Johnny Sins
JF-Expert Member
- Nov 4, 2019
- 2,536
- 3,883
SEHEMU YA 18
TULIPOKOMEA....
Saa nne usiku ilimkuta hapohapo Maseru Bar, na zaidi ya mara nne alizompigia tena Kibutu bado hakuambulia kitu. Ndipo alipoamua kumtumia ujumbe: ‘umenikalisha hapa na kunifanya nipate hasara kwa kunywa bia. Utairejesha gharama niliyotumia. Sasa kesho nitakuja saa kumi na mbili, kama hutaweza tena kuja, basi dili life.
Alijua kuwa atakapoiwasha simu atausoma ujumbe huo.
***ENDELEA***
AKIWA amekerwa na kutokutana na Kibutu kama walivyokubaliana, aliondoka hapo saa tano akiwa pia ameghairi kuondoka na yule mhudumu ambaye saa nzima iliyopita walikuwa wameshakubaliana kuondoka wote.
Saa mbili asubuhi, aliangalia kama ujumbe wake utakuwa umeingia katika simu ya Kibutu. Akashangaa kukutana na maandishi ‘waiting for delivery details.’ Tangu jana mpaka saa hizi hajaiwasha simu! Au kaibiwa? Au imeharibika? Alijiuliza maswali mengi lakini hakuambulia jibu lolote.
Saa nne bado hakukuwa na ujumbe ambao ulionesha kuwa umesomwa. Alipojaribu kupiga akakumbana na jibu kama la jana kuwa namba anayopiga haipatikani. Bado hakujali sana. Alijua kuwa labda simu itakuwa na matatizo ndiyo maana haipatikani. Akaondoka na kwenda kwenye mihangaiko yake.
KWA Scolastica Temu, haukuwa usiku wenye burudani halisi ya usingizi. Hapana. Alizinduka saa tisa na kujikuta aking’aa macho hadi kunakucha. Angeupataje usingizi mzuri ilhali alitambua fika kuwa saa kadhaa zilizopita alikuwa na mtu ambaye alikuwa ni kero kubwa katika historia ya maisha yake tangu azaliwe?
Angeupata vipi usingizi halisi ilhali alitambua fika kuwa saa kadhaa zilizopita alimruhusu mtu huyo ampapase maungoni japo alimchukia zaidi ya alivyomchukia shetani?
Angeupata vipi usingizi uliostahili, wakati alitambua fika kuwa kwa mara ya kwanza amechukua uamuzi mgumu kutokana na tendo la kubakwa zadi ya mwezi mmoja uliopita? Alipozinduka usingizini alikuwa ametoka kuota ndoto isiyoeleweka vizuri. Kwamba, anakimbizwa na mtu asiyemjua na wakati akijitahidi kukimbia mara mbele yake akaona korongo kubwa lenye kiza kinene chini. Kwa kasi aliyokuwa nayo hakuwa na uwezo wa kusimama papohapo. Alijikuta yuko hewani na kuanza kutumbukia ndani ya shimo hilo pana na lenye kina kisichojulikana.
Alipiga kelele kubwa wakati akiwa hewani na ndipo ndoto hiyo ilipokatika ghafla! Alikurupuka na kukuta jasho likimtoka, taa bado ikiwaka. Kalala sebuleni! Akahema kwa nguvu huku akiangaza huku na kule na kushindwa kuelewa kwa nini kaota ndoto ya aina ile. Jambo moja lilimjia wakati huo, kwamba jana aliua! Hilo lilikuwa dhahiri akilini mwake! Nafsini mwake alikuwa na huruma, kiasi hata hakuwa radhi kuchinja kuku au kuua panya! Jana, akitumia tembe moja ya Olanzapin, kwa kudhamiria, aliisaga na kuumimina unga wake ndani ya bia ya Kibutu. Alifanya hivyo akitambua fika kuwa tembe ile itampa usingizi wa zaidi ya saa kumi!
Kama vile haitoshi, kwa kudhamiria tena vilevile, aliifungua chupa ya sumu kali ya PAK na kumvutisha Kibutu wakati akikoroma kwa nguvu ya tembe ya Olanzapin. Aliijua nguvuy ya PAK, kwamba itamchukua mtu sekunde zisizozidi thelathini tu za kuwa hai! Kaua! Hilo alilitambua fika. Damu ya mtu iko kichwani mwake! Kwamba baada ya kuondoka kule chumbani labda Kibutu atafufuka, hilo halikumwingia akilini asilani. Suala ni muda gani itabainika kuwa mtu kafia ndani kwake?
Aliamini kuwa matukio hayo huenda ndiyo yamemsababishia ndoto hiyo ya kutisha. Akaitazama simu yake kwa mara ya pili. Tisa na dakika ishirini. Sasa hakujisikia hata kuingia chumbani kulala. Kwa jumla hakujisikia tena kulala. Lakini ataenda wapi muda huo? Kungekuwa na klabu yoyote ya usiku angekwenda kuumaliza usiku huo. Haikuwapo.
Akautwaa mkoba na kuungalia ndani akivichunguza vitu vyake. Kila kitu kilikuwamo na zaidi ile simu aliyoichukua kwa Kibutu pia ilikuwamo. Alichofanya ni kuitwaa, akaizima kabisa. Kisha aliufunga tena mkoba na kuuweka ndani ya kabati, sehemu ya mafichoni.
Mara akakumbuka kuwa majuzi alipokuwa akirudi kutoka Kawe alikokwenda kunywa bia, alichukua bia mbili pale Pazi Social Club. Hakuzinywa, aliziweka ndani ya jokofu. Mpaka leo zilikuwapo. Sasa akaamua zimsindikize kuumaliza usiku huo kuelekea alfajiri. Saa kumi na mbili asubuhi, nje kukiwa kumepambazuka, mtoto wa kike alikuwa akimalizia chupa ya pili huku akiwa ameamua kuwa siku hiyo asitoke zaidi ya mita mia mbili kutoka humo ndani mwake. Aliamua aipumzishe akili. Lakini ataweza kutawa? Alijiuliza swali hilo na kushindwa kupata jibu sahihi. Akamwomba Mungu ampangie cha kufanya.
Saa moja alikuwa akitoka bafuni kuoga kisha akaenda tena palepale Pazi ambako alikunywa supu kisha akarudi ndani, akajifungia. Nusu saa baadaye alikuwa ametopea usingizini. Huu ukiwa ni usingizi halisi, shibe nzito ya supu ikiwa imeshika hatamu ya umiliki wa fahamu zake.
Kama aliyekuwa amepuliziwa dawa ya nusu kaputi, alijikuta akizinduka saa saba mchana. Akajishangaa. Saa mbili kasoro mpaka saa sita na nusu! Hata hivyo hakujali sana baada ya kuikumbuka ratiba ya jana na kutoupata usingizi wa haki usiku, ulioambatana na ndoto ya kutisha iliyomwondolea utulivu akilini kwa muda. Kwa mara nyingine akaingia bafuni na kujimwagia maji kwa muda mrefu. Alipotoka alijisikia yuko timamu. Akili ilikuwa imetulia. Hakuwa hata na dalili yoyote ya uchovu.
Akawasha runinga na kuangalia vipindi mbalimbali. Hivyo navyo vikamkinai. Akaamua kutoka. Saa yake ilisoma kumi kasoro. Njaa ilimsakama kwa mbali. Alihitaji kula, lakini hakuwa tayari kupika. Hakujisikia tu. Akawaza aende hapo Pazi kula, lakini wazo hilo likaota mbawa. Mazingira ya pale kwake hayakuwa ni rafiki. Kwa jumla hakupenda kujiweka hadharani sana katika kipindi hiki ambacho bosi wake na ofisi yake kwa jumla walijua kuwa yuko Kigoma.
Hivyo, wazo la kwenda tena Kawe likamrudia na akaliona kuwa ni sahihi. Alivaa nguo za kawaida ambazo hata wapangaji wenzake hawajawahi kushuhudia akizivaa, wala wafanyakazi wenzake; dera, kofia la pama kichwani na miwani mieusi machoni. Alionakana kama mwanamke wa taifa lolote la kigeni, na kwa jumla alipendeza. Hakutaka kubeba mkoba wake ule wenye vifaa muhimu. Alijichukulia kijimkoba kidogop tu cha kawaida na kisichokuwa na chochote cha maana zaidi ya pesa.
Alitembea hadi kando ya Barabara ya Kawawa ambako alikodi bajaji iliyompeleka Kawe kwenye baa ileile aliyokuwa akienda siku zote zilizotangulia. Alitoka huko saa mbili usiku, sasa akijisikia kurudi moja kwa moja kulala. Na alifanya hivyo. Aidha, hakutaka kukisumbua kichwa chake kwa lolote kwa usiku huo hasa kuhusu kuipekua simu ya Kibutu. Alipanga kufanya hivyo kesho yake asubuhi.
ALIAMKA mapema, saa moja kasoro. Usiku uliopita ulikuwa tulivu kwake. Hakupata ndoto yoyote iliyomtisha. Kwa jumla hakuota ndoto yoyote. Asubuhi hii akijisikia kuwa timamu zaidi kimwili alishughulikia usafi wa ndani, kisha akaoga na kama jana, alitoka na kwenda baa ambako aliagiza supu. Saa mbili alikuwa yuko vizuri tumboni. Sasa akaamua kuifanya ile kazi ya kuipekua simu ya marehemu Kibutu.
Akiwa amejitanda kanga pekee mwilini, alihakikisha kuwa kafunga milango na geti kwa funguo. Akaitwaa simu ya aliyekuwa Kibutu. Akaiwasha. Sekunde chache baadaye ujumbe tofauti ukaingia. Akatulia akisubiri ujumbe wote uingie. Kisha akajaribu kufungua. Akashukuru Mungu kukuta kumbe Kibutu hakuwa ameweka neno la siri la kuingilia.
Akauona ujumbe wa kwanza ukiwa ni wa kutoka kwa mtu aliysajiliwa kwa jina la Martha, akimuuliza kama atampatia pesa alizomwomba au hampi. Ujumbe wa pili ulitoka kwa mwanamke mwingine aliyekuwa akiomba wakutane leo. Ujumbe wa tatu na wa nne ulikuwa ukitoka kwenye kampuni za bahati nasibu, zikimshawishi kucheza kamari.
Ndipo alipouona ujumbe wa mtu aliyejazwa humo kwa jina la Kisengo. Akashtuka na kutulia. Akausoma ujumbe huo kwa makini. Tabasamu la mbali likamtoka, tabasamu lisilokuwa hata na chembe ya furaha.
***ITAENDELEA
Sent using Jamii Forums mobile app