Riwaya: Scolastica Temu

Riwaya: Scolastica Temu

Bado dakika 40 ,Tunamsubiria Scolastica Temu
 
RIWAYA: SCOLASTICA TEMU (8)
MTUNZI/ MWANDISHI: INNOCENT A. NDAYANSE (ZAGALLO)
MWAKA 2002
MAREKEBISHO: MWAKA 2012
GAZETI: LETE RAHA

TULIPOKOMEA...


Kijana yule alimwangalia Scolastica kwa macho yenye mchanganyiko wa mshangao na matamanio. Hilo, kwa Scolastica halikuwa jambo la kujiuliza. Alijiamini kuwa ni mwanamke aliyetimia. Kwa kupitia kwenye miwani yake hii ya jua alimwona waziwazi kijana huyo akimtamani.

“Usiniangushe,” alimwambia huku akigeuka kuondoka baada ya kumtupia noti ya shilingi elfu kumi.
Wakati akienda hapo Ramos Restaurant, kumsubiri kijana huyo, alijua kuwa anacheza patapotea. Je, kijana huyo atakuja? Na hata kama atakuja, katika maongezi yao, ufumbuzi wa hii ziara iliyomtoa Kinondoni utapatikana?
Hakujua.

***ENDELEA***

WAKATI Mwasia, Ladhu Jaffer, alipokuwa akitoa maagizo ya kufunga duka, akili ya Jose ilikuwa kwenye ule wito aliopewa na Scolastica. ‘Ananiitia nini’ alijiuliza kimoyompyo. Hakukumbuka kama aliwahi kumwona siku yoyote zaidi ya siku hiyo.

Hata hivyo, alitaka aijue sababu ya kumwita huku akimwambia ‘atafurahi.’ Na alipokuwa akiondoka, alimwachia noti ya shilingi elfu kumi! Kwa nini? Alipotoka nje, aliwakwepa wenzake ambao mara kwa mara huwa wanaandamana kwenda kwa muuza mihogo ya kukaanga, ambaye hayuko mbali na duka hilo. Kwa mchana huu, aliwahi kutoka, na wenzake nao walipotoka, aliamini hawakumwona na wala hawatajua kuwa kaenda wapi.

Alitembea kwa hatua ndefu, akienda huko Ramos Restaurant. Dakika kumi hivi baadaye, alikuwa akiingia katika mgahawa huo. Hakukuwa na watu wengi, hivyo aliangaza macho kidogo tu na kufanikiwa kumwona Scolastica. Akavuta hatua taratibu akimfuata. Alipomfikia bado Scolastica alikuwa ameiinamia simu yake kubwa akiperuzi mitandaoni. “Za saa hizi shangazi,” alimzindua.

Ni hapo Scolastica alipozinduka na kuuinua uso. “Poa tu, karibu,” alimwitika huku akiachia tabsamu la kirafiki zaidi, akizinyoosha nywele zake ndefu zilizomwongezea mvuto. Jose aliketi kiti cha pili katika meza hiyo ambayo haikuwa na viti zaidi.

“Agiza chakula,” Scolastica alimwambia huku akiiweka simu mezani na kumtazama Jose kwa kujiamini.
“Jose aliiona kuwa hiyo ni bahati isiyostahili kupotezwa. Mgahawa huo ulikuwa na chakula kilichowavutia wengi katika eneo hilo, lakini bei yake ilimhitaji mtu asiye na ‘pesa za mawazo.’ Hakuwa na aibu, akaagiza ugali wa dona, nusu kuku wa kukaanga na soda kubwa ya baridi. Hakumbuki ni lini mara ya mwisho alikula kuku aliyeandaliwa kwa ubora kiasi hiki.
Wakati akianza kula, huku Scolastica akiwa na juisi ya embe mbele yake, ukimya ukavunjwa kati yao. “Mdogo wangu unaitwa nani?”
“Jose.”
Scolastica akatikisa kichwa huku akiuweka mrija mdomoni na kuifyonza kwa madaha juisi yake ile ya baridi. “Nashukuru kwa kuja. Naitwa Magreth John. Au niite Mage tu. Naishi Kigamboni. Wewe unaishi wapi?”
“Eneo la Tandale jirani na kituo cha Kwa Bi. Nyau.”
Kwa mara nyingine Scolastica alitikisa kichwa akiafiki. Kisha: “Najua, hunijui na labda utashangaa kuona nimekuomba uje tukutane. Us’ogope. N’na swali la kawaida tu.”
Kufikia hapo Scola alishusha pumzi, akaangaza macho pande tofauti za ukumbi huo, kisha akamrudia Jose. “Una muda mrefu katika ajira yako pale dukani?”
“Ni kama miezi kumi sasa. Sijui tuite muda mrefu au mfupi.”
“Ok. Unalipwa mshahara wa kiasi gani?”
Akilini mwa Jose akahisi kuwa huenda huyu mwanamke anataka kumchukua kwenye ajira mpya ambayo huenda yeye ndiye bosi. Hakusema uongo: “ Elfu sabini kwa mwezi.”
“Kula na nauli unajitegemea.”
“Ndiyo.”
Ukimya ukapita kidogo. Kisha Scolastica akaibuka tena. “Ukihitajika sehemu kwa mshahara wa laki mbili utaiacha hii ajira yako ambayo umeshazoeana hata na mabosi wako?”
Jose aliachia tabasamu kubwa. Akamega tonge la ugali huku akimtazama Scola bila kupepepsa. “Hilo halina mjadala dada’angu. Naondoka fasta yaan!”
Kicheko dhaifu kikamtoka Scolastica kabla ya kusema, “Anyway. Hilo tutalizungumza kwa kina keshokutwa. Kwa leo nimekuja kwa lingine. Wakati serikali ilipopiga marufuku utumiaji na uuzwaji wa sumu aina ya PAK ulikuwa umeshaanza kazi hapo kwa mhindi wako?”
Haraka Jose alitikisa kichwa akionesha kukubali huku mdomo ukitafuna pande la nyama. Akameza haraka na kujibu kwa sauti, “Nilikuwepo. Tayari nilikuwa na miezi minne.”
“Kwa hiyo kiukweli ulishiriki kikamilifu kuiuza hivyo unaifahamu vizuri.”
“Nd’o maana’ake, naijua sana,” Jose alijibu kwa sauti ya chini, bado akishindwa kumwelewa Scolastica alikuwa akielekea wapi katika haya maswali yake.
“Ok, baada ya kuipiga marufuku, nyie mlitekeleza agizo la kuiwasilisha au kuisalimisha kwa wahusika serikalini au mliendelea kuihifadhi kwenye maghala yenu?”
Jose alishtushwa na swali hilo. Akasita kujibu. Tendo hilo likampa picha Scola kuwa kijana kakumbwa na wasiwasi. Akamwahi, “Nilishakwambia, usiogope. N’ambie tu kwa kifupi mnayo au hamna?”
“Iliteketezwa.”
Scolastica alikaribia kucheka. Aliyaona macho ya Jose waziwazi yakitangaza woga na uongo. “Nyie nd’o mlioiteketeza?” alimbana.
“Hapana.”
“Sasa Jose, sikia,” Scolastica alisema kwa sauti ya chini. “Tusipoteze muda ukachelewa kwa Mhindi wako. Naitaka chupa moja tu. N’ambie, mnayo humo kwenu?”

Akili ya Jose ikaanza kutulia. Akamtazama sawia Scolastica na kukutana na yale macho mazuri yanayoshawishi na kubembeleza. Akayakumbuka yale maneno kuwa ‘atafurahi ashangae.’ Akahisi kuna biashara inanukia. Ni kweli duka la Ladhu Jaffer lilikuwa likiiuza PAK, na, siku serikali ilipoipiga marufuku, alichokifanya Mhindi huyo ni kusalimisha katoni nne tu kati tisa zilizokuwa stoo.

Kila katoni ilikuwa na chupa kumi na mbili za sumu ya PAK. Jose na wenzake walikuwa wakijua zilipohifadhiwa, lakini hawakuwa na shida nazo kwa kuwa walishajua zimepigwa marufuku. Ndani ya stoo hiyo pia kulikuwa dawa nyingine mbalimbali hususan za mimea.

Chupa moja ya PAK ilikuwa ikuzwa shilingi elfu hamsini kabla haijapigwa marufuku, lakini ikasemekana kuwa thamani yake ilipanda maradufu baada ya kupigwa marufuku! ‘Huyu Scolastica anaitaka, atanipa shilingi ngapi?’ Jose alijiuliza moyoni. Akimwona kuwa na mwanamke asiyekuwa na tatizo la pesa, Jose akaamua kuicheza karata yake. “Sister, ukweli PAK ipo lakini namna ya kuipata huko mhindi alikoifungia ni shugh’li!”
“Jose, wewe ni kijana wa kiume! Ina maana hupajui alikoihifadhi?”
“Siyo kwamba sipajui. Kule stoo tunaingia kuchukua bidhaa, na PAK iko huko kwenye katoni ambazo mojawapo iko wazi.”
“Kwa hiyo?” Scolastica alichoshwa na mizunguko ya Jose.
“Ni mpaka nitumwe huko nd’o naweza kuipata lakini namna ya kuificha itanibidi nichelewe kidogo huko ndani. Hapo sasa ujue najitoa mhanga tu dada’ngu, mhindi akinshtukia….”
“Naelewa. Nimekwambia naitaka na utafurahi. Najua utatumia akili ya kiume. Sema sasa nikupe ngapi?”
Jose aliwaza kidogo kisha kwa kumjaribu, akasema, “Laki nne.”
Kicheko kikamtoka Scolastica kwa mbali. “Nimekuuliza kama utapata ajira nyingine ya mshahara wa laki mbili kwa mwezi uko tayari kumwacha mhindi wako? Ukasema ni fasta yaani! Mimi nakuhitaji baada ya siku chache kwa mshahara huo. Sasa kwa nini unihukumu kiasi chote hicho?”
Kuambiwa kuwa ataajiriwa kwa mshahara wa shilingi laki mbili, Jose alipagawa. Akaropoka: “Ok, sister, sema uwewe unanipozaje.”
Scolastica aligongagonga kidole cha shahada cha mkono wa kulia huku akimtazama Jose usoni sawia kwa macho ya kujiamini. Kisha: “Nakupa laki na nusu kwa kuwa tumeshakuwa karibu. Hapa nakupa elfu kumi ya bure tu, ya kukupa nguvu ya kufanya kazi hiyo. Ukiileta unakutana laki na nusu yako. Pamoja?”
“Pamoja my dada,” tabasamu la kibwege lilichanua usoni pa
Jose bila kukatika.
“Hakikisha tu kuwa ni PAK original iliyotengenezwa Athens, Ugiriki. Sawa?”
“Tuliyonayo sisi ni le original dada Mage.”
“Ok, tusiuweke usiku, nenda kwa mhindi wako. Mnafunga saa ngapi?”
“Kumi na moja kamili.”
“Sasa nd’o kwanza saa nane na kitu,” Scolastica ni kama alikuwa akilalamika. “Utanikuta jirani na kituo cha mabasi ya mwendokasi cha Kisutu. Pale kwa muuza juisi ya miwa unapajua?”
“Sana tu mbona?”
“Utanikuta pale.
“Sasa…” Jose alisema na kusita.
“Vipi, tena?”
“Si ungen’achia namba yako ya simu?”
“Us’jali. N’takuona tu utakapokuja.”
Noti nyingine ya shilingi elfu kumi ikatua mkononi mwa Jose. Kijana wa kiume akaiona siku hiyo kashukiwa na nyota ya jaha!
“Ikifika kumi na moja na nusu hujafika hunikuti!” Scolastica alimwambia kama anyemwonya. Akanyanyuka na kumwacha akimalizia kuguguna pande la paja.

***ITAENDELEA
 
RIWAYA: SCOLASTICA TEMU (9)
MTUNZI/ MWANDISHI:
INNOCENT A. NDAYANSE (ZAGALLO)
MWAKA 2002
MAREKEBISHO: MWAKA 2016
GAZETI: LETE RAHA

TULIPOKOMEA.....

“Si ungen’achia namba yako ya simu?”
“Us’jali. N’takuona tu utakapokuja.”
Noti nyingine ya shilingi elfu kumi ikatua mkononi mwa Jose. Kijana wa kiume akaiona siku hiyo kashukiwa na nyota ya jaha!
“Ikifika kumi na moja na nusu hujafika hunikuti!” Scolastica alimwambia kama anyemwonya. Akanyanyuka na kumwacha akimalizia kuguguna pande la paja.

***ENDELEA***

SAA nane mpaka saa kumi na moja, kwa Scolastica ulikuwa ni muda mrefu sana kumsubiri Jose. Hakuwa na la kufanya. Aende wapi? Alitambua fika kuwa alipaswa kuwa na hadhari kwa kuwa ofisi yake iko humohumo katikati ya jiji. Ingeweza kutokea ghafla anakutana na bosi wake mtaani. Ataeleweka vipi?
Ingawa huku aliko ni mbali sana, Mtaa wa Mkwepu, iliko ofisi ya ED Advocates, lakini hicho hakiwezi kuwa kigezo kwamba haitabainika kaidanganya ofisi kuwa yuko Kigoma. Huenda mtu yeyote anayemjua sekretari Cathy au mkurugenzi, Evarist, akamwona huku mitaa ya mbali, lakini akaja kukutana na kuwaambia hao wenzake kuwa wamekutana au amemwona.

Hakupenda kuwe na hisia zozote ofisini kuwa kadanganya, hivyo aliamua kuwa na hadhari zaidi. Lakini afanye nini? Aende wapi? Wazo moja likamjia, kwamaba atafute kijigrosari atulie na kunywa bia mbili, tatu wakati akivuta muda. Alijiona kuwa sasa ameanza kuwa anaendekeza kunywa pombe tangu akumbwe na ule mkasa kiasi cha zaidi ya mwezi mmoja uliopita. Leo ni pombe za mchana mchana!

‘Ndiyo chanzo cha kuitwa cha pombe nini’alijiuliza kimoyomoyo. Kicheko kikamjia na kukimezea tumboni wakati akimfuata kijana mmoja aliyekuwa na nguo za mitumba akizinadi kwa wateja. Kwa kuwa alikuwa na nguo za kike, Scolastica alimfuata kama anayetaka kununua. Kijana akamchangamkia, “Mali safi shangazi….tena hizi kwa umbo lako zinakufaa sana…”
Scolastica alilishika gauni moja na kulitazama, akiligeuza huku na huku, kisha akamuuliza bei. Alipotajiwa akalalamika kuwa ni ghali sana. Kijana aliposhusha mara mbili zaidi, bado Scola aliruka kihunzi. Kwa jumla hakuwa na nia ya kulinunua gauni hilo. Akamtupia shilingi elfu mbili na kumwomba samahani kwa kumpotezea muda.
Wakati bado kijana akishangaa kwa kupewa noti ile, Scolastica akamdaka, “Sikia we’ chinga, wapi hapa kuna baa iliyostaarabika?”
Kijana huyo akakunja uso kidogo kisha akamjibu. “Naijuaga ile ilikuwa Zanzibar Hotel zamani, lakini siku hizi imebadilishwa jina.”
“Kwa maeneo ya huku hakuna?”
“Labda uende pale Akiba kwenye hosteli sijui ya wanachuo wa wapi? Pale kituo cha daladala cha Akiba utaliona geti ulizia tu watakuonyesha wale chinga wenzangu pale nje.”

SAA kumi na moja kasoro dakika chache, Scolastica Temu akiwa na bia tatu kichwani, alikuwa akilisogelea eneo ambalo kulikuwa na uuzwaji wa juisi ya miwa. Alipobakiza mita kama hamsini hivi, alijiegemeza kwenye nguzo ya korido ya jengo moja la ghorofa tatu. Hapo pia kulikuwa na wajasiriamali waliokuwa na bidhaa mbalimbali wakizinadi.
Alitulia hapo kama mtu wa kawaida ambaye labda anamsubiri mtu fulani. Hakuna aliyejali uwepo wake mahali hapo. Kila mtu alikuwa na pilika zake. Yeye alikuwa makini, macho kayatuliza pale kwenye kituo cha juisi ambako aliwaona watu wachache wakiwa na glasi za juisi wakinywa.

Saa kumi na moja na dakika kumi ilimkuta hapo. Alikuwa akimsubiri Jose, na alitaka Jose ndiye atangulie kufika hapo. Alitaka amwone kwanza ili ajue kama kweli kaja peke yake au kaja na mtu wa kumchuuza. Ingawa ilikuwa ni vigumu kutambua kuwa kuna njama za kumgeuzia kibao kwa kununua PAK, hata hivyo aliamua tu kutega hapo katika kuchukua hadhari.

Hatimaye akamwona Jose akilisogelea eneo hilo kwa mbali. Begi dogo lilikuwa likining’inia mgongoni. Alipokisogelea kituo kile cha juisi, alibaki akiangaza macho huku na kule. Scolastica akaendelea kubana palepale, akimwona kwa usahihi ilhali Jose hamwoni. Mara akaagiza glasi ya juisi na kuanza kunywa huku akiendelea kutupia macho huku na kule. Alikunywa taratibu, labda tu akikumbuka kuwa Scolastica alimwambia ni yeye atayemwona na atamfuata.
Ni hapo Scolastica alipojiwa na wazo. Akatoka pale kwenye nguzo na kuifuata teksi iliyoegeshwa upande wa pili wa barabara. “Kuna mahali nakwenda lakini pitia kwanza pale kwenye juisi ya miwa,” alimwambia dereva huku kishaketi kiti cha mbele.

Dereva akaligeuza gari na kukifuata kituo cha juisi. Alipokanyaga breki, Scolastica akamwambia apige honi. Dereva akatekeleza na papohapo watu kadhaa waliokuwa hapo waliligeukia gari hilo, Jose akiwa mmojawao. . Jose akamwona. Papohapo Scolastica akamwashiria kwa mkono aende. Haraka Jose akaitua glasi na kumfuata.

Mlango wa nyumba ulikuwa umeshafunguliwa, alipoingia tu gari likaondoka.

*****ITAENDELEA WAKATI WOWOTE*****
 
RIWAYA: SCOLASTICA TEMU (10)
MTUNZI/ MWANDISHI: INNOCENT A. NDAYANSE (ZAGALLO)
MWAKA 2002 GAZETI LA LETE RAHA
MAREKEBISHO: MWAKA 2016

TULIPOKOMEA...


Dereva akaligeuza gari na kukifuata kituo cha juisi. Alipokanyaga breki, Scolastica akamwambia apige honi. Dereva akatekeleza na papohapo watu kadhaa waliokuwa hapo waliligeukia gari hilo, Jose akiwa mmojawao. . Jose akamwona.
Papohapo Scolastica akamwashiria kwa mkono aende. Haraka Jose akaitua glasi na kumfuata. Mlango wa nyuma ulikuwa umeshafunguliwa, alipoingia tu gari likaondoka.

***ENDELEA***

Walishika Barabara ya Morogoro na walipofika mbele kidogo waliachana nayo, wakashika Barabara ya Bibi Titi Mohamed, uelekeo wa Mahakama ya Kisutu. Kwa maelekezo ya Scolastica, walipoivuka mahakama, gari likakata kushoto na kuifuata Barabara ya Magore. Wakaivaa Upanga. Wakaenda hadi walipoikaribia Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert.

Scolastica akamwambia dereva aegeshe gari pembeni. Kisha akamgeukia Jose. “Vipi, uko kamili?”
“Nd’o maana’ake.”
Scolastica akamrudia dereva huyu aliyeonekana kukaribia umri wa miaka sitini. “Babu, nisubiri kidogo. Bado tuko pamoja, lakini nina maongezi kidogo ya faragha na huyu dogo.”
“Wewe tu mjukuu wangu, mi’ nipo kwa ajili yako. Hizi nd’o kazi zetu.”
Scolastica akafungua mlango na kumfungulia Jose. Walikwenda kwenye boneti la gari na kuliegemea. “Enhe, mzigo uko wapi?” Scola alimuuliza.

Jose aliyekuwa amevaa shati refu bila kuchomekea, suruali pana ya kitambaa chepesi, aliingiza mkono ndani ya mfuko wa kulia na kutoa kitu kilichozungushiwa kipande cha gazeti. Akageuza macho kwa chati pande zote za barabara. Kulikuwa tulivu. Watu wawili, watatu walionekana kwa mbali wakitembea, magari yakipita kwa uchache sana. Kwa jumla mazingira yalikuwa rafiki kwao.

Jose akampatia Scolastica bila ya kufunua hicho kipande cha gazeti. Kwa mkono wa kushoto Scolastica alikipokea kifurushi hicho kisha akakifunua. Sasa akakutana na kipaketi cheusi kilichofungwa madhubuti na juu kukiwa na herufi tatu tu kubwa; PAK. Akaishuhudia chupa yenye kijikaratasi cheupe na msitari mwekundu uliokizunguka. Chupa hiyo ya mviringo, ilikuwa na maandishi makubwa meusi; PAK.

Aliiangalia sehemu mbili muhimu na kuigundua kuwa ni halisi siyo feki. “Hapa umecheza,” alimwambia Jose huku akiufungua mkoba wake. Akachomoa bunda la shilingi laki mbili na kupunguza shilingi elfu hamsini. Akampatia Jose huku akiongeza, “Ni kama tulivyoongea. Sawa?”
Jose alikuwa akizihesabu fedha zile. Alipohitimisha akasema, “Shukrani anti. Sasa kuhusu ile ishu?”
“Ipi?”
“Ile ya job. Nd’o itakuwaje?”
Scolastica alicheka kimoyomoyo huku akimhurumia Jose. Akamtazama kwa makini na kutoa jibu: “Us’konde. Nipe namba yako. Wiki ijayo n’takucheki.”
Haraka Jose akamtajia.
“Unasema unaishi Tandale?”
“Ndiyo.”
“Twende tukuache pale Palm Beach.”
Wakarudi garini. Walipofika kituo cha daladala cha Palm Beach, Scolastica akamwambia, “Unasikia dogo, panda hapa daladala za Mwananyamala mpaka Kinondoni. Pale utapata usafiri wa kukupeleka kwenu Tandale. Uliza tu pale kituoni utaelekezwa. Kuna daladala za kutoka Masaki zimeandikwa Masaki- Simu 2000.”
“Asante, anti,” Jose alisema huku akiteremka.

Akiwa bado anajali kuchukua tahadhari katika kila alifanyalo, mara tu teksi ilipofika kituo cha daladala cha Morocco, Scolastica akaamua kuteremka. Kutoka hapo alitembea hadi kwake, Mtaa wa Kairuki mbele kidogo ya Kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka.

Akiwa ndani ndipo alitwaa karatasi iliyokuwa ndani ya pakiti ya sumu ya PAK na kuanza kuyasoma maelekezo juu ya matumizi ya sumu hiyo. Zikamchukua dakika kama kumi akisoma kwa umakini mkubwa na kuzingatia kila lililoandikwa hapo.

Aliporidhika, akaihifadhi ndani ya saraka moja kabatini. Kijigiza kilipoanza kuingia, akatoka na kwenda Pazi Social Club. Pale, kama kawaida akanywa bia tatu na kula mishkaki kadhaa, kisha akarejea nyumbani saa nne kasoro. Alipokwishaoga, akakitazama kitanda ambacho kilimlaki, usingiza ukatwaa nafasi.

Siku iliyofuata, alishinda hapo nyumbani kwake tangu asubuhi hadi mchana, akifanya usafi wa ndani kisha akafua nguo kabla ya kwenda kujichukulia chakula chepesi palepale Pazi; chipsi na nusu kuku. Alipokwishapata mlo huo, alijilaza sofani na kuangalia vipindi hivi na vile kwenye runinga. Hata hivyo nusu saa haikufika, usingizi ukamvaa.

Alizinduka saa kumi na moja jioni. Akafikiri huku akiangaza macho nje. Akaona bado mapema sana kwa kufanya kile alichokikusudia. Ilipotimu saa kumi na mbili ndipo alipoingia bafuni, akaoga na kubadili mavazi. Alivaa gauni la kitambaa chepesi lililomshika mwili hususan sehemu za nyonga na hivyo kulifanya robota la kiuno chake liwe katika mtikisiko kila alipotembea.

Akazirekebisha nywele zake nyingi na nyeusi tii zilizomwagikia mgongoni, Aliposimama kwenye kioo kikubwa kilicholibeba umbo lake lote, akajiona kuwa kapendeza. Aliridhishwa na maandalizi yake. Sasa akautwaa mkoba wake, akaufungua na kuipachika ile chupa ya PAK. Ndani ya mkoba huo pamoja na chupa hiyo pia kulikuwa nia vikorokoro vingine vingi ambayo wanawake hupenda kuvibeba.

Kabla ya kuondoka akajipulizia manukato makali na kujiona sasa kakamilika. Akatoka, mkoba, bega la mkono wa kushoto, simu mkono wa kulia. Alitembea taratibu tu, kwa madaha na kuwa kivutio kwa kila kijana wa kiume aliyekutana naye.

Sasa kijigiza kilikuwa kikizidi kuitawala anga. Alipotokeza Barabara ya Kawawa, akaiona bajaji imeegeshwa kwa muuza machungwa. Akamfuata dereva na kumtaka ampeleke Kinondoni ‘A.’
“Pale kituo cha daladala?” dereva alimuuliza wakati wakiondoka.
“Hapohapo.”
Dakika chache baadaye Scolastica alikuwa ameteremka kwenye kituo cha daladala cha kwenda katikati ya jiji cha Kinondoni ‘A’. Eneo hilo lilikuwa tulivu sana. Madereva watano walikuwa juu ya pikipiki zao wakisubiri wateja. Nyuma kidogo ya kituo hicho, kulikuwa na mti ambao chini yake biashara ya tangawizi na kahawa ilikuwa ikiendelea.
Pia kulikuwa na wapigadebe wachache waliokuwa wakizagaazagaa katika eneo hilo, baadhi wakionekana wamechangashwa kwa ulevi wa aina fulani na wengine wakiwa katika hali ya kawaida.

Alisimama kituoni pale kama abiria wengine wachache waliokuwa wakisubiri daladala za kwenda aidha Posta au Stesheni, lakini yeye akiwa lengo lake. Macho yake yalikuwa yakitambaa kwa huyu na yule hususan hawa wapigadebe.
Hatimaye alivutiwa na mpigadebe mmoja aliyeonekana hajachangamka bila mpangilio na hakuwa na dalili ya kupata kilevi.. Akajitoa kituoni na kumsogelea taratibu. “Habari yako?” alimwingia, sauti yake ikiwa ya upole na ya chini.

“Fresh tu, shangazi,” kijana huyo aliitika kwa sauti yenye kijimkwaruzo kama sauti za wapigadebe wengi wa eneo hilo. Akamtazama Scolastica juu hadi chini. Kwa mbali alikumbwa na mshtuko kwani ingawa hakuwa mgeni machoni mwake, akiwa amekwishamwona mara nyingi jioni anapoteremka kwenye daladala, hata hivyo hakuwa na matarajio ya siku moja kukutana kwa ukaribu kiasi hiki.

Akaonekana kujawa na maswali mengi yasiyokuwa na majibu huku pia macho yake yakionesha kumkubali kutokana na jinsi alivyopendeza.
“Nina shida kidogo,” Scolastica alimwambia bila ya kujali ile tazama yake yenye mchanganyiko wa uchu wa matamanio na kujiamini.
“Mimi?” kijana huyo aliuliza.
“Yeah, wewe! Usihofu. Una ‘chance’ kidogo?”
“Kuhusu nini?”
“Kawaida tu. Unaogopa nini mwanaume mzima?” tabasamu likachanua usoni pa Scolastica.
Kijana yule aliwaza kisha akauliza, “Tuzungumzie wapi? Si unajua tena niko ofisini kwangu hapa shangazi?”
“Najua,” Scolastica alijibu huku akifungua mkoba, akaingiza mkono na kuchakurachakura kisha akatoa noti kadhaa. Akazichamba na kuchomoa moja ya shilingi elfu mbili. Akampatia mpigadebe huyo akijua kuwa hawezi kuikataa kwa kuzingatia hesabu ya kupigia debe daladala moja haizidi shilingi mia tatu.

ITAENDELEA SIKU YOYOTE
 
Huu mpango wa scala mbona kama hatar
 
RIWAYA: SCOLASTICA TEMU (11)
MTUNZI/ MWANDISHI: INNOCENT A. NDAYANSE (ZAGALLO)
MWAKA 2002 GAZETI LA LETE RAHA
MAREKEBISHO: MWAKA 2016

TULIPOKOMEA...

“Najua,” Scolastica alijibu huku akifungua mkoba, akaingiza mkono na kuchakurachakura kisha akatoa noti kadhaa. Akazichamba na kuchomoa moja ya shilingi elfu mbili. Akampatia mpigadebe huyo akijua kuwa hawezi kuikataa kwa kuzingatia hesabu ya kupigia debe daladala moja haizidi shilingi mia tatu.

***ENDELEA***


Tabasamu la mbali likamtoka kijana huyo wakati akiipokea noti hiyo. Kisha akasema, “Tusogee huku dada’angu. Hapa wanga wengi, siyo kwamba kila mtu ni msafiri.”
Wakaelekea mbele kidogo ya kituo hicho kama wanaokwenda Mtaa wa Wibu. Walipofika umbali wa mita kama hamsini hivi wakasimama.

“Sikia anko,” Scolastica alianza, “hapa tunaongea mimi na wewe. Ya kwetu ni ya kwetu.” Akasita kidogo. Akaangaza macho kulia na kushoto, nyuma na mbele kisha: “Kuna anko mmoja hivi, mfupi, mweusi, huwa mara nyingi nadhani yupo eneo hili. Ana teksi. Na nadhani huwa anaegesha hapa. Lakini muda huu naona hapo hakuna teksi hata moja. Unamfahamu?”
Kijana huyo alikunja uso, akaguna. Kisha akauliza, “Yukoje? Nadhani sijakuelewa vizuri shangazi.”
“Yaani ni mfupi,” Scolastica alijitahidi kufafanua. “Anapendelea kuvaa hii mijezi ya timu za soka za Ulaya.”
“Na ni dereva teksi?”
“Ndiyo. Nimeshamwona mara nyingi akiwa na teksi lakini ni hizi teksi bubu.”
“Ya aina gani?”
"Nyeupe ya kawaida tu. Ni kama Corolla ile.”
Kijana alizama mawazoni huku kakunja uso. Kisha akaibuka tena na swali, “Hana kitu chochote kingine kinachomtambulisha viziuri? Mana’ake mie niko hapa ‘longi’ sana, kama mvua kumi hivi.”
Scolastica alifikiri ikdogo kisha akasema, “Ana pengo, tuseme kwenye meno ya juu katikati kuna jino moja limevunjikia kati. Halafu, kwenye kiganja cha mkono wa kulia ana kovu, ni kama aliunguaga zamani.”
Kijana huyo akaachia cheko la mbali huku akimtazama sawia Scolastica. “Siye Kibutu huyo?!”

KITU kama radi kilipenya masikoni mwa Scolastica Termu pale jina la Kibutu lilipotajwa na mpigadebe! Halikuwa jina geni kwake. Wakati Kibutu alipokuwa akimtongoza kwa nia ya kuwa na uhusiano wa mapenzi, na kumpa lifti mara kwa mara hata kufikia hatua ya kumteka, alikuwa amekwishajitambulisha kwa jina hilo.
“Anaitwa Kibutu?” alimuuliza kama asiyejua.

“Nadhani nd’o unamsema wewe,” mpigadebe alijibu. “Ni dereva teksi, huwa anapaki hapa, ila ikifika jioni huwa ana tenda zake mbili kubwa. Na akiondokaga harudi. Mida hii hawezi kuwa hapa. Yuko hivyo kama unavyosema. Anapenda kuvaa jezi za timu za Manchester, mara Barcelona, mara Simba. Na ana jino lililovunjika. Ni mweusi. Ni mfupi kidogo, ana mwili. Na hilo kovu la mkononi analo kweli huyu ninayesema mimi.”
“Unasema jioni huwa hayupo hapa?”
“Mida hii huwezi kumpata hapa. Una shida naye sana? Ni nani yako, anti?”
Lilikuwa ni swali ambalo Scolastica hakulitarajia. Hata hivyo hakukosa jibu. “Nina maagizo yake kutoka kwa girlfriend wake.”
“Huna namba yake?”
“Sina kaka’angu. Unadhani anaweza kuwa wapi mida hii kama anakuwa ameshatoka kwenye kituo chake hiki?”
Kijana huyo akacheka kidogo huku akitoa kipisi cha sigara ndani ya mfuko wa shati. Akamsogelea kijana aliyekuwa akitembeza kahawa na kumsimamisha. Akakiwasha kipisi chake na kumrudia Scolastica. “Unajua sista yule ni mtu wa maji sana,” alimwambia. Akaongeza, “Kama mkwanja umemkubali huwezi kumwona hapa saa hizi. Na karibu kila siku mambo yake ni supa tu. Mida hii anaweza kuwa kwenye baa fulani anakopendaga kwenda.”
“Wapi huko?” Scolastica alimdaka.
“Mood Bar. Ni pale Mtaa wa Togo. Unajua mtaa huo?”
“Scolastica alitikisa kichwa kukataa.
“Ukitoka hapa,” kijana alianza kumwelekeza, “utauacha huo Mtaa wa Wibu. Ule unaofuata ndiyo Togo. Shika kushoto, ukienda mbele utasikia midundo ya muziki kwa nguvu. Ni hapohapo. Pameshangamka kiasi. Ni baa mpya na unajua tena walevi kwa kukimbilia baa mpya…!”
“Kila siku huwa anakuwa hapo?” Scolastica alimuuliza kama asiyemwamini.
“Deile yaaan dada’angu,” jibu la kijana huyo lilitoka huku akipuliza moshi wa sigara angani. “Hata mimi nikiwa na vijisenti kidogo nafikaga pale kushtua vitu vikali vya kupima. Nakutaga wakati mwingine akiwa na wash’kaji zake. Na kwa kuwa pale kuna ‘maskrini’ ya kuonyesha mechi za soka, basi hakosagi.”
“Saa hizi anaweza kuwepo?” Scolastica aliuliza huku akitazama muda kwenye simu yake kubwa.
“Sina hakika. Lakini ningekushauri ujaribu. Unaweza mkuta. Huwa haondokagi mapema yule. Saa nne, tano zinamkutaga pale.”
Scolastica aliona kuwa ile noti ya shilingi elfu mbili haikupotea bure. Huku akiwa na imani ya kupata chochote huko Mood Bar, alimwongeza mpigadebe huyo shilingi elfu moja na wakaachana.

Kichwani alikuwa ameshajiwa na wazo lingine aliloamini kuwa likifanyiwa utekelezaji, tena bila kuchelewa, ratiba zake zitakuwa na mafanikio. Upande wa pili wa kituo hicho kulikuwa na duka la dawa. Jirani na duka hili kuna baa. Ndani ya baa hiyo hakukuwa na watu wengi. Akaamua kwenda hapo baa ili afanye kile alichofikiria kuwa ni kwa manufaa yake.
Alipoingia ndani ya baa hiyo, akachagua meza ambayo hakukuwa na mtu mwingine. Akaketi na kama kawaida akaagiza bia moja. Wakati akiisu bri bia hiyo, akaitoa simu yake kubwa na kuingia mtandaoni.

Alikuwa akisaka aina fulani za dawa alizowahi kusikia kuwa zilihusika sana katika matibabu makubwa na yaliyowahusu wagonjwa ambao iliwalazimu kupewa dawa za aina hiyo. Kwa dakika kadhaa alikuwa akiperuzi mitandao hiyo ya kimataifa na akafanikiwa kuziona dawa ambazo alizihitaji. Tabasamu a mbali likamtoka. Dawa alizozisoma hapo mtandaoni ndizo alizozihitaji. Lakini mara akakunja uso na kujiuliza, kwa hapa Dar es Salaam dawa hizo zipo?

Swali hilo akaliponda papohapo alipotambua kuwa dawa hizo ni halali na hazijapigwa marfuku kutumiwa ila tu labda mtumiaji azitumie kwa malengo tofauti, yasiyostahili kwa matumizi ya binadamu. Ni dawa za kawaida, kwa matumizi ya kawaida. Kwa kutambua hivyo, aliinywa bia haraka na kunyanyuka. Hakwenda mbali. Aliingia ndani ya duka maarufu la dawa lililokuwa jirani.

Alimkuta mhudumu wa kike, mweupe, akiwa amejitanda lile jaketi jeupe la uuguzi. Baada ya kumsalimia, alimwomba kijikaratasi ili amwandikie dawa alizozihitaji. Alifanya hivyo kwa kuwa muda huo aliingia mteja mwingine. Scolastica hakutaka suala hilo liyafikie masikio mengine yasiyohusika. Alipopewa karatasi na kalamu, aliandika majina ya dawa hizo; Olanzapin, Lorazepam na Diazepam. Kisha akasubiri yule mteja ahudumiwe, na alipokwishaondoka, akampatia huyo dada hicho kijikaratasi huku akimuuliza, “Naweza kupata dawa yoyote kati ya hizo?”

Yule mhudumu alizisoma dawa hizo na kuguna kimoyomoyo. Kwa kanuni za afya, dawa hizo hutolewa kwa utaratibu maalum na kwa kibali cha daktari. Siyo dawa za kununuliwa ovyoovyo madukani. Kwa hali hiyo, japo dawa hizo zilikuwapo hapo dukani, mhudumu huyo hakuwa na muda wa kumpa maelezo mengi Scolastica, zaidi alimshangaa.
Akajiuliza, anazitaka za nini? Ni dawa zinazotumiwa kwa nadra sana na kilichopaswa kufanywa hapo, ni kumjibu kuwa dawa zipo ila haziuzwi mpaka mteja awe na cheti rasmi cha daktari kutoka hospitali. Hata hivyo hakuwa na muda wa kumpa maelezo hayo. Alihisi yanaweza kufuata maswali mengi ambayo kwa wakati huo yeye hakuwa tayari kuyajibu. Hakuwa na muda wa kukisumbua kichwa kutoa maelezo mengi.

“Hizo dawa hapa hatuna dada’angu,” ndivyo alivyomjibu huku akimrudishia kile kijikaratasi.
Scolastica alishusha pumzi ndefu na kuonekana kukata tamaa. “Naweza kuzipata wapi?”
“Kwa kweli sijui, jaribu kwenye ‘famasi’ nyingine labda utapata.”

Scolastica aliondoka akidhamiria kutoahirisha mchakato huo, lakini aliona muda siyo rafiki. Alihitaji kupata tembe hizo kwa udi na uvumba. Nje ya duka hilo kulikuwa na bodaboda kadhaa zimeegeshwa. Akamfuata kijana mmoja na kumwambia ampeleke Magomeni. Sasa aliamua kufanya kusudi kwenda kwenye maduka yaliyo mbali na eneo hilo la Kinondoni. Walipofika Magomeni Mapipa, akaenda kwenye duka moja na kumkuta mhudumu akichati na simu.
Alipomwambia hitaji lake, mhudumu huyo wa kimue, kijana ambaye Scolastica alimwona ni mdogo kwake kiumri, akaonesha kushtuka.
“Mbona unashtuka?”
“Unajua sister, dawa hizo hazitolewi kienyeji. Una cheti cha daktari?”
“Cha nini?”
“Siruhusiwi kukuuzia mpaka uwe na cheti cha daktari.”
Scolastica alimtazama kwa sekunde chache kijana huyo. Wazo kwamba pesa ni sabuni ya roho na kato la ukata, likamjia akilini. Akawaza, kijana mdogo kama huyu anaweza kukataa pesa eti kwa kufuata kanuni za kuuza dawa baada ya kuoneshwa cheti cha daktari? Kijana wa Tanzania ya leo ana msimamo huo? Akajaribu bahati.
“Kwani dawa hizi zinauzwaje?”
“Shilingi elfu mbili kwa tembe moja.”
Scolastica aligeuka nyuma, mlangoni. Hakuona dalili ya mteja mwingine anayekuja. Akamrudia kijana huyo. “Sikia, nipe vidonge vitatu vya Olanzapin. Nina elfu thelathini yako hapa. Achana na sera zako za cheti cha daktari. Uko Magomeni kwa wajanja halafu bado unakuwa na sera za kizee-zee!”

Dakika mbili za awali kijana huyo alikuwa akizifungia tembe hizo kwenye kibahasha maalumu, dakika ya tano, Scolastica alikuwa nje ya duka hilo akiifuata bodaboda huku nyuma mhudumu huyo wa duka akizipachika noti tatu nyekundu ndania ya pochi, tabasamu likichanua usoni.
“Wapi, sister?” dereva wa bodaboda alimuuliza Scolastica wakati wakiondoka.
“Kinondoni, Togo Street.”

ITAENDELEA
 
RIWAYA: SCOLASTICA TEMU (12)
MTUNZI/ MWANDISHI: INNOCENT A. NDAYANSE (ZAGALLO)
MWAKA 2002 GAZETI LA LETE RAHA
MAREKEBISHO: MWAKA 2016

TULIPOKOMEA....

Dakika mbili za awali kijana huyo alikuwa akizifungia tembe hizo kwenye kibahasha maalum, dakika ya tano, Scolastica alikuwa nje ya duka hilo akiifuata bodaboda huku nyuma mhudumu huyo wa duka akizipachika noti tatu nyekundu ndani ya pochi, tabasamu likichanua usoni.
“Wapi, sister?” dereva wa bodaboda alimuuliza Scolastica wakati wakiondoka.
“Kinondoni, Togo Street.”


***ENDELEA***


Wakati dereva wa bodaboda hiyo alipokuwa akiiacha Barabara ya Morogoro na kushika Barabara ya Kawawa, Scolastica alikuwa akiwaza kitakachojiri huko alikokuwa akienda. Ni Mtaa wa Togo, mtaa amabao hana uzoefu nao. Lakini kwa kuwa alijua mitaa mingi ya Kinondoni, hususan Kinondoni ‘A’ imepangika vizuri, hakuwa na shaka yoyote kuhusu kuifikia hiyo Mood Bar.
Dakika zisizotimu kumi baadaye, walikuwa wameshafika Kinondoni. Scolastica akamwambia dereva amwache mbele kidogo ya kituo cha daladala. Hakutaka kukutana tena na yule mpigadebe, wala hakutaka ajue kuwa bado yupo maeneo hayo.

AKITEMBEA taratibu, kama asiyekuwa na malengo yoyote, Scolastica alivuta hatua akiuvuka Mtaa wa Wibu na kuufuata Mtaa wa Togo. Akiwa ameyazingatia maelekezo ya yule mpigadebe, muda si mrefu aliisikia mirindimo ya muziki, na hapo akajua hajapotea.

Alipofika eneo alilolikusudia, akazishuhudia taa mbalimbali za rangi, ndani na nje kiasi cha kupafanya mahali hapo pavutie. Hakukuwa na watu wengi, lakini takribani kila aliyekuwamo alikuwa kachangamka. Aliingia kwa mwendo wake uleule wa taratibu na kwa chati akiyashuhuhdia macho ya baadhi wanaume yakimfuata. Hakushangaa; gauni lake hili la kitambaa laini, lililomshika vilivyo katika umbo lake lenye kushawishi na kutamanisha, lilitoa taswira ya kuwafanya wanaume, hususan wakware, wamkodolee macho ya uchu wa matamanio. Alishazoea.

Tangu alipoingia, alikwishaliona eneo ambalo kulikuwa na viti na meza lakini hakukuwa na wateja. Eneo la kulia mwa ukumbi huo, viti vyote vilikuwa na wateja, chupa za vinywaji mezani. Akahisi kuwa huenda ni kwa kuwa lile eneo ambalo halina watu kuna spika zilizorindima muziki ambao labda wateja wangekosa utulivu na wasingesikilizana katika maongezi.

Hakujali. Akalifuata eneo lile ambalo kulikuwa na meza nne, kila meza ikiwa na viti vinne lakini kote kukiwa tupu. Akavuta kiti kimoja na kuketi. Kaunta ya baa hiyo haikuwa mbali na pale alipoketi na kwa chati, aligundua kuwa wanaume wachache kati ya waliokaa pale kwenye viti virefu, walizigeuza shingo na kumtazama. Hakujali vilevile. Akaitoa simu mkobani na kuanza kupotezea muda akiiwasha kisha akaingia mitandaoni. Haikutimu hata dakika, mhudumu alikuwa mbele yake.

“Karibu dada,” mhudumu alisema. “Umeshasikilizwa?”
“Ndiyo kwanza nimefika.”
“Ok, nakusikiliza.”
Scolastica akaagiza bia. Wakati akisubiri, alikuwa katika uchunguzi, macho yake yakijitahidi kupita hapa na pale kwa huyu na yule kati ya wateja waliokuwa humo. Kwa eneo la jirani na alipokuwa ameketi, alifanikiwa katika kuzungusha macho yake kwa kila aliyekuwa kitini. Lakini kwa mbali kidogo, kule kulikokuwa na kaunta hakuweza kumjua kila aliyeketi. Afanyeje? Aendelee mwenye kule kaunta na kujitia kuagiza chochote ili dhamira yake itimie?
Kitu kilichomtia matumaini ni pale alipotupa macho kwa makini katika ukuta, kulia mwa kaunta na kuyaona maandishi; TOILET / VYOO kisha mchoro mmoja wa mwanamke na mwingine wa mwanaume, ukionesha kutofautisha eneo la huduma kwa watu wa jinsi tofauti.

Ili mtu aifikie njia ya kwenda huko msalani, ilimpasa apite umbali mfupi na kaunta. Scolastica akakumbuka taarifa aliyopewa na yule mpigadebe. Akayakumbuka baadhi ya maneno yake; ‘Kama mkwanja umemkubali huwezi kumwona hapa saa hizi. Na karibu kila siku mambo yake ni supa tu. Mida hii anaweza kuwa kwenye baa fulani anakopendaga kwenda.’ Kisha tena baadaye alimwambia, ‘Lakini ningekushauri ujaribu. Unaweza mkuta. Huwa haondokagi mapema yule. Saa nne, tano zinamkutaga pale.’

Hata hivyo, alitulia kwanza. Hakuwa na papara. Akainywa ile bia ya kwanza kwa kasi kisha akaagiza nyingine. Alijenga imani kuwa bia mbili, tatu zitakapopenya tumboni, huenda akajisikia kujiamini maradufu, hali aliyoihitaji sana.
Idadi ya watu ilikuwa ikiongezeka. Pale mezani akajikuta yuko na mwanadada ambaye alifika hapo kwa ajili i ya kupata mlo pekee. Wakati akiendelea kula, Scolastica akaamua kutoendelea kupoteza muda. Ilikuwa imeshatimu saa mbili na dakika arobaini na tano.

Akajitoa kitini, akasimama na kulivutavuta gauni lake lililombana mapajani. Akaitwaa chupa ya bia na kunywa kwa mfululizo hadi tone la mwisho. Watu wawili, watatu katika meza za jirani, na hata huyu mwanadada aliyekuwa hapo mezani, wakamtazama kwa mshangao. Yeye kama kawaida, hakuwajali; akawaacha waendelee kushangaa. Kwa usalama wake aliamini kuwa hakupaswa kwenda msalani na kuacha kinywaji ndani ya chupa eti ili akirudi aendelee kukinywa.

Mjini ni mjini tu, kuna hila nyingi. Anaweza kujuta kwa kufanya upuuzi wa aina hiyo. Akamtazama yule dada na kumwambia, “Dada, nafika toilet mara moja.” Yule mwanadada aliitika kwa kutikisa kichwa. Wakati Scolastica akiondoka, akakutana na yule mhudumu aliyekuwa akimletea vinywaji. Akamsimamisha na kumwagiza bia nyingine aipeleke pale mezani. Akaendelea kwenda msalani huku akiamini kuwa macho yake yasiyokuwa na dosari yoyote, yangeweza kumwona yeyote ambaye alihitaji kumwona.

Wakati akielekea msalani, akiwa anapita jirani na kaunta kulikokuwa na wanaume watano na vinywaji vyao, alitupia macho hapo. Akasimama kidogo na kutazama kwa makini japo ni kwa namna isiyomshangaza yeyote. Akatikisa kichwa na kuendelea na safari yake.

Dakika chache baadaye alipotoka msalani, kwa mara nyingine aliwatupia macho wateja hao waliokuwa kaunta wakizungumza kwa sauti kali, huku wakicheka na kutaniana, baadhi wakionekana dhahiri kukolewa na kilevi. Macho yake yaleyale aliyoyaamini kwa asilimia mia moja, yalimfanya aachie tabasamu la mbali huku akitikisa kichwa kuonesha ishara ya kukubali. Aliona alichokuwa akihitaji kukiona! Akarudi mezani kwake.

KIBUTU alikwishaigeuza sheria badala ya kawaida, ile tabia yakwenda Mood Bar kunywa bia kila siku. Jioni ya siku hii, kama jana na juzi, akiwa na kiburi cha kulipwa shilingi milioni tatu kutokana na zabuni hewa aliyopewa na kampuni iliyokuwa ikitumia teksi yake kwa kutoa huduma, alijisikia kuwa katika sayari nyingine. Nani kama yeye?

****ITAENDELEA
 
RIWAYA: SCOLASTICA TEMU (13)
MTUNZI/ MWANDISHI: INNOCENT A. NDAYANSE (ZAGALLO)
MWAKA 2002 GAZETI LA LETE RAHA
MAREKEBISHO: MWAKA 2016

TULIPOKOMEA...


KIBUTU alikwishaigeuza sheria badala ya kawaida, ile tabia yakwenda Mood Bar kunywa bia kila siku. Jioni ya siku hii, kama jana na juzi, akiwa na kiburi cha kulipwa shilingi milioni tatu kutokana na zabuni hewa aliyopewa na kampuni iliyokuwa ikitumia teksi yake kwa kutoa huduma, alijisikia kuwa katika sayari nyingine. Nani kama yeye?

***ENDELEA***


Juzi jioni aliingia hapo Mood Bar akiwa na shilingi laki tano, akaondoka na elfu hamsini! Hakujali. Jana kaondoka na laki moja japo aliingia na laki tatu. Alimnunulia yeyote kinywaji au kitafunwa. Jioni hii, alikuja na vijana wawili, marafiki zake, ambao walikuwa ni ndugu wa mwenye nyumba wake. Kibutu alielewana sana na vijana hao na katika kuonesha kuwa anawajali, ndipo alipowapigia simu ili waje hapo Mood Bar saa kumi na moja jioni.

Hadi kufikia hii saa tatu kasoro usiku, tayari Kibutu alikuwa na bia tano kichwani na wale vijana nao kila mmoja akiwa ameshusha bia kadhaa. Walizungumza hoja hii na ile lakini zaidi, hoja iliyozikamata ndimi zao ni kuhusu soka la Ulaya, wakizungumzia usajili wa timu mbalimbali maarufu za huko.

Pia, kilifika kipindi, vijana hao ambao kiumri walikuwa wadogo kwa Kibutu, walianza kumshawishi ajiingize katika mchezo wa bahati nasibu, maarufu ‘kubeti’ kufuatia matokeo mabalimbali ya mechi mbalimbali za soka duniani.
Wakati wakiendelea kuongea, wakicheka na kutaniana, sauti zao zikiwa za juu, mara macho ya Kibutu yaliganda kwa mwanamke aliyepita jirani, nao akielekea msalani. Macho hayo yakazidi kumganda mwanamke huyo, yakiwa yametua kwenye lile robota la kiuno, ambalo ni kama lilikuwa limeamua kuwadhihaki na kuwanyanyasa kusudi wote waliolikodolea macho.

Ugonjwa wa Kibutu ni wanawake wenye maumbile ya aina hiyo. Bia tano zilizokuwa zimekwishaichangamsha damu yake, zilimvuta awasahau kwa muda hawa vijana. Na kwa jumla pia, pamoja na kwamba kwa kiasi fulani uchangamfu kutokana na bia hizo, ulikuwa umeongezeka, hata hivyo haukumpotezea ule ugonjwa wa kuhitaji warembo.
Akaguna wakati akimshuhudia yule mwanamke akitokomea msalani. Alipoyarejesha macho kwa vijana hawa, akakuta nao wakimtazama huku tabasamu zikichanua nyusoni pao. Mmojawao akamchokonoa, “Kaka, kama kawaida yako, viumbe wa aina hiyo hawakupiti! U’shasahau hata tulichokuwa tukiongea!”

Wote wakacheka.
“Acheni tu wadogo zangu,” hatimaye Kibutu aliipata sauti yake. Akaitwaa glasi ya bia na kuipeleka mdomoni. “Unajua wadogo zangu, wanawake wengine ni kama hawakuzaliwa duniani; walishushwa toka mawinguni maja kwa moja daaaadek! Mana’ake dah!”
Vijana wale wakacheka na kumuunga mkono, kila mmoja akionekana kumsifia huyo mwanamke aliyekuwa kaingia msalani. Muda mfupi baadaye, mwanamke huyo aliporejea, Kibutu na vijana hao walijifanya kama hawana mpango naye. Lakini kisirisiri, walimtupia macho, kila mmoja kimoyomoyo akivutiwa na tembea yake na umbo lake. Kibutu alijiepusha kumwangalia moja kwa moja usoni, ila alipowapita, kama awali aliunyanyua uso na kumtazama tena.
Alipoyarejesha macho kwa vijana hawa ambao sasa walikuwa wamezirejea bia zao, nao wakamtazama sawia.
“Kaka vipi? Umeuona mzigo huo?” mmojawao alimuuliza.

“Siuachii!” Kibutu alijibu kwa sauti ya kujiamini, macho yake mekundu yaliyoshiba kilevi, yakiwatazama kwa zamu.
Vijana wakacheka.
“Siwatanii!” Kibutu alisisitiza huku akiangalia mwanamke yule anakoishia. Alipomwona kaketi, naye akairejea bia yake.
“Mnasikia wadogo zangu,” alisema, “kuna wakati ukiwa katika rika la ujana, inabidi uutumie ujana wake ipasavyo. Mambo mengine, usipoyafanya ujanani, utajikuta unayakurupukia uzeeni. Hapo ndipo utalkapoonekana chizi na limbukeni wa kutupwa! Changamkeni katika miaka hii. Mimi sifanyagi uzembe. Kama mfukoni kuna mkwanja kidogo kwa nini usiyafaudi maisha?

“Kuna maisha gani zaidi hapa duniani kama haya? Ni kunywa na kuwafaidi mademu wazuri. Kesho Mungu akikwambia njoo, unaenda ukiwa umeyatekeleza majukumu yako yote!” Vijana wale walitikisa vichwa wakionesha kuafikiana naye, labda kinafiki kwa kuwa kawanunulia bia. Kuna ule usemi kuwa ‘anayekupa ofa ya bia, akizungumza uongo au hata akizungumza jambo aambalo huwezi kuafikiana naye, usimpinge; kubaliana naye.’ Watoto hawa wa mwenye nyumba wake waliifuata sera hiyo.

Wakaendelea kuzungumzia soka la Ulaya huku akili ya Kibutu ikiwa zaidi kwa yule mwanamke mzuri aliyeikamata akili yake. Kitu kimoja kilichomsumbua kidogo, ni kwamba, kanywa bia lakini hizi bia ni kama zimelijaza zaidi tumbo kuliko kuiweka akili katika ujasiri aliouhitaji. Alihitaji kuwa jasiri na kujiamini hasa atakapokuwa anaongea na yule mwanamke mzuri. Akaamua kuagiza toti tano za pombe kali. Alipoletewa, alizinywa kama maji ya kawaida na kumrejeshea mhudumu glasi. Akakunja uso kidogo na kushusha pumzi ndefu. Sasa akajihisi yu katika hali aliyoihitaji.

Akaagiza bili yake. Alipoletewa, alilipa kisha akawaagizia vijana wale bia mojamoja na kuwaambia, “Wadogo zangu, ngoja nikabeti kwa yule mrembo.”

SCOLASTICA TEMU alishangaa kumwona Kibutu akiisogelea meza hii huku akiwa na glasi ya bia mkononi. Alitembea huku mkono wa kushoto ukiwa ndani ya mfuko wa suruali na alionekana kuwa na maringo fulani, labda kutokana na pesa alizozimiliki jioni hiyo.

Wakati huo yule dada aliyekuwa kaagiza mlo alikuwa kishaondoka. Kibutu alipoifikia meza hiyo, aliitua glasi mezani kisha kwa sauti yenye kijimkwaruzo cha kilevi, akamuuliza Scolastica, “Mama mdogo, naweza kuketi, au kuna wenyewe?”
Sema yake ya majidai, sauti yake ya kilevi, harufu kali ya jasho la pombe kwenye mavazi yake, vilimfanya Scolastica amcheke kimoyomoyo huku akimdharau kwa kiwango cha juu. Akajifanya kama hajamsikia, akaendelea kuyagandisha macho kwenye simu yake, akichati ‘kimagumashi.’
“Shangazi, naruhusiwa kukaa?” swali lingine.
“Kaa tu,” Scolastica alijibu huku akiendelea kuyaepuka macho yake.
Kibutu akaketi. Papohapo mhudumu alikuwa mbele yake. “Lete bia na mwongeze shangazi hapa kinywaji,” alisema kwa sauti yake ileile ya kilevi. Mhudumu alipoondoka ndipo sasa, kwa nguvu ya mchanganyiko wa bia na zile toti kadhaa za pombe kali, ujasiri ukamzidia Kibutu. Hakujali wa kuogopa chochote. Alimhitaji huyu mwanamke mrembo aliyeyateka macho ya wengi humo ukumbini.

Lakini mara akashtuka alipomtazam kwa makini usoni. Haikuwa sura ngeni machoni mwake. Japo alikuwa na bia kadhaa kichwani, akachanganya na toti kadhaa za pombe kali kiasi cha kuunda ulevi wa kiasi fulani ubongoni, hata hivyo hakuwa mwehu. Nani kasema kuwa mtu akilewa anakuwa mwehu? Mwehu ni mwehu na mlevi ni mlevi! Mbona mtu anakunywa bia kumi au mizinga kadhaa ya pombe kali na anafika nyumbani kwake?
Imani hiyo ilikuwa kichwani mwa Kibutu na alijiamini kuwa hata kama kanywa kiasi gani, lakini hawezi kusema kuwa jana alimtukana mtu kutokana na kuzidiwa na kilevi na kwamba hakuwa na kumbukumbu.

Hivyo, mshtuko alioupata hapa, aliamini kuwa haoti wala hajajichanganya. Hapana. Hii siyo sura ngerni. Ni yule Scolastica ambaye mara kadhaa alikuwa akimchukua kwa teksi pale Kinondoni Kwa Manyanya, kwenye kituo cha daladala na kumpeleka kwake, eneo la Biafra.

Kwa hili hakutaka kujidanganya. Ni mwenyewe. Swali likanjia, na yeye anamkumbuka? Hii inama yake ni ya kweli au anazuga? Huyu anazuga, alijisemea moyoni. Hata hivyo akaamua kuwa makini zaidi. Akamtupia salamu huku akimtazama kama asiyemtambua. Scolastica aliunyanyua uso na kumtazama. Macho yakakutana. Akaipokea salamu yake, kistaarabu bila ya mwonekano wowote wenye taswira ya chuki au dharau. Hata bia ya ofa ilipoletwa, Scolastica alikubali ifunguliwe na akainywa. Dakika kumi baadaye walikuwa mbali kimaongezi.

Alianza Kibutu, kwa kuwa alikwishaamua kumvalia njuga iwe, isiwe, akatema cheche. Akashusha risala ya kuomba radhi, Scolastica akimsikiliza kwa utulivu, mara chache akimtazama usoni na kuyarejesha macho kwenye simu yake.
Kilichomtia kiburi zaidi Kibutu ni milioni kadhaa zilizokuwa bado ndani ya begi lake ambalo hakuling’atua begani hata alipokuwa kaketi. Milioni moja aliyoitenga sasa ilikwishapungua na kubaki laki kadhaa. Hata hivyo aliamini kuwa kwa Scolastica atalainika tu, atake, asitake. Atamwomba radhi na atampa laki kadhaa za kumpoza. Atakataa? Hana ubavu huo!
Kiburi cha Kibutu kilikuwa katika ubora wake!

**ITAENDELEA***
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom