Riwaya: Mke wa Rais

ibra87

R I P
Jul 22, 2015
5,614
5,337
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 002

Mwanaume akageuka kumtazama mwanamke akashangaa kukutana na mdomo wa bastola, bastola ambayo ilikuwa mikononi kwa mwanamke Yule. Macho Yalikuwa mekundu kwa Hasira.. Bastola Ikakohoa mara Mbili Risasi mbele Zikapenya Katika Paji la Uso la Mwanaume Yule. Ubongo Ukaruka na Kusambaa Chumba Kizima. Mwanaume Akaanguka chini na Kutulia.. Alikuwa Tayari ni Maiti.

Mlio wa bastola Uliosikika kutoka ndani uliwashtua walinzi wake na kila mmoja akaupeleka mkono wake kiunoni wakaibuka na Silaha.. Hawakuta kuingia kwa Kupitia getini... Wote walichupa hewani na kudondokea ndani.. Wakauendea mlango wa ndani kwa Kasi Ya Ajabu.. Kazi ambayo haikuwahi kutokea.. Sekunde kumi baadae walikuwa ndani ya Jumba lile. Wakapigwa na butwaa baada ya kukuta kiza totoro.. Wakatazamana na Kupiga hatua kuelekea ndani Zaidi... Walipofika karibu na Mlango wa Kutokea Upande wa Pili wa Jengo lile.. Wote wakahisi kukanyaga kitu kama Maji.. Lakini Uzito wa kitu kile kikawafanya walinzi Wainame na Kugusa yale maji.. Kila mmoja Kengele Ya Hatari Ikalia kichwani mwake.. Wakajua mke wa Mheshimiwa Alikuwa Hatarini.. Hawakusubiri.. Mmoja Akarudi nyuma na Kuruka Flyng kick Na Kuingia na mlango mpaka ndani... Kufika ndani Walichupa tena kila Mmoja Akaangukia pembeni Huku Bastola Mkononi.. Chumba Kilikuwa giza na Hawakusikia Hata mkoromo wa Binadamu... Mmoja Alipoangukia Akachupa tena Mpaka Iliposwtch ya Kuwashia taa na Kuifyatua..

Chumba Kizima Kiliwaka taa.. Kitu cha kwanza kuonekana machoni kwa walinzi wale ilikuwa maiti, maiti ambayo ilikuwa imelala katikati ya dimbwi kubwa la damu. Ubongo ulikuwa umesambaa mule ndani... Wakahamisha macho Yao na Kuyapeleka Kitandani wakapigwa na Butwaa Baada Ya kumuona Mke Wa Rais akiwa na Bastola Ya Kirusi Mkononi Huku akionekana MachoZi Kumtoka na Kumlowanisha. Hawakutaka kusubiri... Wakamuinua pale na Kumkokota Mpaka nje.. Walipofika Nje Cha kwanza kukifanya Waliichukua Ile Bastola Mikononi mwake kisha wakamuingiza ndani Ya Gari na kuliondoa maeneo Yale kabla polisi Hawajafika Eneo lile.

Gari Ikatembea kwa Mwendo Wa kasi sana kuelekea Nyumbani kwa Mheshimiwa maeneo Ya Kinondoni... Gari ikafika na Moja kwa Moja Kuingia ndani.. Maafisa Usalama Waliokuwepo waliiona Hali Ile ya kuonyesha kuchanganyikiwa kwa Mke Wa Rais lakini kwa kuwa Alikuwa na Walinzi Wake maalum Walimuacha bila Ya Kumuuliza.

Baada ya kuingia pale na Kushuka kwenye gari Kisha kuingia Ndani, aliongoza moja kwa moja bafuni huku akionekana ni Mwenye huzuni na Majuto Usoni. Aliingia bafuni na kuyavua mavazi Yake... Akafungulia maji na kuyaacha yaendelee kushuka katika mwili wake. Tukio zima la kupigwa Picha Lilimuumiza sana.. Hakujua ni Watu gani waliofanya vile na Walifanya kwa Lengo lipi... Akaiona Heshima yake kama Mke wa Rais Ikianza Kushuka.. Akawaza kile ambacho alikuwa akikifanya kikimfikia Rais au Wananchi Wakiona Atakuwa katika Wakati Gani? Aliuona Mwisho Wake mbaya, alijiona Mjinga Kushawishika kufanya ujinga.. Je ni Wakina nani lakini? Na Walifanya kwa Lengo lipi na ni Upi mwisho wangu katika Kadhia hii? Hakuwa na Majibu kwa Muda ule.. Hakuwa na jibu la kumfanya Ajisikie Vizuri.. Akakata Tamaa na Kukaa Juu Ya Sinki La Kuogea.. Macho Yake yakitazama Paa la Jumba lile la Kifahari... Mawazo Juu ya Mumewe Yakawa yanapita Usoni Mwake... Akajilazimisha Kutabasamu Lakini Haikuwa Hivyo.. Hakukuwa na Tabasamu Wala Hakukuwa na Kicheko.... Yalikuwa machozi, machozi Na Majuto.. Akainuka pale na Kuchukua Vali lake Maaulum... Akajiangalia kisha Kwa Sauti Ya Kujiamini Akanena... NITAMUUA YOYOTE NITAKAE MUHISI.. kisha akatoka Mle Bafuni na Kuingia Chumbani Kwake... Alipoingiza Mguu wake Ndani akapokelewa na Mlio Kuonyesha Kulikuwa Sms Kwenye Simu Yake.... Moyo Ukampiga Paaa!! Kisha Mikono kumtetemeka. Hakujua kwanini lakini alijikuta Akiiogopa mpaka simu yake. Akapiga hatua kisha Akaichukua Simu na Kuusoma Ujumbe Ule... Alichokiona Kwenye Simu kilimfanya Aanguke Chini Kama Mzigo.....

UNADHANI AMEONA KITU GANI?
 
MKE WA RAIS



Akapiga hatua kuifuata Simu yake pale mezani Huku akitetemeka mikono na Miguu.. Akaishika na kuileta usawa wa Uso wake, kisha akaifungua na Kuisoma. Pale pale akalegea na kupiga mweleka kama mzigo.. Hakuwa anaamini kile alichokiona kwenye simu yake na Hakutaka kuamini kama ni kweli lile suala litafikia pale. Akaichukua tena Simu yake Akiwa pale pale chini na kuitazama tena ile meseji.. Akajikuta akikutana na umbo lake akiwa uchi wa mnyama tena akiwa na mwanaume kitandani.... Aliendelea kuitazama ile picha huku wakati mwingine akifikicha macho kutoamini ama kudhani kuwa Alikuwa kwenye ndoto tena ndoto ambayo Haikuwa na Ukweli wowote. Kila alichokuwa akikifanya kilimpa majibu kuwa Hakuwa ndotoni bali alikuwa Akitazama picha yake tena akiwa kama Alivyozaliwa na Mbaya Zaidi Akiwa na Mwanaume kitandani. Machozi Yakaunda mfereji machoni mwake.. Akatamani kuyazuia Yasitoke lakini alikuwa Amekwisha kuchelewa... Machozi Yalikuwa Yakishuka katika Mashavu Yake Taratibu. Akaiona Safari Yake ya Kuiacha Ikulu ikikaribia.. Aliuona mwisho wa ndoa Yake na mwisho wa U first lady wake. Tena mwisho wa kuondoka katika Jumba la Mchi kwa kashfa mbaya.. Kashfa ya kuisaliti ndoa yake na Kashfa ya Kupigwa picha Za utupu.. Akawaza na kuwazua.. Hakuwa tayari Hilo litokee na Hakuwa tayari Kuiona ndoa Yake ikisambaratika. Akaapa kufanya kitu kwasababu ya kuilinda Hadhi Yake... Lakini Angewezaje kulizuia Hilo lisitokee? Atafanyaje kupambana na Hilo? Akainuka na Kwenda Moja kwa Moja mpaka ndani Ya Chumba cha Mawasiliano... Akaitafuta namba fulani, alipoipata akainakili kwenye Simu Yake kisha Kuipeleka Sikioni....

''Hellow,'' ilikuwa sauti ya Upande wa pili wa Simu.

''Ikulu hapa,'' alijibu mke wa Rais...

''Najua, kuna tatizo gani?'' ikauliza sauti ya upande wa pili..

'''Nakuhitaji muda huu''' akatoa amri mke wa kiongozi.

Kisha akakata simu na kutulia.

Muda mfupi baadae Akaonekana mwanaume mkakamavu Akiingia kwenye Viunga vya Ikulu.. Akapokelewa na Watu ambao kwa kuwaangalia tu walionyesha heshima kubwa kwa mwanaume Yule. Akaingia ndani na kuingia katika Chumba cha Mazungumzo Ambapo alimkuta Mke Wa Rais akimsubiri.

Mwanaume Yule baada ya kukaa na kusalimiana na mke wa bosi wake, akashangazwa na hali aliyomuona nayo. Akagandisha macho yake katika Uso wa mwanamke yule kwa muda wa kama Dakika mbili... Kwa macho yake Ya kijasusi Yaliyozoea kusoma kusoma vitu vilivyojificha aligundua kitu ambacho hakikuwa Cha kawaida. Lakini hakujua nikitu gani ambacho kilikuwa kikisumbua katika Moyo wa mke wa Bosi wake. Licha ya kugundua Hilo lakini Hakutaka kumwambia Chochote kile mpaka pale mwenyewe atakapoinua kinywa chake na kumtakia.. Mwanaume yule Hakuwa mtu mwingine bali alikuwa Mkurugenzi Wa Usalama Wa Taifa Mr Adinan.

Baada ya Kukaa kwa muda huku akitafakari cha kumwambia mkurugenzi hatimaye mke Wa Rais akasimama na Kupiga hatua Kuelekea pale Alipokuwa Amekaa Mr Adnan.... Alipomfikia akanyoosha mkono na kumkabizi Mr Adnan ile Simu ambayo tayari Ilikuwa imeshafunguliwa sehemu ya Ujumbe mfupi. Bila kuongea kitu Akarudi alipokuwa amekaa. Mr Adnan akaitazama ile simu kwa muda kisha akapeleka Machoni mwake na Kuangalia kile ambacho amekusudiwa akiangalie. Mshtuko mkubwa aliyouonyesha Ukamfanya Hata Mke Wa Rais Mwenyewe Apatwe na Mshtuko. Mr Adnan akatazama kwa Mara Ya pili kile kitu alichokiona kisha, akamtupia macho mke wa Rais akakutana na Machozi Yake. Hakujali machozi Yake, tayari Ndita zilishatokea Usoni mwake kuonyesha kutokupendezwa na Hali ile. Akainuka na kumkabidhi simu yake.. Kisha kwa hatua Za Ukakamavu akaanza Kupiga Hatua Kuondoka ndani ya Chumba kile. Wakati alipopigiwa simu na kuambiwa anahitajika Ikulu hakuwaza kukutana na Jambo kama Lile... Hakujua kama mke wa boss wake ni mtu wa Aina Ile... Wakati anakaribia Mlango wa Kutokea Nje, Akashtushwa na Kishindo kilichotokea Nyuma Yake.. Mkono wake Ulikuwa Tayari Ushaifikia Bastola Yake na Tayari Alikuwa Amegeuka Huku Bastola Ikiwa Mkononi. Akakutana na Kitu cha kushangaza na Kutisha... Mke wa Rais alikuwa chini akiwa Ametulia.. Lilikuwa tukio la Kutisha sana ambalo hakulitarajia kabisa. Akapiga hatua kusogea pale alipoangukia mke wa mkuu wao...... Akakutana na Dimbwi La damu, dimbwi ambalo juu yake alilala Mke wa Rais... Akachoka...

UNADHANI NINI KIMEMSIBU MKE WA MHESHIMIWA?

TUKUTANE JUMATATU
 
MKE WA RAIS

Mwili wa Mke wa Rais ulikuwa umelala katikati ya Dimbwi la damu.. Akahamanika na kushangaa... Akayatembeza macho yake juu ya mwili wa mke wa Rais akakutana na kitu kilichomshangaza.. Kitu kilichomshtua na kupatwa na Baridi.. Juu ya mwili wa mke wa Rais kulikuwa na Matundu mawili ya Risasi. Akabaki kugandisha Macho yake bila kufanya chochote kile, alikuwa kwenye kipindi ambacho hakuwahi kukutana nacho... Akahisi ubaridi ukiingia mwilini mwake.. Ulikuwa ubaridi wakushangaza na kusikitishwa.. Nani atakuwa amemuua mke wa Rais? Nani Amepiga risasi? Na je risasi imepitia wapi? Yalikuwa maswali kutoka kichwani kwa Mkurugenzi Wa Usalama Wa Taifa Mr Adnan Kassim.

Yalikuwa Maswali mazito Sana, maswali ambayo yalihitaji majibu kwa muda ule, lakini hakuwa na Jibu Lolote.. Alihitaji kupanda ufumbuzi lakini hakuupata.. Akaendelea kuutazama mwili wa Mke wa Rais huku akifanya kila aina kukwepa kuvuruga ushahidi.. Akahamisha macho yake kutoka Mwilini na Kuipeleka mkono wake Wa kulia... Akazidi kuchanganywa na alichokuwa akikiona.. Katika mikono Yake Kulikuwa na Simu tu.. Hapakuwa na bastola wala Silaha Ya aina Yoyote. Mr Adnan Kassim akazidi kushangaa.. Hatimaye akasimama na kupiga hatua mbili kuangalia usalama wa Chumba kile... Alikutana na Usalama ule ambao ulikuwa Siku Zote katika Ikulu yoyote pale Duniani. Hapakuwa na Sehemu yoyote Ambayo yangeweza kuruhusu kupenya kwa risasi.. Sasa ni Yupi aliyemuua Mke wa Rais? Je Hizi risasi Zimetokea Wapi? Au Zinauhusiano gani na Picha Zile? Yalikuwa maswali Yasio na Majibu.... Alichokifanya ni kuirudisha bastola Yake Sehemu Yake... Akawataarifu Usalama wa Taifa wa pale Ikulu.. Kisha Akachomoa Simu Yake na Kumpigia Rais Moja kwa Moja Kumtaarifu Kilichotokea.

Ilikuwa ni Habari ambayo Haikutegemewa na Rais, taarifa ambayo Ilimshtua... Licha Ya kujua kilichotokea muda mfupi kupitia kwa Watu wake Aliyowapandikiza Lakini taarifa ya kuuawa kwa mkewe Hakikuwa kitu ambacho Alikitegemea wala kukitarajia na Hata Alipoelezwa mazingira ya Tukio Hakukubaliana.

Hali Ya Taharuki Ikaizidi ndani Ya Ikulu ya Nchi.. Hatimaye Shirika la Utangazaji Tanzania Likatangaza kifo Kile. Wananchi wakakumbwa na Mshangao uliyochanganyikana na Huzuni. Hakukuwa na Mwenye Taarifa ya Ugonjwa wala Ajali achilia mbali hata kuumwa mafua. Kifo chake kilitangazwa bila kutaja Ugonjwa Uliyomuua marehemu.

Wakati Wananchi Wakiwa kwenye Huzuni, Maafisa Usalama Wa Ikulu Ya Tanzania Walikuwa Wakihaha ndani Ya JenGo lote kuangalia kila Sehemu, lakini Jibu lilikuwa Pale pale. Hakukuwa na Chochote Walichogundua.. Na Kilichowaacha mpaka Wachanganyikiwe ni Pale walipotazama Camera Za Usalama Zinazoonyesha Jengo lote na Kukuta Camera Zile Zikiwa Zimeharibika. Kengele Ya Tahadhari Ikagonga katika Vichwa Vyao.. Wakaiona Hatari Ambayo Ilikuwa mbele yao. Haiwezekani Mtu Wa Kawaida Aingie Ikulu na Kufanya Mauaji kisha Aharibu Camera Za Usalama na kutoka Pasipokuonekana. Lilikuwa ni jambo lisilowezekana.. Jambo ambalo liliwaacha wanausalama wote na Viongozi Wa Nchi katika Tafakuri Ya Hali Ya Juu.

*************

Habari Ya kuuawa kwa Mkewe Ilimchanganya Sana Mheshimiwa Rais.. Hakuwa amewapa ruhusa ya kuua.. Hakuwa amewapa Ruhusa ya Kutumia nguvu Vijana wake. Sasa hii Taarifa Ya kuuawa kwa mkewe Imetoka wapi na ni nani ambaye amefanya mauaji hayo tena Ndani Ya Ikulu? Ni Maswali Yake Hayo Yaliomfanya Awatafute Vijana Wake Watatu Ambao Aliwapa ile kazi Ya Kumfuatilia mke Wake... Simu Ikapokelewa Kisha Sauti Ya Kanali Jamila Hassan Ikasikika upande Wa pili...

Baada Ya Maswali Ya Hapa na Pale kutoka kwa Rais na Kujibiwa vizuri; Rais Alikata Simu Huku akiacha maagizo ya Kufuatiliwa kwa Walinzi waliokuwa wanamlinda Mkewe Ilikujua kama Watakuwa Wanajua Kilichotokea Au Kuhusika katika Tukio Hilo.

Baada Ya Agizo Lile, Muda Mfupi gari ya Kifahari Aina ya Ranger Rover ilikuwa njiani kuelekea kinondoni huku ndani ya Kukiwa na Vijana Watatu.. Vijana ambao walikuwa wametumwa Mahususi katika kuwafuatilia Walinzi wa mke wa Rais ambao walikuwa Zamu Muda Mfupi kabla Ya Tukio la kuuawa kwake. Gari Ikaingia Maeneo Ya Kinondoni Manyanya na Baada ya Muda Walikuwa Wakisimamisha Gari Nje Ya Jumba la Mlinzi Yule. Wakashuka Kisha Wakaliendea Geti na Kutaka Kugonga... Lakini kabla hawajafanya Hivyo Wakagundua Geti Lilikuwa wazi... Wakaingia bila Ya kubisha hodi, wakaongoza mpaka mlangoni... Wakaugonga kwa Mara Ya Kwanza lakini palikuwa na Ukimya. Wakagonga kwa Mara Ya Pili.... Lakini bado hali ilikuwa vile Vile... Kanali Jamila Hassan Akausukuma Mlango.. Ukafunguka.. Wote wakaingia ndani katika Aina fulani Huku bastola mikononi... Wakapokewa na Maiti Ya Mlinzi Wa Mke wa Rais ikiwa Imelala katikati Ya dimbwi la Damu Huku shingo ikiwa amechinjwa..
 
MKE WA RAIS



wakakutana na tukio la kutisha. Mlinzi aliyekuwa na mke wa Rais muda mfupi kabla ya kifo chake naye alikuwa ameuawa, tena kinyama kwa kuchinjwa Shingo. Wakatizamana katika namna ya kujiuliza maswali.. Lakini hawakujiuliza sana.. Wakajua ni lazima wamuwahi mlinzi Aliyebaki kabla naye hajauawa na Muuaji. Wakarudisha mlango Ili watoke lakini wakashangaa macjo yao kukutana na Kitu, kitu ambacho kila mmoja alikishangaa.. Kwenye ukuta wa Jumba lile waliyaona Maandishi. Maandishi ambayo Yalikuwa yameandikwa kwa damu na kukolezwa kwa Damu. Maandishi Ambayo Yalisomeka hivi (MKE WA RAIS) wote wakaangaliana kwa mara moja na sekunde Iliyofuata Wote walikuwa kwenye Gari kuelekea Nyumbani kwa Mlinzi Aliyebaki. Matukio ya Mauaji yale kwa Mke wa Rais na kisha mlinzi wake Yaliwaumiza Vijana Wale watatu. Hawakutarajia kutokea kwa kile kilichotokea.... Na bado walikuwa katika giza.. Kwanini muuaji Aandike Neno mke wa rais ukutani? Kuna uhusiano gani kati ya mke wa Rais na Mauaji haya? Mke wa Rais anahusika vipi hapa wakati hata yeye amekwisha uawa tena ndani ya Ikulu ya nchi? Maswali hayo na Maswali mengine kibao ni kati ya maswali ambayo Yalikosa majibu kabisaa kutoka kwa Kanali Jamila Hassan, Luteni Sevenlee na Captain George simon. Licha Ya kupitia kwao katika mafunzo ya juu katika Mashirika mbali mbali ya kijasusi Kama CIA, KGB, MOSSAD pamoja na M16 Lakini tukio la kuuawa kwa mke wa Rais na Sasa Mlinzi Wake Lilikuwa ni Tukio ambalo liliwasisimua sana.. Tukio ambalo lilionyesha kufanywa na mtu mtaalam na Mwenye ujuzi Sana. Ni vigumu sana Kuuwa mtu ikulu tena Sehemu ambayo hakuna mwanya wowote.. Sehemu ambayo ilikuwa ikilindwa kwa mitambo na Camera maalumu za Usalama.. Lakini mtu huyu aliyafanya hayo je mtu Huyu anauwezo gani? Na ni nani? Kumfikiria kwao mtu Huyo kukawafanya wawe na Hamu ya Kumpata.....

Gari ikaendelea kutimua mbio na Muda mfupi baadae Walikuwa wakisimamisha gari Maeneo ya Tabata Shule. Wakashuka Wote kwa pamoja Kisha Wakatangulia Luteni Sevenlee na kanali jamila Hassan huku Captain George Simon akibaki Nyuma kuangalia Iwapo kulikuwa na mtu ambaye alikuwa Akiwafuatilia. Wakatembea kwa Mwendo wa haraka huku kila mmoja akiwa makini kwa kila hatua. Wakaifikia Nyumba ya Mlinzi wa pili... Wakati wanataka kugonga geti macho yao yakatua Chini ya Ardhi.. Kulikuwa na Matone ya Damu.. Sekunde moja kila mmoja alikuwa amekwisha chomoa Bastola Yake na Sekunde Ya Pili Wote walikuwa wapo ndani huku midomo Ya Bastola ikiwa imetangulia mbele.. Walitembea kwa tahadhali mpaka walipoufikia mlango wa kuingilia ndani bila kuona tone jingine la damu lakini walipoushika mlango ili waingie ndani wakashtushwa na Damu Iliyokuwa Ikichuruzika Kutoka ndani... Hawakutaka kusubiri, teke moja mlango ukatii na wote wakaingia ndani tayari kwa chochote kitu... Wakapokewa na kitu kama walichokiona walipotoka.. Mwili wa Mlinzi Mwingine Ulikuwa Umelala Katikati ya Dimbwi la Damu huku Shingo ikiwa imetenganishwa na kichwa. Wote wakachoka.... Kama waliambiana pia wote wakatupa Macho Ukutani wakakutana Na Maandishi yale yale waliyokutana nayo kule walikotoka (MKE WA RAIS)......

Kila mmoja akamuangalia mwenzake.. Wote walikuwa wamechoka na sasa walikuwa wakiogopa. Walikuwa wakiogopa kwa kuwa kama mke wa Rais waliyekuwa wametumwa wamfuatilie ameuawa pamoja na Walinzi wake, je ni nani ambaye atafuatia? Wakapata Majibu kuwa waliyobaki ni wao na wasipokuwa makini nao watauawa. Kanali Jamila Hassan akachomoa simu na kubonyeza namba fulani lakini kabla hajaipeleka Simu Sikioni, wakamuona Captain George Simon akiingia pale ndani huku akionekana ni mwenye wasiwasi mkubwa.. Wote Wakamtizama kwa Macho Yenye maswali na kabla hawajaanza kumuuliza, captain George Akasema... Mr Adnan Kassim Mkurugenzi wa Idara Ya Usalama wa Taifa Ametekwa na Hajulikani Alipo mpaka Muda huu... Lakini Licha ya Kutekwa kwake lakini pia Mke na Watoto wake Wote Wameuawa kwa kuchinjwa shingo na Ukutani Kukakutwa Maandishi Yale yale tuliyoyakuta kule na Hapa tulipo.... Kwahiyo Huu ni Mchezo Hatari tunaoucheza, mchezo ambao nadhani tunaofuatia ni Sisi. Kama wameweza kumuua mke Wa Rais pamoja na Walinzi Wake.. Wakamteka Mkurugenzi Wa Usalama wa Taifa ikiwa ni Pamoja na kuwachinja watoto na Mkewe, unadhani Sisi tutaachwaje?

Ni wakati wakutumia silaha na Ujuzi tulionao kumsaka Huyu Muuaji kwani tukizubaa, Tutakuja kuchinjwa na Sisi... Wakati wa Mapambano Umefika hivyo ni lazima tupambane.
 
MKE WA RAIS

Wakati Akishangaa utokaji wa watu wale, muda mfupi baadae akasikia mlio wa bastola ukitokea chumbani kwa boss wake na kabla hajaamua kipi cha kufanya alishangaa kuwaona wasichana wawili wakifanya vitu ambavyo hakuwahi kuviona Live isipokuwa kwenye Video tu. Akili yake ikapumbazwa na tukio la kusikika kwa mlio wa Risasi kutokea chumbani kwa Bosi Wake pia Uingiaji wa wanawake wale katika aina moja ambayo Ilipendeza kuitizama. Aliendelea kukaa pale kuangalia kila kitu kilichokuwa kikiendelea na baada ya kuwaona wale wadada wakiingia ndani, akachukua nafasi ile kuchupa Haraka na kutua nje kisha Akajisogeza mpaka ilipo ile gari Iliyokuja na Mke Wa Rais.. Huku bastola Ikiwa mkononi, macho Yake yakiangaza huku na Huku akaona nafasi Nzuri Ya kwenda Kumuua mke wa Rais ni yeye kuingia kwenye Ile gari. Baada ya kupata wazo Hilo Hakutaka kusubiri.. Aliifunua bUti ya Gari na Kujiingiza kisha Kuifunga vizuri harafu akatulia Huku bastola ameishikilia vizuri mkononi mwake.

Muda mfupi tu baada ya kuingia, mara akasikia Vishindo vya Watu na muda mfupi baadae Akahisi mlango wa Gari Ukifunguliwa kisha Ukafungwa na muda mfupi baadae Gari ikaondoshwa kuelekea Sehemu ambayo alijua kabisa kuwa Ni Lazima Watakuwa wanakwenda Ikulu. Kila alipokuwa Akiufikilia uwezo wa wale walinzi Alikuwa Akiogopa kwani Alijua Hakuwa na Uwezo wa kupambana nao iwapo wangemtia mikononi. Ndivyo ilivyotokea, alifanikiwa kuingia Ikulu bila kushtukiwa.. Akatoka kwenye buti la gari katika Aina ambayo hakuna Ofisa Usalama Yoyote wa pale Ikulu aliyemuona. Baada Ya Kushuka akaongoza kuingia ndani alikoelekea mke wa Rais na Walinzi wake. Alipofika mbele kidogo Aliacha Njia Iliyokuwa inaingia ndani Yeye Akaenda Moja kwa Moja mpaka Sehemu ya Kuongozea Camera Za Usalama. Alipofika pale Aliangalia kwa Muda Alipofanikiwa kuiona Sehemu aliyokuwa Akiitafuta Akafanya kile ambacho alitaka kukifanya. Muda mfupi baadae camera Za Usalama Zote Zilikuwa hazifanyi kazi. Sekunde Ya kwanza Alikuwa Akiondoka sehemu ya Mitambo ile na Sekunde ya pili Alikuwa Anatazamana na tukio ambalo alikuwa Analitamani. Mbele ya Macho Yake Alikuwa Akimuona Mke Wa Rais Akiongea na mtu ambaye Alimfahamu sana.. Mtu ambaye Alikuwa ni mwalimu wake katika Mbinu Za Kimapigano kwa kutumia silaha na Hata Mikono. Alikuwa Akitazamana na Mr ADNAN KASSIM mkurugenzi Wa Usalama Wa Taifa. Wakati akishangaa kitendo kile, mara Akamuona Mr Adnan Akiondoka.. Sekunde ile ile Bastola Yake ilikuwa mkononi na Alikuwa ameielekeza pale Aliposimama Mke Wa Rais. Akawa anahesabu hatua Za Mkurugenzi Wa Usalama Wa Taifa. Alipomuona Mr Adnan Amepotelea.. Muda Ule ule Bastola yake Yenye Kiwambo cha Kuzuia Mlio Ikakohoa mara Mbili... Risasi Zikatua pale alipopataka. Risasi Zilitua katika Kifua Cha Mke Wa Rais.. Akaitazama Bastola na Kuibusu Kisha Kuichomeka bastola sehemu yake.

Wakati Mkurugenzi Wa Usalama wa Taifa akigeuka kuangalia kishindo kilichotokea Nyuma Yake, Yule Msichana Alikuwa Akiimalizia kuumaliza Ule Ukumbi na Kutoka Zake Nje bila Kuwa na Wasiwasi Wowote. Alikuwa tayari ameshakamilisha kumuua Mke wa Raisi.

HIVYO NDIVYO ILIVYOKUWA.

Ulikuwa ni Usiku Wa saa tatu, katika maeneo mengi ya Jiji la Dar es salaam Yalikuwa yamechangamka Huku mazungumzo mengi yaliyotawala yakiwa ni mauaji ya Mke wa Rais. Ingawa watu wengi hawakuambiwa kilichomuua, lakini watu wachache walikuwa wameshadaka tetesi kuhusu kilichomuua mke wa Rais. Katika watu wachache waliopata kutambua mapema kuuawa kwa Mke wa Rais Akiwa ndani Ya Ikulu, alikuwa ni Kijana Mmoja Aliyejulikana kwa Jina la Mohamedi. Akiwa ni mkazi wa Jiji la Dar es salaam, Mudy Alikuwa ni mtu mwenye marafiki Wengi wakiwamo Wazito Wa Ikulu huku Wengine Wakiwa ni Watu wajuu katika Vitengo Nyeti Vya Serikali. Akiwa Amesimama katikati Ya Jiji la Dar es salaam maeneo Ya Posta. Mohamedi Alikuwa Akitafakali na Kujiuliza maswali mengi ambayo hakuwa na Majibu... Alishangazwa na Maelezo kuwa Mke Wa Rais ameuawa Akiwa Ikulu.. Kilichomshangaza zaidi ni pale alipoambiwa kuwa Mtu huyo Aliyefanya Mauaji Alianza kwanza kwa Kuzima Mitambo Yote Inayowezesha kusukuma kamera za Usalama na baada ya Hapo ndipo alipofanikiwa kumuua mke wa Rais tena huku Mkuu wa Upelelezi Akiwa ndani. Kitendo Hicho kilimsisimua sana Mohamedi.. Aliuhusudu sana Uwezo Wa mtu huyo. Walikuwa ni watu wachache sana Wenye uwezo Wa Kujiamini na Kufanya kitu Kama hicho.

Wakati Akifikiria Kuhusu hilo mara Ikaingia Taarifa Nyingine kuwa Chief ametekwa kisha Mke na Watoto wake Kuchinjwa kama kuku... Habari Hiyo ndio Iliyomsisimua Mohamedi.. Habari ambayo Ilimuonyesha kuwa kulikuwa na Mtu katili na Asiye na Huruma.. Wakati habari Ya kutekwa kwa Chief Haijaisha, Ikaingia Habari kuwa Walinzi Wawili waliokuwa Wakimlinda mke wa Rais Saa Chache kabla Ya Kuuawa nao Wameuawa tena kwa Kuchinjwa.. Ilikuwa Taarifa Iliyomsisimua Mohamedi... Akaupeleka Mkono Sehemu Alipohifadhi bastola Yake.. Alipohakikisha Ipo akatabasamu
 
MKE WA RAIS

Mkono wake Ukashuka sehemu ambayo Huhifadhi bastola yake. Akaigusa na kugundua kuwa Ilikuwepo. Mohamedi akatabasamu, tabasamu ambalo hata yeye mwenyewe alishangaa kwanini alitabasamu. Lakini jibu alikuwa nalo kichwani mwake kuwa matukio manne yaliyotokea mchana wa leo yalimsisimua na kumtia hamu sana ya kupambana. Kuuawa kwa Mke wa Rais na walinzi wake.. Kutekwa na kuuawa kwa Familia Ya mkurugenzi wa Usalama wa Taifa ni Moja kati ya Mambo ambayo Yalimpa hamu sana Ya kujua kipi kilichopo nyuma ya Matukio yale. Je angewezaje kujua wakati hakuwa mtu wa usalama? Angejuaje wakati suala Hili linafanywa Kuwa Siri kubwa? Muda mfupi akajipa tumaini kuwa lazima afanye jambo, jambo ambalo lingeweza kumfanya apate angarau chochote ambacho kingemsaidia katika kujua kile ambacho kimejificha nyuma ya Matukio Hayo. Kutoka Posta mpya, muda huu Mohamedy alikuwa Akiiacha posta akitembea kwa miguu kuifuata barabara ambayo Ilikuwa ikielekea ufukweni mwa bahari Ya Hindi.. Aliamua kuelekea maeneo ya kivukoni ambapo aljua angeweza kupata Chochote kutoka kwa mateja na wafanya biashara wa Soko la samaki pale feri. Akitembea kwa hatua za kawaida Zilizomfanya Aonekane kama Mtu wa Kawaida, Mohamedi alikuwa makini kwa kila kitu na kila hatua ambayo alikuwa akipiga. Licha ya kujulikana na wanausalama wengi kutokana na kazi yake lakini hakuwa mjinga Kumuamini kila mmoja.

Baada ya kupita hapa na pale nakutokea maeneo ya NBC alichepuka upande wa pili wa barabara, alipochepuka upande ule akahisi kitu, kitu ambacho kilimsisimua kiasi fulani. Kitu ambacho kilimfanya atabasamu na kujua kuwa hakuwa peke Yake katika Safari ile. Hakuwa peke yake kwa kuwa Alihisi kuna mtu au kitu kinamfuatilia kwa nyuma. Kwa kuwa hakuwahi kuyapuuza mawazo Yake na Hisia Zake, akatumia Hila Kulitambua hilo. Akatembea kwa kutokuwa makini mara akajikwaa na Kudondoka, wakati anaamka kujifuta vumbi macho Yake Yaliangalia kwa Chati Upande aliyotokea... Macho Yake yakamuona mwanaume wa makamo ambaye alikuwa akitembea kama ameshika mkongoja.. Mudy akatabasamu.. Akajua kuwa alikuwa ni kweli akifuatiwa, akifuatiwa na Mtu, mtu ambaye hakuweza kuiona Sura Yake Zaidi Ya Kuuona Utu uzima wake kutokana na Kutembea kwa mkongojo. Kengera Za Hatari Zikamgonga, kwa mara Ya pili mkono Wake Ulishuka mpaka palipohifadhiwa bastola.. Akavuta tena hatua kwa mwendo wa machale... Alipofika maeneo Ya Wizara Ya Ardhi Akaacha Ile njia Inayokwenda Feri, akaingia kushoto akawa Anaenda Ikulu. Alipofika karibu na Jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu.. Akauona Utepe wa Njano ukiwa umezungushiwa eneo lote Kuonyesha Kuwa hapakuwa na Uwezekano wa kupita.. Naam, alitakiwa kurudi Nyuma.. Kurudi kule kule alipotoka.. Kule ambapo kulikuwa na Yule Mzee anayetembelea Mkongojo. Hakutaka kuwaza wala kuzuzuka.. Akavuta Hatua kwa kurudi Nyuma.. Mara Hii hakurudi kulr wizara ya Ardhi.. Bali alipita Mbele ya Jengo la Wizara Ya Elimu, akanyoosha njia kama Anaelekea Maeneo Ya Chuo Cha Usimamizi Wa fedha (IFM) alipofika maeneo ya shule ya Msingi Bunge akasimama kwa sekunde kama Mbili.. Sekunde Hizo alizitumia kuangaza macho yake katika maeneo yote.. Hatimaye Akakiona Alichokuwa Akikitafuta.. Yule Mzee bado alikuwa Akimfuatilia kwa nyuma.. Tena Safari Hakuwa peke yake bali alikuwa na mtu mwingine, mtu ambaye alionekana ni kama Mtoto wa Kike. Kitu kikamwambia kutoka Moyoni mwake.. Kuwa Makini Mohamedi huo ni mpango wa kukuzuia Usiingie katika sakata hili... Sauti Hiyo ilimfanya Atabasamu.. Hakuwahi kuogopa wala hakukuwa na Mwenye uwezo wa kumzuia kufanya ile ambacho ataamua. Baada ya kuwaona wale watu Sasa wakiwa wameongezeka Mohamedi akageuza na Kuanza kurudi alipotokea ambapo ndipo walipo wale watu waliokuwa Wakimfuatilia. Aliamua kufanya hivyo huku akiwa Makini kwa kila kitu.. Alitembea huku mkono ukiwa mfukoni.. Mfukoni huku ukiwa Umekamatia bastola yake Vizuri. Akatembea kwa hatua ndefu.. Alipowakaribia watu wale akajifanya kama Ameangusha kitu, akainama katika namna ambayo iliwasisimua baadhi ya watu waliokuwepo eneo lile.. Alipokuja kuinuka Akajikuta akitazamana na Mitutu ya Bunduki Ikimtizama... Mudy Alilitegemea Lile.. Akatulia kwa kuwatazama Watu wale... Kwa jinsi Walivyoshikilia bastola Zao, hakukuwa na mpita Njia Aliyeugundua Ule mchezo. Wote walijua ni watu Wanaojuana...hawakujua Walikuwa Wakipambana na mtu wa Aina gani.. Hawakujua kuwa Mudy alikuwa nani katika Taaluma Hii ya Upiganaji hasa akikutana na watu wa Aina yake. Hatua Ya kwanza Alikuwa amenyanyua mikono juu kutii, na hatua Ya pili akageuka kwa Teke aina ya Round kick ambalo lilitua sawia kwa Yule msichana na kumtupa chini... Wakati Huyu aliyejifanya kikongwe akishangazwa na wepesi ule, akajikuta Naye akiisalimia Ardhi baada ya kupigwa karate moja Ambayo Ilimuangusha chini... Mudy hakuwa na papara ya kuwahi pale walipoangukia.. Akawasubiri wainuke... Lakini wakati akifanya Hivyo akaiona gari moja ikija kwa kasi Huku mdomo wa bunduki ukichungulia.. Akajua nini kinafuata.. Muda Ule ule ukachupa na ......
 
MKE WA RAIS



Wakati Mudy Akitaka kupiga hatua kuwafuata wale wakora walioanguka chini, ghafla Akaiona gari Ikija kwa kasi huku vioo vyake vikiwa Vimeshushwa Chini huku midomo ya Bunduki Ikichungulia kuelekezwa kwake: alijua kipi ambacho kingetokea kama angechelewa.. Muda ule ule alikuwa amechupa hewani na kutua Upande wa ndani ya Shule ya Msingi Bunge, risasi Zikapita pasipo kumgusa. Alipotua Chini bastola Ilikuwa mkononi tayari kukabiliana na maadui wale lakini Ukimya uliotokea pale Ulimfanya Mudy Atulie. Kweli alitulia na Kuanza kuangalia huku na Huku lakini bado ukimya Uliendelea kutanda. Hapakuonekana uwepo wa watu sehemu ile na vile vile hapakuonyesha kama palitokea kitu muda mfupi uliyo pita. Akainuka huku bastola Yake ikiwa ameishikilia sawa sawia. Maswali lukuki yakikizonga kichwa chake.. Hakuwajua watu wale walikuwa wakina nani na walikuwa wakitaka nini kwake. Kitendo cha kufuatwa mapema na watu wale kilimjulisha kuwa na Yeye Alikuwa mmoja kati Ya Watu ambao walikuwa wakihitajiwa, aidha na Muuaji wa mke Wa Rais au na Idara Ya Usalama wa Taifa. Haiwezekani watu wasiomfahamu wamfuatilie bila kuwepo kwa sababu na nilazima Sababu Yenyewe iwe kubwa. Akajikuta Akiwatamani watu wale, watu anbao hawakuwa na Uwezo wa kupambana nae.. Watu ambao wangempa mwanga wa kujua wao ni nani na walikuwa wakitoka Wapi, na Walitumwa na nani. Hapo akajiambia kuwa Muda wa mapambano unawezekana umefika au Unakaribia kufika. Akatabasamu kisha akaondoka pale kwa mwendo wa tahadhali huku mluzi mdomoni ukimchangamsha. Kutoka Shule Ya msingi Bunge akanyoosha na kupita Nje Ya Makao makuu ya Jeshi la Magereza.. Akakata kushoto kuelekea maeneo ilipo benki kuu ya Tanzania.. Alipofika pale akachepuka na kuingia mtaa wa pili. Alipotokea maeneo ya Posta mpya Akaiendea tax Aliyokuwa Imepaki pale posta akaomba apelekwe Mbezi Beach... Sehemu ambayo alihitaji kuanza uchunguzi Wake kujua kipi ambacho kilisababisha kuuawa kwa Mke wa Rais.

*********

Wakati Mudy Akiondoka pale posta kuelekea mbezi beach nyumbani kwa Yule Marehemu aliyeuawa kwa Kupigwa Risasi na mke Wa Rais. Huku Nyuma Vijana Watatu ambao walipewa kazi ya kufuatilia mauaji yale Walikuwa ndani ya Chumba fulani katika nyumba moja Ambayo Ilikuwa Tabata Bima. Walikuwa wamejifungia Humo ndani kwa Muda mrefu... Kujifungia kwao hakukuwa kujifungia kwa kuogopa bali walikuwa katika mikakati Mizito kuhusu mauaji Ya kinyama na Kutoweka kwa Mkurugenzi Wa Idara Ya Usalama wa Taifa Mr Adnan Kassim. Kila mmoja alikuwa akikaribia kuwehuka, hawakujua nani alikuwa Nyuma ya Matukio Yote. Kuanzia Kuuawa kwa Mke wa rais, Kuuawa kwa walinzi wake kisha kuuawa kwa familia Ya mkurugenzi pamoja na kutoweka kwake. Matukio Yote yametokea katika mfululizo ambao Mtekelezaji alionekana kuwa Alishajipanga muda mrefu katika Hilo. Lakini aliwezaje kuingia Ndani Ya Ikulu Bila kuonekana na Watu? Au Muuaji Alikuwa ndani Ya Ikulu? Na kama Alikuwa ndani ya Ikulu aliingilia wapi? Na kwanini hakuwaua wote na Mkurugenzi Akamuua mke Wa Rais tu? Ni maswali hayo ambayo Yalimlazimu mkuu wa Kitengo Cha Kijasusi Fraidy Wellah kuwaamuRu Vijana Wake Waingie Kazini.. Kazi ambayo Ilitakiwa kuanzia Nyumbani kwa Mwanaume Aliyeuawa na Mke Wa Rais kabla ya Kuuawa na Yeye... Lilikuwa Agizo ambalo lilitakiwa kutekelezwa muda ule ule. Licha ya kutakiwa kuanzia kule Lakini kwanza walitakiwa kwenda ikulu kuangalia Mazingira Ya kifo cha Mke Wa Rais... Vijana Wale Wakaamua Kugawana Majukumu.. Luteni Sevenlee na Kanali Jamila Hassani wao walielekea Ikulu, Huku Kapteni George Simon Akielekea Mbezi Nyumbani Kwa Mwanaume Aliyeuawa.

Muda Mfupi Baadae Gari Yao ilikuwa ikiingia katika lango la Ikulu. Baada ya kusimamisha gari Wakashuka na kuongoza Moja kwa moja mpaka sehemu Ambapo palikuwa na Askari Wengi waliokuwa wakilinda sehemu yote pamoja na Wanausalama wengine. Wakatoa Vitamburisho Vyao kisha Wakaeleza Kilicho wapeleka pale.

Wakaruhusiwa Kuingia katika Eneo ambalo lilizuiWa kwa sababu za Kiusalama. Baada Ya kuingia Cha Kwanza Walichokifanya ni Kuelekea Moja kwa Moja ilipogari ambayo Aliitumia Mke Wa Rais kabla ya Kuuawa kwake. Wakaitazama kwa macho kwa Muda kisha Kanali Jamila Akamuonyesha Luteni Ishara ambayo Ilipokelewa na Muda Ule ule Ile Buti Ya Gari Ikafunguliwa.. Wote wakatizamana kwanza.. Ndani Ya buti Ya Ile gari Kulikuwa kunatoa Harufu, harufu ambayo Ilikuwa ni ya pafyumu ya Kike... Macho yao yakaongeza Umakini huku wakihakikisha hawakigusi kitu Chochote Kupoteza Ushahidi. Licha Ya kukutana na Harufu ile ya Manukato lakini wakakiona Kitu Kingine, kitu Ambacho Kiliwafanya Watizamane kwanza... Wakakichukua kitu kile na kukitizama.. Ilikuwa Picha, picha ya Mtu ambaye Walimfahamu, mtu ambaye Alikuwa Rafiki Yao Kwenye Mapambano... Haikuwa Picha Ya Mtu Mwingine, Bali Ilikuwa Picha Ya Mohamedi Abdallah mpelelezi Maarufu katika Africa. Wote Wakatizamana huku kila Mmoja Akishindwa Kuamini Kile Alichokuwa Akikitizama.
 
MKE WA RAIS

kitambulisho walichokikuta kwenye buti ya gari ya Mke wa Rais kilikuwa kitamburisho cha mtu waliyemfahamu... Si kumfahamu tu bali walikuwa wameshafanya kazi nAye kwa muda mrefu sana. Hawakuweza kukiamini walichokuwa wakikiona katika macho Yao. Wakatizamana kwa mara nyingine.. Wakakichukua kile kitambulisho kisha Jamila Akakiweka kwenye mfuko wake. Kutoka pale Ikulu wakaondoka kuelekea katika nyumba yao ili kumsubiri mwenzao Kapteini George Simon ili awaeleze kile ambacho wamekishuhudia. Licha ya kuelekea huko bado kitendo cha kukuta kitambulisho cha Mohamed kwenye gari la mke wa Rais kabla hajauawa kiliwafanya waanza kuiona Hatari katika kazi ambayo wameianza. Hawakutaria kukutana na MOA katika kisanga hiki.. Lakini kama walivyowapelelezi Wengine hawakutaka kumhusisha MOA moja kwa moja kwa kuwa harufu ya manukato waliyoyakuta kwenye alilotumia mke wa Rais kabla Hajauawa hayakuwa manukato Ya Kiume, bali yalikuwa manukato Yaliyopendwa sana na Watoto wakike. Na yalikuwa kwa ajili ya matumizi na Wanawake tu.. Sasa kwani kitamburisho Cha Mohamed Abdallah au MOA kwa kufupisha Jina lake Kikutwe kwenye gari hilo? Kuna uhusiano gani kwa MOA na Hili tukio la kuuawa kwa Mke Wa Rais? Yalikuwa maswali magumu ambayo hayakuwa na Majibu kwa muda na Wakati Ule. Wakaamua kuingia kazini Kudili na MOA ili kuangalia kama Watapata Chochote ambacho kitawasaidia katika Uchunguzi wao..........

Wakati wao wakiamua kumchunguza MOA, yeye ndio kwanza Alikuwa akisimamisha gari umbali wa Hatua mia nne kutoka ilipo nyumba ya mwanaume aliyeuawa kwa kupigwa Risasi na Mke wa Rais. Baada ya kuipaki gari, Moa aliongoza kwa kupitia nyuma kwa nyuma kuiendea Nyumba ile ambayo Ilikuwa Akilindwa na polisi kutokana na kuuawa kwa mwenyewe. Hakuwajali sana Askari waliyokuwepo pale wakilinda, alichokifanya ni kuendelea kutembea kwa Tahadhali kubwa huku akiwa tayari kwa chochote kile na alipokaribia kufika katika Uzia wa Jumba akashtushwa na kitu alichokiona pale Chini... Kilikuwa kitu ambacho alikuwa akikijua lakini Hakuwa anajua wapi ambapo alikuwa amepata kukiona. Kilikuwa kitufe kidogo ambacho hutumiwa sana na maafisa usalama wa Taifa. Vitufe ambavyo Vilikuwa ni Silaha Hasa pale Inapotokea Mtu husika kukamatwa ama kutaka kujiokoa.. Akakichukua kile kitufe na kukiweka Mfukoni mwa koti lake kubwa.. Akapiga hatua kwa mwendo wake wa kawaida huku mkono wake ukiigusa bastola Yake kwa kila hatua.. Kitufe alichokiona pale kilimpa picha kuwa kulikuwa na Sababu ya kuuawa kwa mke wa Rais na kama sio kuuawa na Wana usalama bali aliuawa na watu ambao walikuwa ama wakilipa kisasi ama kutaka kuficha kitu ambacho hakitakiwi kujulikana.

Sasa alikuwa Ameufikia Uzio uliozungushwa katika Jumba lile.. Akauangalia Usio ule, akajikuta Akitabasamu. Ulikuwa Uzio ambao haukuwa mrefu kumsumbua Moa... Akautizama kwa sekunde moja na Sekunde ya pili alikuwa akichupa na Sekunde ya Tatu alikuwa Akitua ndani Ya Jengo lile bila kutoa kishindo chochote. Alipotua Akatulia kwa muda akisikilizia huku na huko alipoona kuna Ukimya wa kutisha, MOA alisimama na kutembea kwa Tahadhali kuendea mlango wa Kuingilia ndani... Akachomoa funguo ambazo huzitumia mara nyingi sana katika kuifungua milango kama ile. Muda Mfupi alikuwa amekwisha Ingia ndani na Kujikuta Yupo kwenye Sebule pana na Nyeupe. Hapakuwa na Taa lakini Giza lile halikuwa tatizo kwa Macho ya MOA, ambayo Yalikuwa yamezoea giza. Akapekuwa pekuwa maeneo ya pale sebuleni, mara Akaibuka na kitu, kitu ambacho kilimfanya atabasamu.. Ilikuwa Simu ya Mwanamume... Akahisi ni Simu Ya Mwanaume Aliyeuawa kwa Kupigwa Risasi.... Akaitazama kwa Mara Nyingine kisha akataka Kuitumbukiza Mfukoni. Lakini Kabla Hajafanya Hilo akasikia sauti Ya mwanamke kutoka nyuma ikimwambia... '''Tulia kama Ulivyo na Ukijaribu Kusogea Ubongo wako ni Halali Yangu'''' MOA akatulia na Kutii.. Kisha Sauti Akamuamlisha tena Achomoe kile alichonacho na Kukitupa Chini... MOA akatii bila matatizo. Alikuwa Akipanga Jinsi ya kujiokoa Lakini Hakuwa Akijua Adui wake Yupo umbali gani.. Akaendelea kutulia Huku akiipa akili yake muda wa kuwaza na kuwazua.... Hakuwa anajua Huyu mwanamke ni Yupi.. Na Hakujua ameingiaje mle ndani. Wakati Akiendelea kuwaza na kuwazua, mara Akahisi mlango ukifunguliwa na mtu mfano wa kivuli akiingia katika namna ambayo Ilimfanya MOA atabasamu. Ulikuwa Uingiaji wa watu ambao walikuwa ni wajuzi na Wataalamu kupindukia katika medani Ya Mapigano na uchunguzi... Lilikuwa kosa kubwa kwa binti kusogea, lilikuwa ni kosa kubwa la binti Kugeuza Kichwa kutizama kule mlangoni.. Naye Alikuwa amemuona mtu Yule.. Lakini Kuangalia kwake Kulimpa MOA nafasi Ya kugeuka mithili ya Ninja na Kuachia Pigo kali Sana ambalo lilitua sawia kwenye Mikono Ya mwanamke Yule na Muda Huo huo bastola Ikirushwa na Kuanguka umbali kutoka pale walipokuwa wamesimama... Kilikuwa kitendo kilichotokea Ndani Ya Sekunde.. :
 
MKE WA RAIS



Aliingia kama kivuli ndani ya Jumba lile... Kuingia kwake hapakuonyesha kishindo wala michakato ya Miguu.. Macho yake yakakutana na kitu kilichomshtua.. Kitu ambacho kiliifanya Akili Yake Iduwae na kushindwa kufanyakazi kwa muda. Mwanamke alikuwa ameishika bastola katika mikono Yake.. Ushikaji wake wa bastola Ulikuwa katika utaalamu wa hali ya juu. Wakati Akishangaa ushikwaji ule wa Bastola, Ukaja mshangao mwingine, mshangao ambao haukuondoka kirahisi katika macho Yake. Kitu alichokifanya mwanamume aliyekuwa ameshikiwa bastola hakikuwa kitu cha kawaida. Kilikuwa kitendo cha ghafla na kilichofanyika katika kipimo sahihi. Sekunde bastola Ilikuwa imenyooshewa kwake na Sekunde ya pili bastola ilikuwa hewani baada ya kupigwa kwa teke ambalo hutumiwa sana na Mcheza Sinema wa Kimarekani Jean Claud Van Damme... Lilikuwa Teke lililouburudisha macho na kuusisimua mwili wa Kepteni George Simon.. Teke ambalo lilimkumbusha Alipokuwa kwenye mafunzo Ya Kijasusi katika Shirika la Kijasusi la Marekani CIA. Akiwa bado katika mzubao ule akajikuta akiachwa peke yake katika sebule ile kwa mbinu ambayo licha ya kuwa kwake Jasusi lakini hakuwahi Kuona utokaji wao, kwani alipokuja kugutuka Alikuwa amebaki mwenyewe katika sebule Ile pana. Akajitizama na kujisonya mwenyewe.. Hakuweza kuficha kuhusu kwake uwezo wa maadui wale.. Lakini akashangaza na ule ugomvi na mapigano katika jumba lile. Ingawa alijua kwa upande mwingine kuwa wanapambana na Adui mmoja lakini pambano la Muda mfupi aliloliona mle ndani Lilimfanya Aamini kuwa kulikuwa na pande mbili katika tukio la uchunguzi Wa kifo cha mke Wa Rais. Akaanza kuichunguza sebule ile katika Aina ya kutokuacha kitu. Alipoona sebule haikuwa na Chochote Akajikuta Akipiga hatua na Kuelekea upande wa kilipochumba ambacho alikuwemo mke Wa Rais kabla ya Kuuawa. Akakiangalia kitasa na alipotoka kukishika ili aingie akasita kwanza baada Ya Kusikia kitu kama Nyayo Za Watu, tena Zaidi ya mmoja. Akajiondoa haraka na kujibana kando Ya mlango wa Chumba cha pili kinachotizamana na Mlango wa kuingilia. Hapo akauona mdomo wa bastola Ukiwa Umetangulizwa mbele, punde wakaingia watu watatu ambao wote walikuwa wamekamatia bastola Zao... Kila kilichokuwa kinatendeka kilikuwa kikishuhudiwa na kepteni George Simon... Muda wote mkono wake Ulikuwa umepelekwa mahala ambapo aliihifadhi bastola Yake. Macho Yake Yalikuwa yakicheza sehemu Zote... Walipoingia watu wale wakaongea kitu kisha akawaona Wakitoka mle ndani na baadae akausikia mlango ukifungwa kisha Ukimya Wa Ghafla Ukatanda katika mjengo ule.

***********

Mudy alitoka katika jumba lile huku kichwa chake kikiwa kimechanganyikiwa kwa tukio ambalo limetokea mle ndani. Kitendo cha kuwekwa Chini ya Ulinzi na Mwanadada kilimshangaza sana.. Sio kwamba alichanganyikiwa kwa kuwa ni mwanamke.. La hasha kilichomchanganya ulikuwa ni uwepo wa Yule mwanamke ndani ya Jumba lile. Alikuwa nani? Alifuata nini? Na alikuwa na nani? Hayo na mengine Yalikuwa ni maswali Yaliyokiumiza kichwa Cha Mudy.... Kitu kingine ambacho kilimpa wakati mgumu Ulikuwa ni Uingiaji wa Mtu ambaye alikuwa Ameingia mfano wa kivuli.. Uingiaji wa mtu yule ulimpa Mudy uhakika kuwa tukio la kuuawa kwa Mke Wa Rais kutakuwa kunasababu nyingi.. Kumuona Mtu Akiingia katika Aina ile kulimpa picha Kuwa Yule mtu alikuwa ni Adui tena jasusi ambaye ameiva katika mbinu Zote. Hakukuwa na Watu Wenye uwezo Wa kuingia mfano Wa Yule mtu aliingia pale.. Watu pekee Wenye uwezo Wa Kufanya Vile Walikuwa ni Watu Wawili, Watu Hao Sio Wengine Bali ni JORAM KIANGO NA WILLY GAMBA (pumzikeni katika amani BEN MTOBWA NA ELVIS MUSIBA nyie ndio chachu ya mimi kuandika hadithi) watu hao ndio pekee katika ukanda huu wa Afrika na Hata Duniani kote. Kuingia kwa mtu yule kukampa picha Ya kuwa kuna siri kubvwa Juu Ya kuuawa kwa Mke wa Rais.

Kutokana na kuwaza huko akajikuta akiipata hamu ya Kuingia katika kazi ya kumgundua muuaji.. Ni hapo wakati Akijipa hiyo kazi akamuona mtu Mmoja Umbali wa Mita mia tano.. Ingawa palikuwa na Umbali mrefu Ila uwepo wa mtu yule pale na Usiku ule kulimpa Hamu Mudy Ya Kushuhudia nini ambacho kitafanywa na Mtu Yule. Akasogea kwa mwendo wa taratibu huku bastola mkononi... Akaendelea kusogea kwa kutembea katika giza, Alipofika Umbali wa Mita kama mia kutoka pale alipomuona yule mtu, alijikuta akitizamana kwa umbali mfupi na mtu ambaye alikuwa akimtizama alikuwa ni Yule mwanamke aliyepambana nae ndani Jumba muda mfupi Uliyopita. Wakati anaendelea kutizama, akamuona yule binti akiingia katika gari iliyokuwa imesimamishwa pale.. Lakini Uingiaji ule ulimfanya Mudy Autilie mashaka na kuwaza labda yule Msichana hakuwa mwenyewe. Wazo lake lilikuwa na Ukweli kwani Muda mfupi akamuona mtu ambaye alimfanya asisimkwe na Damu. Alikuwa ni Mtu Yule Aliyeingia ndani Ya Jumba Lile Mfano Wa Kivuli. Hapo akaingiwa na Hamu ya kuangalia mchezo ule ambao ungeweza kumpa mwanga na kuwajua wao ni Nani......
 
MKE WA RAIS



Mara akamuona mtu ambaye aliifanya damu yake kusisimka.. Akamuona mtu yule aliyeingia mfano wa kivuli katika Jumba lile. Na yeye alikuwa Akiisogelea ile gari.. Mudy akatulia tuli kutizama mchezo ule.. Mchezo ambao ulimpa Hamu Ya kujua watu wale ni wakina nani. Akamuona mtu yule akiifikia gari na kuufungua mlango Ili kuingia, lakini kabla ya kufanya hivyo akashuhudia yule mtu akirushwa pale aliposimama na kwenda kuangukia mbali kidogo. Kabla hajajua nini kilichotokea akamuona Yule mwanamke akishuka kutoka katika Gari Ile na kuanza kuelekea pale alipoangukia Yule mwanamume.. Hakumfikia kama Alivyotarajia, na hakuweza kupiga hatua kama alivyotaka kwani alikutana na mapigo matano Ya kung fu Yaliopigwa kitaalam na kumtupa umbali mrefu... Hapo mudy akaendelea kuangalia maoigano kutoka kwa Watu wale.. Alikuwa akiangalia ufundi na Utaalamu wa Mapigano.. Hasa kutoka kwa mwanamume Yule ambaye mapigo yake yalikuwa yakimvutia na Kumburudisha Mudy.. Yalikuwa yakimpa Uhalisia kuwa Yule mwanamke alikuwa ameingia sehemu ambayo Haikuwa saizi Yake... Kwani wakati alipopigwa mapigo yale na kuanguka Alijiinua haraka kwa kuchupa lakini kabla Hajakaa sawa ndipo alipopelekewa pigo ambalo lilimfanya atulie pale pale Chini.. Lilikuwa pigo ambalo hutumiwa sana na wapiganaji hasa wanapohitaji kukimaliza Kitu.. Mudy Hakutaka kuona mwanadada Yule Akiuawa kwani alijua kwamba anaweza kumsaidia katika Kuujua mwanga Sahihi wa Matukio Ya kuuawa kwa Mke Wa Rais.... Muda Mfupi alikuwa akichupa Angani na sekunde Ya Pili Alikuwa Akitua mbele Ya Kepteni George Simon... Wote Wakatizamana... Alikuwa ni George Aliyewahi kumtambua Mudy... Kwa Sauti Ya Kikazi Kepteni George Akaita '''MOA''' Lilikuwa Jina ambalo hakulitegemea kuitwa na Mtu ambaye hakumfahamu.. Kuitwa kwa jina lake la Siri kulimfanya Mudy Asite kidogo.. Katika kusita Huko kulitoa nafasi kwa George Kujitambulisha... ''GEORGER SIMON'' ILikuwa kauli Iliyokifanya Kichwa chake kutambua haraka, kuwa George Alikuwa mpelelezi kutoka makao makuu anayeifuatilia tukio la Kuuawa kwa Mke wa Rais na Walinzi Wake pamoja na familia Ya Mkuu Wa Usalama nchini. Kutambuana kwao kukaondoa Ule Ushari, Ushari ambao Alikuja nao Mudy baada Ya kumuona George Akimuadhibu Yule msichana. Lakini Kitu ambacho kilikuwa kikimtatiza yalikuwa ni Maswali Juu Ya Mwanamke Aliyekuwa Amemshikia bastola kule ndani na Ambaye alikuwa akipambana na kepteni George Simon hapa.. Atakuwa ni nani? Swali hilo likamfanya Amuache George Kisha Yeye kupiga hatua Kuelekea pale alipoangukia Yule Msichana... Lakini hakufika.. Hatua ya kwanza, hatua ya pili akasikia kitu kama michakato ya Miguu kilichofuatia ni mapigo mfululizo ambayo Alichelewa kuyakinga akajikuta Akianguka chini baada ya mapiho kazaa kumuingia.. Hakuchelewa kuinuka na hata alipoinuka akayaona mapigo mengine yakielekezwa kwake... Safari Hii aliyaona mapigo Yale akayakwepa kwa Ustadi mkubwa kabla ya kuachia mapigo mawili ambayo yalimuingia mtu yule na Kumtupa Chini... Hakutaka kumpa nafasi.. Akamuwahi kabla ya kusimama na kumtia teke moja la Tumboni ambalo lilimuingia Yule mtu na kumfanya Apige Ukelele mkubwa sana, huku akitepeta na Kujiinamia chini.. Wakati Mudy Anamsogelea Ili kumbana Aseme Yeye ni nani, kitu cha ajabu Kikatokea, Kitu cha Baridi kikagusa katika kisogo Chake.. Kitu ambacho Hata Akiamshwa Usingizini usiku wa manane angekigundua tu. Ulikuwa Mdomo wa Bastola ikigusa kisogo Chake, Bastola Ambayo Ilikuwa imekamatwa na Mtu mwenye Sauti Yakike.. Haikuwa Sauti Ngeni masikioni kwa Mudy, Ilikuwa Sauti ambayo aliwahi kuisikia Zaidi ya Mara Tano, Lakini hakuweza kujua kuwa Ilikuwa Sauti Ya Nani.. Akatulia kutaka kujua kitakachotokea... Bado bastola Ilikuwa Ikigusa kisogo Chake... Hakuwa na Shaka Juu ya Hilo na hukuwa na shaka na watu waliomteka, lakini sauti ya mwanamke Aliyemshikia bastola Ilikuwa ikimjia kila wakati... Wakati bado Akiwa ameshikiwa bastola ndipo palipotokea Tukio ambalo lilimuacha Mudy na Maumivu... Wakiwa bado hawajajua Wafanye nini, ghafla Wakaibuka watu watatu wakaanza Kurusha Risasi mfululizo Kuelekea pale alipokuwa amesimama Mudy na Yule mwanamke.. Mudy Akachupa pembeni lakini Wakati Huo huo Kitu cha Moto Kilikuwa kikipenya katika Bega lake la kushoto na muda mfupi baadae, Damu Ikaanza Kuvuja... Mudy hakutaka kujiuliza akajua tayari Alikuwa amepigwa Risasi.... Akaangalia pale alipoangukia, alipoona pana ukimya wa HaLi Ya Juu Akaanza Kuburuzika Ili kuondoka katika Eneo Lile Huku Akiwa na Chuki na Hasira Juu Ya Mwanamke Yule aliyemsababishia Yeye kupigwa Risasi. Akachomoa bastola yake na kusimama, maumivu katika bega lake Yalikuwa makali sana... Akatembea kwa Uangalifu Mpaka alipoliacha eneo lile la Tukio.. Kuondoka kwa Mudy na Kushambuliwa kwa Risasi na Watu wasiojulikana kulileta kurushiana kwa maneno Kati Ya Kanali Jamila na Kepteni George simon.. Kitendo Cha kumuweka Mudy Chini Ya Ulinzi na Kusababisha kilichotokea kilimkera sana Kepteni GEORGE na Moja kwa Moja Akaamua Kujitoa Katika kikosi kile....
 
MKE WA RAIS

Hakuuona umuhimu wa kuendelea kuwa katika upande wa mission ile.. Kepteni George Simon Alimuangalia kanali Jamila kwa muda wa sekunde kama mbili tatu hivi, kisha kwa heshima ya kijeshi Akasaluti kabla ya Kutaka kuondoka kwenda uelekeo tofauti na Wenzake lakini lile ambalo hakulitegemea likatokea mbele ya Macho Yake.. Hakutaka kuamini lakini alipotazamana na midomo miwili ya bastola kutoka kwa Kanali Jamila na Luteni Sevenlee. Kepteni George akagundua kuwa wenzake hawakuwa wakitania na walikuwa tayari kutimiza kile walichokusudia kukifanya juu yake. Akaachia tabasamu la kalagha, tabasamu ambalo halikuwa tabasamu sawa katika macho ya Majasusi Wale... Tabasamu ambalo lilikuwa katika shari.... Lakini hakuwa na nafasi Ya kufanya wenzake walikuwa hawacheki wala kutabasamu.. Midomo miwili ya bastola Ilikuwa Imemtazama Yeye... Wote wakaduwaa wakitazamana na kusomana.. Wote walikuwa makomandoo walioiva katika mapigano ya aina yoyote..... Wakiwa bado hawasemeshani Huku bastola zimeinuliwa kuelekezwa kwa kepteni George, Hatimaye macho Yao yaliokuwa yakitizamana yakaongea, yaliongea katika aina ya pekee ambayo niwataalamu wa fani ile ya upelelezi tu ambao wanaweza kuitambua lugha ile inayozungumzwa kwa macho.

*********

bado alikuwa akihisi maumivu makali katika bega lake la kushoto, bega ambalo risasi iliyorushwa kutoka kwa watu wawili waliowavamia ilikuwa imemuumiza sana Mudy.. Kutoka pale alikongoja kuondoka katika sehemu ile kabla hajatiwa mikononi mwao.. Licha ya kuondoka lakini bado alikuwa katika sintofahamu.. Sintofahamu ni pale alipokutana na Kepteni George Akimsulubu Yule mwanamke... Na sintofahamu ya pili nikuhusu Yule mwanamke.. Yeye alikuwa nani? Na kwanini alikuwa ndani ya Jumba lile? Maswali hayo katika kichwa chake Yakampa hamu ya kutaka kumjua Yule Msichana... Kumuacha yule msichana ni kutaka kuendelea kulifumba fumbo la mauaji ya mke wa Rais pamoja na Walinzi wake... Wazo la mwanzo lilikuwa ni kutoweka pale, lakini wazo la pili likamwambia arudi pale.. Wazo la pili lilikuwa na nguvu... Sekunde ya kwanza Shati la Mudy Lilikuwa limechanwa na Sekunde ya pili alikuwa akiifunga sehemu Aliyejeruhiwa kwa Risasi na Sekunde ya Tatu alikuwa akirudi Sehemu alipoangukia Yule msichana.. Akatembea akiwa makini kwa kila kitu, Alitembea kwa kutizama huku na kule.. Bastola ilikuwa mkononi kumuondosha yoyote... Umbali mdogo akaona kitu kilichomvutia... Ingawa palikuwa na giza lakini halikuwa tatizo kwa Mudy... Macho Yake Yalikuwa na Uwezo wa kuona katika giza lolote.... Watu watatu Walikuwa wamesimama huku wawili kati Yao wakiwa wamekamata basstola na Kuzielekeza kwa mtu mmoja...

Haikuwa kazi kwake kumtambua mtu Yule.. Hakuwa mgeni katika masuala yake.. Alikuwa ni Kepteni George akiwa amelekezewa bastola. Kitu kile kikamvutia Mudy, akataka kuwajua watu wale... Akasogea karibu kwa Zaidi, nipo alipowaona watu wale, ni watu ambao Alikuwa akiwatambua kama Anavyotambua kiganja cha mkono Wake... Mbele Ya macho Yake umbali mfupi alikuwa akitizamana na Watu wa kazi, watu ambao walizidi kumuonyesha kuwa kazi Hii Ni Nzito... Kuwaona Kanali Jamila Hassan na Luteni Sevenlee pamoja na Kepteni George kuliusisimua mwili wa Mudy.. Lakini kilichomchanganya Zaidi ni Kuelekezwa bastola Upande wa Kepteni George... Kitendo kile kilimpa picha ambayo bado hakuwa Akiipata wala Kuijua. Akaamua kufanya kilichomrudisha sehemu ya tukio.. Safari hii akiifanya kazi Yake kwa uangalifu mkubwa kuepuka kuonekana. Akayapeleka Macho Yake Sehemu ambapo aliangukia Yule msichana wakati akipigwa na kepteni George... Hapakuwa na Mtu... Akaduwaa na kushangaa... Akasogea karibu Zaidi hapo nipo alipouona mbuluziko.. Mbuluziko ambao aliamua kuufuata huku akiwa tayari kwa chochote.. Bastola Mkononi akaongoza zaidi.. Hatua kumi mbele alikumkuta mtu aliyemkusudia Akiwa amepoteza fahamu... Mudy akamsogelea pale kwa Tahadhali kubwa sana... Akainama na kumgusa katika mguso ambao haukuwa mguso tu bali kama njia ya Kugundua kama amepoteza fahamu au Amezuga.

Akakuta ni kweli mapigo ya Kepteni George Yalikuwa yamemuingia... Mudy Hakutaka Kuchelewa katika eneo lile. Akamuinua na Kumuweka begani kisha kuanza kuondoka nae katika Eneo lile... Alikimbia naye mpaka Sehemu Alipoiacha gari Yake... Wakati Anamtua Yule binti Ilikuweka Chini afungue mlango ili amuingize, Akahisi Vishindo Vikija Nyuma Yake.. Hisia Zake Hakuwahi Kuzidharau Hata Siku Mmoja.. Akageuka Kwa Haraka Huku Bastola Mkononi Tayari kwa Mashambulizi.. Akajikuta Akikutana na Teke Kali ambalo liliipiga mikono Yake na Kuitupa bastola Yake umbali mrefu.. Hapo Akajikuta Akitazamana na Kanali Jamila Hassan, Akiwa katika Ule mwendo na Sura ya Kimapigano.. Hakuonyesha kuwa na Mzaha machoni Mwke.... Mudy Akatabasamu huku akicheka, kicheko ambacho kilikatishwa baada ya kanali Jamila kurusha ngumi mfululizo Kumuendea Yeye.. Badao Mudy Alikuwa akikwepa Huku Akicheka... Hakikuwa kicheko Cha furaha Bali alikuwa katika Kiwango kikubwa Cha Hasira.... Sasa Akaamua kumuonyesha... Hakuwa na mudy...
 
MKE WA RAIS



Alikuwa akitizamana na kanali Jamila... Mudy akatambua kitu kimoja kuwa kuchelewa kwake katika kuondoka eneo lile kungesababisha kuharibu mipango yake. Sasa akaamua kumkabili kanali Jamila.. Alikuwa akimjua Jamila katika nyanja Za kimapambano... Sio mapambano tu lakini hata katika namna ya kumdhibiti mtu.. Mudy akaondoka katika mzaha, akaivaa sura ya kazi katika pambano lile.. Akatisha kumfuata kanali Jamila katika aina fulani ya Mapigano.. Kila pigo alilokuwa akirusha lilikuwa likitolewa au kukwepwa kwa ustadi mkubwa. Kila pigo alikuwa akiliona na kulikwepa.. Lakini alikuja kubugi pale aliposhindwa kuyaona mateke mawili Aina ya Martials Combart.. Mateke ambayo Yalikuwa ndio silaha ambayo alikuwa akiitegemea Mudy.. Hakuweza kuzuia nguvu Ya Mateke Yale, kwa mara ya kwanza alijikuta akiisalimia ardhi baada ya Kuanguka kama fulushi.. Akainuka haraka huku akiachia ngumi na mateke mfululizo lakini alijikuta akipiga hewa na Dakika moja baadae ngumi Mbili nzito Zilitosha Kumzimisha Kanali Jamila, akatulia Chini Huku akiwa amepoteza fahamu... Mudy Hakutaka kusubiri, Akambeba yule Msichana na muda mfupi baadae alikuwa njiani akielekea Maeneo Ya Nje ya Jiji la Dar es salaam. Hakutaka kwenda nyumbani kwake kwa kuwa hakupenda na wala hakuwa akiuamini Usalama wa nyumba ile.

*********

Katikati Ya Jiji la Dar es salaam Katika Jengo la Ofisi fulani watu watano walikuwa wameizunguka meza kuonyesha kuwa kuna kitu kizito ambacho walikuwa wakitizamana... Muonekano wa watu wale ulikifanya Chumba kile kuwa kimya huku zikibaki kusikika sauti za viyoyozi... Machoni mwa watu wale kulikuwa na Ishara Ya kila Hatari.. Kutokurudi kwa msichana ambaye alikuwa akiwajua na Kujua baadhi ya Siri Zao, Alikuwa amepotea katika mazingira ambayo Yaliwatia Hofu. Kuonekana kwa mwanamke Yule mara ya mwisho akiwa na Mpelelezi mashuhuri Mohamed Abdallah, kuliwaumiza na kuwatisha sana... Wakauona Mwanzo wao mbaya katika Suala Hili... Licha Ya kuizunguka Meza ile lakini bado hakuna hata mmoja ambaye aliufumbua mdomo wake kuzungumza chochote.. Kila mmoja Alikuwa kimya katika kutafakari.. Kitendo cha kujua kuwa Mudy Ameingia katika Suala Lile.. Kuliwapa kiwewe na kuuamua kuitisha mkutano wa haraka.. Mkutano ambao bado haukuwa tayari kuanza.. Wakiwa wameinama katika tafakuli Zito Huku ukimya Ukitawala, mara Wote wakainua vichwa vyao kutizama mlangoni... Wote wakasimama Baada Ya kumuona mwanaume wa makamo akiingia katika chumba kile.. Alikuwa mwanaume mkakamavu sana, licha Ya umri Mkubwa Alionao lakini bado alionekana kama Kijana... Alikuwa akiingia ndani huku uso wake Ukionekana kutokuwa na tabasamu. Alitembea kwa mwendo wa kujilazimisha mpaka alipokifikia kiti na kukaaa... Alipokaa kila mjumbe alikuwa kimya akisikiliza kipi ambacho kitazungumzwa na Mkuu wao.... Kile walichokitegemea ndicho walichokutana nacho... Mwanaume Yule akawatazama wote kwa pamoja kisha kwa sauti Yake nzito Akawauliza juu ya taarifa ambayo wanayompaka sasa Kuhusu kutekwa na kuonekana kwa mwanamke Huyo akiwa sambamba na mpelelezi Mohamed Abdallah..... Wote hawakuwa na Majibu na kila mmoja alikuwa amehangaika kila Sehemu tokea kulipokucha lakini hawakufanikiwa kujua wapi alipo Mudy na Msichana Yule mpaka Muda ule.. Licha Ya kutokumuona kwao lakini Hata Vijana Wao ambao walitumwa kuichunguza Nyumba Ya Mohamed kwa Siri wakiangalia anayeingia na Anayetoka Bado Hawakuwa wamemuona Mpelelezi Huyo.

Majibu Hayo Ya Vijana wao waliowasambaza katika Jiji lote la Dar es salaam na mikoa Ya Jirani kuwa hawajapata Kumuona Mohamed Kuliibua mjadala mkubwa katika kikao kile. Kila mtu alikuwa akilaumu kwa Upande Wake.. Hawakuwa Tayari Kusikia mwanamke Yule Yupo mikononi Mwa Mohamedi.. Kilichofikiwa katika Kikao kile nikuendelea kusambaza Vijana katikati Ya Jiji na Sehemu Zote Za Mahoteli Ili kuendelea kumuangalia Mohamedi..

*****

Alishtushwa na Mwanga wa jua ambalo lilikuwa likimmulika Machoni mwake kwa kupitia katika upenyo wa Dirisha. Akafumbua macho Yake katika Aina fulani:.. Akashangaa kukuta akiwa amelala katika Chumba kizuri na Nadhifu.. Chumba ambacho kilionyesha kuwa alikuwa yupo katika Hoteli. Akaituliza Akili Yake katika kujua Alifikaje pale.. Akautazama Mwili wake Akakuta kulikuwa na Michubuko mbalimbali katika Mwili.. Akayafumba Macho Yake na kuivuta kumbukumbu.. Kumbukumbu Yake ikamrudisha Alipokuwa ndani Ya Jumba la Bosi wake.. Bosi Ambaye alimpa Dili la kumuua Mke Wa Rais.. Akakumbuka Alipomuona Mtu akiingia katika Aina fulani Ya Kuogofya.. Alipofikia Hapo Akafumbua Macho Yake tena na Kuanza Kuangalia Huku na huko katika namna Ya kujua Yupo Wapi.. Macho Yake Yakatua Juu Ya meza na kukutana na Bastola Yake Ikiwa pamoja na Vitu Vyake... Akainuka na Kuendea ile bastola.. Akaitizama kwa Muda kisha Akajikuta Akitabasamu... Akageuka Nyuma Ili arudi Tena pale kitandani... Akashtuka lakini muda huo huo akauficha Mshtuko Ule.. Alikuwa Akitizamana Uso kwa Uso na MOA.... Akiwa katika mavazi Ya Mazoezi.... Wakatizamana kwa Muda Kabla Ya Kila mmoja kutabasamu... NOMAAA
 
MKE WA RAIS

Alikuwa akitizamana na sura ya mwanaume, sura ambayo haikuwa ngeni katika macho yake. Mbele yake Alisimama Mudy Akiwa kwenye mavazi Ya Mazoezi.. Mikononi mwake alikuwa amekamatia Sinia ambalo lilikuwa na Vikombe viwili vya maziwa... Mwanamke Yule akaganda kama sanamu.. Hakuwa akiamini kile alichokuwa akikiona mbele Yake. Licha ya kuishika bastola yake katika mikono yake lakini alikuwa ameshindwa kuitumia.. Muda wote Mudy alikuwa akitabasamu.. Tabasamu ambalo halikuweza kumlewesha mwanamke Yule na kumfanya amuamini Mudy.. Tabasamu ambalo lilikuwa tofauti katika macho Ya mwanamke Yule.. Mudy Hakumjali mwanamke yule.. Akaufungua Zaidi mlango na kwenda kulitua sinia lile katika meza Ile.. Muda wote alikuwa akitembea katika umakini wa hali ya Juu... Aliujua uwezo wa mwanamke Yule.. Ingawa hakuwahi kupambana naye lakini alishuhudia pale alipokuwa akipambana na kepteni George. Alipolitua Sinia lile akageuka Kutaka kumwambia mwanamke Yule asogee pale mezani.. Lakini Akashtuka baada Ya kukutana na midomo miwili ya Bastola Ikimtizama katika kichwa chake. Ingawa alikuwa akijiamini katika mapambano lakini Hakutarajia Kuiona bastola tofauti na Ile ambayo Aliiona pale mwanzo. Mudy Akaendelea kutabasamu kama hakukuwa na kitu cha hatari mbele yake.. Tabasamu ambalo lilivuka na Kuwa kicheko.. Kicheko chake kikaifanya Sura Yake Iwe katika mikunjo... Lakini kwa mwanamke Yule kicheko kile kilimfanya akipeleke kidole Chake katika kiwambo cha kuruhusu kutoka kwa Risasi... Hakuujua Uwezo wa Mudy na Hakumjua Mudy ni nani... Hakuipata nafasi Ya kuifyatua risasi yake... Sekunde mbili alikuwa Chini Ya Sakafu baada ya kupigwa Pigo moja la karate ambalo lilimmaliza nguvu na Kumfanya abaki pale chini Akitweta....

Mudy Hakutaka kumuendea pale na Vile vile hakutaka kumuua kwa kuwa alijua binti Yule alikuwa akijua mambo Mengi sana katika kisanga kile cha kuuawa kwa mke wa Rais.. Akamuendea pale alipoangukia kwa Sura Ya Upole.. Akamuinua na kumkalisha.. Akaanza kumfuta damu Iliyokuwa ikivuja ikitokea Puani...Kumfuta damu Mwanamke Yule kulimfaya Mudy Akumbuke Tukio ambalo Hatokaa Alisahau. Tukio ambalo litaendelea kubaki katika kumbukumbu Zake... Hasa pale aliporudi nyumbani na kuukuta Mwili wa mkewe na mwanawe kipenzi Wakiwa wamechinjwa. Ni Kisa hicho kilichomfanya awahurumie wanawake.. Licha Ya kuwahurumia huko lakini Bado alikuwa katili kwa kila mwanamke ambaye atakuwa kinyume na Sheria.. Akaifuta Ile damu Ya mwanadada Yule na baada ya Muda walikuwa wamekaa katika Meza Moja wakinywa maziwa Huku Waiongea Hili na Lile kama Watu ambao walikuwa wakifahamiana tokea Zamani.

*******
muda wa dakika kumi mbele wakaonekana wanaume wawili wakitoka katika hoteli ile.. Walikuwa wanaume watupu ambao walikuwa katika mavazi ya kanzu huku vichwa vyao vikiwa vimefunikwa kwa baraghashia.. Wakati Watu wake wakiondoka wakapishana na wanaume wengine watano ambao walikuwa Wamevaa mavazi meusi. Kupishana kwa Wanaume wale kukawafanya wanaume waliovalia Kanzu na baraghashia kutabasamu... Watu wale Watano Wakaingia katika Hoteli ile.. Kila mmoja alikuwa ameupeleka mkono wake Mfukoni.. Hawakuuliza mapokezi bali wakaongoza moja kwa Moja mpaka ghorofa Ya pili ambapo kulikuwa ndipo kwenye kitu walichokuwa wakikihitaji. Safari Ya Wanaume wale Ikaishia kwenye mlango Wa Chumba ambacho alikuwemo Mpelelezi mashuhuri Mohamed Pamoja na Mateka wake.. Kuufikia Mlango kukafuatiwa na Kitendo kingine cha Kuburudisha Machoni katika Kuutazama.. Mlango Ulipigwa teke kisha kila Mmoja Akizama ndani Huku akiruka samasoti na Kuangukiwa upande Mwingine.. Ukimya Wa Ajabu ukatawala Mle ndani.... Hata pale wanaume wale kila mmoja alipoingia hawakukuta kitu chochote Cha maana Zaidi Ya damu ambayo Ilionekana kusambaa katika Chumba kile. Wote Wakachoka Huku wakitizamana... Walikuwa wameachwa katika Mazingira Ambayo Kila mmoja akajua kuwa walikuwa wameingia katika Vita na Mtu mmbaya na mwenye mbinu kali Kushinda wao... Mmoja wa Vijana Wale akatoa simu na kuongea maneno mawili matatu Kisha Akakata..
*******
wanaume wale ambao walionekana katika mavazi Ya kanzu hawakuwa wote wanaume bali mmoja alikuwa mwanamke na Mwingine alikuwa mwanaume. Hawakuwa wengine bali alikuwa mohamedi na Yule mwanamke wakiondoka katika staili ambayo Ilikuwa vigumu Kushtukiwa. Na hata walipopishana na Wanaume wale watano walikuwa wamewatambua..

Safari Yao ikaishia maeneo sinza Mori, Wakatafuta Guest moja nzuri Wakalipia kwa kuandikisha MaJina ya Bandia, muda mfupi baadae walikuwa katika chumba kizuri Wakiwa wao wenyewe wawili... Mohamedi akamsaidia mwanamke Yule kulivua lile vazi kisha wakakaa kitandani Wakitizamana Huku kila mmoja Akisoma mawazo Ya Mwenzie... Walitizama kwa muda kisha Mudy akasimama na Kusogea pale ambapo Alikuwa amekaa Yule msichana, lakini hakufanikiwa kumfikia kwani Alishangaa mwanamke Yule Akijirusha na kumsukuma, Hapo hapo Akashangaa kumuona mwanamke Yule akivuja Damu katika Paji La Uso huku ametambalanyika Chini..
HALI ILITISHA SANA...
 
MKE WA RAIS



Risasi ilikuwa imepenya katika paji la uso la mwanamke Yule na kumtupa umbali wa hatua mbili.. Macho ya Mudy yakatua kwenye jambo lile.. Risasi ilikuwa imepigwa kwa kupitia Dirishani.. Risasi ambayo ilimrudisha Mudy katika giza, giza totoro la kushindwa kupata chochote. Mwanamke Yule alikuwa Amelala katikati ya Dimbwi la damu.. Hakuwa na Uhai tena.. Mudy akaona ni Wakati wa kuondoka Eneo lile... Hakutaka kupitia mlango wa mbele bali alichokifanya ni kuondoka kupitia mlango wa Nyuma. Bastola ikiwa tayari kumlipua mtu yoyote Yule.
Alitembea huku akiwaza hili na lile.. Alianza kuuona ugumu wa kazi Yake, kuuawa kwa mwanamke yule mbele yake kulionyesha kuwa watu hao ni Hatari na kama wange hitaji kumuua yeye wasingeshindwa. Kutoka Sinza Mori alichukua bajaji mpaka maeneo ya Sinza africasana, alishuka na kuingia katika duka moja ambalo lilikuwa limefunguliwa asubuhi hii.. Alipoingia katika duka lile akachagua mavazi mawili matatu na kutoka katika duka lile na kuvuka upande wa pili na kuingia katika pub moja maarufu iitwayo Hongera pub... Wakati akikaribia kuingia katika pub ile, macho Yake yakawanasa watu wawili ambao walikuwa upande wa pili kule alipotoka.. Kwa kuwaangalia tu kwa macho Ya kawaida ungedhani ni watu wa kawaida, lakini kwa watu mfano wa mudy, Walikuwa ni Watu Zaidi ya watu wakawaida. Hawakuwa watu wa kawaida kwake na walikuwa pale kwa kitu ambacho Mudy alikijua . Akatembea mwendo wa kawida na kuingia katika pub ile. Alipoingia hakusimama bali alijichanganya na watu mpaka alipofikia mtaa wa pili ambapo ulikuwa ni mkabala na Chuo Cha Ustawi wa Jamii pale kijitonyama. Hapo akaingia katika Uchochoro fulani ambao ulikuwa ukimrudisha katika pub ile lakini safari hii kwa Njia tofauti na Kwa upande wa pili... Alikuwa makini kwa kila Hatua na alikuwa haraka kwa kila kile ambacho alikuwa akikiwaza... Hatimaye Akaingia tena katika pub ile kwa siri kubwa na kutulia akiangalia kule alipotokea... Macho yake yalikuwa Yakiangaza kuangalia kila Atokaye na Aingiae.. Watu waliokuwa Wakimfuatilia Hawakuwepo... Akatabasamu Kisha Akaagiza Supu Ya Utumbo wa Kuku.... Muda mfupi Mhudumu Alikuwa amefika akiwa na bakuli la Supu... Akaliweka Juu Ya meza Kisha kumkaribisha Mudy... Ni wakati Huo akitaka kulipeleka bakuli mdomoni Akawaona Watu Wawili wakiingia.... Uingiaji wa watu wale eneo lile Ulimshangaza sana Mudy... Kushangazwa kwake ni pale alipomuona Mwanamke Ambaye Aliuawa wakiwa wote Chumbani Akiwa hai na Alikuwa amesimama katika Mlango wa pub Ile.. Lilikuwa Tukio lililomtia kimuhemuhe na hamu ya kujua ni kipi kilichotokea pale Hotelini.. Kupigwa kwa Risasi kwa Mwanamke Yule Kisha Kuonekana pale, kulimsisimua Mudy.. Akaliona eneo lile Likiwa Hatari kwake.. Aliinuka bila hata ya kuinywa Supu Yake... Sekunde kadhaa alikuwa Kwenye Gari linalofanya Safari Zake kati Ya Mwenge na Posta, akielekea posta...

********

Kanali Jamila alikuja kushtuka dakika Hamsini baadae akajikuta akiwa Amelala katika chumba tulivu huku pembeni Yake wakiwa wamesimama Luteni Sevenlee na Kepteni George Wakimtizama katika aina fulani ambayo Macho yake Yalikuwa Yakimsoma kila Mmoja... Hapo ndipo alipokumbuka Mapigo Mawili ambayo alipewa na Mudy.. Mapigo ambayo Yalimfanya ainuke na Kuanza kuzunguka katika chumba kile. Alikuwa Akienda huku na kurudi kule.. Hakufurahishwa na kipigo alichokipata kutoka kwa Mudy... Kila mmoja katika chumba kile alikuwa akimuangalia Jamila... Alionekana kuzama katika mawazo mazito Sana... Bila kusema kitu aliiendea bastola yake, akaichukua na kuichomeka katika kiuno chake kisha kuufungua mlango na Kutoka nje.. Alitembea mpaka alipoikuta gari Yake.. Akaifungua na kuingia ndani yake, akaliwasha na kuliondoa gari Moja kwa moja kuelekea Katikati Ya Jiji la Dar es salaam. Hakuwa mtu wa kutabasamu wala Kucheka tena,, hakufurahishwa na kile kilichotokea Wakati Akipambana na Mudy. Kutoka na Mawazo Aliyokuwa nayo, Alijikuta Akifika kivukoni bila Kutarajia... Akaipaki Gari Yake Pembeni mwa kituo cha Polisi.. Akashuka na kwenda kukaa Juu ya Ukuta uliyokuwa umejengwa kando kando Mwa Bahari Ya Hindi... Hakujua Kipi ambacho kilimpeleka pale.... Aliendelea kukaa huku akiangalia kila Mtu ambaye alikuwa Akitoka na Kuingia Kivukoni... Alifanya hivyo Kwa muda wa dakika kadhaa mpaka pale macho Yake yalipokutana na kuvutiwa na mwanaume ambaye Alikuwa amevaa Kanzu na Baraghashia.. Ingawa Mwanaume Yule alikuwa amejibadilisha sana lakini bado hakuweza kumpoteza Jamila... Macho Yake Yalikuwa Yakimtizama Mudy, Mudy ambaye alikuwa amejaribu kujibadili Ili kutojulikana... Alimuangalia Mudy Mpaka alipoingia katika Uzio Wa kivuko... Naye Akasimama na Kuanza kumfuatilia kwa Nyuma Huku Akihakikisha kuwa Mudy Hapotei Katika Macho Yake. Muda wote mkono Wake Ulikuwa Ukipelekwa sehemu palipo na bastola, Hakuwa Mjinga wa kutaka kumuamini Mudy. Wakati akiwa macho Yake Ameyaelekeza Upande ambapo alikuwa Amesimama Mtu Wake, Akashangaa Kuwaona Watu Wengine Wawili Wakiwa pale Tena Wakimtizama Mud
 

Similar Discussions

24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom