Riwaya: Mke wa Rais

Riwaya: Mke wa Rais

MKE WA RAIS

SEHEMU YA 27

Nyumba ilikuwa giza kuonyesha kuwa hapakuwa na mtu.. Mudy akazunguuka upande wa nyuma wa nyumba ile. Muda mfupi alikuwa amechupa na kuangukia kwa ndani. Alipotua ndani alinyata mpaka karibu ya mlango wakuingilia ndani.. Hapo akasimama kwa muda kusikiliza iwapo patakuwa na watu. Ukimya bado ulikuwa ukiendelea vile vile.. Akachomoa funguo zake Za bandia muda mfupi baadae mlango ulikuwa umemtii.. Akaingia ndani huku mdomo wa bastola ukiwa umetangulia mbele. Alipohakikisha Yupo ndani kabisa Ya nyumba ya mwanamke yule aliyeuawa... Mudy alilakiwa na Sebule nzuri Yenye thamani kubwa sana.. Aliitizama Nyumba ile katika namna ya kipekee macho Yake yakatua juu ya kipisi Cha Sigara ambayo kilionyesha kutumika muda mfupi Uliyopita. Akaongeza Umakini Huku Sikio lake likiwa limetega kuisikia iwapo mtu aliyekuwa akivuta Alikuwa ndani Ya Nyumba ile. Muda sio mrefu akasikia mngurumo wa gari Ukisimama nje Ya nyumba. Mudy akajiinua Haraka haraka na Kujisogeza Sehemu Ya maficho.. Muda mfupi akauona mlango ukifunguliwa kisha akawaona watu wawili wakiingia kama kivuli.. Uingiaji wa watu wale ulikuwa burudani machoni mwa Mudy.. Uingiaji ambao ulikuwa ukisadifu ufundi na Usalama wa watu ambao wameingia pale ndani... Mudy akaendelea kubana pale huku akitegemea kama watu wale walioingia kuwa watawasha taa .

Lakini Akashangaa kuwaona Watu wale wakitulia kanakwamba kulikuwa na kitu ambacho walikuwa wakikisuburi. Kuwaona viumbe wale wakiwa katika mkao wa kusubiri, kulimpa mudy hamu kubwa ya kusubiri.. Kwa kujua mbinu Za kijasusi Mudy Alijua kuwa palikuwa na mtu ambaye Alikuwa akisubiriwa. Kitendo hicho kilimfanya muda wote ajiweke tayari kwasababu ya kukabiliana na hatari Yoyote ambayo Ingetokea Mbele Yake.

Akiwa bado ametulia huku macho Yake akiyazungusha kwa hila katika Nyumba ile.. Mara akaliona pazia la Dirisha likisukumwa kisha akaingia mtu mfano wa Upepo... Uingiaji wa mtu huyu wapili ndio ulikuwa umemburudisha Mudy. Ni uingiaji ambao hutumiwa sana na Majasusi kutoka shirika la kijasusi la Israel MOSSAD. mtu yule alipoingia hakuinuka kwa wakati bali alikuwa amebaki pale chini katika namna ambayo ilionyesha kuwa alikuwa ametambua Uwepo wa Mtu au watu pale ndani. Mudy alikuwa akikitizama kitu kile kama Picha ya Sinema.. Licha ya mtu yule kuingia kwa staili ambayo Ilimsisimua Mudy, lakini tayari Alikuwa ameshamtambua kuwa ni kepteni George... Akaendelea kutulia akiusoma Mchezo.. Kila alipohisi labda kepteni george atasimama kutoka pale Chini. Haikuwa hivyo.. Bado GEORGE alikuwa ametulia chini. Sasa hapo Mudy akaingia na Hamu ya kuusoma Mchezo Zaidi. Akaokota chupa ambayo ilikuwa kando Yake kisha akaitupa upande ambapo hapakuwa na mtu.. Muda mfupi akashuhudia watu wale wawili walioingia Mwanzo wakirusha risasi Mfululizo kuelekea kule ilipoangukia Chupa Aliyoirusha... Licha ya watu wale kuinuka na Kuanza kurusha risasi, lakini Bado Kepteni George aliendelea kutulia pale chini. Kitendo hicho kilimfurahisha Sana Mudy.. Hapo ndipo alipoutambua Uwezo wa George..

Kupita kwa dakika mbili tu baada ya Mudy kurusha ile chupa, likatokea Tukio la Kusisimua... Tukio ambalo hata Mudy Mwenyewe Hakuwa Ameliona kisawasawa lakini alishuhudia mtu akianguka Chini tena karibu Yake na kuanza kugugumia kwa maumivu.. Akiwa ameshangazwa na kitendo kile akaduwaa Zaidi Baada ya kumuona Yule Mtu mwingine wa pili akitambarajika Chini na kutulia... Hali ya ukimya Ikarudi pale pale.... Msisimko ukampata Mudy.. Alikuwa ameshuhudia kitu ambacho alikuwa akikipenda kupindukia.. Hali ilikuwa kwenye Utulivu na Ukimya kama hapakuwahi kuwa na purukushani.

Muda mfupi gari Nyingine ilikuwa ikisikika ikisimama nje ya Nyumba ya Msichana.. Mlango Ukafunguliwa na Kuingia watu watatu ambao wao wakakimbilia Ilipo switch Ya kuwashia taa mle ndani.. Paaa! Wakawasha.. Wote wakatahamaki baada ya kukutana na Maiti Za wenzao Wawili.. Mudy Hakujivunga wala kepteni George Hakuchelewa... Wote waliamka katika namna ambayo haiwezi kueleweka... Mudy Akaachia Flying kick huku George akiachia mapigo matakatifu Ya kung fu.. Wote wakajikuta Wakiangaliana... Kabla wakora wale Hawajakaa sawa zikafuatia Ngumi Ambazo Ziliwafanya Waanguke Chini kama Mizigo... Hawakuwapa nafasi Za kujiandaa, pale pale Chini walipoangukia waliwawahi na Kuwafunga Pingu...

Wakawasogeza pembeni na kuanza kuwahoji mawili matatu lakini hapakuwa na Hata mmoja ambaye alifumbua kinywa Chake kuongea Chochote na kitendo Cha kushangaza zaidi watu wale wakaanza kutokwa na Damu mdomoni na kilichofuatia Wote wakakata Roho mikononi mwa Wanausalama wale. Kukata Roho Kwa Watu wale tena Mbele yao, kuliwafanya Mudy na George Kutizamana.. Kutizamana kwao kulikuja baada Ya kuliona tukio la Watu wale kujiua. Hapo walionyesha kuwa Walikuwa Wakipigana na Watu ambao walikuwa na Mafunzo Yote Ya Kijasusi... Wakasachi Vitu Muhimu kutoka kwa Marehemu Wale.. Hapo katika kupekwa ndipo walipokuta Picha Ya Kanali Jamila Ikiwa Mfukoni mwa mmoja wa Marehemu wale.. Mudy na George Wakaangaliana
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 60

AKAUSIKIA MLIPUKO WA BUNDUKI, KISHA AKAISIKIA SAUTI YA MTU ANAYEMFAHAMU AKILALAMA. Hakusubiri kuambiwa, hakuosubiri kitokee kingine. Alirudi katika muda ule ule.. Mkononi kwake akiwa amekamatia bastola mbili. Haikumchukua muda kufika sehemu ya tukio. Sehemu amboyo ilitapakaa Moshi na Harufu ya Damu. Maiti za Wazungu wanne zikiwa zimetambarajika chini katikati kwa madimbwi ya Damu. Macho ya Mohamedi hayakuhitaji kuwaona wale Wazungu. Macho ya Mohamed hayakuhitaji kushangaa hilo, bali macho yake yalihitaji kuwaona watu. Watu ambao aliwahitaji kuliko alivyoihitaji Roho Yake. Alikuwa akiwatafuta Jenifer na Revina. Hakuwa akiwaona katikati Ya Moshi, hakuwa akiwaona katikati ya mapambano. Hakuwaona wakionyesha ujuzi wao na wala hakuwaona wakiwa sehemu. Macho yake yakashangaa, kichwa chake kikaunda maswali kisha mdomo wake ukaropoka wako wapi hawa? Hakuwa na Majibu kwa kipindi kile. Punde akavisikia ving'ora vya polisi. Punde akawaona Makomandoo wakitokea katikati Ya Moshi, Makomandoo ambao hawakujulikana wapi walipotokea. Wote wakanyoosha Bunduki Zao kuelekezwa pale alipo Mohamedi. Mshangao na bumbuwazi vikatamalaki usoni kwa Mohamedo Hasira Zikaupanda moyo Wake, akatamani afanye kitu, akatamani awaanzishie kuwaonyesha kuwa ni zaidi Ya wao.

Lakini alipomuwaza Revina na Jenifer alikubali kuwa mpole. Upole ambao ulikuwa katikati Ya mshangao. Mbele ya Uso wake akatokea mkuu wa kitendo cha kijasusi ndani ya Idara ya Usalama Wa Taifa. Pembeni alikuwa na Watu wawili, watu ambao walifunikwa nyuso Zao kwa vitambaa. Mmoja alikuwa Wa kiume na Mwingine alikuwa wa kike. Kutokea kwa Mr Fraidy Wellah kukaibua maswali kwa Mohamedi.. Bado alitamani kitu kinachoendelea kiwe hadithi. Ni wakati huo akishangaa, Akahisi kitu kama Sindano kikitua katika Mwili wake, kitu ambacho alishakijua kuwa ni Dawa ya kusaidia kumlevya. Ni kweli alilewa. Muda Mfupi baadae Macho Yake yalikuwa yameingia Giza. Yalikuwa mazito Yasioweza kufunguka. Akakubali kwa Mara ya kwanza kumezwa na Hali ile. Akakubali kwa Mara Ya kwanza kufungwa na kubebwa kama maiti.

*****
pembeni ya jengo moja kubwa katikati ya jiji la Dar es salaam, Maeneo ya Posta. Watu wasiopungua kumi walikuwa wameizunguka meza kubwa huku kila mmoja akionekana kuwa busy na computer Yake mpakato. Walikuwa wanaume saba na wanawake watatu. Wote walionekana wakifuatilia kitu fulani. Kitu ambacho kilionekana ni Muhimu. Taarifa Zilikuwa zikitumwa huku na huko, maswali Yakiulizwa na Mengine kujibiwa. Kikao kilikuwa kizito, kikao kilikuwa kizito kupindukia. Tayari Rais wa Nchi alikuwa haonekani wapi alipo. Huku baadhi ya Walinzi wake wakiokotwa wakiwa maiti. Bado taarifa Zilikuwa ndani kwa ndani, bado taarifa hazikuweka bayana katika hilo. Lakini wakiwa katika Jengo lile wakijadili hicho kitu ilikuja taarifa kuwa kuna baadhi ya Makomandoo walikuwa Wameasi. Na Sio hao tu, bali Mkuu Wa Ujasusi na Mkurugenzi Wake walikuwa ni wamojaapo katika Suala hilo. Kila mmoja alikuwa akihaha kutaka kujua ni wapi Rais wa Nchi Amepelekwa. Ni wapi atakuwa amehifadhiwa Rais wa nchi? Yalikuwa maswali yaliyopita Vichwani mwa wajumbe wa kikao kile. Wakati suala la Mheshimiwa Rais kupotea likiwa halijapatiwa Ufumbuzi, Likaja Suala kuwa Mpelelezi Mashuhuri Nchini Mohamedi naye ametekwa na Hajulikani alipo. Hapo wajumbe wote wakapigwa na butwaa, wote walikuwa wakiitambua harakati inayofanywa na Mohamedi, na Wote walitambua kuwa Mohamedi alikuwa ndio mtu pekee wa kulitatua hili. Sasa hii Taarifa ikazima ndoto Zao za kuisaidia Serikali kubaki Madarakani. Na taarifa iliyoingia Punde iliwajulisha kuwa Raisi alikuwa amehifadhiwa sehemu akishurutisha alitangazie Taifa kuwa Anaachia Madaraka ya kuongoza Nchi. Kila Mmoja akapagawa na kikao hakikuendelea tena.

*****

alikuwa mwanamke pekee na mtu pekee aliyeshuhudia kutekwa kwa wasichana wawili waliokuwa wakisaidiana na Mudy na Pia ni Yeye pekee aliyeshudia Mudy akitekwa baada ya Kudungwa Sindano Ya madawa Yenye kutia Usingizi. Huyu hakuwa mwingine bali alikuwa Inspekta Ummu Sammy. Kila kilichokuwa kikitendeka alikuwa akikishuhudia kutoka umbali mdogo jirani na Sehemu ya Tukio. Alikuwa hapo kwa muda mrefu sehemu ile akiwafuatilia Nyuma Mohamed, Jenifer na Revina walipotoka nyumbani kwa Waziri Wa Katiba.

Baada ya Mohamed, Revina na Jenifer Kuondolewa pale. Ummu hakutaka kuchelewa kuondoka pale. Alichokifanya ni kuchukua sura yake ya Bandia na kuivaa. Muda Mfupi alikuwa akionekana kama Msichana wa kizungu akitembea eneo lile umbali ule ule bila kuonyesha kushangazwa na kitendo kinachotokea pale. Alikuwa akitembea huku kila hatua yake ikiwaza kitu, alikuwa akitembea huku akili yake ikahama pale. Bastola Mbili Zilikuwa kiunoni. Alikuwa akihesabu kila Hatua yake, alikuwa akiupangia mkono wake kipi cha kufanya. Akazishuhudia gari zilizowachukua Mudy, Revina na Jenifer Zikiondoka.. Naye akaunga Nyuma akiwa katika pikipiki.. Pikipiki aliyompora mtu aliyekuwa akiiendesha. Akaunga msafara katika Kuzifuatilia Gari Zile. ULIKUWA MCHEZO HATARI SANA KUUCHEZA.....
Mudy daah
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 066

Wote walikuwa wamepoa na wote walikuwa wakitokwa na mapovu mdomoni. Mohamed na Ummu Wa katizamana. Hawakuwahi kupambana na watu wenye Roho mbaya kama hawa. Kitendo kilichofanywa na wasichana wale kilionyesha ni jinsi gani walikuwa Majasusi wa kutisha. Ilikuwa ni kawaida kwa majasusi Kutoka kundi la Mafia la kule Nchini Italy kutumia njia ya kujiua kuliko kukubali kutoa Siri papote pale. Hii mbinu ikazagaa katika mashirika mbali mbali ya kijasusi. Nao wakaona ndio njia pekee ya kuficha siri hata kama ukiwa kwenye mateso makali kiasi gani. Licha ya kutambua hilo lakini hawakuwaza kukutana na watu tena watoto wa kike wenye kufanya hivyo. Waliporidhika na kila kitu walichokichunguza, ikiwemo kuwapekua wakatoka ndani ya kile chumba na Kuanza kukiendea chumba kingine.

*****
wakati Mohamed na Ummu wakiendelea upande wa jumba lile. Jenifer alikuwa ndio kwanza anaingia katika Chumba kimoja kipana Sana. Alitembea kwa makini huku kila kitu kikiwa tayari. Bastola mkononi na Bunduki kubwa Mgongoni vilimpa nguvu ya kutembea katika chumba kile bila kuogopa. Mfujoni alikuwa na funguo za Chumba walichofungiwa watoto wa Rais. Akaendelea kutembea mdomo wa Bastola ukimtangulia. Kidole kilitulia sawia kwenye Triggle. Alikuwa tayari kufyatua Ama kuua. Alikuwa tayari kuachia risasi pale ilipobidi. Akakivuka Chumba kile kwa Usalama. Akaingia katika chumba cha pili. Kuufungua mlango na kuchungulia kwa ndani akapokewa na Ukimya wa Ajabu. Ukimya wa kila kitu. Hapakuwa na taa wala feni. Hapakuwa na mchakato wa kitu chochote bali ukimya wa Ajabu. Jenifer akatulia kwa Muda Akiuruhusu Ubongo wake kufanyakazi. Akiiruhusu akili Yake kufanya usahihi katika chumba kile. Ukimya ulimuogopesha, ukimya Ulimtisha. Akasita kuingia na kusimama nje. Lakini Ghafka akaisikia Sauti ya mwanamume ikimkaribisha kutokea ndani ya kile Chumba. ''karibu binti Mzuri'' hilo la kukaribishwa likausisimua mwili wake,l likaisisimua damu yake. Akajiuliza aitikie ama aache kuutikia. Akabaki katikati akiwaza hilo. Hakuwahi kuwa Muoga katika kufa. Daima damu ndio kitu alichopenda kucheza nacho. Sasa kwa nini leo naogopa? Lilikuwa Swali lililopita kichwani mwake. Akajiona ni Mjinga kukiogopa kifo, akajiona mpumbavu kuogopa kupambana. Punde akauruhusu Mguu wake utangulie katika kile Chumba.

Kuingia kwake kukafuatia na mlango kujifunga kwa nyuma. Moyo wake ukapiga mapigo kadhaa. Wakati akiangalia huku na huko kumuangalia aliyemkaribisha. Akashangaa kumuona mwanaume wa Kizungu akitokea kwa Mbele yake. Uingiaji wa mwanamume Yule Ulikuwa Uingiaji wa Ajabu sana. Jenifer hakumuona wakati anaufungua mlango na hakumuona wakati alipompita na Kusimama mbele yake. Alishtukia mtu mfano wa kivuri akisimama mbele Yake. Akisimama mfano wa mzimu. Macho yake yalikuwa yakiwaka kama yawakavyo macho ya paka Usiku. Hakuwa na Tabasamu hakuonyesha kicheko. Sura Yake ilionekana ni Sura iliyozoea kuua. Sura Iliyozoea Kuondoa Roho Za Watu. Hapa ndipO Jenifer alipokikumbuka kitabu alichowahi kusoma Udogoni kwake. Kitabu kilichoandikwa na HAYATI BEN MTOBWA kiitwacho MALAIKA WA SHETANI ingawa huyu mtu hakufanana na yule wa kwenye kitabu lakini kwa kuiangalia Sura Ya Mtu Huyu alikiona kile ambacho kinaendana ama kufanana na Jitu lililoelezewa kwenye kitabu kile. Hapo alihitajika kuwa Jasiri kama Alivyokuwa NURU. Hakujisumbua wala kuhangaika nalo, akabaki kuzuga kama hakuwa amemuona. Lakini akishtukia akipigwa pigo moja la Haja. Pigo ambalo lilimfanya apepesuke hadi kuufikia ukuta. Wakati anataka kujiandaa kukabilana na Mtu Yule, ajashtulia na ngumi pamoja na Mateke Mfululizo kuelekea kwake. Akajaribu kukinga kwa ufundi wake lakini Safari hii akajikuta akienda Chini baada ya mapigo matatu kumuingia Sawa sawia
. Hakuchelewa pale chini hasa pale alipomuona yule mwanaume akiruka Juu kumfuata pale alipo. Alichokifanya Jenifer ni Kuchupa kutoka pale chini na kusogea pembeni, yule mtu akatua patupu lakini wakati huo huo akajigeuza kutoka pale chini na kupeleka mateke kadhaa Kwa Jenifer.

Safari Hii Jenifer Aliyaona, aliyaona kwa ukaribu na kuyakwepa kwa Ufundi Mkubwa na wakati huo huo akiruka martials Combart Moja ambayo iliingia sawa sawia kwa mtu yule na Kupepesuka. Wakati akijitahidi kukaa sawa Jenifer aliruka Angani na kumshindilia na Ngumi tatu za Hewani. Ngumi ambazo zilimfanya yule Jasusi Wa kizungu kuzamisha mikono mfukoni na Kuibuka na Bastola. Lakini Hakuweza kushindana na Mkono mwepesi wa Jenifer, Mkono ambao ulitumia nukta moja kuzama mfukoni kuchomoa bastola, Kisha nukta ya pili Kuiruhusu bastola kufanyakazi Yake. Risasi Zikapenya Kichwani kwa Mzungu Yule na kumrusha hewani. Alipokuja Kutua chini alikwisha kuwa maiti. Jenifer akampekuwa hapa na pale Katika mifuko yake. Akakutana na Kitambulisho. Kitambulisho kinachoonyesha Mzungu Yule Anaitwa Dimitri Poloshkovic na Alikuwa Jasusi Wa Shirika la Kijasusi la Urusi KGB. AKATASAMU KISHA KUONDOKA NDANI YA CHUMBA KILE.
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 067

AKATABASAMU NA KUTOKA NDANI YA CHUMBA KILE. Akaongoza ndani kabisa ya Chumba kingine. Bastola mkononi huku mwili ukiwa kwenye utayari wa kupambana. Akaupita uchochoro fulani na kutokea upande wa pili. Hapo akauona mlango wa chumba alichokuwa akikihitaji. Chumba walichofungiwa watoto wa Rais. Akaongeza umakini huku hatua zake zikiendana na utazamaji wa macho yake. Kila mguu mmoja ulivyokuwa ukisogea ndipo jicho lake lilipozidi kuangalia. Jicho lilikuwa likitupwa kwa Hila kutizama katika aina ya utizamaji kwa wale wahitimu na wakufunzi Wazuri katika medani ya mapambano. Mdomo wa bastola ulitizama mbele, macho yakatazama mbele. Akili yake ikapelekwa ndani ya Chumba kile. Hatua tano kabla ya kuufikia Mlango akaichomoa funguo, funguo ambayo alipewa na Mohamed. Akautizama ufunguo Huku tabasamu hafifu likiifunuka Sura Yake yenye kila ishara Ya Uovu. Sura Iliyobeba mtu mpambanaji. Kuutoa ufungua kukafuatiwa na Hatua mbili tatu mbele. Hatua ya Nne akausikia mchakato katika masikio Yake. Mchakato ambao ulipenya na kugundulika katika ngoma za Masikio ya Jenifer. Aliutambua uwezo wake na Aliziheshimu Hisia Zake. Hakuudharau mchakato aliousikia masikioni mwake.

Hata pale alipousikia mtikisiko wa kitu mfano wa bomu likitokea umbali mdomo kutoka pale alipo. Aliweza kuruka kabla na kuangukia pembeni. Hakuinuka kwa Muda ule, aliendelea kujificha pale chini macho Yake yakitembea katika Ukungu. Ukungu uliyomuwezesha kuwaona watu sita wakiwa wamemuweka Rais wa Nchi katikati. Akaupa mwili wake nguvu ya kusimama. Akaupa mkono wake Nguvu ya Kuifikia bastola iliyokuwa imeanguka pembeni. Akaivuta na kuisogeza karibu Yake. Akakiruhusu kidole kuelekea kwenye kitufe cha kuruhusu Risasi. Sekunde mbili bastola ilikuwa akitema cheche, bastola ilikuwa ikimwaga mwani. Risasi Zake zikatua pale alipozitaka Ziende. Watu wawili kati ya Sita walikuwa wameanguka Chini. Wanne waliobaki kila mmoja alikuwa amechupa pembeni Huku wakimuacha Rais akibabaika peke yake. Punde wakatokea watu wawili, watu ambao aliwatambua kwa Haraka Zaidi. WAlikuwa Mohamed na Ummu, walitokea kusikojulikana na kumkumba Rais kisha kuanguka naye pembeni. Wakamuondoa Ile sehemu na Kumuingiza ndani kabisa ya Jengo lile. Walipoona Sehemu walipomuacha ilikuwa ni Salama. Wakarudi katika uwanja wa mapambano. Uwanja ambao ungekuwa mwisho ya Wapanga mapinduzi wote. Mwisho wa Waroho wa Madaraka na Mwisho wawafuja Mali. Waliamua kuteketeza kila walichokiona mbele ya Upeo wa Macho Yao. Yalikuwa mapambano makali, mapambano yaliyosababisha kukamatwa kwa Makamu Wa Rais, mtu ambaye alikuwa akiratibu mpango wote Wa Mapinduzi kwa kuwatumia Viongozi Wa Chama na Wa Serikali. Wakisaidiwa na Makomandoo pamoja na Askari Wa kikosi maalum Walifanikiwa kuiondoa familia ya Mheshimiwa Rais Kuipeleka mafichoni. Licha ya hilo kufanyika lakini bado Mohamedi, Ummu na Jenifer Walitaka kujua. Walihitaji kujua nani ambaye alipigwa Risasi ndani ya Ikulu na Nani ambaye aliuawa wakati mtu aliyesemekana kuuawa Alikuwa hai? Yalikuwa maswali yenye uwezo wa kujibiwa na Mke wa Rais pekee. Yeye ndiye aliyekuwa anajua kila kila kitu.

Lakini haikuwa rahisi kufanya naye mazungumzo kwa kipindi kile. Kipindi ambacho bado alikuwa katika matatizo Ya kiafya. Kipindi ambacho alihitajika kuwa Chini ya Uangalizi wa Madaktari ..

Lakini Bado Mohamed Alihitaji kujua, bado alitaka kufahamu kwa kuwa kitendo kilichofanyika ndani Ya Ikulu Ya Nchi. Kuliitangazia Dunia kuwa Sehemu hiyo haikuwa salama tena kwa kufanywa makazi Ya Kiongozi wa Nchi. Kama watu wanaweza kuingia Ikulu na kutengeneza mchezo Mchafu watashindwaje kuingia na kumuua Rais? Yalikuwa maswali mazito yaliyokuwa yakipishana kwenye vichwa vya Wapelelezi wale Watatu. Hawakutaka kumuacha mtu yoyote iliyehusika kutengeneza hili tukio.

*****
Zilipita Siku tatu tokea litokee lile tukio la kuokolewa kwa Rais. Mohamedi akiwa amekaa sehemu na Jenifer wakipata chakula cha Usiku, wakamuona kijana mmoja mtanashati akiingia pale Hotelini. Kijana yule hakuwa mgeni machoni kwake kwani alishawahi kumuona sehemu, lakini bado hakuwa akijua ni Sehemu gani.. Baada ya yule kijana kuingia wakamuona Akiangaza Huku na Huko kanakwamba alikuwa akitafuta kitu ama mtu. Macho yake yalipokutana na Macho ya Mohamed akatabasamu kisha Akapotea eneo lile. Punde Mohamedi alikuwa amesimama na Jenifer alikuwa ameshafika mlangoni akitoka nje Huku Mkono wake ukishuka kiunoni ilipohifadhi bastola yake. Akaupita mlango na kutoka nje kabisa, Nyuma yake Alifuatiwa na Mohamed mikono yake Ikiwa mifukoni. Hatua kumi mbele wakakutana na Kitu Ambacho walikitarajia. Yule kijana aliyetoka pale ndani Alikuwa Amelala Chini ya Ardhi huku damu ikichuruzika na Kusambaaa. Wote hawakusimama wakapita kanakwamba hawakuwa wao.. Vichwani Vyao walishajua Ule ni Ujumbe. Ujumbe Uliyoletwa kwa Kuwakumbusha kuwa Mambo Badoo tena BADO SANA..
 
Back
Top Bottom