Riwaya: Mke wa Rais

MKE WA RAIS

SEHEMU YA 023

Mudy akaondoka pale kuzuga kama ataona akifuatiliwa na watu katika eneo lile. Hakuwa mbali na hisia Zake, kwani kupiga kwake hatua ya kwanza macho yake Yakanasa watu wawili wakiondoka kutoka miongoni mwa watu waliokuwa wamekusanyika pale, lakini wao wakizuga kama hawajuani na kila mmoja alikuwa akipita njia yake. Kilikuwa kitendo kilicholeta msisimko mkubwa sana.. Msisimko ambao uliongezeka baada ya kumuona mtu mwingine wa tatu akitokea mbele yake kufuata usawa wake.. Hakumjali wala kumtizama, lakini angalia ya mtu wa mbele ilimfanya kukigeuza kichwa chake kutizama mbele.. Akaziona gari za polisi Zikiingia kwa fujo eneo la msiba Huku Askari Wenye Silaha nzito wakishuka mithili ya makomandoo na kusambaa Huku na huko.. Mudy hakuhitaji kusoma au kuambiwa chochote kujua kuwa Askari wale walikuwa wamemfuata Yeye na ile ilikuwa ni Oda kutoka kwa mawaziri wale. Hakutakiwa kuchelewa kuondoka katika Eneo lile lakini angeondokaje Wakati kuna wakora wawili wakimfuata kwa nyuma? Hapo ndipo alipoongeza kwendo huku hisia na Masikio YaKe Yakiwa makini kusikiliza Ama kuhisi Vishindo vya watu.. Akamvuka mtu Yule Aliyekuwa Anakuja mbele Yake, akapiga hatua mbili tatu bila kugeuka Nyuma.. Kuifikia hatua Ya nne Akasikia sauti Ikimuita kwa Amri Zote, lakini kabla Hajaamua Kutii ama kutokutii,,, akashtukia gari Ikisimamishwa mbele yake Huku mlango ukifunguliwa kwa kasi ya Ajabu... Mudy akajitupa ndani Ya gari na Muda huo huo gari Ikaondoshwa kwa Mwendo Ule ule iliyokuja nao huku Nyuma wakiacha Risasi Zisizo na Idadi Zikimiminwa kama Njugu, kuelekea kule inapoelekea gari Ile.

Gari Ilikuwa Ikiendeshwa kwa kasi ya Hali ya juu... Mudy Akageuza kichwa kumtizama Dereva Huyo ambaye aliyaokoa maisha Yake.. Akapigwa na butwaa baada ya kugundua kuwa Dereva ni Yule Yule mwanamke Mwenye Baibui.. Mshangao uliyompata Ulisababisha Ajipapase kwanza kama Alikuwa na Bastola ama lah.. Akazikuta bastola Zake Zikiwa Zipo pale pale.. Mwanamke Yule Hakumjali Mudy wala kumuangalia.. Alichokuwa akifanya ni kubadili gia na kukanyaga mafuta.. Kuja kutahamaki walikuwa maeneo Ya Tandika... Hapo wakaingia barabara Ya vumbi na Muda Mfupi baadae Walikuwa wakisimamisha gari Maeneo Ya Buza Kanisani kwenye Jengo moja ambalo halikuwa geni machoni mwa Mudy. Mwanamke Yule bila kujifunua Lile baibui akashuka kisha akamtaka Mudy naye afanye vile... Mudy akashuka na Muda mfupi Walikuwa wakiingia Ndani Ya Jengo lile.. Licha ya Mudy kulijua jumba lile kwa nje, lakini hakuwa analijua kwa ndani.. Kiingia kwake ndani na kukutana na Ukimya Ule wa Ajabu Mudy Akajiweka tayari kwa chochote ambacho kingetokea.. Aliendelea kutembea mle ndani Huku akiwa nyuma Ya Yule mwanamke mwenye baibui na Juba.. Alikuwa akiitizama Hatua moja baada Ya Nyingine Ya mwanamama Yule.. Si kuangalia hatua tu bali kila wakati alikuwa akiyatembeza macho Yake katika staili ya kipelelezi kila sehemu kuangalia kama Angeweza kupata Chochote kitu ambacho kingemsaidia katika upelelezi wake....

Baada ya kutembea kwa muda wakatokea katika upande mwingine.. Lakini kilichomshangaza Mudy, ni upande ule waliyotokea.. Haukuwa Upande Wa Nyumba bali walijikuta wakitokea nje tena kwenye mtaa wenye watu wengi tofauti na kule mwanzo.. Kitendo hicho kilizidi kutengeneza maswali katika maswali Ya Mpelelezi Mudy.. Sasa alikuwa akianza kuipata picha Ya mtu aliyenae... Kutokea pale mtaani tena kukiwa na Mchanganyiko na mkusanyiko wa watu kukampa Mudy Mashaka.. Akajua labda kuna Watu watakuwa wanawafuata lakini Haikuwa hivyo.. Kila ulipoyapeleka Macho Yake kwa Hila.. Hakuweza Kumuona Mtu yoyote Akiwafuatilia. Baada ya kuumaliza Ule mtaa sasa Walikuwa Wakiingia katika Nyumba ambayo tokea aanze kutembelea maeneo yote ya Dar es salaam.. Hakuwahi kuiona Sehemu Ile hata Siku Moja.. Licha Ya kutokuijua Nyumba ile lakini watu wachache AliOwaona nje Ya Nyumba Ile wakaanza kumtia Wasiwasi.... Macho Yake Yaliyozoea kuwasoma majasusi sasa Yalikuwa yakikutana na Watu hao tena wakiwa Hatua mbili ama tatu kutoka alipo yeye... Mudy akashangazwa na Hilo ma licha Ya kushangazwa na Hilo lakini pia alishangazwa na aina Ya Watu wale.. Hawakuwa Wakimtizama kabisaa... Hatua nne mbele baada ya kuwapita Watu wale, Akakutana na Mtu ambaye kwa mara Ya kwanza akatabasamu.. Lilikuwa tabasamu Shadidi kutoka kwa Watu Wanaotambuana.. Mbele Ya Macho Ya Mpelelezi Mudy alikuwa Akitazamana na Mku wa kitengo Cha Kijasusi ndani ya Usalama Wa Taifa Mr FRAIDY WELLAH..

Licha Ya kukutana pale lakini Hawakusalimiana, bali alipewa Ishara Ya Kuendelea kumfuatilia Mwanamke Yule mpaka hapo watakapofika Sehemu ambayo alitakiwa kufika. Mudy Hakuwa mbishi, bado aliendelea kumfuata Yule Mwanamke mpaka Pale Walipofika kwenye mlango Wa Chumba Fulani ambapo kwanza Alitakiwa Kusimama na Kisha Kuchukuliwa kwa Silaha Zake alizonazo kisha Akaruhusiwa Kuingia ndani tena peke Yake.

Mudy Akatii.. Akaingia huku akijisemea moyoni, LIWALO NA LIWE... Hapo Akakutana na Mtu ambaye Hakumtegemea.. Hakuwa mtu Mwingine bali RAIS WA NCHI....
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 24

Alikuwa amesimama akitizamana na mtu ambaye hakuamini kama anaweza kumuona wala kumkuta pale. Alikuwa akitizamana na Rais Wa Nchi, Nchi Yenye Amani Iliyoingia kwenye Simanzi kwa kifo cha mke wa Rais. Alimjua rais kitambo tokea akiwa waziri.. Aliujua Uchangamfu wake na Mzaha wake.. Lakini siku ya leo hakuwa Yule aliyemzoea.. Hutu alikuwa mtu mwingine mwenye mawazo kupindukia. Mtu ambaye alionekana kupoteza ule mwili wake alionao.. Rais alikuwa amedhoofu mwili.. Mudy akajua Rais alikuwa katika kiwango Cha juu cha mawazo.. Ni kweli lazima awe na mawazo.. Mawazo ambayo yamempa kihoro cha kuhisi na Kudhania kuwa Kuna watu walikuwa Nyuma Ya kifo cha mkewe na Walinzi wake.. Pia alihisi watu hao walikuwa na Uwezo wa kumpindua. Mudy akasimama kwa unyenyekevu mbele ya Rais... Lakini bado Rais hakuwa ana muangalia... Muda mfupi alichomoa kitu kama mfano wa Bahasha Ya kaki na kumkabidhi Mudy mkononi huku akisindikiza na Maneno ambayo Yaliuonyesha Uchovu na kukata tamaa kwa Rais wa Nchi... '' Chukua bahasha hii kuna kila kitu ambacho kitakusaidia kumvumbua muuaji wa mke wangu. Nilimpenda mke wangu lakini nadhani alidanganywa na watu.. Naomba umtafute Aliyemdanganya mke wangu.. Siku Ukirudi hapa naomba uwe na Majibu ama ufumbuzi wa Suala hili. Baada Ya Rais kumaliza tu kuongea, mlango ukafunguliwa kisha Mudy Kutolewa na Mwanamke Yule aliyevaa Baibui. Safari Hii hakuwa na wasiwasi lakini Mawazo Yake Yalikuwa Yakiwaza kile kilichopo ndani ya bahasha aliyopewa na Mheshimiwa Rais.

*********

kuchoropa kwa mudy katika mikono Yao kuliwaumiza sana mawaziri wale. Licha ya kuumia pia walikuwa wakihofia kwa siri Zao kujulikana na kufikishwa sehemu ambayo ingekuwa mbaya kwao. Wote walikuwa wakimjua Mudy. Wote walikuwa wakitambua uwezo wake katika Suala la Ujasusi.. Walimjua mudy katika kupambana na hata kuua.. Na walipofikiria kuwa Mudy ameshawajua na kuwagundua kuwa wanahusika na kile ambacho kimeikumba nchi hii.. Kikao Cha Dharura kikaitishwa Huku kikihudhuriwa na Viongozi Wa ngazi Za Juu kutoka katika Jeshi, Polisi na Taasisi nyingine Za kiusalama. Kila kiongozi alishtushwa na kikao kile kwani kila mmoja hakuwa ameambiwa Uwepo wa kikao kile. Muda mfupi ukumbi wao wa siri Ulikuwa Umejaa watu Wote wakiwa kimya Kumsikiliza Mwanaume Yule Yule, mwanaume mkakamavu na Mwenye Sauti Na Amri kubwa katika nchi hii... Wote walikuwa kimya wakimtizama Yeye. Kwanza alianza kwa kuwaeleza kile kilichotokea Muda Mfupi Uliyopita na haswa kule kunaswa kwa Mudy katika Chumba Cha hotel fulani kule masaki na Kutoroka mikononi mwa Watu wao watatu tena Wazito katika Nchi hii. Kwahiyo kutoroka kwa Mudy mikononi mwa Watu wetu ni dalili mbaya kwa upande wetu.. Na hata tulipomfuatilia na kumuona msibani bado alikufanikiwa kuwatoroka Vijana Wetu tena kwa kusaidiwa na Mtu ambaye watu wetu wa usalama Wanahisi ni Mlinzi binafsi Wa rais. Pia Rais hajulikani alipo na kama ni kweli Mudy Atakuwa ametoroshwa na Mlinzi binafsi Wa Rais, basi hali itakuwa tete kwa upande wetu hasa kama mudy ataamua kwenda kumwambia Rais juu ya Kile alichokiona. Tukiondoa Hilo kuna mtu mwingine ambaye anasemekana ni mtu kutoka Usalama wa Taifa ameonekana kwenye kampuni yetu Pale mlimani city na Mbaya Zaidi amefanikiwa kumteka Msichana Ambaye tulikuwa tukimtegemea katika kuendesha mawasiliano Kati Yetu na baadhi Ya wafanyabiashara na Wabia wetu katika mpango Huu.

Hivyo basi ni lazima watu hawa wapatikane ndani ya muda mfupi ujao.. Kumbukeni tunalifanya hili bila kuwepo wakuu wengine, sasa tukishindwa kufika katika malengo na kumruhusu Mohamed Azungumze na Rais, Basi muda mfupi Ujao tutakuwa wafu tena tukiwa tumehukumiwa kunyongwa. Ni lazima tumnyamazishe Mudy, ni lazima tumuwahi Yule msichana na nilazima tumuue Yeyote ambaye ataonyesha dalili ama nia ya kutufuatilia katika mpango wetu huu... Mimi nikitoka hapa naelekea Ikulu kuchunguza wapi alipopelekwa Rais.. Na Nyie mkitoka Hapa Sambazeni Vijana Wetu tuhakikishe tunawapata watu hawa... Haya Wote Tutawanyike.... Huku tukijua tumeingia kwenye mapambano.. Alimaliza Kuongea Kiongozi Yule kisha Wajumbe Wote wakaanza kutoka ndani ya Ukumbi na kusambaa kunakojulikana. Ili kuuandaa mpango wa kuwanyamazisha Mudy pamoja na Wengine.

********

Wakati Wao wakimjadili Mudy; huku Upande wake Mudy alikuwa Hotelini akichambua zile kalatasi ambazo alipewa na Rais. Kile alichokuwa akikiona ndani Ya kalatasi Zile kilimfanya asisimkwe na damu.. Hakuwahi kufikiria kile alichokiona kwenye makalatasi Yale. Yalikuwa mawasiliano kati ya mke Wa Rais na Watu wengine, Watu ambao hawakuwa katika majina yao Rasmi bali yalikuwa majina ya kiherufi na Hata unapoangalia jina kwenye usajili huwa kunaonekana Herufi ama Jina ambalo halikuwa likifahamika. Wakati anafungua kalatasi nyingine Ili kutazama kilichokuwemo ndani, mlango ukasukumwa kwa nguvu kisha kwa kasi wakaingia watu wakiwa na Silaha mikononi.. Mudy akaruka na Kutua Nyuma Ya kitanda huku bastola Yake ikiwa tayari mkononi...

Akatulia
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 025

Wakati anaendelea kutazama kilichokuwemo kwenye makablasha aliyopewa na rais, Mlango ukafunguliwa kwa kasi watu wenye silaha wakaingia kwa kasi ile ile.. Mudy alikuwa amewahi kuruka na kuangukia Nyuma ya kitanda huku bastola Yake ikiwa Imara mkononi. Akatulia kuwaangalia watu wale katika namna ambayo walionyesha kuhamanika kutokana na kutokumuona Mudy. Hawakujua alipo mudy na hawakujua Jinsi alivyojitoa pale.. Muda Mfupi baadae Bastola ya Mudy Ikakohoa Mfululizo.. Watu watatu wakaanguka chini wakiwa wanavuja damu. Mudy akainuka kwa samasoti na kutua sehemu nyingine kutoka pale alipo. Bado bastola yake ilikuwa mkononi alipowaendea maiti wale na kuanza kuwasachi mifukoni.. Alichukua kila alichokiona kina Umuhimu kisha Muda mfupi alikuwa Akiondoka katika Chumba kile akiwaacha maiti wale wakiwa wamelaliana. Kutoka pale hoteli safari yake ilimpeleka mpaka maeneo ya vingunguti.. Akatafuta guest ya kawaida na baada ya kupata akalipa na kuingia Chumbani... Muda mfupi alikuwa akipangua na kupekuwa baadhi ya kadi na vitambulisho ambavyo vilikuwa ni moja kati ya Vitu alivyovichukua kutoka kwa Maiti Wale.

Kila alichokuwa akikichukua alikuwa akikisoma kwa umakini mkubwa... Hakutaka kudharau kila alichokiona kutoka katika mifuko ya wakora wale aliyowaua kule hotelini. Katika kuangalia huko akakutana na picha ya mwanamke Mzuri Sana.. Alikuwa mzuri kuliko wale ambao hakuwahi Kuwaona au kuwa nao.. Licha Ya Uzuri wa mwanamke Yule, lakini hilo halikumvutia katika picha ile. Kilichomvutia ni kule kuliona neno WANTED katika picha ile. Neno ambalo lilimpa ugumu kidogo katika kujua kwani picha ile Iwe na neno kama lile. Aliendelea Kuingalia Ile picha kwa muda huku akiwaza hiki na kile mpaka pale ambapo aliamua kuigeuza ile Picha kwa nyuma. Hapo ndipo alipokutana na namba ya Simu na namba ya Nyumba ya mwanamke Yule... Mudy akatabasamu. Baada Ya kuridhika na Kile alichokiona akayachukua makablasha Aliyopewa na Rais na kuanza kuyapekua.

*******

Ulikuwa muda mzuri kwa kepteni George na Luteni Sevenlee kuelekea kwenye hoteli alipowekwa yule msichana mfanyakazi wa kampuni ya Simu Ili kumdodosa mawili matatu kama wataweza kupata mwanga katika Kazi Inayowakabiri. Walikuwa bado hawakupata Usingizi lakini waliona ni lazima waende kwanza wa kamuhoji mwanamke yule. Gari ilitembea kwa mwendo wa Taratibu Huku wakitizama huku na huko kuona kama wanafuatiliwa, lakini haikuwa hivyo.. Walipofika maeneo ya Morocco wakashangaa wakipitwa na gari moja kwa kasi sana.. Kasi Ya ile gari Iliwafanya kepteni George na Luteni Sevenlee watizamane kwa muda. Lakini kwa kuwa walikuwa wakiwahi sehemu wakaona waongeze Mwendo Ili kuwahi sehemu husika. Wakiwa hatua Hamsini kutoka Ilipo hoteli alipowekwa Yule Mhudumu, wakaiona ile gari Iliyowapita kwa kasi pale Morocco ikiwa imepaki pale. Kengele ya Tahadhali Ikagonga katika kichwa Cha Kepteni George.. Akajikuta akiipapasa na kuishika bastola Yake.. Kisha akamwangalia luteni Sevenlee na muda ule ule akaufungua mlango wa gari Yao na kushuka kwa Ustadi bila kuonekana. Akatembea kwa mguu kama wafanyavyo wateja Wengine.. Alipokaribia mapokezi Macho Yake yakatua kwa vijana Wawili ambao tazama Yao tu ilimpa picha kuwa mwanamke yule yupo msambweni. Akazama ndani ya Hoteli ile kama mteja, lakini hatua tatu mbele akatizama Nyuma kwa Chati, akawaona watu wale wawili aliyowaona Nje wakimfuata lakini Uzuri Zaidi Nyuma Ya Vijana wale alikuwepo Luteni Sevenlee Akiingia kama mtu tofauti na ambaye hajui kile kilichokuwa kinaendelea. Ikawa mbele George, Kati Wale Wakora na Nyuma Alikuwepo Luteni Sevenlee... George Akaendelea kusonga mbele.. Wakati anapanda ngazi kuelekea Ghorofa ya Pili, akamuona mtu, mtu huyo aliyemuona alikuwa ni mtu ambaye Hakukusudia kumuona Pale... Kwa mbali macho Ya kachero George Yalikuwa Yamemuona Mudy Akitoka Juu wanapoelekea akishuka Chini Huku tabasamu lake likiwa katika uso wake.. Tabasamu ambalo lilimpa George hamu ya kujua kile ambacho kilikuwa kimefanywa na Mudy. Wakapishana na Mudy Kama hawajuani lakini kupishana kwao kulifuatiwa na Tukio ambalo hakuna ambaye alitarajia... Kupishana kwao kulifuatiwa na Tukio la Vijana Waliokuwa Wakimfuatilia Kepteni George kuanguka chini Huku damu zikivuja, na Muda Huo Mudy akiondoka kwa kumpita Luteni Sevenlee bila Hata kumuangalia . Kepteni George hakushuhulika na Mudy, alichofanya nikuongeza kasi Kuelekea Chumba Ambacho alimuwacha Yule msichana... Akaufikia mlango huku bastola Ikiwa mkononi mwake.. Akanyonga kitasa, akatanguliza macho kutizama ndani.. Macho Yake yakakutana na Dimbwi la Damu Huku juu yake kukiwa na Miili mitatu Ya Wanaume. Kuiona Hali ile, akajichoma ndani kabisa.. Alichokutana nacho kilimfanya atamani kupiga kelele.. Mwanamke Waliyedhani Angewapa Siri katika kuwapa mwanga katika upelelezi wao, Alikuwa Ameuawa kinyama kwa kuchomwa Kisu katikati Ya Tumbo Huku Utumbo Wote Ukiwa Nje tena akiwa amelazwa Uchi katikti ya Kitanda, Damu Zikichuruzika Kama Maji..
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 26

Macho Yake yakatua kwenye tukio la kikatili lililousononesha Moyo wake na Kumshtua. Katika Yote aliyoyategemea, Hakutegemea kuliona lile ambalo amelikuta pale Chumbani. Mwanamke Yule alikuwa amelala kitandani huku kisu kikubwa kikiwa kimesimama katikati ya Tumbo lake, Huku utumbo Ukiwa nje. Kepteni George alimtizama Yule mhudumu kwa muda pale kitandani alipolala.. Akaliona Chozi lake likishuka Chini. Akamuinamia na kumchunguza Vizuri mwanamke yule. Alikuwa kama amelala, alikuwa kama Yupo katika Ndoto za usingizi... Lakini dimbwi la damu na Utumbo uliotokea Nje ukamfanya kuondoa mawazo kuwa binti Yule alikuwa amelala. Sasa akajua alikuwa akimuangalia marehemu na sio mtu ambaye amelala. George akainuka pale na kutaka kupiga hatua kupekua kitu, lakini macho Yake yakatua ndani Ya mapaja ya binti Yule... Hapo akaona kama kulikuwa na kitu, kitu ambacho kiliwekwa kwa Ajili yake. Akarudi pale kitandani kisha kuipandisha Nguo Ya mwanamke Yule.. Hapo macho Yake yakatua katika kikalatasi cheupe.. Kilikuwa kimechomekwa kwenye lastiki ya Chupi ya mwanadada yule aliyeuawa. Huku akiwa anatetemeka kwa Hasira Kepteni George akakichomoa kile kikalatasi kisha kukikunjua.. Akakutana na Maandishi Yaliyoandikwa kwa Damu Yakisomeka kama ''KUNA MSALITI KATI YETU''' Kitu kama kengele kikaugonga Ubongo wa kepteni George.. Akajikuta akilirudia lile neno zaidi ya mara Mbili.. Aligutushwa kuambiwa kuna msaliti kati Yao... Alikuwa akiliwaza hilo tokea mwanzo lakini hakulipa nafasi.. Akamuinamia Yule marehemu pale kitandani kisha kwa sauti Yenye Uchungu mwingi Akatamka. ''Kwa yoyote Yule aliyehusika na Mauaji Yako.. Nakuapia nitalipa kisasi kwa mikono Yangu mwenyewe.

Baada ya kutamka maneno hayo akatoka ndani ya chumba kile akiwa amemtanguliza mbele Luteni Sevenlee. Kichwa chake kilikuwa hakipo sawa na hakuonekana kuwa na hata Chembe Ya Furaha. Katika nafsi Yake alihitaji kukutana na Mudy kwani Alihisi Mudy kuna Vitu vingi anavijua na hata kuwalipua wale Vijana mbele Ya Macho yake kulimpa picha kuwa Mudy ndio amehusika na Vifo vya Watu wale kasoro Cha Yule mhudumu tu. Je ni nani aliemuua Binti Yule? Na Mudy Alijuaje kuwa Yule binti Yuko pale? Maswali hayo ndiyo Yakampa Kepteni George Shauku Ya Kukutana na Mudy, maana kulikuwa na Hatari Alizozigundua muda mrefu. Wakati wakitoka Nje kabisa Ya Hoteli Ile kuelekea walipopaki gari Yao, mara Wakaona kitoto kidogo Kikiwakimbilia huku kikiwaita.. Mwanzo Kepteni George Alitaka kupuuza lakini kengele Ya Hadhali Ilipogonga katika kichwa Chake, Akasimama kukisubiri kitoto kile. Kilipomfikia Akashangaa kile kitoto kikimnyooshea mkono.. Kepteni George Naye akafanya Hivyo.. Akashangaa akipewa kikaRatasi Cheupe kama kile alichokipata ndani.. Lakini Hiki utofauti wake Ulikuwa ni kwenye Maandishi na Wino uliotumika kuandikia.. Safari Hii haikuwa Damu bali ulikuwa wino wa kalamu lakini Wino Mwekundu. Akakifungua kwa Tahadhali.. Hapo akasoma kitu kilichoandikwa Humo ndani Kisemacho '''MSILITUMIE GARI LENU''' mwili Ukamsisimka.. Akatambua kweli walikuwa matatani, lakini ni nani anayewaachia Ujumbe Wa aina hii? Yalikuwa maswali ambayo yalikosa Majibu kabisaa.....

*****

tangu mudy alipotoka kwenye ile hoteli kengele za kuashilia hatari zilikuwa zikikigonga kichwa chake. Kuchelewa kumuokoa Yule msichana kulimuumiza sana. Alikuwa amewahi Vizuri katika Eneo la hoteli, lakini kutokukijua Chumba ambacho alikuwa akiishi Yule mhudumu ndicho kilichosababisha Kushindwa kumuokoa Msichana Yule. Alipotoka pale ndani alitokea upande wa pili wa hoteli ile na kwenda kujibanza pembeni kidogo Ya hoteli aliyotoka. Kujibanza pale kulifanyika baada ya pale alipowaona Vijana wawili wa Usalama wa Taifa Wakiingia pale. Kitendo cha kepteni George na luteni Sevenlee Kuingia pale ndani kulimfanya Ashuku kitu. Kwani ni Muda mfupi tu alipokuwa kule ndani Alimuona Kanali Jamila Akitoka ndani ya Hoteli. Na alipotoka wakati anashuka ngazi akamuona kwa macho yake akiwakwepa Wapelelezi wale. Hilo la Kanali Jamila kuwakwepa Kina Kepteni George kikampa hofu Mudy. Akaamua kukaa Pale akiangalia Ulipo mlango wa kutokea wa Hoteli Ile. Kukaa kwake pale kukamfanya amshuhudie Kanali Jamila atume vijana ambao walikwenda kuweka kitu katika gari Ile kisha Wakaondoka maeneo yale. Hilo likawa Jipya machoni Kwa Mudy, hisia Za Usaliti Zikamuingia... Hapo ndipo alipoandika kikaratasi Akampa Mtoto fulani na kukiagiza wapi kipeleke. Baada ya kufanya kitu hicho akaondoka pale na Safari Ya kuelekea Nyumbani Kwa Yule mhudumu Aliyeuawa ikaanza.

Aliamua kuanza na mhudumu Yule Kwa kuwa alikuwa mmoja kati ya Watu waliokuwa WaMewasiliana na mke Wa Rais Muda mfupi kabla Ya kuuawa pia alikuwa amewasiliana na watu wengine watatu ambao walitakiwa kutafutwa Kwa Usiku huo huo.

Saa Mbili Usiku alikuwa Akishuka Maeneo Ya Sinza.. Akatembea kwa haraka mpaka karibu na Nyumba ya Marehemu Yule. Hapo akakutana na Ukimya Wa kutisha.. Baada Ya Kuangalia Huku na Huko na kuridhika na Hali ya Usalama. Mudy Akazunguka Kwa Upande Wa Uwani kisha Akachupa na?
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 27

Nyumba ilikuwa giza kuonyesha kuwa hapakuwa na mtu.. Mudy akazunguuka upande wa nyuma wa nyumba ile. Muda mfupi alikuwa amechupa na kuangukia kwa ndani. Alipotua ndani alinyata mpaka karibu ya mlango wakuingilia ndani.. Hapo akasimama kwa muda kusikiliza iwapo patakuwa na watu. Ukimya bado ulikuwa ukiendelea vile vile.. Akachomoa funguo zake Za bandia muda mfupi baadae mlango ulikuwa umemtii.. Akaingia ndani huku mdomo wa bastola ukiwa umetangulia mbele. Alipohakikisha Yupo ndani kabisa Ya nyumba ya mwanamke yule aliyeuawa... Mudy alilakiwa na Sebule nzuri Yenye thamani kubwa sana.. Aliitizama Nyumba ile katika namna ya kipekee macho Yake yakatua juu ya kipisi Cha Sigara ambayo kilionyesha kutumika muda mfupi Uliyopita. Akaongeza Umakini Huku Sikio lake likiwa limetega kuisikia iwapo mtu aliyekuwa akivuta Alikuwa ndani Ya Nyumba ile. Muda sio mrefu akasikia mngurumo wa gari Ukisimama nje Ya nyumba. Mudy akajiinua Haraka haraka na Kujisogeza Sehemu Ya maficho.. Muda mfupi akauona mlango ukifunguliwa kisha akawaona watu wawili wakiingia kama kivuli.. Uingiaji wa watu wale ulikuwa burudani machoni mwa Mudy.. Uingiaji ambao ulikuwa ukisadifu ufundi na Usalama wa watu ambao wameingia pale ndani... Mudy akaendelea kubana pale huku akitegemea kama watu wale walioingia kuwa watawasha taa .

Lakini Akashangaa kuwaona Watu wale wakitulia kanakwamba kulikuwa na kitu ambacho walikuwa wakikisuburi. Kuwaona viumbe wale wakiwa katika mkao wa kusubiri, kulimpa mudy hamu kubwa ya kusubiri.. Kwa kujua mbinu Za kijasusi Mudy Alijua kuwa palikuwa na mtu ambaye Alikuwa akisubiriwa. Kitendo hicho kilimfanya muda wote ajiweke tayari kwasababu ya kukabiliana na hatari Yoyote ambayo Ingetokea Mbele Yake.

Akiwa bado ametulia huku macho Yake akiyazungusha kwa hila katika Nyumba ile.. Mara akaliona pazia la Dirisha likisukumwa kisha akaingia mtu mfano wa Upepo... Uingiaji wa mtu huyu wapili ndio ulikuwa umemburudisha Mudy. Ni uingiaji ambao hutumiwa sana na Majasusi kutoka shirika la kijasusi la Israel MOSSAD. mtu yule alipoingia hakuinuka kwa wakati bali alikuwa amebaki pale chini katika namna ambayo ilionyesha kuwa alikuwa ametambua Uwepo wa Mtu au watu pale ndani. Mudy alikuwa akikitizama kitu kile kama Picha ya Sinema.. Licha ya mtu yule kuingia kwa staili ambayo Ilimsisimua Mudy, lakini tayari Alikuwa ameshamtambua kuwa ni kepteni George... Akaendelea kutulia akiusoma Mchezo.. Kila alipohisi labda kepteni george atasimama kutoka pale Chini. Haikuwa hivyo.. Bado GEORGE alikuwa ametulia chini. Sasa hapo Mudy akaingia na Hamu ya kuusoma Mchezo Zaidi. Akaokota chupa ambayo ilikuwa kando Yake kisha akaitupa upande ambapo hapakuwa na mtu.. Muda mfupi akashuhudia watu wale wawili walioingia Mwanzo wakirusha risasi Mfululizo kuelekea kule ilipoangukia Chupa Aliyoirusha... Licha ya watu wale kuinuka na Kuanza kurusha risasi, lakini Bado Kepteni George aliendelea kutulia pale chini. Kitendo hicho kilimfurahisha Sana Mudy.. Hapo ndipo alipoutambua Uwezo wa George..

Kupita kwa dakika mbili tu baada ya Mudy kurusha ile chupa, likatokea Tukio la Kusisimua... Tukio ambalo hata Mudy Mwenyewe Hakuwa Ameliona kisawasawa lakini alishuhudia mtu akianguka Chini tena karibu Yake na kuanza kugugumia kwa maumivu.. Akiwa ameshangazwa na kitendo kile akaduwaa Zaidi Baada ya kumuona Yule Mtu mwingine wa pili akitambarajika Chini na kutulia... Hali ya ukimya Ikarudi pale pale.... Msisimko ukampata Mudy.. Alikuwa ameshuhudia kitu ambacho alikuwa akikipenda kupindukia.. Hali ilikuwa kwenye Utulivu na Ukimya kama hapakuwahi kuwa na purukushani.

Muda mfupi gari Nyingine ilikuwa ikisikika ikisimama nje ya Nyumba ya Msichana.. Mlango Ukafunguliwa na Kuingia watu watatu ambao wao wakakimbilia Ilipo switch Ya kuwashia taa mle ndani.. Paaa! Wakawasha.. Wote wakatahamaki baada ya kukutana na Maiti Za wenzao Wawili.. Mudy Hakujivunga wala kepteni George Hakuchelewa... Wote waliamka katika namna ambayo haiwezi kueleweka... Mudy Akaachia Flying kick huku George akiachia mapigo matakatifu Ya kung fu.. Wote wakajikuta Wakiangaliana... Kabla wakora wale Hawajakaa sawa zikafuatia Ngumi Ambazo Ziliwafanya Waanguke Chini kama Mizigo... Hawakuwapa nafasi Za kujiandaa, pale pale Chini walipoangukia waliwawahi na Kuwafunga Pingu...

Wakawasogeza pembeni na kuanza kuwahoji mawili matatu lakini hapakuwa na Hata mmoja ambaye alifumbua kinywa Chake kuongea Chochote na kitendo Cha kushangaza zaidi watu wale wakaanza kutokwa na Damu mdomoni na kilichofuatia Wote wakakata Roho mikononi mwa Wanausalama wale. Kukata Roho Kwa Watu wale tena Mbele yao, kuliwafanya Mudy na George Kutizamana.. Kutizamana kwao kulikuja baada Ya kuliona tukio la Watu wale kujiua. Hapo walionyesha kuwa Walikuwa Wakipigana na Watu ambao walikuwa na Mafunzo Yote Ya Kijasusi... Wakasachi Vitu Muhimu kutoka kwa Marehemu Wale.. Hapo katika kupekwa ndipo walipokuta Picha Ya Kanali Jamila Ikiwa Mfukoni mwa mmoja wa Marehemu wale.. Mudy na George Wakaangaliana
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 28

Katika kuwapekuwa wakora wale, wakaikuta picha ya kanali Jamila Ikiwa moja kati ya vitu walivyovikuta katika mifuko Ya watu wale. Mudy na George wakatizamana kwa muda.. Hapo hapo wakapeana mikono kuonyesha kuwa wameshakuwa wa moja. Cha kwanza kilichotakiwa kutoka pale ni Mudy kuelekea Nyumbani kwa Jamila.. Huku Kepteni George akienda kwenye ile kampuni ya Simu.. Licha ya kuonyesha kuungana lakini Mudy bado hakutaka kumwambia George kuhusu kuitwa kwake na Rais. George akatangulia kuondoka Huku akimuacha Mudy pale. Baada ya mudy kubaki peke Yake Alichokifanya ni kukiendea Chumba Cha marehemu. Katika chumba hicho hakujua kilichokuwemo lakini Kutokana na kuambiwa kuwa aje aangalie... Akajikuta akipatwa na Hamu ya kuchunguza na kugusa hapa na pale. Akaiendea sehemu ambapo palikuwa na kabati kubwa sehemu ambayo aliambiwa na yule msichana kuwa kuna kitu na atapata mwanga katika kile alichokuwa akikitafuta pale. Kulifikia kabati lile kikafuatia kitendo cha kulisogeza pembeni. Kulisogeza kabati hilo, akapokewa na mlango mbele ya Macho Yake. Hapo akainua mkono na kupapasa juu ya kabati, akakiona kile ambacho alikuwa akikitafuta. Ulikuwa ufunguo wa kukifungulia kimlango kile ambacho kilikuwa kimetengezwa ukutani.

Akauingiza ufunguo, mlango ukakubali.. Kukubali kwa mlango kukafuatiwa ni Mudy kuzama ndani. Hapo akalakiwa na Meza kubwa ambayo Juu yake palikuwa na makaratasi mengi. Akaisogelea ile meza huku moyo ukimdunda.. Alipoifikia Akajipweteka Juu yake na kuanza kupekua hiki na Kile. Punde katika upekuzi Wake akakutana na Bahasha kubwa Ya kaki.. Ilikuwa imetuna kuonyesha kuwa kulikuwa na Vitu ndani Yake. Kabla hajaifungua akaigeuza Nyuma kuitizama.. Hapo akakutaNa na maandishi Yaliyosomeka kama TOP SECRET maandishi ambayo Yaliandikwa Kwa kalamu Yenye Wino mwekundu. Mudy Akifungua.. Ndani akakutana na karatasi kibao ambazo Zimechapwa.. Akaifungua Karatasi Ya kwanza akakutana na Neno MKAKATI WA KUMPINDUA RAIS.. damu Zikamsisimka Mudy.. Hakutegemea Msichana yule kutunza Siri nyeti kama ile. Akatulia akili na kuanza kuisoma. Ulikuwa mpango mahususi Uliowahusisha watu wengi sana.. Mkakati ambao Ulionekana kusimamiwa na Watu watatu ambao wote walikuwa wakijulikana kwa Herufi tu. Mkakati huo pia ulikuwa ukiwashirikisha watu Wengine hasa wanausalama. Na kila mwisho wa Neno kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kikiandikwa ambacho Mudy Hakukitambua kwa wakati Ule.

Karatasi ya pili ilikuwa na neno kubwa lisomekalo KIAPO. hapo kwa Mara ya Kwanza akaliona Jina la Mke wa Rais na Jina la Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa taifa. Pia chini kulifuatiwa na yale Majina ambayo yalikuwa yameandikwa kwa Herufi tu. Na Mwisho kabisa lilikuwa likiandikwa Neno ambalo bado lilikuwa Vigumu Mudy Kulitambua. Mudy akaona kuendelea kusoma akiwa pale ni kuupoteza Muda. Akazikusanya Zile karatasi na kuzichomeka katika Shati lake kisha akapekuwa hiki na kile na alipoona ameridhika akatoka katika Chumba kile.. Lakini Wakati anataka kuufungua mlango wa chumba ili atokee Sebuleni, akahisi Uwepo wa watu katika Sebule. Mkono wake Ukashuka na kuichomoa Bastola Yake Aina Special Colt48.. Akaikamata mkononi kisha kwa macho Yake yaliozoea giza akakiona kivuli cha mtu kikiwa mbele yake. Hapo akaongeza Umakini na kuendelea kuangalia iwapo kulikuwa na Mtu mwingine.. Yeah! Akagundua Uwepo wa mtu mwingine ambaye Alikuwa kwa nje na mtu kwenye Simu. Mudy akaingia pale sebuleni mfano wa kivuli.. Alikuwa hajaonekana kwa Watu Wale. Wakati hajajua kipi cha kufanya akasikia mngurumo wa Gari Ukisimama Nje Ya Nyumba. Mudy akatabasamu.. Alihitaji kuwajua waliokuja na Waliokuwepo. Punde tu mlango ukafunguliwa na Kuingia watu kama Watano Hivi.. Ingawa kulikuwa na Giza lakini hapakuwa na Ugumu Mudy kuwagundua. Kwa Mara Ya pili alimuona Kanali Jamila akiwa na Watu wale.. Ile imani kuwa kanali Jamila Alikuwa msaliti ikajengeka katika kichwa Cha Mudy.

Akasogea taratibu huku umakini ukiongezeka.. Punde akasikia kitu cha baridi kikitua katika kisogo Chake kisha sauti nzito Ikasikika Nyuma Yake. ''' Usijaribu kutingishika.. Ukifanya Hivyo nitausambaratisha Ubongo Wako.. Mudy akatii na Kutulia... Punde akamuona mtu mmoja kati Ya watu wale waliongia na Kanali Jamila Akielekea ilipo swichi Ya kuuwasha Umeme.. Lakini Hakupiga hata hatua moja mlio wa Risasi Ukasikika.. Mudy akashangaa kumuona mtu yule aliyekuwa nyuma yake Akianguka Chini.. Mudy Hakuchelewa alichupa na kuangukia karibu na Swichi.. Kuanguka pale kukafuatiwa ni Risasi Mfululizo Kuelekezwa kwake.. Mudy Akachupa na Kuangukia Nyuma Ya sofa ambalo lilikuwa pale Sebuleni.. Punde akasikia gari Ikiondolewa kwa Kasi Huku milio ya Risasi Ikirindima.. Mudy akaendelea kutulia... Punde Ukimya Wa ajabu Ukatokea... Sehemu Yote ilikuwa kimya Lakini Punde tu akasikia Ving'ora Va Magari Ya polisi.. Mudy akainuka na Kuondoka kwa kupitia Dirashani kabla ya Magari Ya polisi Kufika na Akaianza Safari Kuelekea Nyumbani kwa Kanali Jamila huku kichwani Akijiuliza ni nani amemuokoa Pale?

KESHO
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 025

Wakati anaendelea kutazama kilichokuwemo kwenye makablasha aliyopewa na rais, Mlango ukafunguliwa kwa kasi watu wenye silaha wakaingia kwa kasi ile ile.. Mudy alikuwa amewahi kuruka na kuangukia Nyuma ya kitanda huku bastola Yake ikiwa Imara mkononi. Akatulia kuwaangalia watu wale katika namna ambayo walionyesha kuhamanika kutokana na kutokumuona Mudy. Hawakujua alipo mudy na hawakujua Jinsi alivyojitoa pale.. Muda Mfupi baadae Bastola ya Mudy Ikakohoa Mfululizo.. Watu watatu wakaanguka chini wakiwa wanavuja damu. Mudy akainuka kwa samasoti na kutua sehemu nyingine kutoka pale alipo. Bado bastola yake ilikuwa mkononi alipowaendea maiti wale na kuanza kuwasachi mifukoni.. Alichukua kila alichokiona kina Umuhimu kisha Muda mfupi alikuwa Akiondoka katika Chumba kile akiwaacha maiti wale wakiwa wamelaliana. Kutoka pale hoteli safari yake ilimpeleka mpaka maeneo ya vingunguti.. Akatafuta guest ya kawaida na baada ya kupata akalipa na kuingia Chumbani... Muda mfupi alikuwa akipangua na kupekuwa baadhi ya kadi na vitambulisho ambavyo vilikuwa ni moja kati ya Vitu alivyovichukua kutoka kwa Maiti Wale.

Kila alichokuwa akikichukua alikuwa akikisoma kwa umakini mkubwa... Hakutaka kudharau kila alichokiona kutoka katika mifuko ya wakora wale aliyowaua kule hotelini. Katika kuangalia huko akakutana na picha ya mwanamke Mzuri Sana.. Alikuwa mzuri kuliko wale ambao hakuwahi Kuwaona au kuwa nao.. Licha Ya Uzuri wa mwanamke Yule, lakini hilo halikumvutia katika picha ile. Kilichomvutia ni kule kuliona neno WANTED katika picha ile. Neno ambalo lilimpa ugumu kidogo katika kujua kwani picha ile Iwe na neno kama lile. Aliendelea Kuingalia Ile picha kwa muda huku akiwaza hiki na kile mpaka pale ambapo aliamua kuigeuza ile Picha kwa nyuma. Hapo ndipo alipokutana na namba ya Simu na namba ya Nyumba ya mwanamke Yule... Mudy akatabasamu. Baada Ya kuridhika na Kile alichokiona akayachukua makablasha Aliyopewa na Rais na kuanza kuyapekua.

*******

Ulikuwa muda mzuri kwa kepteni George na Luteni Sevenlee kuelekea kwenye hoteli alipowekwa yule msichana mfanyakazi wa kampuni ya Simu Ili kumdodosa mawili matatu kama wataweza kupata mwanga katika Kazi Inayowakabiri. Walikuwa bado hawakupata Usingizi lakini waliona ni lazima waende kwanza wa kamuhoji mwanamke yule. Gari ilitembea kwa mwendo wa Taratibu Huku wakitizama huku na huko kuona kama wanafuatiliwa, lakini haikuwa hivyo.. Walipofika maeneo ya Morocco wakashangaa wakipitwa na gari moja kwa kasi sana.. Kasi Ya ile gari Iliwafanya kepteni George na Luteni Sevenlee watizamane kwa muda. Lakini kwa kuwa walikuwa wakiwahi sehemu wakaona waongeze Mwendo Ili kuwahi sehemu husika. Wakiwa hatua Hamsini kutoka Ilipo hoteli alipowekwa Yule Mhudumu, wakaiona ile gari Iliyowapita kwa kasi pale Morocco ikiwa imepaki pale. Kengele ya Tahadhali Ikagonga katika kichwa Cha Kepteni George.. Akajikuta akiipapasa na kuishika bastola Yake.. Kisha akamwangalia luteni Sevenlee na muda ule ule akaufungua mlango wa gari Yao na kushuka kwa Ustadi bila kuonekana. Akatembea kwa mguu kama wafanyavyo wateja Wengine.. Alipokaribia mapokezi Macho Yake yakatua kwa vijana Wawili ambao tazama Yao tu ilimpa picha kuwa mwanamke yule yupo msambweni. Akazama ndani ya Hoteli ile kama mteja, lakini hatua tatu mbele akatizama Nyuma kwa Chati, akawaona watu wale wawili aliyowaona Nje wakimfuata lakini Uzuri Zaidi Nyuma Ya Vijana wale alikuwepo Luteni Sevenlee Akiingia kama mtu tofauti na ambaye hajui kile kilichokuwa kinaendelea. Ikawa mbele George, Kati Wale Wakora na Nyuma Alikuwepo Luteni Sevenlee... George Akaendelea kusonga mbele.. Wakati anapanda ngazi kuelekea Ghorofa ya Pili, akamuona mtu, mtu huyo aliyemuona alikuwa ni mtu ambaye Hakukusudia kumuona Pale... Kwa mbali macho Ya kachero George Yalikuwa Yamemuona Mudy Akitoka Juu wanapoelekea akishuka Chini Huku tabasamu lake likiwa katika uso wake.. Tabasamu ambalo lilimpa George hamu ya kujua kile ambacho kilikuwa kimefanywa na Mudy. Wakapishana na Mudy Kama hawajuani lakini kupishana kwao kulifuatiwa na Tukio ambalo hakuna ambaye alitarajia... Kupishana kwao kulifuatiwa na Tukio la Vijana Waliokuwa Wakimfuatilia Kepteni George kuanguka chini Huku damu zikivuja, na Muda Huo Mudy akiondoka kwa kumpita Luteni Sevenlee bila Hata kumuangalia . Kepteni George hakushuhulika na Mudy, alichofanya nikuongeza kasi Kuelekea Chumba Ambacho alimuwacha Yule msichana... Akaufikia mlango huku bastola Ikiwa mkononi mwake.. Akanyonga kitasa, akatanguliza macho kutizama ndani.. Macho Yake yakakutana na Dimbwi la Damu Huku juu yake kukiwa na Miili mitatu Ya Wanaume. Kuiona Hali ile, akajichoma ndani kabisa.. Alichokutana nacho kilimfanya atamani kupiga kelele.. Mwanamke Waliyedhani Angewapa Siri katika kuwapa mwanga katika upelelezi wao, Alikuwa Ameuawa kinyama kwa kuchomwa Kisu katikati Ya Tumbo Huku Utumbo Wote Ukiwa Nje tena akiwa amelazwa Uchi katikti ya Kitanda, Damu Zikichuruzika Kama Maji..
Duuh
 
MKE WA RAIS

Macho Yake yakatua kwenye tukio la kikatili lililousononesha Moyo wake na Kumshtua. Katika Yote aliyoyategemea, Hakutegemea kuliona lile ambalo amelikuta pale Chumbani. Mwanamke Yule alikuwa amelala kitandani huku kisu kikubwa kikiwa kimesimama katikati ya Tumbo lake, Huku utumbo Ukiwa nje. Kepteni George alimtizama Yule mhudumu kwa muda pale kitandani alipolala.. Akaliona Chozi lake likishuka Chini. Akamuinamia na kumchunguza Vizuri mwanamke yule. Alikuwa kama amelala, alikuwa kama Yupo katika Ndoto za usingizi... Lakini dimbwi la damu na Utumbo uliotokea Nje ukamfanya kuondoa mawazo kuwa binti Yule alikuwa amelala. Sasa akajua alikuwa akimuangalia marehemu na sio mtu ambaye amelala. George akainuka pale na kutaka kupiga hatua kupekua kitu, lakini macho Yake yakatua ndani Ya mapaja ya binti Yule... Hapo akaona kama kulikuwa na kitu, kitu ambacho kiliwekwa kwa Ajili yake. Akarudi pale kitandani kisha kuipandisha Nguo Ya mwanamke Yule.. Hapo macho Yake yakatua katika kikalatasi cheupe.. Kilikuwa kimechomekwa kwenye lastiki ya Chupi ya mwanadada yule aliyeuawa. Huku akiwa anatetemeka kwa Hasira Kepteni George akakichomoa kile kikalatasi kisha kukikunjua.. Akakutana na Maandishi Yaliyoandikwa kwa Damu Yakisomeka kama ''KUNA MSALITI KATI YETU''' Kitu kama kengele kikaugonga Ubongo wa kepteni George.. Akajikuta akilirudia lile neno zaidi ya mara Mbili.. Aligutushwa kuambiwa kuna msaliti kati Yao... Alikuwa akiliwaza hilo tokea mwanzo lakini hakulipa nafasi.. Akamuinamia Yule marehemu pale kitandani kisha kwa sauti Yenye Uchungu mwingi Akatamka. ''Kwa yoyote Yule aliyehusika na Mauaji Yako.. Nakuapia nitalipa kisasi kwa mikono Yangu mwenyewe.

Baada ya kutamka maneno hayo akatoka ndani ya chumba kile akiwa amemtanguliza mbele Luteni Sevenlee. Kichwa chake kilikuwa hakipo sawa na hakuonekana kuwa na hata Chembe Ya Furaha. Katika nafsi Yake alihitaji kukutana na Mudy kwani Alihisi Mudy kuna Vitu vingi anavijua na hata kuwalipua wale Vijana mbele Ya Macho yake kulimpa picha kuwa Mudy ndio amehusika na Vifo vya Watu wale kasoro Cha Yule mhudumu tu. Je ni nani aliemuua Binti Yule? Na Mudy Alijuaje kuwa Yule binti Yuko pale? Maswali hayo ndiyo Yakampa Kepteni George Shauku Ya Kukutana na Mudy, maana kulikuwa na Hatari Alizozigundua muda mrefu. Wakati wakitoka Nje kabisa Ya Hoteli Ile kuelekea walipopaki gari Yao, mara Wakaona kitoto kidogo Kikiwakimbilia huku kikiwaita.. Mwanzo Kepteni George Alitaka kupuuza lakini kengele Ya Hadhali Ilipogonga katika kichwa Chake, Akasimama kukisubiri kitoto kile. Kilipomfikia Akashangaa kile kitoto kikimnyooshea mkono.. Kepteni George Naye akafanya Hivyo.. Akashangaa akipewa kikaRatasi Cheupe kama kile alichokipata ndani.. Lakini Hiki utofauti wake Ulikuwa ni kwenye Maandishi na Wino uliotumika kuandikia.. Safari Hii haikuwa Damu bali ulikuwa wino wa kalamu lakini Wino Mwekundu. Akakifungua kwa Tahadhali.. Hapo akasoma kitu kilichoandikwa Humo ndani Kisemacho '''MSILITUMIE GARI LENU''' mwili Ukamsisimka.. Akatambua kweli walikuwa matatani, lakini ni nani anayewaachia Ujumbe Wa aina hii? Yalikuwa maswali ambayo yalikosa Majibu kabisaa.....

*****

tangu mudy alipotoka kwenye ile hoteli kengele za kuashilia hatari zilikuwa zikikigonga kichwa chake. Kuchelewa kumuokoa Yule msichana kulimuumiza sana. Alikuwa amewahi Vizuri katika Eneo la hoteli, lakini kutokukijua Chumba ambacho alikuwa akiishi Yule mhudumu ndicho kilichosababisha Kushindwa kumuokoa Msichana Yule. Alipotoka pale ndani alitokea upande wa pili wa hoteli ile na kwenda kujibanza pembeni kidogo Ya hoteli aliyotoka. Kujibanza pale kulifanyika baada ya pale alipowaona Vijana wawili wa Usalama wa Taifa Wakiingia pale. Kitendo cha kepteni George na luteni Sevenlee Kuingia pale ndani kulimfanya Ashuku kitu. Kwani ni Muda mfupi tu alipokuwa kule ndani Alimuona Kanali Jamila Akitoka ndani ya Hoteli. Na alipotoka wakati anashuka ngazi akamuona kwa macho yake akiwakwepa Wapelelezi wale. Hilo la Kanali Jamila kuwakwepa Kina Kepteni George kikampa hofu Mudy. Akaamua kukaa Pale akiangalia Ulipo mlango wa kutokea wa Hoteli Ile. Kukaa kwake pale kukamfanya amshuhudie Kanali Jamila atume vijana ambao walikwenda kuweka kitu katika gari Ile kisha Wakaondoka maeneo yale. Hilo likawa Jipya machoni Kwa Mudy, hisia Za Usaliti Zikamuingia... Hapo ndipo alipoandika kikaratasi Akampa Mtoto fulani na kukiagiza wapi kipeleke. Baada ya kufanya kitu hicho akaondoka pale na Safari Ya kuelekea Nyumbani Kwa Yule mhudumu Aliyeuawa ikaanza.

Aliamua kuanza na mhudumu Yule Kwa kuwa alikuwa mmoja kati ya Watu waliokuwa WaMewasiliana na mke Wa Rais Muda mfupi kabla Ya kuuawa pia alikuwa amewasiliana na watu wengine watatu ambao walitakiwa kutafutwa Kwa Usiku huo huo.

Saa Mbili Usiku alikuwa Akishuka Maeneo Ya Sinza.. Akatembea kwa haraka mpaka karibu na Nyumba ya Marehemu Yule. Hapo akakutana na Ukimya Wa kutisha.. Baada Ya Kuangalia Huku na Huko na kuridhika na Hali ya Usalama. Mudy Akazunguka Kwa Upande Wa Uwani kisha Akachupa na?
 
MKE WA RAIS

Nyumba ilikuwa giza kuonyesha kuwa hapakuwa na mtu.. Mudy akazunguuka upande wa nyuma wa nyumba ile. Muda mfupi alikuwa amechupa na kuangukia kwa ndani. Alipotua ndani alinyata mpaka karibu ya mlango wakuingilia ndani.. Hapo akasimama kwa muda kusikiliza iwapo patakuwa na watu. Ukimya bado ulikuwa ukiendelea vile vile.. Akachomoa funguo zake Za bandia muda mfupi baadae mlango ulikuwa umemtii.. Akaingia ndani huku mdomo wa bastola ukiwa umetangulia mbele. Alipohakikisha Yupo ndani kabisa Ya nyumba ya mwanamke yule aliyeuawa... Mudy alilakiwa na Sebule nzuri Yenye thamani kubwa sana.. Aliitizama Nyumba ile katika namna ya kipekee macho Yake yakatua juu ya kipisi Cha Sigara ambayo kilionyesha kutumika muda mfupi Uliyopita. Akaongeza Umakini Huku Sikio lake likiwa limetega kuisikia iwapo mtu aliyekuwa akivuta Alikuwa ndani Ya Nyumba ile. Muda sio mrefu akasikia mngurumo wa gari Ukisimama nje Ya nyumba. Mudy akajiinua Haraka haraka na Kujisogeza Sehemu Ya maficho.. Muda mfupi akauona mlango ukifunguliwa kisha akawaona watu wawili wakiingia kama kivuli.. Uingiaji wa watu wale ulikuwa burudani machoni mwa Mudy.. Uingiaji ambao ulikuwa ukisadifu ufundi na Usalama wa watu ambao wameingia pale ndani... Mudy akaendelea kubana pale huku akitegemea kama watu wale walioingia kuwa watawasha taa .

Lakini Akashangaa kuwaona Watu wale wakitulia kanakwamba kulikuwa na kitu ambacho walikuwa wakikisuburi. Kuwaona viumbe wale wakiwa katika mkao wa kusubiri, kulimpa mudy hamu kubwa ya kusubiri.. Kwa kujua mbinu Za kijasusi Mudy Alijua kuwa palikuwa na mtu ambaye Alikuwa akisubiriwa. Kitendo hicho kilimfanya muda wote ajiweke tayari kwasababu ya kukabiliana na hatari Yoyote ambayo Ingetokea Mbele Yake.

Akiwa bado ametulia huku macho Yake akiyazungusha kwa hila katika Nyumba ile.. Mara akaliona pazia la Dirisha likisukumwa kisha akaingia mtu mfano wa Upepo... Uingiaji wa mtu huyu wapili ndio ulikuwa umemburudisha Mudy. Ni uingiaji ambao hutumiwa sana na Majasusi kutoka shirika la kijasusi la Israel MOSSAD. mtu yule alipoingia hakuinuka kwa wakati bali alikuwa amebaki pale chini katika namna ambayo ilionyesha kuwa alikuwa ametambua Uwepo wa Mtu au watu pale ndani. Mudy alikuwa akikitizama kitu kile kama Picha ya Sinema.. Licha ya mtu yule kuingia kwa staili ambayo Ilimsisimua Mudy, lakini tayari Alikuwa ameshamtambua kuwa ni kepteni George... Akaendelea kutulia akiusoma Mchezo.. Kila alipohisi labda kepteni george atasimama kutoka pale Chini. Haikuwa hivyo.. Bado GEORGE alikuwa ametulia chini. Sasa hapo Mudy akaingia na Hamu ya kuusoma Mchezo Zaidi. Akaokota chupa ambayo ilikuwa kando Yake kisha akaitupa upande ambapo hapakuwa na mtu.. Muda mfupi akashuhudia watu wale wawili walioingia Mwanzo wakirusha risasi Mfululizo kuelekea kule ilipoangukia Chupa Aliyoirusha... Licha ya watu wale kuinuka na Kuanza kurusha risasi, lakini Bado Kepteni George aliendelea kutulia pale chini. Kitendo hicho kilimfurahisha Sana Mudy.. Hapo ndipo alipoutambua Uwezo wa George..

Kupita kwa dakika mbili tu baada ya Mudy kurusha ile chupa, likatokea Tukio la Kusisimua... Tukio ambalo hata Mudy Mwenyewe Hakuwa Ameliona kisawasawa lakini alishuhudia mtu akianguka Chini tena karibu Yake na kuanza kugugumia kwa maumivu.. Akiwa ameshangazwa na kitendo kile akaduwaa Zaidi Baada ya kumuona Yule Mtu mwingine wa pili akitambarajika Chini na kutulia... Hali ya ukimya Ikarudi pale pale.... Msisimko ukampata Mudy.. Alikuwa ameshuhudia kitu ambacho alikuwa akikipenda kupindukia.. Hali ilikuwa kwenye Utulivu na Ukimya kama hapakuwahi kuwa na purukushani.

Muda mfupi gari Nyingine ilikuwa ikisikika ikisimama nje ya Nyumba ya Msichana.. Mlango Ukafunguliwa na Kuingia watu watatu ambao wao wakakimbilia Ilipo switch Ya kuwashia taa mle ndani.. Paaa! Wakawasha.. Wote wakatahamaki baada ya kukutana na Maiti Za wenzao Wawili.. Mudy Hakujivunga wala kepteni George Hakuchelewa... Wote waliamka katika namna ambayo haiwezi kueleweka... Mudy Akaachia Flying kick huku George akiachia mapigo matakatifu Ya kung fu.. Wote wakajikuta Wakiangaliana... Kabla wakora wale Hawajakaa sawa zikafuatia Ngumi Ambazo Ziliwafanya Waanguke Chini kama Mizigo... Hawakuwapa nafasi Za kujiandaa, pale pale Chini walipoangukia waliwawahi na Kuwafunga Pingu...

Wakawasogeza pembeni na kuanza kuwahoji mawili matatu lakini hapakuwa na Hata mmoja ambaye alifumbua kinywa Chake kuongea Chochote na kitendo Cha kushangaza zaidi watu wale wakaanza kutokwa na Damu mdomoni na kilichofuatia Wote wakakata Roho mikononi mwa Wanausalama wale. Kukata Roho Kwa Watu wale tena Mbele yao, kuliwafanya Mudy na George Kutizamana.. Kutizamana kwao kulikuja baada Ya kuliona tukio la Watu wale kujiua. Hapo walionyesha kuwa Walikuwa Wakipigana na Watu ambao walikuwa na Mafunzo Yote Ya Kijasusi... Wakasachi Vitu Muhimu kutoka kwa Marehemu Wale.. Hapo katika kupekwa ndipo walipokuta Picha Ya Kanali Jamila Ikiwa Mfukoni mwa mmoja wa Marehemu wale.. Mudy na George Wakaangalia..
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 29

Kilikuwa kitu ambacho hakikuaminika machoni kwa mpelelezi Yule. Kila alipokuwa akitafuta mwenye majina yenye herufi tu hakuweza kugundua lolote lile. Mudy akaondoka katika Nyumba ile Kwa kupitia njia ile ile alioingilia. Kichwani alikuwa ameshapata mwanga kuwa chanzo cha mauaji Ya mke wa Rais ni kutaka kwao kumpindua Rais.. Lakini licha ya kuhisi Hivyo, lakini bado kitendo cha mke wa Rais kuuawa kulikuwa na Sababu ambazo bado hakutaka kuziamini kwa wakati Ule. Maswali mengi kwa nini mke wa Rais alienda Kule mbezi yalikuwa ni Mashaka. Mashaka ambayo yalileta Hisia. Hakutaka kuzidharau Hisia Zake akaamua kutafuta na kujua kiini cha tatizo lililopo.. Pia kuwajua wale Watu watatu ambao majina yao yapo kwa herufi tu. Ingawa katika akili Yake alijua kuwa Waziri Wa Mambo Ya ndani na Waziri Wa ulinzi Walikuwemo katika kile ambacho alikuwa akikitafuta. Akaiendea Tax moja kati Ya nyingi Zilizojipanga Pale. Akaingia na kumuamuru Dereva Ampeleke kibaha. Kupelekwa kwake kibaha kulikuwa tofauti na Mawazo Yake ya Kwanza kwamba aende kupekuwa nyumbani kwa kanali Jamila.

Aliamua kwenda kibaha kwa sababu ya kuhitaji utulivu pia akihitaji kupekua mafaili mengi sana ambayo aliyachukua kutoka nyumbani kwa mwanamke Yule aliyeuawa. Tax ilitembea katika mwendo wa kawaida huku Muda Mwingi Mudy Akiutumia kutupia macho Yake nje kuangalia Iwapo kuna watu wanaomfuatilia. Lakini hakukuwa na kitu Cha Aina Hiyo.

*********

Gari Ya Captain George Ilisimama mtaa wa Tatu kutoka Sehemu ambayo Alikuwa akielekea. Akashuka na Kuingia katika barabara Ambayo kwa Usiku ule haikuwa na Watu Wengi kutokana na kuwa Usiku Mwingi sana. Alitembea kwa Umakini katika Eneo lile la Mlimani mpaka alipoivuka barabara na kuingia Eneo la mlimani City.. Hapo akahisi kuwa hakuwa peke yake katika safari Yake hiyo.. Hakumuona mtu lakini katika hisia Zake ambazo hutakiwa kuheshimiwa alikuwa amehisi kuwa kulikuwa na mtu sehemu fulani akimuangalia ama Kumfuatilia. Akaendelea kutembea huku Akiangaza Jicho lake katika namna ambayo ingeweza kuona Chochote hata kama pangekuwa na Giza la Aina gani. Licha ya kutizama kote lakini Hakumuona mtu. Akaendelea kutembea Huku Kengele Ya Hadhari akimkumbusha. Muda Wote mkono wake ulikuwa ndani ya Mifuko Ya Suruali Yake alipohifadhi bastola Tayari kwa kumlipua Yoyote ambaye angetokea. Akatokea Upande Wa chini ambapo palikuwa giza Lengo likiwa ni kuwazuga endapo kulikuwa na Watu wakimfuatilia. Baada ya kuingia upande Wa Chini akaanza kurudi kinyumenyume mpaka alipolifikia lango la Kuingilia Ndani akachomoa Funguo zake Malaya na Kuamza kufungua.. Lakini kabla hajafanikiwa Mlinzi Wa Eneo Lile akafika akiwa na Kirungu na kumtaka Kepteni George Atulie. Hakujua alikuwa anaongea na Mtu gani.. Akiwa amemsogelea kwa ukaribu Sana.. George akafyatuka teke kali ambalo lilimpata Yule mlinzi kwenye Korodani. Akapiga Yowe kubwa kwa maumivu.. Lakini hapo hapo akakutana na pigo jingine la Karate Mlinzi Akaanguka Chini kama Mzoga. George akamburuza na Kumuweka Kando. Akaliendea lango tena lakini kabla hajalifungua Akahisi Vishindo vikitokea Nyuma Yake. Akatulia tuli. Mara akamuona mlinzi Na wakati huo huo akasikia mlinzi Yule Akimuita Mwenzake. Hakumpa nafasi.. Alimnyatia na Kumtia Pigo moja la Shingo akazimia.. Akamchukua na kuweka pamoja na mlinzi Wa mwanzo.

Akaliendea geti na Kulifungua.. Muda Mfupi alikuwa ndani Sehemo iliyoonekana kuwa kama Ukumbi Wa mikutano. Akatembea Haraka Haraka mpaka pale alipouona Mlango Wa Chumba kilichoandikwa MAWASILIANO. Akausogelea kisha Akachoa funguo na kuanza kuufungua.. Kabla Hajafika popote Taa za Ukumbi Ule Zikawaka... Hapo hapo akasikia Sauti za makofi kutoka kwa watu ambao Walionekana kuwa Zaidi Ya Mmoja wakimpongeza kwa Kuingia Mle ndani.. Mkono wake Mwepesi Ulikuwa Tayari Umeshafika mahali alipoihifadhi bastola Yake.. Lakini vile vile Hakujua Wepesi wa Watu ambao walikuwa ndani Ya Ukumbi ule.. Akajikuta akikutana na Teke kali... Ingawa alijaribu kulikinga lakini kiasi fulani Lilimuingia. George Akasimama Vizuri kisha akawatazama watu waliomo.. Hapo ndipo alipobaki mdomo Wazi... Mbele Yake Kulikuwa na Watu Saba.. Wote walikuwa watu ambao aliwajua. Macho Yake Yalikuwa Yakiwaangalia Kanali Jamila, Luteni Sevenlee... Mkurugenzi Wa Usalama Wa Taifa Mr Adnani Kassim Kwangaya pamoja Viongozi Waandamizi katika Serikali Ile.. George akaduwaa Zaidi.. Alikuwa ameduwaa kwa kuwa Hakuwa na Ujanja tena.. Alipowaza kuhusu Mudy Kwenda Nyumbani kwa Kanali Jamila Akauona Mwisho Wake. Hakuona Atatokaje na Kuwa hai katika Mikono ile. Kwa Mara Ya kwanza marafiki Zake ambao walitoka Wote Masomoni katika Chuo Cha makomandoo kule Urusi Walikuwa Ameshamsaliti.

Wakati Akifikiria Hilo akawaona Watu wale Wakimsogelea Kwa Karibu Zaidi na Mbaya Zaidi Kila mmoja Alikuwa na Bastola Tayari kuifyatua na kuusambaratisha Mwili Wa Kepteni George. Hapo George Akakaa tayari Kwa Mapambano.. Hakuwa Tayari kufa kikondoo. Hatua Tano kabla HawaJAfikia TAA ZIKAZIMWAAA

SEHEMU YOTE IKABAKI GIZA
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 30

Wakasogea pale alipo George huku wakichomoa silaha Zao tayari kumuangamiza George.. Hatua Tano kabla hawajamfikia Taa Zikazimwa. Sehemu Yote ikawa giza.. Kilikuwa kitendo kilichofanywa Haraka sana bila kutarajiwa. Wote wakahamanika Wasijue kwanza cha kufanya.. George alikuwa Tayari Ameruka na kuangukia pembeni Toka pale alipokuwa amesimama. Kuanguka kwake kando kukapishana na mvua Ya Risasi Mfululizo Kuelekea pale alipotoka. Kutua kwake pembeni kukafuatiwa na Milipuko kadhaa kutoka Nje. Milio Ya Risasi ilikuwa Imetanda eneo lote la Mlimani City. Licha Ya Kusikia milio Hiyo bado George Alikuwa ametulia Huku bastola mkononi. Macho Yake Ya Hila yalikuwa Yakitambaa katika ukumbi Ule. Aliangalia hapa na pale lakini bado palikuwa na Ukimya Wa ajabu.. Lakini Ukimya Wa ndani Ulikuwa Ukisindikizwa na Mapigano Ya Risasi Kwa Nje. George akataka kuinuka kutoka pale alipo.. Lakini kabla Hajafanya Hivyo, akashangaa Taa Kuwashwa na Sehemu Yote pakiwa peupe. Bado alikuwa ametulia pale pale Chini.. Mara Akauona Mdomo Wa Bastola Ukiwa Umetangulia mbele, Kisha kufuatiwa na Sura Ya Mwanamke ambaye kwa kumuona tu alimtambua kuwa Alikuwa mmoja kati Ya walinzi Wa Rais.. George akasimama na Kujitokeza.

Kwa mara ya kwanza George Akamshukuru mwanamke Yule. Hawakukaa Sana pale ndani Kwani George Aliambiwa hapakuwa na Muda Wa kupoteza. Walikuwa wakitakiwa waondoke pale kabla polisi Hawajafika. George Akatii. Wakatoka mle ndani.. Kila Alipokuwa akipita George Alikuwa Akishangaa kukutana Na Watu wakiwa wamelaliana Wakiwa maiti. Wakatoka Eneo la Tukio kila mmoja Akifikiria wapi pa kwenda. Hawakuwa na imani na magari Yao tena. Walichokifanya ni kutembea kwa Miguu mpaka Maeneo Ya Changanyike.. Hapo wakasubiri wakasimama Kusubiri Usafiri. Lakini Walikaa muda mrefu bila kupata Usafiri kwa kuwa ulikuwa usiku mkubwa Sana. Lakini Muda Mfupi waliiona Pikipiki Ikitokea Maeneo ya Mwenge.. George Akaisimamisha.

Iliposimama Wakajipakia wakaondoka eneo la Tukio Huku wakitoa maagizo kwa Vijana Wao wafuate magari Yao ambayo waliyaacha Eneo la Tukio.

*********

Tax ilimshusha Mudy maeneo Ya kibaha maili moja. Akamlipa Dereva Ujira Wake kisha akaanza kutembea kwa miguu kutafuta Hoteli Nzuri Ya kupanga. Ingawa ulikuwa usiku sana lakini bado Mudy alitembea bila wasiwasi Wowote. Aliingia Chochoro mbili na Alipokuja kutokea Mtaa wa Tatu alikuwa amefika kwenye Nyumba ya kulala Wageni Ambayo alikuwa akiifikaga na ndio Ilikuwa sehemu Yake Nzuri Ya Kujificha pindi pale alipokuwa akiiona Hatari katika kazi Zake Hizi Za kipelelezi.

Kwa kuwa ulikuwa Usiku Sana Alikuta Sehemu Yote Imetulia Sana.. Wakati akipiga hatua kulifuata Geti la nyumba ile.. Kwanza Akasita baada ya Kuona kitu ambacho hakikuwa Cha kawaida.. Wakati huo huo mkono wake ulikuwa Tayari Umeshaifikia Bastola yake. Mbele Ya macho Yake alimuona Mtu akiwa Amelala kwa ndani Ya Geti. Ulalaji wa Mtu Yule Haikuwa Ulalaji wa kawaida. Alikuwa ni Mtu aliyeonekana Kama Mfu. Kengele Za hatari Zikakigonga Kichwa Chake.. Akatulia na Kuangalia Huku na Huko.. Alipoona Hakuna Mtu Yoyote.

Akalishika Geti na Kujaribu Kulisukuma. Kweli likafunguka kuonyesha kuwa Halikuwa Limefungwa. Akaingia ndani Kisha Akalifunga geti kama Alivyolikuta. Akavuta hatua mbili kwa kupitia kwenye Giza.. Macho Yake Yakashuhudia Miili Ya Wahudumu Watatu Wa Hoteli Ile wakiwa wametambarajika Hovyo. Kengele Ya Tahadhali Ikaendelea kumgonga Mudy.. Sasa alikuwa akiendelea kutembea kuifuata miili Ya Watu wale.. Mwili wa Kwanza ulikuwa wa Mwanamke ambao Ulionekana kuwa na Tundu la Risasi kwenye Paji la Uso.. Mudy Akainama na kuigusa damu ile.. Bado ilijuwa mbichi kuonyesha kuwa mauaji alikuwepo muda mfupi Uliyopita, Ama bado alikuwepo maeneo yale. Akaachana na marehemu Yule akaiendea Maiti ya pili ambayo ilikuwa imelala kwenye ngazi Za kuingilia ndani Ya Hoteli Ile.. Hata Huyu alikuwa na Tundu la Risasi katika Paji la Uso, lakini tofauti Ya Huyu Risasi Aliyopigwa ilikuwa imekifumua kichwa chake kitendo kilichosababisha Ubongo Kuzagaa Sehemu Yote.

Mudy akaendelea kuingia ndani.. Mbele kidogo akakutana na mtu mwingine akiwa amepigwa Risasi kifuani. Lakini Huyu bado alionekana kuwa Anapumua.. Kwa tahadhali kubwa Mudy akamuinamia na Kujaribu Kumzungumzisha lakini hakupata Jibu lolote kutoka kwake. Akiwa amekata Tamaa kupata chochote akashangaa kumuona mtu Yule Akinyoosha mkono Wake.. Mudy Akautizama Ule mkono.. Akiona Simu Mkononi mwa Mtu Yule. Alichokifanya ni kuipokea.. Wakati anataka kuipekuwa Simu ili kangalia kitu akasikia Mngurumo Wa Gari kuonyesha kuna gari imesimama Nje Ya Hoteli Ile.

Mudy akachepuka pale na Kujibanza kando kabisa. Muda mfupi akawaona Wanaume Watatu waliojazia Vifua vyao Wakiingia katika Ile Hoteli. Walikuwa wanaume Wenye miili ambayo Ilionekana Dhahiri Shahiri kuwa Walikuwa watu wa Mazoezi. Mudy akawatizama Kila Hatua waliyokuwa wakipiga.. Alikuwa akiwasubiri Waingie pale anapopataka Yeye ili Iwe ni Rahisi Kuwamaliza... Hakutaka Kuitumia bastola Yake.. Bali alitaka kupambana
 
MKE WA RAIS

Mudy Hakutaka kuitumia bastola aliyonayo.. Bali alitaka kupambana kwa mikono yake. Akajivuta katika namna ya kipekee bila Ya kuonekana na wakora wale. Akaifikia Sehemu Ambayo alikuwa akiitaka... Sehemu ambayo alikuwa akiwatizama watu wale kwa ukaribu Zaidi. Akairudisha bastola mahala pake, kisha kwa mwendo wa kinyonga au kobe akatamalaki mbele Yao.. Kwa kuwa hawakutegemea Uwepo wa mtu katika eneo lile kutokea kwa Mudy mbele yao kuliwafanya Wote washtuke vibaya mno. Licha ya kushtuka Huko lakini Hawakupewa nafasi Ya kujiuliza Huyu ni nani.. Mapigo matano matakatifu Yaliweza kuwanyamazisha watu wale. Yalikuwa mapigo mazito ambayo Yaliziacha Shingo Za wakora wale Zikiwa pembeni... Mudy Hakuchelewa Eneo lile... Akawapekuwa kwa haraka.. Hapo akakutana na Vitambulisho vya Watu wale kuonyesha kuwa wanatola kitengo Cha kijasusi ndani Ya Usalama Wa Taifa. Wakati Akiendelea kuangalia mara Simu ya mmoja kati Ya watu wale ikaita.. Mudy akatulia kwanza.. Kengele Za tahadhali bado zilikuwa katika kichwa chake.. Moyoni akajua ulikuwa mtego Ama? Lakini akaona aichukue ile Simu.. Akaupeleka mkono wake na kuigeuza ili kuangalia Jina la mpigaji.. Damu Zikamsisimka na Wakati huo huo alikuwa akitupa simu chini na Wakati huo huo akachupa na kutua pembeni na kuruka tena.. Mlipuko Mkubwa ukasikika katika Eneo lote la Kibaha... Moto Mkubwa ulikuwa Ukiwaka.. Mudy alikuwa ameshatoka katika eneo lile... Huku akinusurika kufa kutokana na simu ile kutegwa bomu la Mionzi. Utaalam Uliotumika katika kulitengeneza Bomu lile kulimpa picha Mudy kuwa Hakuwa Anapambana na Watoto. Akapita Uchochoro Huu na Ule Muda mfupi alikuwa kwenye Kituo Cha Tax...

Muda uliyofuata Alikuwa barabarani akirudi Dar es Salaam. Dereva aliyempakiza alikuwa ni Mzee wa makamo ambaye alikuwa ni mwenye maneno Mengi sana.. Mudy naye akaamua kumpeleka Hivyo Hivyo.. Alipoangalia Saa Yake Ilikuwa Saa saba na Nusu Usiku. Alitamani Sana kwenda kulala lakini alitaka kwanza kufika Nyumbani Kwa Kanali Jamila na Baada Ya hapo ndipo angefikiria kupumzika. Baada ya Dakika Arobaini tax ilikuwa ikisimama Tabata Aroma.. Mudy Akashuka na kumlipa Dereva Ujira Wake kisha akatambaa Na Chochoro Kuelekea Nyumbani kwa Kanali Jamila. Hatua kumi na Tano kabla hajaifikia Nyumba Anayoishi Kanali Jamila, Sms Ikaingia Kwenye Simu Yake... Akaichomoa Simu na kuifungua Kisha kuusoma ujumbe Ule... Ulikuwa ujumbe kutoka Kwa George. Ujumbe ambao ulikuwa Umeandikwa katika Lugha Ambayo Waliiijua Wale majasusi hasa Kutoka kitengo Cha Ujasusi Cha Marekani CIA na Hata M16 cha pale Uingereza. Ulikuwa Ujumbe Uliyomtaka Afike Haraka Katika Hoteli Ya Mkendo Kati maeneo Ya Kigamboni.

Mudy Akapiga hesabu Ya Kurudi ama kuendelea na alichokipanga lakini alipoufikiria Ujumbe na Lugha ambayo imeandikwa akaamua kuondoka. Hakutaka kupitia barabara Ya kivukoni. Alichofanya nikuchukua Pikipiki ambayo Ilipitia kulasini kisha Kuvuka Kwenye Daraja la Kigamboni... Muda Mfupi Alikuwa amesimamisha Pikipiki maeneo Ya kigamboni sehemu Maarufu kama Chagani. Akaongoza na kuuendea Mlango wa Hoteli Ile. Lakini Ukimya Ambao aliukuta pale Ulimtisha. Pia hata kuzimwa kwa taa za nje na ndani kulimfanya Abadili njia ya kuingilia. Alizunguka upande Wa nyuma Wa Jengo hoteli ile akauparamia Ukuta na kuangukia kwa ndani.. Kutua kwake chini kulifuatiwa na kuchomoa Bastola Yake.. Akapiga hatua Ya kwanza.. Bado Ukimya na Giza viliendelea kumshangaza. Aliijua Vizuri Hoteli ile na hapakuwahi kuwa Vile Hata Siku Moja.. Hatua Ya pili Akakutana na Kile alichokihisi Tokea aliposhuka kwenye pikipiki. Mwili wa mwanaume Ulikuwa Umelala Kwenye Dimbwi la Damu. Mudy Akaongeza Umakini tenma.. Hatua Ya Sita Alikuwa Akakutana na Mwili Wa mwanaume na Mwanamke Wakiwa Wameuawa Huku Wakiwa Uchi Wa Mnyama. Walikuwa wamekumbatiana Huku Ubongo Wa vichwa Vyao ukiwa umetapakaa. Hali alikuwa tete kwa Mudy.. Bado alikuwa Akimfikiria Kepteni George.. Bado hakuwa na Imani Kama Alikuwa hai Au la!

Akairuka ile miili na Kuendelea kusonga mbele. Sasa alikuwa ameutanguliza Mdomo wa bastola Mbele Yake. Alipopiga hatua mbili nyingine akakutana na Wahudumu wa Tatu Wa Hotel wakiwa Wamelaliana katikati Ya Dimbwi la Damu. Wahudumu hawa ndio waliomtia hasira Mudy.

Akaing'ata Midomo yake kwa Hasira.. Akaanza kukiendea Chumba kimoja baada kimoja. Kila alipokuwa akichungulia Alikuwa akiwaona Watu Wakiwa Wamelaliana huku wakiwa Maiti. Chumba Cha Tisa kufungua Akapigwa na Butwaa Baada Ya kumuona Mtu Ambaye alimtambua Akiwa Chini.

Alikuwa Kepteni George Akiwa Amelala katikati Ya Dimbwi la Damu. Kifua Chake kilikuwa kimefumulia kwa risasi na Kuufanya mwili Wake Mzima kulowa Damu. Mudy Akapiga Hatua kwa Mwendo wa Tahadhari.. Akaufikia Mwili Wa mpiganaji Mwenzie.. Akamuinamia... Akapatwa na Mshangao baada Ya Kumuona George Anapumua... Akataka kumuinua kutoka naye nke kuutafuta Msaada... Lakini George Akamzuia.. Akamuangalia Huku akikohoa Damu... Akanyoosha Mkono kumpa Mudy Kalatasi Fulani. Kisha Yeye akageuza Macho Shingo ikalala Kushoto
KESHO
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 32

Mudy Akataka kumbeba Ili kujaribu kumpeleka Hospitali kujaribu kuyaokoa maisha Ya Kepteni George. Lakini George Alikataa kwa kumzuia. Alichokifanya ni Kunyoosha mkono na kumpa Mudy Kikalatasi Fulani.. Mudy akakipokea Huku bado akiwa ameushika mkono Wa George. Akashuhudia George Akiyageuza Macho Yake na Shingo kuilaza Pembeni. George Alikuwa amekufa mikononi mwa Mudy. Mudy akaduwaa kwa dakika.. Hakutaka kuamini kama George alikuwa amemuacha peke Yake katika Mapambano Yale. Akajaribu kumtingisha huku akimuita Jina lake.. Lakini George hakuwa akiongea tena, wala kuhema. Alikuwa amekufa kifo kibaya sana... Machozi Ya kiume yakamtoka Mudy... Akauachia Mkono wa George. Akayafumba Macho Yake katika namna Ya kusikitisha... '' Tangulia George.. Nakuahidi kwa Yeyote aliyehusika na Kifo chako nitamuua kwa mikono Yangu''' aliongea Mudy Huku akiuhifadhi mwili wa George kwa kuufunika Shuka.. Akasimama kwa Heshima kubwa.. Muda Mfupi alikuwa Nje Ya Hoteli Ile akielekeA katika Vichochoro Vya Tungi Kigamboni.

Alikuwa amezama kwenye Mawazo mazito sana.. Kifo Cha george kilimuumiza na kumtesa sana. Ni wakina nani waliomua George? Inamaana wauaji ndio waliomtumia Ujumbe Ule? Kama ni hivyo walitaka nini nifanye wakati walishamuua George? Hayo Yote Yalikuwa ni Maswali ambayo yalikizonga kichwa Cha Mohamedi. Hapo akakumbuka kwamba alipewa Simu kule kibaha na Marehemu.. Pia alikuwa na kikaratasi Ambacho amepewa na Hayati Kepteni George. Baada Ya kuingia Mitaa miwili mitatu. Hatimaye Mudy akatokea maeneo Ya Tuamoyo: hapo akanyoosha mpaka maeneo ya Mikadi Beach.. Alipofika Hapo akaiendea Nyumba Moja ambayo Ilikuwa Pembezoni Mwa Barabara Iendayo Mjimwema. Alipoifikia Nyumba ile Akaugonga... Akagonga kwa Mara Ya pili... Mara akasikia Nyayo za Miguu Ya mtu Zikisogea pale Mlangoni. Punde mlango Ukafunguliwa huku Mdomo Wa Bastola Ukiwa Umetangulizwa Mbele. Kisha Ikafuatiwa na Sura Ya Mwanamke Mrembo Sana... Tabasamu likatamalaki katika Uso Wake. Lakini tabasamu hilo lilikata ghafla Baada Ya kumuona Mudy Akiwa ametapakaa Damu kwenye mavazi Aliovaa.

Mwanamke Yule akaufungua mlango Zaidi na Muda mfupi Mudy Alikuwa ndani. Alikuwa Amekaa huku amejiinamia. Machoni kwake kulikuwa kukisoma Hasira tu. Alikuwa Anahasira Juu Ya Waliomuua Kepteni George. Alikuwa ni msaada kwake na Alikuwa ni mpiganaji pekee ambaye alikuwa Akimuamini. Lakini alikuwa amelala Akiwa maiti... Akauinua Uso Wake kumuangalia Mwanamke Yule. Akakutana na Macho Yaliyojaa Maswali. Macho Yenye udadisi Wote wa kijasusi. Alikuwa mbele Ya mwanamke ambaye nae alikuwa kama yeye. Mwanamke Shupavu na mwanamke Katili kupindukia. Licha Ya Urembo Wa Mwanamke Yule Lakini alichokifanya Kwenye Tukio ambalo Mwandishi fulani Alilitungia mkasa na Kuliita NITAKUFA NA WEWE kila kuwa kitu kikubwa sana. Hakuwa Mwingine bali Alikuwa ni Mwanadada Jenipher Dominic. Mwanamke ambaye hapo mwanzo alikuwa akitafutwa na Jeshi la polisi na idara Zote Za Usalama kwa makosa Ya mauaji ya kutisha ikiwa ni pamoja na Kumuua Mkurugenzi Wa Makosa Ya Jinai.

Alikuwa akimuangalia Mudy Katika namna Ya kutamani kujua kilichotokea. Alikuwa akiitamani Damu kila alipoiona Damu. Akashangazwa Zaidi pale Mohamedi Aliponyoosha Mkono Wake na kumpa kikaratasi.. Kikaratasi Ambacho kilikuwa kimelowa na kutapakaa Damu. Jenipher Akataka kukikunjua lakini akasita baada Ya kuliona Chozi la Mohamedi Likidondoka. Kwake kilikuwa kitu Cha Ajabu sana.. Kitu ambacho Hajawahi kukiona tokea Alipoanza Urafiki na Mudy. Mudy analia? Kuna nini kinachomliza Mudy? Kipi kimemsibu katika kazi Aliyopewa na Rais? Kutoka na mshangao Uliyompata Akapatwa na Shauku Ya Kutaka Kujua kile kilichopo Kwenye Kikaratasi Alichopewa. Akataka kukikunjua tena, lakini Aliacha baada kumsikia Mudy akitamka kitu ambacho Hukutaka kukiamini... ''Hii Damu ni Damu Ya George! Rafiki Zake Wamemsaliti na kumuua George.. Wamemuaa George kifo kibaya Sana.''

ilikuwa zamu ya Jenipher kupigwa na butwaa.. Alimjua George kwa kila kitu. Alikuwa mpiganaji mahiri Sana. Ambaye Daima hakuogopa kupambana na mtu. Hilo likamfanya Akikunjue kile kikaratasi.. Akakutana Na neno Arusha Kisha Namba 132 harafu Chini ya karatasi kuliandikwa Kanali Jamila and luteni Sevenlee. Hakuwa mgeni wa Jumbe Za Kijasusi Kama Zile.. Alishatambua kwa nini marehemu George alimpa Mudy Ujumbe Ule. Muda Mfupi alikuwa Akiingia Chumbani kwake na Dakika Mbili Baadae Alikuwa ametoka Akiwa katika Mavazi Ambayo.. Hata Mudy Alipoyatazama Alijua kuwa huu Ulikuwa wakati Wa kazi. Jenipher alikuwa Tayari Kuelekea Arusha Usiku Ule... ''' Narudi Ulingoni Kwa Ajili Yako pamoja na George.. Naomba niruhusu Niondoke Usiku Huu..'' Ilikuwa kauli Shadidi Ya mwanadada Yule.. Mudy Akamtizama Usoni Kwa Muda. Ni kweli Jenipher Alikuwa akimaanisha Alichokuwa Akiongea. Machoni Mwake Hapakuonyesha Masihara, alikuwa Tayari kwenda Arusha.... Mudy hakuwa na Jibu , Bado alikuwa akimtizama Jenipher Usoni.... Punde mlango Ukagongwa... MUDY NA JENIPHER Wakatizamana..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom