yanayoendelea
hapa Tanzania nilitaka
kumpigia simu Ruby kujua
kama yuko salama lakini simu
yake haipatikani nakumbuka
Najma alikiona kitabu kile
nilichokuwa nimeandika
namba za simu na akaiona
namba ya simu ya Ruby
akaniuliza Ruby ni nani?
Nadhani kuanzia pale alianza
kuwa na mashaka na
nilipoondoka akaamua
kumpigia simu Ruby akitaka
kumfahamu kama ni mpenzi
wangu.Hata hivyo tumefikia
mwisho kwani Habiba
alinitaka nisirejee tena Saudi
Arabia.Kama misheni hii
ikimalizika na nikabahatika
kuwa mzima nitarejea
Tanzania na kumuoa Ruby”
akawaza Mathew na kuvuta
pumzi ndefu
“Kuna nyakati ninaingiwa
na hofu kubwa kuhusiana na
misheni hii ninayokwenda
kuifanya.Ni misheni ya hatari
sana na itagharimu damu ya
watu wengi” akawaza
“Lakini sipaswi
kuogopa.Bila kuifanikisha hii
misheni nchi zetu zitaendelea
kuwa uwanja wa
vita.Machafuko yataendelea
huku mabepari hawa
wakiendelea kuchota mai zetu
na kunufaisha nchi zao.Lazima
nijitoe mhanga kuhakikisha
hili haliendelei.” akawaza
Mathew na kijiusingizi
kikaanza kumpitia akalala.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 3 : EPISODE 8
Saa kumi na mbili za
asubuhi ilimkuta Ruby akiwa
bado ofisini kwake.Hakupata
usingizi hivyo aliendelea
kufanya kazi
usiku.Wafanyakazi walipoanza
kuingia ofisini asubuhi
walimkuta akiwa ofisini
akiendelea na kazi.Saa mbili za
asubuhi akawakusanya wote
kwa ajili ya kuwapa taarifa
muhimu.
“Habarini za asubuhi
ndugu zangu.Naamini nyote
mnaendelea vyema” Ruby
akawasalimu wafanyakazi wa
SNSA
“Usiku wa kuamkia jana
watu wasiojulikana walimuua
Mufti wa Tanzania ikiwa ni
katika muendelezo wa mauaji
ya viongozi wa dini ambayo
ndiyo chanzo cha vurugu hizi
zinazoendelea.Kutwa nzima ya
jana tulikuwa katika kutafuta
nani waliomuua kiongozi huyo
wa dini bila mafanikio lakini
usiku wa jana tulipata taarifa
kutoka katika chanzo chenye
uhakika kwamba mauaji haya
yanayoendelea yanafanywa na
kikundi cha kigaidi cha IS”
akasema na kunyamaza
akawatazama wafanyakazi
“Vurugu hizi zote ambazo
zinaendelea nchini hivi sasa IS
ndio waliozichochea.Walifanya
mauaji ya kule Tanga ambayo
ndicho kilikuwa chanzo cha
vurugu kwa hapa
Tanzania.Walihamia Dar es
salaam na kuendelea na zoezi
lile lile la kuua viongozi wa
dini kwa ajili ya kuchochea
vurugu baina ya waumini wa
dini za kikristu na
kiislamu.Juzi mufti wa
Tanzania alikutana na Rais
wakazungumza faragha na
baadae wakazungumza na
watanzania akawaomba
waislamu wasiendelee na
vurugu lakini usiku wa siku
hiyo akauawa kwa bomu yeye
na familia yake.Kwa nini Mufti
aliuawa? Akauliza Ruby
“Hotuba aliyoitoa Mufti
kuwataka watanzania
wasiendelee kushambuliana na
kuuana ilionekana kuwa na
mapokeo mazuri kwani vurugu
zilipungua kwa kiasi kikubwa
baada ya hotuba ile na hii
iliwapa hofu wale wanaotaka
vurugu kuendelea ndiyo
maana wakamuua” Ruby
akanyamaza
“Haikuishia hapo katika
mauajiya Mufti.Usiku wa
kuamkia leo nyumba ya
imevamiwa na watu wenye
silaha kwa lengo la kufanya
shambulio lakini walikutana
na upinzani mkali kutoka kwa
askari polisi waliokuwa hapo
wakilinda kwani serikali
imeweka ulinzi mkali katika
nyumba zote za watawa,shule
za dini,makanisa na
misikiti.Wavamizi hao
waliokuwa na silaha nzito
walishindwa kutekeleza lengo
lao baada ya kuzidiwa nguvu
na kukimbia huku
wakitelekeza silaha
zao.Waliofanya shambulio
hilo tunaamini ni kikundi cha
IS ambao lengo lao ni
kuchochea vurugu.Wamemuua
kiongozi wa waislamu ili
ionekane ni wakristu
wamefanya hivyo na wakataka
tena kuua watawa wa kikristu
ili ionekane kwamba waislamu
wamefanya mauaji hayo ili
kulipiza kisasi kwa kiongozi
wao kuuawa na lengo kubwa ili
waumini wa dini hizi mbili
waendelee kushambuliana”
akanyamaza Ruby na kushika
kitanza mbali akabonyeza na
picha kubwa ikatokea katika
runinga
“Anaitwa Assad
Ismail.Huyu ni kiongozi wa IS
katika eneo la Afrika
Mashariki na kati na makazi
yake ni Mombasa Kenya ila
kwa sasa yuko hapa nchini kwa
ajili ya misheni ya kuchochea
vurugu.Assad yuko hapa Dar
es salaam lakini hatujui ni
sehemu gani na huyu ndiye
ambaye anaongoza kikosi cha
magaidi wanaoua viongozi wa
dini na kuchochea machafuko
zaidi” akabonyeza tena kitanza
mbali ikatokea picha nyingine
“Anaitwa Marwan
Hossam.Huyu anaishi hapa
Dar es salaam eneo la kwa
Botha nyumba namba
604.Huyu ndiye anayefahamu
mahala anakoishi Assad hapa
Dar es salaam.Kwa taarifa
tulizo nazo ni kwamba nyumba
hii ndimo ambao IS
wamekuwa wakipanga
mipango yao yote ya mauaji”
akasema Ruby akatulia kidogo
“IS hawako peke yao.Kuna
watu wanashirikiana nao
katika kuchochea vurugu
hizi.Watu hao lazima wapo
hapa nchini.Kama
mtakumbuka tumekuwa na
zoezi la kuwafuatilia watu
kadhaa ambao tunahisi wana
mahusiano na vurugu hizi
zinazoendelea lakini
tumegundua wote
wametoweka na hawajulikani
walipo.Tunaamini upo
mtandao ambao unashirikiana
na magaidi hawa katika
kuanzisha vurugu.Swali
ambalo tunatakiwa kujiuliza ni
je IS wanafanya haya yote kwa
faida ya nani?Je kuna nchi au
kikundi cha watu kimewatuma
wafanye haya? Hayo ndiyo
maswali ambayo tunatakiwa
kuyatafutia majibu.Usiku wa
leo tunakwenda kuvamia
nyumba hiyo wanamoishi
magaidi wa IS na kumchukua
Marwan Hossam ambaye
atatusaidia kujua mahala alipo
Assad.Tukifanikiwa kumpata
Assad tutajua kuhusu mtandao
wa watu wanaoshirikiana nao
katika kuchochea vurgu hizi
wale wa ndani na nje ya nchi”
akasema Ruby
“Mchana wa siku ya leo
tutaelekeza drone yetu katika
nyumba hiyo wanamoishi hao
magaidi kufuatilia kila
kinachofanyika hapo ndani
huku makomando wetu
wakijipanga namna ya kuingia
ndani na kuwachukua magaidi
hao.Mmoja wa madereva wetu
atapeleka gari hadi mbele ya
nyumba hiyo ili tuwe na
uhakika wa nyumba
tunayoilenga.Mchana kutwa
wa leo tutaanza kufuatilia kila
kinachoendelea ndani ya
nyumba hiyo na usiku wa leo
kikosi cha makomando wetu
kitavamia hapo.Tutachukua
kila atakayekuwepo mahala
hapo na kuja kuwafanyia
mahojiano lakini mlengwa
mkuu katika misheni hiyo ni
Marwan Hossam ambaye
atatuongoza kujua mahala
alipo Assad Ismail” akasema
Ruby na kutaka maandalizi
yaanze mara moja kisha
akaelekea ofisini kwake.
Baada ya dakika kumi
akaingia Gosu Gosu
“Tayari dereva amekwisha
ondoka na moja ya gari kuu
kuu ambalo limewekewa
mkanda maalum kwa juu ili
kutuwezesha
kumfuatilia.Baada ya kupata
picha za nyumba hiyo
wanamoishi magaidi
makomando wataanza
maandalizi ya namna
wakatavyoweza kuingia humo
ndani” akasema Gosu Gosu
“Good” akajibu Ruby
“Ruby kwa nini
hujawaeleza ukweli kwamba ni
Marekani ndio wako nyuma ya
haya yote yanayoendelea hapa
nchini?akauliza Gosu Gosu
“Hapana hawapaswi
kufahamu jambo hilo.Litabaki
kati yetu kwa sasa.Nina hofu
yawezekana jambo hili likivuja
linaweza kuvurga kila kitu na
tukashindwa kuwapata watu
wanaojihusisha na machafuko
hayo” akasema Ruby
“Ruby macho yako mazito
sana.Hujalala usiku wa
kuamkia leo.Unahitaji kwenda
kupumzika kidogo” akasema
Gosu Gosu
“Hapana Gosu Gsou siwezi
kwenda kulala.Tuna kazi
nyingi za kufanya kuhakikisha
tunaupata mtandao wote wa
watu wanaochochea vurugu
hizi.IS wanaendelea kufanya
mauaji hivyo lazima
tuhakikishe kwamba
tunawapata wote na kufahamu
watu wanaoshirikiana nao”
akasema Ruby
“Tutawapata Ruby
usihofu.Mathew amekwisha
tupa mwanga na kuanzia hapa
tunajua wapi tuelekee”
akasema Gosu Gosu
“Nilidhani ninamfahamu
vizuri Mathew Mulumbi
kumbe nilikuwa
najidanganya.Bado simfahamu
vizuri ni mtu wa aina
gani.Mambo yake
yananishangaza sana.Ni
misheni gani aliyonayo
ambayo inamfanya ashirikiane
na hawa magaidi? Kitu gani
kitatokea ambacho anasema
tusikiamini
tutakapokisikia?akauliza Ruby
“Lazima itakuwa ni
misheni kubwa sana lakini
tusubiri tutajua” akasema
Gosu Gosu
RIYADH – SAUDI ARABIA
Bado watu waliendelea
kufika katika makazi ya
Habiba Jawad kumpa pole
kufuatia vifo vya mfululizo vya
watoto wake wawili Najma na
Abu Dahir.Saa tatu za asubuhi
gari moja lilifika katika makazi
yale ya Habiba na watu watano
wakashuka.Walipokewa na
Sayid Omar ambaye alikuwa
anawapokea wageni mbali
mbali wanaofika pale
nyumbani akawapeleka katika
nyumba Fulani
akawakaribisha sebuleni nzuri
halafu akamfuata Habiba
Jawad akamjulisha kuwa
wageni wamefika.Habiba
akiwa ameongozana na Nawal
wakaelekea katika nyumba
walikopelekwa wale wageni.
“Yule mtu kutoka IS
ameletwa” Habiba
akamwambia Nawal.
Waliingia katika nyumba
ile wakasalimiana na watu
wale wakampa pole nyingi
Habiba kwa msiba mzito
uliompata.Baada ya hapo
yakaanza maongezi kuhusiana
na Yule mtu ambaye Habiba
alimuhitaji kutoka IS kwa ajili
ya kwenda kutumika katika
zoezi la kusambaza kirusi
nchini Tanzania.Aliitwa Sattar
Sayf Al Din.
Habiba na wale jamaa
walikuwa na mazungumzo
marefu yaliyochukua saa mbili
kisha wakafikia makubaliano
na wale jamaa wakamuaga
Habiba wakaondoka ila Sattar
akabaki.Baada ya wale jamaa
kuondoka Habiba akamtaka
Nawal kumpiga picha Sattar ili
aweze kuzitma Marekani
wamfahamu kwani alitarajia
kuondoka jioni ya siku ile na
ndege kuelekea
Marekani.Baada ya kuzipata
picha zile akamkabidhi Sattari
kwa Sayid Omar ili ampeleke
katika mojawapo ya nymba za
wageni akapumzike wakati
safari yake ya kwenda
Marekani ikiandaliwa.
“Tayari tumemfahamu
mtu ambaye atatumiwa na
Marekani kusambaza virusi
nchini Tanzania” akasema
Habiba
“Ndiyo mama” akasema
Najma
“Kinachofuata ni wewe
kwenda kumsubiri nchini
Tanzania” akasema Habiba
“Hakuna tatizo mama
mimi niko tayari kwenda huko
Tanzania”
“Vizuri.Nitawasiliana na
Yule mtu ambaye Najma
aliwasiliana naye anaitwa
Ruby ili nimuombe akupokee
kwani ni mara yako ya kwanza
kufika Tanzania” akasema
Habiba
“Nitajuaje kama Sattar
amewasili Dar es salaam?
Naamini safari yake ya
Tanzania itakuwa ya kimya
kimya sana” Akauliza Nawal
“Nitawasiliana na watu wa
IS ili wanipe mawasiliano ya
mtu wa IS aliyeko Dar es
salaam.Ninaamini yeye
atakuwa na mawasiliano na
Marekani na lazima atafahamu
kuhusu Sattar na jibu
nitakalolipata
nitakujulisha.Utakapofika
huko jitahidi upate
mawasiliano”akasema Habiba
“Nitajitahidi mama.Lakini
ni vipi kama huyo mtu wa IS
aliyeko Tanzania akakosa
taarifa za Sattar?akauliza
Nawal
“Sattar lazima awe na mtu
wa kumsaidia akiwa nchini
Tanzania na mtu pekee
ambaye anaweza akatumiwa ni
aliye katika mtandao wa
IS.Usihofu nitafanya kila
niwezalo kupata taarifa za
kuhusiana na Sattar” akasema
Habiba
“Sattar anaondoka leo
kwenda Marekani na hatujui
ni lini ataondoka Marekani
kwenda Tanzania hivyo wewe
utaondoka Kesho hadi Nairobi
Kenya.Uwanja wa ndege wa
Nairobi Kenya haujafungwa
unaendelea kupokea ndege na
kutoka pale utatafuta usafiri
wa kukuingiza nchini
Tanzania.Nitazungumza na
Ruby nijue kama anaweza
akakusaidia ukaweza kuingia
Tanzania.Endapo hatakuwa na
uwezo wa kukusaidia
nitatafuta namna ya kuweza
kukuingiza nchini Tanzania
siwezi kushindwa” akasema
Habiba halafu akaenda
kuchukua kitabu ambacho
Mathew alikuwa ameandika
namba za simu akapekua na
kuupata ukurasa ambao
ulikuwa na namba za simu za
Ruby,akaziandika katika simu
yake na kupiga.
“Simu inaita” akasema
Habiba
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Ruby alihisi uchovu
mwingi akakiegemeza kichwa
chake kitini.Mara simu yake
ikaanza kuita akanyoosha
mkono akaichukua na
kutazama mpigaji zilikuwa ni
namba ngeni katika simu yake.
“Hizi ni namba za simu za
Saudi Arabia.Huyu lazima
atakuwa ni Najma.Ngoja
nimsikie anachotaka
kunieleza” akawaza Ruby na
kupokea ile simu
“Hallow” akasema
“Hallow,naongea na
Ruby?akauliza mwanamama
wa upande wa pili.Sauti ile
haikuwa ya Najma.Ruby
akastuka kidogo
“Nani anaongea?akauliza
Ruby
“Naitwa Habiba
Jawad,ninapiga simu kutoka
Saudi Arabia”
“Habiba Jawad?Ruby
akauliza
“Ndiyo.Nazungumza na
Ruby?akauliza Habiba na
Ruby akawa kimya.Alistuka
sana
“Hallow” akaita Habiba
“Hallow umesema wewe ni
nani?Ruby akauliza
“Naitwa Habiba Jawad
ninapiga simu kutoka Saudi
Arabia.Wewe ni Ruby?akauliza
Habiba
“Ndiyo naitwa
Ruby.Umenifahamuje?Umetoa
wapi namba zangu?akauliza
Ruby
“Unamfahamu Mathew
Mulumbi?akauliza Habiba na
kuendelea kumstua zaidi Ruby
“Ruby ! akaita Habiba
“Nimekuuliza
unamfahamu Mathew
Mulumbi?akauliza Habiba
“Umemfahamuje Mathew
Mulumbi?
“Mathew ni kijana wangu
amemuoa binti yangu Najma
ambaye alikupigia simu hivi
majuzi” akasema Habiba na
Ruby akahisi baridi ikimpenya
“Ruby sikiliza
mwanangu.Ninamfahamu
Mathew Mulumbi na anaishi
hapa kwangu na binti yangu
Najma.Ni mimi niliyemtoa
katika taabu na mateso
aliyokuwa nayo na kuanza
maisha mapya hivyo
namchukulia kama
mwanangu.Nimepata namba
zako kutoka katika kitabu
chake maalum” akasema
Habiba
“Unahitaji nini
Habiba?akauliza Ruby huku
sauti yake ikionekana
kutetema
“Nina shida naomba
msaada wako”
“Msaada gani unauhitaji?
“Kuna binti yangu anakuja
Tanzania.Ni mara yake ya
kwanza hivyo nakuomba
ukubali kumpokea na
kumsaidia”akasema Habiba
“Binti yako anakuja
Tanzania?Najma? Ruby
akauliza
“Hapana si Najma.Anaitwa
Nawal” akasema Habiba na
Ruby akavuta pumzi ndefu.
“Ruby ! akaita Habiba
“Anakuja kufanya nini
Tanzania? Akauliza Ruby
“Kuna kazi anakuja
kuifanya.Nakuomba umpokee
tafadhali na umsaidie.Kwa
kuwa uwanja wa ndege wa Dar
es slaam umefungwa
atalazimika kupita nchini
Kenya atashukia jijini Nairobi
na kutokea pale atatumia
magari ya kawaida kuingia
Tanzania kupitia mpaka wa
Namanga akielekea Dar es
salaam” akasema Habiba
“Hakuna haja ya kwenda
kushukia jijini Nairobi.Uwanja
wa ndege wa kimataifa wa
Kilimanjaro umekwisha
funguliwa kwa sasa na
unaendelea kutoa
huduma.Ndege zote ambazo
zilipaswa zitue katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere Dar es salaam
sasa zinakwenda kutua uwanja
wa Kilimanjaro.Mikoa ya
Kaskazini hakuna vurugu
kubwa kama ukanda huu wa
pwani hivyo nashauri kama
anakuja ashukie Kilimanjaro
na mimi nitakwenda
kumpokea hapo”
“Ahsante sana
Ruby.Nitalifanyia kazi hiyo ili
aweze kushukia uwanja wa
ndege wa
Kilimanjaro.Nategemea
aondoke kesho asubuhi na
ndege ya shirika la ndege la
Ethiopia”
“Mimi niko Dar es salaam
lakini nitafanya utaratibu wa
kuhakikisha huyo mwanao
anafika Dar es salaam”
“Nashukuru sana Ruby .Ni
namna gani nitaweza
kukutumia fedha za
kufanikisha jambo hilo?Sitaki
uingie gharama kwa kutumia
fedha zako.Kama kuna namna
yoyote naweza kukutumia
fedha nielekeze tafadhali”
akasema Habiba
“Usijali mama.Huna haja
ya kutuma fedha.Kwa kuwa
umemsaidia Mathew basi
nami nitamsaidia
mwanao.Unaweza ukaniambia
anakuja kufanya nini Tanzania
wakati huu wa
machafuko?akauliza Ruby
“Kuna jambo muhimu
sana linamleta hapo
Tanzania.Tafadhali naomba
umsaidie” akasema Habiba
“Nitamsaidia usijali”
“Sawa.Nitakutumia picha
zake ili umfahamu” akasema
Habiba na kuagana na Ruby
“Haya ni mambo gani
yanaendelea? Mathew
anashirikiana na Habiba
Jawad? Ruby
akajiuliza.Alishangaa sana
“Nini kimetokea hadi
Mathew akaamua kujiunga na
Habiba Jawad?Huyu mama
ndiye anayefadhili makundi ya
kigaidi duniani. Dah ! ni
vigumu kuamini ! akawaza
Ruby
“Ninahisi mwili unakosa
nguvu kwa kulifahamu
hili.Mathew anafahamu kabisa
Habiba Jawad ni nani lakini
ameamua kushirikiana naye na
kama haitoshi amemuoa hadi
mwanae Najma.Nini
kimemtokea Mathew Mulumbi
hadi akaamua kushirikiana na
magaidi? Ndiyo maana
alinionya nisimfuatilie kwa
kuogopa ningeweza kugundua
anashirikiana na Habiba
Jawad mfadhili mkubwa wa
ugaidi duniani.Kadiri
ninavyoendelea kumfahamu
Mathew ninazidi kugundua
mambo mengine ambayo
yananitisha na kunifanya
nimuogope.Mathew
ninayemuona sasa si Mathew
Yule ambaye nilimfahmau
miaka kadhaa iliyopita ambaye
nilitokea kumpenda kupita
ninavyojipenda
mwenyewe.Nadhani
ninachokipata mimi ndicho
alichokipata Peniela na
akaamua waachane.Ninaanza
kuona maamuzi ya Peniela
kuachana na Mathew yalikuwa
sahihi.Ninampenda sana
Mathew kwa moyo wangu
wote lakini sina hakika kama
nina kifua cha kuvumilia haya
yanayomzunguka” akawaza
Ruby na kutazama juu
“Kama tayari ameanzisha
mashirikiano na Habiba Jawad
ni wazi ameamua kushirikiana
na kundi la IS na hapa nchini
anadai amekuja kwa ajili ya
misheni maalum.Lazima
alichokuja kukifanya
kinahusiana na kundi la
IS.Nini amekuja kukifanya?
Huyo Nawal naye anakuja
kufanya nini?Naamini huyu
Nawal naye kuna kitu anakuja
kukifanya hapa Tanzania
ambacho kinahusiana na IS”
akaendelea kuwaza.
“Hapana siwezi kumuacha
Mathew akapotea namna
hii.Lazima nimsaidie japo
hatapenda lakini lazima
nifanye kitu kumsaidia kwani
akiendelea kushirikiana na
mtandao huu wa kigaidi
maisha yake yatakuwa
mashakani.Siwezi kukubali
Mathew awe gaidi.Kwa kuwa
tayari amekwisha tuelekeza
nyumba walimo magaidi wa IS
nitaelekeza vikosi kuvamia
nyumba hiyo na kuwachukua
magaidi wote akiwamo
Mathew.Atashikiliwa kwa
muda ili kumuhoji kujua ni
kitu gani kimemsababisha
akabadilika kutoka Jasusi hadi
Gaidi.Siwezi kuvumilia lazima
haraka sana makomando wetu
wakavamie nyumba hiyo”
akawaza na kuchukua simu
akampigia Gosu Gosu
akamtaka aende ofisini kwake
mara moja
“Kuna nini Ruby? Akauliza
Gosu Gosu
“Gosu Gosu ninazidi
kuchanganywa na huyu
Mathew”
“Kuna nini tena kuhusu
Mathew?akauliza Gosu Gosu
na Ruby akavuta pumzi ndefu
“Nimepokea simu muda si
mrefu kutoka Saudi Arabia”
“Kutoka kwa
Najma?akauliza Gosu Gosu
“Unamkumbuka Habiba
Jawad?akauliza Ruby
“Habiba Jawad Yule
mfadhili wa
ugaidi?Ninamkumbuka”
akajibu Gosu Gosu
“Huyo ndiye aliyenipigia
simu”
“Habiba Jawad
amekupigia simu?! Gosu Gosu
akashangaa
“Ndiyo amenipigia simu”
“Amepataje mawasiliano
yako?
“Ni mambo ya ajabu sana
Gosu Gosu”
“Niambie Ruby.Habiba
Jawad amepataje namba
zako?Alikupigia kwa dhumuni
gani? Akauliza Gosu Gosu
“Habiba Jawad ni mama
yake Najma ambaye ameolewa
na Mathew” akasema Ruby na
mstuko ukaonekana usoni kwa
Gosu Gos
“Najma ni mtoto wa
Habiba Jawad?
“Ndiyo.Habiba
amenihakikishia kwamba
Mathew anaishi kwake na
amemuoa mwanae Najma”
“Haya ni
maajabu.Inawezekanaje
Mathew akajiunga na Habiba
ambaye anafadhili
ugaidi?akauliza Gosu Gosu
“Nimejiuliza swali hilo
sijapata jibu.Mathew
anafahamu fika kwamba
Habiba ni mfadhili wa ugaidi
lakini amekubali kujiunga
naye.Gosu Gosu,Mathew huyu
wa sasa si Yule
tuliyemfahamu.Hata siku moja
Mathew Mulumbi hawezi
akajiunga na magaidi !
akasema Ruby
“Yawezekana hii ni sababu
kwa nini alikwambia
usimfuatilie atakapoondoka”
akasema Gosu Gosu
“Exactly.Alijua nitafahamu
kuwa anashirikiana na Habiba
Jawad”
“Mungu wangu ! Mathew
kwa nini amefanya maamuzi
haya ya kushirikiana na
magaidi wa IS?
“Hata mimi najiuliza swali
hilo sijapata jibu” akasema
Ruby
“Habiba alitaka nini
alipokupigia simu?
“Amenieleza kuwa
mwanae anaitwa Nawal
anakuja Tanzania akaniomba
nimsaidie aweze kuingia
salama”
“Mwanae anakuja
Tanzania? Anakuja kufanya
nini wakati huu wa
machafuko?
“Hajanieleza anakuja
kufanya nini ila amesema kuna
jambo muhimu linalomleta
hapa Tanzania. Akaniomba
nimsaidie aweze kufika Dar es
salaam.Naamini kinachomleta
hapa ni mojawapo ya shughuli
za IS kama ilivyo kwa Mathew”
“Anakuja lini?
“Kesho.Nitakwenda
kumpokea katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa
Kilimanjaro”
“Haya mambo
yanachanganya sana” akasema
Gosu Gosu
“Gosu Gosu huyu Mathew
si Yule tumjuaye.Huyu ni
Mathew tofauti kabisa.Hata
siku moja Mathew Mulumbi
hawezi kushirikiana na
magaidi hivyo nimefanya
maamuzi ya kutuma
makomando wetu wakavamie
nyumba ile mchana huu na
wawachukue wote
watakaowakuta akiwemo
Mathew .Tutamshikilia
sehemu salama kwa mahojiano
ili atueleze kwa nini amefanya
maamuzi haya ya kushirikiana
na magaidi?akasema
Ruby.Gosu Gosu akafikiri kwa
muda kisha akasema
“Hapana Ruby hatuwezi
kufanya hivyo”
“Kwa nini Gosu
Gosu?Mathew amebadilika na
hatuwezi kumuacha
akaendelea namna
hii.Anashirikiana na magaidi
na hata sasa kuna kitu
wanapanga kukifanya hapa
Dar es salaam siku ya leo ndiyo
maana alituzuia tusivame ile
nyumba hadi usiku wa leo.Kwa
hiki anachokifanya Mathew
maisha yake tayari yapo
hatarini na kama mtu wetu wa
karibu ni jukumu letu
kuhakikisha
tunamsaidia.Yawezekana
haoni hatari iliyoko mbele
yake au anashirikiana nao kwa
shinikizo.Tunatakiwa
tufahamu kila kitu” akasema
Ruby
“Ruby sikubaliani na wazo
lako kwa sababu Mathew ni
mtu anayejua nini
anakifanya.Kama ameingia
katika mashirikiano na
magaidi basi ni kwa sababu
maalum.Si mara moja Mathew
ameingia katika sehemu za
hatari kwa ajili ya kufanikisha
misheni muhimu.Naamini
hata huku aliko sasa hajaenda
kwa bahati mbaya,ana sababu
maalum na kama unakumbuka
jana amezungumza nasi na
akatutahadharisha kwamba
tutakachokisikia kuhusu yeye
tusikiamini.Sasa nimeelewa
kwa nini alitupa taarifa ile
mapema kwani alijua
tungeweza kufahamu mambo
kama haya kuhusu yeye
kushirikiana na
magaidi.Alituandaa tusistuke
tutakapogundua hilo na
alitupa maelekezo vile vile
kwamba tusifanye chochote
hadi usiku wa leo.Hii ina
maana kwamba kuna misheni
inaendelea na kama angekuwa
hana nia njema asingefanya
jitihada za kututafuta na
kutupa taarifa muhimu.Ni
yeye ambaye ametupa mwanga
kuhusiana na vurugu hizi
zinazoendelea na sasa tuna
sehemu ya kuanzia.Hatua
zozote za kwenda kinyume na
maelekezo ya Mathew
kinaweza kupelekea kwanza
tukavuruga misheni ya
Mathew na vile vile tunaweza
kujikuta tumevuruga kila kitu
kuhusu misheni yetu” akasema
Gosu Gosu
“Gosu Gosu !
“Hapana Ruby
hatutafanya chochote tutafuata
maelekezo ya
Mathew.Ninamuamini
Mathew sana na kama wewe
umeanza kupoteza imani
kwake mimi bado namuamini
na nitaendelea kufuata
maelekezo yake” akasema
Gosu Gosu
“Papii,Mathew huyu si
Yule ambaye
tunamfahamu.Hata siku moja
Mathew Mulumbi
tunayemfahamu hawezi
akakubali kushirikiana na
magaidi” akasema Ruby
“Ruby hakuna sababu
yoyote ya kuvamia yumba
wanayoishi Mathew na watu
wa IS mchana huu.Operesheni
itaendelea usiku kama
tulivyopanga.Kitu kingine
ambacho ninakiona cha msingi
tumsubiri huyo mtoto wa
Habiba Jawad anayekuja
kesho anaweza akatueleza
mambo mengi zaidi.Hatupaswi
kwenda haraka haraka
tutavuruga kila kitu.Kumbuka
tulikuwa tumekwama na
hatukujua sehemu ya kuanzia
lakini ni Mathew aliyekuja
kutukwamua.Nakuomba Ruby
tuwe na uvumilivu katika
hili.Mathew anajua kwamba
watu wake wa karibu lazima
watafahamu kuwa
anashirikiana na magaidi na
wataumia hivyo alitutaka
tusitetereke.Naomba tubaki
hivyo” akasema Gosu Gosu na
Ruby akabaki akimtazama
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 3 : EPISODE 9
Licha ya kutokea kwa
mauaji ya kiongozi mkuu wa
waislamu Tanzania lakini jiji la
Dar es salaam na viunga vyake
halikuwa na vurugu ambazo
zilitegemewa kutokea.Maelfu
ya waumini wa dini ya
kiislamu walihudhuria mazishi
ya kiongozi wao yaliyofanyika
mchana wa siku hiyo.Ulinzi
ulikuwa mkali sana wakati wa
mazishi hayo na viongozi
waliokuwepo walitumia muda
mwingi kuwaomba waumini
wasilipize kisasi kwani kitendo
hicho kingeongeza vurugu
zaidi na damu nyingi
ingeendelea
kumwagika.Walitumia muda
mwingi zaidi kuhubiri uwepo
wa amani kama njia ya
kumuenzi kiongozi Yule
aliyeuawa ambaye alipenda
kuona amani inapatikana
nchini.
Kiza kilianza kutanda
angani bado jiji la Dar es
salaam halikuwa na vurugu
kama zilizokuwepo siku
chache zilizopita.Saa moja na
nusu geti la nyumba alimo
Mathew Mulumbi na watu wa
IS lilifunguliwa na gari mbili
zikaingia mojawapo likiwa ni
gari la jeshi la
Marekani.Kutoka katika gari
lililokuwa mbele akashuka
Assad Ismail na kusalimiana
na Marwan.Wanajeshi wawili
wakashuka kutoka katika lile
gari la jeshi wakaongozana na
Assad kuelekea ndani.
Mlango wa chumba cha
Mathew Mulumbi ukagongwa
akaenda kuufungua akakutana
na Marwan ambaye alimtaka
ajiandae kwani muda
umefika.Mathew akatoka
katika kile chumba akaelekea
sebuleni akasalimiana na
Assad kisha wakaongozana
kuelekea katika bohari
lililokuwa likitumika kuunda
bomu.Tayari bomu lilikuwa
limekamilika.Assad akalikagua
kisha akawapongeza
wataalamu waliounda bomu
lile halafu akaelekeza lipelekwe
katika gari la jeshi.Ndani ya
lile gari la jeshi kulikuwa na
watoto wadogo sita wenye
umri wa miaka mitano hadi
nane.Gari lile likafunguliwa
sehemu ya nyuma na bomu lile
kubwa likawekwa
vizuri.Wakati wataalamu wale
wakiendelea na kuliweka
bomu katika gari Assad
akamchukua Mathew
wakarejea ndani.Mmoja wa
wale wanajeshi akavua mavazi
yake ya kijeshi na kumpa
Mathew akavaa.
“Abu Zalawi sasa uko
tayari kwa kazi uliyokuja
kuifanya.Tumezungumza
mengi mchana wa leo
kuhusiana na kazi hii na nina
imani hakutakuwa na
usumbufu wowote.Vyovyote
itakavyokuwa hakikisha bomu
hilo linalipuka.Umenielewa
Abu? Akauliza Assad
“Nimekuelewa Assad”
“Sawa.Basi kila kitu ni
kama tulivyopanga.Nakutakia
kila la heri” akasema
Assad.Mathew akatoka mle
ndani akiwa ameongozana na
wale wanajeshi hadi katika
gari lile akapewa maelekezo
kadhaa na wale wanajeshi
halafu akaingia garini
akaliwasha na kuondoka
“Nawaonea huruma sana
watoto hawa wadogo.Laiti
ningekuwa na uwezo wa
kuwasaidia ningefanya hivyo
lakini hawa ndio
watakaoniwezsha kuingia
katika ubalozi wa
Marekani.Inauma sana lakini
hakuna namna” akawaza
Mathew akiendelea na safari
ya kuelekea katika ubalozi wa
Marekani.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 3 : EPISODE 10
Wakati Mathew Mulumbi
akiwa njiani kuelekea ubalozi
wa Marekani,katika makao
makuu ya SNSA kikosi cha
makomando kilikuwa
kinajiandaa kwa ajili ya
kwenda kuvamia nyumba
wanamoishi watu wa IS
waliyoelekezwa na
Mathew.Mchana kutwa
walikuwa wameelekeza drone
kubwa inayotumiwa na SNSA
katika nyumba hiyo
wakifuatilia kwa karibu kila
kilichokuwa kinaendelea ndani
ya nyumbe ile na kupanga
mikakati namna
watakavyoweza kuingia ndani.
Ndani ya jengo la SNSA
kulikuwa na heka heka nyingi
wakiwa wamejielekeza katika
kuhakikisha operesheni ile
inafanikiwa.
“Tusikilizane ndugu
zangu” akasema Ruby
aliyetoka kuagana na
makomando waliopanda
helkopta kuelekea katika
misheni yao.
“Toka asubuhi ya leo
tulikuwa na zoezi la
kuchunguza nyumba ambayo
wanaishi watu wa IS na watu
wale tunaowalenga Marwan na
Assad tumewaona katika
nyumba hiyo.Muda umefika na
makomando wetu tayari
wameondoka kuelekea
huko.Ni jukumu letu
kuhakikisha tunawasaidia kwa
kila namna
tuwezavy😵peresheni hii ni
muhimu mno na kwa namna
yoyote lazima iende kama
ilivyopangwa hivyo kila mmoja
ahakikishe kwa upande wake
anafanya kila kinachotakiwa
kuhakikisha makomando wetu
wanafanikiwa” akasema Ruby
na kutaka kazi ziendelee.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 3 : EPISODE 11
Mathew akiwa katika gari
la jeshi la Marekani alikata
kona ya kuelekea katika
ubalozi wa Marekani.
“I must do this ! akawaza
Katika geti la kuingilia
ubalozini hapo kulikuwa na
ulinzi wa wanajeshi wa
Marekani.Gari lile alilokuwa
analiendesha Mathew
likasimamishwa na Mathew
akawahi kuwaeleza kuwa
ndani ya gari ana watoto
ambao wamewaokoa katikati
ya mapigano na akatumwa
kuwakimbiza pale ubalozini
kupata hifadhi ya muda kabla
ya kupelekwa katika kambi
maalum hapo kesho.Hakuna
aliyetia shaka yoyote kuhusu
gari lile wote walijua Mathew
ni mwenzao.Geti likafunguliwa
na gari likaingia ndani.
Mchana wa siku ile
Mathew na akina Assad
walitumia muda mrefu kujadili
suala lile na kumpa Mathew
maelekezo yote juu ya
utekelezaji wa jambo
lile.Mathew akaenda kuegesha
gari mahala alikoelekezwa na
kuwashusha wale watoto
akawapeleka katika mahema
yaliyokuwa yamewekwa nje ya
ubalozi kwa ajili ya baadhi ya
raia wa Marekani na wa nchi
nyingine waliokwama Dar es
salaam.Baada ya kuwakabidhi
watoto wale Mathew akaelekea
getini akaomba kutoka
akaeleza kuna watoto
anawafuata ambao amewaona
wakiwa njiani hawana
msaada.Alielekezwa achukue
gari lakini akadai kwamba
hana haja ya gari anakwenda
kwa miguu kwa sababu si
mbali na pale
ubalozini.Wanajeshi
waliokuwa wanalinda getini
hawakuwa na wasi wasi naye
kwani waliamini kwa asilimia
mia moja ni mwenzao hivyo
wakamuacha akatoka.Akiwa
na bunduki yake mkononi
alikimbia akifuata
barabara.Katika jengo moja la
mgahawa ambao ulikuwa
umefungwa kuliegeshwa gari
jeupe.Mathew alipolikaribia
taa zikawashwa na kuzimwa
ikiwa ni ishara akaliendea
mlango ukafunguliwa akaingia
ndani ambamo alimkuta Assad
Ismail akiwa na watu wengine
wanne.
“Nimekamilisha kazi”
akasema Mathew
“Hakuna tatizo lolote?
Hawakutia shaka?akauliza
Assad
“Hakuna tatizo
lolote.Waliamini mimi ni
mwenzao” akajibu Mathew
“Safi sana” akasema Assad
na kumpatia Mathew kifaa
Fulani akakiwasha kikaanza
kuanzika namba haraka
haraka na kufikia sifuri.
“Bonyeza kitufe hicho
chekundu ili kazi yako iwe
imekamilika” akasema Assad
na Mathew bila kupepesa
macho akabonyeza kile kitufe
na mlipuko mkubwa ukatokea
na hadi mahala pale
walipokuwa wakahisi
mtikisiko kutokana na bomu
lile lililolipuka kuwa zito.Assad
akampa Mathew mkono
“Hongera Abu Zalawi
umekamilisha kazi yako”
akasema na kisha gari
likawashwa
wakaondoka.Walipishana na
magari ya jeshi na zimamoto
yakielekea mahala ulikotokea
mlipuko.Assad alikuwa
anaelekeza njia za kupita na
kisha wakafika katika jengo la
hoteli ambayo ilikuwa katika
hatua za mwisho za ujenzi.Geti
la hoteli ile kubwa
likafunguliwa gari la akina
Assad likaingia ndani na
kuelekea moja kwa moja
mahala ilikokuwa imeegeshwa
helkopta ya jeshi la Marekani.
“Abu Zalawi kazi yako
hapa Tanzania imekamilika na
sasa unaelekea Nairobi
Kenya.Utaondoka na helkopta
hii hadi nchini Kenya na
mambo yataendelea kama
nilivyokupa
maelekezo.Tafadhali usiende
kinyume na maelekezo
niliyokupa” akasema Assad
“Ahsante Assad kwa
ushirikiano na msaada
mkubwa ulionisaidia katika
kukamilisha kazi yangu”
akasema Mathew na kumpa
mkono Assad wakaagana
akaingia katika helkopta
mlango ukafungwa na
helkopta ikawashwa.Assad
alisimama pembeni ya gari
lake hadi helkopta ile ilipopaa
na kuondoka.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 3 : EPISODE 12
Helkopta maalum ya
operesheni za usiku ya
makomando wa SNSA
iliyotengenezwa kwa teknolojia
ya hali ya juu ya kutokutoa
sauti,ilifika usawa wa nyumba
ile walimokuwamo watu wa
IS.Bado sehemu kubwa ya jiji
la Dar es salaam ilikuwa
gizani.
Makomando nane
waliokuwa wamevaa miwani
ya kuwawezesha kuona gizani
wakashuka kwa miavuli huku
kila mmoja akitua katika
sehemu aliyoelekezwa kwani
walikwisha fanya mazoezi
mchana wa siku ile.Walinzi
waliokuwa zamu usiku ule
wakilinda nyumba ile
hawakuweza kuwaona
makomando wakishuka
kutokana na giza na hii
iliwasaidia makomando wale
waliokuwa na miwani ya
kuonea gizani kuwaona na
kuwamaliza kwa bunduki zao
nzito zilizofungwa viwambo
vya kuzuia sauti.Makomando
wote walitua salama na
hakukuwa na mtu hata mmoja
aliyekuwa nje ya ile nyumba
alibaki hai.Walimiliki eneo lote
la nje la ile nyumba.Baada ya
kujipanga vizuri makomando
wanne wakaenda katika
mlango wa mbele wa kuingilia
katika ile nyumba na mmoja
akachungulia ndani akawaona
watu wanne wakiwa sebuleni
wakizungumza.Hawakuwa na
habari kama wenzao
waliokuwa nje wamekwisha
uawa wote.Komando Yule
akawapa ishara wenzake
kwamba kuna watu wanne
kisha wenzake wakasogelea
mlango,kiongozi wao
akakinyonga kitasa cha
mlango ukafunguka
wakajitoma ndani.Wale jamaa
waliokuwa wamekaa katika
zuria walipigwa na butwaa
wakakosa la kufanya baada ya
kujikuta wamezingirwa na
wanajeshi wenye silaha
nzito.Mmoja wa wale jamaa
akageuka haraka ili aweze
kuchukua bastora yake lakini
mkono wake haukufika katika
bastora kwani kichwa chake
kilifumuliwa kwa risasi toka
katika bunduki nzito ya mmoja
wa makomando.
“Yuko wapi Marwan
Hossam? Akauliza kiongozi wa
makomando.Wale jamaa
hawakujibu kitu.
“Nawauliza tena yuko wapi
Marwan?
Bado wale jamaa
waliendelea kuwa
kimya.Akaamuru wafungwe
pingu.Wakati komando mmoja
akijiandaa kuwafunga pingu
mmoja wa wale magaidi
akainuka na kupiga ukelele
huku akitaka kumvaa mmoja
wa makomando lakini
hakufanikiwa kitendo
alichokusudia baada ya
kunyeshewa mvua ya risasi na
mara mlango mmoja
ukafunguliwa.
“Omar kuna nin.....”
akauliza jamaa aliyekuwa kifua
wazi na kaptura akionekana
kutoka kulala
“Omar ! akaita Yule jamaa
huku akielekea sebuleni
“Yarkud ! Yarkud !
akasema mmoja wa wale
magaidi kwa lugha ya kiarabu
akimtaka Yule jamaa
akimbie.Yule jamaa akageuka
na kutoka mbio akipita jikoni
akaufungua mlango wa nyuma
ili aweze kutoka lakini
akapigwa teke zito akaanguka
chini na kabla hajafanya
chochote akajikuta
amezungukwa na makomando
wanne wakamuinua na
kumfunga
pingu.Walipommulika
wakagundua kwamba Yule
alikuwa ni Marwan Hossam.
“Tumempata Marwan !
SNSA ofisi kuu wakajulishwa
“SNSA tumempata
Marwan” akasema Yule
komando
“Hakikisheni
mnawachukua wote
mtakaowakuta hapo”
akaelekeza Ruby.Marwan
alipelekwa sebuleni
akaunganishwa na wale
wenzake wawili.Nyumba ile
ikapekuliwa hakukuwa na mtu
mwingine na kiongozi wa wale
makomando akaelekeza
makomando wake wakavamie
yale majengo mengine
mawili.Makomando wawili
wakabaki wakiwalinda wale
magaidi na wengine wakaenda
kuvamia katika yale majengo
mawili.Watu waliokuwa ndani
ya majengo yale mawili
walikuwa wamejilaza
wakipumzika hawakuwa na
habari kama
wangevamiwa.Walistukia
wakiwa wamezingirwa na
makomando na hawakupata
nafasi ya kujitetea.Wote
wakajikuta wakitiwa
nguvuni.Upekuzi ukafanyika
katika nyumba zile mbili na
ikagundulika kwamba
kulitengenezwa bomu kwani
kulikutwa na baadhi ya vifaa
vya kutengenezea
mabomu.Chumba cha Marwan
Hossam kikapekuliwa na vitu
kadhaa vikachukuliwa
ikiwemo simu yake ya
mkononi.
Baada ya kukamilisha kazi
waliyotumwa walitoa taarifa
ofisi kuu SNSA na helkopta ile
waliyokwenda nayo ikashuka
chini na kamba
ikashushwa.Marwan
akafungwa ile kamba maalum
kisha akiwa ameshikwa na
komando mmoja kamba ile
ikapanda taratibu na Marwan
akaingizwa katika helkopta
ikaondoka.Makomando
wengine walibaki wakiwalinda
wale magaidi wapatao tisa.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 3 : EPISODE 13
Helkopta ya SNSA ilitua
katika sehemu yake ikitokea
katika operesheni maalum ya
makomando waliovamia
nyumba ya magaidi wa
IS.Mlango wa helkopta
ukafunguliwa akashuka
komando mmoja kisha
akamshusha Marwan
Hossam.Gosu Gosu akasogea
na kumchukua Marwan
akaelekea ndani na helkopta
ile ikaondoka kwenda
kuwachukua watu
wengine.Gosu Gosu
akamchukua Marwan na
kumpeleka katika chumba
maalum cha mahojiano
kilichopo mita kadhaa chini ya
jengo lile akamfungia katika
chumba chenye baridi kali
kisha akamfuata Ruby
aliyekuwa katika ofisi yake
“Ruby tayari tumempata
Marwan hakuna haja ya
kuendelea kusubiri .Tukaanze
kumuhoji mara moja ili
ikiwezekana usiku huu huu
tumpate pia Assad kwani hana
taarifa kama wenzake
wamevamiwa.Tukichelewa
hadi kesho atagundua
kilichotokea na atajificha
itakuwa kazi ngumu kwetu
kumpata” akasema Gosu Gosu
kisha Ruby akaelekeza
Marwan atolewe katika
chumba kile cha baridi
apelekwe katika chumba cha
mahojiano halafu wakashuka
chini
“Nina muda mrefu
sijawahoji watu kama
hawa,ana bahati mbaya sna
Marwan ameingia katika anga
zangu.Leo atanena lugha zote
anazozifahamu” akawaza Gosu
Gosu wakiwa ndani ya lifti
wakishuka chini.
MPENZI MSOMAJI
MATHEW AMELIPUA
UBALOZI WA MAREKANI
NCHINI TANZANIA IKIWA
NI MWANZO WA MISHENI
NZITO YA KUELEKEA
IRAN,JE MISHENI YAKE
ITAFANIKIWA?
GOSU GOSU NA RUBY
WAMEANZA KUUSAKA
MTANDAO WA CHANZO
CHA VURUGU TANZANIA JE
WATAFANIKIWA
KUWAPATA WOTE
WANAOHUSIKA?
NAWAL ATAFANIKIWA
MISHENI YAKE YA KUZUIA
KIRUSI KISISAMBAE
TANZANIA?
USIKOSE SEHEMU IJAYO..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom