Riwaya: Scolastica Temu

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
SCOLASTICA TEMU

MTUNZI:
INNOCENT NDASANYE
NAMBA: 0755 040 520

“KWA nini iwe hivi?” msichana huyu mrembo, Scolastica Temu alijikuta akijiuliza swali hilo mara nyingi huku akiwa chumbani peke yake akilia kwa uchungu.

Ulikuwa ni usiku, saa tatu kasoro dakika chache. Akatwaa kioo kidogo na kujitazama usoni. Akayaona macho yalivyo mekundu. Nywele zake hazikuwa katika mvurugiko wowote. Lakini akahisi maumivu ya mbali kwenye viwiko vya mikono. Alipojitazama vizuri mikononi akaziona vumbi. Hakushangaa, alijua ni matokeo ya kile kilichomkuta. Machozi yakaendelea kumtiririka mashavuni. Machozi ya uchungu.

Huu ulikuwa ni mwezi wa saba tangu alipoajiriwa katika kampuni ya uwakili ya Sam Advocates jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza miaka mitatu huko Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda alikosomea taaluma ya Sheria.

Alikuwa yeye kama yeye. Hakuwa na mdogo au mkubwa aliyemwita ndugu wa tumbo moja. Hata mama yake hakumjua. Hata baba yake hakumjua. Mimba yake ilipatikana wakati mwanamke mmoja wa mrembo wa Kimarangu aliyekuwa akifanya biashara ya mamalishe huko Kasulu mkoani Kigoma alipobakwa na dereva wa gari kubwa la mizigo lililokuwa likielekea Burundi. Mwanamume huyo aliitwa Temu. Jina la pili halikujulikana.

Tukio hilo la kubakwa lilitokea wakati mwanamke huyo na dereva walipokuwa wakijadiliana kuhusu biashara fulani ambayo wangeshirikiana. Kwa kuwa walifahamiana tangu wakiwa huko Marangu na ikatokea wakakutana hapo Kasulu, mwanamke huyo alijisikia kumwamini na kumchukulia huyo mwanamume kama ndugu yake.

Siku ya tukio, wakiwa ndani ya gari wakizungumzia hiyo biashara, ghafla, mwanamunme alimtolea kisu na kumtishia kumchoma kama asingemruhusu kufanya naye mapenzi. Janneth aligwaya na alipomtazama usoni akaziona dalili zote za kuua. Akamwachia mwili wake. Baada ya tukio hilo Janneth alitimuliwa humo garini huku akitishiwa kuuawa kama angeripoiti tukio hilo polisi.

Temu hakulala hapo Kasulu siku hiyo na hawakuonana tena!
Kubakwa huko kuliiunda mimba tumbon I mwa mwanamke huyo. Akaishi na mimba yake bila furaha moyoni, amani ubongoni. Miezi tisa ilipotimu, akajifungua salama motto mzuri wa kike. Akampatia jina la Scolastica. Alikuwa na hasira na Temu lakini ni ubini gani atampa huyu motto pale kwenye usajhili wa vizazi na vifo. Akamtaja baba yake yuleyule, baba mbakaji; Temu. Akawa ni Scolastica Temu.

Alimlea motto huyo katika mazingira magumu kwani biashara yake ya umama lishe ilitetereka na kujikuta akiwa katika hali ngumu. Hstimaye siku isiyo na jina, janneth a,liamka asubuhi na kwanagalia mwanaye huyo aliyekuwa na umri wa mwaka mmoja na miezi kumi, akampakata na kumbusu. Mtoto akafurahi.

Akamketisha chini na kupatia chai na mayai ya kukaanga. Kisha akatwaa kalamu na karatasi na kuandika maandishi machache na kuiweka ndani ya bahasha. Juu ya bahassha hiyo akaandika KWA YEYOTE ASOME UJUMBE HUU. Akaiweka mezani ili iwer rahisi kuonwa. Mtoto alipotosheka, janneth akambeba na kumpeka kwa jirani ambako alimwomba mama huyo jirani akae na Scola wakati anakwenda kuteka maji bombani.

Hakwenda bombani, alirudi nyumbani ambako alikoroga dawa ya mimea kwenye kikombe, kisha akanywa. Akajilaza sofani Dakika chache baadaye alianza kutapika damu. Hakupumua zaidi ya dakika tano!

Maiti ya janneth iligundulika jioni baada ya jirani kutomwona akirudi. Na ndipo pia baada ya taarifa kufika Pilisi, na sakari kufika hapo, ikagundulika bahasha hiyo. Ndipo uliposomwa ujumbe uliokuwama.

MAISHA YAMEKUWA MAGUMU. NAMPENDA MWANANGU LAKINI ACHA NITANGULIE. TAFADHAQLIA WASAMARIA WEMA NITUNZIENI MWANAGU, MUNGU ATAWABARIKI.
Mtoto SCOLASTICA AKALELEWA NA jirani huyo kwa moyo mkunjufu. Akiwa ni mmumini mzuri wa kanisa, mzee Ndayikize alimlea motto huyo kama watoto wake wa kuzaa.

Umri wa kuanza shule ulipotimu, Scolastica alipelekwa kuanza masomo. Ada za masomo yake kuanzia elimu ya msingi hadi cghuo kikuu alilipiwa kwa msaada wa baadhi ya waumini wa kanisa wakishirikiana na mlezi wake, mzee Ndayikize.

Ni wakati yupo chuo kikuu ndiponaliposimuliwa kwa kina kuhusu historia yta maisha yake na kuoneshwa kaburi la mama yake. Sasa akatambua kuwa ana mlezi, hana baba wala mama. Watu walimfahamu mama yake, lakini hawakumjua baba yake na wala Janneth hakuwa kuwaambia lolote kuhusu mzazi wa kiume wa mwanaye.

Aliwapenda sana walezi wake hao na hata alipokuwa ameanza ajira katika kampuni hiyo ya uwakili alikuwa akiwatumia pesa mara kwa mara mara na mara mbili alikuwa ameshakwenda Kasulu kuwasalimia.

Ajira yake ilikuwa ikimpatia mshahara mzuri uliomweka katika maisha bora. Tayari alikuwa ameshanunua kiwanja eneo la Kigamboni na alikwishaanza ujenzi wa nyumba ya vyumba vinne.

Aliishi Kinondoni, jirani na Uwanja wa Biafra, akiwa amepanga vyumba viwili huku akijitegemea bafu, choo na jiko. Ilikuwa ni nyumba yenye mvuto nje na ndani…..


TUENDELEE?
 
KITABU: SCOLASTICA TEMU (2)

TULIKOMEA HAPA...


Ajira yake ilikuwa ikimpatia mshahara mzuri uliomweka katika maisha bora. Tayari alikuwa ameshanunua kiwanja eneo la Kigamboni na alikwishaanza ujenzi wa nyumba ya vyumba vinne.
Aliishi Kinondoni, jirani na Uwanja wa Biafra, akiwa amepanga vyumba viwili huku akijitegemea bafu, choo na jiko. Ilikuwa ni nyumba yenye mvuto nje na ndani…..

TUENDELEE

Kila alipotoka ofisini eneo la katikati ya jiji, Mtaa wa Jamhuri, alikuwa akipanda daladala na kushukia Kinondoni ‘A.’ Kutoka hapo alitembea taratibu na kuvukia Barabara ya Rashid Kawawa ambako alipanda tena daladala hadi Biafra.
Mara kadhaa alikuwa akiwaza kununua gari dogo la kutembelea lakini wazo hilo mara nyingi tena lilijitoa kichwani. Hakuona umuhimu wa kununua gari kwa kuwa hakuwa na tatizo lolote linalomlazimu awe na gari. Na aliona ununuzi wa gari ataufanya mara atakapoingia ndani ya nyumba yake.

*****
MACHO ya wengi yalikuwa yakimganda mwanamke huyu mrembo, Scolastica Temu kila alipoteremka kituoni Kinondoni ‘A’ jioni na hata alipopanda tena daladala asubuhi akielea ofisini. Si wanawake, si wanaume, wote walivutiwa na ubora wa mavazi yake, umbo lake na sura yake nzuri.

Kati yao ni Kibutu, aliyekuwa akiendesha teksi na kituo chake kikuu kilikuwa hapo Kinondoni ‘A.’ Yeye hakukubali kuishia kumwangalia tu, hapana. Aliamua kumvalia njuga, amwambie kilicho moyoni mwake. Ukweli si kwamba alimpenda, bali alimtamani sana. Katika maisha yake, Kibutu hakuwa na kumbukumbu ni wanawake wangapi aliwahi kuwapenda kutoka moyoni. Huenda hawazidi wawili. Zaidi alivutiwa na maumbile ya wanawake na sura zao. Hivyo tamaa ya mwili ilimtawala .

Ikatokea siku akamwona Scolastica ameteremka kituoni hapo. Kibutu akamvutia pumzi. Alipomwona anavuka barabara kama kaawaida yake akielekea kwenye kituo cha Kwa Manyanya, naye akatia moto teksi yake na kuondoka taratibu. Alitaka ahakikishe mara tu Scolastica atakapokuwa anaingia kituoni naye afike. Siku hiyo anga ilikuwa inaashiria mvua kubwa muda mfupi ujao, hali iliyompa matumaini Kibutu ya kufanikisha lolote alilolidhamiria. Wakati Scolastica alipoingia tu pale kituoni, Kibutu naye akaingia na kuegesha teksi kando yake.

“Twende nikusogeze, shangazi,” Kiburtu alimwambia.
Scolastica alishangaa na kukunja uso kidogo. Akamtazama Kibutu kujaribu kufikiria kama anamfahamu. Hakuwa na kumbukumbu yoyote kuhusu mwanamume huyo. Hatimaye akasema, “Asante. Siendi mbali ni hapo tu Biafra.”
“Najua, shangazi. Mimi nakwenda zaidi ya hapo. Twende tu nikakuache hapo.”

Scolastica aliitazama anga na kuingiwa na hofu kutokana na wingu lile zito. Isitoshe kwa mbali akaanza kuyasikia matone ya mvua yakidondoka. Akajiuliza ya nini kuukata msaada huo wa lifti? Akaingia garini, Kibutu akang’oa gari.
Mvua ikaanza kumwagika kabla hata hawajafika Biafra. Kibutu akauzidisha usamaria wake kwa kumfikisha Scolastica mlangoni pa nyumb aaliyoishi, baada ya kupewa maelekezo.

Ni siku hiyo Kibutu alipoamua kutomchelewesha, akaondoka hapo akiwa ameshatamka kile alichoamini kuwa mwanamke huyo atajua nia na madhumuni yake. Scolastica hakumpa jibu lolote la maana, zaidi alikuwa akiachia tabasamu la mbali.

Hawakuishia hapo, Kibutu aliendelea kuwa king’ang’anizi, akimvizia kila jioni. Mara nne zaidi alizokuwa akikutana naye jioni na kumsindikiza alijikuta akigonga mwamba katika hoja yake. Na zaidi, hakuna kilichomuumiza akili kama siku Scola alipomwambia, “Sikiliza we’ mkaka, usiwe na matumaini kabisa kuhusu hilo! Nakwambia hivyo. Mbona hunielewi? Mara zote nimekujibu kistaarabu najua wewe ni mtu na akili zako, siyo mtoto mdogo, lakini naona bado tu unang’ang’ania!
“Samahani sana, leo naomba uelewe hivyo. Nina mambo yangu kichwani yananisumbua kuusu maisha. Masuala ya mapenzi nimeweka pembeni kwanza. Elewa hivyo tafadhali.”

Wakati Scolastica akitoa maelezo hayo na msimamo huo, alikuwa akifungua mlango wa gari na kuteremka nyumbani kwake, baada ya kuletwa kama mara kadhaa zilizopita.

Kibutu alihisi kama kasikia ngurumo kali ya radi. Hakumbuki ni lini mara ya mwisho aliwahi kupokea kauli ya kukata maini kutoka kwa mwanamke yeyote kama hii. Alipoondoka siku hiyo, hakurudia tena kumvizia jioni na kumpa lifti yake. Lakini huo haukuwa mwisho. Hakuwa tayari kushindwa. Akaamua kuzungumza na rafikizake wawili; Machemba na Kisengo.
Dhamira yake ilikuwa ni kumwonesha tu Scolastica kuwa yeye ni mtoto wa mjini. Kwa siku tano wakawa wakimwinda bila yeyey kujua. Na sasa Kibutu hakulitumia tena gari lake. Walikubaliana watumie gari lingine ambalo lilikuwa katika gereji bubu eneo la Kinondoni’B’. Gereji hiyo ndiko Machemba alikofanya kazi. Mwenye gari hilo alikuwa safarini Mtwara ambako alikuwa na miradi yake na hakutarajiwa kurejea karibuni.

Walichofanya wanaume hawa ni kubadili vibati vya namba za usajili na kulitumia gari hilo kwa mambo yao. Wakati lile gari la Kibutu lilikuwa jeupe, hili walilodhamiria kulitumia kwa mpango huu lilikuwa jeusi. Siku waliyopanga walifika kituo cha daladala cha Kwa Manyanya mapema kidogo, saa kumi na moja kasoro dakika chache. Kwa mujibu wa Kibutu, mara nyingi Scolastica hufika eneo hilo saa kumi na moja na kuendelea lakini hakutaka kubahatisha. Bora kuwahi kuliko kuchelewa.

Wakiwa hapo hawakutaka kuleta taswira yoyote itakayowafanya watu wengine wawatile shaka, hivyo, wakajichanganya na watu wengine waliokuwa eneo hilo baadhi wakinywa kahawa, wengine wakicheza bao na kuna waliokuwa kituoni wakisubiri tu usafiri. Hata hivyo, Kibutu alikuwa makini zadi kwa kuwa ndiye aliyemfahamu vizuri mlengwa aliyesubiriwa. Hatimaye baada ya muda, kwa usahihi macho ya Kibutu yalimwona Scolastica akivuka barabara na kuja hapo kituoni. Wanaume hao wakapeana ishara na kuwa tayari kwa utekelezaji.

“Ingia garini na ukae mkao wa kung’oka,” Kibutu alimwambia Machemba huku akifungua mlango taratibu. Kisengo aliusogelea mlango wa kushoto, nyuma na kuufungua. Akauacha wazi kidogo.
Akiwa hajui chochote kinachoendelea, Scolastica alipita jirani na gari hilo huku akiwa ameyagandisha macho kwenye simu yake kubwa, akichati na rafiki zake wa mitandaoni. Alitembea taratibu, akiwa hana haraka na zaidi alionekana kutekwa na kuchati mtandaoni.

Kisengo hakumpa muda zaidi na aliona kuwa ni mazingira sahihi ya kukamilisha kazi yao. Papohapo alimvuta na kumsukumizia garini kwa kasi yta ajabu huku akimfuata na kumwagukia kisha akamwonya, “Tulia! Ukijitia kujua nakuzimisha!”
Tayari Kibutu alikwishaingia kiti cha mbele na Machemba akaling’oa gari kwa makeke likielekea upande wa Kinondoni ‘B.’ Hata hivyo, hawakwenda mbali, mbele kidogo likakata kushoto na kutokomea.
Lilikuwa ni tukio ambalo baadhi ya walioshuhudia walidhani ni uigizaji wa sinema. Hata hivyo, hisia hizo hazikudumu vichwani mwao, mara wakajenga imani kuwa ni utekaji nyara.

Ni kwa sababu gani kumetokea tukio hilo? Ni kwa nini mwanamke huyo mzuri atekwe? Baadhi ya waliokuwa wakifanya biashara hapo walikiri kuwa hakuwa mgeni machoni mwao. Mara kwa mara walikuwa wakimwona akipanda daladala hapo na wakati mwingine alikuwa akichukuliwa na gari moja dogo jeupe.

Sasa ni kipi hiki kilichotokea? Kila mmoja alijiuliza hivi n a vile na ikazuka hoja ya kwamba huenda ni utekaji nyara, kwa kuwa matukio ya aina hiyo kwa Tanzania ya sasa yamekuwa lyakikariubia kuwa ya kawaida. Hata hivyo gari lilikwishatokmoea. Na kati ya hawa walioshuudia hakukuwa na yeyote aliyekuwa akimfahamu Scolastica Temu. Dakika kadhaa baadaye kila mmoj akaendelea na mambo yake.
*****
LILIKUWA ni tukio la kipekee akilini mwa Scolastica. Alitahayari kwa kiwango kikubwa. Akahema kwa nguvu huku akitetemeka. Alitamani kupiga yowe lakini sauti haikutoka. Simu yake iliyoanguka kitini alifikia kuikalia, lakini hata akili yake wakati huo haikuweza kuwaza lolote kuhusu kuitwaa na kuitumia. Onyo alilopewa na Kisengo lilitosha kumpotezea uwezo wa kufikiri chochote.

Mara Kisengo akamshika shingo na kumlaza mapajani kwake akitaka asione njia wanayopita na wapi wanakokwenda. “Ukitulia, utafaidi zaidi baada ya muda mfupi,” alimwambia kwa dhihaka. Dakika kumi baadaye, gari likasimama. Ilikuwa ni nje ya nyumba moja eneo la Komakoma ambako Kibutu alikuwa akiishi. Nyumba hiyo ilikuwa na vyumba vitatu na sebule. Vyumba viwili wapangaji wake walkuwa wamesafiri hivyo kwa muda mrefu sasa Kibutu alikuwa akiishi peke yake.

Waliamini kuwa kwa eneo hilo lilivyo, haitakuwa rahisi kwa Scolastica kupakumbuka baada ya kuondoka. Yalikuwa ni mazingira yaliyokaa katika hali inayoweza kumsumbua mgeni yeyote. Jua lilikuwa likitokomea hivyo wanaume hawa hawakuwa na muda wa kupoteza, walitaka ratiba zao ziende haraka na waachane na mrembo huyo.
“Teremka na utembee kama kawaida, usionyeshe hali yoyote ya ajabu,” Kisengo alimwambia wakati akimfungulia mlango.

Wakaingia ndani ya nyumba hiyo kama watu wanaoelewana na ni marafiki wakubwa. Scolastica akaongozwa chumbani mwa Kibutu ambako zaidi ya masofa mawili na kitanda, hakukuwa na cha ziada. Wasiwasi ukazidi kumtawala mtoto wa kike. Akawatazama wanaume hawa wenye miili mikubwa na macho makali. Wawili kati yao hakuwafahamu kabisa na hii ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuwatia machoni. Lakinii mmoja, huyu hakuwa mgeni kabisa. Alikumbuka kuwa ndiye aliyekuwa akimtongoza mara kadhaa huku akimpa lifti siku chache zilizopita. Na hata aliwahi kujitambulisha kuwa anaitwa Kibutu.

Alibaki akiwatazama kwa zamu na kuziona dalili zote za ukatili hasa katika macho ya Kibutu. Akajiuliza ni kitendo cha kumkatalia uhusiano wa mapenzi ndicho kilichosababisha haya yote? Hisia hizo zilimjia akilini lakini bado hakuwa na uthibitisho. Badala yake, kwa unyonge, akawauliza, “Jamani nimewafanya nini?”

“Usijali mrembo,” Kibutu alimjibu. “Ni mambo ya kawaida tu. Si unanikumbuka my dear?” Kisha akawageukia wenzake na kuwaambia, “dakika kumi tu tafadhali. Nahitaji faragha kidogo na mtoto mzuri.” Machemba na Kisengo walielewa. Wakatoka. Ndipo Scolastica alipopata picha kamili pale Kibutu alipomwambia, “Vua mwenyewe, tusiuweke usiku bure! Sitakuchelewesha. Hupendi kuwahi nyumbani?”

Ulikuwa ni wakati mgumu zaidi kwa Scolastica. Akaiwaza historia ya maisha yake tangu mama yake alipofariki dunia. Akauona mwisho wa maisha yake ukimjia kwa kasi kabla hata hajaifaidi elimu yake. Akajiuliza, amemkosea nini Mungu? Alibaki kaduwaa. Akamtazama Kibutu huku akilengwa machozi. Punde akamwona Kibutu akichojoa suruali yake. Shati likafuatia.

“Scola,” alimwita kwa sauti ya chini huku akimfata pale sofani na kumshika matiti. “Wewe ni mwanamke mzuri sana. Na unaonyesha ni mtaalamu sana na mjanja zaidi, unayejua kumfurahisha mwanaume yeyote mwenye njaa.”
Scolastica alijitahidi kuyaziba matiti kwa mikono lakini Kibutu aliikwanyua na kuendelea kumchezea huku akimtazama kwa dhihaka. Kisha akamuuliza, “Nikusaidie kupunguza nguo mwilini?”

Lilikuwa ni swali ambalo lilizidi kumpa taswira halisi Scolastica kuwa ni kipi kitafuata. Badala ya kujibu akaamua kuchukua uamauzi mgumu alioamini kuwa ungeweza kumsaidia. Kama aliyepagawa, alipiga yowe kali: “Jamani nakufaaaa!”

Likawa ni kosa kubwa! Kofi kali kutoka katika kono la kulia la Kibutu lilitua katika shavu lake la kushoto. Sekunde ya pili kofi la pili likatua shavu la kulia. Akaliegemea sofa huku akiona kizunguzunngu. Kiza kikamtanda machoni! Akakosa uwezo nwa kufumbua tena kinywa! Ndipo kilipofuata kile alichohisi kuwa kilidhamiriwa na watu hawa!

TUTAENDELEEEEAAAA
 
KITABU: SCOLASTICA TEMU (3)

TULIKOMEA HAPA...

Likawa ni kosa kubwa! Kofi kali kutoka katika kono la kulia la Kibutu lilitua katika shavu lake la kushoto. Sekunde ya pili kofi la pili likatua shavu la kulia. Akaliegemea sofa huku akiona kizunguzunngu. Kiza kikamtanda machoni! Akakosa uwezo nwa kufumbua tena kinywa! Ndipo kilipofuata kile alichohisi kuwa kilidhamiriwa na watu hawa!

ENDELEA...

Kibutu alimnyanyua kwa nguvu na kumwegemeza kifuani kisha akaanza kumchojoa nguo. Muda mfupi baadaye Scolastica alilazimika kustahimili wakati Kibutu alipokuwa kifuani pake akifanya kile alichodhamiria, akitumia nguvu kwa ukomoaji!

Dakika tano baadaye mwanamume alikuwa akivaa nguo zake. Wakatazamana. Macho ya Scolastica yakiwa hayana hata chembe ya aibu wala woga! Alimtazama Kibutu kwa namna nyingine kabisa, akionekana kutojali chochote! Mara machozi yakamtoka tena, na akayaacha yabubujike mashavuni huku akiendelea kumtazama bila hata ya kujishughulisha kuvaa suruali yake.

“Vipi?” Kibutu alimuuliza huku akimtazama kwa macho yaliyojaa dharau. “Vipi mtoto mzuri, bado unanihitaji?”

Lilikuwa ni swali lingine ambalo Scolastica alilichukulia kama tusi. Hakujibu. Aliendelea kumtazama bila ya kutamka chochote. Mara mlango ukafunguliwa tena. Kisengo akaingia. Kibutu akamnyooshea dole gumba huku akitabasamu. Kisha akamgeukia Scolastica na kumwambia, “Nipo nje mrembo wetu. Napunga hewa kidogo. Msikilize huyu msh’kaji.”

Kisengo hakuhitaji kupoteza muda. Ni kama alikuwa na miaka kumi hajampata mwanamke, lakini zaidi haya mapaja makubwa ya Scolastica yalimchanganya maradufu.

Scolastica akaipokea adha yab pili!

Dakika kumi baadaye Kisengo alikuwa akiikunja kondomu aliyoitumia, akaihifadhi kwenye kipande cha gazeti kisha akatoka huku akimpungia mkono. Akakutana na macho makali yasiyopepesa, macho yaliyofurika machozi!

Wakati Scolastica akimshuhudia Kisengo akiondoka, mara akamwona Machemba akiingia. Yeye, kama alivyokuwa Kibutu, hakujali kuchukua pakiti ya kondomu iliyokuwa ndani ya boksi, kando ya sofa la pili. Alimvamia Scolastica kwa namna yake, akatumia nguvu kubwa kama Kibutu huku akihema kama nguruwe pori.

Naye hakutumia zaidi ya dakika tano, akajing’atua huku akimbusu Scolastica shavuni. Akashangaa kumwona akiachia tabasamu la mbali huku akimtazama usoni bila aibu. ‘Amenikubali?’ alijiuliza huku akivaa nguo zake.

“Kwa leo inatosha, mtoto mzuri,” hatimaye Machemba alimwambia huku akimpigapiga mgongoni. Kisha akaongeza, “Vaa twen’zetu. Giza limeingia. Siku nyingine utafaidi zaidi.”

Yalikuwa ni maneno mengine ambayo yalipenya masikioni mwa Scolastica mithili ya radi. Yalimwingia kwa usahihi na kumtikisa vilivyo akilini! Akajisikia kumchukia kila mwanamume, hata baba yake mzazi ambaye hakubahatika kuiona sura yake hadi anafikia umri huo.

“Vaa!” sasa Machemba alibadilika sura. “Usitarajie kubembelezwa zaidi. Hatuna muda mchafu wa kuendelea kuwa na mwanamke mchafu ka’ wewe! Vaa usepe fasta!”

Scolastica aligwaya. Akayaona macho ya Machemba yakiwa yamejitenga na huruma, masihara wala upendo kwa umabali wa kilometa mia moja! Akakiona kifonkiwa umabaliu mfupi mbele yake. Akalazimikla kutii. Akajinyanyua pale sofani huku akiwa haamini kama yaliyotokea ni ndoto au matukio halisi.

Akapiga moyo konde na kuamua kuyanusuru maisha yake japo adha aliyoipata ilikuwa imekwishaivuruga akili yake kwa kiasi kikubwa. Akasimama na kuitwaa suruali yake kisha akaivaa taratibu, macho ya Machemba yakimshuhudia. Alipojiona kuwa yu tayari, akatwaa mkoba wake. Machemba akafungua mlango na kumpisha.

Kule nje, Scolastica aliwakuta Kibutu na Kisemgo wakiwa wameegemea gari. Kibutu alikuwa akivuta sigara huku Kisengo akiwa na kichupa kidogo cha pombe kali, akinywa taratibu.

Pamoja na eneo hilo kutawaliwa na kijigiza, hata hivyo Scolastica hakushindwa kuziona nyuso za wanaume hao zikitabasamu. Akasimama na kuwatazama kwa zamu, macho yake yakiwa hayaoneshi kuwa na wasiwasi.

Kisha Kibutu akamwambia, “Mrembo wetu, pita njia hiyo. Usiliogope giza. Hakuna atakayekudhuru. Hiyo ndiyo njia ya mkato. Huko mbele ndipo utaikuta stendi ya daladala na hata bodaboda au bajaji.”

Alimwonesha njia ambayo aliamini kuwa muda huo wa usiku, isingekuwa tarahisi kuweza kuikumbuka tena kama ataamua kujua mchana kwa lengo lolote lile.

Bado Scolastica alishindwa kuamini chochote kilichofanyika dakika kadhaa zilizopita. Akaendelea kuduwaa akiwatazama. Ni Machemba aliyemzindua. Akampigapiga mgongoni polepole huku akimwambia, “Naomba nikwambie kistaarabu kabisa kuwa, ukiendelea kuzubaa hapa na sisi hatutaendelea kukuchekea. Hujui kuwa kuendelea kukutazama tu hivi ni huruma sana tumekufanyia?”

Scolastica alizinduka. Na kwa kuwa sasa alikwishakuwa katika hali nyingine, woga ukiwa umemtoka, akiwa tayari kwa lolote hata kama ni kufa, akafumbua kinywa na kutamka, “Simu yangu, please.”

“Simu?” Machemba alimuuliza huku akimtazama kwa mshangao.

Kumbukumbu ya kuikalia simu garini wakati alipotekwa kule kituoni ilimrejea akilini. Akawatazama tena kwa zamu bila kutishwa na macho yao yaliyomtazama kwa namna ileile ya dhihaka. “Ilikuwa kwenye siti, humo garini,” alisema.

Mara Kibutu akafungua mlango wa nyuma wa gari hilo na kupapasa kidogo kwenye kiti. Aliponyanyuka, alikuwa na simu mkononi. Akamnyooshea Scoalastica kumpa lakini Machem,ba akamdaka na kumpokonya. Akaitazama kidogo kisha, akamgeukia Scolastica na kumwambia, “Chukua simu yako, lakini utoe laini zote na uzivunje hapahapa mbele yetu, kisha nenda zako na simu yako.”

Ilikuwa ni amri ambayo Scolastica hakuitarajia. Akajiuliza, kama wameshambaka, ni kwa nini wanaendelea kumnyanyasa? Haikumwingia akilini kuwa sababu ya kuamrishwa azitoe hizo laini ni kuondoa uwezekano wa yeye kuwasiliana na yeyote muda mfupi baada ya kuondoka hapo na hivyo kuleta uwezekano wa wabaya wake kukamatwa kwa urahisi.

“Toa!” Machemba alifoka alipomwona anasuasua.

Haraka Scolastica akazitoa laini zote mbili na kumkabidhi.

“Mkuu uko vizuri,” Kibutu alinwambia Machemba. “Uliwaza ni kuhusu hilo?”

“Mjini hapa msh’kaji wangu,” Machemba alijibu huku akizivunja zile laini za simu, Scolastica akishuhudia. “Kumwachia huyu malaya aende kama alivyokuja, tutajuta.”

“Ni kweli,” Kisengo aliafiki huku akipeleka chupa ya pombe kinywani na kunywa funda dogo. “Hapa alipo akili yake ni kwenda kuripoti Polisi.”

Wakacheka kwa pamoja.

Maneno hayo na vicheko vyao zilikuwa ni dhihaka nyingine zilizomuumiza Scoalastica kwa kiwango kisichokadirika. Lakini afanye nini wakati huo? Alilazimika kuvumilia, wakati akivishuhudia vipande vya laini zake za simu vikitupwa chini. Angefanya nini mbele ya wanaume hawa watatu ambao tayari wameshambaka na yuko bado katika himaya yao muda huo? Angefanya nini wakati yeye ni msichana mdogo tu ambaye mbele ya wanaume hawa wenye mioyo isiyokuwa hata na chembe ya ubinadamu ni kama vile sisimizi mbele ya tembo?

Machemba akamgusa tena begani na kumwambia kwa upole bandia, “Kwaheri mpenzi.”

Scolastica aliondoka taratibu lakini akiwa kama anayeendeshwa kwa mitambo maalum. Akaifuata ile njia aliyoelekzwa. Akatembea taratibu bila ya kugeuka, mkoba begani, simu mkononi.

Hakutofautiana na roboti!

***ITAENDELEA***
 
Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony@Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey@KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie@Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi @Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future@nancy1983 Bulah binsaad @Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter@apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N.@Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki@deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii@mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave@ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya Lee empire wigo MJINI CHAI Asprin@mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo @Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO @multiphill90 GEORGE Dalali@mwanamalundi90 MwaFreeca @Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto@Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack @GoodluckMchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa@mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee@dawa yenu The Certified DON SINYORI mij @addenbwii ONTARIO Kobe The Vein mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya SITAKI ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo@mgumu2 troublemaker Linamo @shedede kamtu33 SteveMollel Ngushi DONALD stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove@SingleFather Santi DEOD 360 Ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU@VILLAIN mwayena donbeny @Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu@painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje@Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema@mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche@kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east@SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush mossad 03 white wizard xtaper Mzigua90@Ollachuga Oc Gidbang Mateja M.G Yango jipu abaa4all DIBAJI Agenda1 Grahnman The MaskmaN Slim5 Xubzero@agprogrammer JoJiPoJi @Architectus blance86 Mamtolo monde arabe Ngao Ya Imani stardust JK naiman64 Dharra seledunga@ABB @SHAMMA Richard Waziri wa Kaskazini @Mwinjuma1 Kanungila Karim baracuda Mwamba028 besaro Pyepyepye Bilionea Asigwa ibn Kiti Chema Tugas Royal Warrior mederii mmangO manzi james LIKUD adrenaline Royal Son Mhadzabe salaniatz@Natasha Ismail jiwe jeusi chibalangunamchezo
John Mloy conjuget Van Pauser great G Mtoto wa nzi Zeus1 hindustan Sci-Fi MAN OF PEACE kashata emnly danny baraka bb MTOTELA kbosho TEMLO DA VINCA Shunie Madame B Madame S
 
Mtoto Scola amekutana na hali inayoonekana kuwa ya kawaida Tanzania, utekaji
 
SCOLASTICA TEMU (4)

TULIKOMEA HAPA...


Maneno hayo na vicheko vyao zilikuwa ni dhihaka nyingine zilizomuumiza Scoalastica kwa kiwango kisichokadirika. Lakini afanye nini wakati huo? Alilazimika kuvumilia, wakati akivishuhudia vipande vya laini zake za simu vikitupwa chini. Angefanya nini mbele ya wanaume hawa watatu ambao tayari wameshambaka na yuko bado katika himaya yao muda huo?

Angefanya nini wakati yeye ni msichana mdogo tu ambaye mbele ya wanaume hawa wenye mioyo isiyokuwa hata na chembe ya ubinadamu ni kama vile sisimizi mbele ya tembo?
Machemba akamgusa tena begani na kumwambia kwa upole bandia, “Kwaheri mpenzi.”
Scolastica aliondoka taratibu lakini akiwa kama anayeendeshwa kwa mitambo maalum. Akaifuata ile njia aliyoelekzwa. Akatembea taratibu bila ya kugeuka, mkoba begani, simu mkononi.
Hakutofautiana na roboti!

***** ENDELEA***

KUBAKWA ni tukio ambalo Scolastica alilichukulia kuwa ni nuksi zaidi nuksi ambazo humpata mwanadamu. Na nuksi hiyo aliona kuwa imemkumba na y eye! Alichanganyikiwa! Akatembea katika barabara hiyo finyu huku akiwa kama mwendawazimu, na hata honi za pikipiki na magari wakati mwingine ni kama hakuzisikia. Baadhi ya madereva wa pikipiki ambao walilazimika kumkwepa, walimrushia maneno makali yasiyostahili kutolewa kwenye vinywa vya wanadamu wastaarabu na wenye akili timamu.

Hakujali, alendelea kutembea kama aliyeziba masikio kwa pamba nzito. Hatimaye akajikuta akiibukia kwenye kituo cha daladala cha Komakoma. Hata hivyo, bado hakujiona kuwa yu mwanadamu kamili. Kumbukumbu ya yaliyomkuta muda mfupi uliopita, ikazidi kumfanya ajisikie yu nusu mfu.

“Kwa nini niendelee kuishi? Nina faida gani ya kuendelea kuishi? Nimemkosea nini Mungu?” alinong’ona kwa uchungu, machozi yakianza kumtoka tena. Akiwa ameduwaa hapo kituoni, swali likamjia, je, itakuwa vyema kama atatumia usafiri wa daladala ilhali katoka katika mkasa uliomwathiri kimwili na kiakili? Hiyo daladala atakayopanda itakwenda kumwacha Kinondoni ‘A.’ Na hapo angepaswa kuirudia njia ileile anayoitumia kila atokapo kazini, njia ambayo hata jioni ya siku hii aliitumia na kumzulia tukio hili la kipekee.

Akaufungua mkoba wake na kukuta kuna shilingi elfu arobaini. Akashukuru Mungu kwa kujua sasa atatumia usafiri mwingine zaidi ya daladala. Hatua chache kutoka pale alipokuwa kasimama, kulikuwa na bajaji kadhaa, akaifuata moja na kuondoka eneo hilo.
*****
ALIWEZA kuificha hasira iliyomjaa baada ya kubakwa. Alijitahidi kuonekana yu katika hali ya kawaida pale alipoingia ndani ya bajaji na kuondoka. Na alionekana yu katika hali ya kawaida hata pale alipoteremka nje ya nyumba aliyoishi na kumuaga dereva wa bajaji huku akitabasamu.

Wapangaji wenzake wawili katika nyumba hii walikuwa nje wakipunga hewa. Nao hawakubaini chochote walipomwona. Alikuwa katika mwonekano wa kawaida usoni na alipowasalimia, mmojawao alimdaka kwa swali, “Leo umepitia wapi mwenzetu?” Zinduna alimuuliza. “Si kawaida yako kurudi ‘leiti’ hivi? Au ulipita kwa shemeji yetu?”
“Nd’o maana’ake,” Scolastica alijibu huku akiyaepuka macho ya mwanamke huyo.

“Siku nyingine umletage hapa tumwone, tumjue, mana’ake sie wengine vicheche, isije ikatokea tunamwona huko mtaani, hatujui hili wala lile, tunaanza kujigongagonga,” mpangaji mwingine, Janeth naye alichochea.
Scolastica aliliunda tabasamu dogo akitaka kuonesha zaidi kuwa yuko kawaida kisaikolojia. Kisha: “Msiwaze, atakuja siku moja mumwone.”
Hakuzungumza zaidi. Akazungukia upande wa pili kulikokuwa na geti la kuingia kwake. Mara tu alipokwishaingia ndani na kufunga mlango, alijitupa sofani na kuanza kulia tena. Uchungu wa tukio la kule Komakoma ulimrudia kwa nguvu kubwa.

“Mungu wangu nimekukosea nini mimi? Sina mama, sina baba, sina kaka, sina dada, sina mjomba wala shangazi.Niko kama nilivyo ee Mungu wangu. Ni wewe pekee ninayekutegemea maishani mwangu Mungu wangu.
“Kwa mapenzi yako umeniwezesha kupata elimu. Kwa mapenzi yako nimepata ajira. Natarajia nipate mwanamume mwenye mapenzi ya kweli, atakayekuwa mume wangu, nami niwe mke wake. Nami nifurahie maisha ya ndoa kama wengine Mungu wangu. Nipate mtoto hata watoto wa kuweza kuifariji nafsi yangu maishani.

“Lakini Mungu wangu naona kama ndoto hiyo haitatimia tena. Leo nimebakwa na sijui kama nimesalimika. Mungu wangu, nimekukosea nini?Au wazazi wangu walitenda makosa gani ambayo uzito wake unanielemea mimi?
“Hapana, bado naamini Mungu wangu unanipenda sana. Hata kama hao walionifanyia ukatili huu watakuwa wameniambukiza Ukimwi, bado naamini utakuwa nami Mungu wangu. Na ninaamini utanipa ujasiri wa kujilinda na madhila mengine. Ee Mungu wangu, nakuomba sana uwaonyeshe watu hao wenye mioyo ya kishetani, kwamba walichonifanyia siyo kitu kizuri. Wape fundisho Mungu wangu!

“Mungu wangu sina hakika kama nitaweza kupata ujasiri wa kwenda kazini kama kawaida na kutekeleza majukumu yangu kwa ufanisi. Nahitaji mapumziko Mungu wangu! Lakini pia Mungu wangu naomba unipe uwezo wa kuifanya akili yangu iliwazike na moyo wangu ufarijike.”
Aliomboleza, akisema hili na lile, machozi yakiendelea kububujika na kulilowesha sofa hilo. Macho yalivimba, yakawa mwekundu! Usingizi ulimpitia huku kajilaza hapohapo sofani, kihasarahasara. Haukuwa usingizi bora, usingizi aliouhitaji, usingizi wa kumburudisha akili na kuupumzisha mwili. Huu ulikuwa usingizi uliomjia kiajabu na hata kukatika kiajabu vilevile. Aliposhtuka kwa kukurupuka, aliiangalia saa.

Saa tano! Alishangaa. Mungu wangu! Nina nini leo? Au nd’o kifo kinaniita? Akanyanyuka haraka na kuchojoa nguo. Muda mfupi baadaye alikuwa bafuni akioga. Aliporejea chumbani alikuwa na wazo moja tu; kesho asubuhi afike ofisini na kuomba likizo ya dharura.
“Lazima iwe hivyo!” alinong’ona kwa hasira.
*****
SAA tatu asubuhi, Evarist Dickson, Mkurugenzi wa ED Advocates, kampuni iliyoanza kujipatia umaarufu nchini, alikuwa ofisini kwake na alikuwa makini akifuatilia taarifa iliyotumwa kwake kwa baruapepe kutoka Mahakama Kuu. Taarifa hiyo muhimu ilimchukulia muda kiasi cha kuisahau kahawa iliyokuwa mezani hadi pale sekretari wake alipoingia na kumzindua, “Bosi kahawa inapoa hiyo.”

Ni hapo Evarist alipozinduka na kucheka kidogo. Kisha akasema, “Basi kaimwage tu. Kuna kitu kimeteka akili hapa. Na nilitaka nicheki kwenye intaneti lakini naona nayo iko ‘low’ sana.”
“Tangu jana, bosi,” sekretari alisema. “Sijui kwa nini ‘network’ siku hizi inakuwa hivi. Kero sana.”
Wakati akibeba kikombe cha kahawa na kuondoka, Evarist alitikisa kichwa huku akilikodolea macho umbo hilo la Cathy, binti wa Kinyamwezi, lililokuwa likijitupatupa kwa namna yake.
Hata hivyo, wakati akiushika mlango ili atoke, Evarist alimwita, “Cathy.”
Cathy alishtuka na kugeuka. “Ndiyo, bosi.”
“Scolastica kishaingia ofisini kwake?”
Cathy alikunja uso na kujibu, “Bado, bosi. Hata mimi leo nashangaa. Huwa si kawaida yake. Mara nyingi mbili kasorobo hadi mbili kamili huwa tayari ofisini. Sijui kapatwa na nini leo. Labda nimpigie simu.”
“Hapana,” Evarist alimkataza. “Subiri kwanza. Kwa kuwa si kawaida yake, basi tumfanyie subira. Labda ana dharura. Ikifika saa nne nd’o unaweza kumpigia.”
“Sawa, bosi.”
Saa nne haikutimu, Scolastica akaingia ofisini. Lakini siku hii alikuwa katika mwonekano ambao hata Cathy aliushtukia. Alionekana bayana kutopata usingizi wa kutosha. Hata uso wake huu mzuri ulionesha dhahiri kutokuwa na furaha hata chembe.
Kuna kitu, Cathy alijisemea moyoni. Walipokwishasalimiana, Scola alikwenda ofisini kwake bila ya kuongea zaidi, hali ambayso huwa si kawaida yake. Mara nyingi afikapo asubuhi, baada ya kusalimiana huzungumza machache kabla ya kuingia ofisini kwake.
Dakika tano baadaye alitoka na kumuuliza Cathy, “MD yupo?”
“Yupo tangu saa mbili.”
Scolastica aliufuata mlango uliokuw ambele yake na kukishika kitasa. Akakizungusha, mlango ukafunguka taratibu na yeye akaingia taratibu vilevile. Mbele alimwona bosi wake, Evarist akiwa kitini macho kayakodoa kwenye kompyuta.
Mara Evarist aliunyanyua uso na kukutanisha macho na Scola. Kitu fulani kikamwambia Evarist, huyu ana tatizo. Akamwangalia kwa makini na kumwambia, “Karibu Scola.”
“Asante, bosi,” Scola aliitika huku akivuta kiti na kuketi.
Baada ya kusalimiana Evarist alimwambia, “Vipi, naona kama hauko sawa. Una tatizo?”
“Ni kweli bosi, siko vizuri.”

****ITAENDELEA SAA 10 JIONI*****
 
KITABU: SCOLASTICA TEMU (5)

TULIPOKOMEA....


Mara Evarist aliunyanyua uso na kukutanisha macho na Scola. Kitu fulani kikamwambia Evarist, huyu ana tatizo. Akamwangalia kwa makini na kumwambia, “Karibu Scola.”
“Asante, bosi,” Scola aliitika huku akivuta kiti na kuketi.
Baada ya kusalimiana Evarist alimwambia, “Vipi, naona kama hauko sawa. Una tatizo?”
“Ni kweli bosi, siko vizuri.”

***** ENDELEA*****


“Nini tatizo?”
Nimepatwa na msiba.”
“Pole sana. Umefiwa na nani?”
Scolastica alijiweka vizuri kitini. Akashusha pumzi ndefu kisha akaanza kujieleza. “Baada ya wazazi wangu kufariki dunia nililelewa na wasamaria wema tangu elimu ya msingi hadi sekondari. Wakati niko Makerere, mlezi wa kiume alifariki, akabaki mkewe; naye hakunitupa, alinilea kama mwanaye. Kwa kweli siwezi kumsahau. Sikuacha kuwasiliana naye na kumtumia pesa za matumizi hata nilipoanza kazi hapa. Yeye ndiye aliyebaki kuwa mama yangu.
“Lakini mama yangu huyo mlezi, alipatwa na tatizo la maradhi ya presha. Lakini, pamoja na jitihada za kutumia dawa mbalimbali kwa ushauri wa daktari, hata hivyo Mungu alimhitaji zaidi na akamtwaa. Jana usiku ndiyo nimepata simu kuwa kafariki dunia!
“Majirani wote pale nyumbani wananisubiri mimi ndipo maziko yafanyike. Kila mmoja pale nyumbani anajua jinsi mama huyo alivyokuwa akinipenda na kunitegemea kwa kila jambo!”
Kufikia hapo, Scolastica aliinamisha uso, machozi yalishatanda usoni. Uchungu ulimrudia kwa nguvu kubwa. Je, ulikuwa ni uchun gu wa msiba? Hilo alilijua mwenyewe.

“Basi Scola, usilie,” Evarist alimpoza. “Mungu amempenda zaidi mama yetu. Hayo ni mapito tu kwetu sote wanandamu hapa duniani. Wote hii ni njia tu, tunapita. Hakuna aliyezaliwa hapa na ataishi hapa milele.”
Scolastica alipangusa machozi huku kainamisha uso. Kisha kwa upole akasema, “Mkurugenzi naomba likizo fupi.”
“Hakuna shida Scola, “ Evarist alijibu haraka. “Chukua wiki tatu za mapumziko. Unahitaji kupata muda wa kuituliza akili na kujiweka sawa kisaikolojia. Au unaona muda huo ni mfupi Scola?”
Hapana, bosi,” Scolastica alijibu. “Unatosha sana. Nashukuru sana…”
“Unatarajia kuondoka lini?”

Scolastica aliunyanyua uso juu, akafikiri kidogo kisha akajibu, “Nikipata tiketi leo, kesho asubuhi naondoka. Nitaingia Kigoma nadhani keshokutwa.”
“Kwa njia ya basi?”
“Ndiyo, bosi.”
“Hapana,” Evarist alipinga. Papohapo akaivuta saraka mezani na kuchomoa kitabu cha hundi. Akaandika hundi ya shilingi milioni moja. Kisha akasaini na kumpatia Sciolastica huku akisema, “Iko ‘open.’ Fanya mpango wa usafiri wa ndege ya kesho asubuhi saa mbili.”
“Asante sana, bosi.”

“Na ‘salary’ yako i’shaingizwa benki tangu jana,” Evarist aliongeza.
“Nashukuru sana, bosi,” Scolastica alisema huku akinyanyuka. “Naweza kuondoka?”
Evarist alifikiri kidogo kisha akasema, “Subiri kidogo. Ofisi kama ofisi huwa ina fungu la mchango kwa ‘staff’ wake yeyote anayepatwa na tatizo kama msiba na kadhalika. Hivyo subiri nikupe mchango huo wa ofisi ikiwa ni rambirambi.”
Akatwaa funguo na kufunguo za saraka moja kati ya nne mezani hapo. Akatoa bunda la noti za Tanzania zenye thamani ya shilingi milioni moja na kumpatia.

Scolastica alipokea fedha hizo huku moyoni akishangaa. Hakutarajia kama ofisi ingemfanyia yote hayo. Eti kapatwa na msiba! Msiba! Eti kafiwa na mama yake mlezi! Kwa mbali alijisikia kucheka, lakini kumbukumbu ya yaliyompata jana ilipomrudia, alijisikia kulia, jambo ambalo pia alijitahidi kujizuia kwa nguvu zote.
Huku akijitahidi kuyaepuka macho ya bosi wake, na akijihisi kuwa mwenye hatia kubwa, akasema, “Sijui nikushukuru vipi bosi. Kwa kweli ofisi imenithamini sana.”
“Usijali, Scola,” Evarist alisema. “Ni jukumu la kampuni kumthamini na kumjali kila mfanyakazi wake inapotokea akapatwa na lolote linaloweza kumwathiri kimwili na kiakili.”
“Asante sana. Basi naomba nikuache.”
“Nakutakia safari njema.”
Scolastica alipoingia ofisini kwake kwa mara nyingine, hakukaa. Alichukua baadhi ya vitu alivyovihitaji, kisha akafumba macho na kusali: “Ee Mungu wangu, nakutegemea wewe Mungu kwa klla kitu.”
Akafumbua tena macho na kuangaza huku na kule ofisini humo. Hakuona kitu kingine chochote ambacho labda kingekuwa ni muhimu kuondoka nacho.
Akatoka.

*****
KITUO cha kwanza baada ya Scolastica kuondoka ofisini humo kilikuwa ni Hospitali ya Tumaini, Upanga.

ITAENDELEA....
 
SCOLASTICA TEMU (7)

MTUNZI/ MWANDISHI:
INNOCENT A. NDAYANSE (ZAGALLO)
MWAKA: 2002
MAREKEBISHO: MWAKA 2012
GAZETI: LETE RAHA

TULIPOKOMEA.....

Asingeweza kuisahau kirahisi siku hiyo na ni hicho kilichomkurupusha sofani, akaifuata kompyuta mpakato na kuamua kupekua jambo ambalo aliamini kuwa litaanza kumletea ufumbuzi katika ratiba aliyopanga kuanza utekelezaji. Akaingia mtandao na kuisaka taarifa yoyote inayohusu PAK. Kwanza akaandika ‘google’ kisha hatua nyingine zikafuata.
Dakika kumi baadaye aliizima kompyuta hiyo huku akitabasamu zaidi!

***ENDELEA***

Alikuwa amepata taswira halisi kuhusu PAK na alikuwa ameyasoma maelezo yanayoihusu. Hayakuwa maelezo mapya kwake. Wakati Serikali ya Tanzania ilipopiga marufuku uagizaji na utumiaji wa sumu ya PAK yeye aliyapata maelezo hayo. Yalikuwa ni maazimio ya Shirika la Afya la Dunia (WHO), baada ya kubainika kuwa idadi kubwa ya watumiaji, huitumia kwa malengo yasiyokusudiwa.

Hata hivyo, Scolastica aliwajua Watanzania jinsi walivyo. Wapo baadhi ambao ni wajanja zaidi ya ujanja wanaostahili kuwa nao. Leo serikali itatamka kuwa noti bandia zimezagaa mitaani, eti zitabadilishwa. Haitasaidia, kesho Mtanzania mwingine atakuletea noti mpya kama zile ambazo serikali imezigharimia katika kuepuka hujuma. Hadi zitakapobainika kuwa noti fulani ni halali na noti fulani ni haramu, tayari walioghushi watakuwa ni mamilionea kama sio mabilionea.
Kwa tamko hili la Umoja wa Mataifa kuhusu sumu ya PAK, Scolastica aliamini kuwa hakuna tatizo. Aliihitaji na aliamini kuwa ataipata. Kama iliwahi kutapakaa katika masoko mbalimbali ya mataifa mbalimbali, kwa vyovyote Tanzania pia ilifika. Kuna kisichoingia Tanzania? Runinga feki zipo, simu feki hazikosekani, dawa feki zimefurika, magari feki yanatamba barabarani, wanawake feki wapo macho juu-juu, wanaume feki nao wanahangaika mitaani wakirembua macho na kubibitua midomo.

Aliamini kuwa hakuna kitakachoshindikana. Kutokuwa na uhaba wa fedha ilikuwa ni nyenzo madhubuti katika mafanikio aliyoyahitaji. Siku alipoondoka ofisini alitoka na fedha taslimu shilingi milioni mbili, achilia mbali mshahara wa milioni kadhaa uliokwishaingizwa kwenye akaunti yake Benki ya CRDB.
Hakuwa ametumia hata laki tatu tangu siku ile. Na isitoshe, zaidi ya fedha hizo, katika akaunti nyingine ya Benki ya Standard Chartered alikuwa na shilingi milioni ishirini na tatu ambazo alikuwa hajagusa hata senti tano tangu alipoziweka miezi sita iliyopita katika akaunti maalum. Hizo alizipata baada ya kufanya kazi binafsi iliyohusu kampuni moja ya nchini Kenya.

Akaunti ya Benki ya Stanbic alikuwa na shilingi milioni nane ambazo nazo alizipata baada ya kuitumia taaluma yake ya Sheria kwa kufanya kazi moja binafsi. Kwa jumla hakuwa na tatizo la fedha. Hivyo, hakuona kama kutakuwa na kikwazo chochote katika ratiba zake alizozianza.
*****
JUMATANO hii ilikuwa tofauti na siku nyingine. Ikiwa ni siku ya kwanza ya mwezi Mei, Siku ya Wafanyakazi Duniani, hali ya hewa ya Jiji la Dar es Salaam ilikuwa ya kijimvua cha wastani, kijiupepo cha kisichokera na kijiubaridi cha mbali.
Scolastica Temu aliamka alfajiri, saa kumi na moja. Akafanya usafi katika eneo lake alikoishi na ilipotimu saa moja na dakika kadhaa akatoka. Alikwenda buchani ambako alinunua kilo moja ya nyama ya ng’ombe, kidari kwa minajili ya kuchemsha supu.

Hakuwa na hakika ya muda atakaorejea kutoka huko kwenye safari yake, hivyo aliona ni vyema akajitengenezea stafutahi nzito itakayomlinda kwa muda mrefu. Wakati akirejea, akanunua viungo vingine atakavyotumia katika stafutahi hiyo bila kukosa chapati tatu zenye uzito wa kutosha.

Saa nne alikuwa kishalijaza tumbo kwa stafutahi ya kutosha. Alijihisi kushiba kiasi cha kuwa na uchovu. Akajilaza sofani pa le huku glasi iliyojaa juisi baridi ya embe ikiwa kando yake juu ya kistuli. Hii hali ya kijiubaridi, mvua na kijiupepo haikuweza kumsumbua hata chembe. Zaidi, yeye alihisi mwili una joto japo hakulihisi joto kali. Baada ya kupumzika kwa dakika kadhaa, hatimaye aliamua kuondoka. Wakati akiondoka nyumbani alikuwa akiwaza, atumie usafiri upi. Alipaswa kuchagua kulingana na mapenzi yake si kulingana na uwezo wake wa pesa.

Hata hivyo, wakati akiifuata Barabara ya Kawawa iliyokuwa mbele yake, mita kama mia moja na hamsini hivi, akaiona teksi ikija nyuma yake taratibu. Akaamua kutumia usafiri huo. Akasimama na kuitazama. Dereva naye ambaye wakati huo alikuwa katika hesabu za kusaka vichwa, haraka akapunguza mwendo na kisha akakanyaga breki kando kabisa ya Scolastica.

“Town,” Scolastica alisema huku akiwa amekwishafungua mlango na kuingia kiti cha nyuma. Hata hivyo alikuwa makini akimtazama huyo dereva akihofia kuwa anaweza kujikuta amemkodi mmoja kati ya wale watatu waliomchukua siku ile jioni isiyosahaulika.
“Upande wa Selander Bridge au njia ya Kariakoo?”
“Pitia Selander Bridge, na usipite Kinondoni kwa Manyanya. Tumia njia ya Morocco, Barabara ya Ali Hasssan Mwinyi.”
Dakika kama ishirini baadaye alikuwa akiachana na teksi hiyo, makutano ya mitaa ya Zanaki na Jamhuri, katikati ya jiji. Sasa akaanza kuufuata Mtaa wa Jamhuri taratibu, akiangaza macho kwenye jengo hili na lile. Maduka kadhaa ya dawa yalikuwa kando ya barabara hiyo. Akaamua kwenda kwenye duka mojawapo.
Humo akawakutwa wateja wengi na pilika nyingi. Akatulia kwa dakika chache na kuondoka. Alihitaji kuingia sehemu ambayo haitakuwa na pilika nyingi lakini pia kusiwe kumepooza sana.

Alipitia maduka kadhaa, akiingia na kutoka, hatimaye akalifikia duka ambalo alivutiwa nalo. Hilo lilikuwa Mtaa wa Mosque, eneo ambalo kulikuwa na msongamanowa watu mtaani. Na hata ndani ya duka hili hakukuwa na uhaba wa watu lakini kulikuwa na utulivu kiasi. Wahudumu wanne wa kiume, Waafrika, vijana, walikuwa wakiwasikiliza wateja na kuwahudumia ilhali Wahindi wawili waliokuwa wakipokea malipo, walikuwa nyuma ya vijana hao katika meza zilizojitenga.

Scolastica alitulia kwa muda akiwatazama vijana hao na mwisho akavutiwa na mmoja wao. Huyu alikuwa na uso wenye utulivu na tabasamu muda wote. Alionesha bayana kuwa msikivu kwa kila mteja aliyehitaji huduma.
Alipopata nafasi alimsogelea na kumsalimia kwa sauti ya chini, “Habari yako.”
“Nzuri, shangazi, karibu,” kijana huyo alijibu huku akimtazama Scola kwa makini.

Scolastica akasogea kando kidogo na kijana akamfuata. “Ninahitaji tuonane,” alimwambia kwa sauti ya chini ambayo kwa hakika haikuweza kuyafikia masikio ya wengine. Kutoka pale alipo kijana yule na kwa wale vijana wengine, wenzake kulikuwa na hatua kama tano za mtu mzima. Na upande ule kulikuwa na sauti za juu; huyu akiulizia dawa hii, yule akitaka kuelewa gharama ya dawa fulani kwa mauzo ya jumla au rejareja.
Hakuna aliyewajali Scolastica na huyo kijana na hasa kwa kuzinga tia muda huo ulikuwa umekaribia saa saba, ambao maduka hufungwa kwa muda.

“Mimi?!” kijana huyo alionesha kushtuka.
“Ndiyo, usiogope. Unaweza kuja pale Ramos Restaurant, Mtaa wa Jamhuri?”
“Kuna nini?” bado kijana huyo aliyekuwa ni wa umri wa kati ya miaka ishirini na ishirini na tatu, alionekana kujawa na udadisi.
“Nina maongezi kidogo. Na utanufaika ushangae mwenyewe. Tupunguze maongezi; utakuja?”
“Labda tukifunga saa saba.”
“Nitakusubiri. Utafurahi.”
Kijana yule alimwangalia Scolastica kwa macho yenye mchanganyiko wa mshangao na matamanio. Hilo, kwa Scolastica halikuwa jambo la kujiuliza. Alijiamini kuwa ni mwanamke aliyetimia. Kwa kupitia kwenye miwani yake hii ya jua alimwona waziwazi kijana huyo akimtamani.

“Usiniangushe,” alimwambia huku akigeuka kuondoka baada ya kumtupia noti ya shilingi elfu kumi.
Wakati akienda hapo Ramos Restaurant, kumsubiri kijana huyo, alijua kuwa anacheza patapotea. Je, kijana huyo atakuja? Na hata kama atakuja, katika maongezi yao, ufumbuzi wa hii ziara iliyomtoa Kinondoni utapatikana?
Hakujua.

***ITAENDELEA SAA 11 JIONI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom