Johnny Sins
JF-Expert Member
- Nov 4, 2019
- 2,536
- 3,883
SEHEMU YA 23
TULIPOKOMEA....
Kisha alinyanyuka na kuelekea huko maliwatoni. Akakumbuka kuwa wakati Kisengo akipelekwa kuoneshawa, yeye alibaki, hivyo hakupajua. Akaamua kwenda mapokezi haraka kumwona yule kijana. Alimkuta akiendelea kuikodolea macho ile tamthiliya kwenye runinga. Akamuuliza na akaelekezwa. Muda mfupi baadaye alikuwa akitoka huko maliwatoni huku akiwa amenawa mikono vizuri kwa sabuni. Na sasa alijiamini kuwa yuko salama zaidi.
Alipokuwa akirudi chumbani, alikutana na Kisengo naye akiingia.
***ENDELEA***
“Nimepata,” Kisengo alisema huku akimwangalia Scolastica sawia usoni.
Aliyetangulia kuingia ni Scolastica, naye Kisengo alipoingia, kama awali aliufunga mlango kwa funguo. Akamfuata Scolastica kitandani ambako kile kijimeza chenye bia nacho kilikuwa kimesogezwa zaidi hapo kitandani. Akajikalisha kwa madaha huku akimtazama Scolastica na kuachia tabasamu la kilevi, mkono wa kushoto ukimpapasa shingo taratibu na wakati mwingine ukiteleza kwenye zile nywele zilizomwagika mgongoni.
Pale alipoketi alikuwa akitazamana na chupa zake mbili kubwa za bia na moja ilikuwa mbele zaidi, ikiwa imewekwa hivyo na Scolastica. Akamkabidhi Scolastica ile vocha aliyomwagiza.
“Nakupenda kwa kunijali,” Scolastica alimwambia huku akiliachia lile tabasamu lake la kinafiki lakini lililonekana kama tabasamu halisi machoni mwa yeyote asiyemjua kwa kina.
“Usijali Flora, mi’ ninajisikia kukupenda zaidi,” Kisengo
alibwabwaja kwa sauti yenye kitetemeshi cha mbali huku akiendelea kumpapasa mgongoni na sasa wakati mwingine akihamia kwenye mapaja yale makubwa yaliyotanuka ndani ya gauni lake lililomshika maungoni.
“Kipi kinakufanya ujisikie kunipenda wakati umeniona tu leo? Kama si uongo ni nini? Kama huo si umalaya ni nini?” tabasamu la Scolastica liliendelea kuchanua kwa namna ya kirafiki zaidi. Alionesha kuwa hata hayo maswali yake ni masihara tu.
Sasa naye akionesha kuwa na ushirikiano, aliutumia mkono wake wa kulia kutua katika maungio ya miguu ya Kisengo na kupapasa taratibu, akitomasa na kuminyaminya kwa namna ambayo ilimchanganya Kisengo na kumtia msisimko mkali. Alimwona anavyotaabika, yeye akaendelea kumfanyia vituko hivyo kisha ghafla akaacha. Akaishika vocha, akaikwangua, kisha akaziingiza namba.
Kisengo alishusha pumzi ndefu baada ya ule mkono wa Scolastica kuahirisha kufanya kile ulichokuwa ukikifanya. Macho yake yaliyokolea ulevi wa ashiki na ulevi wa pombe, yakawa yametua usoni kwa Scolastica kwa namna ya kuzidiwa na hawaa, hanjam na uchu usiokadirika. Ni kama alikuwa akitaka kutamka neno asiweze.
Kwa mbali Scolastica alijisikia kucheka lakini hakufanya hivyo, badala yake alitwaa chupa yake ya bia na kuipeleka kinywani. Alipokunywa kidogo na kuirudisha mezani, akamgeukia Kisengo na kumwambia, “Tumalize kwanza bia zetu, tukisogeze kimeza hiki mbali ndipo tuanze mambo yetu.” Tabasamu la kibwege likamtoka Kisengo. Kama aliyekurupushwa, akaitwaa ile chupa iliyokuwa mbele yake, akagugumia funda zito. Wakati funda hilo likishuka kooni, alisimama na kuanza kuchojoa nguo. Alianza na shati. Alipomaliza, aliangaza huku na kule, labda akitafuta pa kulitundika shati hilo. Hakupaona. Akaamua kuliweka kwenye kingo ya kitanda upande wa kichwa.
Akaitwaa tena chupa na kushusha funda lingine zito. Akakunja uso kidogo, akaukunjua lakini tena akaukunja. Akafumba macho na kuyafumbua. Akaonekana kujishangaa. Wakati alipokwishafungua kifungo cha suruali na zipu yake, akaishusha suruali, hapo akayumba na kurudi nyuma hatua mbili. Hata hivyo, akastahimili na kusimama vizuri. Lakini alipoinama ili aitoe suruali nzima mwilini, hakuweza, Alikwenda mbele na kuiangukia meza akionesha dhahiri kutokuwa na uwezo wa kujizuia. Chupa zilizokuwa mezani zikaanguka kitandani, bia zikilimwagikia godoro!
Scolastica alishaiona picha nzima tangu mwanzo, hivyo alikuwa ameshajitoa kitandani na kusimama kando akishuhudia. ‘Ungangari’ wa Kisengo uliendelea kuwa juu. Pamoja na kuiangukia meza ya vinywaji, hata hivyo aliamini kuwa ni ajali tu, hivyo, akajitahidi kunyanyuka tena na akafanikiwa.
Hata hivyo, hakujua kuwa bado hajawa timamu. Alijikakamua na kusimama lakini muda huohuo, alianza kurudi kinyumenyume. Hatua tatu tu, akaenda chini mzima-mzima, bila hata kuonesha dalili yoyote ya kujitetea. Alianguka kama furushi! Akauma meno kwa hasira. Akajaribu kutoa macho kwa nguvu labda ili aone vizuri!
Scolastica akamsogelea na kumuinamia huku akiendelea kuchanua lile tabasamu lake maridhawa. Kisengo akaachia kinywa wazi, akimtazama Scolastica kama asiyeyaamini macho yake. Scolastica akamuinamia zaidi na kumpapasa kidevuni kwa dhihaka, kisha kwa mnong’ono akamuuliza, “Unaikumbuka siku ile kule Komakoma uliponibaka wewe na Kibutu na Machemba?”
Uwezo wa kusikia bado ulikuwa kichwani mwa Kisengo. Kwa swali hili alimsikia vizuri na alimwelewa. Kwa jumla, ingawa nguvu katika viungo vyake ilikuwa ikmtoka kwa kasi, lakini bado alikuwa na uwezo wa kuona na kusikia huenda hata kutambua hili na lile kwa kiasi fulani.
Aliufungua mdoma na kujaribu kutamka, “Wewee…we…unasema nini…unase…” hakuweza kumalizia, mdoma ukarudi kuwa mzito.
“Umenisikia na kunielewa?” Scolastica alimuuliza kwa sauti yake ileile kama akinong’ona. “Mimi siyo Flora, ni Scolastica. Sasa umenikumbuka? Unaikumbuka vizuri ile siku mliponiteka na kuniingiza kwwenye gari pale Kinondoni kwa Manyanya na kunipeleka Komakoma? Unakumbuka mlivyonifanyia ukatili kwa kunibaka kisha kunilizamisha nizivunje laini zangu za simu?”
Kisengo aliendelea kumkodolea macho Scolastica, hali yake ikiwa vilevile, mdomo mzito, japo alimsikia kila alichokisema!
“Ningekuacha upumzike hadi kesho mchana, uamke na kwenda
zako,” Scolastica aliendelea kumwambia huku sasa akimtazama kwa macho makali bila hata chembe ya tabasamu. Sauti yake hiyo ya chini, sasa ilikuwa nzito na iliyoashiria jambo lingine tofauti kabisa na usalama. “Lakini dhamira itanisuta. Huenda malaika wangu pia akanishangaa. Na hata wewe hutanisamehe nikikuacha hai kenge mkubwa! Unapaswa kumfuata Kibutu!”
Kisengo alivuta pumzi ndefu na macho yakaanza kumlegea. Scolastica Temu akaufuata mkoba wake na kuitoa chupa ya PAK. Hakutaka kuendelea kupoteza muda. Mara baada ya kujifunga kitambaa vizuri eneo la pua na mdomo, kwa jumla uso mzima isipokuwa macho, akaifungua chupa hiyo na kumsogelea Kisengo. Alifanya kama ilivyompasa; wakati Kisengo akivuta pumzi ndefu mara mbili, chupa hiyo ilikuwa jirani sana na pua yake.
Ilitosha!
Alikufa macho yakiwa yanakodoa, kinywa wazi!
Sasa Scolastica aliamua kuangalia namna ya kuwa na hakika ya kupata mawasiliano na Machemba. Alijua kuwa kwa kitendo kile cha kumbaka siku ile, wakishirikiana bila ya soni, kwa vyovyote ni marafiki wakubwa, ambao kwa pia huenda kila mmoja ana namba ya simu ya mwingine.
Akaifuata suruali na kuipekua. Akakuta kuna simu mbili; moja kubwa nyingine ndogo. Akaanza na ile ndogo ambayo alihisikuwa ndiyo itakayokuwa inatumika zaidi kwa kuongea na watu. Hakupata shida kubonyeza hapa na pale na kuanza kuona orodha ya majina yaliyosajiliwa na Kisengo. Aliliona jina la Machemba mapema zaidi.
Akaenda kwenye eneo la ujumbe mbalimbali. Humo pia akakuta kuna ujumbe wa mwanamke mmoja ambaye alikuwa akituma maneno ya kimahaba yaliyokosa tafsida. Upande wa pili kulikuwa na ujumbe mwingine uliokuwa ukitumwa na Machemba kwenda kwa mwanamke huyo ambaye alisajiliwa kwa jina la Mwatum, naye akitumia maneno hayohayo makali kama vile wako chumbani wakistarehe.
Aliendelea kupekua na hatimaye akafarijika alipopata ujumbe uliooneshwa kuwa ni Kisengo kautuma kwa Machemba. ‘Inakuwaje?’ Ujumbe huo ulioneshwa kuwa umetumwa siku hii saa saba mchana. Akarudi kule ‘inbox’ na kuchunguza ujumbe ulioingia japo mwingi ulikuwa ni wa yule mwanamke, Mwatum. Akauona ujumbe kutoka wa Machemba uliosomeka, ‘Kila kitu tayari. Njoo kesho Maranatha Grocery saa 11 jioni.’
Scolastica akatikisa kichwa juu, chini huku akiiweka ile simu kubwa ya Kisengo kule mfukoni alikoitoa, na hii ndogo akaizima, akaipachika ndani ya mkoba wake.
Dakika tano baadaye alikuwa akiufungua mlango na alipotokeza koridoni, aliufunga kwa funguo. Hakuwa tayari kuziacha funguo hizo mapokezi, alizipachika mkobani mwake kisha akavuta hatu taratibu akielekea mapokezi.
ITAENDELEA KESHO
Sent using Jamii Forums mobile app