Riwaya: Scolastica Temu

Riwaya: Scolastica Temu

Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni http://www.equatorstory.com/
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
 
Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni http://www.equatorstory.com/
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
Wee bwege utahangaika sana mwaka huu
 
SEHEMU YA 53



*** *** *** *** ***
ILIPOKOMEA...

Scolastica aliguna. Kisha: "Uchovu?!"

"Ndiyo ni uchovu tu," Ndonya alijibu. "Kazi za leo zimenichosha sana."

Kwa mara nyingine Scolastica aliguna, lakini kabla hajatamka lolote akamwona Ndonya akigeukia upande wa pili, akionesha kuwa hahitaji kuendelea kuzungumza.

***ENDELEA***

Scolastica aliishia kuguna tu, kisha akaanza kuchojoa nguo kabla hajazima taa na kurejea kitandani. Alitarajia kumwona Ndonya akimwamuru awashe taa, ili naye achojoe nguo zake, lakini badala yake alijisogeza pembeni huku akionekana kama usiku huo ungepita akiwa ndani ya mavazi yake yote, achilia mbali vile viatu alivyovisukumia uvunguni mwa kitanda.
*****
NAAM, kwa Scolastica Temu, huu ulikuwa ni usiku wa aina yake tangu atoke rumande Gereza la Keko.

Kwa mara ya kwanza alishuhudia Ndonya akilala na nguo! Ndonya ambaye kila usiku alikuwa msumbufu, akihitaji mara kwa mara. Usiku huu, Ndonya alikuwa tofauti na siku nyingine, akiwa haoneshi kujishughulisha kwa lolote mbele ya mwili mtupu wa Scolastica uliokuwa ubavuni mwake.

Hilo lilikuwa ni miongoni mwa mambo yaliyomzidishia mashaka Scolastica dhidi ya Ndonya. Na kwa hali hiyo, alijikuta akishindwa kupata usingizi kama ilivyo kawaida, matokeo yake saa nane u nusu usiku alikuwa bado katumbua macho darini. Na ni wakati huo pia, ndipo alipomfumania Ndonya akiwa chali, naye macho kayatumbua darini, akionekana kuwa na jambo analolifikiria!

Hilo nalo likamzulia mshangao, na labda ungeishia kuwa mshangao, tena mshangao wa kawaida tu, kama asingeligundua jambo lingine ambalo sasa limzulia kitu kingine moyoni mwake.

Hofu!

Kwa muda wote ambao ukimya ulikuwa umekigubika chumba hicho, alijifanya kasinzia, na huenda hata Ndonya aliamini kuwa ni kweli kasinzia.

Hivyo, wakati Ndonya alipojitoa kitandani kwa kunyata, alimwona kwa usahihi. Hata aliposimama katikati ya chumba akikodoa macho ukutani, alimwona.

Muda mfupi baadaye, Ndonya alinyata, akielekea sebuleni ambako kwa mara nyingine tena aliifungua ile saraka.
Kisha akakitoa kile kitu kilichozungushiwa kijipande cha karatasi. Sasa akakitupa chini kile kijipande cha karatasi, mkononi akabaki na kichupa kidogo kilichobandikwa karatasi nyekundu. Akakiinua juu na kukitazama kwa makini kupitia taa iliyoning’inia darini.

Ni hilo lililomzulia hofu Scolastica. Kama ndoto, alihisi kukiona kitu kisichokuwa kigeni machoni pake. Kitu hicho kikiwa mkononi mwa Ndonya!

Japo hakuweza kukiona vizuri kitu hicho, hata hivyo hisia zake ziliegemea kuwa ni kitu chenye madhara. Mwonekanao aliokuwanao Ndonya, wakati aliporejea, na hadi kufikia usiku huu wa manane, ulitosha kumfanya yeyote aliyemzoea, amtilie shaka.

Tayari Scolastica alimtilia shaka, kwa alikuwa akimjua vizuri.
Kiasi cha mwezi mmoja uliopita, alifika katika duka moja la ‘uhindini’ katikati ya jiji ambako alinunua sumu kali aina ya PAK. Sumu hiyo ilihifadhiwa katika chupa ndogo huku ikiwa imezungushiwa karatasi nyekundu. Aliinunua sumu ile kwa sababu maalum na akaitumia kwa malengo aliyopanda.

Alipoitumia PAK kwa malengo yake, siku chache baadaye baadhi ya magazeti yakaiweka hadharani habari hiyo kwa vichwa tofauti. Moja likiandika; LIWALO NA LIWE. Lingine likawa na kichwa cha habari; DAKIKA ZA MAJERUHI. Yeye hakujali, alizisoma habari hizo akiwa rumande Keko.

Kwa kuwa utekelezaji wa azma yake ulihitaji matumizi ya PAK kwa asilimia mia moja, basi ni dhahiri PAK ilikuwa katika himaya yake kwa saa ishirini na tatu kwa siku.

Hivyo, aliijua na kuizoea vizuri kama ambavyo yeyote awezavyo kukizoea chochote anachokijali na anachokithamini.
Kwa hali hiyo, hisia kuwa chupa iliyoshikwa na Ndonya pale sebuleni huenda ikawa ni chupa yenye chochote chenye kuleta madhara makubwa mwilini mwa kiumbe yeyote, zilimjia papohapo kiasi cha kumzulia hofu kubwa moyoni!

Sasa akawa makini zaidi. Akaendelea kumtazama Ndonya kwa macho makali. Kwa sekunde kadhaa akaahirisha upepesaji wa macho kwa kile alichoamini kuwa ni katika kutokukikosa chochote akifanyacho Ndonya.

*****

“ALIYEUA kwa upanga atakufa kwa upanga,” Ndonya alinong’ona, akiyakariri maandiko ya Kitabu Kitakatifu cha Kikristo, Biblia.

Wakati akiyatamka maneno hayo kwa mnong’ono ambao haukuzidi hatua moja kutoka pale alipo, bado alikuwa na ile chupa ya PAK.

Aliendelea kuitazama kwa muda, kisha akaachia tabasamu dogo na kuirudisha sarakani. Na kama alivyokwishaigeuza kawaida kuwa sheria, safari hii pia aliifunga saraka hiyo kwa ufunguo. Aliporudi chumbani, hakuubadili ule utaratibu aliouanza usiku huo, utaratibu wa kulala na ‘miguo’ yake maungoni.

Huyu alikuwa Ndonya mwingine!

*****

KULIPOPAMBAZUKA bado hakukuwa na mabadiliko yoyote humo ndani. Ndonya hakuwa tofauti na alivyokuwa usiku. Na zaidi, alifanya yale ambayo kwa siku zote zilizopita ulikuwa ni wajibu wa Scolastica kuyafanya.

Alipotoka kitandani alikwenda bafuni huku akiwa na ndoo ya maji mkononi. Na wakati huo alikuwa na mavazi yaleyale, tofauti ya sku nyingine anapokuwa kavaa taulo pekee.

ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom